You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Tele: +255 026 2322761-5 Ofisi ya Bunge,


Fax No. +255 026 2324218 S.L.P. 941,
E-mail: cna@bunge.go.tz DODOMA.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO


LA BUYUNGU, MAREHEMU MWL. KASUKU SAMSON BILAGO

Kikao cha pamoja baina ya Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya


Uongozi ya Bunge kimefanyika leo Jumapili tarehe 27 Mei, 2018 na
kukubaliana kuwa, mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu,
Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago utaletwa Bungeni Jijini Dodoma
siku ya Jumanne ya tarehe 29 Mei, 2018 kwa ajili ya Waheshimiwa
Wabunge kutoa heshima zao za mwisho.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Uongozi wa Bunge kushauriana na


kukubaliana na Uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) pamoja na familia ya marehemu.

Baada ya Waheshimiwa Wabunge kutoa heshima zao za mwisho, siku


hiyo hiyo mwili wa marehemu utasafarishwa kuelekea Kakonko Mkoani
Kigoma.

Mheshimiwa Mwl. Bilago aliyefariki siku ya Jumamosi tarehe 26 Mei, 2018


katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anatarajiwa kuzikwa tarehe 30 Mei,
2018 katika Kijiji cha Kasuga Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Ofisi ya Bunge inaendelea kuratibu taratibu za mazishi kwa kushirikiana na


uongozi wa CHADEMA pamoja na familia ya Marehemu, taarifa zaidi
zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu
mahali pema peponi.

Imetolewa na: Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,


Ofisi ya Bunge,
DODOMA.

27 Mei, 2018.

You might also like