You are on page 1of 2

TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI

Ndugu Wanahabari na Watanzania wote,


Sisi Wanataaluma ya Habari hapa nchini tumeamua
kuungana pamoja. Lengo kubwa likiwa kusaidiana katika
matatizo mbali mbali hasa ya kiafya.
Muungano huu hasa umechagizwa na kuugua kwa baadhi ya
wenzetu magonjwa sugu ikiwemo saratani.
Tumeungana wanataaluma kutoka vyombo vya habari
mbalimbali yakiwemo magazeti, Televisheni, Radio na Blogu
anuai.
Tuko chini ya mwamvuli wa kampeni maalum iitwayo Media
Car Wash for Cancer. Tumelenga kusaidiana kupitia kampeni
hii kutimiza lengo letu.
Kama mnavyo fahamu, hivi sasa tuna wenzetu 3 wagonjwa
na hali zao haziridhishi. Waandishi wa habari ambao
tumekusudia kuwasaidia hivi sasa kutokana na ukubwa wa
matatizo yao ni Bwana Adolf Simon Kivamwo, aliyekuwa
Mhariri wa Gazeti la Sunday Observer na The Guardian,
ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa
Habari za Ukimwi, (AJAAT), ambaye ana kansa ya utumbo.
Mwingine ni Bwana Danstan Bahai ambaye ni Mwandishi wa
gazeti la Nipashe ambaye amepooza upande mmoja na hivi
sasa yupo nyumbani kwao Muheza.
Pamoja na Bwana Athumas Hamis, ambaye ni Mwajiriwa wa
Gazeti la Habari Leo, ambaye amepooza kuanzia sehemu ya
kiunoni mpaka chini. Hawa wana mahitaji mbalimbali,
ikiwemo gharama za matibabu pamoja kujikimu. Wote
hawana bima za afya.
Wanahabari hawa mtakubaliana name kuwa ni
mahiri
ambao mchango wao kwenye sekta habari na utumishi wao
kwa umma wa watanzania unajulikana.

Ili
kufanikisha
hili tumeunda Kamati
ya
Maalum
inayojumuisha wajumbe kutoka vyombo mbalimbali vya
habari.
Lengo la kamati hii, ni kuchangisha fedha kwa ajili ya
madhumuni hayo. Kabla ya kampeni hii tumekuwa
tukiwasaidia kwa michango mbali mbali, lakini misaada yetu
imekuwa ikipungua siku hadi siku, hivyo tumeona tuujulishe
umma ili nao watuchangie.
Kamati imeandaa harambee ya kuchangisha fedha kwa
mtindo wa kuosha magari katika viwanja vya Leaders Club,
siku ya Jumamosi Julai 4, 2015.
Fedha zitazopatikana zitagawanywa miongoni mwa wenzetu
hawa.
Aidha, kiasi kingine kitatumika kuwasaidia wanahabari
wengine hususani wasioajiriwa ambao wangependa kujiunga
na mifuko ya Bima ya afya nchini.
Tunaomba Wadhamini mbali mbali wajitokeze kutuunga
mkono katika kampeni hii.
Akaunti ya Michango inapokelewa na kamati hii kupitia
namba
MEDIA CAR WASH FOR CANCER CAMPAIGN
AC No. 111-00000356
TANZANIA POSTAL BANK (TPB)
AU HUDUMA ZA FEDHA KUPITIA
Tigo Pesa:0653 155808
M Pesa :0766 970240
Imetolewa na
Benjamin A.Thompson Kasenyenda
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi

You might also like