You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


20 KIVUKONI
FRONT,
P.O. BOX
9000,
11466 DAR ES

Simu: 255-22-2114615, 21190612


Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600

SALAAM,
Tanz
ania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


WATANZANIA WALIOKUWA AFRIKA KUSINI WAMEREJEA NYUMBANI

Kundi la Watanzania 26 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini


leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi
ya wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11
alfajiri na Ndege ya Fast Jet.
Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za
Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi
nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini,
Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao
lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika
Kusini.

Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata


taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi
kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma
Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo
kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka
iwezekanavyo.
MWISHO.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015

You might also like