Professional Documents
Culture Documents
Jumiki - Taarifa Juu Ya Hali Halisi Na Matukio Ya Kesi
Jumiki - Taarifa Juu Ya Hali Halisi Na Matukio Ya Kesi
(JUMIKI)
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR
25 Mei, 2013
Tarehe 19 Oktoba 2012 Sheikh Farid Hadi Ahmed alitekwa nyara na baadaye kuachiwa
tarehe 22/10/2012. Tarehe 23 Oktoba 2012 Sheikh Farid alitakiwa afike Kituo cha Polisi,
Madema kwa mahojiano kuhusu kutekwa nyara kwake. Masheikh wengine - Sheikh
Msellem, Sheikh Azzan, Sheikh Mussa Juma na Sheikh Hassan walikwenda
1
Baada ya hapo mashtaka kadhaa yakafunguliwa katika mahkama mbali mbali ikiwemo
Kwerekwe (mahkama mbili za Wilaya), Mfenesini na Vuga (Mahkama Kuu). Dhamana
ziliwekewa masharti magumu mwanzoni lakini baadae masharti yakalainishwa na
washtakiwa kupewa dhamana katika kesi zote isipokuwa ile ya Mahkama Kuu. Kwa
upande mwengine, kesi moja ya Mahkama ya Wilaya Kwerekwe ikafutwa na ile ya
Mfenesini pia ikafutwa na Mkurugenzi wa Mashtaka.
Lengo la Jumuiya sio kuingilia kazi za mahkama, bali tunahaki ya kikatiba ya kupinga
uvunjifu wowote wa Katiba ya Zanzibar ya 1984. Kwa kawaida inapotokea uonevu kama
huu tumekuwa tukishuhudia Jumuiya za Kitaifa na za Kimataifa, Taasisi za kutetea Haki
za Binaadamu, Vyombo vya habari duniani, Asasi za Kijamii, Vyama vya wanasheria na
wengineo wakipaza sauti zao kulaaani, kushtumu na hata kukemea waziwazi dhulma
hizo; lakini kwa masikitiko makubwa hali imekuwa ni tofauti kwa Viongozi
waliokumbwa na kadhia hii. Jee taasisi hizo ziko wapi? Au kwa sababu wahusika ni
Viongozi wa Kiislam?
2
Ikumbukwe kama hawa ni viongozi wa juu wa Jamii kubwa ya Kiislam nchini, hivyo kila
mtu linamgusa na kumuuma jambo ambalo likiendelezwa linaweza kusababisha uvunjifu
wa amani usiotarajiwa. Kwa hali hii Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam
(JUMIKI) imewaita Wanahabari, Mabalozi wa chi za nje, na Wadau mbali mbali
kuwaeleza jinsi ya dhulma, ukandamizaji, na uonevu unavyoendelea dhidi ya Viongozi
wetu kama ifuatavyo.
Jumuiya ya Kimataifa; wakiwemo:Mabalozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya, Marekani, na Magharibi kwa ujumla kwa
kukaa kimya kinyume na kawaida yao ya kutetea haki za binaadamu.
Kuvunjwa kwa katiba ya nchi mfano; kuingiliwa uhuru wa habari na maoni kwa
jeshi la polisi kukama CD za mawaidha ya kiislam na kuzuia redio kutangaza
matangazo ya Jumuiya na Kamisheni ya Habari ya Zanzibar na Waziri wa
Mambo ya ndani Mhe: Emanuel Nchimbi kuzuia kutoa taarifa za JUMIKI katika
vyombo vya habari. Mfano: Redio Nour na Adhana FM.
3
Shutma kwa vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, na
Vikosi vya SMZ, kwa kupachuliwa kwa nguvu bendera za Jumuiya katika
sehemu mbali mbali nchini kwa lengo la kuudhalilisha UISLAM, kupigwa na
hata kuuliwa baadhi ya watu kwa kukataa kupachua bendera hizo.
Matumizi ya nguvu kubwa, kuweka hali ya hatari, taharuki na kuzuia hata jamaa
za washtakiwa kukaribia mahkamani ambapo hata kesi ya uhaini ndugu na jamaa
waliruhusiwa kuhudhuria na kusikiliza kesi za ndugu na jamaa zao.
2. Kwa vile Msingi mkuu wa katiba zote za nchi zinazoendeshwa kwa misingi
ya kidemokrasia ikiwemo Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ni kuheshimu na
4
Wabillah Taufiq
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MKUU
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAM
ZANZIBAR