You are on page 1of 1

CHAMBO ni mfumo wa hatua nne wa kufanya bidhaa au huduma ambazo zitampelekea mteja kutaka

kuendelea kuzitumia tena na tena. Mfumo huu unaanzia mwanzoni mwa tangazo ama katika
uwasilishwaji wa taarifa Fulani ambayo inahusu bidhaa au huduma itolewayo na biashara yako.
Hatua hizo ni:

1. Kichocheo: Mfumo huu huanza kwa kichocheo ambacho kinamshawishi mtumiaji kufanya hatua
fulani. Kichocheo kinaweza kuwa cha nje (kama vile tangazo) au cha ndani (kama vile mawazo,
taarifa au hamu ya kutaka fahamu zaidi juu ya kitu).

2. Hatua: Hatua inahusisha kitendo kinachofanywa na mteja, kwa mfano kusoma kilicho andikwa au
kutaka kujua zaidi kuhusu bidhaa au huduma. Mteja atachukua hatua kuelekea juu ya kile
alichokiona kimemvutia. Hatua hii inapaswa kuwa rahisi mteja kuifanya na ya haraka.

3. Tuzo: Baada ya mtumiaji kuchukua hatua, anapaswa kupata tuzo ambayo inamfanya aendelee
kufanya alichokua akikifanya. Tuzo hii inaweza kuwa ya kipekee au ya kawaida, lakini inapaswa kuwa
ya thamani kwa mteja. Mfano huenda ikawa ni ofa mbalimbali ambazo zenye thamani kwake.
Kikubwa aone kama anathaminiwa na kafika sehemu sahihi.

4. Uwekezaji: Mwisho, mteja atajikuta anapaswa kuwekeza kitu, kama vile muda au pesa, katika
bidhaa au huduma. Hii inaweza kumaanisha kufolow profaili au kuwasiliana na wahusika kuusu
bidhaa au huduma. Kwa kufanya hivi, mteja anajihusisha zaidi na bidhaa na anakuwa na uwezekano
mdogo wa kuachana nayo.

Mfumo huu unatumika sana katika kucheza na akili ya mteja. Na unaanza kufanya kazi baada tu ya
kutanguliza zawadi ama ofa mbali mbali kwanza kwa mteja, kabla mteja ajaanza kuamua kununua
unchokiuza, kuendelea kukusikiliza, kukufolow au kufanya chochote kile ambacho kina manufaa
katika biashara yako. Mfumo huu ukifuatwa vizuri kwa ufanisi matokeo yake ni makubwa.

You might also like