You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI


JESHI LA POLISI TANZANIA

Anuani ya Simu MKUUPOLISI


Ofisi ya Inspekta Jenerali wa
Polisi,
Simu : (022) 2110734
Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556
S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:
DAR ES SALAAM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

DAR ES SALAAM FEBRUARY 04, 2017

Kufuatia tuhuma zilizotelewa na mkuu


wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul
Makonda tarehe 02/02/2017
zikiwahusisha askari wa Jeshi la Polisi
kujihusisha na biashara ya dawa za

1
kulevya, na kwa kuzingatia dhamira
ya serikali ya awamu ya tano ya
kupambana na tatizo ya dawa za
kulevya na kwamba Jeshi la Polisi
ndiyo chombo kinachoongoza
mapambano dhidi ya vita hii ya dawa
za kulevya, ni lazima Jeshi la Polisi
lichukue hatua kali dhidi ya yeyote
atayetuhumiwa kujihusisha na
vitendo hivyo hata kama atakuwa ni
askari polisi.

Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini,


linachukua hatua madhubuti za
kuchunguza askari na wasanii
waliotuhumiwa na baada ya
uchunguzi huo kukamilika hatua kali
za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote
atakayethibitika kujihusisha na
uhalifu huo.

Wakati uchunguzi ukiendelea Jeshi la


Polisi limechukua hatua za
kuwasimamisha kazi askari wote
waliotuhumiwa kama sehemu ya
kuwachukulia hatua za kinidhamu na

2
kisha hatua za kisheria kwa
watakaobainika.

Aidha, wakati tunaendelea na


uchunguzi, niiombe jamii ya
watanzania kuendelea kutupatia
taarifa za uhalifu wa aina yeyote ili
nchi yetu iendelee kuwa salama.

Imetolewa na:
Ernest Jumbe Mangu,
Inspekta Jenerali wa Polisi,
MAKAO MAKUU YA POLISI.

WAFUATAO WAMESIMAMISHWA KAZI


NA MKUU JESHI LA POLISI KUPISHA
UCHUNGUZI WA TUHUMA ZA
KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA
ZA KULEVYA.

1. PF 14473 SACP CHRISTOPHER


FUIME

3
2. PF. 17041 INSP JACOB HASHIMU
SWAI
3. D 3499 D/ SGT STEVEN APELESI
NDASHA
4. E 8431 D/SGT MOHAMEDI JUMA
HAIMA
5. E. 5204 D/SGT STEVEN JOHN
SHAGA
6. E. 5860 D/CPL DOTTO STEVEN
MWANDAMBO
7. E.1090 D/CPL TAUSEN LAMECK
MWAMBALANGANI
8. E.9652 D/ CPL BENATUS SIMON
LUHAZA
9. D 8278 D/ CPL JAMES SALALA
10. E 9503 D/ CPL NOEL MASHEULA
MWALUKUTA
11. WP 5103 D/C GLORIA MALLYA
MASSAWE
12. F 5885 D/C FADHILI NDAHANI
MAZENGO

You might also like