You are on page 1of 2

TAARIFA KWA UMMA (PRESS RELEASE)

TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO

SN JINA LA ZAMANI JINA JIPYA


01. TTCL PESA T-PESA
NEMBO YA ZAMANI NEMBO MPYA
02

TTCL PESA, Kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, ambao ni watoaji
wa huduma za fedha mtandao inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla kwamba,
imefanya mabadiliko ya Jina na Nembo zinazoitambulisha Kampuni hiyo.

TTCL PESA ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama
Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Julai 2017 ikiwa na lengo kuu la kuwapa Wananchi huduma za kiwango
cha juu kabisa cha ubora na unafuu wa gharama za kutuma fedha, kupokea fedha, kulipia huduma na
kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia simu zao.

Mabadiliko haya yanakuja miezi 9 baada ya TTCL PESA kuanza huduma zake kwa Mafanikio makubwa.
Hatua hii ni kuridhia ushauri wa Wateja na wadau wetu waliopendekeza kufanyika mabadiliko ya jina
na Nembo ili kuongeza mvuto wa huduma, kukidhi mahitaji ya Soko na urahisi wa kuitambua huduma
hii miongoni mwa huduma zinazotolewa na Taasisi nyingine.

Huduma za fedha Mtandao ni Sekta inayokua kwa kasi duniani kote. Hapa Nchini Tanzania, miamala
inafanyika katika jamii kupitia njia hii na kusaidia sana katika kuokoa muda, kurahisisha manunuzi, kutoa
ajira kwa Makundi mengi ya wananchi hasa Wanawake na Vijana, kuongeza Mapato ya Nchi kupitia
tozo za kodi, kuongeza usalama wa fedha na kuepusha uwezekano wa vitendo vya kihalifu kama wizi
na utapeli visiweze kutokea kwa urahisi.

Kwa kutambua umuhimu wa Jina la huduma na Nembo kuwa ni nyenzo muhimu sana katika mikakati
ya Biashara na hasa biashara yenye ushindani mkubwa kama hii ya Fedha Mtandao, TTCL Corporation
inaamini kuwa, Jina na Nembo mpya zitakidhi mahitaji ya Wadau na Ushindani wa soko sambamba na
kusaidia harakati za kuongeza kasi ya kusambaa kwa huduma za Fedha Mtandao zinazotolewa na Shirika
letu kupitia Kampuni yake tanzu ya TTCL PESA.

Tunaileta T-Pesa kuja kuwa muhimili mkuu wa miamala ya kifedha Tanzania. Tunamlenga kila
mwananchi kufaidika na huduma za tpesa ambazo zimekuwa nafuu na salama zaidi. Uzinduzi wa
nembo hii ni mwanzo wa mambo mazuri na makubwa yatakayoletwa na T-Pesa. Nia yetu ni kuwa
sehemu ya kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa kuhakikisha tunatoa suluhisho la uhakika
katika miamala ya kifedha hususani katika malipo ya huduma za umma and ukusanyaji wa malipo
hayo. T-Pesa itashirikiana na taasisi zote za umma, mabenki na taasisi binafsi katika kufikia malengo
haya na mwisho kutoa huduma bora nafuu na za uhakika kwa watanzania.

Imetolewa na;

Ofisi ya Uhusiano,

TTCL Makao Makuu,

Dar Es Salaam.

3 Machi, 2018

You might also like