You are on page 1of 2

TAARIFA KWA UMMA

Dar es Salaam, 20 Februari, 2018

MATOKEO YA UCHUNGUZI KUHUSU KAULI YA ASKOFU


ZACHARY KAKOBE
Kufuatia kauliiliyotolewa na Askofu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full
Gospel Bible Fellowship katika mahubiri ya Ibada ambayo alisema kuwa
“Yeye ana pesa kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania”, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanya uchunguzi ili
kubaini usahihi wa kauli hiyo.

Yafuatayo ni mambo ambayo yalibainika baada ya kufanyika uchunguzi


kuhusu kauli ya Askofu Zachary Kakobe;

1. Askofu Zachary Kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yoyote ya
fedha hapa nchini. Aidha uchunguzi ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni mmoja
wa wasimamizi wakuu wa akaunti za kanisa (signatories) zilizopo katika
benki ya NBC zenye jumla ya kiasi cha shilingi 8,132,100,819.00, kiasi hiki
cha fedha kimetokana na sadaka, zaka na changizo ambazo zinatolewa na
waumini wa kanisa tajwa hapo juu, hivyo kwa mujibu wa Sheria hakitozwi
kodi.

2. Kanisa lilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 20,834,843.00 ambazo


zilitokana na uwekezaji katika makampuni ya kukuza mitaji.Kodi hiyo
imelipwa baada ya uchunguzi.

3. Kampuni inayomilikiwa na watoto wa Askofu Zachary Kakobe ilikwepa


kulipa kodi kiasi cha shilingi 37,280,030.00 ambazo zimelipwa baada ya
uchunguzi. Kwa ujumla, kiasi cha kodi kilicholipwa kutokana na uchunguzi
huu ni shilingi 58,114,873.00.

4. Kanisa linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na ‘majaba’


kinyume na taratibu za utunzaji wa fedha, lakini pia uwekaji na utoaji wa
fedha nyingi kutoka benki haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa
ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika.
1
5. Pia ilibainika kwamba Kanisa halitengenezi hesabu za Mapato na Matumizi
ya Fedha kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya Kanisa pamoja na sheria
za usimamizi wafedha ambayo imepelekea matumizi mabaya ya fedha za
waumini kama vile safari za nje ya nchi ambazo zimedhaminiwa na Kanisa
lakini wanaosafiri ni Askofu na familia yake. Vile vile fedha za Kanisa
zinatumika kujenga nyumba ya mke wa Askofu, kwa jina lake na wala si
kwa jina la Kanisa, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za Kanisa.

Aidha, wakati uchunguzi huo ukiendelea,mnamo tarehe 24.01.2018 Askofu


Kakobe aliandika barua kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuomba radhi kutokana na kauli yake ya kebehi pamoja na
matamshi yake ya dharau kwamba ana pesa nyingi kuliko Serikali.

WITO:
 Mamlaka ya Mapato Tanzaniainatoa wito kwa Taasisi zote za dini ambazo
zinajihusisha na shughuli zozote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na kwa
wakati kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kodi.

 Mamlaka ya Mapato Tanzania inazitaka Taasisi zote za kidini kufuata katiba


zao ikiwa ni pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumizi.

Charles E. Kichere
KAMISHNA MKUU
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”

You might also like