You are on page 1of 1

Namna ya kuhiji

Mwenye kuenda hija, ima huwa ametia nia ya kufanya (Tamattu’ ) Kufanya umra kisha kupumzika
mpaka wakati wa haji au ametia nia ya ( Qiraan ) nayo nikutia nia ya umra na hija pamoja, na ima awe
ametia nia ya(Ifraad) hija pekeyake mwenye kutia nia yatamatt’ huwa ametoka kwenye amali ya hija na
akatoka kwenye ihram, ama mwenye kufanya qiraan na ifraad watabaki kwenye ihram zao, na shughuli
za Hijja zinaanza terehe nane Mfungotatu. Mpaka siku ya kumi na tatu, Na maelezo yake ni kama
yafuatayo kwa masiku:

Siku ya nane ya Mfungotatu (siku ya Tarwiyah)

1. Siku ya nane ni sunna kwa mja kuhirimia hijja kabla ya adhuhuri atahirimia pale alipo, ataoga, atajitia
manukato, na atavaa nguo za ihramu na atasema: LABBAYKA ALLAHUMMA LABBAYKA, LABBAYKA LAA
SHARIKA LAKA LABBAYKA, INNAL-HAMDA, WANNI’MATA LAKA WALMULKA, LAA SHARIIKA LAKA
(Nimekuitikia, ewe Mola, kwa Hija! Nimekuitika ewe Mola nimekuitika! usiokuwa na mshirika
nimekuitika! Sifa njema zote na neema ni zako, na ufalme, Usiokuwa na mshirika) [Imepokewa na
Bukhari.].

2. Ataelekea Mina, ataswali huko Adhuhuri, Alasiri, na Magharibi, Isha na Alfajiri ya siku ifuatayo.
Ataswali kila Swala kwa katika wakati wake. Atazipunguza Swala za rakaa nne-nne azifanye mbilimbili.
Na atasalia hapo Mina mpaka kutokea jua la siku ya tisa.

You might also like