You are on page 1of 32

NEXT SEMESTER

Written by

Maximilian Rioba

Based on true events

mrioba@me.com
+255715167419
EXT. MTAANI - MORNING

Tunafungua shot yetu na kumuona mtu mzima Mr. Malamsha (65)


amevaa koti jeusi, amebeba mfuko wa nailon anakimbia kwa kasi
kuwahi basi kituoani. Anapigiwa simu na kondacta kumhimiza ni
yeye tu amebaki ili basi liondoke.

MALAMSHA
Yaani naingia hapo dakika sifuri
mwanangu msiniache tafadhali
nawaomba.Stendi hii hapa naiona.

Anaongeza kasi huku akitweta na kuamini kwamba atawahi basi.


Ghafla wanakuja watu watatu nyuma yake wanakimbia zaidi yake
na kumpita, anawasemesha bila bila wao kumjibu chochote,
anaongeza kasi huku akipumua kwa nguvu.

MALAMSHA (CONT'D)
Jamani, kwema? Wote kumbe
tumechelewa? Mbona huyu kijana
kanidanganya kwamba ni mimi peke
yangu nimechelewa?

Tunaanza kusikia sauti ya radio call ya polisi kisha


tunawaona askari wawili wa kiume wakikimbia kuelekea upande
anakotokea mzee Malamsha. Kisha tunamuona askari mmoja wa
kike Detective Aysha (34) akiwa anashuka kutoka kwenye gari
akiwapa tahadhari wale askari wawili waliokuwa wanakimbia
huku wakiwa wameshikilia bunduki.

DETECTIVE AYSHA
Do not shoot until you hear from
me. Hakuna risasi hata moja
inayopigwa mpaka tuhakikishe ni wao
kweli. Copy?

Kunakuwa na ukimya kidogo. Detective Aysha anarudia


kuwasikitizia Kazola (36) na Masha (32).

DETECTIVE AYSHA (CONT'D)


Boys have you copied?

Wanajibu wote “Copy” huku wakiwa kwenye kasi kuwafukuza


wahalifu.

DETECTIVE AYSHA (CONT'D)


Wallah mpuuzi yeyote atakayeshuti
bila amri yangu atanijua mimi ni
nani. Enhe so what do we have here?

KAZOLA
Wauza unga wanne tumewakurupusha
wakiwa maeneo ya chuo cha ICU.
(MORE)
2.

KAZOLA (CONT'D)
Wakakimbia, wawili wameingia mtaa
wa Kizera nyuma ya hoteli ya Kusini
mmoja aliyekuwa ndiye prime
anaelekea mashariki karibu na hapo
ulipo afande. Najaribu kumtega
aingie kumi na nani then unipe amri
nimtoe roho.

DETECTIVE AYSHA
Okay, sikiliza Mazola, nakujua
vizuri sana. Kama unaweza kumkamata
bila kumpiga risasi get his ass
atatusaidia sana upelelezi. Do not
shoot hadi uone imeshindikana. And
besides unajua kabisa bila evidence
kwamba anauza au amebeba dawa za
kulevya hurudhusiwi hata kumfinya,
Umenisoma?

KAZOLA
Kuna haja gani afande kufanya kazi
kwa vikwazo kiasi hicho? Eddy Big
na Kalito wanajulikana.

DETECTIVE AYSHA
So huyo ni Kalito au Eddy Big?
Which one is he?

KAZOLA
Huyu atakuwa ni Kalito.

DETECTIVE AYSHA
Kazola, please don’t make my
morning stressful. Narudia tena, Do
not freaking shoot hadi uwe na
uhakika. Copy?

KAZOLA
Tunakimbizana na wahalifu wanaouza
dawa za kulevya kwa wanafunzi wetu
and then unanipangia namna ya
kumkamata? Kweli afande? Ni sawa
hiyo?

DETECTIVE AYSHA
Have you copied?

Wakati Kazola akijieleza ofisa wa pili Masha anawapa tip


kwamba amemuona mtuhumiwa akikimbia kuelekea mashariki ambapo
ofisa wa kwanza anatokea.

DETECTIVE AYSHA (CONT'D)


Masha una uhakika umemuona?
3.

MASHA
Nimemuona afande, anakuja upande
huo ameshikilia mfuko ana koti
jeusi na T-shirt nyeupe
iliyochafuka chafuka.

Kazola anasikika akionge kwenye radio kwa sauti ya pole pole


akisisitiza kwamba anamuona suspect mbele yake na ana uhakika
ni yeye. Detective Aysha anamkataza kushuti, anamwambia
amkimbize na kumuamuru asimame. Kazola anakaidi boss wake
anachomwambia. Nakimbia kwa kasi zaidi kumsogelea suspect.

DETECTIVE AYSHA
Do not shoot. Kazola, narudia do
not shoot. Mkamate bila kumjeruhi.

MASHA
Afande hao watu ni wabaya sana.
Akigeuka akamuona Kazola
anamkimbiza atamuua. I suggest a
shoot.

DETECTIVE AYSHA
I said do not shoot.

KAZOLA
Suspect ana mfuko nahisi una gun.

DETECTIVE AYSHA
Kazola, usiipime imani yangu. How
far are you to the suspect?

KAZOLA
Kama mita 25 hivi.

DETECTIVE AYSHA
And you are sure ni yeye?

KAZOLA
Asilimia mia moja afande.

DETECTIVE AYSHA
Mita 25 unaweza kumuamuru asimame
anyooshe mikono juu na aweke chini
kila alicho nacho.

KAZOLA
Anaongeza mbio afande. Please let
me finish him, atatuponyoka huyu.

Ghafla Kazola anapiga risasi tatu na zote zinampata suspect


mgongoni. Anaanguka huku Kazola akikimbia kuelekea alipo.
4.

INT. LUXURIOUS HOTEL ROOM - NIGHT

Tunamuona mwanamama tajiri WaColor (54) akiwa amekaa


anaangalia video kwanye iPad huku akiongea na simu akiwa
amevaa AirPods. Anaonekana kumpa maelekezo mtu aliyekuwa
kwenye party.

WACOLOR
Nimempenda huyo mwenye nguo ya
njano hapo. Get her. Also mchukue
huyo mweusi hapo nyuma.

JACKIE
What about this one nanayeingia?

WACOLOR
I don’t like her chest.

Music unaendelea tunaingia kwenye house party tunaona


wanafunzi wamependeza sana wana enjoy. Kuna wengine
wanaogelea kwenye swimming pool. Tunamsikia DJ Wonder (29)
akiwarusha kwa muziki na kuwapaisha waliopendeza.

WONDER
Oh yes, I see the leadies looking
steaming hot. Kama una u feel mziki
don’t feel shy to show us what your
momma gave you, step to the dance
flow baby, you only live once.
Where my first year ladies at? Let
me hear you say yeeeeah!

First year wanaitikia wote “Yeeeeeeah”

WACOLOR
Get that one anayeongea na mwenzake
pale pembeni.

JACKIE
Nimemuongelesha alivyoingia, she’s
kinda shy. Do you think atakufaa?

WACOLOR
Shy girls are the best. Get her.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - DAY

Tunawaona wanafunzi watatu wakihudumiwa kwenye meza yao


kwenye house party. Wanaonekana wenye furaha sana.
5.

Hawa ni Sam (22) Nayda (18) na Maria (18) Ni marafiki amabao


pia wamekuja kwenye party. Nayda anamnong’oneza Maria kitu,

NAYDA
Mbona you told me it was just a
birthday party ya Sam? What’s with
all this?

MARIA
Ask him, si huyu hapa? Eti babe
Nayda anasema mbona hii party is
more of a house party than a
birthday party? What’s up?

SAM
Hey, it’s a combo. Let’s just have
fun guys, okay? Drink, eat, merry,
and do whatever you want to lit up
the vibe.

NAYDA
You know sinywi pombe, right?

SAM
Oh, I din’t know, kwa nini?

NAYDA
Beacuse nimeamua, I don’t want to
consume alcohol or smoke. Do you
have a problem with me not drinking
and smoking?

MARIA
Kwani is it a must, babe leave
Nayda alone. There are a million
ways to have fun in this world than
drinking and smoking.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY PARKING LOT - NIGHT

Tunaona vijana wanne kwenye parking lot wanavuta bangi na


sigara wameegemea gari kali. Mmoja anauliza.

BOY ONE
Yoh, hivi mnauhakika kweli Vamps
halijui hili so?

BOY TWO
Mwana kwanza mchana mimi nilikuwa
naye chuo. Hajui chochote. Angekuwa
anajua angeshakinukisha
6.

BOY ONE
Ameshafika hapa kwani?

BOY THREE
Nimemuona na pisi yake ile ya first
year and another chic. Wako ndani.
Twenzetu.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - NIGHT

Nayda anaona mtu anapitisha edible cup cakes. Wakati huo


tunamuona kwenye background Maria amejitenga pembeni akiongea
na simu wakati Nayda na Sam wanaongea huku wakionekana busy
kila mmoja na simu yake.

NAYDA
I can have a cup cake and soda. It
that okay Sam?

Sam anajua kuwa cake zina bangi. Anamuangalia kwa jicho flani
akiamini kwamba baada ya kula cake Nayda atapagawa na bangi.

SAM
Sure, you can definitely have cup
cakes, and have them abundantly.
Usijali, nalipia mimi. Excuse me
miss, can you bring my friend some
cup cakes and a cold glass of coke
please?

NAYDA
Diet coke!

USHER
Sure, nimletee cup cakes ngapi?

SAM
Kama mbili hivi. Au unataka ngapi
Nayda?

NAYDA
Nne, please. And the coke should be
very cold, okay?

SAM
Sure, mletee mambo. Coz after that
we are really gonna party for real.
Afu Maria anaongea na nani at this
hour while I’m here, on my
birthday?
7.

NAYDA
Heh, Sam embu acha hizo basi, you
think she’s cheating? Anaongea na
sister ake bana hebu chill kha!

Kamera inaondoka na Sam akielekea alipokuwa amesimama Maria.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - NIGHT

Sam na Maria wanaonekana wanaongea in a romantic way huku


Maria akimalizia kuongea na simu.

MARIA
Yaani mpaka summer ndiyo uje?
That’s like forever sis.

MARIA’S SIS
Girl summer is just around the
corner. Ntakuja tu. Vipi birthday
boy hajambo?

MARIA
He’s here thinking that I’m talking
to some guy. Kaniganda like an eel.
Talk to him.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - NIGHT

Tunamuona msichana mrembo Tracy (21)akiwa na rafiki zake wa


kike kwenye VIP lounge wanavuta shisha wanakunywa drinks za
bei ghali na ku enjoy. Tracy anaongea na mtu kwenye simu
ambaye ni lecturer wake wa chuo Mr. Kitanjei (54)

TRACY
She’s here with her nerdy little
boyfriend.

KITANJEI
Kwa hiyo tunafanyaje sasa?

TRACY
You know nimesikia semester hii una
course mbili unatufundisha, right?

KITANJEI
Absolutely.
8.

TRACY
You want Maria, I want my grades,
it’s a fair trade.

CUT TO:

INT. MARIA’S HOUSE - NIGHT

Tunamuona Aysha (38) akiamka na kuangalia saa kwenye simu.


Anamuangalia mume wake ambaye anaonekana amelala. Aysha
anaamka na kushuka kitandani. Anaangalia kwenyenight stand
ambapo anaamini aliweka ufunguo wa nyumba anaukosa. Anatoka
chumbani kwao na kwenda chumbani kwa Maria. Anapoingia
anawasha taa na kuona Maria amelala. Anasogea kitandani na
kumgusa. Anakuta ni nguo zimepangwa tu. Maria hayupo.
Anazitupatupa hizo nguo na kurudi chumbani kwa haraka.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - NIGHT

Tunamuona Maria akiangalia kwa mbali na kushangaa Nayda


anachokula.

MARIA
Baby, is she...

SAM
Relax baby, she’s going to be okay
bana. Just a couple of edibles
nothing much.

MARIA
Sam, what do you mean nothing much?
It’s edibles! Ni bangi!

SAM
Why are you shouting?

MARIA
Hivi do you have any idea
nimewezaje leo ijumaa kutoka and
come to your stupid birthday? Any
freaking clue?

CUT TO:

INT. MARIA'S HOUSE - NIGHT

Tunamuona baba Maria akijaribu kumpigia Maria simu arudi


nyumbani haraka. Simu ya Maria haipatikani.
9.

Anasikia mke wake akija anaiweka simu pembeni anazuga kama


amelala. Aysha anaingia chumbani kwao. Anawasha taa na
kumuangalia mume wake ambaye anazuga kwamba kalala na
amegeukia upande mwingine.

AYSHA
Where is Maria?

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - NIGHT

Tunarudi kuwaona Sam na Maria wakiendelea kulumbana

SAM
Maria why are you making a big deal
out of this?

MARIA
You, mh….. grow up Sam.

SAM
What? Seriously?

MARIA
Mh.. you know what, we are leaving.
Enjoy your birthday.

Maria anamuacha Sam na kuanza kutembea kutembea kuelekea


alipokuwa amekaa Nayda.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - NIGHT

Tunamuona Tracy akifatilia malumbano ya Maria na Sam kwa


mbali. Ananyanyuka na na kuweka shisha yake chini na kuanza
kumfuata Maria haraka.

TRACY
Hey, Is he acting a fool?

MARIA
No, he’s just being himself

TRACY
Boys always do, you need a man.

MARIA
But I love my boy.
10.

TRACY
Maria, stop wasting your time. Hivi
unajua bado anakuulizia? Nilikupa
namba yake but hujampigia wala kum
text, kwa nini?

MARIA
It’s hard for me to give him what
he wants. I wish anielewe tu. I
have one boyfriend and that’s it. I
can’t mix men like clothes.

TRACY
Who said he wants to be your
boyfriend?

MARIA
Tracy, the answer is no. I can’t be
his sex buddy, side chic, mistress,
one night stand or anything like
that.

TRACY
Sweetie, there’s sex that takes you
nowhere.

Anatokea mtu mtanashati sana amevalia vizuri sana.


Anamsalimia Tracy kwa kumbusu mkononi. Tracy anamuita usher
na kumwambia ampeleke mgeni wake VIP.

TRACY (CONT'D)
I’ll meet you at the VIP darling.

MARIA
Wait, is that Oscar Delarento?

Tracy anachukua champagne kutoka kwa mhudumu kwa madaha na


kuendelea kuongea na Maria.

TRACY

And there’s sex that takes you


everywhere.

MARIA
I have never had sex before. Not
even with my boyfriend. So I’m
definitely going somewhere, if you
ask me.

TRACY
There is always a power dynamic at
play, sweetheart. Even a broken
clock is correct.
11.

MARIA
Twice a day!

TRACY
You know there’s a first time for
everything Maria, right?

MARIA
Right! And when the first time of
anything is done at the right time,
the right way it becomes more
meaningful than kukurupuka bila
mpango.

Tracy na Maria wanaendelea kuongea wakati kamera imehamia kwa


Nico na Sam.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY

Tuna muona mtu mmoja mwanaume Nico (30)anatembea kuelekea


pale Sam aliposimama kwa madaha na kumtoa pembeni kidogo.

NICO
Kitu chochote kile kisije
kukutenganisha na upendo wa kweli
Sam. Hiyo ndiyo hulka ya uanaume wa
kweli.

Kunatokea ukimya kidogo.

NICO (CONT'D)
Wakati unajitahidi kuendelea
kulinda na kulithamini penzi lako
kumbuka kwamba adui halai hata
kidogo. Hata usiku kama sasa hivi
yuko macho. Look at her! Una kazi
bro. Na hiki kilichotokea leo, hii
party, drinks, music and all ni
sehemu ndogo sana ya mengi
tuliyokuandalia. Lakini ni lazima
unifanyie favor kidogo. Maelekezo
yote yako humo kwenye zawadi.
Ukikwama nipigie. Happy birthday
boy!

Sam anamshangaa Nico huku anaangalia mfuko aliopewa na Nico.


Kuna simu kwenye mfuko. Inaita. Nico anamwambia aipokee.
Kisha Nico anaondoka. Sam anashangaa kisha anaipokea.

SAM
Hallo!
12.

WACOLOR
Happy birthday Sam.. Rafiki zako
wamekuingiza kwenye matatizo
makubwa sana. Sijui kama unalijuia
hilo.

SAM
We ni nani?

WACOLOR
Mimi ni msamaria mwema na nataka
nikusaidie usiku huu huu yaishe.

SAM
What are you talking about?

WACOLOR
Wiki mbili zilizopita kuna watu
walikuletea assignment uwasaidie.
In the process waka botnet computer
yako.

A moment of silence.

WACOLOR (CONT'D)
Najua unawasaidia wanafunzi wengi
sana wa IT chuoni. Na sio rahisi
kuwakumbuka wote. But hawa watatu
walikuletea assingment inayohusu
hacking ya system, ukawasaidia
ukidhani ni assignment tu kumbe
ilikuwa ni real deal. Wakafanya
Exfiltration, wakaiba fedha za chuo
shilingi milioni kumi na
kusababisha leakage ya mitihani. Do
you remember?

SAM
No, I don’t.

WACOLOR
You know Vamps right?

Sam anashangaa kusikia hivyo maana Vamps ni jina analotumia


kwenye kikundi chao cha wanafunzi wa IT.

WACOLOR (CONT'D)
I am Vamps.

WACOLOR (CONT'D)
Then you know what I’m talking
about.
13.

WACOLOR (CONT'D)
You are facing 25 years maximum
jail time and this will escalated
by the judges based on the nature
of the crime.

SAM
They said it was an assignment

WACOLOR
Which turned out to a be punishable
offense.

WACOLOR (CONT'D)
You are a good kid and I know
hukuhusika kwenye huo wizi. Ndo
maana tunataka kukutoa from this
ASAP.

WACOLOR (CONT'D)
You are aware that your birthday
party is mixed with my house party
kwa makusudi kabisa na tumeingia
gharama just to have you enjoy your
day, right?

SAM
Ameniambia Nico, asante sana.

WACOLOR
Ondoka hapo sasa hivi, nenda mbezi
beach mtaa wa Duma nyumba namba 7
utakutana na mtu atajitambulisha
kama Tisha. Atakusaida, kila kitu
kitaisha leo leo.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - NIGHT

Nayda akiwa ameanza kuwaka anamuona yule mhudumu aliyemletea


cup cakes before. Ananyanyuka kumuita. Tunamuona Nayda
anamkumbatia mhudumu huku akiwa ameshikilia cake moja ambayo
inamomonyokea mgongoni mwa yule dada.

NAYDA
Mimi napenda sana keki lakini
sijawahi kula keki tamu kama hizi.
(MORE)
14.

NAYDA (CONT'D)
Naomba niongezee nne tafadhali,
okay darling?

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - NIGHT

Maria akiwa na Tracy anamuona Nayda anavyokumbatiana na yule


dada. Anaondoka pale waliposimama na Tracy anaelekea mezani
Nayda alipo. Wakati huo mhudumu ameleta edibles nne kama
alivyoagiza. Anashika moja kutaka kuanza kuila, Maria
anamnyang’anya na kumwambia mhudumu arudishe tu.

USHER
But nimesha punch kule dear, nani
atazilipia?

MARIA
But hatujazigusa

NAYDA
Si tuziguse tu jamani? Kwani kuna
tatizo gani kwenye kugusa tu? “Just
a touch of love, a little bit”
Hahahaha. I bet you don’t know
nothing about that, do you?

MARIA
Can I use your phone?

NAYDA
Sure, simu yako imekuwaje kwani?

MARIA
Imezimika.

NAYDA
Washa mama, washa washa, washa moto
wa imani watu waungue, watubu
waache dhambi.

Maria anapumua kwa mshangao, anampigia Sam aje amsaidie


kumpeleka Nayda kwenye gari lakini Sam hapokei ameshaondoka
kwenye party.

CUT TO:

EXT. LUXURIOUS HOTEL BALCONY - NIGHT

WaColor anampigia Nico kushangaa kwa nini Tracy yuko hapo


kwenye party na bado huko hai.
15.

WACOLOR
Kwa nini huyo mgonjwa bado yuko
hai?

NICO
Hatakuwa hai baada ya masaa mawili
madam. Nimeshapanga kila kitu.

CUT TO:

INT. HOUSE PARTY TOILET - NIGHT

Tunamuona Maria akijaribu kumsaidia Nayda ambaye anatapika


chooni na ammtapikia Maria kidogo.

MARIA
What the hell? Why did you take all
that shit Nayda?

NAYDA
Achana na mimi Maria. Mi sio mtoto
wako. Mimi ni mtu mzima na uzima
wangu. Sihitaji chochote from you.
Niache.

MARIA
I need to help you clean and take
you to your room niende zangu home.
This is messed up for real Nayda.
You jumping on things you’ve never
tried before. Look at yourself now.

NAYDA
Kwenda zako mtoto wa mama wewe.
Kwanza you should stop worrying
about me. Mama ako anakuja
kukuchukua chuo kila Ijumaa kama
kitoto cha daycare basi
unajikuuuuta. Tena inawezekana
anakutafuta right now, Maria
Mariaaaaaaaa!

MARIA
Nayda, stop. Stop it right there.

NAYDA
Kwenda mtoto wa mama wewe. Mimi
mgumu sana Sio maandazi maandazi
kama wewe. Familia yangu ilishindwa
kuja kwenye graduation yangu.
Nilijidai tu niko pa lakini
niliumia sana.
(MORE)
16.

NAYDA (CONT'D)
Watu walikuja na ma V8, coster,
wakajiachia na familia zao kasoro
mimi tu. Lakini niliwatandika na
division one moja baab kubwa. Nalia
lakini naumia, mamamamamae. Usini
dictate kwenye vitu kama hivi
Maria. Let me have some fun. Kama
unasepa, sepa. Achana na mimi.

CUT TO:

INT. AYSHA’S CAR - NIGHT

Tunawaona Aysha na mume wake kwenye gari. Aysha anaendelesha


kwa kasi huku akiendelea kumgombeza mume wake.

AYSHA
Haki ya Mungu tusipompata mwanangu
leo utaondoka nyumbani kwangu.

CUT TO:

INT. HOUSE PARTY TOILET - NIGHT

Nayda na Maria wanaendelea kurushiana maneno pale chooni


wakati Maria akijaribu kumsafisha Nayda.

MARIA
I’m so sorry Nayda. Your past has
nothing to do with your present or
future. You can shape your future
from now baby.

NAYDA
Naumia sana. Hujui tu.

MARIA
I know baby, I do.

NAYDA
Sometimes natamani tu nife nipotee.
Nina uchungu sana Maria hujui tu.
My life we acha tu, usinione hapa
ukadhani niko poa naumwa moyo,
naumwa, naumia sana Maria, naumia
kuliko unavyojua.

Nayda anatapika tena kwa nguvu na kuanguka.

CUT TO:
17.

EXT. KIJIWENI WAZEE PLAYING BAO - DAY

Tunafungua shot yetu na drone shot ya kijiweni kamera


inaingia na kutuonesha wazee wakiwa wanacheza bao na kunywa
kahawa huku wakibishana huhusu Simba na Yanga. Tunamuona mzee
mmoja Bwana Malamsha (65) akigeuka kuangalia simu yake
ikiita. Anasogea pembeni kupokea huku akiwa na matumaini ni
simu ya heri. Anapokea huku akiongea kwa utani bila kuangalia
ni nani amepiga.

MALAMSHA
Kama ya kheri halo, kama ya shari
kata, mwenye simu hii hapokei tena
habari mbaya. Keshapigwa na maisha
vya kutosha. Halo nani mwenzangu?

Inasikika sauti kwenye simu, ni sauti ya binti yake Nayda


(18) ambaye yuko masomoni mkoani.

NAYDA
Asalaam Waleikhum Warahmatullah
Wabarakatuh. Mie jina langu Nayda
Bit Said Suleiman Hafidh.

MALAMSHA
Daaah, Waleikhum Salaam moyo wangu.
Nisamehe mama yangu mie, mama mzaa
chema Bit Said mwenyewe, moyo wa
mwanao Malamsha Bin Kombo, enhe,
vipi habari mwanangu, kwema?

NAYDA
Alhamdullilah baba, mie nimekupigia
kukupa habari njema.

Mr. Malamsha anajisogeza pembeni zaidi ili aweze kumsikia


mwanaye vizuri.

MALAMSHA
Enhe, nipe habari bibie.

NAYDA
Mwanao nimemaliza kidato cha sita
na wiki ijayo ndiyo tuna
graduation, baada ya hapo tunakaa
tena wiki moja tunafanya mtihani wa
Taifa, kisha narudi zangu nyumbani
kusubiria matokeo.

MALAMSHA
Daaah, ama kweli siku hazigandi,
tunmshukuru sana Mungu maana baba
yako hapa naona kama ndoto vile.
(MORE)
18.

MALAMSHA (CONT'D)
Ni juzi juzi tu ulikuwa la kwanza
leo umemaliza? Alhamdullilah kwa
kweli. Enhe sasa tunafanyaje mama
yangu?

NAYDA
Najua hali ya nyumbani ilivyo, ila
kama kungekuwepo uwezekano wewe na
mama mkaja kwenye mahafali nadhani
ningekuwa mwnafunzi mwenye furaha
kuliko wanafunzi wote hapa. Lakini
kama itashindikana baba usijali
naelewa kabisa.

Mr. Malamsha anatulia kwa sekunde kadhaa akitafakari ni nini


cha kusema huku akiwa amejaa huzuni kwamba ni jambo gumu sana
kwenda kwenye mahafali ya mwanae.

NAYDA (CONT'D)
Hello, baba upo?

MALAMSHA
Ninajisikia vibaya sana kwamba
sijawahi kufika shuleni kwako
mwanangu hadi leo unamaliza. Ni
aibu mimi kama baba yako kukosa
fedha hata za nauli tu Nayda.

NAYDA
Sio lazima baba, naelewa hali ya
nyumbani.

MALAMSHA
Nakushukuru mwanangu kwa uelewa.
Hiyo Kradeshin ni wiki ijayo tarehe
ngapi?

NAYDA
Ijumaa tarehe ishirini na saba.

MALAMSHA
Sawa mwanangu, kila la kheri.

Tunamuona mzee Malamsha akirudi kijiweni kinyonge tofauti na


alivyokuwa awali.

CUT TO:

INT. NYUMBANI KWA MZEE MALAMSHA - DAY

Tunamuona Mzee Malamsha akiongea kwenye simu na mdogo wake


aitwaye Farid (54) kuomba achangiwe kwenda kuhudhuria
mahafali ya binti yake mpendwa.
19.

MALAMSHA
Unajua yale mnayoyasema hamyajui
hata kidogo. Kumpa mtoto wa kike
fursa ya elimu ni jambo la pekee
sana.

FARID
Na ndiyo maana tulikwambia umuoze
alipomaliza form four ili kaka
uepukane na hizi adha za kuomba
omba msaada. Akina Zuwena si rika
lake huyo? Mbona wameolewa na
hatushughuliki nao tena?

MALAMSHA
Farid, wewe ni mdogo wangu kabisa
ujue.

FARID
Mama mmoja baba mmoja lakini kaka
wewe mbishi sana, ulitaka
kutuaminisha kwamba Nayda ndiye
mtoto mwenye akili kuliko watoto
wote wa ndugu zako. Beba sasa
msalaba umsaidie.

Wakati anaongea hivyo mama yake Nayda aitwaye Bi Nusrah (56)


anaonekana kutamani kuingilia mazungumzo. Anakatishwa

NUSRAH
Shemeji Farid mbona uonaongea
maneno kama hayo? Ni nani
aliyewahi....

FARID
Tena shemeji wewe ndo usiseme
kabisa. Wewe unaamini kwamba mmezaa
professor mwenye ma PhG yake kama
yote wengine wote mavi.

Kisha Mzee Malamsha anaingilia kati mazungumzo yao


kuyamaliza.

MALAMSHA
Farid, huko unakoenda unavuka
mipaka. Nimekuomba unikopeshe fedha
niende kumuona mwanao. Kama hutaki
basi sema tu sitaki yaishe mdogo
wangu.

FARID
Sitaki!
20.

Malamsha anakata simu na kumuangalia mke wake na kuongea kwa


uchungu sana.

MALAMSHA
Nayda atafika mbali sana mke wangu.
Watakuja hawa wanatembelea matako
kuomba awasaidie wallah nakwambia
nikiwa hai mimi Malamsha Bin Hafidh
hapewi mtu thumni. Kweli mtoto ana
akili tusimpe nafasi ya kusoma
tuishie kumuoza kwa mwanaume? Na
hiyo kradesheni nitaenda, na
watashangaa na roho zao kavu kama
korosho za kiangazi.

NUSRAH
Usijali mume wangu, tumetoka mbali
sana na binti yetu. Kama ni mapenzi
ya Mungu utaenda, na kila jambo
litafanyika sawasawa na apangavyo
yeye.

Wakati wakitafakari, mama Nayda anamtengea chakula na kumsihi


ale. Mzee anashikwa na hasira na kulia kwa sauti kubwa
akiulaani umasikini.

MALAMSHA
Kwani kwa nini sisi? Kwa nini sisi
tumekuwa watu wa shida tu kuomba
omba, kuishi kwa dhiki,
kudhalilishwa hata na ndugu wa
damu? Eh Mola wetu tumekukosea nini
sie ukoo wa Malamsha?

Bi Nasrah anamtuliza mumewe na kumfariji kwa maneno ya upole.

NUSRAH
Ni nani walioandikiwa laana na
Mwenyezi Mungu? Wapo watu hospitali
leo hii tunavyoongea wanakata roho,
wengine wamevunjika vunjika kwenye
ajali, sie tumepewa pumzi ya uhai,
afya, na amani. Hakuna tena utajiri
duniani hapa zaidi ya afya, pumzi
ya uhai na amani mume wangu.
Yatapita tu tusimdhihaki Mwenyezi
Mungu kwa mitihani tunayoipitia.
Tuseme Alhamdullilah kwa kila kitu
mume wangu. Siku moja tutaivuka hii
hatua.

MALAMSHA
Amin Yarab. Asante sana mke wangu.
Mungu hatatutupa.
21.

Just then simu yake inaita. Imeshachakaa kiasi kwamba ikiita


hawezi kuona ni nani anampigia. Anamuuliza mke wake ni nani
huyo tena anapiga. Mkewe anacheka na kumwambia kwamba hajui
maana simu haineshi. Anamwambia mke wake apokee wakati yeye
anakula.

NUSRAH
Hallo, ni nani mwenzangu?

Ni rafiki yake Malamsha ambaye anaitwa Twalib Juma Khatib


(60) aliongea naye jioni na kumueleza shida yake wakiwa
kwenye mchezo wa bao.

TWALIB
Mwambie sheikh nimetafakari sana
kuhusu mwanetu. Na mimi namchukulia
Nayda kama mwanangu kabisa wa
kumzaa ingawa Mnyaz Mungu
hakunijaalia watoto.

NUSRAH
Nayda mwanao kabisa shemeji.
Usiseme Mungu hajakujaalia. Amekupa
Nayda.

TWALIB
Alhamdullilah kwa kweli. Na binti
ametuheshimisha kwa kweli
mashallah.

NUSRAH
Kabisa. Nayda sio mpenda makuu
engineer wetu.

TWALIB
Ah kabisa. Na uinjinia ataupata
tukiwa hapa hapa In Sha Allah.
Sasa mwambie huyo bwana
nimefanikiwa kupata kiasi kidogo
kama elfu tisini tu. Nimtumie aende
bwana kwa mtoto. Mwambie namrushia
sasa hivi kwenye simu yake. Yeye
akijaaliwa kuipata atanirudishia
siku yoyote In Sha Allah.

NUSRAH
Wallah shemeji yangu sijui nikupe
zawadi gani. Na anakusikia hapa
anakula michozi inamtoka. Mwenyezi
Mungu mwingi wa Rehema na Barka
akujaalie na kukuongezea pale
ulipotoa.
(MORE)
22.

NUSRAH (CONT'D)
Tisini kwa usawa huu sio kidogo ni
nyingi sana hadi naogopa
tutarudisha lini mwenzangu au hadi
huyo Nadya akipata ajira labda ndo
akulipe mwenyewe.

Wanakumbatiana wote baada ya kumaliza kuongea na simu. Mama


Nayda anamwambia mume wake kuwa kila kitu kitaenda sawa.

EXT. NYUMBANI KWA MZEE MALAMSHA - DAY

Tunamuona Bi Nusrah akikinga maji nje kwenye bomba na


kuyapeleka bafuni. Tunaliona bafu la nje lenye bati
limeegeshwa kama mlango. Bi Nusrah analisogeza bati na
kuingiza maji bafuni. Kisha mzee anaingia kuoga. Huku
tunamuona Bi Nusrah akimuandalia mumewe chai ya rangi na
mihogo ya kuchemshwa na kachumbari. Mzee anaonekana ameshavaa
anakunywa chai yake aondoke.

MALAMSHA
Chochote ntakachopata kitatosha tu.
Hii tisini inatosha nauli ya kwenda
na kubaki thelathini. Wallah
nikipata hamsini tu zingine leo ah
hiyo kradesheni yatanitambua mzee
Malamsha mie.

NUSRAH
Nguo ushajua utavaa ipi? Maana
wenzio watalipuka ile mbaya ujue?
Watu watakuja na ma Vx kama yote
mwenzangu. Uchague nguo nzuri
angalau upendeze kidogo mume wangu.

MALAMSHA
Hahahaha, waje na mav8, ma costa,
ma renji, mimi sijali. Koti langu
lile lile jeusi la kutokea, na ile
suruali yangu pendwa. Wakitaka
kunijua mie wawaweke watoto wao
kwenye mtihani mmoja na mama yangu
waone akavyowagalagaza. Maaaanisha.
Hebu ngoja nikimbie nisije
nikachelewa mke wangu.

NUSRAH
Sasa ukipata siupitie huko huko tu
ukate tiketi moja kwa moja baba?

MALAMSHA
Habari ndo hiyo!
23.

INT. NDANI YA GARI LA DETECTIVE AYSHA - DAY

Detective Aysha na askari mwenzake wakiwa wamevalia nguo za


kiraia. Wamejitegesha mahali kuwasuburia wahalifu wapite
wawakamate. Ni genge la wauza unga ambao Aysha ameapa kula
nao sahani moja hadi waishe wote. Anamuonesha afande mwenzake
noti iliyoandikwa “Wema hauna mwisho”

DETECTIVE AYSHA
Hivi kwa nini watu wanapenda
kuandika kwenye noti?

MASHA
Eti wema hauna mwisho. Sasa sijui
anategemea atajibiwa siku moja?

DETECTIVE AYSHA
Hivi unajua ni kosa kisheria
kuchafua noti?

MASHA
I know afande but tatizo ni kumpata
mchafuzi. Hapo ndio kimbembe.

DETECTIVE AYSHA
I know, right?

Ghafla wanaarifiwa kupitia radio call kwamba wahalifu hao


wanakuja kwa miguu wakitembea kwa kasi. Aysha anachukua ile
noti na kuchanganya na noti zingine na kuziweka mfukoni na
kushuka haraka kwenye gari.

EXT. BUS STAND - DAY

Mzee Malamsha anashuka kwenye daladala akiwa na bahasha mkoni


mwake na simu yake. Anaposhuka tu anagongwa na mtu mwanamke
aliyekuwa anakimbia kumfukuza mtu aliyedhaniwa kuwa ni
mhalifu. Simu ya mzee Malamsha inaanguka na kupasuka pasuka.
Betri kule, line haionekani, mzee Malamsha anaangaliana na
huyu mwanamke.

CUT TO:

EXT. HOUSE PARTY - NIGHT


24.

Mwanamke huyu ambaye ni afisa wa polisi anamuomba sana radhi


na kumpa shilingi elfu 50 kama pole huku akikimbia na
kumuacha pale chini.

Mzee Malamsha anajikusanya na kutafuta line yake ambayo ni ya


muhimu sana. Anaipata anachukua betri na kuliweka kwenye simu
yake na kuiwasha. Inawaka vizuri. Anampigia mzee mkude jirani
yake.

MALAMSHA
Eh bwana eh, uko nyumbani?

MKUDE
Nipo swaiba vipi, kwema?

MALAMSHA
Naomba umkimbizie bibie simu yako
niongee naye mara moja ndugu yangu,
tafadhali.

MKUDE
Malamsha ntaanza kuwa nakuchaji
hela ujue. Mnunulie mkeo simu bwana
simu yangu sio ya kijiji.
Hahahahaha.

MALAMSHA
Mwanangu akiwa injinia tutagawa
simu kama peremende mtaani. We
ngoja tu.

MKUDE
Hahahaha, haya bwana tena Bi Nusrah
huyu hapa alikuwa amekuja kupiga
umbea na shoga yake kidawa.

Anampa Nusrah simu na kusogea pembeni.

MALAMSHA
Bibie,

NUSRAH
Naam mume wangu.

MALAMSHA
Mungu si Athumani. Yaani huku
nilikokuwa naenda siendi tena.
Nimepata ajali narudi nyumbani.

NUSRAH
Hebu ngoja kidogo. Sasa umepata
ajali unarudi nyumbani maana yake
nini?
25.

MALAMSHA
Mke wangu, yaani kazi ya Mungu siku
zote haina makosa. Nimepata hela,
elfu hamsini.

NUSRAH
Sasa na hiyo ajali unayosema
imekuwaje?

MALAMSHA
Sikiliza sasa, mie nilikuwa nashuka
zangu kwenye daladala, ile kushuka
tu kumbe sijui kuna mwizi huko
polisi wanamkimbiza. Mara mdada
mmoja sijui askari yule akanigonga
wakati nashuka nikaanguka nikiwa
nimeshikilia simu na ile bahasha.
Basi kiswaswadu changu pangala,
kikasambaratika. Mie sasa mawazo
yangu yote wala sio simu
kuharibika, naiwazia ile line yenye
hela maana ikipotea tena hapo
mtihani. Sasa yule dada bwana si
akanionea huruma. Kainama chini
kunisaidia kutafuta akaona
anachelewa. Mara ghafla naona
anaingia mfukoni ananipa elfu
hamsini. Elfu hamsini kahesabu noti
moja hadi tano. Kaniambia niende
kureneu line yangu. Sasa mimi kwa
ubishi si nikaendelea kuitafuta
line? Mara hamad! Hii hapa,
nimeipata. Nikachukua betri lile na
simu nikaiweza fresh ndo nikampigia
Mkude.

NUSRAH
Eh, embu ngoja kwanza. Kwa hiyo
yote haya yametokea saa ngapi?

MALAMSHA
Bwana wewe nakwambia sasa hivi
hapa. Kwa hiyo mie kwa kina Omary
siendi tena, naenda zangu kukata
tiketi kabisa ili niwe tayari,
yasije kutokea ya kutokea.

NUSRAH
Heh, makubwa mwenzangu. Ama kweli
ya Mungu mengi. Haya kuwa makini
basi mume wangu barabarani huko.
Nakuombea ufanikishe. Dooh hii nayo
historia.
26.

MALAMSHA
In Sha Allah mke wangu.

EXT. NYUMBANI KWA MZEE MALAMSHA - EVENING

Tunamuona mzee Malamsha akiingia nyumbani kwake mke wake


akimpokea kwa furaha kubwa sana. Mzee anauonesha bahasha
yenye tiketi na kumwambia kwamba safari sasa ni dhahiri.
Lakini cha kushangaza Nusrah anasisitiza kwamba ni bora tu
hizo hela wangemtumia mtoto wao anunue keki na kusherehekea
kuliko kununua tiketi na kwenda.

MALAMSHA
Unajua wewe huelewi mke wangu.
Nayda sijamwambia hata kwamba
nitaweza kwenda. Kwa hiyo hategemei
mimi kwenda. Ila takaponiona furaha
yake itakuwa kubwa ajabu.

NUSRAH
Sikatai mume wangu lakini fedha
hazitoshi. Siku ya kurudi
utarudije?

MALAMSHA
Siku ya kurudi anaijua Mungu. Kama
alivyopanga kwenda ndivyo
atakavyopanga kurudi. Ondoa
wasiwasi. Niandalie moka zangu, na
ile suruali yangu na koti langu.
Mengine tumuachie Maulana.

Mama anamuandalia mzee vitu vyote. Anamyooshea suruali yake


na T-shirt yake nyeupe iliyochoka choka. Anaviweka kwenye
kiti na viatu vyake na socks.

INT. NYUMBANI KWA MZEE MALAMSHA - NIGHT

Tunawaona Mzee Malamsha na mkewe wakiwa wamelala. Mzee


Malamsha anakoroma sana na kuweweseka. Mama anaamka na kuwa
macho anaonekana ana mawazo sana. Anamshtua mzee.

NUSRAH
Malamsha, unakoroma sana bwana hebu
lala vizuri.

MALAMSHA
Muda wa kuamka umeshafika?
27.

NUSRAH
Bado. Lakini sijui kwa nini nawaza
siumtumie tu mtoto hizo hela? Kwani
ni lazima uende?

MALAMSHA
Ah, jamani mke wangu kweli?
Unaendelea na hiyo hoja hadi saa
nane usiku? Sasa nimeshakata
tiketi, tufanyeje? Niiache iende
bure, tupoteze elfu sitini kweli
mama?

NUSRAH
Ukienda hutakukuwa na chochote cha
kumpa mtoto kama zawadi. Ukiwa na
upweke utaendelea tu kuwepo.

MALAMSHA
Mama, hebu tulale, mwenzio kesho
nina safari ndefu sana.
Atakusimulia mwanao akirudi. Sawa
mke wangu?

NUSRAH
Mh. Sawa mume wangu! Haya tulale.

INT. NYUMBANI KWA MZEE MALAMSHA - MORNING

Alfajiri na mapema Mama Nayda anaamka kumuandalia mumewe chai


anywe kabla ya kuanza safari. Tunamuona akiwa jikoni ambamo
pia ndiyo chumbani kwa Nayda. Anaona mdoli ambao Nayda
anaupenda sana tangu akiwa mtoto. Anauchukuwa na kuusafisha
vizuri na kuuweka kwenye nfuko maalumu na kuuweka karibu na
nguo za mume wake.

MALAMSHA
Mke wangu, mbona hujaniamsha
mapema?

NUSRAH
Kwani basi linaondoka saa ngapi?

MALAMSHA
Saa kumi na mbili kamili. Sasa hivi
saa kumi na moja na robo bado
sijaondoka.

NUSRAH
Kunywa chai haraka mume wangu
utawahi tu.
28.

MALAMSHA
Hapana mama, ntachelewa acha
nijimwagie maji nikimbie.

NUSRAH
Haya maji nimeshakupashia na
kukuwekea bafuni wahi basi.

Malamsha anaingia bafuni chap chap anaoga na kuvaa na


kujiandaa kutoka. Mkewe anampa mfuko ambao ndani kuna mihogo
ya kuchemsha.

EXT. NYUMBANI KWA MZEE MALAMSHA - MORNING

Tunamuona mzee Malamsha akitoka mbio huku mke wake akimwita


arudi maana amesahau mfuko uliokuwa na mdoli na waraka mfupi
mama alioandika kwa penseli kumuandikia mwanae uliosomeka,

“Nayda mwanangu, mama wa mume wangu. Mimi mama yako


nilitamani pia kufika kushuhudia mahafali yako lakini kama
unavyojua hali yetu. Nakupenda, nakuamini, najua utapasua
sana kwenye mtihani wako wa mwisho, na In Sha Allah utakuwa
namba wani. Furahia siku yako na baba yako. Mimi nakuandalia
jogoo mkuuubwa ukija nakuchinjia mwanangu. Umetuheshimisha,
umepambana, umesoma, asante sana. Mdoli wako nimekufungashia
kama zawadi ukufariji na kukutia moyo wakati wa mtihani.
Ukirudi urudi nao tafadhali, nakupenda sana. Ndimi mama yako
kipenzi Nusrah”.

Mzee anarudi haraka, anauchukua ule mfuko mdogo na kuuweka


ndani ya ule mfuko mwingine na kutimua mbio.

CUT TO:

EXT. MTAANI - MORNING

Kwenye eneo la tukio tunamuona Detective Aysha akijaribu


kuokoa maisha ya Mzee Malamsha anayeonekana kutokwa damu
nyingi sana. Aysha anampigia kelele afande Kazola aite
ambulance haraka huku akiendelea kujaribu kumsaidia Mzee
Malamsha asipoteze uhai. Anararua mavazi ya mzee na kumfunga
kifuani kwa nguvu Mzee anaongea lakini kwa shida huku damu
zinamtoka mdomoni na kifuani.

MALAMSHA
Angalia kwenye simu yangu kuna
namba imeandikwa SHULE NAYDA
umpigie Matroni umtumie hela zote
zilizoko kwenye simu yangu elfu
thelethini. Na zingine elfu hamsini
ziko kenye koti. Mtumie ampe
mwanangu anunue keki ale.
(MORE)
29.

MALAMSHA (CONT'D)
Sitaweza kuwahi kwenye mahafali.
Mwambie asiache kusomea uinjinia
amsaidie mama yake. Mpe na mdoli
wake na barua yake kutoka kwa mama
yake.

Mzee Malamsha anafumba macho na kukata roho. Tunamuona Aysha


anatokwa na chozi zito, anabubujikwa na machozi akitembea
pole pole kuelekea kwenye gari. Anaanguka kabla hajafika.

INT. HOSPITALI - MORNING

Wodini tunamuona Aysha akiwa amelala kitandani amewekewa drip


akiwa bado hajitambui. Tunaziona mashine za mapigo ya moyo na
mashine zingine zikiendelea kufanya kazi. Ghafla anafumbua
macho na kuonana na mume wake Godfrey Banda (39) ambaye
alipewa taarifa za hali yake na kukimbia kuja hospitalini.

GODFREY
Good afternoon detective.

DETECTIVE AYSHA
Hey baby, umefikaje hapa?

GODFREY
Nimepigiwa simu ikabidi nitoke
ofisini chap nije. How are you
feeling my love?

DETECTIVE AYSHA
There was a sack alikuwa nayo yule
mzee and some cash like 50k. Wait a
minute, naomba simu yangu baby mara
moja please.

GODFREY
Sweetheart huruhusiwi kushika
chochote right now hadi daktari
apite round jioni atupe maelekezo.
You’re not on duty sasa hivi
unaumwa na ni lazima utibiwe kwanza
upone.

DETECTIVE AYSHA
Baby I need to go, like right now,
Oh my God.

GODFREY
But why baby. Nadhani kila kitu
kilikuwa taken care of. Please
relax. Okay?
30.

Aysha anaamka na kufumua mipira aliyokuwa amewekewa.


Ananyanyuka na kuchukua mkoba wake na kupiga simu kituoni
kuulizia mfuko aliokuwa nao mzee Malamsha.

DETECTIVE AYSHA
Masha are you sure hakuna
kilichochomolewa? Please nenda sasa
hivi ukaangalie uniambie.

MASHA
Niko hapa storage afande na
nauangalia mfuko wa marehemu. Kila
kitu kimehifadhiwa salama including
mihogo yake ya kuchoma, pesa
taslimu 50k, barua, simu na mdoli
afande.

DETECTIVE AYSHA
Nakuja, right now. Do not let
anybody touch that sack. Umesikia?

MASHA
Copied afande.

Aysha anaagana na mume wake na kuondoka hospitali bila


kuruhusiwa na wauguzi.

INT. OFISINI KITUO KIKUU CHA POLISI - DAY

Aysha anaingia moja kwa moja kuangalia ule mfuko aliokuwa nao
mzee Malamsha. Anaziangalia zile noti anagundua ni zile fedha
ambazo alimpa walipogongana kituoni. Anaumia zaidi. Anachukua
simu ya mzee Malamsha ambayo imeharibika sana. Anabadilisha
housing na simu nyingine iliyoko hapo storage room ili aweze
kuangalia data zilizomo. Anaikuta namba ya Matron wa shule na
kumpigia.

DETECTIVE AYSHA
Habari, naitwa Aysha. Ni ndugu yake
Nayda Malamsha upande wa baba yake.

MATRON
Oh, karibu sana Aysha, mnakuja
kwenye graduation? Maana Nayda
anatazamiwa kutunukiwa vyeti kama
vyote. Top in Physics, Chemistry,
na Math. Pamoja na Mahudhurio,
Nidhamu, Uadilifu, Usafi. Aisee kwa
kweli Nayda ni mfano wa kuigwa hapa
shuleni. Karibuni sana. Atafurahi
sana kuwaona.
31.

DETECTIVE AYSHA
Matron, kwa bahati mbaya hatutaweza
kufika ila akimaliza tu mitihani
nitakuja mimi binafsi kumfata. Mzee
Malamsha amefariki leo alfajiri
akiwa anajaribu kuwahi basi la kuja
huko.

MATRON
Mungu wangu! Poleni sana. Daaaah
habari ya kusikitisha sana.
Nimeumia kwa kweli. Binafsi
nilikuwa naongea naye mara kwa mara
na kumpa update za mtoto. Ni nini
kimepelekea kufikwa na mauti?

DETECTIVE AYSHA
Tutaongea vizuri. Nakutumia hela
shilingi laki moja unisaidie
kumnunulia keki na zawadi zingine
at least asiwe mpweke sana. Naomba
asijue kuhusu msiba hadi
nitakapomfata shuleni. Hii ni namba
yangu isevu.

MATRON
Nimeishiwa cha kusema. Kwa nini
lakini hii dunia?

DETECTIVE AYSHA
Hey, yameshatokea. Sio wakati wa
kulia. Tufarijiane tumsaidie Nayda
maisha yaendelee. Kuna mambo ni
vigumu sana kuyaelewa sisi kama
binaadamu. Nikutakie siku njema.

You might also like