You are on page 1of 72

HUENDA TUKAONGOKA

(Riba na Athari zake ndani ya


jamii na dhana za Uchumi)

Abuu Farheen Farid

i
HUENDA TUKAONGOKA – Riba na Athari zake
ndani ya jamii na dhana ya Kiuchumi
Abuu Farheen Farid
Barua pepe: faridhamad78@gmail.com
Simu: +255 748 202 226
Whatsapp: +255 777 002 226
Tanga, Tanzania
ISBN: 978-9912-40-529-5
Toleo la Kwanza (2022)

ii
KUKIRI
Ndugu yangu msomaji, kufanikiwa kwa ukamilishaji
wa kitabu hichi kumetokana juhudi nyingi za
kusoma na kukusanya mafunzo mengi kutoka kwa
wanazuoni wakubwa ambao walishafanya
uchambuzi huu kabla yangu, hivyo tambua kuwa
kila nukta ambayo nitaibanisha ndani ya kitabu
hichi haitokani tu na ujuzi wangu bali imebebeshwa
elimu kubwa kutoka kwao.
Aidha nukuu za Aya za Qur’an na Hadith za Mtume
(Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam) zimekusanywa
kutoka kwenye vitabu mbali mbali ikiwamo Qur’an
tukufu. Fafanuzi na fatawa ambazo nimekusanya
ndani ya kitabu hichi nimezitoa ndani ya Vitabu
mashuhuri vya wafasiri wakubwa kama vile Ibn
Kathir (Rehma za Allaah ziwe juu yake) na Imam
al-Kurtubi (Rehma za Allaah ziwe juu yake).
Fatawa na majibu yote ya kisharia yametokana na
kitabu cha Fatawa Islamiya cha Ibn Baz, Ibn
Uthaimin na Ibn Jabreen kama walivyo zieleza.
Tafiti na takwimu zote zimetoka kwa watafiti na
wasomi wa mfumo wa fedha na uchumi duniani.
Na nakiri kuwa kukamilika kwa kitu hichi
kumetokana na mchango mkubwa wa wengi katika
jamii ambao naweza kuwataja ni Muhammad
Kifosha kwa mchango wake wa dhati, na kila hatua
ya kitabu hichi hakika anayo nafasi kubwa. Nakiri
kuwa ukamilishaji wa kitabu hichi umetokana na

iii
juhudi za dhati za ndugu yangu Ibn Rajab
Allhassany kwa kukirejea na kuhakiki kitabu hichi
pamoja na heshima ya kuandika dibaji ya kitabu
hichi. Pamoja na familia yangu haswa mke wangu
Firdaus Mohammad Ally ambao wote kwa namna
moja ama nyengine wamechangia ukamilishaji wa
kitabu hichi. Namuomba Allaah (Subhanahu)
awalipe kila kheiri na aweke juhudi zao katika
mizani ya mema yao.
Na napenda kukiri kwamba kitabu hichi nimekifanya
kiwe ni zawadi kwa MAMA yangu mpenzi (Allaah
amuhifadhi) kwa dua zake na moyo wake ulio wazi
kwetu sisi watoto wake katika kutuombea na
kutupa baraka zake ili Allaah (Ta’ala) aendelee
kutubariki ufahamu na nia njema ya kuitumikia
jamii.

iv
MAKOSA YA UANDISHI
Ndugu msomaji, ukamilifu ni wake Allaah
(Subnahanu) kila kazi ya mwanadamu ina makosa
na ndio asili ya mwanadamu kukosea, natanguliza
udhru kwa hatua ambayo nimekosea kwa maneno
ama kwa kwa maelezo huenda malezo yakawa na
makossa yoyote. Lengo langu ni kuelimisha jamii
yetu kwa wema na kukataza maovu yote ambayo
yanaingamiza jamii. Hivyo natoa rai kwa yoyote
ambaye ataona makosa ndani ya kitabu hichi,
asiache ipokuwa kurekebisha kwa wema ili lengo
kuu la chapisho hili lifikiwe.
Abuu Farheen Farid

v
DIBAJI
BISMILLAHI RAHMAANI RAHIIM
Kila sifa njema anastahiki AllaahMola mlezi wa
viumbe vyote, kisha sala na amani zimfikie Mtume
wetu Muhammad pamoja na ahli na maswahaba
zake na wote watakaomfuata kwa wema mpaka
siku ya mwisho.
Baada ya utangulizi mfupi ambao umekusanya
kumshukuru Allah na kumswalia mtume wake ikiwa
ni mwenendo mzuri ambao umekuwa ukifuatwa na
waandishi wengi wa maudhui za dini ya kislamu
zama hadi zama, napenda kuchukua fursa hii baada
ya kumshukuru Allah nifatishe kumshukuru ndugu
yangu Abuu Farheen Farid Bakari Hamad kwa
jitihada zake katika kuelimisha jamii kupitia
uandishi wake mzuri wa Makala na vitabu mbali
mbali kama vile “HAYA NDIYO QURAN
IMENIFUNZA” hiki ni moja kati ya vitabu vizuri sana
katika mafunzo ya Quran tukufu.
Kama tunavyo fahamu kwamba jamii yetu ni kubwa
sana na ukubwa huu unapelekea uwepo wa
harakati mbali mbali za mtu mmoja mmoja au watu
baina yao katika nyanja mbali mbali za kijamii hasa
katika utafutaji wa riziki, na tumekuwa
tukishuhudia kila uchao aina kadhaa za ubunifu
katika jamii zetu, ubunifu ambao msingi wake

vi
mkubwa ni kutaka kujikwamua kimaisha kutoka
sehemu (duni) moja kwenda sehemu nyingine(ya
juu) hili ni jambo zuri sana lakini je! wabunifu wetu
huzingatia mipaka ya sharia iliyowekwa na muumba
wao katika ubunifu wao? au hubuni tu alimuradi
mkono upate kwenda kinywani?
Ni mengi sana hubuniwa katika jamii zetu na
mbaya zaidi wabunifu huangalia hasa upande wao
kwa namna gani wataweza kupata faida bila
kuangalia athari ya ubunifu wao kwa mtu mmoja
mmoja ama jamii kwa jumla, ubunifu uliokuja
katika kuanzisha asasi na vikundi mbali mbali
vyenye kivuli cha kukwamuana kwa kukopeshana
mikopo yenye riba ambayo humkandamiza mlipaji
hasa kinapofika kipindi cha marejesho, wangapi
wamepoteza rasilimali zao na vitu wanavyomiliki
kwa sababu ya riba, ndoa ngapi zimevunjika kwa
sababu ya marejesho, ni watu wangapi wamepata
mshtuko wa moyo kwa sababu ya mikopo ya riba?
ni wengi sana kiasi kwamba katika jamii ukichukua
watu kumi basi wawili wanaishi kutokana na
mikopo yenye riba.
Kitabu hichi ni miongoni mwa hazina kubwa sana
kwa jamii kuwa nayo ili kujikwamua kutoka katika
gereza hili ambalo ni rahisi kuingia lakini ni vigumu
kutoka, kutokana na nidhamu haramu iliyowekwa,
mwandishi ameelezea kwa kina kuhusu riba,

vii
madhara yake kiimani na kijamii na ni kwa namna
gani riba inaathiri katika kujenga uchumi. Maudhui
hii ni moja kati ya maudhui chache ambazo
zimeandikwa, bali watu wengi huizungumzia
maudhui hii (Riba) kwa ujumla bila ya kubainisha
athari zinazopatikana kutokana na riba ndio mana
athari ya yale yanayozungumzwa imekuwa ni
ndogo sana, kwa sababu watu bado
hawajakinaishwa kwa kujua athari hasi
zinazopatikana kutokana na riba.
Allah namuomba amlipe kila la kheri ndugu yetu
kwa sababu amefanya juhudi kubwa sana katika
kukusanya maudhui hii na nimependa njia yake ya
uandishi na mpangilio wake wa dalili, pia kuoanisha
baina ya dalili na uhalisia tuliokuwa nao,
akajumuisha pia fatawa za wanazuoni mbali mbali,
na kisha kutaja njia za kujikwamua kutoka katika
dimbwi hili, hakika ni jambo la kushukuriwa sana
na Allah ajaalie hizi juhudi ziwe katika mizani ya
mema yake. Aaamiin.
Wa billahi taufiiq
MOHAMED RAJABU HASSAN (IbnuRajab
Allhassany)
Ibnurajabalhassany@gmail.com
KHARTOUM-SUDAN
05/11/1443 = 04/06/2022

viii
ix
YALIYOMO
Utangulizi ……………………………………..
Chimbuko la Miamala ya Riba na jamii ya
Kiislam………………………………………….
Maana ya Riba na Aina zake…...…………
Hukmu za Riba ndani ya Uislamu
Hukmu na Makatazo ya Riba ndani ya
Qur’an……………………………………………………..
Hukmu za Riba ndani ya
Hadith……………………………..………………………
Fatawa za wanazuoni juu ya miamala ya Riba na
Sura zake………………………………………………..
Mkusanyo wa wala Riba mbele ya
Allah……………………………………………
Athari za Riba ndani ya jamii na dhana za
kiuchumi……………………………………………..
Vipi tutajikwamua kutoka hapa tulipo…………

x
1
‫ٱلر ِح ِيم‬ ‫ِب ْس ِم ﱠ ِ ﱠ‬
‫ٱلر ْحم ٰـ ِن ﱠ‬

UTANGULIZI
Alhamdulillah, ametakasika Allaah ambaye
ametujaalia nuru ya Imani na kamteremshia Mtume
wake (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) na Kitabu
kitufu cha Qur’an kiwe ni ubainifu kwetu. Mkononi
mwake Allaah kuna uhai na umauti. Swala njema
na Salam ziende kwake Mtukukufu wa darja,
kipenzi cha Allah na Waislam wote Mtume
Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa sallam).
Ndugu yangu msomaji, kitabu hichi kitaelezea kwa
uchache makatazo na ufafanuzi juu ya Riba kupitia
kitabu Kitukufu Qur’an na Sunnah ya Mtume wa
Allah. Qur’an tukufu imekamilisha mfumo mzima
wa mwanadamu katika kutoa miongozo na
makatazo mbali mbali, na kwa ubainifu
yakakatazwa mambo tofauti ambayo huleta athari
kwa viumbe wake katika mfumo wa maisha kama
vile alivyoikemea riba. Allah (‘Azzah wa Jalla)
hakatazi jambo lolote isipokuwa jambo hilo litaleta
fitna na maafa makubwa kwa viumbe na madhara
yake huwa ni makubwa zaidi kwa wenye ubainifu
wa mambo.

2
Asili ya miamala ambayo wanadamu wanaifanya
kutafuta riziki ni miamala ya halali, pamoja na yale
ambayo yanapatikana kama riziki ndani yake zote
asili yake ni riziki halali isipokuwa katika miamala
ambayo ameiharamisha Allaah (Subhanahu) na
Mtume wake, na hakutakuwa na aina yoyote ya
kichumo cha riziki ambacho kimeharamishwa
kupatikana faida na neema ndani yake isipokuwa
khasara na adhabu zake.
Asili ya miamala yote halali ndani ya Uislamu ni ile
ambayo itahakikisha inachunga maslahi na uadilifu
kwa pande mbili za miamala hiyo kwa maana kuwa
kila upande ndani ya muamala huo usitwezwe wala
kudhulumiwa na upande mwengine. Kwenye msingi
huu miamala yenye kuzingatiwa ndani ya sheria
ikawekewa kanuni nne (04) ambazo zitailinda na
kuihakikisha miamala hiyo haivuki mipaka ya uhalali
wake, hivyo yoyote katika waumini wanaofanya
miamala basi achunge kanuni hizi.
1. Muamala sahihi na ulioruhusika uchunge
kanuni ya riba kwa kila aina yake na sura
zake.
2. Muamala sahihi na uliohalalishwa uchunge
kanuni ya kutokupatikana hali yoyote
ambayo itaonekana inaingia kwenye
ubahatishaji na kutazamia jambo ambalo

3
halina uhakika wa kutokea kwa kila aina
zake na sura zake zote.
3. Muamala ulio sahihi na wenye kuhalalishwa
uchunge pande moja kuficha uhalisia wa
jambo lolote linalojumuishwa ndani ya
makubaliano ya muamala huo kwa kila aina
zake na sura zake (Hadaa).
4. Muamala ulio sahihi na kuhalalishwa
uchunge kusababisha madhara ya aina
yoyote kwa pande moja dhidi ya nyengine
huku ukiepuka dhulma na unyonyaji wa kila
aina na sura zake.
Endapo miamala itachunga na kuzingatia kanuni
hizi basi hakutakuwa na dhara wala lawama juu ya
yoyote anayetumia kanuni hizi kwenye kuamiliana
kiuchumi ndani ya sharia za Kiislam. Na kupitia
machapisho haya miongoni mwa kanuni
tunakusudia kufanya uchambuzi wa kanuni hizi
huku kwa awali tukiangalia juu ya kanuni ya Riba.
CHIMBUKO LA MIAMALA YA RIBA NA JAMII
YA KIISLAM
Kutoka kwa Jabir ibn Abdillah (Radhi za Allah ziwe
juu yake) amesema: Mtume (Swalla Allaahu alayhi
wa Sallam) amesema: ((Enyi watu! Mcheni Allaah
na mtumie njia nzuri katika kutafuta riziki zenu,
hakika nafsi haitakufa katika huu ulimwengu mpaka
itakapo maliza riziki yake hata kama itachelewa.

4
Mcheni Allaah na mtafute njia nzuri za Halali,
chukueni katika riziki zilizo Halali na muache katika
riziki za Haramu.)) Imepokelewa na Ibn Maja’a.
Umesema kweli Ewe Mtume wa Allaah! na
umekataza jambo ambalo limekuwa ni giza lenye
kufunika maisha ya walio wengi katika karne yetu.
Hakika kauli hii inapaswa kila Muislam aiandike kwa
wino wa rangi nyekundu machoni kwake na ndani
ya uvungu wa moyo wake. Shetani amezighuri nafsi
za walio wengi katika jamii na kuwasahaulisha juu
ya kuchunga mipaka ya Allaah katika utafutaji wa
riziki. Vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake
wote wametahamaki wakiteleza kwenye mteremko
kuziendea ghadhabu za Allaah kupitia mwevuli wa
Riba.
Hili limekuwa ni janga kubwa ndani ya jamii ya
Kiislamu ukizingatia kwamba uwanda wa Riba
umegusa sehemu kubwa za mfumo mzima wa
fedha na uchumi. Miamala mingi imekuwa
ikifanywa kwakujumuisha riba ndani yake kuanzia
mikopo hadi huduma nyengine za kifedha huku
yakichagizwa vyema na utandawazi (teknologia).
Jamii ya Kiislamu inapaswa kuzingatia na
kuchukuwa tahadhari juu ya kujihusisha ama kutoa
au kupokea Riba katika miamala mbali mbali,
ingawaje walio wengi bila ya kuzingatia mipaka ya
Imani yao wamekuwa kwa makusudi wakikimbilia

5
Riba kwa sababu moja ama nyengine huku wakiwa
na kisingizio cha ugumu wa maisha, ama kutafuta
mitaji, ama sababu nyengine zisizokuwa hizo.
Kwa kadiri jamii inavyoingia kwa undani kwenye
dimbwi la Riba ndivyo inavyoendelea kudhoofisha
Imani zao huku wakiendelea kuwa duni kimaisha
kutokana na unyonyaji unao patikana kupitia
miamala ya riba. Tunapaswa kurudi tena kupitia
mafundisho na makatazo ya riba ndani ya Qur’an
sambamba na miongozo mbali mbali ambayo
Mtume wa Allaah (Swallah Allaahu alayhi wa
Sallam) ametuachia na ndiyo msingi na dhumuni la
kufungua ukurasa huu kwa Hadith hii ili kila mmoja
kati yetu atambue ni wapi aliteleza na kuenda nje
ya mipaka ya Allaah, ili arudi na kutubia kabla
hayajamkuta mauti hali akiwa ndani ya miamala ya
Riba. Tambua! Kama ni hofu ya maisha, ama
mahitaji ya mitaji kwa ajili ya kuendeleza biashara,
basi Allaah (Subhanahu) amesema:

‫َو َكأَيِّن ِ ّمن دَآبﱠ ٍة ﻻﱠ تَحْ ِم ُل ِر ْزقَ َها ٱ ﱠ ُ يَ ْر ُزقُ َها َوإِيﱠا ُك ْم َو ُه َو ٱل ﱠ‬
‫س ِمي ُع‬
﴾٦٠﴿‫ْٱل َع ِلي ُم‬
“Na wanyama wangapi hawawezi kujimilikia riziki
zao! Mwenyezi Mungu anawaruzuku hao na nyinyi
pia. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.”
(29:60)

6
Allaah amesema pia:
ً ‫ٱلر ْزقَ ِل َمن يَشَآ ُء َويَ ْقد ُِر إِنﱠهُ َكانَ بِ ِعبَا ِد ِه َخبِيرا‬
ِّ ‫ط‬ُ ‫س‬
ُ ‫إِ ﱠن َربﱠكَ يَ ْب‬
﴾٣٠﴿ً ‫صيرا‬ ِ َ‫ب‬
“Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtaye,
na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa waja
wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona.” (17:30)
Allaah amesema aidha:

ُ ‫سكَ ِر ْزقَهُ بَل لﱠ ﱡجواْ فِى‬


‫عت ُ ّ ٍو‬ َ ‫أ َ ﱠم ْن َه ٰـذَا ٱلﱠذِى يَ ْر ُزقُ ُك ْم إِ ْن أ َ ْم‬
﴾٢١﴿‫ور‬ ٍ ُ‫َونُف‬
“Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama
Yeye akizuia riziki yake? Bali wao wanakamia tu
katika jeuri na chuki.” (67:21)
Hutosha Allaah (Subhanahu) kuwa mfunguaji wa
riziki za halali na wala hatupaswi kuitafuta nje ya
mipaka ya halali. Kutokana na uzito wa jambo hili
(la Riba) ndio maana tukafungua mlango huu ndani
ya kitabu hichi kuielezea maana, hukumu zake
sambamba na athari zake ndani ya jamii ili iwe ni
fundisho kwa wote wenye kujihusisha na dhambi hii
na tunataraji huenda kupitia machapisho haya jamii
yetu ikaongoka na kupata radhi za Allah
(Subhanahu wa Ta’ala). Tukiwa tunaizungumzia
riba kwa upana wake utaelewa kuwa tunagusa
moja kwa moja uchumi na mfumo mzima wa fedha
katika jamii. Kwa maana athari zake huwaathiri kwa
7
kiwango kikubwa baina ya wenye mali
(Wakopeshaji) na wale wahitaji (Wakopeshwaji).
Riba ina uwanda mpana kimaana na katika hilo
baadhi ya wasomi na wanazuoni wa mfumo wa
fedha na uchumi wamezungumza na kuibainisha
riba katika mitazamo tofauti.
Katazo na uharamu wa riba ndio msingi mama wa
mfumo wa kiuchumi wa kiislamu ambao unahusisha
moja kwa moja sekta za fedha na benk ambazo
ndiyo chimbuko la mitaji ya biashara na mikopo.
Uislamu umeweka misingi sahihi juu ya makatazo
ya Riba kwa maana athari yake katika jamii inauzito
mkubwa. Misingi hiyo ilipovunjwa na kukiukwa
ndipo ikajumuishwa ndani yake mifumo ambayo
Allaah (Ta’ala) ameikataza, ikaibuka ndani yake
dhulma, udanganyifu, hadaa na mengine
yasiyokuwa hayo. Na haya yote yanaaminika kuwa
yametokana na dhana kuwa mwanadamu
anapaswa kufanya njia yoyote ile ajipatie riziki bila
ya kujali na kuchunga ipi ni ya halali na ipi ni ya
haramu. Mifumo hii ikachagiza matendo mengi
maovu ya kuzidisha ama kupunguza kwenye
vipimo, kujilimbikizia mali na fedha hata
iliyopatikana kwenye njia hizo, kukaibua ndani ya
mifumo hiyo tabaka kubwa kati ya wenye mali
(Matajiri) na wale wanyonge wasio na mali
(Masikini) huku wakitengenezwa matajiri wakubwa
ambao wanaweza hadi kuteteresha na kuathiri

8
mifumuko ya bei katika eneo husika na wakiwaacha
wale wanyonge kuendelea kuwa duni kwa
umasikini mkubwa, huku hali hiyo ikilipua hisia za
chuki, uadui na ubinafsi baina ya jamii.
Tabaka la wanyonge wanaohitaji mitaji na vipato
kutoka kwa wale matajiri, wakawekewa utaratibu
wa miamala ambayo hubebeshwa mzigo mkubwa
wa ongezeko la madeni ya dhulma (Riba) ndani
yake ili tu matajiri waendelee kufaidika kutokana na
kima cha mitaji na fedha wanazowakopesha
wanyonge. Kwa kuzingatia athari ya mifumo hii
yote ndani ya jamii, Uislamu ukaja kuweka
muongozo wa namna ambayo watu watafanya
miamala ya kuuza na kununua, kukopa na
kukopeshana huku ukiweka utaratibu maalumu
ukizingatia miongozo ndani ya Qur’an na Sunnah za
Mtume (Swallah Allaahu alaih wa Sallam) ili
kupunguza na kuondoa matabaka ya mali na
umasikini, kukomesha dhulma na hadaa katika
miamala, na haya yote huenda yakakomeka ndani
ya jamii baada ya elimu sahihi juu ya maana,
hukmu, na athari za riba kuelezwa kwa upana kwa
jamii na kwa uwezo wa Allaah (Subhanahu wa
Ta’ala) huenda tukaongoka kwani Allaah
(Subhanahu) anasema katika Qur’an:

9
ِ َ‫يَا أَيﱡ َها ٱلﱠذِينَ آ َمنُواْ ﻻَ ت َأ ْ ُكلُ ۤواْ أ َ ْم َوالَ ُك ْم بَ ْينَ ُك ْم بِ ْٱلب‬
َ‫اط ِل إِﻻﱠ أَن ت َ ُكون‬
‫اض ِ ّم ْن ُك ْم‬
ٍ ‫عن ت ََر‬ َ ً ‫ارة‬ َ ‫تِ َج‬
“Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma,
isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe”
(04:29)
RIBA, MAANA NA AINA ZAKE
Katika istilahi za lugha, neno riba maana yake ni
kama thamani ya wakati wa pesa, kama
inavyoelezwa na usemi wa kawaida “wakati ni
pesa”. Hata hivyo wanazuoni wa Kiislamu
wanapinga kuwa wakati si pesa, bali “wakati ni
uhai”. (Dkt. Usmani, 2021). Thamani ya wakati wa
pesa ni dhana ambayo hutumika katika fani ya
usimamizi wa mifumo ya fedha huku ikiwa na
maana ya kwamba shilingi unayoitoa (kwa mkopo)
leo haitakuwa sawa na shilingi ambayo utaipokea
baada ya muda kadhaa kupita. Hivyo dhana hii
ndiyo ambayo haswa imezalisha hitaji la nyongeza
ya kiwango (rate) ya thamani fulani ili kufidia
thamani ya pesa kwa kipindi ambacho fedha ile
imetolewa kwa mtu mwengine bila ya faida yoyote
kwa mtoaji. Hivyo kupitia dhana hii (Thamani ya
wakati wa pesa) ndiyo inayoifanya fedha kuwa
kama bidhaa ambayo huuzwa na kununuliwa kwa
kwa thamani maalumu (Riba) ili mkopeshaji
kujifidia anguko la thamani kwa kadiri ya kipindi
chote cha marejesho ya mkopo huo.

10
Jambo hili linakinzana na shariah na muongozo wa
Uislamu ambao hutambua fedha kama njia tu ya
kubadilishana isiyo na thamani ya ndani yenyewe,
kwa msingi huu sasa ndipo taarifu ya kuwa katika
Uislamu hairusiwi kukopesha na kupata kiwango
cha uhakika (riba) cha pesa wakati wa marejesho,
na hili limekuja na kurudi katika zile kanuni za
miamala halali ya kisharia kwamba muamala
wowote ni lazima kuchunga kanuni ya kuepuka hali
yoyote isiyo tabirika mwisho na matokeo yake kwa
maana kesho ni jambo lisilo tabirika na kwa kupitia
mwanzo huu tunaweza sasa kutumia misingi hii
kuieleza haswa nini maana ya riba.
Riba ni neno la kiarabu kihalisi lenye maana ya
nyongeza au ziada juu ya bei asili ya bidhaa au
huduma. Na katika istilahi ya kishariah,
linamaniisha fidia yoyote ya ziada bila ya kuzingatia
ujumuishaji wa thamani ya wakati wa pesa. Kwa
mujibu wa Dkt. Usmani, ufafanuzi huu wa maana
ya riba umetokamana na Qur’an na unakubaliwa
kwa kauli moja na wanazuoni wote wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na Iqbal (Msomi
wa mfumo wa fedha na benki wa Kiislam)
amesema; Riba maana yake ni nyongeza, kukuwa,
kuzidisha na kupandisha kwa bei asili. Na
akaongeza kwamba katika dhana ya kiuchumi
inakusudiwa kuwa ni makubaliano ya kimkataba ya
kuongeza katika thamani asili ya mkopo wa fedha

11
au bidhaa ili kufidia thamani ya muda hadi kufikia
wakati wa makubaliano wa marejesho.
Kwa mujibu jarida la shirika la Zakat Foundation
(2020) waliandika na kubainisha kuwa Riba maana
yake ni faida inayopatikana kutokana na ukopeshaji
wa fedha bila ya kufunganishwa na uuzaji wa
bidhaa ama huduma fulani. Na wakaongeza kuwa
riba ni mfumo dhalimu wa fedha ambao
unawafaidisha matajiri (Wenye ziada ya utajiri)
huku wakiongeza bila ya haki kutoka kwa mali za
wanyonge (Wakopaji) na ukiambatana na muamala
ambao unahakikisha faida kwa upande mmoja (wa
matajiri) na khasara kwa upande mwengine
(Masikini wahitaji wa mitaji).
Aina za Riba na Sura zake
Riba, kama tulivyoifafanua hapo awali imetajwa na
kuelezewa kwa uwazi ndani ya Qur’an na Hadith
sahihi za Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam)
na kupitia ufafanuzi huo imeelezwa kuwa kuna aina
mbili za Riba, na ambazo hadi sasa zimetambuliwa
na wanazuoni ni ‘Riba Al-Nasia’ na ‘Riba Al
Fadl’. Baadhi ya wanazuoni wakatafsiri kupitia
Hadith za Mtume wa Allaah na kuenda mbali zaidi
kuongeza aina nyengine mbili za riba ambazo
miongoni mwao wanasema kuwa aina hizi mbili
zinaweza kuwa zimejumuishwa ndani ya aina ya

12
Riba Al-Nasia nazo ni ‘Riba ya Wazi’ na ‘Riba ya
bidhaa’
i. Riba Al-Nasia:
Ni aina ya riba ambayo inatambulika zaidi na pia
aina hii huitwa ‘Riba katika mkataba wa Mkopo’ au
‘Riba Al Jahilia’. Al-Nasia maana yake ni
kughairisha, kuchelewesha ama kusubiri kwa muda
fulani. Hivyo riba ya Mikopo inasemwa kwamba ni
makubaliano ya kimkataba kuongeza, iwe kawaida
ama kwa ziada, juu ya mkopo wa fedha ama mtaji
ambao unaweza kuwa kwenye fedha ama bidhaa.
Kwa maana nyepesi ni kusema kwamba riba ya
mikopo ni aina ya riba ambayo mkopaji hutakiwa
kulipa kiasi cha ziada juu ya kiasi ambacho
amekopeshwa. Na hii imesemwa kwamba ndiyo
riba ambayo Allah ameizungumzia kwenye Qur’an.
Makubaliano mengi ya mikopo ya nyakati za sasa
yanaingia katika kundi hili la riba kwa kuwa
miamala mengi hupelekea kuongezeka kwa kiasi
juu ya kiasi cha asili kutokana tu na kucheleweshwa
kwa muda. Ongezeko lolote lililoamulia awali
(wakati wa makubaliano), au kiasi chochote cha
ziada juu cha mkopo halisi kinachotozwa na
mkopeshaji kinachukuliwa kuwa ni ‘Riba Al-Nasia.

13
ii. Riba Al Fadl:
Aina hii ya pili huitwa ‘Riba Al Hadith’ ama wengine
huita ‘Riba katika mkataba wa mauzo. Riba Al Fadl
inajumuisha nyongeza yoyote ya bidhaa ambapo
bidhaa mbili zenye kufanana zinapo tumika
kubadilishana. Hii imethibi katika Hadith Sahihi za
Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam) akiikataza
na kuwakataza waumini juu ya miamala ambayo
ilibeba sifa na sura za aina hii ya riba. Aidha aina hii
ya riba inaweza kufafanuliwa kuwa ni fidia ya ziada
inayotokana na mauzo ya bidhaa. Tofauti na aina
ya kwanza, riba hii inaweza kutokea katika mauzo
au kubadilishana muamala wa bidhaa kama vile
mchele, ngano, tende, shayiri, mafuta, sukari,
pamba, n.k.
HUKMU ZA RIBA NDANI YA UISLAMU
Riba ina athari kubwa kwa jamii haswa kwa
masikini wahitaji wa fedha na bidhaa kwa ajili yao
na biashara zao, riba kwa yakini ni dhambi kubwa
mbele ya Allah na haina katika malipo isipokuwa
moto wenye kudumu milele. Uharamu wa Riba
hauna pingamizi ndani ya Uislamu kwa kuwa
Qur’an imefafanuwa wazi wazi juu ya hukmu na
uharamu wa riba na mafunzo ya Mtume (Swalla
Allaahu alaiyh wa Sallam) yakasisitiza juu ya
uharamu wake huku wanazuoni wote

14
wakakubaliana kwa kauli moja kwa riba kwa upana
wake ni Haram.
Katika kueleza Hukmu za riba, tutatoa na
kubainisha makazo ya Riba kama yalivyokuja ndani
ya Qur’an tukufu huku tukifanya uchambuzi na
kutoa ufafanuzi juu ya ufahamu wa wafasiri mbali
mbali wa Qur’an juu ya kauli hizo. Aidha tutaelezea
makatazo na hukmu za riba kupitia Hadith sahihi za
Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam)
sambamba na kauli na fatawa mbali mbali za
wanachuoni juu ya miamala ya riba ili kila mmoja
wetu aweze kuifahamu hukmu na makatazo yake
na tunataraji kwa Allaah (Ta’ala) jamii itafaidika na
kuelimika juu ya haya yote tuliyo yakusanya.
Kwa ufupi Qur’an imeeleza vyema kuhusu riba na
imeizungumza takribani kwenye Surah nne (04)
kama ambavyo jeduali lifuatalo linavyo onyesha:

15
Hukmu na Makatazo ya Riba ndani ya Qur’an:
Allaah (Subhanahu) amesema ndani ya Qur’an:
i. Surat Al-Baqarah:
ُ ‫ط‬
‫ان‬ َ ‫ش ْي‬ ‫طهُ ٱل ﱠ‬ ُ ‫ٱلر َبا ﻻَ َيقُو ُمونَ ِإﻻﱠ َك َما َيقُو ُم ٱلﱠذِى يَت َ َخبﱠ‬ ّ ِ َ‫ٱلﱠذِينَ َيأ ْ ُك ُلون‬
ّ ِ ‫س ٰذلِكَ بِأَنﱠ ُه ْم قَالُ ۤواْ إِنﱠ َما ْٱلبَ ْي ُع ِمثْ ُل‬
‫ٱلربَا َوأ َ َح ﱠل ٱ ﱠ ُ ْٱلبَ ْي َع‬ ّ ِ ‫ِمنَ ْٱل َم‬
ُ‫ف َوأَ ْم ُره‬ َ َ‫ظةٌ ِ ّم ْن ﱠر ِبّ ِه فَٱ ْنت َ َه ٰى فَلَهُ َما َسل‬
َ ‫ٱلربَا فَ َمن َجآ َءهُ َم ْو ِع‬ ّ ِ ‫َو َح ﱠر َم‬
﴾٢٧٥﴿ َ‫ار ُه ْم فِي َها خَا ِلدُون‬ ِ ‫اب ٱلنﱠ‬ ُ ‫ص َح‬ ْ َ ‫ِإلَى ٱ ﱠ ِ َو َم ْن َعادَ فَأ ُ ْولَ ٰـئِكَ أ‬
“Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo
simama aliye zugwa na Shetwaan kwa kumgusa.
Hayo ni kwa kuwa wanasema: Biashara ni kama
Riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha
biashara na ameiharamisha riba. Basi aliye fikiwa
na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha
akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na
mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na
wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni,
humo watadumu.” (02:275)
Ufafanuzi:
Ukiangalia mtiririko wa aya hii ya katazo juu ya riba
umebeba hukmu, sababu na matokeo ya pande
mbili za viumbe ambao wanajihusisha na miamala
ya riba kisha Allaah akatoa bishara juu wale ambao
kupitia mawaidha na ujumbe unaopatikana ndani
yake juu ya matokeo ya watao jiepusha na wale
ambao watadharau na kupuuza maamrisho haya.

16
Hii ni miongoni mwa aya ambazo zinatoa hukmu na
kukataza moja kwa moja miamala yote ya riba na
Allaah (Subanahu) akatofautisha na kuvunja dhana
yao wakisema kwamba biashara ni kama riba, kwa
hakika Allaah (‘Azza wa Jalla) hafananishi baina ya
vitu viwili vyenye kutofautiana na wala hatofautishi
baina ya vitu ambavyo vinafanana.
Kwa kauli ya Allaah ‘hawasimami ila kama
anavyo simama aliye zugwa na Shetwaan’;
Ibn Kathir (Rehma za Allaah ziwe juu yake)
amesema; Aya hii inabainisha adhabu za wale
ambao wanajihusisha na miamala ya riba na Allaah
(Subhanahu) anafafanuwa hali za watu hao kuwa
watafufuliwa mbele ya Allaah wakiwa kama
wamepandwa na wazimu au wameingiwa na
shetani mbaya huku wakiwa wanatetemeka kwa
mfadhaiko kama alivyo mnukuu Ibn Abbas. Kisha
akanukuu Hadith ya Al-Bukhari aliyepokea kutoka
kwa Samurah bin Jundub alisema katika Hadith juu
ya ndoto ya Mtume kuwa; ((“…Basi tukaenda
tukafika kwenye mto – nadhania yeye alikuwa
akisema: “(mto huo) ni mwekundu mithili ya damu”
– tahamaki mtoni humo yumo mtu anaogelea. Na
tahamaki ukingoni mwa mto huo kuna mtu
amekusanya mawe mengi. Yule muogeleaji
ataogelea kiasi atakacho ogelea, kisha atamuendea
yule aliye kusanya mawe, atafungua mdomo, yule
(mwenye mawe) atamrushia jiwe. Ataondoka zake

17
akiogelea kisha atarudi (tena) kwake (yule mwenye
mawe) na kila akirudi hufungua mdomo wake, na
yule akamsokomeza jiwe.”)) Ibn Kathir akaeleza
kuwa yule mtu anayeogelea alikuwa ni mtu ambaye
akijihusisha na miamala ya riba. Kwa upande
mwengine, Imam Al-Kurtub (Rehma za Allaah ziwe
juu yake) amesema kwa kauli hii, Allaah
anakusudia kusimama kutoka katika makaburi yao
na akaegemea kauli ya Ibn Abbas, Mujahid na Ibn
Zayd kuwa Allaah atachagua miongoni mwa shetani
na kumpa amri ya kumzuga mtu huyo awe mwenda
wazimu na kumfanya achukiwe na kila kiumbe
katika kisimamo cha siku ya Kiyama.
Imam Al Kurtuby (Rehma za Allaah ziwe juu yake)
akaongeza pia; Aya hii inajumuisha hukmu za riba
pamoja na namna ambavyo Allaah (Ta’ala)
ameruhusu miamala mengine ya kibiashara. Na
Allah kupitia aya hii akatoa vitisho juu wale ambao
wanaifananisha riba na biashara na kuifanya kuwa
ni Halali na wakaendelea kushungulika nayo hata
baada ya kuwajia ubainifu. Aidha akaongeza kuwa
kwa kauli ya Allaah ‘wale walao riba’ ina maana
ya kujihusisha na miamala ya riba maana yake
kihalisi ni kula riba hiyo kwani hufaidika na mali
iliyochumwa kupitia miamala hiyo. Akaongeza pia
katazo la riba ndani ya aya hii halijafunga juu ya
kipato ndani ya mwamvuli wa riba tu bali kila kipato
ama utajiri unaopatika kupitia njia ambazo sio halali

18
zimeharamishwa na kutolewa hukmu yake juu ya
kauli hii ya Allaah (Subhanahu).
Kwa kauli ya Allaah (Ta’ala) ‘Hayo ni kwa kuwa
wanasema: Biashara ni kama Riba’: Al-Kurtub
(Rehma za Allaah ziwe juu yake amesema: ((Kauli
hii inawalenga wale wasiokuwa Waislam na
wanaelekezwa kuchukuwa kile walichopokea katika
kipindi cha nyuma (kabla ya katazo) na hili
haliwahusu wale wasiotwii amri miongoni mwa
walio amini kwani wao hupaswa kuacha na kuwa
mbali kabisa na miamala iliyoharamishwa ambayo
wakiifanya kabla ya kuharamishwa. Na hili kusema
kwamba biashara ni kama riba amesema kuwa kwa
sababu watu hao wanasema nyongeza ya kiasi juu
ya bei ya asili kinachopatikana na mkopeshaji
mwisho wa mkataba ni kwa sababu ya makubaliano
yao wakati wa mauziano au kukopeshana.
Allaah (Subhanahu) akasema; ‘Lakini Mwenyezi
Mungu ameihalalisha biashara na
ameiharamisha riba’: Ibn Kathir (Rehma za Allah
ziwe juu yake) amefafanua kauli kwa kusema hii ni
majibu ya Allaah kwa wale waifananishao riba na
biashara na kusema kwamba Allaah (Ta’ala) ni
mjuzi zaidi na mwenye hekima juu ya kila maamuzi
anayoyafanya kwa viumbe wake, hakika yenye
ndiye mwenye kujuwa lipi ni lenye manufaa kwa
viumbe wake (akaliruhusu) na lipi lina madhara

19
makubwa kwao naye akalikaza. Allaah ni mwenye
hekima na Rehema nyingi kwa viumbe wake zaidi
ya rehema na huruma za mama kwa kichanga
chake.
ii. Surat Al-Baqarah:
Allaah (‘Azza wa Jalla) ametoa hukmu ya riba pia
ndani ya Surah hii aliposema:

ٍ ‫ت َوٱ ﱠ ُ ﻻَ ي ُِحبﱡ ُك ﱠل َكفﱠ‬


‫ار‬ ‫يَ ْم َح ُق ٱ ﱠ ُ ْٱل ِ ّربَا َوي ُْر ِبى ٱل ﱠ‬
ِ ‫صدَقَا‬
﴾٢٧٦﴿‫أَثِ ٍيم‬
“Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na
huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi
kila mwenye kukana na afanyae dhambi.”
(02:276)
Ufafanuzi:
Kitendo ama amali yoyote ya mja ambayo huifanya
hapa duniani hutegemea moja kwa moja baraka za
Allaah (Subhanahu) ili iwe na manufaa kwake,
hivyo hivyo pato lolote ambalo kiumbe hulitafuta
kwa taabu na mihangaiko pia huhitaji kupata
baraka za Allaah ili pato lile liweze kunawiri na
kukidhi mahitaji yaliyokusudiwa, na pindi pato hilo
likinyimwa baraka haliwezi kufaa kwa chochote
wala kutosheleza. Wafasiri wa Qur’an
wameifafanua aya hii na kubainisha kwamba ni

20
miongoni mwa aya za hukmu za riba kama
ambavyo tunawanukuu kwenye ufafanuzi huu.
Imam Al-Kurtubi amesema kuwa, kwa kauli ya
Allaah (Subhanahu) ‘Mwenyezi Mungu
huiondolea baraka riba’ ina maana ya kwamba
huondoa baraka zote ndani ya kipato kutokana na
riba, hata kama kipato hicho kitakuwa kikubwa. Na
hili amelileta kutokana na nukuu ya Ibn Mas’ud
amesema; Mtume (Swalla Allahu alaiyh wa Sallam)
amesema: ((Hata kama kipato cha riba ni kikubwa
kiasi gani, huisha kikiwa kichache sana (au kama
alivyotamka Mtume wa Allaah) akimanisha
Akhera)). Al-Kurtubi amemnukuu Imam Ibn Abbas
kuwa amesema juu ya kauli hii; ((Sio sadaka, hija,
jihadi wala zawadi kwa ndugu zitakubaliwa mbele
ya Allaah zikiwa kipato chake kitatokamana na
riba.))
Ibn Kathir (Rehma za Allaah ziwe juu yake)
amefafanua kauli ya Allaah kuwa, kwa kusema
‘Huiondolea baraka riba’ inakusudiwa kuwa huenda
akawatia ufakiri kwa kuziondoa pesa zinazopatikana
kutokamana na riba ama akaondoa baraka na
kuzifanya zisiweze kumfaa kwa chochote. Aidha
akaongeza pia maana ya kauli hii ni kwamba
atawafanya wenye dhiki hapa duniani mbali na
utajiri wao na atawaadhibu adhabu kali huko

21
akhera na kauli hizi zote akazifunganisha na kauli
ya Allaah aliposema ndani ya Surat Ar-Rum;

ِ ‫َو َمآ آت َ ْيت ُ ْم ِ ّمن ِ ّربا ً ِلّ َي ْرب َُو ِفى أ َ ْم َوا ِل ٱلنﱠ‬
ِ ‫اس فَﻼَ َي ْربُو ِعندَ ٱ ﱠ‬
“Na mnacho kitoa kwa riba ili kiongezeke katika
mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi
Mungu.” (30:39)
‘Na huzibariki sadaka’ kuzibariki, kwa kauli ya
Imam Al-Kurtubi (Rehma za Allaah ziwe juu yake)
amesema kuwa Allaah, huziongezea baraka hapa
duniani na akazipa malipo ya juu huko Akhera.
Akasema pia katika Sahihi Muslim imesemwa
kwamba ‘Mtu anapotoa sadaka, Allaah huziongeza
na kuwa kubwa hata kama ni chembe moja ya
chakula, kama vile mmoja wenu anavyo mkuza
mnyama wake hadi kufikia urefu wa Mlima Uhud.’
Kisha baada ya kauli hizi Allah akamalizia aya hii
kwa kusema ‘Na Mwenyezi Mungu hampendi
kila mwenye kukana na afanyae dhambi’ Ibn
Kathir amefafanua kuwa huu ni uwiyano juu ya
namna aya hii ilivyoanza kuhusu riba na ilivyoishia,
na kusema kwamba uwiyano huu umetokana kuwa
wale wanao kula riba ni kuwa hawatosheki na yale
ambayo Allaah (Subhanahu) amewahalalishia waja
wake. Na badala yake wanajaribu kuchukuwa mali
za wengine wanyonge kwa dhulma huku wakitumia
njia chafu. Na hili linadhihirisha ukosefu wao wa

22
shukurani kwa neema ambazo Allaah (‘Azza wa
Jalla) amewaruzuku na kuwaneemeshea.
iii. Surat A’al-Imran
Allaah (Subahanahu) aidha amekemea Riba na
kubainisha hukmu zake ndani ya Surah hii kama
ambavyo aya ya 130 inafafanuwa kauli ya Allah
(Ta’ala);

َ ‫عفَةً َوٱتﱠقُواْ ٱ ﱠ‬ َ ‫ض َعافا ً ﱡم‬


َ ‫ضا‬ ّ ِ ْ‫يَآ أَيﱡ َها ٱلﱠذِينَ آ َمنُواْ ﻻَ ت َأ ْ ُكلُوا‬
ْ َ ‫ٱلربَا أ‬
﴾١٣٠﴿ َ‫لَ َعلﱠ ُك ْم ت ُ ْف ِل ُحون‬
“Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu,
na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa”.
(03:130)
Ufafanuzi:
Katika kuifafanua aya hii ya Allaah (Subhanahu), Al-
Kurtubi (Rehma za Allaah ziwe juu yake) amesema
kuwa kauli hii ni katazo juu ya kujihusisha na
miamala ya riba na akaifunganisha na habari ya
Uhud akimnukuu Mujahid kuwa amesema: ((Wakati
wa ujahilia waarab wakiuziana kwa mkopo na
wakati wa muda unapoisha, wakiongeza bei ya
bidhaa kwa sababu ya kucheleweshwa kwa malipo
na ndiyo Allaah aliteremsha aya hii kuwakataza
kuzidisha juu ya bei ya asili juu kwa juu.)) Al-
Kurtubi ameongeza pia riba imefafanuliwa kuwa ni
vitendo vya waovu kwa sababu inaenda kinyume

23
na maakatazo ya Allaah (Subhanahu) na ndiyo
maana akatangaza vita dhidi yao kama
alivyobainisha ndani ya Surat Baqarah akiwa anatoa
katazo juu ya kuacha kila kilichobaki katika riba
kuwa:

ُ ‫سو ِل ِه َوإِ ْن ت ُ ْبت ُ ْم فَلَ ُك ْم ُر ُؤ‬


‫وس‬ ٍ ‫فَإِن لﱠ ْم ت َ ْف َعلُواْ فَأْذَنُواْ ِب َح ْر‬
ُ ‫ب ِ ّمنَ ٱ ﱠ ِ َو َر‬
﴾٢٧٩﴿ َ‫ظلَ ُمون‬ ْ ُ ‫أ َ ْم َوا ِل ُك ْم ﻻَ ت َْظ ِل ُمونَ َوﻻَ ت‬
“Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi
Mungu na Mtume wake. Na mkitubu basi haki yenu
ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe”.
(02:279)
Al-Kurtubi akaendelea kusema ni kawaida na
inaruhusiwa kuuwa ndani ya vita, hivyo kwa kauli
hii, Allaah ni kama anasema kama hamtaacha na
kuogopa juu ya kuendelea kula riba, basi mtapigwa
vita na mtauliwa. Na Allaah ni mjuzi zaidi. Kisha
akamalizia ufafanuzi wake kwa kusema kuwa,
kuhusu kauli ya Allaah, ‘Mcheni Mwenyezi
Mungu ili mpate kufanikiwa’ inamaanisha kila
kiumbe anapaswa kumuogopa Allaah (Subhanahu)
juu ya kila kipato anachokipata kutokamana na riba
na aache kabisa kula chochote ndani ya kipato
hicho.

24
iv. Surat An-Nisa’
Hukmu za riba hakika zimeenea ndani ya Qur’an
kwa makatazo makali na yenye uzito mkubwa,
huku Allah (‘Azza wa Jalla) akiyafungamanisha na
matokeo mabaya mbele yake. Kupitia aya nyingi
ambazo Allaah (subhanahu) amekataza na
kukemea riba ameshikanisha matokeo ya adhabu
yenye kudhalilisha ndani yake. Baadhi za Riwaya
zinasema kwamba walao riba watakusanywa siku
ya Kiyama huku wakiwa matumbo yao yamefura
mno, na wakasema kwamba ndani yake kutakuwa
na fukuto la moto, na wapo waliosema (kama
tulivyonukuu Hadith ya ndoto ya Mtume wa Allaah)
kuwa watakuwa wakimezeshwa mawe huku
wakiwa wanaogelea ndani ya ziwa la damu,
kadhalika zipo dalili zikionesha kuwa walao riba
watakusanywa mbele ya Allaah (Ta’ala) wakiwa
kana kwamba wamepandwa na kichaa, kichaa hiki
wakasema kuwa ni kwa sababu walikula riba
wakiwa wanazipoteza akili zao kwa kudharau
makatazo ya Allaah na kujisahaulisha. Kupitia Surah
hii pia Allaah (‘Azza wa Jalla) anaeleza hukmu za
riba huku akifafanuwa namna ya idhlali ya adhabu
ambayo watakuwa nayo watu hao.

25
Allaah anasema ndani ya Surat An-Nisa’;

‫اط ِل َوأ َ ْعتَ ْدنَا‬


ِ َ‫اس بِ ْٱلب‬
ِ ‫ٱلربَا َوقَ ْد نُ ُهواْ َع ْنهُ َوأَ ْك ِل ِه ْم أ َ ْم َوا َل ٱلنﱠ‬
ّ ِ ‫َوأ َ ْخ ِذ ِه ُم‬
﴾١٦١﴿ً ‫ِل ْل َكافِ ِرينَ ِم ْن ُه ْم َعذَابا ً أَ ِليما‬
“Na kuchukuwa kwao riba, nao wamekatazwa, na
kula kwao mali ya watu kwa dhulma. Basi
tumewaandalia makafiri katika wao adhabu yenye
uchungu.” (04:161)
Ufafanuzi:
Ibn Kathir (Rehma za Allaah ziwe juu yake)
amefafanuwa aya hii ya Allaah akisema; Allaah
(Ta’ala) amekataza kula riba, na bado wanaendelea
kula na kutoza kwa mbinu mbali mbali na hadaa
huku wakichukuwa na kujimilikisha mali ya watu
wengine kwa dhulma. Dhulma hapa ni kuwa
mikataba na makubaliano wanayoyafanya baina ya
hao wahitaji ni yenye usiri mkubwa huku undani wa
dhulma zao wakizijua wao tu, na dhamira zao
zikiwa wamezificha.
Hili tunalishuhudia katika nyakati zetu, walio wengi
miongoni mwa matajiri wanaotumia mlango wa
kuwasaidia wanyonge kwa mikopo wakifanya
hadaa na mbinu mbali mbali za kuhakikisha
wanachukuwa mali za wengine kwa dhulma kama
vile nyumba, magari, viwanja na mali nyengine kwa
sababu tu walishindwa kulipa madeni yao kwa

26
wakati, taarifu za kijamii zinatueleza kuwa kuna
baadhi yao wanakopesha huku wakichukuwa hati
za nyumba ama viwanja kama dhamana kisha
wakiwakimbia wadeni wao katika siku ya malipo ili
tu iwe sababu ya kuchelewa kulipa na kujimilikisha
mali zile zilizowekewa dhamana. Basi kama ni hivi
tujiandae na adhabu yenye uchungu ambayo
itadhuru miili yetu na nafsi zetu daima, dawamu.
Hili linadhihiri kwa kuogopesha sana, tumezifunga
nyoyo zetu juu ya kuzingatia maamrisho ya Allaah,
tumeziba masikio yetu katika kuisikia Haki,
tumezilaza akili zetu zisiamke katika kujikemea
katika kuendea kula riba. Tumeshau maelekezo ya
namna Allaah alivyobainisha namna ya kufanya
muamala na wale wanaopitia kipindi kigumu cha
malipo ya madeni waliyokopa. kwa kauli ya Allaah
(Ta’ala) ndani ya Qur’an alisposema:

‫صدﱠقُواْ َخي ٌْر لﱠ ُك ْم ِإن‬


َ َ‫س َرةٍ َوأَن ت‬ ُ ‫َوإِن َكانَ ذُو‬
َ ‫عس َْرةٍ فَن َِظ َرة ٌ ِإلَ ٰى َم ْي‬
﴾٢٨٠﴿ َ‫ُك ْنت ُ ْم ت َ ْعلَ ُمون‬
“Na ikiwa (Mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi
(mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkifanya deni
kuwa ni swadaqah basi ni kheyri kwenu mkiwa
mnajua” (02:280)
Je! Makatazo haya ya Allaah (Subhanahu)
tumeyaweka nafasi gani, kwanini kila uchwao
tunaona na kusikia vilio vya wale waliofilisiwa kwa

27
madeni yaliyobebeshwa mzigo wa riba, ni kwamba
nafsi zetu hazitosheki na makatazo ya Allaah (‘Azza
wa Jalla) na Mtume wake kupitia Qur’an? Je! Mioyo
yetu imekuwa sugu hadi kukataa amri za Muumba
wetu kwa Kibri na jeuri ya kuvuka mipaka? Basi
tujiandae na adhabu chungu yenye kudhalilisha. Na
hizi ni aya ambazo Allaah (Ta’ala) ameitaja riba
moja kwa moja ukiacha zile ambazo ameficha kauli
zake kwa kutumia neno Haramu kama ambavyo
amesema Allaah (Subhanahu) ndani ya Surat Al-
Mai’dah:

َ‫ان َوأَ ْك ِل ِه ُم ٱلسﱡحْ ت‬


ِ ‫ٱﻹثْ ِم َو ْٱلعُد َْو‬ ِ ‫َوت ََر ٰى َكثِيرا ً ِ ّم ْن ُه ْم يُ َس‬
ِ ‫ارعُونَ فِى‬
﴾٦٢﴿ َ‫س َما َكانُواْ يَ ْع َملُون‬ َ ْ‫لَبِئ‬
“Na utawaona wengi miongoni mwao wanakimbilia
katika dhambi na uadui na kula kwao haramu. Bila
shaka mabaya mno waliyokuwa wanatenda”
(05:62)
Allaah (Subhanahu) amesema pia:

َ‫ٱﻹثْ َم َوأَ ْك ِل ِه ُم ٱلسﱡحْ ت‬


ِ ‫عن قَ ْو ِل ِه ُم‬ ُ َ‫ٱلربﱠانِيﱡونَ َوٱﻷَحْ ب‬
َ ‫ار‬ ‫لَ ْوﻻَ يَ ْن َها ُه ُم ﱠ‬
﴾٦٣﴿ َ‫صنَعُون‬ ْ َ‫س َما َكانُواْ ي‬ َ ْ‫لَبِئ‬
“Mbona hawawakatazi wanachuoni waswalihina na
wanachuoni mafuqahaa wa dini kuhusu kauli zao za
dhambi na ulaji wao wa haramu. Bila shaka
mabaya mno waliyokuwa wanatimiliza.” (05:63)

28
Wafasiri wa Qur’an wanasema kuwa kauli ya Allaah
juu ya kula haramu katika aya hizi zinamaanisha ni
riba na rushwa ambazo zote zimekusanywa kwenye
ulaji wa haramu ikiwa na maana ya kichumo
kinachopatika kutokamana na riba na rushwa na hii
ndio kauli yenye nguvu katika tafsiri ya aya hizi.
Tumuombe Allaah (Subahanahu wa Ta’ala)
aisafishe jamii yetu juu ya dhulma hizi na atukinge
na kutuonyesha njia iliyo ya sawa kuiendea ili
tuepukane adhabu na ghadhabu zake.
Hukmu za Riba ndani ya Hadith:
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Rehma
za Allaah ziwe juu yake) kwamba Mtume (Swalla
Allaahu Alaiyh wa Sallam) amesema: ((Jiepusheni
na mambo saba yanayoangamiza!)) Wakauliza: Ni
yepi hayo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Ni
kumshirikisha Allaah, sihri [uchawi], kuua nafsi
Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula
ribaa, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa
kupambana na adui na kuwatuhumu uzinifu
wanawake Waumini waliohifadhika
walioghafilika)). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Msingi mkubwa wa kuileta na kuanza kwa Hadith
ya Mtume wa Allaah, ni kubainisha juu ya makatazo
makali ambayo Nabii wa Allaah ameyawacha juu ya
kujikinga na mambo haya saba na kwa kauli yake
kama alivyoyaita kuwa ni yenye kuangamiza, na

29
maangamizo haya ni kwa pande zote (Duniani na
Akhera). Katika mtiririko wa Hadith hii, Imam Bin
Baaz amesema kuwa dhambi hizi zinauzito kwa
kadiri ambavyo Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa
Sallam) alivyozitaja na ameanza kwa kutaja shirki
(ambayo tutaifanunua katika kitabu kijacho) kisha
akaendelea na kuitaja Riba ikiwa ni dhambi kubwa
yenye daraja la nne katika dhambi hizo saba.
Katika Hadith iliyopokelewa na Imam Muslim na
Imam Ahmad (Radhi za Allaah ziwe juu yao wote),
Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam)
amesema: ((Allaah amemlaani mla riba, mlisha
riba, mashahidi wake na muandishi wake, wao
wote katika madhambi ni sawa sawa.)) na
amesema pia Mtume wa Allaah: ((Dirham moja ya
riba anayo ila mtu ilihali akijua, (dhambi zake) ni
kubwa mno mbele ya Allaah kuliko zinaa thelathini
na sita.)) Imam Ahmad na Twabaraaniy (Rehma za
Allah ziwe juu yao wote)
Katika kuendelea kutoa mafunzo juu ya hukmu za
riba, Mtume (Swallah Allaahu alaiyh wa Sallam)
amesema: ((Riba ina milango sabini na mbili, wa
chini yake (madhambi yake) ni kama mtu kulala na
mama yake mzazi. Na hakika riba kubwa kuliko
zote, ni mtu kufanya uadui katika heshima ya
ndugu yake.)) Twabaraaniy (Rehma za Allaah ziwe
juu yake)

30
Riba katika jamii yetu imetangamaa kwa kiasi
kikubwa huku wahusika wote wakiwa na nafasi
kubwa katika jamii na wakiisanifu kwa mbinu na
majina tofauti, huku jamii wakiikimbilia bila kujali
uzito na matokeo yake, na hili linadhihirisha kuwa
uoza wa jamii yetu ni mkubwa, hivyo basi tujiandae
na adhabu ya Allaah kutokea pande zote. Na hili
linathibitishwa na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu
alaiyh wa Sallam) aliposema: ((Itakapo dhihiri zinaa
na riba katika kitongoji, hakika bila ya shaka (watu
wa kitongoji hicho) wamekwisha jihalalisha adhabu
ya Allaah.)) Twabaraaniy.
Miamala ya riba imekuwa katika jamii tangu zama
za zamani na hili linadhihiri katika Hadith ya Mtume
(Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam) katika Hijja yake
ya kuaga katika Hadith ya Rabii al-Muraad akisema
(kutoka kwa Jaabir (Radhi za Allaah ziwe juu yake)
kwamba Mtume wa Allaah amesema siku ya Arafa:
((Riba za jahiliya zimeporomoshwa. Na riba ya
mwanzo ninayoondoa ni ya Mjomba wangu Al-
Abbas bin Abdil Mutwalib, kwa hakika imeondoshwa
yote.)) ama katika riwaya nyengine zinasema kuwa
amesema Amr bin Ahwasy: nilimsikia Mtume wa
Mwenyezi Mungu akisema: ((Jueni na mtambue,
hakika kila riba katika riba za jahiliya
zimeondoshwa, zenu ni rasilimali, msidhulumu na
hamtodhulumiwa.))

31
Kwa mujibu wa wanachuoni wa Hadith
wamebainisha kuwa riba kwenye mauzo hupatikana
isipokuwa kwenye vitu sita ambavyo amevieleza
Mtume (Swalla Allaahu alayih wa Sallam) ama
kwenye mikopo riba imetangaa kwenye miamala
mingi, kwa msingi huu wakasema si halali
kukopesha kitu chochote ili urudishiwe kingi zaidi
badala yake urudushiwe mfano wa ulichokopesha.
Hili lina athari kupitia Hadith ya Imam Muslim
kutoka kwa Ubadah ibn Swamit kuwa Mtume
(Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam) amesema:
((Dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha,
Shairi kwa shairi, na ngano kwa ngano, na tende
kwa tende, na chumvi kwa chumvi, zibadilishwe
sawa kwa sawa, mkono kwa mkono, na hizi aina
zikitofautiana basi uzeni mtakavyo itakapokuwa ni
mkono kwa mkono.))
Na katika riwaya nyengine, amepokea Abu Dawud
katika Sunani yake kutoka kwa Ubaada Ibn Swamit
kwamba Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam)
amesema: ((Dhahabu kwa dhahabu: ambayo
haijatengenezwa na ilio tengenezwa (dinar), na
fedha kwa fedha: ambayo haijatengenezwa na ilo
tengenezwa, na shairi kwa shairi: kipimo kwa
kipimo (sawa sawa), ngano kwa ngano: kipimo kwa
kipimo (sawa sawa), na tende kwa tende: kipimo
kwa kipimo (sawa sawa), na chumvi kwa chumvi:
kipimo kwa kipimo (sawa sawa) na yeyote

32
atakayezidisha au kutaka ziada basi atakuwa hakika
amefanya riba. Na hapana neno kuuza dhahabu
kwa fedha na fedha ikawa nyingi zaidi, iwe ni
mkono kwa mkono. Ama kwa kuchelewa: hapana,
na hapana neno kuuza shairi kwa mawele na
mawele yakawa mengi zaidi, iwe mkono kwa
mkono: ama kuchelewesha: hapana.”))
Riba imeenea sana ndani ya jamii na madhara
makubwa imekuwa ikileta katika maisha ya
wanadamu na hili limethibiti katika Hadith ambayo
Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam) amesema
kuwa, Kuna zama zitawafikia watu, wakati ambao
hakutakuwa na yeyote ambaye atasalimika na kula
Riba, na kama atakuwepo aliyesalimika basi hata
vumbi lake litamkumba. (Rejea Hadith hii katika
Sunan Abu Dawud) jamii inapaswa kuelimika juu ya
janga hili kupitia Hadith za Mtume (Swalla Allaahu
alayih wa Sallam) ambayo ni maneno ya haki, ni lipi
lengine litatukanya zaidi ya Qur’an tukufu na kauli
hizi za Mtume wa Allaah, ambazo hazitokani na
chochote isipokuwa kwa Wahy na miongozo kutoka
Mola Mlezi wa viumbe vyote. Athari za jambo hili
zipo wazi kwa jamii na kila mmoja wetu ni
muathirika kwa namna moja ama nyengine hivyo
kila mtu aliyefikiwa na ukumbusho huu hana budi,
kuacha na kukatazika juu ya kujihusisha na
miamala yote yenye hata chembe ya Riba.

33
FATAWA ZA WANAZUONI JUU YA MIAMALA
YA RIBA NA SURA ZAKE
Tumekwisha tanguliza hukmu za riba na makatzo
yake ndani ya Qur’an tukufu huku tukifanya
uchambuzi na kutoa fafanuzi mbali mbali za
wanazuoni wafasiri wa Qur’an ikiwa ni katika
kuzibanisha hukmu hizo ziwe wazi zaidi, kisha
tukafanya nukuu mbali mbali za maneno matukufu
ya Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam) ili
tuweze kubainisha zaidi makatazo ya dhambi ya
riba kwa jamii. Kwa hatua hii ni dhahiri sasa
tunaelewa kwa kiasi kwanini haswa Allaah
(Subhanahu) na Mtume wake wameiharmisha na
kuikemea Riba kwa aina zake na kila sura zake.
Wanazuoni mbali mbali kwa nafasi zao pia
wametoa Fatawa na fafanuzi nyingi juu ya miamala
ndani ya jamii zao huku wakitumia ushahidi wa
Qur’an na Sunnah katika kuweka misimamo yao juu
ya kadhia nyingi walizokutana nazo ama kuulizwa.
Sehemu hii Insha’Allah tunakusudia kuleta nukuu
ya baadhi ya Fatawa zao juu ya Riba na miamala
mingi na hukmu zake ndani ya jamii. Lengo kuu
likiwa ni kuhakikisha tunaifahamisha jamii husika
juu ya madhara na uharamu wa Riba huku
tukibainisha namna na sura mbali mbali za riba
katika nyakati zao na zetu. Si katika malengo
kumkwaza wala kumgusa yeyote katika jamii bali ni
kufikisha kwa kadiri Allaah (Subhanahu)

34
alivyoturuzuku katika mapitio na makusanyo ya
kitabu hichi. Namuomba Allaah (Subahanahu) awe
shahid kwa huku kufisha na lengo la mafundisho
haya kufika ndani ya nyoyo za wahusika bila ya
chuki wala lawama.
Ufafanuzi wa Fatawa hizi utakuwa na sura kuu
mbili, kwanza tutabainisha majibu ya wanazuoni
mbali mbali juu ya maswala ambayo yanahusu
miamla ambayo inajumuisha riba ndani yake na
kwa kauli zao wakatoa uchambuzi juu ya uharamu
wake, pia tutanukuu aina ya fatawa ambazo
zilitolewa kwa ile miamala ambayo haijumuishi riba
na kwa kauli zao wakafafanuwa kuwa inaruhusiwa
na shariah. Majumuisho ya Fatawa hizi
tumeyanukuu kutoka katika Kitabu cha ‘Fatawa
Islamiyah’ mjaladi wa tatu (Volume 3) katika
mlango wa ‘Miamala ya Mauziano’ ambacho
kimejumuisha Fatawa za wanazuoni mashughuri wa
fiqihi ya Kiislam; ‘Shaykh Abdul Aziz bin Abdullah
bin Baz’, ‘Shaykh Muhammad bin Salih Al-Uthaimin’,
‘Shaykh Abdullah bin Abdur-Rahman Al-Jibreen’
wakishirikiana kwa pamoja na ‘Jopo la Kamati ya
Kudumu na maamuzi ya Kifiqihi’
i. Katika kutoka ufafanuzi huu, kwa kuanzia
tunaangalie Swali lilioulizwa mbele ya
kamati hii juu ya mtoto kutumia mali za

35
baba yake ambazo zilichumwa kwa
miamala ya riba;
Swali:
Je! Inaruhusiwa mtoto kutumia sehemu ya mali za
baba yake ambazo zilichumwa kwa njia za kula
riba?
Jawabu:
Riba imeharamishwa kwa mujibu wa Qur’an,
Sunnah (Hadith) pamoja na makubaliano ya
wanazuoni (Ijma’). Ikiwa baba yako amechuma
mali hizo kwa miamala ya riba, ni wajibu kwako
kumuelimisha juu ya Riba, Hukmu zake na yale
ambayo Allaah (Subhanahu) ameyandaa (Akhera)
kwa ajili ya walao riba. Hairuhusiwi kwako
kuchukuwa katika mali za baba yako alizozipata
kupitia kula riba huku ukiwa unajuwa kwamba
ndani yake kuna mali za riba. Unapaswa
kutegemea riziki kutoka kwa Allaah (Subahanahu)
na kutumia njia ambazo Allaah ameziruhusu
kujipatia riziki. Kwani Allaah (Subhanahu)
amesema:

ُ ‫﴾ َو َي ْر ُز ْقهُ ِم ْن َحي‬٢﴿ً ‫ق ٱ ﱠ َ َيجْ َعل لﱠهُ َم ْخ َرجا‬


َ‫ْث ﻻ‬ ِ ‫َو َمن َيت ﱠ‬
﴾٣﴿‫ِب‬ ُ ‫يَحْ تَس‬

36
“Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea
njia ya kutokea. Na humruzuku kwa jiha asiyo
tazamia” (65:02-03)
Allaah (Ta’ala) amesema pia:

﴾٤﴿ً ‫ق ٱ ﱠ َ يَجْ َعل لﱠهُ ِم ْن أ َ ْم ِر ِه يُ ْسرا‬


ِ ‫َو َمن يَت ﱠ‬
“Na anaye mcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi
Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi”
(65:04)
[Jawabu hili lilitolewa na Jopo la Kamati ya Kudumu
ya Fiqihi na Maamuzi]
ii. Fatawa ya pili ni juu ya suali kuhusu
miamala ya mtu na Benki za Riba kama
lilivyoulizwa:
Swali:
Je! Ni ipi hukmu za Kiislamu juu mambo yafuatayo;
 Mtu ambaye anaweka fedha zake ndani ya
benki kisha zikakaa huko kwa mwaka na
kuzidishiwa kiasi cha riba kwa kuziweka
kwake?
 Mtu ambaye amechukuwa mkopo benki ili
aje kulipa baadae na ziada ya riba?
 Mtu ambaye ameweka (dipositi) ndani ya
benki ila hapati wala kuchukuwa chochote
kilichozidi katika riba?

37
 Mfanyakazi wa benki wa ngazi na cheo
chochote?
 Mmiliki wa majumba mwenye kupangisha
nyumba yake kwa taasisi za benki?
Jawabu:
Akajibu swali hili, As-Shaykh Ibn Baz (Rehma za
Allaah ziwe juu yake) kuwa; Hairuhusiwi kuweka
fedha ndani ya benki ili upate ziada ya riba ama
kuchukuwa mkopo wenye makubaliano ya riba. Hii
ni kwasababu yote hayo ni miamala ndani ya
miamala ya riba. Hivyo hivyo hairuhusiwi kuweka
fedha popote pasipokuwa benki kukiwa kuna
makubaliano ya kupata ziada ya riba, kama
ambavyo hairuhusiwi kuchukuwa mkopo wenye
makubaliano ya riba kwani haya yameharamishwa
kwa kauli za wanavyuoni wote. Na hii ni kwasababu
Allaah (Ta’ala) anasema:

﴾٢٧٥﴿ ‫ٱلربَا‬
ّ ِ ‫َوأ َ َح ﱠل ٱ ﱠ ُ ْٱلبَ ْي َع َو َح ﱠر َم‬
“Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na
ameiharamisha riba” (02:275)
Na Allaah (Subahanahu) amesema aidha:

﴾٢٧٦﴿ ‫ت‬ ‫يَ ْم َح ُق ٱ ﱠ ُ ْٱل ِ ّربَا َوي ُْربِى ٱل ﱠ‬


ِ ‫صدَقَا‬
“Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na
huzibariki sadaka” (02:276)

38
Na Allaah amesema:

َ‫ٱلربَا إِن ُك ْنت ُ ْم ﱡمؤْ ِمنِين‬ ّ ِ َ‫ى ِمن‬ َ ‫ٰيأَيﱡ َها ٱلﱠذِينَ آ َمنُواْ ٱتﱠقُواْ ٱ ﱠ َ َوذ َ ُرواْ َما بَ ِق‬
‫سو ِل ِه َوإِ ْن ت ُ ْبت ُ ْم فَلَ ُك ْم‬ ٍ ‫﴾ فَإِن لﱠ ْم ت َ ْفعَلُواْ فَأْذَنُواْ بِ َح ْر‬٢٧٨﴿
ُ ‫ب ِ ّمنَ ٱ ﱠ ِ َو َر‬
﴾٢٧٩﴿ َ‫ظلَ ُمون‬ ْ ُ ‫وس أ َ ْم َوا ِل ُك ْم ﻻَ ت َْظ ِل ُمونَ َوﻻَ ت‬
ُ ُ‫ُرؤ‬
“Enyi mlio amini, mcheni Mwenyezi Mungu, na
acheni riba zilizo bakia ikiwa nyinyi ni Waumini. Na
mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na
Mtume wake. Na mkitubu basi haki yenu ni
rasilimali zenu. Msidhulumu (kwa kudai ziada ya
mali yenu) wala msidhulumiwe (kwa kupokea
pungufu ya mlicho kitoa)” (02:278-279)
Na baada ya hayo yote Allaah akasema tena:

﴾٢٨٠﴿ ٍ‫س َرة‬ ُ ‫َوإِن َكانَ ذُو‬


َ ‫عس َْرةٍ فَن َِظ َرة ٌ ِإلَ ٰى َم ْي‬
“Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje
mpaka afarijike” (02:280)
As-Shaykh Ibn Baz (Rehma za Allaah ziwe juu
yake) akaendelea kufafanua kuwa, Allaah
ameyaeleza haya kwa waja wake kwa sababu
hairuhusiwi kudai mtu akiwa katika kipindi kigumu
kulipa kile anacho daiwa (akiwa hana namna ya
kulipa) na wala hairuhusiwi kumuongezea mzigo
juu ya kile anacho daiwa hadi atakapo kuwa sawa
katika hali yake, na hi imetokana na huruma za
Allaah (Subhanahu) kwa waja wake, ni kwa hekima

39
zake na kuwalinda juu ya udhalimu wa
wanaodhulumu kwani dhulma haitawafaa chochote.
Na katika kuweka fedha kwenye benki pasi na
kupata chochote cha ziada kutokamana na riba, hili
halina tatizo lolote ikiwa tu Muislamu amewiwa
kufanya (kuweka pesa huko). Na kuhusu kufanya
kazi kwenye benki ambayo inafanya miamala ya
riba, hili haliruhusiwi, bila ya kujali cheo chake wala
nafasi yake anaweza kuwa ni meneja, karani,
muhasibu au nafasi nyengine yoyote. Na hii ni kwa
mujibu wa kauli ya Allaah;

ِ ‫علَى ْٱلب ِ ّر َوٱلت ﱠ ْق َو ٰى َوﻻَ تَعَ َاونُواْ َعلَى ٱ ِﻹثْ ِم َو ْٱلعُد َْو‬
‫ان‬ َ ْ‫َوتَعَ َاونُوا‬
﴾٢﴿ ‫ب‬ ِ ‫َوٱتﱠقُواْ ٱ ﱠ َ إِ ﱠن ٱ ﱠ َ َشدِيد ُ ْآل ِعقَا‬
“Na saidianeni katika wema na uchamungu. Wala
msisaidiane katik dhambi na uadui. Na mcheni
Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali
wa kuadhibu” (05:02)
Jambo hili limethibiti katika Hadith ya Mtume
(Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam) kuwa amemlaani
mtu anae kula riba, mtu anae lisha riba, na anae
iandika na shahidi na akasema wote ni sawa (katika
dhambi). [Hadith hii imesahihishwa na Imam
Muslim (Radhi za Allaah ziwe juu yake)]

40
Hivyo basi, Aya na Hadith kama hizi zipo nyingi
ambazo zinathibitisha uharamu wa kusaidia katika
matendo yote yaliyo haramishwa. Vivyo hivyo,
kupangisha nyumba ama jengo kwa taasisi ya benki
inayojihusisha na riba, hairuhusiwi kwa mujibu wa
ushahidi nilioeleza. Na hili ni kwasababu linasaidia
katika kuwezesha miamala ya riba. Tunamuomba
Allaah (Subhanahu) awabariki wote (wanaotoa
hukmu na waulizaji) katika njia ya uongofu na
kuendelea kupiga vita masuala ya riba, kwa
kuikimbia na kujitosheleza na yale ambayo Allaah
na Mtume wake ametuhalalishia kuwa ni miamala
halali, bila shaka yeye ndiye Mwenye nguvu na
hayo yote. [As-Shaykh Ibn Baz]
iii. Fatawa juu ya swali lililoulizwa kuhusu
walimu au kikundi cha watu
kuchangishana pesa kila mwisho wa
mwezi na kumpa mmoja wao kila mwezi.
Aliulizwa Ash-Shaykh Ibn Baz (Rehma za Allaah
ziwe juu yake) “Kikundi cha Walimu hukusanya
kiasi cha fedha kila mwisho wa mwezi kutoka katika
mishahara yao, na kumpa mmoja wao. Kisha mwezi
unaofata akapewa mwengine na mwengine hadi
wote wakafikiwa na mzunguko ule (wengine huita
upatu) Je! Ni ipi hukmu yake ndani Uislamu?”

41
Jawabu:
Amejibu As-Sheikh Ibn Baz (Rehma za Allaah ziwe
juu yake) kuwa; Sioni ubaya katika hilo. Ni mkopo
ambao hauna athari zozote kwa mmoja wao
kufaidika zaidi juu ya kile alichokopesha awali.
Wanazuoni wameliangalia hili na wameona na
kuamua (walio wengi) kuwa linaruhusiwa kwa vile
ni muamala unaowafaidisha wote na hakuna
madhara yoyote kwa mmoja wao. Na Allaah ndiyo
mtoaji wa mafanikio. [As-Shaykh Ibn Baz]
iv. Fatawa juu ya swali kuhusu mikopo
yenye kumpa faida mwenye kukopesha.
Aliulizwa Ibn Uthaimin (Rehma za Allaah ziwe juu
yake) “Kuna mtu alikopa pesa kutoka kwa
mwenzake lakini mkopeshaji aliweka sharti kwamba
atachukuwa sehemu ya ardhi ya mkopeshwaji iwe
kama dhamana ya kiasi cha fedha alizokopa. Kisha
mkopeshaji akaanza kutumia ile sehemu ya ardhi
kwa kilimo hadi ikafikia katika hatua ya mavuno
karibia nusu ya shamba na kabakisha sehemu
(nusu) au zaidi kwa mwenye eneo lake hadi pale
atakapo kamilisha malipo ya mkopo wake. Ulipofika
wakati ambao mkopeshaji anatakiwa kurejesha lile
shamba kwa mmiliki wa awali, takribani shamba
lote lilikuwa chini ya umiliki wa mkopeshaji (kwa
kilimo) ni ipi hukmu ya muamala huu kwa mtazamo
wako?”

42
Jawabu:
Bila shaka, muamala wa mkopo huo ni miongoni
mwa mikataba ya ukarimu ambao una lengo la
ukarimu kwa mkopaji. Na umetokana na jambo
ambalo linapendeza mbele ya Allaah, kwa sababu
ni kitendo cha ukarimu kwa mja wa Allaah
(Subahanahu) ambaye amesema;

﴾١٩٥﴿ َ‫َوأَحْ ِسنُ ۤواْ إِ ﱠن ٱ ﱠ َ ي ُِحبﱡ ْٱل ُمحْ ِسنِين‬


“Na fanyeni wema. Hakika Mwenyei Mungu
huwapenda wafanyao wema” (02:195)
Hivyo mkopeshaji anapaswa na kuwajibika kufanya
wema kwa mkopaji. Na kwa mkopaji anaruhusiwa
na inapendeza. Kwa hakika imethibitishwa kuwa
Mtume (Swalla Allahu alaiuh wa Sallam) aliazima
ngamia mdogo kutoka kwa mtu na akamrejeshea
mwengine aliyekuwa bora zaidi ya yule (aliye
azima). Hivyo kwa sababu muamala huu ni wa
ukarimu, hairuhusiwi kuubadilisha kuenda kwenye
muamala wa kulipana kwa kila juhudi na faida za
ziada. Ninaposema faida, namaanisha faida yenye
thamani kubwa na hivyo kitendo cha kupata faida
kubwa ya ziada hubadilisha maudhui ya muamala.
Kwa kuyazingatia hayo yote, hakika kwenye swali
hili mkopeshaji alitoa sharti la faida ya ziada kutoka
kwa mkopaji, na ameuondoa mkopo huo kutoka

43
katika muamala wa ukarimu na huruma, hivyo basi
muamala huu umeharamishwa.
Kwani kanuni mashughuri ya wanazuoni ni kuwa
mkopo wowote ambao huleta faida ya ziada (kwa
Mkopeshaji) ni muamala wa Riba na hauruhusiwi
ndani ya shariah ya Uislamu. Hairuhusiwi
mkopeshaji kuweka sharti kwa mkopaji kuwa ampe
sehemu ya ardhi anayomiliki kwa ajili ya kilimo,
hata kama atampa mkopaji sehemu ya mazao
yatakayo patikana. Kwa sababu hilo litasababisha
mkopeshaji kupata faida ya ziada na huutoa mkopo
huo kutoka katika kanuni ya msingi ya ukarimu na
huruma. [Ash-Shaykh Ibn ‘Uthaimin]
v. Fatawa kuhusu kuuza bidhaa kwa bei
kubwa kuliko bei yake ya asili na malipo
kupokelewa badae (Kucheleweshwa)
Aliuliza, muulizaji kuwa “Nilinunua gari lenye
thamani ya Riyals 12,100 na nikaliuza kwa Riyals
14,100 na tukakubaliana na mnunuzi kuwa atanilipa
kwa kipindi cha miezi mitano (05) lengo likiwa ni
kuumpa muda. Nahitaji kupata hukmu juu ya
muamala huu, Je! Mauziano ya haya hujumuishwa
ndani ya msingi wa Riba.”

44
Jawabu:
Ikiwa muamala huo umefanyika kama ulivyoeleza,
mauziano ya gari hilo kwa utaratibu huo
yanaruhusiwa. Na unaruhusiwa kwa sharti tu ikiwa
ulishalimiki gari hilo kutoka kwa mmiliki wa kwanza
aliyekuuzia wewe. Na hili msingi wake ni kauli ya
Allaah aliposema:

َ ‫ٰيأَيﱡ َها ٱلﱠذِينَ آ َمنُ ۤواْ ِإذَا تَدَايَنتُم بِدَي ٍْن ِإلَ ٰى أ َ َج ٍل ﱡم‬
ُ‫سمى فَٱ ْكتُبُوه‬
“Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda
ulio wekwa, basi andikeni. (02:282)
Na hili pia limethibiti katika Sahihs mbili (Sahih
Muslim na Sahih Al-Bukhariy) katika Hadith ya
A’ishah (Rehma za Allaah ziwe juu yake) kuwa
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alaiyh wa Sallam)
alinunua chakula kutoka kwa Mpagani kwa mkopo
na alimpa (Mpagani) koti lake la vita kama
dhamana. Hakuna Riba katika hili kwa uwezo wa
Allaah, hata kama bei ya bidhaa iliyouzwa ni kubwa
kuliko bei yake ya asili. [Kamati ya Kudumu ya
Fiqh]
Katika kuendelea kufafanua kwa kunukuu fatawa
mbali mbali juu ya miamala ambayo imetolewa
ufafanuzi na Wanazuoni wa Kiislamu, tunaweza
kuona kuwa miamala mingi ambayo inaulizwa kwa
nyakati hizo inalingana kabisa na baadhi ya
miamala ambayo hata katika wakati tulio nao

45
inafanyika huku wahusika bila aidha kujuwa
kwamba wanaingia ndani ya Riba ama wakijuwa na
huku wakiendelea bila kujali athari zake hapa
duniani na madhara yake mbele ya Allaah
(Subhanahu), bila kujali kuwa kufanya hivyo tayari
wametangaza vita na Allaah (Ta’ala), vita ambayo
hawaiwezi. Tulibainisha awali kuwa mara nyingi
dhulma inayopatikana ndani ya miamala ya riba
hutokana na mambo mengi ikiwamo hadaa na
mbinu chafu za kuhakikisha mmoja hufaidika zaidi
huku mwengine ndani ya muamala huo akidhurika.
Aliulizwa Ash-Shaykh Ibn Baz (Rehma za Allaah
ziwe juu yake) kuwa “Ni ipi hukmu ya kukopesha
kwenye kuuza na kununua bidhaa ambazo kwa
wakati wa mauziano havipo vitu hivyo katika
mikono na umiliki wa muuzaji?” Ash-Shaykh alijibu
kwa kusema kuwa ((Hairuhusiwi kwa Muislamu
kuuza bidhaa kwa malipo ya papo hapo ama kwa
mkopo, hadi muuzaji awe amemiliki bidhaa hiyo.
Na hii kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu
alaiyh wa Sallam) alipomwambia Hakeem bin
Hizam: “Usiuze kitu ambacho huna umiliki nacho.”
Na hii pia inathibitishwa na kauli ya Mtume (Swalla
Allaahu alaiyh wa Sallam) katika Hadith ya Abdallah
bin ‘Amr bin Al-‘Aas (Radhi za Allaah ziwe juu yake)
alisema: “Hairuhusiwi kukopesha na kuuza (ndani
ya muamala mmoja), na hairuhusiwi kuuza kitu
usichokimiliki.”))

46
Imam Salih Al-Fawzan (Rehma za Allaah ziwe juu
yake) ameandika katika kitabu chake ‘Miamala ya
Biashara Iliyoharamishwa’ kuwa kuhusu jambo la
mmoja kuuza bidhaa ambayo hana umiliki nayo
alisema; Haturuhusiwi kulichukulia jambo hili kwa
wepesi. Yeyote anayetaka kuuza bidhaa au kitu
chochote kwa mtu mwengine, hulazimika awe
amekimiliki kitu hicho na amekihifadhi kwenye
ghala ama dukani kwake, au sehemu ya kuhifadhia
bidhaa kwa ajili ya kuuzwa, au ofisini kwake, ama
hata kwenye gari lake. Ili iwapo atatokea mtu
kutaka kukinunua aweze kumuuzia kwa fedha
taslimu ama kwa mkopo. Akaongeza Ash-Shaykh
Al-Fawzan kuwa; kufanya muamala huo,
huhesabika kana kwamba uliyefanya biashara ya
kuuza deni kwa deni, na Mtume (Swalla Allaahu
alaiyh wa Sallam) ametukataza aina ya miamala
hiyo kama ilivyokuja katika Hadith ya Hakeem bin
Hazaam (Radhi za Allaah ziwe juu yake) alipoenda
kwa Mtume wa Allaah na kusema: “Ewe Mjumbe
wa Allaah, itakuwaje akitokea mtu anataka
kununua kutoka kwangu, lakini mimi sina kitu
hicho. Kisha nikaenda kwenye soko na nikakinunua
kwa ajili yake?” Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa
Sallam) akasema: “Usiuze kitu usichokimiki.”
Tumeleta sehemu ndogo za nukuu za fatawa hizi
kwa lengo la kubainisha na kutoa mafunzo kwa
jamii juu ya aina mbali mbali za miamala ambapo

47
kupitia nukuu hizi, jamii itaelewa na kujiepusha na
miamala ambayo imeharamishwa na kuhakikisha
tunaepuka. Kwa ujumla lengo ni kuhakikisha kila
mmoja wetu anao mchango wake katika
kuhakikisha tunaisafisha jamii yetu kutokamana na
Riba huku tukinusuru mali za ndugu zetu na wazazi
wetu dhidi ya dhulma ambayo inapatikana ndani ya
miamala hiyo. Kila mmoja wetu ndani ya jamii
analo jukumu la kuhakikisha hadhulumu naye
hadhulumiwi kwani dhulma ni kiza na kina malipo
mabaya mbele ya Allaah (Subhanahu wa Ta’ala).
Tunaugusa jamii yetu kwa sababu tunaishi nayo na
tunashuhudia mifano ya wazi juu madhila na
manyanyaso wanayokutana nayo wale wanyonge
walioingia katika miamala ya riba. Huachi kuona
mara kadhaa minada ya mali za walioshindwa
kulipa mikopo ya riba, huku mali za ndani
zikitolewa na kuuzwa hadharani kiasi cha kufikia
mtu kuuziwa hadi godoro alilolalia usiku uliopita,
wakiachwa watoto bila hifadhi wala malazi salama.
Je! Haitoshi kuwa ni dhara na mateso ya riba na
Allaah (Subhanahu) anatusubiri kwa adhabu.
Huachi kusikia maugomvi ndani ya familia za
wakopaji, wazazi wakigombana kwa matusi
makubwa sababu zikiwa ni kucheleweshewa mke
kupewa pesa za marejesho, huachi kuona
wanawake walio wengi wakivuka mipaka ya

48
heshima za waume zao kwa sababu ya kukosa pesa
za marejesho. Huachi kuona watu wakisengenyana
juu ya madeni na marejesho. Haya hayatoshi
kutuamsha akili zetu juu ya athari za riba? Huachi
kuona watu wakiyakimbia majumba yao na
kujificha maporini wakikwepa kufuatwa na wale
wanao wadai. Haitoshi kutupa mazingatio? Na
huenda namna tunavyoona jamii yetu
ilivyoporomoka kimaadili na Imani, ni kwa sababu
ya kuenea kwa Riba. Huenda hizi zote
zinadhihirisha ile ahadi ya Allaah (Ta’ala) juu ya vita
aliyoitangaza kwetu, basi Je! Hatuna akili?
Hatufikiri? Allaah kwa hakika anasema ndani ya
Qur’an:

﴾٣٠﴿‫ير‬
ٍ ‫ت أَ ْيدِي ُك ْم َويَ ْعفُواْ َعن َك ِث‬ َ َ ‫َو َمآ أ‬
ِ ‫صابَ ُك ْم ِ ّمن ﱡم‬
ْ َ‫صيبَ ٍة فَ ِب َما َك َسب‬
“Na misiba inayo kusibuni ni kwa sababu ya vitendo
vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi”
(42:30)
MKUSANYO WA WALAO NA KULISHA RIBA
MBELE YA ALLAAH (SUBHANAHU)
Tumezungumza kwa upana uharamu wa riba na
athari zake katika jamii ya kiislam na hatma ya
viumbe ambao wanajihusisha na miamala ya Riba.
Kupitia kitabu hichi tumebainisha aina za riba,
makatazo yake ndani ya Qur’an pamoja na athari
ambazo miamala ya Riba inaleta katika jamii

49
ambapo ni pamoja na kuongeza dhiki ya maisha na
umasikini.
Athari za Riba hazikomi kwenye maisha ya hapa
duniani, bali viumbe ambao wanatoa na kupokea
Riba watajikuta na hali ngumu sana siku ya
mkusanyo wa kufufuliwa kutoka ndani ya makaburi
yao kuelekea katika viwanja vya hisabu kwani Allah
(Subhanahu Wataala) anasema ndani ya Qur’an
tukufu kupitia Surah Al-Baqarah kwamba:
ُ ‫ط‬
‫ان‬ َ ‫ش ْي‬
‫طهُ ٱل ﱠ‬ ّ ِ َ‫ٱلﱠذِينَ يَأ ْ ُكلُون‬
ُ ‫ٱلربَا ﻻَ يَقُو ُمونَ إِﻻﱠ َك َما َيقُو ُم ٱلﱠذِى يَت َ َخبﱠ‬
‫س‬ ّ ِ ‫ِمنَ ْٱل َم‬
“Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo
simama aliye zugwa na Shet’an kwa kumgusa.”
(02:275)
Ibn Kathir amesema juu ya Kauli ya Allah “Wale
walao riba hawasimami ila kama anavyo simama
aliye zugwa na Shet’an kwa kumgusa” Maana yake
ni kwamba, siku ya Kiyama, wale viumbe
waliokuwa wakila riba watafufuliwa kutoka katika
makaburi yao wakiwa kama wamepandwa na
kichaa ama wamekumbwa na shetani mbaya. Ibn
Abbas, naye amefafanua kauli hii na kusema
kwamba “Siku ya Kiyama watu hao watafufuliwa
kana kwamba wamepandwa na kichaa na
wanatetemeka” Ndugu zangu wasomaji, sote
tunajuwa madhila anayokumbana nayo kiumbe

50
ambaye yupo kwenye hali ya ukichaa ama
amekumbwa na shetani, basi hiyo ndio itakuwa hali
yao mara tu watakapofufuliwa kutoka kwenye
makaburi yao. Baadhi ya wanazuoni wanasema
kwamba watu hawa watakusanywa wakiwa
wamechanganyiwa, hawajitambui wanagaragara
kisha wanainuka, na wataendelea na hali hiyo hadi
wafike kwenye viwanja vya hukumu. Hakika hii
tosha kuwa ni adhabu juu ya adhabu, huku
wakisubiri hukumu kwenye kisimamo kirefu
ambacho wafasiri wa Qur’an wanakieleza kwamba
ni kisimamo ambacho jua litasogezwa karibu na
utosi wa viumbe. Huku wakisubiri mkusanyo wa pili
kuelekea Jahannam na huko adhabu hazita simama
wala kupunguzwa. Na namna hiyo ndivyo kundi hili
litakavyo kusanywa na Allah na huo si mzaha.
ATHARI ZA RIBA NDANI YA JAMII NA DHANA
YA KIUCHUMI
Allaah (Subahanahu) hakatazi jambo lolote
isipokuwa lile lenye madhara makubwa kwa viumbe
wake, ukifanya tathmini ya mambo yote ambayo
yameharamishwa utaona wazi wazi kuwa athari
yake kwa viumbe na jamii kwa ujumla ni kubwa.
Kuharamishwa kwa Riba ni miongoni mwa Rehema
za Allaah (Subhanahu) na hekima zake kwa viumbe
wake kwani athari (Hasi) sio tu katika jamii bali pia
huathiri uchumi kwa ujumla kuanzia uchumi mdogo

51
(wa mtu mmoja mmoja) hadi katika uchumi wa
taifa. Haya yanadhirishwa na tafiti mbali mbali za
wasomi wa mifumo ya fedha na uchumi huku
wakibainisha wazi juu changamoto ambazo
zimekuwa zikiikumba jamii kutokana na miamala ya
riba. Baadhi ya wasomi wa Uchumi wanasema
kuwa Riba imekuwa na athari kubwa sana ndani ya
Uchumi kwa ujumla haswa haswa ikiwa ina changia
kwa kiasi kikubwa katika kudhoofisha ukuwaji wa
biashara, huku wakikubiana moja kwa moja na
mifumo ya fedha ambayo imeacha matumizi ya
miamala ya riba (Interest-free transactions/fiqhu
Mu’amalat).
Uislamu umeiharamisha Riba kwa msingi kuwa
inapelekea kuondoka kwa haki na uwazi ndani ya
miamala huku ikizalisha hisia za chuki baina ya
jamii kutokana na dhulma na uonevu unaopatikana
ndani yake. Riba imekuwa ikivunja msingi huu huku
wanyonge wakitwezwa kwa madeni yasiyo malizika
na wengine kufilisiwa na hata kupokonywa kwa
baadhi ya mali zao. Kila mmoja katika jamii
anapaswa kujipamba na haki, uadilifu na ihsaani
katika muamala, kwani Allah (Ta’ala)
ameyaamrisha hayo kama alivyosema ndani ya
Qur’an;

َ ‫ان َو ِإيت َِآء ذِى ْٱلقُ ْربَ ٰى َو َي ْن َه ٰى‬


‫ع ِن‬ ِ ‫س‬َ ْ‫ِإ ﱠن ٱ ﱠ َ َيأ ْ ُم ُر ِب ْٱل َع ْد ِل َوٱﻹح‬
﴾٩٠﴿ َ‫ظ ُك ْم لَ َعلﱠ ُك ْم تَذَ ﱠك ُرون‬ُ ‫َاء َو ْٱل ُم ْن َك ِر َو ْٱل َب ْغ ِى َي ِع‬
ِ ‫ْٱلفَحْ ش‬

52
“Hakika Allaah Anaamrisha uadilifu na ihsaani na
kuwapa (msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza
machafu na munkari na ukandamizaji.
Anakuwaidhini ili huenda mkapata kukumbuka”
(16:90)
Ibn Taymiyyah (Rehma za Allaah ziwe juu yake)
alisema katika mitazamo yake ya Kiuchumi kuwa
kuharamishwa kwa Riba kumetokana na madhara
yake kwa wahitaji wanyonge kwa namna ambavyo
husababisha hasara za fedha na mali nyengine
zinazochukuliwa kwa njia ya Dhulma. Kwa upande
mwengine, Ibn al-Qayyim (Rehma za Allaah ziwe
juu yake) alisema pia katika mtazamo wake kuwa
((Ikiwa watu wangeliruhusiwa kufanya miamala ya
kubadilishana chakula kwa mkopo, wengi wao
wasingelifanya hivyo isipokuwa katika kipindi
ambacho kina faida zaidi na wasingeli uza bidhaa
hizo moja kwa moja badala yake wangelizihifadhi
hadi kipindi ambacho kitakuwa ni faida zaidi
kuziuza. Hivyo kutokana na hili, wahitaji wanyonge
wangelikosa chakula kwa wakati, na itambulike
kuwa jamii iliyokubwa inaishi katika hali ya
kutomiliki fedha kila wakati))
Baadhi ya wasomi wa mifumo ya fedha na uchumi
wa Kiislamu wanasema kuwa mikopo na miamala
ya riba huwaumiza zaidi masikini na ikiongeza
kiwango cha umasikini katika jamii kwa sababu

53
masikini wamekuwa wakiishi na malipo ya mikopo
isiyoisha kutokana na Riba iliyopandikizwa ndani
yake. Wanaongeza kusema kuwa wakopeshaji wa
mikopo ya Riba wanachojali ni kuwa mikopo hiyo
inalipwa bila kujali wala kuangalia pesa za malipo
zinapatikana vipi, ukizingatia ugumu wa hali za
kiuchumi za wakopaji. Miamala hii pia imekuwa
ikiwafanya masikini kuendelea kuwa masikini huku
wakitumia njia mbali mbali kujikwamua katika
kulipa deni hata kama itakuwa ni kuuza baadhi ya
rasilimali zao, na inawezekana kabisa kwamba
biashara zao hazina matunda kutokana na
kuzungukwa na utiriri wa marejesho yenye Riba
zilizo ongezwa juu kwa juu.
Profesa, Faridul Islam, msomi na mtafiti wa mambo
ya Kiuchumi ametaja athari nane (08) za Riba huku
akizielekeza moja kwa moka katika Uchumi na
Biashara kwa ujumla. Dkt. Islam alisema katika
tafiti yake hiyo ya mwaka 2016 kuwa; Riba
huongeza mfumuko wa bei kwa maana mitaji
hupatikana kupitia mikopo ya Riba ambayo
mfanyabiashara itampasa kupandisha bei ya bidhaa
zake ili aweze kufidia kiwango cha riba anachokilipa
huku madhara yake yakielekea kwa mlaji wa
mwisho ambaye hununua bidhaa yenye ongezeko
la fidia ya gharama pamoja na fidia ya riba.
Akaeleza kwamba Riba inachochea kiwango cha
ukosaji wa ajira ndani ya jamii kutokana na

54
biashara kuporomoka kwa sababu ya kuongezeka
kwa gharama za uendeshaji. Dhana hii ameitetea
kuwa, gharama za marejesho ya mkopo ambayo
mfanyabiashara anazilipa zinakuwa ni sehemu ya
gharama za uzalishaji hivyo bila ya kuzifidia katika
bei ya bidhaa hakuna faida na ndio inayopelekea
biashara nyingi kufungwa na mwisho kiwango cha
kujiajiri kushuka.
Tukiendelea kuyafafanua madhara ya Riba ndani ya
jamii na Uchumi kwa ujumla, inaelezwa kwamba
Riba husababisha na kuzalisha tabaka kubwa ndani
ya jamii katika wale wenye mali (Matajiri) na wale
wanyonge, ambao kwa kutumia miamala ya riba
huonekana kuwa ni watumwa wa kuwachumia mali
matajiri. Matajiri wenye mali huwakopesha wahitaji
huku wakiwabebesha mzigo wa riba ili iwe ni faida
ya ziada katika mali yake aliyotoa, hivyo kila chumo
au riziki inayopatikana na masikini huishia mikononi
mwa matajiri ikiwa ni kama fidia (Riba). Kupitia
mikopo ya Riba, matajiri wanajihakikishia
marejesho yenye ziada kutoka kwa wanyonge hata
kama wakiwa katika kipindi kigumu cha biashara.
Tafiti zinaonyesha pia, Riba inachangia kwa kiasi
kikubwa kuzorotesha uanziashaji wa biashara mpya
kutokana na kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha
gharama za mikopo kwa ajili ya mitaji. Aidha
wachambuzi wa masuala ya Uchumi wanasema

55
kuwa kama kusingelikuwa na Riba, basi watu
wasingelikubali kukopesha fedha zao kwa sababu
bila ya riba, hakuna faida yoyote ya ziada kwa
mkopeshaji. Na haya yanarudi katika kauli ya Ibn
al-Qayyim (Rehma za Allaah ziwe juu yake) katika
nukuu ya mtazamo wake wa Kiuchumi kuhusu riba
ambao tumeunukuu hapo awali. Duru za Kiuchumi
zinaonesha kwamba uwepo wa Riba umesababisha
upatikanaji wa uhakika wa fedha za ziada kwa wale
matajiri huku wakibaki kuwa mabwana bila kufanya
shughuli yoyote zaidi ya kukopesha kwa Riba na
kusubiri marejesho yenye ongezeko la Riba na
kuwafanya waendelee kuwa matajiri huku
wakiwaacha wengine kuzidi kuwa masikini wa
mfano.
Tafiti zinaonyesha pia, Riba inakinzana na dhana ya
udugu na huruma badala yake huzalisha na
kupandikiza ubabe, ubinafsi na ususuavu wa mioyo.
Badala ya kushirikiana katika biashara ama
uwekezaji, Riba hutengeneza mahusiano mabaya
kati ya Mkopeshaji na Mkopaji, huku Mkopeshaji
akiwa na fursa za kifedha na kuzitumia
kuwakandamiza wakopaji kwa kadiri anavyoweza
kuhakikisha anarudisha mkopo aliokopa bila ya
kujali hali ya kifedha na kibishara ya mkopaji. Ndio
maana inasemwa kwamba mifumo ya riba ni ya
unyonyaji na sio ya ushirika.

56
Baadhi ya manguli wa Kiuchumi duniani wanasema
kuwa Riba hutumika kama kidhibiti cha kupanda na
kushuka kwa uwekezaji na mitaji hivyo kadiri
kiwango (rate) cha Riba kinavyoongezeka ndivyo
gharama za uwekezaji na mitaji zinaongozeka na
kuzingatia kuwa kiwango cha Riba hutegemea sana
mahitaji ya mitaji kwa kipindi husika. Kwa dhana hii
ndipo wakatamatisha kuwa uwepo wa Riba ndani
ya Uchumi na tabia yake ya kupanda na kushuka
kila wakati husababisha kuwa na hali ya uchumi
usiyo na uhakika na kuongeza kiwango kikubwa
cha khasara kwa wawekezaji.
Kwa hakika tumeeleza athari za riba kwa jamii yetu
huku tukitoa ufafanuzi wa kisomi juu ya athari hizo
kwa uchumi, haya ni miongoni mwa madhara
yanayopatika kupitia miamala ya Riba na mengine
mengi ambayo hatujayagusia, na kuziacha kwake
sio kwasababu ya udhaifu wake bali kwa sababu
idadi yake ni nyingi kiasi cha kwamba kingetosha
kitabu hichi na vyengine kuzielezea, ila huu ni
ufunguo na changamoto kwa waandishi wenye
elimu zaidi kuyaendelea kwa ubainifu wa
kuyafafanua. Yatoshe haya niliyoyabainisha ndani
ya kitabu hichi kuwa ni mawaidha kwa nafasi yangu
na udogo wa elimu yangu. Natambua wapo ambao
watapata hamasa zaidi ya kuielewesha jamii

57
kutumia machapisho mbali mbali na namuomba
Allaah (Subhanahu) awawezeshe kila mwenye nia
njema juu ya hilo. Huenda tukaongoka na tukavuka
ndani ya mkondo mkali wa Riba.
VIPI TUTAJIKWAMUA KUTOKA HAPA TULIPO
Ndugu yangu msomaji, duru za kijamii zinaonyesha
kuwa asilimia kubwa ya watu kwa njia moja ama
nyengine wanajihusisha na miamala ya Riba, na
mbali na lile kundi ambalo wanafanya kutokana na
kutokuwa na elimu, kundi kubwa la watu wafanyao
(kula na kulisha riba) wanafahamu uharamu wake,
madhara yake na hata uzito wa dhambi yake mbele
ya Allaah (Subhanahu), hilo husababisha kuwa na
mazingira magumu kwa jamii yetu kuepukana na
riba. Baadhi ya wasomi wa Uchumi wanasema
kuifuta riba moja kwa moja ndani ya jamii ni jambo
ambalo linawezekana, isipokuwa kikwazo kikubwa
ni mifumo ya fedha na benki ambayo inayotumika
ndio inasababisha jamii kuendelea kuangamia (wao
na mali zao) ndani ya kiza kinene cha riba.
Juhudi kubwa tumeona zikifanyika, zikiwepo za
uanzishaji wa mfumo wa fedha na benki wa
Kiislamu ambao msingi wake mkubwa ni kuiondoa
Riba katika miamala yote. Tunashuhudia mabenki
ya kiislamu yakifunguliwa huku yakija na bidhaa
ambazo ndani yake riba imeondolewa, na badala
yake wanashirikiana katika uwekezaji na mwisho

58
kugawana faida itayopatikana au khasara ambayo
imetokea hivyo hali hio kwa uchache imeanza kutoa
nuru na bishara njema kwetu. Ingawaje bado
changamoto kubwa inarudi kwenye mfumo mama
wa fedha na uchumi ambao ndio unazisimamia
taasisi hizo. Kwa mujibu wa tafiti niliyoifanya
mwaka (2016) katika kuangalia changamoto
wanazopata taasisi za fedha na benki za Kiislamu
katika ukuwaji na kuwa na mafinikio yaliyowekwa,
nilibaini kuwa kukosekana kwa mifumo sahihi ya
usimamizi wa taasisi za fedha na benki za kiislamu
ambao utakuwa unasimamiwa na kutekelezwa kwa
Shariah imekuwa ni kikwazo kikubwa cha
maendeleo ya taasisi hizo.
Kutokana na hali hiyo, jambo la msingi na lililo la
sawa kwa nyakati zetu, nyakati ambazo riba
imekuwa ndio msingi wa kila muamala, tunayo haja
sasa ya kurudi kwa Allaah (Subhanahu) na kukinai
kwa kila ambacho ametuhalalishia na kuyaacha
yale yote aliyo yaharamisha kama vile Riba. Turudi
katika mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu alaiyh
wa Sallam) kwa vitendo na kwa kuweka nia ya
dhati kabisa juu ya kukoma na kukoma kabisa
kushiriki katika kila aina ya muamala ambao
umebebeshwa riba ndani yake. Ibn Baz (Rehma za
Allaah ziwe juu yake) alisema, njia pekee ya
kuondokana na uchafu wa riba kuwa ni kuchunga
taqwa ya Allaah, pili ni kuacha kuendelea kutumia

59
mali yoyote ambayo uliichuma kwa njia za dhulma
za riba na kurudi kwa Allaah kwa istighfar na kutoa
sadaqa kwa sehemu yote ya mali iliyochumwa kwa
njia za riba.
Kwa hakika njia pekee ya haki ni kuzilainisha nafsi
zetu juu ya Twa’a kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) na
kufanya juhudi kujizuia na kukemea kuongozwa na
matanio ya nafsi zetu bali tuongozwe na misingi ya
Qur’an na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu alaiyh
wa Sallam). Tujitosheleze na kukinai na kile
ambacho ameturuzuku Allaah (Ta’ala) na kujitahidi
kuondoa tama za utajiri wa haraka ama mali bila
jasho kwani Mtume (Swalla Allaahu alaiyh wa
Sallam) amesema; Hakika ya kizuri miongoni mwa
unachokimiliki ni kile ambacho umekipata kwa
mikono yako na juhudi zako. Kila mmoja wetu awe
ni msimamizi wa mwenzake, kuhakikisha hakuna
kati yetu anaingia kwenye jambo hili na hapo ndipo
tunaweza kuongoka.
Ibn Taymiyyah (Rehma za Allaah ziwe juu yake)
alisema wakati akitoa nasaha zake juu ya
kuharamishwa kwa riba na madhara yake alisema
kuiambia jamii; Kwanza lazima jamii iwe na Imani
juu ya kumpwekesha Allaah, na kutambua hakuna
Mungu isipokuwa Allaah, Muumba na Mlezi wa
ulimwengu wote. Ambaye amewapa viumbe wake
muongozo wa maisha ambao unahakikisha ustawi

60
mwema kwa dunia nzima na Akhera. Mwanadamu
hawezi kuishi kwa kujitegemea mwenyewe pasi na
kuhitaji mwengine, hivyo wanapaswa kuishi pamoja
na kushirikiana kwa kheiri katika kukuza ustawi
wao na kupiga vita uadui na matendo maovu.
Akaendelea kutoa nasaha kuwa; muislam anaweza
asiwe mchumi, lakini akawa na lengo la kupata
radhi za Allaah kupitia matendo mema na kuwa
msaada mzuri kwa wengine. Nia na matendo mema
hukuwa pale yanapopata mwitikio mzuri kutoka
kwa mwengine, hivyo hivyo kujikurubisha kwa
wema na kushindana katika wema ni jambo linalo
zingatiwa. Wema na ukarimu ushike hatamu ndani
ya jamii, watu wanapaswa kujali mahitaji ya
wengine zaidi ya mahitaji yao. Kwa upande
mwengine tamaa ya fedha na uchoyo upigwe vita
katika mazingira yote. Maisha ya kifaghari
yaepukwe kwa maana uzuri wa maisha ni kuishi
maisha ya wastani. Ndani ya jamii kusiwe na
ukiritimba, unyonyaji, ufisadi, wala miamala ya
riba. Jamii inapaswa kuamrishana mema na
kukataza mabaya. Viongozi wanatakiwa kuwa
mstari wa mbele katika kuhakikisha watu
wanakuwa kiuchumi na wawe karibu kuingilia kati
pale uhuru unapotumiwa vibaya na wachache na
pale wengine wasipotimiza wajibu wao. Ndugu
yangu msomaji, na hiyo ndiyo misingi ya jamii ya
kiislamu, Riba haina nafasi ndani ya jamii hiyo kwa

61
maana huzalisha ubinafsi, uchoyo na tama za
fedha, chuki, wivu na unyonyaji. Badala ya jamii
kufanya miamala yenye riba, wahimizane kutoa
Zakah na sadaqa. Na kupitia misingi hii kwa uwezo
wa Allaah (Subahanahu) “HUENDA TUKAONGOKA”
kutokana na Riba.
Wabillah Tawfiq
Wallahu A’ala wa A’alam

62

You might also like