You are on page 1of 3

Maazimio toka Taasisi zisizokuwa za kiserikali zinazoshughulika

na Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi kwa serikali na viongozi


watakaochaguliwa
Wawakalishi wa Taasisi zinazojishughulisha katika kuwasaidia wakulima wadogo wadogo
kupambana na umasikini kwa kuboresha njia zao za kilimo na kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi nchini walikutana tarehe 22/09/2015 mkoani Morogoro katika ukumbi wa Midland
hoteli kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wadogo wadogo
na kufikia maazimio yanayoitaka serikali na viongozi watakaoingia madarakani kufanya
mabadiliko ya

kisera na mikakati ili kutoa kipaumbele kwa wakulima wadogo wadogo

kupambana na umasikini na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Mkurugenzi wa


Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG) Bw. Charles Meshack aliwasilisha
maazimio hayo mbele ya waandishi wa habari kama ifuatavyo:
1. Bajeti ya Kilimo iwe zaidi ya 10% ya bajeti yote kwa mwaka kama inavyoagizwa na
mkataba wa Maputo na Malabo 2014 ambapo TZ iliridhia. Bajeti hiyo itolewe kwa wakati na
ifike kwa walengwa ambao ni wakulima wadogo wadogo
2. Serikali itakayoingia madarakani ihakikishe inaimarisha uwezo wa mamlaka ya hali ya
hewa ili iweze kutoa taarifa zilizo sahihi na ziwafikie mapema wakulima wadogo wadogo
3. Kuwepo na kitengo cha kuratibu katika ngazi ya wilaya na kitaifa kitakachotatua
migongano inayohusiana na sekta za kilimo, mifugo, maji, misitu, mazingira,ardhi na
uwekezaji
4. Itungwe sera mahususi ya mabadiliko ya tabia nchi
5. Kuongeza wataalamu na maafisa ugani katika fani za kilimo, misitu, maendeleo ya jamii,
mazingira ili waweze kuwafikia wananchi katika ngazi za vijiji
6. Serikali itenge bajeti kwa ajili ya kuziwezesha taasisi zisizokuwa za kiserikali (Asasi za
kiraia) kutekeleza shughuli za maendeleo vijijini

7. Serikali ifanye marekebisho katika sheria ya ardhi ya vijiji no. 5 mwaka 1999 ili
kuonyesha ukomo wa eneo la ardhi ya kijiji
8. Serikali itengeneze sera ya namna ya kuandaa mipango ya maendeleo ya wilaya
itakayotoa kipaumbele kwa wakulima wadogo wadogo ili waweze kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi
9. Serikali izuiye matamko yanayotolewa na viongozi wa kisiasa ambayo hudhoofisha
juhudi za wakulima katika kupambana na umasikini na athari za mabadiliko ya tabia nchi
10. Serikali isimamie utekelezaji wa sheria ya kutokulima mita 60 toka chanzo cha maji
11. Serikali itakayoingia madarakani itoe ruzuku kwa mazao yote ya kilimo kwa wakulima
wadogo wadogo katika maeneo husika.
12. Mamlaka zinazosimamia ubora wa mbegu na usambazaji ziimarishwe.
13. Serikali ihusike kuweka bei elekezi ya mazao ya kilimo
14. Serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji

Mkurugenzi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (katikati) akiwasilisha


maazimio ya taasisi zisizo za kiserikali kwa waandishi wa habari.

Washiriki wa mkutano wa taasisi zisizo za kiserikali kutengeneza maazimio kwa


serikali na viongozi watatakaochaguliwa.

You might also like