Professional Documents
Culture Documents
KAZI
Andikeni kazi ifuatayo ndani ya madaftari yenu ya
Darasani
MADA KUU : FIQHI.
MADA NDOGO : FUNGA YA RAMADHANI NASWAUMU
NYINGINE .
1- MAANA YA SWAUMU
i) Maana ya Swaumu : KILUGHA NI : Kujizuia
kufanya jambo lolote la kawaida ulilolizoea.
ii) KISHERIA NI: Kujizuia na kila chenye kufunguza
kuanzia Alfajiri ya kweli hadi kuzama Jua .
2- AINA ZA SWAUMU
- Kuna aina kuu mbili za Swaumu
i) Funga za Faradhi
ii) Funga za Sunna
- Funga za Faradhi ni mbili
i) Funga ya Ramadhani
ii) Funga za Kafara
3 - UMUHIMU WA FUNGA YA RAMADHANI
a)Funga ya Mwezi wa Ramadhani ni Nguzo ya nne
katika Nguzo za Uislamu.
b)Kufunga Mwezi wa Ramadhani ni utambulisho wa
Uislamu wa Mtu
c) Kufunga Mwezi wa Ramadhani ni kutekeleza Amri
ya Mwenyezi MUNGU (s.w )
d)Kufunga Mwezi wa Ramadhani ni Utambulisho wa
Uislamu wa mtu
e) Kutofunga Mwezi wa Ramadhani makusudi
hupelekea kustahiki kupara Ghadhabu na Adhabu
za Allah (s.w )