You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

Simu: 026-2322480 Sera, Uratibu na Bunge


2 Mtaa wa Reli
Nukushi: 026-2324534
S. L. P. 980,
Barua-pepe: ps@pmo.go.tz 40480 – Dodoma,
Tovuti: www.pmo.go.tz Tanzania.

18 Aprili, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAELEKEZO YA HATUA ZINAZOPASWA KUENDELEA KUCHUKULIWA NA


TAHADHARI DHIDI YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MAENEO
MBALIMBALI NCHINI
Serikali inatoa pole kwa walioathiriwa na mvua za masika, ambazo zilianza Machi
mwaka huu, kwenye maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,


Bunge,Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama,
amesema, kupitia kamati za usimamizi wa maafa katika ngazi zote, Serikali
itaendelea kuchukua hatua kuhakikisha maisha na mali za wananchi zinakuwa
salama dhidi ya madhara yanayosababishwa na mvua hizo.

Hata hivyo, ameagiza umma na mamlaka za ngazi mbalimbali, kuzingatia


maelekezo yaliyotolewa na ofisi yake, Februari mwaka huu.

“Tumeshuhudia ajali za barabarani, magojwa yaliyochochewa na mafuriko,


hatuna budi kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa hali ya hewa,”
amesema Mhe. Mhagama.

Februari mwaka huu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Idara ya Uratibu wa Maafa,


ilielekeza umma na mamlaka katika ngazi mbalimbalii kuchukua tahadhari ili
kuzuia, kujiandaa, kupunguza na kukabiliana na madhara yaliyotarajiwa
kutokana na mvua za masika.

Mhe. Mhagama amasema maelekezo hayo yalitokana na utabiri uliotolewa na


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ambao ulieleza kuhusu Msimu wa Masika;
Machi hadi Mei 2018, mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika
maeneo ya mashariki na magharibi mwa Ziwa Viktoria na maeneo ya Mikoa ya

1
Dar es Salaam, Pwani, kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Visiwa vya Unguja na
Pemba.

Mvua za wastani katika maeneo ya kusini mwa Ziwa Victoria, kaskazini mwa
mkoa wa Kigoma na Nyanda za juu kaskazini mashariki na mvua za chini ya
wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Tanga.

Mhe. Mhagama, amesema mpaka sasa utabiri huo wa kitaalamu umethibitika.


Hivyo, ametoa rai kwa umma kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri
wa hali ya hewa, ambazo hutolewa na kutangazwa kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo, amesema Serikali inatambua na kupongeza hatua zinazochukuliwa


na viongozi, kamati za maafa na wataalam katika sekta mbalimbali kwa
kushirikiana na wananchi, kukabiliana na madhara yaliyotokana na mvua hizo.

Pamoja na hayo, Mhe. Mhagama ameelekeza hatua stahiki ziendelee


kuchukuliwa ili kuhakikisha mvua hizo haziendelei kusababisha madhara.

Kwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Maafa Namba 7 ya Mwaka 2015 na


Kanuni za Usimamizi wa Maafa za Mwaka 2017, Mhe. Mhagama ameelekeza
Kamati za Usimamizi wa Maafa katika ngazi za vijiji hadi mikoa, kuendelea na
utekelezaji wa majukumu yake hususan kwa kushirikiana na wananchi, ili
kukabiliana na kurejesha hali kwa maeneo ambayo madhara yametokea.

“Nazielekeza kamati za usimamizi wa maafa katika ngazi zote kuendelea


kuwahamasisha wananchi kuondoka katika maeneo hatarishi, hususan
mabondeni na maeneo yenye historia ya maporomoko ya ardhi,” ameeleza
waziri.

Wananchi nao wametakiwa kuchukua hatua katika kuchukua tahadhari dhidi ya


maafa hayo, kwasababu kisheria kila mtu anapaswa kushiriki kikamilifu katika
jitihada za kuzuia, kupunguza madhara, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali
endapo maafa yametokea.

Akizungumzia athari za mvua migodini, Mhe. Mhagama ameelekeza Kamati za


Usimamizi wa Maafa ziangalie namna bora ya kuepusha madhara, kwenye
migodi ambayo imeathiriwa na mvua hizo.

“Ninazielekeza Kamati za Usimamizi wa Maafa kuangalia namna bora ya


kuepusha madhara katika maeneo hayo. Hivyo basi, kila ngazi ihakikishe
inaendelea kuchukua hatua na kujiandaa ipasavyo ili kutekeleza wajibu wake
kwa ufanisi,”alisisitiza Waziri

2
Amesema pamoja na athari hizo, mvua hizo zimekuwa na manufaa kwa shughuli
mbalimbali za kiuchumi na kijamii na hivyo ameshauri wataalamu kuzitumia
katika uzalishaji mali.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA RELINI,
S. L. P. 980,
40480 - DODOMA.
JUMATANO, APRILI 18, 2018

You might also like