You are on page 1of 44

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

r aft
D
MUHTASARI WA ELIMU YA MSINGI
DARASA LA I NA LA II
2023
© Taasisi ya Elimu Tanzania, 2023
Toleo la Kwanza, 2023

aft
Taasisi ya Elimu Tanzania
S.L.P 35094

r
Dar es Salaam, Tanzania.

Simu: +255 735 041 168 / 735 041 170

D
Baruapepe: director.general@tie.go.tz
Tovuti: www.tie.go.tz

Muhtasari huu urejelewe kama: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. (2023). Muhtasari wa Elimu ya Msingi Darasa la I
na II. Taasisi ya Elimu Tanzania.

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kurudufu, kuchapisha, kutafsiri wala kutoa muhtasari huu kwa namna yoyote
ile bila idhini ya maandishi kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania.

ii
Yaliyomo

Orodha ya majedwali................................................................................................................................................................... iv
Vifupisho ................................................................................................................................................................................... v
Shukurani ................................................................................................................................................................................... vi

ft
1.0 Utangulizi......................................................................................................................................................................... 1

a
2.0 Malengo Makuu ya Elimu Tanzania................................................................................................................................ 1

r
3.0 Malengo ya Elimu ya Msingi Darasa la I na la II............................................................................................................ 2
4.0 Umahiri wa jumla wa Elimu ya Msingi Darasa la I na la II............................................................................................ 2
5.0 Umahiri Mkuu na Umahiri Mahususi.............................................................................................................................. 3

D
6.0 Majukumu ya Mwalimu, Mwanafunzi na Mzazi/Mlezi katika Ufundishaji na Ujifunzaji.............................................. 3
6.1 Mwalimu................................................................................................................................................................ 5
6.2 Mwanafunzi............................................................................................................................................................ 5
6.3 Mzazi/mlezi............................................................................................................................................................ 6
7.0 Mbinu za Ujifunzaji na Ufundishaji................................................................................................................................ 6
8.0 Zana za Ufundishaji na Ujifunzaji................................................................................................................................... 6
9.0 Upimaji............................................................................................................................................................................ 7
10.0 Idadi ya Vipindi................................................................................................................................................................ 7
11.0 Maudhui ya Ufundishaji na Ujifunzaji............................................................................................................................ 8
Bibliografia.................................................................................................................................................................................. 32

iii
Orodha ya majedwali

Jedwali Na. 1: Umahiri Mkuu na Mahususi kwa Darasa la I na la II........................................................................................ 3

Jedwali Na. 2: Mgawanyo wa Muda na Vipindi Darasa la I na la II kwa Wiki......................................................................... 8

ft
Jedwali Na. 3: Maudhui ya Darasa la I...................................................................................................................................... 9
Jedwali Na. 4: Maudhui ya Darasa la II..................................................................................................................................... 21

r a
D
iv
Vifupisho

LAT Lugha ya Alama ya Tanzania

TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

ft
TET Taasisi ya Elimu Tanzania

a
WyEST Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

D r
v
Shukurani

Maandalizi ya muhtasari wa Elimu ya Msingi Darasa la I na la II yamehusisha wataalamu mbalimbali kutoka taasisi za serikali
na zisizo za serikali. Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), inatambua na kuthamini michango ya washiriki wote waliofanikisha
kupatikana kwa muhtasari huu. Aidha, TET inatoa shukurani za pekee kwa wahadhiri, wakufunzi, wathibiti ubora wa shule,

ft
walimu pamoja na wakuza mitaala. Vilevile, TET inaishukuru Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu ya Kusimamia Kazi ya Maboresho
ya Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu iliyoteuliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kamati

a
hii ilifanya kazi kwa weledi na kuhakikisha kuwa maudhui ya muhtasari huu yanalenga kuwa na wahitimu wenye maarifa, ujuzi
na stadi zitakazowawezesha kujiajiri, kuajiriwa na kumudu maisha yao ya kila siku, ambalo ndilo lengo kuu la Uboreshaji wa

r
Mitaala ya Mwaka 2023.

Mwisho, TET inatoa shukurani za pekee kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuwezesha uandaaji na usambazaji

D
wa muhtasari huu.

Dkt. Aneth A. Komba


Mkurugenzi Mkuu
Taasisi ya Elimu Tanzania

vi
1.0 Utangulizi
Muhtasari huu una umahiri sita za lazima kwa mwanafunzi anayesoma elimu ya msingi darasa la I na la II kwa kutumia
Kiswahili kama lugha ya kufundishia. Umahiri hizo ni Kusoma, Kuandika, Kuhesabu, Demontsrate Mastary of Basic English
language Skills, Kuthamini Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Kutunza Afya na Mazingira. Aidha, umahiri hizo zina maudhui
yanayolenga kumwezesha mwanafunzi kujifunza stadi za awali za utumiaji wa kompyuta. Lengo kuu la kujifunza umahiri hizi

ft
ni kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), kujenga uelewa wa awali wa lugha ya Kiingereza na kujenga stadi
nyingine za utamaduni, sanaa, michezo, afya na mazingira zitakazomsaidia mwanafunzi kumudu maisha yake ya kila siku.

a
Aidha, umahiri hizi pia zinalenga kujenga uelewa wa awali wa utumiaji wa Kompyuta. Stadi hizi ni msingi muhimu katika
kumwezesha mwanafunzi kujifunza kwa ufanisi na kumudu ujifunzaji wake katika ngazi za juu.

r
Muhtasari wa Elimu ya Msingi Darasa la I na la II umeandaliwa kwa lengo la kumwongoza mwalimu katika ufundishaji na
ujifunzaji wa umahiri sita zilizoainishwa katika muhtasari kwa shule zinazotumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia Tanzania
Bara. Muhtasari huu umetafsiri Mtaala wa Elimu ya Msingi wa Mwaka 2023. Muhtasari utamwezesha mwalimu kupanga

D
shughuli za ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, muhtasari huu unasisitiza matumizi ya mbinu zitakazomwezesha mwanafunzi
kukuza stadi za Karne ya 21 zikiwemo kufikiri kimantiki, ubunifu, ushirikiano, mawasiliano na utatuzi wa matatizo.

2.0 Malengo Makuu ya Elimu Tanzania


Malengo makuu ya elimu Tanzania ni kumwezesha kila Mtanzania:
(a) Kukuza na kuboresha haiba yake ili aweze kujithamini na kujiamini;
(b) Kuheshimu utamaduni, mila na desturi za Tanzania, tofauti za kitamaduni, utu, haki za binadamu, mitazamo na matendo
jumuishi;
(c) Kukuza maarifa na kutumia sayansi na teknolojia, ubunifu, fikra tunduizi, uvumbuzi, ushirikiano, mawasiliano na
mtazamo chanya katika maendeleo yake binafsi, na maendeleo endelevu ya taifa na dunia kwa ujumla;
(d) Kuelewa na kulinda tunu za taifa ikiwa ni pamoja na utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uaminifu, uwajibikaji na
lugha ya taifa;

1
(e) Kujenga stadi za maisha na stadi za kazi ili kuongeza ufanisi katika maisha ya kila siku;
(f) Kukuza tabia ya kupenda na kuheshimu kazi ili kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji na utoaji wa huduma;
(g) Kutambua na kuzingatia masuala mtambuka ambayo ni pamoja na afya na ustawi wa watu (jamii), usawa wa kijinsia,
usimamizi na utunzaji endelevu wa mazingira; na
(h) Kukuza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa, amani na haki kwa kuzingatia Katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa.

ft
3.0 Malengo ya Elimu ya Msingi Darasa la I na la II

a
Malengo ya Elimu ya Msingi Darasa la I na la II ni kumwezesha mwanafunzi:

r
(a) Kukuza stadi za Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu (KKK), ikihusisha kutumia maandishi ya breli, Lugha ya Alama ya
Tanzania (LAT) na lugha mguso;
(b) Kukuza uwezo wa kuwasiliana kwa njia stahiki ikiwemo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na teknolojia saidizi;

D
(c) Kujenga uimara wa mwili, kukuza vipaji, kushirikiana na wenzake na kuwa na mtazamo chanya kuhusu kujifunza;
(d) Kukuza urazini na ujumi, kupenda na kutunza afya na mazingira pamoja na rasilimali zilizopo;
(e) Kukuza maadili na uwezo wa kuthamini na kudumisha tunu za taifa na utamaduni wa jamii yake pamoja na kutambua
tofauti za tamaduni mbalimbali; na
(f) Kukuza uwezo wa kuchangamana katika mazingira jumuishi.

4.0 Umahiri wa Jumla wa Elimu ya Msingi Darasa la I na la II


Umahiri wa jumla utakaojengwa na mwanafunzi wa Darasa la I na la II ni:
(a) Kutumia stadi za Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu (KKK), ikihusisha kutumia maandishi ya Breli, Lugha ya Alama ya
Tanzania (LAT) na lugha mguso;
(b) Kuwasiliana kwa njia stahiki ikiwemo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na teknolojia saidizi;
(c) Kushiriki katika vitendo vya kuimarisha mwili, kukuza vipaji, kushirikiana na wenzake na kuwa na mtazamo chanya
kuhusu kujifunza;

2
(d) Kuonesha urazini na ujumi, kupenda na kutunza afya na mazingira pamoja na rasilimali zilizopo;
(e) Kuonesha maadili, kuthamini na kudumisha tunu za taifa na utamaduni wa jamii yake pamoja na kutambua tofauti za
tamaduni mbalimbali; na
(f) Kuchangamana katika mazingira jumuishi.

ft
5.0 Umahiri Mkuu na Umahiri Mahususi
Muhtasari wa Elimu ya msingi kwa Darasa la I na la II una umahiri mkuu na umahiri mahususi kama inavyojitokeza katika

a
Jedwali Na.1.

r
Jedwali Na. 1: Umahiri Mkuu na Mahususi kwa Darasa la I na la II
Umahiri mkuu Umahiri mahususi

D
1.0 Kusoma 1.1 Kutambua sauti za herufi
1.2 Kutambua uhusiano wa sauti na herufi
1.3 Kusoma kwa ufasaha
1.4 Kusoma na kusikiliza kwa ufahamu

2.0 Kuandika 2.1 Kumudu misingi ya kuandika


2.2 Kumudu stadi za kuandika
2.3 Kutumia kanuni za uandishi

3
Umahiri mkuu Umahiri mahususi
3.0 
Demonstrate mastery of basic 3.1 Develop listening and speaking skills in different contexts
English language skills 3.2 Develop early literacy and numeracy skills
3.3 Communicate in different contexts
4.0 Kuhesabu 4.1 Kutambua dhana ya namba

ft
4.2 Kutumia matendo ya kihisabati

a
4.3 Kutumia dhana za kihisabati

r
5.0 
Kuthamini utamaduni, sanaa na 5.1 Kuthamini utamaduni wake na wa watu wengine
michezo 5.2 Kuheshimu tofauti za kiimani
5.3 Kuonesha matendo yenye maadili

D
5.4 Kubuni kazi za sanaa
5.5 Kushiriki katika michezo mbalimbali
6.0 Kutunza afya na mazingira 6.1 Kutunza afya yake na jamii inayomzunguka
6.2 Kuchunguza vitu vilivyomo katika mazingira
6.3 Kujilinda na mazingira hatarishi
6.4 Kutunza mazingira
6.5 Kuwa na mtazamo chanya kuhusu mazingira

6.0 Majukumu ya Mwalimu, Mwanafunzi na Mzazi/Mlezi katika Ufundishaji na Ujifunzaji


Ujifunzaji na ufundishaji unategemea ushirikiano madhubuti baina ya mwalimu, mwanafunzi na mzazi/mlezi katika kutekeleza
majukumu mbalimbali. Majukumu yao ni kama yafuatayo:

4
6.1 Mwalimu
Mwalimu anatarajiwa:
(a) Kumwezesha mwanafunzi kujenga umahiri uliokusudiwa;
(b) Kuandaa mazingira salama, rafiki na wezeshi ya kufundishia na kujifunzia;
(c) Kutengeneza au kufaragua zana za kufundishia na kujifunzia;

ft
(d) Kutumia mbinu shirikishi zinazomfanya mwanafunzi kuwa kitovu cha ujifunzaji;
(e) Kuhakikisha kuwa ujifunzaji na ufundishaji unafanyika kwa haki na usawa kwa kila mwanafunzi bila kujali tofauti zao;

a
(f) Kufanya upimaji endelevu mara kwa mara kwa kutumia zana na mbinu za upimaji na tathmini zinazopima nadharia na

r
vitendo;
(g) Kutoa malezi kwa haki na usawa kwa kila mwanafunzi bila kujali tofauti zao;
(h) Kumlinda mwanafunzi awapo shuleni;

D
(i) Kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi ya kila siku;
(j) Kubaini mahitaji ya mwanafunzi na kutoa afua stahiki; na
(k) Kushirikisha wazazi/walezi na jamii katika malezi na ujifunzaji wa mwanafunzi.
(l) Kuchopeka masuala mtambuka na TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.

6.2 Mwanafunzi
Mwanafunzi anatarajiwa:
(a) Kuwa mtendaji mkuu katika mchakato wote wa ujifunzaji;
(b) Kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujifunzaji ndani na nje ya darasa ili kupata umahiri unaokusudiwa;
(c) Kushirikiana na wenzake pamoja na mwalimu katika mchakato wa ujifunzaji; na
(d) Kuzingatia kanuni na taratibu za shule.

5
6.3 Mzazi/Mlezi
Mzazi mlezi anatarajiwa:
(a) Kusimamia na kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi katika ujifunzaji;
(b) Kumsimamia mtoto kutekeleza kazi zake za kitaaluma pale inapowezekana;
(c) Kufuatilia mwenendo wa kitabia wa mwanafunzi;

ft
(d) Kuhakikisha kuwa mazingira ya nyumbani ni rafiki na salama yanayowezesha ujifunzaji;
(e) Kumpatia mwanafunzi vifaa vinavyotumika katika shughuli ya ujifunzaji;

a
(f) Kuhakikisha mwanafunzi anapata mahitaji muhimu; na

r
(g) Kumfundisha mtoto umuhimu na thamani ya elimu na kazi pamoja na kumuhimiza kujifunza kwa bidii.

7.0 Mbinu za Ufundishaji na Ujifunzaji

D
Ujifunzaji na ufundishaji katika Darasa la I na la II utazingatia ujenzi wa umahiri unaotumia mbinu zinazomfanya mwanafunzi
kuwa kitovu cha ujifunzaji na mwalimu kuwa mwezeshaji. Mwalimu atatumia mbinu zinazomshirikisha mwanafunzi katika
tendo zima la ujifunzaji na ufundishaji kwa kuzingatia umri, mahitaji anuai na uwezo wa mwanafunzi. Mbinu hizo ni za ujifunzaji
shirikishi unaomwezesha mwanafunzi kufikiri, kutafuta maarifa kutoka vyanzo mbalimbali, majadiliano katika vikundi na
kushiriki katika kutoa mrejesho. Baadhi ya mbinu hizo ni ziara za kimasomo, kazimradi na kazi nyingine kama hizo kulingana
na muktadha ili kufanikisha ujifunzaji.

8.0 Zana za Ufundishaji na Ujifunzaji


Zana za ujifunzaji na ufundishaji zinapaswa kuwa shirikishi na zinazokidhi mahitaji, umri na uwezo wa mwanafunzi. Mwalimu
anapaswa kuhakikisha mwanafunzi anapata nafasi ya kuona, kusikia na kushika zana. Aidha, zana za ujifunzaji na ufundishaji
zinapaswa zimsaidie mwanafunzi kuelewa kinachofundishwa. Mwalimu anashauriwa kutumia zana zinazopatikana katika
mazingira yanayomzungumka. Orodha ya vitabu vitakavyotumika vitatolewa na TET.

6
9.0 Upimaji
Upimaji ni suala muhimu katika mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji ili kuwezesha ujenzi wa umahiri unaokusudiwa. Upimaji
wa darasa la I na la II utajumuisha upimaji endelevu na upimaji tamati. Upimaji endelevu utazingatia vigezo vilivyoainishwa
katika kila shughuli ya ujifunzaji na utamwezesha mwalimu kubaini uwezo na uhitaji wa mwanafunzi katika ujifunzaji.
Vilevile, utalenga kupima mabadiliko katika maarifa, stadi na mwelekeo wa kutenda, kuthamini, kusimulia na kutumia

ft
stadi anazojifunza katika mazingira yanayomzunguka. Aidha, mwalimu atatumia taarifa za upimaji kuboresha ufundishaji
na kumwezesha mwanafunzi kufikia lengo la ujifunzaji. Zana za upimaji zinazoweza kutumika wakati wa ufundishaji

a
na ujifunzaji ni bunguabongo, orodha hakiki, mazoezi ya darasani, majaribio, majaribio kwa vitendo, dodoso, maswali ya
ana kwa ana, mazoezi, kazi kwa vitendo (kazi binafsi na kazi za vikundi), kazimradi na mkoba wa kazi na zana nyingine

r
kama hizo.

Upimaji tamati utahusisha mitihani ya wiki, mwezi, muhula na mtihani wa mwisho wa mwaka ambayo itatumika kupima

D
maendeleo ya ujifunzaji wa mwanafunzi. Taarifa za upimaji huu pamoja na kutumika kutathimini maendeleo ya mwanafunzi,
zitatumika kutoa mrejesho wa kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji.

10.0 Idadi ya Vipindi


Muhtasari wa Elimu ya Msingi Darasa la I na la II unatoa makadirio ya muda utakaotumika katika ujifunzaji na
ufundishaji kwa kuzingatia uzito wa umahiri mahususi na shughuli za ujifunzaji. Makadirio haya ya muda yamewekwa
kwa mfumo wa vipindi ambapo kila kipindi ni dakika 30. Idadi ya vipindi kwa kila umahiri ni kama ulivyooneshwa katika
Jedwali Na. 2:

7
Jedwali Na. 2: Mgawanyo wa Muda na Vipindi Darasa la I na la II kwa Wiki

Umahiri Idadi ya Vipindi


Kusoma 8
Kuandika 5

ft
Kuhesabu 7
Demonstrate Mastery of Basic English Language Skills 6

a
Kutunza Afya na Mazingira 2

r
Kuthamini Utamaduni, Sanaa na Michezo 2
Jumla ya idadi ya vipindi kwa wiki 30

D
11.0 Maudhui ya Ufundishaji na Ujifunzaji
Maudhui yamepangiliwa katika vipengele sita, ambavyo ni; Umahiri Mkuu, Umahiri Mahususi, Vigezo vya upimaji, Shughuli
za ujifunzaji, Vifaa/zana na Idadi ya Vipindi kama inavyojitokeza katika Jedwali Na.3 na 4.

8
Jedwali Na. 3: Maudhui ya Darasa la I
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
1.0 Kusoma 1.1 Kutambua (a) Kubaini sauti za Sauti za irabu Kadi na chati za picha za 37

ft
sauti za irabu (a, e, i, o, u) zimebainishwa (a, e, i, o, u) vitu vinazoanza na irabu,
herufi katika maneno katika maneno kadi, chati na picha za

a
(b) Kuunganisha sauti Sauti za irabu irabu, maneno, vitu halisi,
za irabu ili kuunda zimeunganishwa ili kuunda sauti za irabu na maneno

r
maneno (oa, au, ua) maneno (oa, au, ua) yaliyorekodiwa
(c) Kutambua sauti za Sauti za konsonanti (b, m,
konsonanti (b, m, k, k, d, n); (l, t, p, s, f, j); (g,

D
d, n); (l, t, p, s, f, j); y, z, h, r, w, v, ch) kwenye
(g, y, z, h, r, w, v, ch) maneno zimetambuliwa
kwenye maneno
(d) Kutambua herufi Herufi kubwa na ndogo
kubwa na ndogo zimetambuliwa
(e) Kuunganisha sauti za Sauti za konsonanti na
konsonanti na irabu irabu zimeunganishwa ili
ili kuunda silabi kuunda silabi
(f) Kutenganisha kwa Sauti za konsonanti na irabu
kutamka sauti za zilizounda silabi na silabi
konsonanti na irabu zilizounda maneno
zilizounda silabi na zimetenganishwa kwa
silabi zilizounda kutamka
maneno

9
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(g) Kutambua sauti za Sauti za herufi
herufi mwambatano mwambatano (sh, th, mb,
(sh, th, mb, ny, ng, ny, ng, nd, kw, mw) kwenye

ft
nd, kw, mw) kwenye maneno zimetambuliwa
maneno kwa usahihi

a
(h) Kuunganisha sauti za Sauti za herufi mwambatano
herufi mwambatano (sh, (sh, th, mb, ny, ng, nd, kw,

r
th, mb, ny, ng, nd, kw, mw) zimeunganishwa ili
mw) na irabu ili kuunda kuunda silabi
silabi

D
1.2 Kutambua (a) K uhusianisha sauti na Sauti na majina ya herufi Kadi na chati za picha 32
uhusiano herufi za irabu (a, e, i, za irabu (a, e, i, o, u) katika na herufi, ubao, maneno,
wa sauti o, u) katika matini matini zimehusianishwa video zenye sauti na
na herufi majina ya herufi za irabu,
(b) Kuhusianisha sauti na Sauti na majina ya herufi za sauti za irabu na maneno
herufi za konsonanti (b, konsonanti (b, m, k, d, n);
yaliyorekodiwa
m, k, d, n); (l, t, p, s, f, (l, t, p, s, f, j); (g, y, z, h, r,
j); (g, y, z, h, r, w, v, ch) w, v, ch) zimehusianishwa
katika matini katika matini
(c) Kuhusianisha sauti na Sauti na majina ya herufi za
herufi za konsonanti konsonanti mwambatano
mwambatano (sh, th, (sh, th, mb, ny, ng, nd, kw,
mb, ny, ng, nd, kw, mw) mw) zimehusianishwa
katika matini katika matini

10
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(d) Kuunganisha sauti za Sauti za herufi za konsonanti
herufi za konsonanti na irabu ili kusoma silabi

ft
mwambatano na irabu katika makundi yote (sh,
ili kusoma silabi katika th, mb, ny, ng, nd, kw,

a
makundi yote (sh, th, mb, mw) zimeunganishwa kwa
ny, ng, nd, kw, mw) usahihi

r
(e) Kuunganisha silabi ili Silabi zimeunganishwa ili
kusoma maneno kusoma maneno
(f) Kutenganisha kwa Sauti zimetenganishwa kwa

D
kutamka sauti mojamoja sauti mojamoja ili kuunda
ili kuunda maneno maneno
(g) Kuunganisha maneno ili Maneno yameunganishwa
kusoma sentensi ili kusoma sentensi
1.3 Kusoma (a) Kusoma kwa sauti Kifungu cha habari/hadithi Kadi na chati za maneno, 20
kwa kifungu cha habari/ linganifu kwa kuzingatia matini, picha za vitu
ufasaha hadithi linganifu kwa matamshi sahihi ya maneno mbalimbali na vifungu
kuzingatia matamshi kimesomwa kwa sauti vya habari au hadithi
sahihi ya maneno zilizorekodiwa
(b) Kusoma kwa sauti Kifungu linganifu cha
kifungu linganifu cha Habari/hadithi kimesomwa
habari/hadithi kwa kasi kwa sauti na kwa kasi
stahiki (maneno 40 kwa stahiki (maneno 40 kwa
dakika) dakika)

11
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa

(c) Kusoma kwa sauti kifungu Kifungu linganifu


linganifu cha habari/hadithi cha habari/hadithi

ft
kwa hisia na kwa kuzingatia kimesomwa kwa sauti,
alama za uandishi (nukta, hisia na kwa kuzingatia

a
mkato, alama ya kuuliza na alama za uandishi (nukta,
alama ya mshangao) mkato, alama ya kuuliza

r
na alama ya mshangao)
1.4 Kusoma (a) Kutafsiri na kuelezea picha Picha zimeelezewa na Kadi na chati za picha za 21
na kutafsiria kwa usahihi vitu mbalimbali, matini

D
kusikiliza ya habari/hadithi, hadithi/
(b) Kubashiri maudhui ya Amebashiri maudhui
kwa habari zilizorekodiwa
habari/hadithi kwa usahihi ya habari/hadithi kwa
ufahamu
kwa kutumia picha, jina la kwa kutumia picha, jina
habari/hadithi na msamiati la hadithi na msamiati
uliochaguliwa uliochaguliwa

(c) Kusikiliza habari/hadithi Habari/hadithi


kwa ufahamu imesikilizwa kwa ufahamu

12
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
2.0 Kuandika 2.1 Kumudu (a) Kutumia stadi za awali Stadi za awali za kuandika Kadi za herufi, viandikio, 14
misingi za kuandika zimetumika video zinazoonesha
ya (b) Kuchora michoro ya Michoro ya herufi misingi ya kuandika

ft
kuandika herufi imechorwa
(c) Kufuatisha herufi kwa Herufi zimefuatishwa kwa

a
kuzingatia hatua kuzingatia hatua

r
2.2 Kumudu (a) Kuandika herufi ndogo Herufi ndogo za irabu Kadi za herufi, video 22
stadi za za irabu (a, e, i, o, u), (a, e, i, o, u), konsonanti zinazoonesha namna ya
kuandika konsonanti (b, m, k, (b, m, k, d, n) ; (l, t, p, kuandika herufi ndogo za
d, n); (l, t, p, s, f, j); s, f, j); (g, y, z, h, r, w, v, irabu na konsonanti kwa

D
(g, y, z, h, r, w, v, ch) ch) zimeandikwa kwa mpangilio kwa kufuata
kwa mpangilio kwa mpangilio kwa kufuata hatua
kuzingatia hatua hatua
(b) Kuandika herufi kubwa Herufi kubwa za irabu na
za irabu (A, E, I, O, U), konsonanti zimeandikwa
konsonanti (B, M, K, kwa mpangilio na kufuata
D, N); (L, T, P, S, F, J); hatua
(G, Y, Z, H, R, W, V,
CH) kwa mpangilio na
kufuata hatua
(c) K uandika herufi Herufi mwambatano (sh,
mwambatano (sh, th, th, mb, ny, ng, nd, kw, mw)
mb, ny, ng, nd, kw, zimeandikwa
mw)

13
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(d) Kuandika silabi Silabi zinazotokana na
zinazotokana na herufi herufi za konsonanti na
za konsonanti na irabu irabu zimeandikwa

ft
(e) Kuandika silabi za herufi Silabi mwambatano za
mwambatano herufi zimeandikwa

a
(f) Kuandika sentensi fupi Sentensi fupi
zimeandikwa

r
2.3 Kutumia Kubaini alama za uandishi Alama za uandishi Alama za uandishi 12
kanuni za (nukta, mkato, alama (nukta, mkato, zilizorekodiwa, matini
uandishi ya kuuliza na alama ya alama ya kuuliza na zinazoonesha alama za

D
mshangao) alama ya mshangao) uandishi na kadi/chati
zimebainishwa zinazoonesha alama za
uandishi
3.0 Demonstrate 3.1 Develop (a) Imitate different sounds Different sounds are Books, realia, pictures, 30
mastery listening (eg. Sounds of animals, imitated (eg. Sounds of word lists, wall charts,
of basic and hand clap etc) animals, hand clap etc) audial/audio-visual
English speaking (b) Relate words with Words are related with materials, paper and
language skills in familiar objects found in objects in the familiar coloured pens/chalks
skills different the environment environment
contexts (c) Follow simple instructions Simple instructions
given at school and home given at school and
(e.g. go out, stand up, home are followed
jump, clap your hands,
touch your head and sit
down)

14
Umahiri Umahiri Shughuli za Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi ujifunzaji na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa

(d) Name parts of the Parts of the body are


body orally named orally

ft
3.2 Develop early (a) Pronounce English English letter sounds Wall chats, letter cards, real 40

a
literacy and letter sounds (a-z) (a-z) are pronounced objects and audial/audio-
Numeracy visual materials

r
(b) Recognise English English sounds are
skills
sounds in different recognised in different
spoken words spoken words

D
(c) Identify words Words with the same
with the same last last sounds (rhyming)
sounds (rhyming) and words with the
and words with the same first words
same first sound (alliteration) are
(alliteration) identified

(d) Blend letter sounds Letter sounds are


to form words blended to form words

(e) Associate letter Letter names are


names with sounds associated with sounds

15
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(f) Recognise numbers Numbers are
and talk about times recognized and

ft
of the day times of the day are
expressed

a
3.3 Communicate (a) Introduce oneself One introduces Books, real objects, 10
in different and others himself/herself and pictures, word lists, wall

r
contexts others charts, audial/audio-visual
materials, paper and
(b) Use common Common greetings
coloured pens/chalks
greetings and polite and polite expressions

D
expressions are used
(c) Say goodbye to One says goodbye to
others others
4.0 Kuhesabu 4.1Kutambua (a) Kubaini dhana Dhana ya namba Video zinazojenga dhana 29
dhana ya ya namba kwa kwa kutumia vitu ya namba, vitu halisi,
namba kutumia vitu katika katika mazingira kadi za namba, kibao
mazingira imebainishwa fumbo, sinia la namba,
chati ya namba, abakasi
(b) Kubaini namba Namba kuanzia
kuanzia 1-100 kwa 1-100 kwa tarakimu
tarakimu na maneno na maneno
zimebainishwa

16
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(c) K
 upanga namba kwa Namba kwa mfuatano
mfuatano 1-100 1-100 zimepangwa

ft
4.2 Kutumia (a) Kutambua namba katika Namba katika makumi na Video zinazohusu matendo 38
matendo makumi na mamoja mamoja zimetambuliwa ya namba, vitu halisi, kadi

a
ya za namba, kibao fumbo,
kihisabati (b) Kutumia vitu/TEHAMA Vitu vimeongezwa kupata sinia la namba, chati ya

r
kumudu dhana ya jumla isiyozidi 99 namba na abakasi
kujumlisha
(c) Kujumlisha namba Namba zimejumlishwa

D
kupata jumla isiyozidi 99 kupata jumla isiyozidi 99
(d) Kutumia vitu/TEHAMA Vitu vimepunguzwa
kumudu dhana ya kutoa usahihi zisizozidi 99
(e) K
 utoa namba zisizozidi Namba zimetolewa kwa
99 idadi zisizozidi 99

4.3 Kutumia (a) Kubaini maumbo ya Maumbo ya msingi Video zinazohusu maumbo 29
dhana za msingi yamebainishwa yaliyorekodiwa, vitu halisi,
kihisabati kadi na chati za picha za
maumbo

17
Umahiri Umahiri Shughuli za Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi ujifunzaji na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
5.0 Kuthamini 5.1 Kuthamini (a) Kubaini vyakula Vyakula vya Sanaa na michezo 8
utamaduni, utamaduni vya Kitanzania Kitanzania iliyorekodiwa, vitu halisi,
sanaa na wake na vimebainishwa vifani mbalimbali, chati

ft
michezo wa watu (b) Kubaini mavazi Mavazi ya Kitanzania za picha zinazoonesha
wengine vyakula, mavazi, ngoma za

a
ya Kitanzania yamebainishwa
kitanzania zilizorekodiwa,

r
(c) Kucheza ngoma Ngoma na nyimbo ngoma na filimbi
na kuimba zimechezwa na
nyimbo za asili kuimbwa

D
5.21 *** (a) Kueleza Ameelezea imani za 8
Kuheshimu imani za watu watu wanaomzunguka
tofauti za wanaomzunguka
kiimani (b) Kushirikiana Shughuli za kijamii
katika shughuli zimefanyika kwa
za kijamii kushirikiana
5.3 Kuonesha (a) Kutenda Matendo ya kimaadili Matendo yenye maadili 8
matendo matendo yenye yametendwa yaliyorekodiwa, kadi
yenye kimaadili za picha zinazoonesha
kimaadili kuthamini watu wengine na
chati za sheria mbalimbali
mfano sheria za shule
1 ***Umahiri mahususi huu wa 5.2 utafundishwa na viongozi wa imani husika katika kipindi cha dini

18
Umahiri Umahiri mahususi Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(b) Kutenda matendo Matendo
yanayoonesha yanayoonesha

ft
kuthamini watu kuthamini watu
wengine wengine yametendwa

a
5.4 Kubuni kazi za (a) Kusuka, kufinyanga, Amesuka, Kazi za sanaa 16
sanaa kuchora, kupiga amefinyanga, zilizorekodiwa vitu

r
chapa, kutunga vitu amechora, amepiga halisi na chati za picha
na kupaka rangi chapa, ametunga vitu zinazoonesha watu
na amepaka rangi wakisuka, kufinyanga,

D
(b) Kuimba nyimbo na Nyimbo na mashairi kutunga vitu, kupaka
mashairi zimeimbwa rangi, kuimba nyimbo na
mashairi yaliyorekodiwa
(c) Kucheza ngoma na Ngoma na muziki
muziki imechezwa

5.5 Kushiriki Kufanya mazoezi sahili ya Mazoezi sahili ya Vitu halisi, chati za 10
katika michezo viungo (wepesi, msawazo viungo yamefanyika picha, na michezo sahili
mbalimbali na uratibu wa mwili) iliyorekodiwa

19
Umahiri Umahiri mahususi Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
6.0 Kutunza 6.1 Kutunza afya (a) Kusafisha mwili wake Mwili umesafishwa Vitu halisi, chati za picha, 7
afya na yake na jamii na video zinazoonesha
mazingira inayomzunguka michezo sahili

ft
(b) Kutunza mavazi yake Mavazi yametunzwa
Vifaa halisi vya kusafishia
mwili na mavazi, chati za

a
picha zinazohusu usafi wa
mwili na mavazi, video

r
zinazohusu utunzaji wa
afya
6.2 Kujilinda na (a) Kuepuka mazingira Mazingira na vitu Chati ya alama za 10

D
mazingira na vitu hatarishi hatarishi vimeepukwa usalama, picha za
hatarishi wanyama, matukio
(b) Kubaini alama za Alama za usalama na maeneo hatarishi,
usalama barabarani na barabarani na katika mazigira hatarishi
katika mazingira yake mazingira yake na alama za usalama
zimebainishwa barabarani zilizorekodiwa
na katika mazingira

20
Jedwali Na. 4: Maudhui ya Darasa la II
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa

ft
1.0 Kusoma 1.1 Kutambua (a) Kubaini sauti katika Sauti katika maneno Vitu halisi, kadi na 98
sauti za maneno zimebainishwa chati za picha, herufi,

a
herufi (b) Kuunganisha sauti za Sauti za herufi za silabi, maneno na video
herufi za konsonanti konsonanti mwambatano zinazohusu sauti za

r
mwambatano na irabu na irabu zimeunganishwa herufi za konsonanti
kusoma silabi (gh, ng’, na silabi zimesomwa mwambatano na irabu
nz, nj, sw, bw, gw, tw, kusoma silabi

D
dh, pw, vy, fy, my, ml,
ky, py, ft, lw)
(c) Kutamka maneno Maneno yenye
yenye silabi silabi mwambatano
mwambatano yametamkwa
(d) Kutambua sauti Sauti zinazounda
zinazounda maneno maneno katika sentensi
katika sentensi zimetambuliwa
1.2 Kutambua (a) Kuunganisha sauti za Herufi ambatani zenye Vitu halisi, kadi na 98
uhusiano herufi mwambatano konsonanti mbili na chati za picha, herufi,
wa sauti zenye konsonanti irabu zimeunganishwa silabi, maneno na video
na herufi mbili na irabu ili ili kusoma silabi zenye sauti za herufi
kuunda silabi (gh, ng’, mwambatano katika mwambatano zenye
nz, nj, sw, bw, gw, tw, makundi yote konsonanti mbili na irabu

21
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
dh, pw, vy, fy, my, ml, ky, py,
ft, lw) na kutambulisha herufi

ft
mwambatano zenye maneno
ya kukopa (bl, sp, sk, pt, st,
ks, kt, pl, al, ar)

a
(b) Kuunganisha silabi kusoma Silabi zimeunganishwa

r
maneno yenye konsonanti kusoma maneno yenye
tatu na irabu (njwa, nywe, konsonanti tatu na irabu
shwa, ngwa, mbwe, ndwa, (njwa, nywe, shwa,

D
ng’we) ngwa, mbwe, ndwa,
ng’we)
(c) Kuunganisha maneno Maneno
kusoma sentensi yameunganishwa
kusoma sentensi
1.3 Kusoma (a) Kusoma kwa kujiamini Kifungu cha habari/ Matini zilizorekodiwa
kwa kifungu cha habari/hadithi hadithi linganifu kwa
ufasaha linganifu kwa kuzingatia kuzingatia matamshi
matamshi sahihi ya maneno sahihi ya maneno
kimesomwa kwa
kujiamini

22
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(b) Kusoma kifungu cha habari/ Kifungu cha habari/
hadithi linganifu kwa kasi hadithi linganifu kwa

ft
stahiki (maneno 50 kwa kasi stahiki (maneno
dakika) 50 kwa dakika)

a
kimesomwa

r
(c) Kusoma kwa kujiamini Kifungu linganifu cha
kifungu linganifu cha habari/ habari/hadithi kwa
hadithi kwa hisia na kwa hisia na kwa kuzingatia
kuzingatia alama za uandishi alama za uandishi

D
(nukta, mkato, alama ya (nukta, mkato, alama
kuuliza, alama ya mshangao) ya kuuliza, alama ya
mshangao) kimesomwa
kwa kujiamini

(d) Kusoma kwa sauti kifungu Kifungu cha habari/


cha habari/hadithi sahili hadithi sahili
kimesomwa kwa sauti

23
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
1.4 Kusoma na (a) Kutafsiri na kuelezea Matukio yametafsiriwa Picha za matukio, kadi za 58
kusikiliza matukio (Kupanga na kuelezewa (Kupanga sentensi, video zinazohusu

ft
kwa ufahamu na kusoma sentensi na kusoma sentensi kwa kusoma na kusikiliza
kwa kufuata mtiririko kufuata mtiririko sahihi kwa ufahamu na matini

a
sahihi wa matukio, wa matukio, kusoma zilizorekodiwa
kusoma sentensi sentensi zenye mtiririko

r
zenye mtiririko sahihi, kupanga na
sahihi, kupanga na kusoma sentensi
kusoma sentensi zilizochanganywa ili

D
zilizochanganywa kuleta mtiririko wenye
ili kuleta mtiririko mantiki)
wenye mantiki)
(b) Kusimulia matini Matini fupi zimesomwa
fupi aliyoisoma kwa kwa mtiririko wa
mtiririko wa matukio matukio yenye mantiki
yenye mantiki
(c) Kusikiliza matini Matini sahili
sahili kwa ufahamu imesikilizwa kwa
ufahamu
(d) Kusoma matini sahili Matini sahili imesomwa
kwa ufahamu kwa ufahamu

24
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
2.0 Kuandika 2.1 Kutumia (a) Kutumia alama za Alama za uandishi Video zinazohusu kanuni 195
kanuni za uandishi (kuandika zimetumika za uandishi na matini

ft
uandishi habari fupi kwa zilizorekodiwa zinazohusu
kuzingatia alama za kanuni za uandishi

a
uandishi, kuandika insha
fupi kwa kuzingatia

r
alama za uandishi,
kubaini alama za
uandishi zinazokosekana

D
katika matini)

(b) Kuandika mwandiko wa Mwandiko wa chapa


chapa wenye kikonyo wenye kikonyo
umeandikwa
(c) Kuandika matini fupi Matini fupi
kwa mtiririko wa imeaandikwa kwa
matukio wenye mantiki mtiririko wa matukio
wenye mantiki

25
Umahiri mkuu Umahiri Shughuli za Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mahususi ujifunzaji na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
3.0 Demonstrate 3.1 Develop (a) Use singular and Singular and plural Books, real objects, 87
mastery of listening and plural forms of forms of names pictures, word lists, wall

ft
basic English speaking names of objects of objects found charts, audial/audio-visual
language skills in found in the in the immediate materials, drawing papers

a
skills different environment environment are used and coloured pens/chalks
contexts
(b) Listen and Questions on simple

r
respond to simple sentences are
sentences answered
3.2 Develop (a) Manipulate Phonemes are Books, real objects, 147

D
early phonemes (delete, manipulated to form pictures, word lists, wall
Literacy and add and substute) new words (delete, charts, audial/audio-visual
Numeracy phonemes add and substute) materials, drawing papers
skills (sounds) to form and coloured pens/chalks
new words
(b) Pronounce English sounds in
English sounds in different written
written words words are pronounced
(c) Read and write Simple English words
simple English are read and written
words (e.g. bag,
ten, did, dog, sun)

26
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi upimaji na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(d) Read words with Words with two

ft
two consonant consonant clusters
clusters (e.g. bl, cl, (e.g. bl, cl, fl, gl,

a
fl, gl, pl, sl, br, cr, pl, sl, br, cr, dr, fr,
dr, fr, gr, pr, tr, sc, gr, pr, tr, sc, sk,

r
sk, sm, sn, sp, st, sm, sn, sp, st, and
tw) and words with
and tw) and words
consonant digraphs
with consonant
(e.g. th, ch, sh, ph)

D
digraphs (e.g. th,
are read correctly.
ch, sh, ph)
(e) Read and write Simple sentences
simple sentences are read and
written
(f) Use basic Basic punctuation
punctuation marks marks are used in
in sentences (target: sentences
full stop, comma
and question mark)
(g) Express days of the Days of the week
week and months of and months of the
the year year are expressed

27
4.0 Kuhesabu 4.1 Kutumia (a) Kutambua namba Namba Vitu halisi, kadi za namba, 173
matendo ya katika mamia katika mamia kibao fumbo, sinia la namba,
kihisabati zimetambuliwa chati ya namba, abakasi,
Video zinazohusu matendo
(b) Kujumlisha namba Namba
ya kihisabati na matini
kupata jumla zimejumlishwa

ft
zinazohusu matendo ya
isiyozidi 999 kupata jumla
kihisabati zilizorekodiwa
isiyozidi 999

a
(c) Kutoa namba Namba zisizozidi

r
zisizozidi 999 999 zimetolewa

D
28
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(d) Kutumia vitu/TEHAMA Kumudu dhana ya
kumudu dhana ya kuzidisha kama kujumlisha

ft
kuzidisha kama makundi yanayolingana
kujumlisha makundi kwa kutumia vitu/

a
yanayolingana TEHAMA vimetumika

r
(e) Kuzidisha namba kwa Namba kwa tarakimu moja
tarakimu moja kupata zao imezidishwa kupata zao
lisilozidi 100 lisilozidi 100

D
(f) Kutumia vitu/TEHAMA Dhana ya kugawanya
kumudu dhana ya kama kutoa makundi
kugawanya kama kutoa yanayolingana kwa
makundi yanayolingana kutumia vitu/TEHAMA
vimetumika
(g) Kugawanya namba Namba zisizozidi 100
zisizozidi 100 bila baki zimegawanywa bila baki

4.2 Kutumia (a) Kubaini dhana ya sehemu Dhana ya sehemu kwa Vitu halisi, kadi na 100
dhana za kwa kutumia vitu halisi kutumia vitu halisi na chati za picha na video
kihisabati na TEHAMA (nzima, TEHAMA (nzima, nusu, zinazohusu dhana za
nusu, robo, theluthi, robo, theluthi, theluthi kihisabati
theluthi mbili n.k) mbili n.k) imebainishwa

29
Umahiri mkuu Umahiri Shughuli za Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mahususi ujifunzaji na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
(b) Kuonesha Ameonesha sehemu
sehemu kwa kwa kutumia namba

ft
kutumia namba ( 41 , 21 n.k)
( 41 , 21 n.k)

a
(c) Kutumia stadi Stadi za vipimo katika

r
za vipimo miktadha mbalimbali
katika miktadha zimetumika
mbalimbali

D
(d) Kutumia Maumbo ya msingi
maumbo ya kuumba maumbo
msingi kuumba mbalimbali
maumbo yametumika
mbalimbali
5.0 Kuthamini 5.1 Kuthamini (a) Kubaini makazi Makazi ya asili Kadi na chati za picha 10
utamaduni, utamaduni ya asili ya ya Kitanzania na video zinazohusu
sanaa na wake na wa Kitanzania yamebainishwa utamaduni, sanaa na
michezo watu wengine michezo
(b) Kubaini shughuli Shughuli mbalimbali
mbalimbali za jamii za Kitanzania
za jamii za zimebainishwa
Kitanzania

30
Umahiri Umahiri Shughuli za ujifunzaji Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu mahususi na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
5.2***2Kuheshimu (a) Kuhusianisha imani na Amehusianisha imani 10
tofauti za maadili mema na maadili mema
kiimani

ft
(b) Kujali matendo ya Amejali matendo ya
imani za watu wengine imani za watu wengine

a
5.3 Kubuni kazi za (a) Kushiriki katika sanaa Ameshiriki katika Kadi, chati za picha 22

r
sanaa za utendaji wa mikono sanaa za utendaji wa na kazi za sanaa
(kufuma, kufinyanga, mikono (kufuma, zilizorekodiwa
kuchonga, kushona, kufinyanga, kuchonga,
kutia nakshi) kushona, kutia nakshi

D
(b) Kushiriki katika sanaa Ameshiriki kufanya
za ubunifu wa sauti sanaa za ubunifu
(ngonjera, majigambo, wa sauti (ngonjera,
vichekesho) majigambo,
vichekesho)
(c) Kufanya sanaa Sanaa zinazohusisha
zinazohusisha utendaji utendaji wa mwili
wa mwili (kuigiza, (kuigiza, mijongeo ya
mijongeo ya mwili) mwili) zimefanyika

2 ***Umahiri mahususi huu wa 5.2 utafundishwa na viongozi wa imani husika katika kipindi cha dini

31
Umahiri Umahiri mahususi Shughuli za Vigezo vya upimaji Zana za ufundishaji Idadi ya
mkuu ujifunzaji na ujifunzaji vipindi
zinazopendekezwa
5.4 Kushiriki Kucheza michezo Michezo sahili Vitu halisi na michezo sahili 16
katika michezo sahili imechezwa iliyorekodiwa

ft
mbalimbali
6.0 Kutunza 6.1 Kuchunguza Kufanya uchunguzi Uchunguzi sahili wa Picha, vitu halisi na video 26

a
afya na vitu vilivyopo sahili wa viumbe viumbe hai na visivyo zinazohusu kuchunguza vitu

r
mazingira katika hai na visivyo hai hai umefanywa vilivyopo
mazingira katika mazingira
yanayomzunguka

D
6.2 Kujilinda na Kuzingatia alama Alama za usalama Picha, vitu halisi na 19
mazingira za usalama barabarani na katika mazingira hatarishi
hatarishi barabarani na katika mazingira yake yaliyorekodiwa
mazingira yake zimezingatiwa

6.3 Kuwa na Kushiriki Ameshiriki katika Kadi na chati ya picha, vitu 19


mtazamo katika shughuli shughuli zinazohusu halisi na matini zinazohusu
chanya kuhusu zinazohusu mazingira shuleni mazingira zilizorekodiwa
mazingira mazingira shuleni

32
Bibliografia
Budgell, G & Ruttle, K. (2015). Cambridge primary english. Cambridge University Press.
Collins, H. (2011). Easy learning english vocabulary. Harper Collins.
Crichton, J & Koster, P. (2006). English made easy. Tuttle Publishing.
Hallwell, S. (1992). Teaching english in the primary classrooms. Longman.

ft
Herring, P. (2016). Complete english grammar rules. FARLEX International.

a
Mauritius Institute of Education (2005). National curriculum framework, grades 1 to 6. Republic of Mauritius.
Ministry of Education and Vocational Training. (2014). Education and training policy. MoEC.

r
Ministry of Education, Science and Technology. (2019). English language syllabus for primary education. Ministry of education
Science and Technology.
Ministry of Education. (2003). Zambia basic syllabi grades 1-7. Ministry of Education.

D
Murphy, R. (2007). Essential grammar in use (3rd ed). Cambridge University Press.
Murphy, R. (2019). English grammar in use (5th ed.). Vivar Printing.
Persekutuan, P. P. K. (2013). Malaysia education blueprint 2013-2025 (Preschool to Post-Secondary Education). Putrajaya:
Kementerian Pendidikan Malaysia.
Random, P. (2016). English for Everyone. Penguin Random House.
Seaton, A. & Mew, Y.H. (2007). Basic english grammar for english language leaners. Saddleback Educational.
Republic of Kenya, (2019). Basic education curriculum framework nurturing every learner’s potential. Kenya Institute of
Curriculum Development.
Taasisi ya Elimu Tanzania. (2022). Ripoti ya maoni ya wadau kuhusu uboreshaji wa mitaala ya elimu ya awali, msingi, sekondari
na ualimu. Taasisi ya Elimu Tanzania.
The United Republic of Tanzania (2019). National curriculum framework for basic and teacher education. Ministry of Education,
Science and Technology.

33
r aft
D
34
r aft
D
35
r aft
D
36
r aft
D
37
r aft
D
38

You might also like