Professional Documents
Culture Documents
Covid 19
Covid 19
HISTORIA
15. Mazao yaliyoletwa Afrika ya Mashariki na Wareno ni pamoja na: A. Mihogo na kahawa B. Kahawa na
karafuu C. Mahindi na mihogo D. Mkonge na mihogo E.Ndizi na korosho.
16. Mataifa ya Ulaya yaliyokuwa yanapigania mto Nile yalikuwa: A. Ufaransa na Ubelgiji B. Uingereza na
Ujerumani C. Ufaransa na Ureno D. Uingereza na Ufaransa E.Ubelgiji na Ureno.
17. Mapambano ya kudai uhuru katika bara la Afrika yalianza baada ya: A. Kuundwa kwa Umoja wa
Mataifa B. Kusambaratika kwa Umoja wa Kisovieti C. Vita kuu ya pili ya dunia D. Kupigwa marufuku
biashara ya watumwa E.Kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
18. Michoro ya mapangoni iliko kondoa Irangi inasadikiwa kuchorwa wakati wa zama za ……………………….
A. Mwanzo za mawe B. Kati za mawe C. Mwisho za mawe D. Chuma E.Ugunduzi wa moto.
19. Mkataba wa kufunga soko la watumwa la Zanzibar ulisainiwa mwaka …………………….. A. 1882 B. 1845
C. 1885 D. 1884 E.1873.
20. Ipi kati ya nchi zifuatazo ilipata uhuru kwa njia ya vita? A. Zimbabwe B. Tanganyika C. Ghana D.
Malawi E.Zambia.
21. Utafutaji wa njia ya kwenda India ulifadhiliwa na …………………… A. Vasco Da Gama B. Bartholomeo
Diaz C. King Henry D. Cecil Rhodes E.Henry Stanley.
22. Mkataba wa kwanza uliotiwa saini mwaka 1822 kukomesha biashara ya watumwa Tanganyika na
Zanzibar uliitwa: A. Mkataba wa Moresby B. Mkataba wa Frere C. Mkataba wa Heligoland D. Mkataba
wa Hamerton E.Mkutano wa Berlin.
23. Kundi lipi la mawakala wa ukoloni lilikuwa la kwanza kuja Tanganyika? A. Wamisionari B.
Wafanyabiashara C. Walowezi D. Wapelelezi E.Mabaharia.
24. Tanganyika ilipata uhuru wake kwa njia ya: A. Matumizi ya bunduki B. Vita vya msituni C. Mikataba
ya kilaghai D. Kikatiba E.Matumizi ya veto.
25. Hadi kufikia mwaka 1914, nchi zilizokuwa huru barani Afrika zilikuwa: A. Tanganyika na Zanzibar B.
Ethiopia na Liberia C. Ghana na Misri D. Somalia na Jibuti E.Afrika ya Kusini na Rwanda.
26. Umoja wa hiari wan chi huru zilizowahi kutawaliwa na Uingereza hufahamika kama: A. Jumuiya ya
Madola B. Umoja wa Mataifa C. Nchi zinazoendelea D. Umoja wa Afrika E.Shirikisho la Mataifa.