You are on page 1of 1

MWANAHAMISI SALUMU NY’EDI

S.L.P 92
MTWARA.

19/01/2021

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA MTWARA (V)
S.L.P 528,
MTWARA.
K.K
AFISA ELIMU SEKONDARI,
HALMASHAURI WILAYA YA MTWARA (V)
S.L.P 528,
MTWARA

K.K
MKUU WA SHULE,
SHULE YA SEKONDARI KITAYA,
S.L.P .............,
MTWARA.
K.K
MKUU WA SHULE,
SHULE YA SEKONDARI MITENGO,
S.L.P 623,
MTWARA.

YAH: MAOMBI YA UHAMISHO WA MWANAFUNZI BARAKA ISMAIL


CHILIMBA WA KIDATO WA PILI 2021 KUTOKA KITAYA SEKONDARI
KWENDA MITENGO SEKONDARI.
Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu,
Mimi mzazi wa mwanafunzi Baraka Ismail Chilimba wa kidato cha pili 2021, ninaomba
uhamisho wa kijana wangu huyu kutoka shule ya sekondari Kitaya kwenda shule ya
sekondari Mitengo kwa sababu mimi mzazi wake nimehama kimakazi kata ya Kitaya
kutokana na matatizo ya kiusalama ambayo yalitokea na kupelekea nyumba yangu
kuchomwa moto, hivyo kwasasa nimehamia kata ya Ufukoni Manispaa ya Mtwara –
Mikindani, ninaomba uhamisho huu ili niweze kuwa karibu na kijana wangu ili niweze
kumfuatilia kwa karibu mwenendo wake wa kitaaluma pindi awapo shuleni na kumpatia
mahitaji yake muhmi kwa urahisi zaidi.

Ahsante

..........................................................
MWANAHAMISI SALUMU NY’EDI

You might also like