Professional Documents
Culture Documents
YANAYOFANYWA NA
MABINTI WENGI
1|P a g e
Kitabu hiki kimeandikwa na Bro. Elihuruma Maruma,
hakimiliki zote ziko chini ya mwandishi.
2|P a g e
YALIYOMO
DEDICATION ................................................................ 7
SHUKRANI ................................................................... 8
UTANGULIZI: ................................................................ 9
MISTAKE 1: .................................................................. 15
MISTAKE 2: ................................................................. 21
MISTAKE 3; ................................................................ 29
MISTAKE 4: .................................................................33
MISTAKE 5: .................................................................35
MISTAKE 6; ................................................................. 37
MISTAKE 7: ................................................................. 41
3|P a g e
MISTAKE 8: ................................................................ 45
MISTAKE 9; ................................................................ 49
MISTAKE 10;................................................................53
4|P a g e
MISTAKE NO 18; ......................................................... 93
5|P a g e
6|P a g e
DEDICATION
I would like to dedicate this book to: -
i. All girls whether you call yourself a lady or a woman
listen “Today is never too late to be brand new” just a
simple principle to apply “Hate the Mistake LOVE THE
LESSON”
7|P a g e
SHUKRANI
Maisha ya mtu na hasa kusudi la Mungu hukamilishwa kwa
michango ya watu mbalimbali, kwangu mimi ni hekima
kuwashukuru wafuatao kwa sababu ya kitabu hiki: -
i. Yehova Mungu (Mola) ambae kwake nimeumbwa,
ninaishi, ninatembea na ninafanikiwa na kuwa na
uzima tele.
8|P a g e
UTANGULIZI:
“The person who doesn’t make mistake is unlikely to make
anything”
Paul Arden.
9|P a g e
au kiwango gani cha elimu ila maadamu bado
hujaolewa kuna makosa kati ya 21 wanayofanya
wasichana wengi mwishoni utakubaliana nami kwamba
unayafanya au uliwahi kuyafanya.
UKUMBUKE TU KWAMBA;
“All men make mistake but only wise men learn from their
mistake”
Winston Churchill.
10 | P a g e
Kwenye maisha ya msichana au binti yeyote kuna hatua za
ukuaji au mchakato ambao ni lazima aupitie kwa mfano: -
kuvunja ungo (Kupevuka) na mengine mengi. Makosa mengi
kati ya haya 21 ambayo wasichana wengi wanafanya, huwa
wanaanza mara tu baada ya msichana kupevuka na kujikuta
anaanza kuwa na hisia au mvuto na watu wa jinsia nyingine
(Ya Kiume). Hatua hii kimsingi inakuhamisha hata kama hutaki
kutoka utoto kuelekea Utu uzima. Viungo katika mwili wako
hubadilika aidha kwa kukua au hata vipya kutokea, ghafla
umbo lako linaanza kuwa na mvuto wa tofauti, ngozi inakuwa
laini na sauti kuwa nyororo wakati mwingine. Haya yote
yanachangia Usumbufu wa maombi na sifa kutoka jinsia ile
nyingine kuwa mkubwa, na hapa ndipo wengi huanza
kukosea. Hebu nisimalize huu utamu badala yake nikufundishe
kitu juu ya makosa
11 | P a g e
S - SIGNPOST: that directs us to the right path.
T - TESTS: that pushes towards greater maturity.
A - AWAKENINGS: that keep us in the game
mentally.
K - KEYS: that we can use to unlock the next door of
opportunity.
E - EXPLORATIONS: that lets us journey where we
have near been before.
S - STATEMENTS: about our development and
progress.
MESSAGE: (Ujumbe),
Makosa ni ujumbe unaotupa urejesho juu ya mfumo sahihi wa
maisha, tunapokosea tunajifunza namna ya kuishi.
INTERRUPTIONS: (Usumbufu/Vikwazo),
Makosa ni usumbufu au vikwazo vinavyotusukuma kuakisi na
kufikiri kwa kina.
12 | P a g e
Makosa ni kibao elekezi cha kutusaidia kwenda njia sahihi.
TESTS: (Majaribio), Makosa ni majaribio yanayotupelekea
kukua na kupevuka.
AWAKENINGS: (Uamsho),
Makosa ni uamsho unaotufanya tutumie akili ipasavyo.
KEYS: (Funguo),
Makosa ni funguo zinazotumika kufungua mlango wa fursa
nyingine.
EXPLORATIONS: (Ugunduzi),
Makosa ni ugunduzi unaotusafirisha mpaka mahali ambapo
hatukuwahi kufika kabla.
STATEMENTS: (Kauli),
Makosa ni kauli juu ya maendeleo yetu.
13 | P a g e
Nakushauri sasa nikiwa kiongozi wako chukua penseli yako na
weka alama ndogo kwa kila kosa linalokuhusu kisha kwa
maarifa uliyoyapata amua kubadilika na kutokukosea tena.
14 | P a g e
MISTAKE 1:
YOU DON’T KNOW YOURSELF! (HUJIJUI)
15 | P a g e
“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla
hujatoka tumboni nalikutakasa; nimekuweka kuwa…”
Yeremia 1:5
Hivyo basi furahia kuzaliwa msichana na jikubali kuwa
msichana, lakini pia furahia familia yako na wazazi
waliokuzaa, hii ni sehemu muhimu ya kujitambua.
16 | P a g e
Ni vile hujitambui tu ila kwa taarifa yako kipaji,
kipawa, karama au uwezo wowote ulionao Mungu
alikupa ili utimize kusudi lake, na ili uishi maisha bora,
mazuri ya mafanikio. Anza kufikiri tofauti juu ya
chochote ulichonacho.
17 | P a g e
na wa pekee, sababu unapenda kusifiwa na kujaliwa
na ni asili yako utajikuta unaangukia pua.
“To be beautiful means to be yourself. You don’t need
to be accepted by others, you just need to accept
yourself”
18 | P a g e
kutumia huu uwezo kufanya mambo ya maana
yatakayokusaidia kufikia ndoto na malengo yako
“The more you know who you are and what you want,
the less you let things upset you” Stephanie Perkins
*Usipojijua wewe binafsi na kujikubali utaendeshwa
sana na matukio. Na kutojijua na kutojitambua ndio
huwasababishia mabinti kujikuta wanakosea kila wakati
“Ukitambua Thamani, Ubora, Uzuri, Uwezo na udhaifu
ulionao itakusaidia kujua ni kwa namna gani unaweza
kushindana na kila changamoto, mitego na mbinu za
kukuharibia maisha yako”
19 | P a g e
20 | P a g e
MISTAKE 2:
YOU DON’T TEST BEFORE YOU TRUST!
(HAUPIMI KABLA YA KUAMINI)
21 | P a g e
mahusiano mpaka amepima na kuamini. Jitahidi iga mfano
huu.
22 | P a g e
SASA WEWE NA TAI JIKE NANI ANA AKILI ZAIDI?
“Trust is an expensive thing; you can’t get it to cheap people”
SHUHUDA MBALIMBALI:
“Naomba unisaidie maombi, nachukia wanaume na sitamani
hata kuolewa na nimezaliwa tarehe 1/1/1980, umri unasogea
lakini ndo hata sitamani hata kusikia neno mwanaume”
23 | P a g e
TATIZO:
“Many girls confused on first impression – love at a first sight”
Siku zote usikurupuke kumwamini mvulana au mwanaume
yeyote kwenye mapenzi au mtu yoyote kwenye jambo lolote
kabla ya kumpima
Kumbuka;
“A relationship without trust is like a car without gasoline. You
can stay in it, but it won’t go anywhere”
24 | P a g e
Marafiki ambao wapo kwa sababu au majira flani, sababu zao
zikiisha au majira yakikamilika huondoka, hawa sio sahihi
kuwaamini wawe wa kike au wa kiume, lakini wapo marafiki au
yupo rafiki ambae unaweza kumwamini.
25 | P a g e
v. NOT SELF-SEEKER: Hatafuti mambo yake, hajaja kwako
kwa sababu au matarajio flani au agenda za siri,
Wenye yao utawagundua mapema Mf; Anadai ngono.
vi. NOT EASILY ANGERED: Haoni hasira upesi, na hata
unapomuudhi ukimuomba msamaha anakusamehe na
kusahau na hatakukumbushia.
vii. NOT DELIGHT IN EVIL: Hafurahii uovu au makosa
yako, unapokosea hukukemea na kukusahihisha,
unapokwenda kinyume na Mungu hukueleza wazi.
viii. REJOICES IN TRUTH: Hufurahia kweli, hata kama
utamuuma na kujitahidi daima kuwa muwazi, mkweli
na mwaminifu hana mambo ya siri.
ix. TRUSTWORTHY & HOPEFUL: Hutumaini na Huamini
yote, daima hukuamini na kuwa na matumaini na
wewe, ndoto zako na mipango yenu na zaidi
humwamini na kumtumaini Mungu.
x. PROTECTOR: Hukulinda katika Nyanja zote kimwili,
kiroho, kimahitaji, kihisia, na kijamii kuhakikisha
kwamba haudhuriki na unasonga mbele.
26 | P a g e
Wasichana wengi wameumizwa kwa kung’ang’ania watu
ambao wanajua dhairi si waaminifu ama hawawapendi kama
wanavyofikiri, imefikia hatua ni lazima sasa useme IMETOSHA
na NG’ATUKA, maana mahusiano bila kuaminiana ni kama
gari zuri bila mafuta unaweza kukaa ndani yake ila halitaenda
popote.
Nina mifano na shuhuda za mabinti wengi ambao
waling’ang’ania mahusiano yasioeleweka kwa sababu ya hisia
zao walizoziita UPENDO wakaambulia VIDONDA.
27 | P a g e
28 | P a g e
MISTAKE 3;
YOU DON’T HAVE EYES TO SEE BEYOND
WHAT YOU CAN LOOK!
Mithali 29:18
29 | P a g e
halijatokea, Kwa mfano msichana ana mitihani mbele,
anajiandaa kupata kazi(ajira), kuingia kwenye ndoa na
kadhalika. Ni Muhimu msichana awe na maandalizi ya
kutosha juu ya matukio yanayokuja mbele yake na huo
ndio uwezo wa kuona zaidi ya kuangalia.
30 | P a g e
mengi ambayo baadae utayajutia maana daima “UNAVUNA
ULICHOKIPANDA NA SI TOFAUTI NA HAPO”
“Go as far as you can see; When you get there; you’ll see
further”
Zig Ziglar
31 | P a g e
32 | P a g e
MISTAKE 4:
YOU ARE THE FEMALE IMPALA IN HAREM
SYSTEM!
(WEWE NI SWALA JIKE KATIKA MFUMO DUME)
HAREM SYSTEM:
Huu ni mfumo wa maisha ya Swala aina ya Impala ambao
dume moja la Impala humiliki kundi kubwa la impala majike.
Katika mfumo huu dume moja la impala limaweza kumiliki
mpaka majike 40 kama wake zake. Basi majike haya huwa na
dume hili kila mahali anapokwenda. Mfumo huu kwa lugha
rahisi huitwa “Polygamism” ambao mwanaume mmoja
anamiliki wanawake wengi kama wake zake.
SIKUHIZI:
Wasichana wengi tena wenye utashi, warembo na wengine
waliosoma kabisa wamejikuta kwenye huu mfumo kama wa
majike ya Impala aidha kwa kujua au kutokujua. Wapo
wanaojiita wamependa na hawako tayari kuwapoteza wavulana
wao kwa hiyo haijalishi yupo na wasichana wangapi
wanamng’ang’ania kama kupe. Wewe sio tairi la ziada (Spare
Tyre).
Sikiliza nikwambie kitu KAMWE usiruhusu heshima, thamani
na uzuri wako upotee kisa hisia, usiruhusu magonjwa ya zinaa
33 | P a g e
na mshtuko wa ubongo na presha ikupate kisa unajiita
unapenda. Zingatia mambo haya mawili kwa sababu Mungu
amekupa utashi na hekima.
“When someone treats you like an option, help him narrow his
choices by removing yourself from the equation. It’s that
simple” JITOE HARAKA
34 | P a g e
MISTAKE 5:
YOU ARE IDENTICAL TO FEMALE AFRICAN
JACANA BIRD
(UNAFANANA NA NDEGE AFRIKAN JACANA JIKE)
WASICHANA JACANA:
Siku hizi pia tuna wasichana wengi sana ambao muonekano
na tabia zao hufanana kabisa na ndege huyu wa kike Africa
Jacana. Wasichana hawa kuanzia vaa yao, tembea yao,
angalia yao na ongea yao huashiria dhairi kujionyesha na
kujipendekeza kwa wanaume wakiwataka kwa lazima. Malengo
yao ni ama kutaka pesa, umaarufu au basi tu kuwakomoa
wanaume, na inapotokea wamepata mimba na kuzaa
huwaacha watoto na bibi zao au babu zao na kisha huendelea
35 | P a g e
na tabia yao. Waswahili walisema; “KIZURI CHAJIUZA KIBAYA
CHAJITEMBEZA”
36 | P a g e
MISTAKE 6;
YOU TALK TOO MUCH!
“UNAONGEA SANA”
GIRLS FOR CONVERSATION:
Hii ni asili na haipingiki kwamba moja ya mahitaji makubwa
kabisa ya mwanamke ni MAONGEZI (Conversation), na
wataalam wamechunguza na kugundua kwamba kwa siku
mwanamke huongea takribani maneno 21,000 tofauti na
wanaume ambao huongea maneno 7,000 tu kwa siku. Na ni
wazi kwamba kuongea sana si tatizo ila tatizo ni nini
unachokiongea na unakiongeaje na ili nini?
37 | P a g e
“Uwe makini sana juu ya unachokizungumza juu yako na juu
ya wengine. Maana ipo nguvu ya uumbaji kwenye kinywa
chako, chochote unachozungumza kinaumbika, ukitamka
uzima, afya, kufaulu, mafanikio na chochote chema hutokea,
halikadhalika ukitamka mauti, udhaifu, kufeli, majanga na
chochote kibaya pia hutokea.
38 | P a g e
ACHA KUONGEA MABAYA JUU YA WENGINE;
Wasichana hupenda kuongea sana juu ya watu kuliko vitu, na
kwa hivyo basi ni muhimu ufahamu kwamba ni hekima na
adabu kutowaongelea wengine vibaya. Maana si vema
kuwatendea wengine lile jambo ambalo usingependa
kutendewa lakini pia; “The things you say about others, also
say a lot about you”
39 | P a g e
JIFUNZE KUZUNGUMZA UKWELI NA KUYAISHI MANENO
YAKO:
o Ni vizuri kutenda unachokisema kuliko kuzungumza
sana bila vitendo. Lakini pia jifunze kusema ukweli na
hasa mambo ambayo una uhakika nayo.
“Your words mean nothing when your actions are the
completely opposite”
“The greatest advantage of speaking the truth is that
you don’t have to remember what you said”
40 | P a g e
MISTAKE 7:
YOU DON’T LIKE TO FLY ALONE!
(HAUPENDI KURUKA MWENYEWE)
Moja ya majanga makubwa waliyonayo wasichana wengi leo
ni kushindwa kujisimamia na kufanya maamuzi yao binafsi.
Maisha yao yamekuwa yakiendeshwa aidha na marafiki zao
(Mashosti), wavulana wao na hata matukio. Wengi wamejikuta
wakiangukia pua kwa sababu tu wameendeshwa na marafiki
na matukio bila kujua kuna madhara makubwa mbele. Wapo
ambao walikuwa hawana wanaume wakapata kwa sababu ya
kampani, halikadhalika wapo ambao leo wanakunywa pombe,
wanavuta sigara, wanavaa nusu uchi, wanaenda club, wanatoa
mimba, wanasengenya wengine n.k. si kwa sababu walikuwa
hivyo ila ni kwa sababu kampani na marafiki walionao
waliwasukuma kufanya hivyo.
41 | P a g e
hukamatwa kwa makundi. Ila Tai huruka mwenyewe juu sana,
huwinda mwenyewe, hula mwenyewe n.k.
- Karibu watu wote waliofanikiwa sana hapa duniani ni wale
waliosimama kama wao kwenye ndoto zao na malengo
yao. Hawakukubali kuendeshwa na marafiki, wala
mashosti, wala matukio walisimamia misimamo yao kwa
bidii bila kujali watu wanasema nini au mazingira yakoje,
na hii iliwafanya mwanzoni kuonekana wajinga,
wanaojisikia, wanaojifanya wanajua ILA mwishoni
walifanya yasiyowezekana na walifanikiwa sana.
“Hautafanikiwa mpaka umejua kuishi kama wewe na sio
mkumbo”
“Pigeons flying in flocks but Eagles fly alone, fly higher without
limits”
“You have only one life to live, and your own life is in your
own hand”
42 | P a g e
Na mtu yoyote asiyependa uhalisia wako au misimamo yako
ambayo hiyo ndio upenyo wa kufikia ndoto na malengo yako
HAKUFAI na achana nae. Amekukuta huvai nusu uchi, hunywi
pombe, hupendi klabu, unasoma sana, huna vinyongo na
watu AKUACHE HIVYO HIVYO na akubaliane na jinsi ULIVYO.
43 | P a g e
Simama kwa miguu yako kwenye imani, maombi, ndoto,
maono, maamuzi na maisha yako na kwa hakika
UTAFANIKIWA.
44 | P a g e
MISTAKE 8:
YOU PUSH OUT FATHERHOOD!
(UNAUSUKUMA UBABA)
Wasichana wengi tulionao leo wanafikiri kwa uzuri tu kuwa na
watoto wao japo si lazima waishi na baba wa hao watoto. Kwa
sababu ya mfumo wa maisha tulionao leo familia nyingi ni
familia za mzazi mmoja na hasa mama, na hii imepelekea
wasichana wengi kutowaamini sana wanaume kwa sababu tu
ya historia na maelezo waliyopewa na mama zao.
Na wakiangalia wamelelewa na mama zao tu na wakavaa,
wakala, wakasoma na hata kufikia ndoto zao. Hii huwajengea
picha ya wao vilevile kuzaa watoto na kuishi nao peke yao bila
baba zao eti kisa ni kwamba WANATAKA UHURU WAO,
HAWATAKI PRESHA, HAWATAKI USALITI, HAWATAKI
USUMBUFU n.k.
45 | P a g e
“Kweli hizi familia za mzazi mmoja ni shida tupu”
“Yaani kweli baba ni mtu muhimu sana kwetu”
“You might not need a husband but your children need their
father, not his provisional but his presence”
UBABA:
Neno BABA limetokana na neno la kiebrania ‘ABBA’ na
Kiitaliano ‘PATTA’ ambayo humaanisha chanzo, mhimili,
mwanzilishi, mwendelezaji, mtoaji, mlinzi.
Hivyo basi BABA WA KWELI (Real Dad) ndani ya familia huwa
mtoa mahitaji muhimu ndani ya familia kwa Mama na Watoto,
Yeye ndio chanzo na mhimili wa familia, lakini zaidi yeye ndie
mlinzi (Protector) ndani ya familia. Huwaadabisha watoto,
huwatia moyo, huwafundisha na kuwaeleza juu ya Mungu na
maisha. Na ndio maana mama peke yake hatoshi kuwa mlezi
ndani ya familia hata kama angekuwa na uwezo wa kifedha
kiasi gani nasisitiza.
46 | P a g e
Watoto wako wa kiume wanahitaji kujifunza uanaume kutoka
kwa Baba yao, na watoto wako wa kike wanahitaji kujifunza
namna ya kuwa na Baba na Mume pia ndani ya familia.
Kamwe usilipotezee hili badala yake anza kujenga fikra ya
kuwalea watoto wako ukiwa na Baba yao yaani Mume wako
mpenzi. Na ni dhahiri kila mwanamke yaani hata wewe
unajisikia vizuri na salama unapokuwa na mwanaume wa
kusimama upande wako kwa ajili yako.
47 | P a g e
SWALI CHOCHEZI; Je na Wewe umewahi kuwaza
kutokuolewa na kutokuishi na mwanaume? Umewahi kufikiri
kwa kina umuhimu wa Mume na Baba katika familia?
48 | P a g e
MISTAKE 9;
YOU ARE THE SEASONAL QUEEN!!
(U MALKIA WA MUDA)
Kiburi, majivuno, kujisikia na kutojali imekuwa tabia ya
wasichana wengi wa siku hizi. Kila msichana ni malkia wa
muda kwa maana hii hapa, vaa unavyovaa, ongea
unavyoongea, tembea unavyotembea, jibu unavyojibu na
angalia kwa dharau unavyoweza ILA tambua hauweza kubaki
ulivyo milele hata kama ungekuwa na uzuri na uwezo wa
kifedha au elimu ya kiasi gani.
49 | P a g e
maringo, dhihaka, kiburi na majivuno. Kuna wengine hata
muda wa kusalimia hawana, na hata ukiwasalimia hawaitikii
HAYO SIO MAISHA.
50 | P a g e
MASHINDANO, Wapo ambao daima wanaishi kwa
kushindana, yaani wapo tayari kufanya chochote kuhakikisha
wanamiliki simu za gharama, wanavaa nguo za gharama na
viatu vya gharama, wanasuka nywele za gharama, basi tu
waonekane wao ni bora kuliko wengine. YOUR BETTER LIVE
YOUR LIFE.
51 | P a g e
Hebu angalia zamani wasichana walikuwa wanavaa underskirt,
baadae ikapunguzwa ikawa ni skintight, na sasa wengi huvaa
chupi tu kama nguo ya ndani, na hivi majuzi wapo walioanza
kuvaa nguo ya juu tu bila nguo yoyote ya ndani, HII NI
HATARI KUBWA SANA.
52 | P a g e
MISTAKE 10;
YOU HAVE A DAY DREAM (WRONG
IMAGINATION)
(UNAOTA NDOTO ZA MCHANA)
53 | P a g e
za mchana mpaka utakapogundua unachoota hakitatokea na
utakuwa umeshaumia.
“You can GIVE without loving, but you never LOVE without
giving”
Victor Hugo
54 | P a g e
Na ndoto yako ya mchana ya kuolewa unaongea nao na ghafla
moyo wako unaamini kwamba ndoa ipo ILA kumbe mwenzako
ana lake jambo, mara amekuweka kwa facebook profile yake
ndio kabisa unachanganyikiwa kumbe mwenzio anajua
ANACHOKITAKA. Wapo wadogo zangu nimewahi kuwauliza,
Una uhakika na jamaa? Kwa mkwara wakaniandikia “I have
been introducing kwao kwa mama na ndugu zake” na mwisho
wa siku walipoteza usichana wao walioutunza muda mrefu na
kuangukia pua.
55 | P a g e
SWALI CHOCHEZI; Je na Wewe huwa unaota ndoto za
mchana? Au pengine labda umewahi kuota ndoto za mchana
na yakakukuta yaliyokukuta??.
56 | P a g e
MISTAKE 11;
YOU DON’T LIKE YOUR SWEATS!
(HAUPENDI JASHO LAKO)
57 | P a g e
na wala hasubiri mpaka mume amletee kila kitu. Hasubiri
mpaka boyfriend ampe hela ya kununua kila kitu, na wala
hakai kivivuvivu akisubiri kupokea tu. Hebu iga mfano wake,
na anza kufanya kitu hata kama ni kidogo ili kujipatia kipato
kwa jasho lako.
58 | P a g e
yanayoweza kukugharimu baadae bila wewe kujua. Chanzo
cha migogoro kwenye mahusiano au ndoa yako ni vitu
ulivyovipokea tena ukidhani unamkomoa huyo mwanaume,
haijalishi labda ulikuwa kidato cha Pili, cha Nne, Sita au
Chuoni.
59 | P a g e
KANUNI YA SIMBA JIKE kwa kujishughulisha kujipatia kipato
ili vile vitu vizuri unavyovipenda ujinunulie mwenyewe.
“You don’t get what you wish for, you get what you work for”
60 | P a g e
utakacho unaweza kupata kama tu utajishughulisha kwa bidii
sana.
Mithali 19:15
61 | P a g e
62 | P a g e
MISTAKE 12;
YOU DON’T KNOW A ROMANTIC FORMULA!
(HUJUI KANUNI YA MAPENZI)
63 | P a g e
- Ila sasa inafika kipindi uzalendo unaanza kuwashinda
na hasa wavulana na hapa sasa utanielewa vizuri.
- Utamsikia mvulana anaanza na hesabu za
KURAHISISHA NA KUTOA yaani ataanza kutoa baadhi
ya misimamo mliyojiwekea na kurahisisha baadhi ya
mambo, kama sio mbaya labda, haina madhara au sio
dhambi huku akikupa mifano ya kutosha.
- Kwa mfano atakuomba akushike mkono mkiwa peke
yenu au labda akubusu na umbusu mkumbatiane tu
(hugs), na ukishakubali hii kwake SAFARI IMEANZA.
Baadae atakubusu kisha atakunyonya mdomo na
kukushika maeneo flani huku akikusisitiza si dhambi na
usipokua makini UTAJIKUTA UMEANGUKIA PUA.
- Fahamu wewe pia una hisia tena kali sana hasa
zikiamshwa kama hivyo. Na utashangaa AKILI
ZIMEHAMA na mwisho wa mchezo ndio utajua ile
ilikuwa DANGANYA TOTO kuhakikisha anakupeleka
mwisho wa safari, ASOMAE NA AFAHAMU.
“We only had wet kiss and zero hugging that’s all”
64 | P a g e
Wengine wakauliza;
1 Korintho 6: 18
65 | P a g e
Kusikiliza radio program za mapenzi,
Kuangalia tamthilia za mapenzi,
Kuchati messages (ujumbe) za mapenzi,
Kushikanashikana, Maongezi laini hasa ya usiku ya
kimahaba, Stori za waliotoka kufanya mapenzi na watu
wao. N.k
66 | P a g e
MISTAKE 13;
YOU WANT TO FINISH BEFORE YOU START!
(UNATAKA KUMALIZA KABLA YA KUANZA)
67 | P a g e
unalinda Penzi kumbe unajitengenezea mazingira ya kutumiwa
na kuchokwa.
Waswahili wakasema;
”Haraka haraka haina Baraka”
“Pole pole ndio mwendo”
“Mvumilivu hula mbivu” I AGREE
68 | P a g e
KULAZIMISHIA MAHUSIANO YA HARAKA NA UPENDO
{KULIPA KISASI i.e REVENGE.}
69 | P a g e
Kamwe usitumie nguvu nyingi na ushawishi mkubwa jumlisha
gharama kubwa kulazimishia ndoa au mahusiano. Mungu
aliyekuumba anajua umuhimu wako na upweke ulionao
LAKINI pia anajua nani anaekufaa, na atakuoa lini. Mungu ni
ALPHA na OMEGA, Mwanzo na Mwisho mpe nafasi maishani
mwako leo, mkimbilie na mtii naye ATAFANYA.
70 | P a g e
MISTAKE 14;
YOU OFFER SEX AS A PROVE OF LOVE &
RETURN!!
(UNATOA NGONO KAMA ISHARA YA UPENDO NA
FADHILA)
*Hapa sasa ndio ipo shida kubwa sana hasa ya ufahamu/
Uelewa kwa wasichana wengi sana. Na hii niliifananisha na
mtu kuchimba shimo refu sana yeye mwenyewe ili hali yupo
ndani ya hilo hilo shimo na hajui ni jinsi gani atatoka (Dig a
deepest hole while your inside).
71 | P a g e
Upendo sio hisia ni kitendo na chaguo (Love is not a feeling
but choice and action) Love doesn’t go against God but LUST
does. (Upendo huwa hauendi kinyume na Mungu ila tamaa ya
ngono huwa inaenda kinyume na Mungu). LUST (Sex feelings)
is temporary but LOVE is permanent (TAMAA YA NGONO ni
ya muda tu ILA UPENDO ni jambo la kudumu)
Na ndio maana hatuwezi kuhakiki tunapendwa au tunapenda
kwa kutumia tamaa ya Ngono (We cannot prove LOVE
through SEX).
Na kama kuna ujinga na kosa kubwa ambalo wasichana wengi
huwa wanafanya ni kutoa NGONO yaani UTU/USICHANA
wao kama ishara ya UPENDO kwa wavulana ambao bado
hawajawaoa. Na wavulana wengi wamekuwa wakitumia sana
hii gia kufanikisha malengo yao ya kulala na wasichana,
utamsikia kwa hasira au ulalamishi anakwambia “NAJUA UNA
MTU NA HUNIPENDI” ndio maana hautaki kulala na mimi
(Sex), au hauniamini?
“LOVE isn’t all about flirting, hugs, kisses and sex. Love is
about having the ability to take all those things away and still
having feelings for that person”
72 | P a g e
akimpa ngono ndio atapendwa zaidi anashangaa inakuwa
kinyume, mara anashangaa yale matunzo, kujali, mawasiliano
taratiiibu yanaanza kupungua kutoka kwa Yule mvulana alielala
nae. Na mwisho wa siku anaweza kuanza kukuchanganya na
wasichana wengine na hata kufikia kuachana (BreakUp).
Unajua Kwa Nini? AMESHAPATA ALICHOKUWA ANATAKA
(No more business)
73 | P a g e
Wote hao walikuwa na malengo ya kuhakiki WANAPENDA ila
WALIISHIA MAUMIVU.
SEX AS A RETURN;
Wapo ambao wao hawakutoa NGONO kuonyesha
WANAPENDA ila WALITOA kama KULIPA FADHILA.
Kisaikolojia wasichana wengi hudhani zawadi kubwa
wanayoweza kumpa mvulana au mwanaume aliyemsaidia sana
kwenye eneo flani maishani mwake ni NGONO. Na ndio
maana wapo waliosaidiwa ADA wakatoa NGONO kama
FADHILA, Wapo waliopewa sana matumizi na wavulana wao
au wanaume wao wakawapa NGONO kama malipo. Wapo
waliopewa ama kusaidiwa MITIHANI wakatoa NGONO kama
MALIPO. Matukio haya ni mengi sana na wasichana wengi
kwa kukosa akili wamejikuta wakiangukia pua.
74 | P a g e
msichana atakapoolewa pia ni ile nguvu ya upatanisho
(Gameo) (Intimacy) inapotolewa kwenye ndoa kama Agano la
ndoa. Agano halisi la ndoa limefichwa kwenye bikira na ndio
maana kibiblia anaekutoa bikira ndie mumeo halali, maana
kwa kukutoa bikira mmeingia nae agano la ndoa. Yaani nafsi
zenu zimeunganishwa ninyi tayari ni mwili mmoja. Hivyo
usifikirie BIKIRA iliwekwa tu kuna siri kubwa mno na faida
kubwa nyuma yake na ndio maana msichana akitolewa bikira
anasema ametolewa usichana wake yaani ule utu, thamani,
heshima na ubora wake unafutika. Na kwa taarifa yako
MATATIZO ya ndoa nyingi za leo yalifunguliwa mlango hapa
kwa sababu tu Mungu aliweka tendo la ndoa ndani ya ndoa,
watu wakakiuka kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa
“NGONO”, kama ulitolewa bikira nje ya ndoa unahitaji TOBA
na kuvunja agano batili uliloweka ili uingie kwenye ndoa
ukiwa na furaha na amani (Zingatia huu ushauri)
75 | P a g e
o Magonjwa ya zinaa kama Ukimwi, Kisonono,
Kaswende n.k.
o Aibu kwa familia na kwa jamii
o Kutoridhishwa kimapenzi na mumeo
o Mlango kwa mapepo na nuksi kukutawala.
76 | P a g e
MISTAKE 15:
YOU WANT MEN TO BE LIKE YOU!
(UNATAKA MWANAUME AWE KAMA WEWE)
*Hili kosa ndicho chanzo kikubwa cha migogoro na
kutoelewana kwa msichana na mvulana ndani ya jamii na hata
kwenye mahusiano. Na kama watu hawatajifunza juu ya hili,
bado na daima litaendelea kuwa tatizo.
77 | P a g e
1. Mwanaume yeyote duniani anahitaji KUHESHIMIWA
(Respect), hii ndio asili yake aliyoumbiwa na Mungu,
na ukitaka mgogoro, vurugu au vita na mwanaume
yeyote usimuheshimu ila ukitaka akupende mpaka
uchanganyikiwe mheshimu.
Mwanamke yeyote duniani anahitaji KUPENDWA
(Love), hii ndio asili yake aliyoumbiwa na Mungu.
Anahitaji aonyeshwe anapendwa, anataka aonekane
yeye ni muhimu, maalum na wa pekee. Umjali na uwe
na muda nae.
Men need RESPECT, Woman needs LOVE!
78 | P a g e
Men needs RECREATIONAL COMPANIONSHIP,
Women needs CONVERSATION!
79 | P a g e
TOFAUTI ZINGINE:
Kwenye tukio lolote fahamu kwamba mwanaume hufikiri kabla
ya kutenda na ndipo hisia juu ya jambo huja baadae, “They
are logical thinker” na ndio maana ni ngumu sana mwanaume
kuonyesha hisia yake kwa haraka kwenye jambo. Na hii ni kwa
sababu ya mfumo wa ubongo wake ILA Mwanamke hisia huja
kwanza kabla ya kufikiri, na ndio maana wanawake ni watu
wenye hisia kali sana juu ya jambo lolote, “They are Emotional
Feeler”
KWENYE TATIZO:
Wanawake wengi linapotokea tatizo kwa sasabu wao hisia
huja kwa haraka huwaona wanaume kama watu wasiojali na hii
ni kwa sababu wanaume si wepesi wa kuonyesha hisia zao,
najua leo umejua kwa nini mwanaume huonekana kama hajali,
ni kwa sasabu hisia zao zipo mbali sana.
MAONGEZI:
Daima MWANAUME huongea jambo alilolifikiri bali
MWANAMKE huongea jambo kutokana na hisia si fikra.
MUONEKANO:
Daima MWANAUME hupenda tu alivyovaa bila kujali
NYUMBA anayokaa imepangikaje au imependezaje i.e.
nyumbani mwanaume hutupa vitu shabalabagala ILA
80 | P a g e
MWANAMKE yeye hupenda nyumba ionekane nadhifu na
imepangika vizuri muda wote, mgogoro mkubwa ni pale
mwanaume anapotupa vitu ovyo.
81 | P a g e
82 | P a g e
MISTAKE 16;
YOU SEARCH FOR GREEN PASTURES!!
[UNATAFUTA PENYE UWEZO (UTAJIRI)]
Ni kweli kwamba karibu wasichana wote huwa wanapenda
sana ulinzi/ uhakika wa maisha (Life Security). Na hii
inatokana na jinsi walivyoumbwa, sina tatizo na hilo ILA sasa
wapo wasichana ambao wamejiwekea akilini kamwe
hawataolewa na wanaume wasio na uwezo mzuri wa kifedha.
Wapo wengi walikuwa na msimamo kama huu na walifanikiwa
kuolewa na watu wenye uwezo mzuri wa kifedha ILA mwisho
wa siku waliishia manyanyaso, mateso na utumwa. Unajua
kwanini? Ni kwa kuwa waliolewa na fedha na sio mtu mwenye
UPENDO wa DHATI kwao. Biblia inasema hivi;
83 | P a g e
KWA DHATI NA UNAEMPENDA KWA DHATI kuliko
kukimbilia mali na fedha bila kujua kwamba NDOA ni mkataba
wa maisha yako yote.
SHUHUDA:
“Mamangu mdogo ameolewa na mtu tajiri sana ila mateso
anayopata ni bora na kuishi maskini, maana fedha, nyumba na
magari havimpi amani kwa jinsi mume wake anavyomfanyia”
Kijana mmoja rafiki yangu alikuwa akinihadithia
“Dadangu ameolewa na tajiri sana ila mateso anayopata
imebidi awe anatoka nje ya ndoa”
Mifano ya shuhuda nilizokupa si maigizo au hadithi za
kutunga au kudhania ni vitu halisi kabisa vinavyotokea.
84 | P a g e
wakubwa zangu watanicheka, na yanayofanana na hayo.
Badala yake huachana nao na kwenda kuolewa na watu
wasiowapenda ila wenye uwezo ili tu kuwafurahisha wazazi,
kanisa, ndugu, jamaa, na marafiki, jambo ambalo ni ujinga tu
kama ujinga mwingine.
85 | P a g e
Mtazamo wa wazazi wako wanapokataa usiolewe na fukara au
mtu asiye na uwezo au ambae hajasoma sawasawa ni
kukuwekea UHAKIKA, ULINZI, WA MAISHA YAKO (Life
Security), KUTUNZA HESHIMA YA FAMILIA (Family Respect)
i.e. Mtoto wetu kaolewa na jamaa mwenye uwezo flani na
elimu flani, KULINDA UANACHAMA / USHIRIKA WA
KANISA e.i. usiolewe na watu dhehebu flani wao hawajaokoka
sawasawa hivyo hatuchangamani nao, na katika haya yote wala
hakuna cha unampenda au la au hata wajiulize kuna kusudi la
Mungu hapo, au mmejipangaje kuishi.
86 | P a g e
walezi au marafiki. Na KAMWE usiolewe na elimu, umaarufu,
pesa, nyumba na magari, Olewa na mume umpendaye.
Nyuma ya kupendana na kukubaliana kwa dhati huku mkimcha
Mungu na kuishi kwenye mahusiano yenye USHUHUDA kuna
Baraka za Mungu haijalishi mkoje.
87 | P a g e
Toka kwa Bro.Elly 24/7; “Ukifahamu kwa kina maana ya
NDOA na yaliyomo ndani ya NDOA, utamuangalia Zaidi
anayekuoa kuliko alichonacho anayekuoa”
88 | P a g e
MISTAKE NO 17;
YOU FORGE TO BE WESTERN GIRL!
(UNALAZIMISHIA UZUNGU)
Wasichana wengi tulionao ni wazuri sana kwenye kuiga
mambo yanayofaa na hata yasiyofaa {Imitation} toka kwa
wanawake wa Magharibi i.e Ulaya na Amerika. Yale mazuri
kama kujituma kusoma na kufanya kazi kwa bidii ni faida
kubwa kwetu tukiiga, LAKINI pia ipo mitindo ya mavazi na
nywele ambayo hayakudhalilishi wala hayaharibu utu wako si
mbaya ukiiga. Ila sasa wanachovaa wengi wa wasichana ni
majanga, aibu na kujidhalilisha kwa maisha ya mwanamke wa
kiafrika. Tukubaliane tu kwamba mazingira yote duniani au
maeneo yote duniani yanaongozwa na namna flani ya
utamaduni, na kwenye hilo eneo ukiishi kulingana na
utamaduni wao hakuna atakaekulaumu wala kukushagaa, ILA
ukienda kinyume na utamaduni wa eneo husika kila mtu ndani
ya eneo hilo atakushangaa, atakulaumu, atakusema na
pengine watakuchukulia hatua ya kinidhamu.
Yapo mambo wanayofanya wasichana wengi siku hizi
yanayotokana na KUIGA NJE ambayo yamewafanya kuonekana
vituko na balaa ndani ya jamii. Na wapo wengine ambao
walizidisha hayo mambo kiasi cha kufundishwa adabu na
heshima kwa kudhalilishwa. Kwa mfano; Nimewahi kuona
baadhi ya wasichana waliovaa mavazi yanayoonyesha sehemu
89 | P a g e
nyeti za miili yao wakikamatwa na kuchaniwa nguo pamoja na
kuchapwa. Mifano hii ni mingi sana, na kumbuka wapo ambao
walitolewa kanisani na kuonywa huku wakipewa kanga
wajisitiri.
90 | P a g e
za kuvaa wakati wa kulala hizo hazifai kutembea nazo mtaani,
zipo nguo watu wanavaa nyumbani wakiwa na wapenzi wao
au honeymoon, hizo hazivaliwi barabarani au kanisani.
Wenzetu wanavaa nguo fupi sana wakija Africa ni kwa sababu
wamezoea baridi kali huko kwao na hapa ni joto kali ndio
maana inabidi wavae hizo ili wapunguze joto. Wewe unaona
UNAIGA ili tukuite umeendelea au umekua mzungu.
91 | P a g e
na kumuhusudu na hata kutamani kuwa kama yeye? Kwa nini
na unafaidikaje?
Toka kwa Bro.Elly 24/7; “Vitu vyote na watu wote ambao
dunia imewapa thamani ni wale ambao walikuwa halisi kwenye
mambo yao na hawakuiga toka kwa wengine. Japo walijifunza
kutoka kwa watu wengine bado walibaki halisi na hawakuiga
kutoka kwao. Ukitaka thamani na heshima kuwa halisi na wa
kipekee”
92 | P a g e
MISTAKE NO 18;
YOU BELIEVE IN MORE THAN IMPOSSIBLE
CHANGE.
{UNAAMINI KATIKA BADILIKO LISILOWEZEKANA KABISA}
Wasichana wengi ni wazuri kwenye kulazimishia mambo
wanayoyapenda. Halikadhalika kwenye mahusiano ndio kabisa
wana imani kubwa isiyo na matendo tena katika
lisilowezekana. Labda nitoe mifano mizuri tu ili ikusaidie
kugundua nini maana ya kuamini katika badiliko
lisilowezekana.
93 | P a g e
kwenye huo uhusiano kuna KUSUDI LA MUNGU njia itafanyika
LAKINI tofauti na hapo ataigiza ameokoka na kanisani ataenda
na haitoshi atanena kwa kugha ILA akishakupata kwa kuwa
ALIKUOKOKEA na ameshapata alichokitaka utaona rangi zote
za Misri. Tena wengine huwa wanasema ukitaka kunioa
HAMIA KANISANI KWETU ni kweli atahamia ila mwisho wa
siku akitimiza lengo ATARUDI ALIPOTOKA. Na ukumbuke si
jambo jepesi sana kufahamu kama kuna kusudi la Mungu au la
ikiwa tayari umeshaingia kwenye hisia za kimapenzi na
mahusiano.
94 | P a g e
KUSOMA NA AELEWE maana INAUMIZA. Hebu PIGA PICHA
YA HATMA YA HIYO NDOA!
“Some people will never fit in your life no matter how much
you want them to”
95 | P a g e
alipopenda. HAKUNA JAMBO LINALOUMIZA NA KUTESA
KAMA KUMPENDA MTU ASIYEKUPENDA. “You better quit
faster”
“If you could love the wrong person that much, imagine how
much you could love the right one”
“We may love the wrong person and cry over the wrong
person, but one thing is for sure. Mistakes help us find the
right person”
96 | P a g e
MISTAKE 19:
YOU THINK BOOK IS EVERYTHING!!
(UNADHANI KUSOMA NDIO KILA KITU)
*Ili pia ni moja katika makosa makubwa wanayoyafanya
wasichana wengi. Wapo wasichana wanadhani KUSOMA
SANA ndio kila kitu kwenye maisha bila kujua KUSOMA ni
sehemu moja tu ya maisha na MAHUSIANO au KUFANIKIWA
ni sehemu nyingine ya maisha. Na ndio maana wapo
waliosoma sana lakini mpaka leo wana MAISHA DUNI, lakini
pia wapo waliosoma sana lakini bado MAHUSIANO na NDOA
zao zinawatesa si kawaida. Kwenye hili ni vizuri tusaidiane
kwa kina ili usiendelee kufikiri unavyofikiri na mwisho wa siku
ukateseka sana. Wengi wa wasichana wanawaza hivi.
97 | P a g e
2. NIKISOMA SANA NITAKUWA NA MALI ZANGU NA
HAKUNA MWANAUME ATAKAENITAWALA WALA
KUNIENDESHA:
Dhana nyingi potofu inayowatesa sana wanawake wasomi
wa leo ni hii ya kudhania kwa sababu ya elimu na mali
walizonazo basi hakuna mwanaume anaweza kumtawala
wala kumuendesha hata kama ni mume wake.
Nikukumbushe tu kwamba moja ya hitaji kubwa alilonalo
mwanaume yeyote alilopewa na Mungu ni kutaka
HESHIMA (Respect). Mwanaume ameumbwa kuwa kichwa
cha mwanamke, na hii ni asili ya kiMungu. Na ndio maana
unaweza kumtawala kwa muda ILA siku akikubadilikia
hutaamini kitakachotokea.
Hii ndio sababu kubwa ya familia za wanawake wasomi
wengi kuwa na migogoro ama hata ndoa kuvunjika.
Mungu akusaidie sana hata kama utasoma kwa kiasi gani
utambue nafasi na heshima ya mume wako ndani ya
familia bila kujali ana elimu gani au uwezo wa fedha kiasi
gani.
98 | P a g e
mahusiano karibu 80% zina matatizo na migogoro
mikubwa, Na wapo waliokua na ndoto kama yako LAKINI
waliangukia kwa wanaume wasiojielewa na wengine
wanazeeka hawajapata bado wanaume waliowataka.
USIJIDANGANYE.
99 | P a g e
afya, mahusiano na chochote kile. UKIMPATA YEYE NA
KUMPOKEA KWA UAMINIFU UMEPATA VYOTE, MPOKEE
LEO, MWITE YEYE ATAITIKA, YU KARIBU SANA KULIKO
UNAVYOFIKIRI.
100 | P a g e
MISTAKE 20:
YOU USE TO GENERALIZE MEN!!
(WANAUME WOTE NI SAWA TU)
Mojawapo ya mambo yanayowaangusha wasichana wengi
kwenye mahusiano ni kitendo cha kudhania kwamba wanaume
wote ni sawa tu. Kiasi kwamba tabia ya mwanaume flani ndio
tabia ya wanaume wote, kwa hiyo kwa sababu wanaume
wengi ni waongo basi wanaume wote si waaminifu. Inaweza
kuwa True but not Truth, na inaweza kuwa Real but not Reality.
101 | P a g e
Lakini pia WASICHANA wengi hudhani kwamba kila mvulana
anaekuonyesha kutaka kukuuliza kitu au kuwa karibu na wewe
eti ni njia ya kukutaka na wengine hii imewatesa sana nafsini,
kiasi cha kudhania labda huyu mvulana anaogopa kumwambia
au si mzima labda, BILA kujua wapo wavulana wanaotaka
urafiki wa kawaida ambao hauna cha kufanya na mapenzi.
102 | P a g e
anamfanyia au afanyiwe kama baba yake anavyomfanyia mama
yake au kaka yake anavyomfanyia wifi yake. Utasikia “MBONA
DAD WANGU HAFANYAGI HIVYO KWA MAMY?” “MBONA
KAKA YANGU HAMFANYIAGI HIVYO WIFI YANGU?” Sikiliza
hili na likufae
103 | P a g e
Toka kwa Bro.Elly 24/7; “Si kila unachokifikiri na kukisikia
kuhusu wanaume kinaweza kuwa sahihi kwa kila mwanaume.
Halikadhalika wapo wanaume waaminifu na wanaojielewa tena
wenye hofu ya Mungu japo hawapatikani kirahisi mpaka
umetengeneza mazingira sahihi ya kiMungu kuwapata. Na
ifahamike wazi hautowapata mpaka umeamini kwamba wapo
na ukamuomba Mungu akukutanushe na wa kwako.”
104 | P a g e
MISTAKE 21;
YOU ALWAYS HAVE A PLASTIC FACE!
(U MZURI WA KUIGIZA) (Pretending)
105 | P a g e
“Don’t be in a relationship, if you’re going to act single”
106 | P a g e
ndani ana maumivu makali anaweza akakwambia “FANYA
UTAKAVYO” ili ndani yake anateseka mno.
“When you say “Yes” to others make sure you are not saying
“NO” to yourself”
Paulo Gelho
107 | P a g e
BE A WOMAN OF INTEGRITY;
“Integrity is doing the right thing when no one is watching”
Myles Munroe
108 | P a g e
Jisamehe wewe binafsi, samehe wengine, sahau
makosa, jifunze kutokana na makosa NA yatumie haya
makosa kwenda kiwango kingine.
2. “Cry as much as you want to, but just make sure when your
finished you never cry for the same reason again”
“Nothing wrong with apologizing but saying
“I’M SORRY” does NOTHING when you continue to
make the same mistakes”
“You can NEVER MAKE SAME MISTAKES TWICE….
Because the second time its not a mistake…...its a
CHOICE”
109 | P a g e
110 | P a g e