You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK
OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo


tarehe 07 Agosti, 2016 ametembelea Msikiti na Makanisa yaliyopo Chato
Mjini Mkoani Geita na kuendelea kuwasihi Watanzania kuombea amani na
utulivu katika nchi bila kujali tofauti za dini, makabila na kanda
wanazotoka.
Rais Magufuli ametoa ujumbe huo mara baada ya kusali ibada ya Jumapili
katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, na baadaye
kutembelea Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Stephano Parokia ya Chato,
Kanisa la African Inland Church la Chato na kumalizia katika Msikiti wa
Omar Bin -L-Khattab wa Chato.
Dkt. Magufuli amesema pamoja na Watanzania wote kuungana kuombea
amani na utulivu pia hawana budi kutekeleza kwa vitendo Maandiko
Matakatifu ya Biblia yasemayo "Asiyefanya kazi na asile" kwa kuhakikisha
kila mmoja anachapakazi kwa juhudi na maarifa ili kuharakisha
maendeleo ya Taifa.
"Ndugu zangu nawashukuru sana, muendelee kuliombea taifa
hili, taifa letu ni la umoja, sisi wote ni Watanzania, tuendelee
kumuomba mola wetu, kudumisha amani yetu, kujenga umoja
wetu kwa dini zote, makabila yote na vyama vyote, kwa sababu
mola wetu anatupenda sisi sote" Amesema Rais Magufuli.
Aidha, mara baada ya kuwasalimu waumini wa Kanisa Katoliki la Bikira
Maria Parokia ya Chato, Rais Magufuli ameendesha harambee ya
kuchangia ujenzi wa jengo jipya la Kanisa hilo ambapo amefanikiwa
kukusanya Shilingi Milioni moja za papo kwa papo.
Tayari Dkt. Magufuli alishachangia ujenzi huo kwa kutoa Shilingi Milioni
kumi tarehe 03 Aprili, 2016 na ametoa wito kwa watu mbalimbali
kujitokeza kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.
Katika Msikiti wa Omar Bin-L-Khattab na Makanisa ya Anglikana na African
Inland Church Rais Magufuli amechangia Shilingi Milioni tano kwa kila
moja kwa ajili kuendeleza na kukarabati majengo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Chato
07 Agosti, 2016

You might also like