You are on page 1of 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

_________

TAARIFA

KUHUSU

UTEUZI WA WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA WAJUMBE WAWILI WA


BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUPITIA KUNDI LA VYAMA VYA
UPINZANI (CHAMA CHA CHADEMA)

____

IMETOLEWA NA:
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI
S.L.P 941
DODOMA

9 MEI, 2017
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA
________

TAARIFA
KUHUSU

UTEUZI WA WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA WAJUMBE WAWILI


BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUPITIA KUNDI LA VYAMA VYA
UPINZANI (CHAMA CHA CHADEMA)

________

1. Tarehe 4 Aprili, 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


lilifanya Uchaguzi wa kuwachagua Wajumbe Tisa (9) wa Bunge la Afrika
Mashariki watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Bunge hilo. Katika Uchaguzi huo, Wajumbe Sita (6) kutoka Chama cha
Mapinduzi na Mjumbe mmoja (1) kutoka Chama cha Wananchi (CUF)
walichaguliwa. Wagombea wawili kutoka Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) walikosa kura za kutosha kuwapatia ushindi.

2. Hivyo, Bunge linapaswa kufanya uchaguzi kwa mara ya pili ili kuwapata
wawakilishi Wawili (2) kutoka katika Kundi la Vyama vya Upinzani
ambapo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndicho
chenye haki ya kujaza nafasi hizo.

3. Katika mazingira hayo na kwa kuzingatia masharti ya Sheria na Kanuni


zinazotawala Uchaguzi huo, na kwa mamlaka niliyonayo kama
Msimamizi wa Uchaguzi nilitoa TAARIFA ya Siku ya Uteuzi na Siku
ya Uchaguzi kwenye Gazeti la Serikali Na. 537 la tarehe 21
2

Aprili, 2017. Taarifa hiyo ilitaja Siku ya Uteuzi (nomination day) wa
Wagombea kuwa ni tarehe 03 Mei, 2017 Saa Kumi Kamili (10:00)
Jioni na Siku ya Uchaguzi (election day) kuwa ni tarehe 10 Mei,
2017.

4. Hata hivyo, tarehe 28 Aprili, 2017 Chama cha CHADEMA kiliandikia


barua na kuiwasilisha kwangu siku ya tarehe 2 Mei, 2017 Jioni. Barua
hiyo ilitoa maelezo kwamba muda waliopewa kuwasilisha majina ya
wagombea kupitia kwenye Taarifa hiyo ni finyu kutokana na kuathiriwa
na kuwepo kwa siku za mapumziko ya mwisho wa wiki pamoja na
Sikukuu ya Mei Mosi iliyoanguakia siku ya Jumatatu hivyo, kuwepo kwa
ugumu wa kufanya vikao vyao.

5. Kutokana na sababu hiyo, Chama hicho kiliomba kuongezewa muda


usiopungua wiki mbili ili kiweze kukamilisha mchakato wa uteuzi wa
wagombea, kupata uthibitisho wa uraia kutoka Idara ya Uhamiaji na
uthibitisho wa sifa za kugombea kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa
mujibu wa Ibara ya 50 (2) ya Mkataba ikisomwa pamoja na Ibara ya 67
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.

6. Kutokana na sababu zilizotolewa, niliongeza muda wa siku 4 kuanzia


tarehe 3 hadi tarehe 7 Mei, 2017 ili kukiwezesha Chama hicho
kukamilisha taratibu hizo za kisheria na hivyo kukitaka kuwasilisha
kwangu majina na nyaraka za wagombea waliowateua tarehe 8 Mei,
2017 kabla ya Saa Kumi Kamili (10:00) Jioni ambayo ni Siku ya Uteuzi
wa Wagombea (nomination day).

7. Kupitia taarifa hii, napenda kuujulisha umma kwamba Chama cha


CHADEMA kimewasilisha kwangu majina sita (6) ya Wagombea wa
nafasi mbili za ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki. Kati ya wagombea
hao wanne (4) ni wanaume na wagombea wawili (2) ni
wanawake. Majina hayo yamewasilishwa kwangu jana tarehe 8 Mei,
2017 kabla ya muda wa Saa 10 Jioni kama nilivyokuwa nimeelekeza.

8. Baada ya hatua hiyo, nilifanya uchambuzi wa Nyaraka zilizowasilishwa ili


kujiridhisha na uzingatiwaji wa masharti ya uteuzi wa Wagombea kwa
mujibu Ibara ya 50 (2) ya Mkataba, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, 1977, Kifungu cha 4 (4) cha Sheria ya
Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki na Kanuni 5 (2),
3

(3) na Kanuni ya 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za
Bunge, Toleo la Januari, 2016.

9. Matokeo ya uzingatiwaji wa masharti hayo yameainishwa katika


Jedwali lifuatalo:

M
U

WASIFU (CV)
UWIANO WA
H

KUGOMBEA
URAIA (TZ)

HIARI YA

MALIPO
T

JINSIA
JINA
NA.

KUGOMBEA
A
S

SIFA YA
A
R
I
1. PROF. ABDALLAH Jumbe SAFARI
(ME)
2. EZEKIA Dibogo WENJE (ME)

3. JOSEPHINE Sebastian LEMOYAN


(KE)
4. LAWRENCE Kego MASHA (ME)

5. PAMELA Simon MAASSAY (KE)

6. SALUM Mwalim JUMA (ME)

TANBIHI:

-Maana yake sharti husika limetimizwa

10. Uchambuzi huo umebainisha kuwa Wagombea wote wamekidhi


vigezo na masharti yanayotakiwa kwa mujibu wa Sheria. Hivyo,
napenda kutoa TAARIFA na KUWATANGAZA wafuatao kuwa
Wagombea katika Uchaguzi wa Wajumbe Wawili (2) kupitia Kundi la
Vyama vya Upinzani kutoka Chama cha CHADEMA uliopangwa
kufanyika tarehe 10 Mei, 2017:
4

NA. JINA JINSIA CHAMA

1. PROF. ABDALLAH Jumbe SAFARI ME CHADEMA

2. EZEKIA Dibogo WENJE ME CHADEMA

3. JOSEPHINE Sebastian LEMOYAN KE CHADEMA

4. LAWRENCE Kego MASHA ME CHADEMA

5. PAMELA Simon MAASSAY KE CHADEMA

6. SALUM Mwalim JUMA ME CHADEMA

Dr. Thomas D. Kashililah


MSIMAMIZI WA UCHAGUZI

9 MEI, 2017

You might also like