You are on page 1of 16

Sauti ya Waislamu

Mh. Rais Kikwete msimamo ni ule ule

ISSN 0856 - 3861 Na. 1027 SHAABAN 1433, IJUMAA JULAI 27-AGOSTI 2, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Waislamu wanasisitiza hawashiriki sensa Hoja sio visima vya maji, hospitali, shule Kuachwa Dini si uzalendo. Ni nia mbaya Itawekwa siku Maaskofu watakapotaka

Afande Azizi mche Mola Zalzala ya Kiama nzito

RAIS Jakaya Kikwete. Uk. 3

Kila anayenyonyesha atamtupa mtoto Wenye mimba wataharibu mimba zao Unaona watu utadhani wamelewa lakini Hawajalewa, ila adhabu ya Allah kali mno

Mansour asema Zanzibar kwanza Ubani wa Emmanuel


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, (ACP) Azizi Juma Mohamed. Uk. 8

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi. Uk. 8

CCM baadae. Asisitiza zile zama za Zidumu kra za Nyerere zimepita Asema Nape aache kuiburuza Zanzibar

kwa wawa Zanzibar

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0652 849227, 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri
AN-NUUR

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

AN-NUUR

Suala la Sensa bado lina utata


Na Bakari Mwakangwale

MAONI YETU

JANA katika kikao cha Bunge, kwenye kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri mkuu, Mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA Mchungaji Msigwa, alimtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutoa msimamo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano kufuatia Serikali ya Zanzibar kuzuia watu kula hovyo mchana na wanawake kuacha kuvaa nusu uchi (vimini) mitaani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani ili kuwapa nafasi wanaofunga swaumu zao zisije kuhatarishwa na vishawishi na kuharibika. Kwa mtazamo wa Mchungaji Msigwa, alisema SMZ imekandamiza haki za imani za watu wengine visiwani Zanzibar. Pia alisema kuwa hatua hiyo ya SMZ zaidi inahatarisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa mtazamo huo alitaka kujua msimamo wa serikali ya Muungano kuhusu hatua ilizochukua SMZ juu ya heshma hiyo kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Katika kujibu swali la Mchungaji Msigwa, Waziri Mkuu kwa busara zake na kwa kuzingatia historia, mazingira na utamaduni wa watu wa Zanzibar, alisema kuwa Zanzibar ni nchi yenye serikali yake, na kwamba hatua zilizochukuliwa na serikali hiyo zinawahusu watu wa Zanzibar. Alisema huo ni utaratibu wa nchi ya Zanzibar ambao umeridhiwa na watu wake ambao ni asilimia 99 Waislamu. Kuhusu nguo fupi alisema hadhani kwamba kuna watu wastaarabu wanaojali utu wao wanaoweza kushabikia vimini. Waziri Mkuu Pinda alifafanua zaidi kwamba ingekuwa hatua hiyo imehusishwa na serikali ya Muungano, hapo lingekuwa suala jingine. Lakini akabainisha kwamba hata kijumla jumla tu ni dhahiri kwamba Zanzibar ina Waislamu wengi zaidi ya silimia 99. Kwa maana hiyo kwa namna yeyote ile hatua hiyo ya SMZ itakuwa imeridhiwa na Wazanzibar ili kulinda swaumu zao katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Alisema inaonekana Msigwa kakwazika na hatua hiyo ya serikali ya SMZ na kuingiwa na dhana (udini) kwa kuwa yeye ni Mchungaji (Mkristo). Lakini alisema kuwa kwa Zanzibar utaratibu huo umekuwepo

Mchungaji Msigwa Wazanzibar wanaupenda ustaraabu wao

muda mrefu, hata siku za nyuma na kwamba haujawahi kulalamikiwa na Wazanzibar ambao ndio wahusika wakuu. Waziri Mkuu alisema hilo sio jambo kubwa kiasi cha kulifanya kuwa linaweza kuhatarisha muungano kwa kuwa linawahusu Wazanzibari na halijawahi kulalamikiwa na wenyewe wameridhia. Hivyo alimshauri Mchungaji Msigwa hakuna haja ya kukuza jambo hilo kwa kuwa linawahusu Wazanzibar, ambao wengi ni Waislamu. Kwa maana kwamba Serikali ya Muungano haiwezi kuingilia matakwa ya watu wa Zanzibar na serikali yao au kutengua hatua hiyo ya serikali ya Wazanzibar. Tunajiuliza, hivi Mchungaji Msigwa, anadhani kuvaa vimini ni ustaarabu wa kidini? Au achilia mbali dini, anadhani ni jambo la kutetewa na serikali hususan kwa eneo kama la Zanzibar? Na kwa kuzingatia kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Hatudhani kuwa kiimani ni sahihi hata kidogo. Kama alihoji masuala ya kula na vimini kisiasa, basi asingehusisha hoja yake ni mfungo wa Ramadhani huko Zanzibar. Ni vyema Mchungaji Msigwa akaheshimu kwamba Wazanzibar wanaheshimu sana mwezi wa Ramadhani. Ustaarabu wao kiimani hususana katika mwezi huu wa toba ni tofauti kabisa na wa bara. Atambue kwamba Wazanzibar karibu wote ni Waislamu. Wengi wao wanafunga, wanajisitiri, wako katika toba. Huwezi kuwakuta wanakula hovyo au kujiachia uchi hovyo kwa kuwa ni watu wa imani, heshma na ustaarabu. Anavyotaka Msingwa, kwamba watu wawe huru kujiachia na vipedo, vimini, kanga moja, kujilia hovyo hata katika Ramadhani, si Zanzibar. Hilo tumezoea Dar es Salaam, Iringa, Mbeya na miji mingine ya bara. Kwa Zanzibar sivyo. Wa z a n z i b a r k a r n e n a karne huo ndio utamaduni wao kuiheshimu Ramadhani. Wanaheshimu utukufu wa dini yao ya Kiislamu kwa kuwa ndio asili ya imani yao. Tusiwabughudhi. Yatosha kuridhika na vimini vya bara. Tusilazimishe wengine wasiovitaka.

WA K A T I O f i s i y a Takwimu ya Taifa (NBS) ikidai kuwachukulia hatua za kisheria watakao goma kuhesabiwa, tayari vipeperushi vimeanza kusambazwa mitaani, majumbani na Misikitini vikionyesha msimamo wa kutoshiriki zoezi hilo. Osi ya Takwimu ya Taifa kupitia mwanasheria wa Osi hizo, Bw.Oscar Mangula, alinukuliwa na gazeti moja la kila siku jumanne wiki hii akidai watakao kiuka agizo la kuhesabiwa, adhabu kali itachukuliwa dhidi yao ikiwemo kwenda jela miezi sita, faini ya sh. 600,000 au vyote kwa pamoja, bila kufafanua ni kwa mujibu wa kifungu gani cha sheria. Pamoja na taarifa hiyo, An nuur imeshuhudia makaratasi yakiwa yamesambazwa mitaani, Misikitini na katika makazi (nyumba) hususani za Waislamu, yamebeba ujumbe unaosomeka hatutaki kuhesabiwa. Ujumbe na maandishi hayo yamejaa katika karatasi ya A4, kwa ujumla yanasomeka hivi. Wakazi wa nyumba hii hatutaki kuhesabiwa hadi kipengele cha Dini kitakapo wekwa katika Dodoso la Sensa. Pamoja na kuwa vipeperushi hivyo havionyeshi vinatolewa na nani au taasisi gani, lakini vinaashiria ni msimamo w a j a m i i y a Wa i s l a m u ambayo kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakidai kutoshiriki katika zoezi la Sensa mpaka Serikali iingize kipengele cha Dini kiingizwe katika Dodoso la Sensa. An nuur, ilipowasiliana na Naibu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ramadhan Sanze, juu ya vipeperushi hivyo kama vimetolewa na Baraza hilo, alisema wao hawajatoa vipeperushi hivyo. Lakini alisema, kama kuna hali hiyo mitaani ichukulike kuwa ni salamu tosha kwa Serikali, huku akikiri kuwa Baraza limekuwa likiwahamasisha Waislamu kutoshiriki Sensa kwa kuwa Serikali imepuuza maoni ya Waislamu. Akifafanua zaid Sanze, alisema baada ya Serikali kuyapuuza mapendekezo yao yaliyowasilishwa Mjini Dodoma katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini na Osi ya Sensa Taifa (NBS), alisema waliamua kurudi kwa Waislamu na

kuwapa taarifa za kupuuzwa na Serikali. Alisema, Jumuiya na Taa n s is i mb alim b a li za Kiislamu ikiwemo Bakwata, zilitoa msimamo wa pamoja kwa niaba ya Waislamu kuwa hawato shiriki zoezi la Senza mpaka hapo Serikali itakapo weka Dodoso la Dini. Alisema, Waislamu kama seheme ya jamii, nao wametoa angalizo lao la msingi ikiwa ni sharti la kuhesabiwa kama ambavyo jamii ya Wahazabe na Wamasai walivyotoa madai yao ambayo Serikali imeyatekeleza. Akizungumzia kauli ya mwanasheria wa Ofisi ya Takwimu, kuwa kutoshiriki Sensa ni kosa la jina na adhabu yake ni kifungo jela au faini ya Tsh. 600,000, Sanze alisema, vitisho si suluhisho la mgogoro huo baina ya Serikali na Waislamu. A l i w a t a k a Wa i s l a m u kutotishika na kauli hiyo huku akidai wanapaswa kuelewa kuwa kosa ni kumzuia osa wa Sensa kufanya kazi yake ya kuhesabu na si vinginevyo. Alisema, ndio maana wamekuwa wakiwataka Waislamu kutojibishana na mosa hao wa Sensa siku hiyo ya zoezi, badala yake watumie makaratasi kubandika milangoni yakionyesha hawako tayari kuhesabiwa. Alisema, ikiwa Serikali imejipanga kuwakamata Wa i s l a m u , b a s i i a n d a e magereza ya kutosha kwani msimamo wao hautorudi nyuma na kuyumba kwa vitisho vyovyote. A l i s e m a , Wa i s l a m u wanajua umuhimu wa Sensa ndio maana wanahitaji pia kipengele cha dini kiwepo. Katika hatua nyingine kumekuwa na taarifa kutoka sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam, kugoma kuandikishwa vitambulisho vya uraia, zoezi linaloendelea hivi sasa. An nuur, imekuwa ikipokea simu na ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa Waislamu wakitaka ufafanuzi wa zioezi hilo, ambapo wengi wao wanashangazwa na hatua ya makarani hao kuwataka kuorodhesha majina ya hata watoto walio chini ya umri wa mika 18. Taarifa zaidi zinasema, makarani hao wa NIDA, wamekuwa wakipata wakati

m g u m u k w a Wa i s l a m u wakitakiwa kutoa ufafanuzi pale wanapovuka mipaka ya kuhoji na kutaka kujua idadi ya familia husika. Bw. Mohammed Ally, aliyemfanyabiashara katika soko la Kisutu Kariakoo Jijini Dar es Salaam, akiongea kwa njia ya simu alisema, alilazimika kutoa ufafanuzi katika Msikiti mmoja maeneo ya Kimara Kingongo, baada ya swala ya Inshai, ambapo palikuwa na mikakati ya kugomea zoezi la vitambulisho wakidhani kuwa ni zoezi la Sensa. Mimi ni mpita njia tu niliamua niswali pale swala ya Insha, wenyeji ndio walikuwa katika mjadala kwamba zoezi linaloendelea ni la sensa au la. Walidhani ni Sensa ili wagome na wamesema wazi hawatoshiriki Sensa. Sasa ombi langu Waislamu wapewe ufafanuzi kuhusu haya masuala. Kwamba tusichotakiwa kushiriki ni Sensa ya watu na makazi ambayo itaanza Agosti 26 na suala la kujiandikisha vitambulisho vya uraia Waislamu hatuna tatizo nalo tujitokeze kwa wingi. Alisema Bw. Ally. Akizungumzia suala hilo Ramadhani Sanze, alisema ni kweli wamekuwa wakipokea taarifa nyingi na kutoka sehemu mbalimbali juu ya susla hilo huku akiwapongeza Waislamu kuwa makini na suala la Sensa. Alisema, baada ya kufatilia waligundua kuwa si kwamba Waislamu hawaelewi au wanachanganya mambo hayo mawili, bali makarani wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) walitaka kutumika na Watu wa Takwimu. Akifafanua alisema, maswali waliyokuwa wakiuliza ni tofauti na mahitaji ya suala lao, ambapo wao wanatakiwa waorodheshe watu wenye umri wa miaka 18 tu, lakini akadai wao (NIDA) wamekuwa wakidaiwa kuuliza hadi watoto wadogo ili wawaorodheshe. Waislamu wanajua zoezi lililopo sasa ni vitambulisho vya urai, na matangazo yao yanasema watu wenye umri kuanzia mika 18, ndio watakao andikishwa, hilo hatuna tatizo nalo lakini wao wanataka kuandikisha na wenye umri chini ya miaka 18, hapo ndipo Waislamu wanapowagomea. Alisema Sanze

Mh. Rais Kikwete msimamo ni ule ule


kwa misingi ya dini. Aidha, Rais Kikwete akasema kuwa swali kuhusu dini halijapata WAKATI naanza kuandika kuwepo katika maswali katika makala hii, mara uliingia sensa zote zilizopita. Halipo ujumbe wa maneno katika na halijawahi kuwepo. s i m u y a n g u . U j u m b e alisema. unasema: Mheshimiwa Rais Kikwete Watu wa sensa wakikuuliza alisema hayo hivi karibuni jina lako nani? Sema Muislamu kwenye mkutano wa wananchi mdhulumiwa. Una umri katika eneo la Swaya, nje gani? Mwambie miaka 50. kidogo ya Mji wa Mbeya Una mke? Mwambie ndiyo. wakati akizindua mradi Anaitwa nani? Mwambie mkubwa wa maji kwa Jiji la Masikini Binti Fakiri. Je, una Mbeya na vitongoji vyake. watoto wangapi? Mwambie Nafahamu kuwepo madai wanne. Wa kwanza anaitwa ya baadhi ya watu kutaka swali Kukosa Elimu, 2. Kukosa la watu kuwa na dini gani Ajira. 3. Ubaguzi wa Kidini. liingizwe. Swali hili halipo 4. Kupuuzwa madai yetu. na halikuwahi kuwepo kwa Kisha ukamalizia kwa nia njema kabisa, alisema maneno yafuatayo: Tuma na kuongeza: Hatupangi kwa watu 10 tu ujumbe huu. mipango yetu ya maendeleo Hii ikiwa na maana kuwa kwa misingi ya dini au rangi ujumbe huu unasambaa za watu bali kwa kuzingatia kwa Waislamu wengi kadiri maeneo na shughuli, mambo iwezekanavyo. ambayo hunufaisha watu wa U j u m b e h u u u n a k u j a dini zote. kufuatia kauli za baadhi ya Akatoa mfano akisema viongozi wa taasisi za Kiislamu kuwa hata mradi wa maji kusisitiza kuwa msimamo wao a l i o k u w a a k i f u n g u a ni ule ule kwamba wataendelea utawanufaisha Waislamu na kuwahamasisha Waislamu Wakristo na sio watu wa dini wasishiriki sensa. Sasa kama fulani pekee. wataweza kusimamia na Binafsi nadhani kuwa kufanikisha msimamo wao huo, hilo ni jambo jingine. Lakini muhimu hadi sasa ni kuwa wamesimama katika msimamo wao na ndio napenda niujadili kidogo. Masheikh hao wametoa Na Mwandishi Wetu msimamo huo kufuatia kauli ya Rais Mheshimiwa M W E K A H a z i n a w a Jakaya Mrisho Kikwete Chama cha Mapinduzi kwamba kipengele cha dini Zanzibar, Mansoor Yussuf hakitakuwepo katika sensa. H i m i d a m e s e m a y u p o Mara baada ya Mheshimiwa tayari kunyanganywa kadi R a i s k u t o a k a u l i h i y o , ya chama hicho lakini i k a t o l e w a t a h a d h a r i a u hataregeza msimamo wake kitisho kwamba atakayekataa juu ya kuitetea Zanzibar kuhesabiwa ataadhibiwa kwa katika Muungano. kupigwa faini au kifungo Kauli ya Mansoor imekuja jela. Sasa Masheikh kutoa siku chache baada ya chama kauli hiyo na ujumbe kama hicho wilaya ya mjini kutoa huu kusambazwa, ni kuwa m a a m u z i y a k u w a t a k a bado wanaamini kwamba viongozi wenye kupingana na wana hoja za msingi katika msimamo wa chama kurejesha msimamo wao. kadi za chama hicho au kuacha Labda kabla ya kuzipitia tabia hiyo mra moja. na kuzijadili hoja wanazotoa Akizungumza na Idhaa Wa i s l a m u n a M a s h e i k h ya Kiswahili ya Radio ya wao nirejee kauli ya Rais U j e r u m a n i ( D W ) j u z i Mheshimiwa Kikwete kule Mansoor alisema kamwe Mbeya. Kama alivyonukuliwa hawezi kuogopa vitisho na vyombo vya habari, Mheshimiwa Rais amesema vinavyotolewa na watu wenye kujipa madaraka na udikteta kuwa Swali la dini kwenye ambao hawataki mabadiliko sensa: Halipo na halijawahi wala mawazo tofauti. Mansoor aliahidi kuendelea kuwepo. na msimamo wake katika Akisisitiza akasema kuwa kipengele cha dini kudai mabadiliko katika h a k i t a i n g i z w a k w e n y e muundo wa Muungano na maswali ya Sensa ya Watu kusema kwamba msimamo n a M a k a z i k w a s a b a b u wake hautabadilika licha ya lengo ni kutaka kufahamu vitisho vya baadhi ya Viongozi idadi ya Watanzania isaidie wa Chama hicho. Nimesema hayo tokea katika kupanga mipango ya muda mrefu chama hiki maendeleo ambayo haipangwi
Na Omar Msangi

Habari

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

AN-NUUR

Mansour asema Zanzibar kwanza


kimetukuka na kina heshima na maadili yake; ni baadhi ya watu wanataka kutuziba midomo lakini mimi sijasema leo, nimesema tokea 2008-2009 juu ya msimamo wangu juu ya mfumo wa muungano na leo naendelea kusema tena hata ikipidi kunyanynganywa kadi mimi narejea tena kuwa mfumo huu wa serikali mbili sikubaliani nao na nitaendelea kusema hivyo hivyo siwezi kubadilisha maoni yangu leo baada ya kuwa na msimamo miaka yote hiyo, alisisitiza Himid ambaye ni Mjumbe wa NEC. Aidha, alisema Chama Cha Mapinduzi wilaya ya mjini hakina mamlaka ya kuitisha kikao na kutoa maamuzi kama hayo ambapo alisema ni watu wachache wenye nia ya kutaka kuwanyamazisha watu wenye maoni tofauti na wao. CCM wilaya ya mjini hawana mamlaka hayo, lakini pia hawana uwezo wa kutunyamazisha kwani CCM haijakataza wanachama wake kuwa na mawazo tofauti, sasa nashangaa hao wanaosema sisi tumekiuka msimamo wa Chama ni msimamo upi maana mchakato wa katiba upo huru na kila mtu anatakiwa kutoa maoni yake. Alisema Himid. Katika kuonesha kukasirika kwake na uamuzi huo wa kutaka kuwanyanganya kazi, Muweka Hazina huyo wa CCM alisema kwamba ni jambo la aibu kwa CCM Wilaya ya Mjini kufanya vitendo vya kibaguzi na vya udikiteta kutaka kuwafunga midomo watu wasitoe maoni yao. Alisema hakuna makosa kwa wana CCM kuwa na mawazo tofauti kwani kila mmoja ana haki ya kutoa maoni na kueleza msimamo wake na tabia ya kikundi cha watu kujiona wao ndio wenye mamlaka na wenye chama ni kosa na halipaswi kuachiwa. Hao ni wabaguzi hawataki watu waseme ukisema unaonekana msaliti, hao ni watu wenye mawazo mgando hawataki kusikiliza fikra nyengine wanataka wanachosema wao ndio kiwe hicho hicho, hilo haliwezekani na hatutakubali. Alisisitiza. Hata hivyo alisema zama za kusema tunakwenda na kra za mwenyekiti umepitwa na wakati na sasa jamii kubwa inakwenda na vijana ambao wanataka mabadiliko nchini hivyo aliwashauri wana CCM kuwaachia watu watoe maoni yao kwa uhuru kwani katiba

kumekuwa na upotoshaji wa makusudi wa hoja za Waislamu. Hakuna Muislamu aliyetaka kipengele cha dini kiingizwe ili katika kutoa huduma katika jamii, kila watu wapewe huduma zao wao wenyewe kwa mujibu wa idadi yao. Katika kujenga hoja zao Waislamu wanasema kuwa toka mwaka 1967, hakuna sensa iliyowahi kufanyika iliyohusisha kipengele cha dini. Lakini taasisi mbalimbali zikiwemo za umma na za serikali zimekuwa zikitoa takwimu zinazoonyesha Waislamu ni asilimia ngapi na Wakristo wangapi. Kwamba ukipitia takwimu za taasisi zote hizo, zikiwemo za serikali husema kuwa Wakristo ni wengi ikilinganishwa na Waislamu. Waislamu wanahoji, serikali imezipata wapi takwimu hizi? Kama hoja ni kuwa serikali haipangi mambo yake kwa kuangalia dini, hizi taasisi za umma zinazotoa takwimu hizi, zinazichapishwa kwa nia gani na wamezipata wapi? Kwa upande mwingine Waislamu wamekuwa wakileta madai kuwa kumekuwa na

upendeleo ambapo Wakristo wanahodhi nafasi za elimu na ajira nchini. Katika kujibu madai haya ya Waislamu, baadhi ya maosa wa serikali na viongozi wa makanisa wamekuwa wakisema kuwa hiyo ni kwa sababu tangu hapo Wakristo ni wengi nchini. Sasa wanachosema Waislamu ni kuwa kama serikali inaona ni muhimu kuonyesha nchi hii ina Wa i s l a m u w a n g a p i n a Wakristo wangapi, basi iingize kipengele cha dini katika sensa ili jambo hili lijulikane kwa uwazi. Sio mtindo huu wa kinyemela ambao makanisa hupika data zake, taasisi za serikali nazo hupika data zao ambazo huwiana na zile za makanisa na kuziingiza katika nyaraka muhimu. La kama serikali haitaki kuingiza kipengele hicho, basi itumie njia zilezile za kinyemela kujua idadi ya Watanzania wote. Kwa hiyo hoja ni mbili: Ama serikali ikanushe takwimu zilizopo katika taasisi zake ambazo zinaonesha idadi ya Waislamu na Wakristo, na ipige marufuku kutolewa kwa takwimu za aina

hiyo kwa sababu hakuna sensa iliyofanyika kutoa data hizo. Lakini kama serikali inapenda takwimu hizo ziendelee kusambazwa, basi iingize kipengele cha dini ili japo hili lijulikane kwa uwazi. Lakini jambo la kuzingatia hapa ni kuwa kwa kuwa tatizo limekuwa ni kutokuaminiana, kuingizwa kwa kipengele hicho itabidi kuweka utaraibu mpya wa kuhesabu, kukusanya takwimu na kuratibu na kutangaza matokeo. Itabidi kuwe na wawakilishi wa kila dini katika kila hatua ili pasiwe na udanganyifu. Udanganyifu sensa ya 1967 Katika maelezo yake Mheshimiwa Rais Kikwete amesema kuwa katika sensa hii Swali la dini halipo na halikuwahi kuwepo kwa nia njema kabisa. Akitaja hiyo sababu njema akasema kuwa: Hatupangi mipango yetu ya maendeleo kwa misingi ya dini au rangi za watu bali kwa kuzingatia maeneo na Inaendelea Uk. 4

tayari imetoa uhuru huo hivyo CCM hawawezi kuwa juu ya sheria. Hii nchi sio ya CCM peke yake, hapa kuna CUF kuna Chadema na pia kuna vyama vyengine lakini wengine hawana hata vyama sasa hatuwezi kuendelea na watu ambao hawataki kuwa na mabadiliko wenye mawazo mgando zama hizo zimeshapitwa na wakati wa kwenda na fikra za mwenyekiti umekwisha, alisema Mansoor ambaye ni Waziri asiye na wizara maalumu. Mweka Hazina huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, alisema kitendo kilichofanywa cha kutishiwa kunyanganywa kadi ya CCM na baadhi ya viongozi hao ni cha fedheha na kimekitia aibu Chama cha CCM mbele ya wana jamii. Himid alisema yeye ametokana na mifupa ya Chama cha Afro Shiraz (ASP) hivyo suala la kuwepo kwa dhana ya wanachama wa madaraja ndani ya CCM halipo kwa kuwa Chama hicho kinaheshimu misingi ya haki za binadamu na kuwataka wenye kudhani kwamba wao Inaendelea Uk. 4

4
Inatoka Uk. 3
ni nia njema, basi nia njema yenyewe labda ni hiyo ya kuficha aibu ya serikali mwaka 1967 ilipofanya pupa kuchakachua matokeo ya sensa kama inavyodaiwa. Lakini pengine jambo la kuzingatia hapa ni kuwa huenda hata juhudi hizi za serikali kuonyesha kuwa Wakristo ni wengi Tanzania, zilikuwa pia na nia njema. Na nia njema yenyewe ilikuwa kutekeleza ahadi ya Mwalimu Nyerere ya kulipa Kanisa fursa nzuri ya kustawi. Hivi sasa bado Waislamu wanasubiri majibu wa risala yao waliyowasilisha kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Katika risala hiyo wameonyesha kwa mifano hai jinsi ambavyo Baraza la Mitihani na vyombo mbalimbali vya kutoa fursa za elimu zinavyohujumu vijana wa Kiislamu. Anaweza kusema leo Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa katika kuteua watendaji wa Baraza la Mitihani, hatizami kipengele cha dini. Bali anafanya kwa nia njema kwa sababu hatupangi mipango yetu ya maendeleo kwa misingi ya dini au rangi za watu bali kwa kuzingatia mambo ambayo hunufaisha watu wa dini zote. Lakini ndio hawa walioteuliwa kwa nia njema ambao wanakata majina ya akina Abdalla na kuweka jina la Jackson kwenda sekondari. Ndio hawa walioteuliwa kwa nia njema ambao hucha majina ya vijana wa Kiislamu waliofaulu vizuri ili wasichaguliwe kwenda High School, akitokea mtu wa kuwauliza, hushangaa na kuhoji wewe mgeni hapa?. Ukisema mimi sio mgeni ila Muislamu, hubaki wakibabaika kwa kuona kaingia mtu asiyetakiwa. Ndio hawa hawa akina Dr. Joyce Ndalichako ambao hujifungia mahali baada ya mitihani kusahihishwa wakachakachua matokeo na hata wakigundulika na kuzomewa, hawajali kuwa ingekuwa busara kwao kuchutama baada ya nguo kuwavuka. Sasa kama haya yote yanafanyika kwa nia njema, nia njema hii itakuwa ni kwa Wakristo pekee. Ndio maana Waislamu wanahoji, nia njema hii lini itakuwa kwa Watanzania wote? Waislamu hawataki nia njema inayowahusu wao peke yao. Hawataki upendeleo hata kidogo. Wanataka haki na uadilifu.

Habari

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

AN-NUUR

Mh. Rais Kikwete msimamo ni ule ule


shughuli, mambo ambayo hunufaisha watu wa dini zote. Labda nikumbushe kuwa katika sensa ya mwisho iliyofanywa na Wakoloni mwaka 1957, Waislamu walikuwa wengi kuliko Wakristo kwa uwiano wa 3:2. Maana yake ikiwa kuwa katika kila watu 100, Waislamu walikuwa 60 na Wakristo 40. Kama Watanganyika Wa i s l a m u n a Wa k r i s t o walikuwa milioni 20, basi Waislamu walikuwa milioni 12 na Wakristo milioni 8. Miaka kumi baadae, mwaka 1967 Tanganyika huru ilifanya sensa ambapo ilidaiwa kuwa Waislamu walikuwa 30%, Wakristo 32% na wanaofuata dini za asili 37%. Takwimu hizi zilizua maswali ambayo serikali ilishindwa kabisa kuyatolea majibu. Ukiongea na watu waliokuwa serikalini wakati ule watakwambia kuwa taasisi za kimataifa ikiwemo ile ya Umoja wa Mataifa inayohusika na idadi ya watu ilitaka kujua nini kimetokea. Kama Waislamu walikuwa asilimia 60 mwaka 1957, kitu gani kimefanya washuke mpaka asilimia 30 huku idadi ya wapagani ikiongezeka? Taasisi za Umoja wa Mataifa zilitaka kujua, je, kumetokea mauwaji ya Kimbari (genocide) ambapo Waislamu kwa mamilioni wameuliwa? Kama si mauwaji ya halaiki, je, kumetokea njaa ambayo imeuwa Waislamu p e k e y a o ? N a k a ma s i moja kati ya hayo mawili, serikali ionyeshe iwapo ama Waislamu wameritadi au kurejea kwa mamilioni katika ibada za kuabudu mizimu au wamehimizana wasizaane tena. Kwa hiyo kwa miaka 10 wakawa wanakufa tu hakuna anayezaliwa. Serikali haikuweza kujibu wala kutoa maeleo. Matokeo yake inasemekana hata ukizitafuta takwimu hizo leo huwezi kuzipata ambazo kwa hakika waliokuwepo zama hizo wanasema kuwa Waislamu walikuwa asilimia 63% ndio matokeo yakachakachuliwa. Kwa hiyo ilipoka mwaka 1978 ambapo serikali ilifanya sensa nyingine, iliona kama itaweka tena kipengele cha dini halafu ionekane Waislamu wengi, itazidi kuumbuka. Ndio ikaona njia nyepesi ya kucha aibu ni kuondoa kipengele cha dini na imekuwa ikifanyika hivyo hadi leo. Sasa kama Likiundwa Baraza la Mawaziri wengi Wakristo, wakiteuliwa Wakuu wa Wilaya, Mikoa na wakuu wengine katika nafasi nyeti za serikali na taasisi za umma, wengi Wakristo. Wakihoji Waislamu, wanaambiwa tunafanya kwa nia njema. Hatuangalii dini katika masuala ya nchi. Nia njema hii mbona imekuwa na makengeza? Inatizama upande mmoja tu? Pengine labda sasa tufanye jaribio ili kuona utamu wa nia njema hii ya serikali. Itokee mara mbili tatu hivi Mheshimiwa Rais ateuwe watu wasomi, wachapakazi, wenye sifa Waislamu katika nafasi nyeti serikalini, kama wanahitajika maofisa 11, aweke Waislamu 7! Kwa nini ni Waislamu pekee wanatakiwa kuonja utamu huu wa Nia njema hii ya serikali? Wa l i s e m a c h u r a kuwaambia wale vijana waliokuwa wakirusha mawe mtoni: mchezo wenu ni mauti kwetu. Sasa nia njema hii ya serikali ya kuendelea kuona kuwa wanaostahiki kupewa nafasi za Ukuu wa Wilaya, Mikoa, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi kwa wingi ni Wakristo pekee, ni mauti kwa umma wa Kiislamu. Itafika mahali hata hiyo huduma ya maji aliyozindua Mheshimiwa Kikwete Mbeya watashindwa kuitumia kutokana na umasikini katika mwendo huu wa kuchangia huduma za afya na kijamii. Leo vijana wa Kiislamu wanashutumiwa kuwa ndio waliojazana katika jela. Lakini tunasahau kuwa vijana hawa wamejikuta wakiwa hawana la kufanya na kuangukia katika uhalifu baada ya kuporwa nafasi zao za kusoma kwa ile nia njema (?) ya kuchukua watoto wa Kikristo kutoka Peramiho, Songea kuja kuchukua nafasi

Inatoka Uk. 3 ndio wana mamlaka zaidi kuliko wengine waache tabia hiyo. Hivi karibuni chama cha mapinduzi CCM wilaya ya mjini kilitoa tamko la kuwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, akiwemo Mweka Hazina wa CCM Zanzibar, Mansoour na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kuacha mara moja kukiuka maadili ya chama chao kwa kuwa na mtazamo hasi dhidi ya muungano. Juzi akihojiwa na DW, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisikika akisema kwamba viongozi wanaokwenda kinyume na madili ya chama chao watatakiwa kwenda kujieleza katika vikao na iwapo watathibitika wamekwenda kinyume, basi watanyanganywa kazi au kufukuzwa. Nape alisema mwana CCM yeyote hawezi kwenda kinyume na maadili ya chama chake na iwapo atakuwa na msimamo mwengine usiokuwa wa chama hicho, basi atatakiwa kuwasilisha maoni yake ndani ya vikao na iwapo maoni hayo wajumbe hawatayaridhia basi atalazimika kurejesha

Mansour asema Zanzibar kwanza


kadi ya chama hicho iwapo yeye hatokubaliana na msimamo wa kikao. Akizungumzia kauli hiyo ya Nape, Mheshimiwa Himid alisema kuwa Nape hawezi kuwagawa wanachama wa CCM katika matabaka, wale wa Tanzania Bara na Zanzibar kwani wote ni wanachama wana haki sawa mbele ya sheria na katika CCM. Sisi Watanzania hatuna uhuru, yeye amegawa kwa utabaka, sisi ni watu wazima tuna haki na uhuru, Nape hawezi kutwambia sisi watu wazima kwamba tukasema anayotaka yeye, ule wakati wa ndio Mwenyekiti haupo kila mtu ana haki yake kutoa maoni na hata Tume ya Jaji Warioba inasema hivyo. Alisema Himid. Mimi naichukulia kuwa hii ni njama ya kutaka kuwaziba midomo Wazanzibari, hatujakiuka miongozo wala sheria tutaendelea kusema kutaka mabadiliko ya muundo wa Muungano, hii nchi asilimia kubwa ni vijana na vijana wanataka mabadiliko na hilo haliwezi kukwepwa. Aliongeza. Mie nadhani kuna baadhi ya watu wana fikra za udikteta, haiwezekani

za watoto wa Kiislamu wa Bagamoyo, Mkuranga, Chalinze, Kisarawe, Dar es Salaam na Pwani kwa ujumla katika shule ya Kichwele (Dar es Salaam) miaka ya 1940s na 1950s. Anasema Dr. Lawrence E. Y. Mbogoni kwamba kwa mchezo huu, kwa nia nzuri hii ya serikali ya kupora nafasi za watoto wa Kiislamu wa Pwani na kuwapa watoto wa Kikristo wa Peramiho, it happened that a government school which previously had a majority of Muslim students came to have a majority of Christians. Na hapana shaka ndio sababu vijana hawa wa Kiislamu wa Pwani ndio wanaonekana kuwa wengi katika vijiwe vya wapiga debe, mateja wa unga, vibaka, waliojazana rumande na magerezani na waliosalimika wanauza korosho, biskuti na maji pale Chalinze katika magari. (Soma makala uk. 10)

twende kwenye kutoa maoni tukasema tunataka Serikali mbili kama ilivyosema CCM, sisi ni watu wazima tuna haki zetu na tusichaguliwe la kusema na kwa nini tuzibwe au tufungwe midogo? Alihoji. Mansoor amesema msimamo wake kuhusu mfumo wa muundo wa Muungano utabakia kama ulivyo kutaka kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika muundo huo kwani kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kutoka Zanzibar ambayo hayapatiwi ufumbuzi kutokana na kuwepo kwa muundo dhaifu wa Muungano. Alisema hakuna mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano, lakini ni lazima kukawepo kwa Muungano wenye maslahi ambayo hautakuwa na kero na ndio maana wamekuwa wakitoa maoni ya kutaka mabadiliko ya muundo na sio kuvunja. Mimi pia nakubali muungano una manufaa, lakini sikubaliani na mfumo wa Muungano na ndio maana tunasema kuwa mfumo huu sebu(sitaki), alisema Mweka Hazina wa CCM Zanzibar.

Kimataifa

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

AN-NUUR

Ujerumani yasema Iran ina haki kumiliki nyuklia


UJERUMANI imetilia mkazo haki ya Iran ya kuendeleza miradi yake ya nyuklia kama nchi mwanachama wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na iliyosaini mkataba unaopiga marufuku uzalishaji na uenezaji silaha za nyuklia NPT. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle, amesema kuwa Iran ina haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa

malengo ya kiraia na kwamba nchi hiyo imeazimia kuiunga mkono Iran katika vipengele vya kiufundi. Westerwelle pia amesema kuwa Berlin inapendelea suala la nyuklia la Iran litatuliwe kwa njia za kidiplomasia. Iran kwa upande wake imesema kuwa ina haki ya kumiliki teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya kiraia kwa kuwa ni nchi mwanachama wa wakala wa IAEA na imesaini mkataba wa NPT.

ADDIS ABABA SERIKALI ya Ethiopia imetoa taarifa na kukiri kwamba hali ya kiafya ya Waziri Mkuu Meles Zenawi ni mbaya na kwamba kiongozi huyo yuko taabani. Taarifa hiyo imetolewa baada ya kuweko wasiwasi mkubwa nchini humo na

Waziri Mkuu Meles Zenawi mahututi


kuenea uvumi kwamba Zenawi amefariki dunia. Awali serikali ilikanusha kwamba Zenawi ni mgonjwa na kusisitiza kuwa amekwenda nje ya nchi kwa ajili ya likizo fupi. Hata hivyo Msemaji wa serikali Bereket Simon, imefikia mahali imelazimu kueleza kwamba Meles

Nakala ya kwanza ya Qurani ya hati ya braille yazinduliwa


NAKALA ya kwanza kabisa ya Qurani yenye hati ya braille kwa ajili ya walemavu wa macho imezinduliwa nchini Yemen. Sherehe ya uzinduzi wa nakala hiyo ya Qur ani ya walemavu wa macho imesimamiwa na Jumuiya ya Aman inayojishughulisha na masuala ya walemavu hao. Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Yemen Ahmad Abiid, ameipongeza Jumuiya ya Aman na kusema iliasisiwa mwaka 1990 na hadi sasa imefanya kazi kubwa katika kuwasaidia walemavu wa macho nchini Yemen ikiwa ni pamoja na kuchapisha nakala za Qurani kwa hati ya braille. Vilevile Waziri wa Wakfu na Miongozo wa Yemen Hamoud Abbad, amesema katika sherehe hiyo kwamba Wizara yake itachapisha

Zenawi yuko Brussels, Ubelgiji anakopata matibabu na kwamba atarejea nyumbani karibuni hivi. Zenawi hakuweza kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa Umoja wa Afrika AU licha ya kwamba nchi yake ndiyo iliyokuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Qurani ya karne ya 16 yagunduliwa Uturuki


NAKALA ya kitabu kitakatifu cha Qurani imegunduliwa katika uchimbaji wa ngome moja ya kihistoria katika mji wa Kemah katika mkoa wa Arzanjan nchini Uturuki. Ugunduwaji wa kitabu hicho kitakatifu pamoja na maandishi mengine ya kihistoria ulifanywa siku ya Jumamosi na timu ya wataalamu wa mambo ya kale wa Chuo Kikuu cha Ataturk. Q u r a n i h i y o iliyogunduliwa ikiwa imefungwa kwenye kitambaa maalumu imepelekwa katika kitengo cha utafiti wa maandishi ya kihistoria yaliyoandikwa kwa mkono katika Chuo Kikuu hicho. Akizungumzia suala hilo, Dakta Huseyin Yurttas, mhadhiri wa masuala ya kihistoria katika Chuo Kikuu cha Ataturk na

nakala nyingi za Qurani hiyo na kwamba inawasaidia na kuwahami walemavu wa macho. Kwa upande wake Mkuu wa Jumuiya ya Aman amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Qurani yenye hati ya braille kuzinduliwa nchini Yemen. Amesema nakala 150 za Qurani hiyo zitakuwa zikichapisha kila mwaka nchini Yemen kwa ajili ya walemavu wa macho.

OIC yaanzisha mpango kubadilishana wanafunzi nchi za Kiislamu


JUMUIYA ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, inapanga kuanzisha Mpango wa Mabadilishano ya Kielimu katika nchi zote za Kiislamu. Kwa mujibu wa tovuti ya OIC, mpango huo wa mabadilishano ya wanafunzi utawezesha utolewaji wa misaada ya kielimu, masomo kwa njia ya intaneti na kuwepo miradi ya utati katika nchi 57 wanachama. Mpango huo wa OIC ukikamilika unatazamiwa kuwa mkubwa zaidi wa aina yake duniani.

Rais wa Iran Ahmad Najed

Mwezi uliopita OIC ilitangaza nafasi 10 za msaada wa masomo (scholarship) katika Chuo Kikuu cha Kuala Lumpur nchini Malayasia. Uturuki pia imetangaza azma ya kutoa msaada wa masomo katika mpango huo wa OIC.

CAIRO Rais Mohammed Mursi wa Misri amemteua Hashim Qandil aliyekuwa Waziri wa umwagiliaji kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo. Qandil ambaye si maarufu sana ambaye ana shahada ya Uzamivu aliyoipata Chuo Kikuu cha North Carolina nchini Marekani mwaka 1993, alichaguliwa mwezi Julai mwaka jana kuwa Waziri baada ya kuondolewa madarakani

Hashim Qandil Waziri Mkuu mpya wa Misri

mkuu aliyesimamia timu ya uchimbaji katika ngome hiyo ya kale, amesema vitu vingine vilivyopatikana katika uchimbaji huo ni pamoja na nakala kadhaa za Qurani zlizoandikwa kwa maandishi ya dhahabu za karne za 18 na 19 na vilevile vitabu kadhaa vya qhi, itikadi na maudhui nyingine za Kiislamu.

utawala wa Hosni Mubarak. Msemaji wa Mursi amesema Qandil, ni mtu anayejitegemea ambaye hakujiunga na chama chochote kabla na baada ya harakati za mapinduzi ya wananchi dhidi ya Hosni Mubarak. Rais Mursi amempa Waziri Mkuu huyo mpya jukumu la kuunda serikali ambayo itakuwa ya kwanza ya kidemokrasia inayotokana na mapinduzi ya wananchi.

Makala/Tangazo

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

AN-NUUR

Na Dr. Emad Rabie HAKIKA katika muongozo wa Uislamu kila Muislamu anatakiwa kuamini kila Mtume na kila Nabii ambao amewaleta Mwenyezi Mungu kwa ujumbe toka kwake. Kwa ajili ya kuwaongoa watu wote kuelekea kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Kwani Mitume yote ni ndugu katika dini, wote wanawaita watu katika ibada ya Mungu mmoja. Na mwisho wao ni mmoja, nao ni kuamini kuwa Mwanyezi Mungu ni mmoja na hana mshirika (mwenzake). Amesema Mwenyezi Mungu ameamini Mtume kwa yale aliyoteremshiwa kwake toka kwa Mola wake, na waumini wote wameamini kwa Mwenyezi Mungu na malaika wake na vitabu vyake na Mitume yake na wala hatutofautishi hata mmoja katika Mitume yake, na wakasema tumesikia na tumetii basi msamaha ni kwako Mola wetu na kwako ndio marudio Surat Baqara. Na katika hadithi ndefu aliyoipokea Imamu Muslimu na wengineo toka kwa Omar Bin Khatwab (R.A) na ndani yake kuwa Jibril (A.S) alikuja kwa Mtume (S.A.W) akiwa na uso wa binadamu akimuuliza juu ya imani na Uislamu na Ihisani? Akasema ni nini Imani? Akasema ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume yake na siku ya mwisho na kuamini uwezo wake kwa heri na shari inatoka kwake Na katika Uislamu hii ni imani thabiti na inahimizwa na wala haiyumbi yumbi kamwe Na yeyote mwenye kumkanusha Mtume yeyote miongoni mwa Mitume atakuwa ni kafiri katika Uislamu kwani hii ni nguzo miongoni mwa nguzo za imani katika Uislamu. Kinachotakiwa kwa Muislamu nikuamini manabii wote na akataye mkanusha mmoja miongoni mwao atakuwa ni kari kwa mwenyezi Mungu Mtukufu kwani kwa kufanya hivyo atakuwa ameipinga

kur-ani kwa uwazi, ambayo imetaja Mitume yote na Manabii wote. Amesema mwenyezi Mungu Mtukufu (hakika ya wale wanaokufuru kwa Mwenyezi Mungu na Mitume yake na wanataka kuwabagua kati ya ALLAH na Mitume yake na wanasema tumeamini baadhi ya Mitume na tunaikufuru baadhi ya Mitume na wanataka kuifanya hiyo ndio njia yao, hao tu ndio makafiri wa kweli, na tumewaandalia kwa makari adhabu yenye kunyongesha, na wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume yake na wala hawawatenganishi hata mmoja kati yao, wao tu tutawapa malipo yao na hakuacha kuwa Mwenyezi Mungu msamehevu na mwenye Rehema) Surat Nisai. Na kutoka katika hadithi sahihi toka kwa Mtume (S.A.W) amesema (yeyote mwenye kushuhudia kwamba hakuna apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa mwenyezi Mungu peke yake, hana mshirika nae na Muhammad ni mja wake na Mtume wake na Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na ni Mtume wake na neno lake amelitupa kwa

Imani ya Mitume yote inatokana na muongozo wa Kiislamu

Kamati Maalumu ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an tukufu kwa shule za Misingi za Kiislamu Jijini Dar es salaam , Inawaalika waislamu wote nchini katika Mashindano ya Sita ya Hifdhul Qur-aan. Siku: Mahala: Muda: Jumapili 29/ 07/2012 Ukumbi wa Diamond Jubilee Saa 2:00 Asubuhi hadi Saa 6:30 Mchana

Mashindano ya Sita ya Hifdhul Qur-aan

Mariam na roho ni kutoka kwake na akaamini kuwa pepo na moto ni kweli vipo. Atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kwa matendo yake yoyote aliyonayo. Na katika surat Nisai anabainisha Mola wetu mtukufu kwamba ameteremsha ufunuo kwa kila Nabii na akasema (hakika sisi tumekuteremshia ufunuo

kama tulivyo wateremshia Nuhu na Manabii wengine baada yake na tuka mteremshia Ibrahimu na Ismaili na Is`haka na Yakubu na Asbat na Issa na Ayubu na Yunus na Haruna na Sulemani na tukampa Daudi Zaburi) ametuamrisha Mola wetu mtukufu tuwapokee wale wanaosilimu kutoka Mayahudi na Wakristo ambao hawajidhulumu na tuwaambie

wao kama alivyosema Mola wetu (Na wala Msijadiliane na Mayahudi na Wakristo (Ahlukitabu) isipokuwa kwa wema isipokuwa wale wenye kudhulumu miongoni mwao na semeni tumeamini yale tulio teremshiwa kwetu na yalioteremshwa kwenu. Na Mola wetu na Mola wenu ni mmoja na sisi kwake tunanyenyekea) Surat Ankabuti.

Shime waislamu wote tuhudhurie kwa wingi kwani ni mpambano wa aina katika Kusherehekea miaka 1442 tangu kushushwa Qur-an tukufu kutoka lauhu mahfoudh ( Uwingu wa saba) hadi Bait El- Izza ( Uwingu wa Dunia). Shule zitakazoshiriki ni :1. Al- Hikma Islamic English Medium Pr. School 2. Al- Furqaan Islamic English Medium Pr. School- Kongowe 3. Asswiddiq Islamic English Medium Pr. School 4. Ibun Jazaar Islamic English Medium Pr. School 5. Ilala Islamic English Medium Pr. School 6. Luqman Islamic English Medium Pr. School 7. Masjid Qiblatain Islamic English Medium Pr. School 8. Matangini Islamic English Medium Pr. School 9. Mtambani Islamic English Medium Pr. School 10. Sheikhat Hissa Seminary English Medium Pr. School 11. Upeo Islamic English Medium Pr. School 12. Yemeni English Medium Pr. School Wabillah Tauq

7
Kwa utajiri wake Zanzibar imekua kivutio cha aina yake na cha pekee kwa wageni wa karibu na wa mbali, wema na waovu pia. Kwa upande mwingine Wazanzibari kwa utukufu wa khulka nzuri na utajiri wa tabia zao za wingi wa busara na uvumilivu huchukuliwa na wale wenye unyu wa hekima kuwa ni mabwege. We n g i n e o h u d i r i k i kuwaona Wazanzibari ni Wajinga, tena wapumbavu mayakhe. Lakini falsafa ya ubinadamu mara nyingi huashiria kwamba vile umkiriavyo mwenzio ndivyo ulivyo wewe. Ndio maana dini zote hututaka daima tutende mema kwa viumbe vyote wala tusimkirie mwengine ila mazuri tu. Zanzibar kama ilivyo tajiri wa mambo tofauti mazuri na ya kupigiwa mfano ulimwenguni, imebahatika vile vile kuwa na utajiri wa watawala au viongozi wengi wa kigeni na wote lao moja. Nalo ni kuwatumia Wazalendo kama vidaraja vya kufikia kilele cha uroho wa matarajio yao. Tumeshuhudia maafa mengi na majanga mazito yalioikumba jamii hii, miaka nenda miaka rudi, jamii ya Wazanzibari imeendelea kunyanyasika, kudhalilika, kusononeka na kuhasimika. Mzanzibari ameamuwa kuishi nje ya mipaka ya kwao, kwa sababu moja au nyengine. Pengine kupunguza joto la roho na dhiki ya kuonewa na kubaguliwa na kubugudhiwa nchini kwao. Tendo hili linamnyima fursa adhimu ya kuchangia maendeleo katika taifa lake. Ukimbizi huu wa kisaikolojia ni mbinu tukufu ya kumfanya mwenyeji, mzalendo atoe mwanya na furaha kwa mtawala. Naye mtawala akie malengo yake kwa kishindo bila ya upinzani na bugudha. Lazima hivi sasa Wazanzibari wajitambue kwamba ni wasafiri wanaokabiliwa na bahari yenye kina kirefu na mawimbi makali, wanapaswa kua imara kwani wasipokua hivyo muda si mrefu kile kidogo kilichobaki nacho kitayoyoma. Nilisoma gazeti la Nipe Habari la June 6-12, 2012 lenye kichwa cha habari kisemacho Mwanakenge anayetamani kundi la mamba makala ilioandikwa na muandishi alijinasibisha kwa jina la Thabiti Jaha Mtwana, Zanzibar. Muandishi ameelekeza lawama na kidole kwa Sheh Farid na kuonyesha kwamba chanzo cha uvunjwaji

Makala

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

AN-NUUR

Siri ya ujasiri wa Sheikh Farid

Na Ibrahim Mohammed Hussein PAHALA popote penye neema hapakosi fitina, choyo na husda. Hujitokeza mtindo wa huyu ndiye, na yule sie. Katika chama na Serikali Viongozi wengi hupenda kujipendekeza na kuegemea kwa yule mwenye sauti na amri, hili hua ni jambo la kawaida. Ta b i a h i i n d i o inayosababisha chuki, kutoelewana, kutoaminiana na kufarakana mmoja kwa mwenziwe au kikundi na kikundi chengine. Iwapo kipo kikundi cha tatu au kuna mtu wa tatu mwenye azma au lengo la kufaidika na tija au neema hiyo, basi urahisi wake ni kusababisha mtafaruku kwa wale wawili au vile vikundi viwili au vyama viwili vihasimiane ili yule mtu wa tatu au kile kikundi cha tatu kifaidike na neema iliyopo kwa hasara ya wale wawili au vile vikundi viwili. Fitina mbaya, tena hana haya wala haoni vibaya, kimaumbile, kitabia kivitendo na ki-khulka. Hivi ndivyo alivyo kiumbe huyu au kikundi hichi au chama hichi. Haridhiki na kitu ila mafanikio ya kufuzu na lake. Hata Qurani maneno ya Mwenyezi Mungu amemueleza mtu wa tna Fitina ni mbaya hata kumzidi muuwaji. Maana yake, muuwaji anaweza kumuuwa mtu, lakini fitna inaweza kusababisha mauwaji ya kijiji kizima. Zanzibar ni njema atakae aje. Huu ni msemo au wito waliourithi mababu zetu na mabibi. Wazanzibari huvuta subira sana katika maamuzi yao, lakini ukapo wakati wa kukata shauri na kutekeleza kamwe huwa si wazito. Huwa wepesi kutenda kila kihitajiwacho. Zanzibar imepita katika hali tofauti ya mitaharuki au mifarakano. Zanzibar imeathirika sana na Muungano huu tulionao hivi sasa. Zanzibar sio nchi masikini kwa idadi ya watu wake walivyo wachache.

SHEIKH Farid Had (wa watatu kutoka kushoto) akiwa na viongozi wengine wa Kiislamu wakiongoza maandamano ya kupinga muundo wa Muungano hivi karibuni, Zanzibar. wa makanisa kimetokana leo Sheikh Farid kuwauliza Makundi yaliyojitokeza n a y e y e k w a k u f a n y a watu mnautakaaa? Jawabu h i v i k a r i b u n i Z a n z i b a r maandamano. Kwanza linalotoka kwa Wazanzibari yakiongozwa na Jumuiya hilo si kweli, maandamano Hatuutakiiii. Mtwana yalifanyika salama usalimin anasema, Farid na wenzake ya Uamsho wa Mihadhara (matembezi ya hiari) wala wameanza kuipigania na ya Kiislamu, yanayopinga h a y a k u s a b a b i s h a h a t a kuitaka iwepo tena Zanzibar M u u n g a n o n a k u t a k a kuvunjika kwa njukuti. b a a d a y a k u p i g w a n a iitishwe kura ya maoni ya wananchi ili kuamua kama M a a n a m a t e m b e z i kupinduliwa mwaka 1964. yalifanyika mchana kweupe, M t w a n a Z a n z i b a r bado kuna haja kuendelea na h a p a n a g h a s i a z o z o t e ilivamiwa na Watanganyika Muungano. Lissu anasema zilizotokea. Mtwana una h a t i m a e i k a m e z w a n a yamesababishwa na hofu chuki kama za kitwana. Muungano ili kupata njia ya kuwaudhi Wazanzibari Sema kweli ghasia hizo ya kuitawala. Sio vibaya Huko mbele ya makala zilisababishwa na Polisi pale kukomboa nchi kwa mara hii nitaweka mambo wazi walipokwenda kumkamata ya pili anakofanya Amiri Sheikh Mussa msikitini Farid. Mtwana inaonyesha ambayo Wazanzibari wengi mbele ya maamuma. Mtwana hukumsikiliza vizuri Mh. hawautaki Muungano kwa kama alivojiita mwenyewe Tundu Lissu alipokuwa sababu hizo, mbali ya wale anasema, Sheikh Farid yeye a k i t o w a m a o n i y a k e wanaoutaka ambao ni jamii na Jumuiya yake walikua Bungeni. Mbuge huyo ya wamezaji. wanataka kupigania lipatikane alisema Katiba mpya ya Mtwana anasema: Farid Taifa jipya la Zanzibar. Zanzibar imejitangazia Uhuru anajiamini mno kama kwamba Mtwana haelewi kwamba na imehakikisha kwamba nyuma yake kuna kundi lenye Zanzibar ni Taifa kongwe sio Uhuru huo utalindwa dhidi nguvu za vita na silaha kamili jipya bali Tanzania ndio Taifa ya tishio lolote la Serikali ya akiamini kuwa litamkinga, jipya. Kinachopiganiwa ni Muungano. litamlinda, kumuokoa na mamlaka kamili ya Zanzibar Sasa Ustadh Farid kazi yake kumsaidia katika kukabili na ipo na watu wake wapo ni nyepesi kwa vile Muungano kila aina ya tishio. sasa Wazanzibari wanataka wa Tanganyika na Zanzibar Kama unaweza kubaini mamlaka yao. umeshavurugwa ndani ya imani hiyo imejengeka Mimi nasema hata hao KATIBA YA ZANZIBAR w a n a o u t a k a M u u n g a n o na wavurugaji ndio hao hao ndani ya moyo wa Amir basi sio huu uliojibebesha Viongozi wa CCM akiwemo Farud na Mwenyezi Mungu mamlaka mbili kwa mpigo. Mh. Makamu Mwenyekiti akaidhihirisha ndani ya akili Mtwana anataka kujua ni wa CCM Zanzibar Dk. yako basi ogopa huyo ni wapi Farid anakoipata ridhaa Ali Mohamedd Shein na mtu wa Mungu kweli kweli inayomfanya ajitokeze na mwenzake Balozi Seif Ali usifanye mzaha. Ishara ya kusimamia matakwa ya Iddi, ni wao walijipinda na pili ni morali inayojitokeza sauti za watu anawaita ni kuibadilisha KATIBA YA kwa Wazanzibari katika kumuunga mkono Shekh Wazanzibari kwa niaba yao. ZANZIBAR. Hiari yashinda Utumwa. Njia Sasa Shekh Farid anamaliza Farid nayo ni ishara tosha hiyo hiyo alioitumia Karume kazi ya kuamsha Wazanzibari kwako. Hayo yote yanatokana kwa kuuliza watu kwamba kwa vile zana zote ziko tayari na kumuamini Mwenyezi wanautaka Muungano au ndani ya Katiba ya Zanzibar. Mungu na kumtegemea yeye hawautaki Muungano na watu Hebu Mtwana soma gazeti la peke yake. Hiyo ndio siri ya wakajibu Tunautakaaa basi Mwananchi la tarehe 11-7- ujasiri aliokua nayo Sheikh ndio hiyo hiyo anayoitumia 2012 uk 4 Lissu anasema: Farid.

8
Na Omar Msangi MOJA ya Adhkari waliyoleta Waislamu pale Masjid Mbuyuni ni kusoma kipande cha aya ya suratut tiin inayosema: Alaisallahu biahkamil haakimiina. Kwamba, Je, Mwenyezi Mungu si Hakimu muadilifu kuliko mahakimu wote? Ikiwa na maana kuwa lazima atawalipa watu wote kwa uadilifu kutokana na matendo yao. Kamanda Azizi Juma Mohamed, amesema kuwa wafuasi wa Uamsho wakiwa na bendera walianza vurugu, kupanga mawe barabarani na kuchoma moto matairi. Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi likaamua kutumia nguvu kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na maji yenye kemikali za kuwasha. Vyombo vingine vya habari vikadai kuwa Uamsho walianza kuwashambulia Polisi kwa mawe. Alaisallahu biahkamil haakimiina. Hapana shaka ipo siku ukweli utadhihiri na kila aliyeumia siku ile ama kupotelewa na kitu, atasimama kudai haki yake. Yote mpaka kauli hii kwamba Masheikh wa Uamsho wakiwa na bendera walianza vurugu, kupanga mawe barabarani na kuchoma moto matairi, itadhihirishwa na kutolewa hukumu na Hakimu Muadilifu. Hiyo ndiyo Siku ambayo vitafunuliwa vitabu ambapo utawaona wakosefu wanavyoogopa kwa yale yaliyomo humo (katika vitabu vyao). Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyo yatenda yamehudhurishwa hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote. (18:49). Hata hili la Msikiti wa Mbuyuni nalo limeandikwa? Watahoji na kushangaa walioamuru kupiga Waislamu mabomu na wale waliotekeleza amri hiyo. Watas ema: O le w etu ! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika. Tunaambiwa Yeye ndiye Mfalme pekee siku hiyoMaalik yaumiddiin. Siku hiyo hatakuwa na nafasi Obama, Kikwete wala Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Leo Kamanda wetu Azizi katika matukio kama hili la kupigwa waumini wakiswalia maiti, ndio msemaji. Ndio tunamsikiliza atupe taarifa rasmi. Ila

Makala

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012


alisema kuwa tutaswali swala ya maiti ghaibu, kisha itapigwa adhana na kufuatiwa na rakaa mbili za suna kabla ya kusimama kwa ajili ya swala ya Alasiri. Aidha ilifahamishwa kuwa baada ya swala kungekuwa na nasaha kwa ufupi kabla ya kuomba dua ya pamoja kufunga shughuli. Mpaka sasa najiuliza, lakini bado sipati jibu. Kitu gani kiliwafanya polisi kuvamia na kuwapiga mabomu Waislamu waliokuwa pale Mbuyuni? Katika kutafakari, nikasema labda ni kutokana na yale yaliyosemwa na Masheikh waliopata fursa ya kutoa nasaha. Hata hivyo kwa vile nilikuwepo, nilisikia mwenyewe kilichosemwa, sio maneno ya kuambiwa, bado nashindwa kukubali kwamba hiyo ndiyo ilikuwa sababu. Wa l i o p a t a f u r s a y a kuzunguza walikuwa watu wawili, Sheikh Farid na Ustadh Suleiman. Ilikuwa asimame Sheikh Msellem baada ya Sheikh Farid, lakini ile anakaa tu Farid, Mvua ya mabomu ikaanza. Sheikh Farid aliongea mambo mawili tu. Kwanza alisema kuwa wanajitahidi katika yale wanayosema kuyaweka pia katika maandishi maana baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha. Akatoa mfano wa Mwakilishi mmoja katika Baraza la Wawakilishi ambaye alidai kuwa Uamsho wanawahimiza watu wakatoe maoni katika Tume ya Katiba na waseme kuwa hawautaki muungano. Akasema, wao wanasema na wanachofanya ni kutetea haki ya Wazanzibari, kutetea heshma ya Rais wa Zanzibar kama Rais wa nchi. Kwamba watu wakatoe maoni ambayo yatawahakikishia Wazanzibari haki yao ya kuwa na nchi huru na serikali yenye mamlaka kamili (Sovereign State). Jambo la pili akaeleza kwa ufupi ni kwa nini wanaungana na Waislamu Tanzania Bara kukataa zoezi la sensa ya watu na makazi mpaka kipengele cha dini kiinginzwe. Hoja alizotoa ni zilezile ambazo zinatolewa na Waislamu Bara. Binafsi sikusikia neno lolote ama linaloweza kuitwa kuwa ni tusi, kutukana au la uchochezi. Ustadh Suleiman ndiye aliongea kwa muda mrefu kidogo na ndiye aliyeanza. Yeye alizungumzia mambo matatu: Kwanza alieleza ni kwa nini wameamua Waislamu kufanya dua ya peke yao kuliko kungoja ile ya kiserikali ambayo hukusanya Waislamu, wanasiasa na Inaendelea Uk. 9

AN-NUUR

Afande Azizi mche Mola Zalzala ya Kiama nzito

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, (ACP) Azizi Juma Mohamed. Siku hiyo tunaambiwa laayataka l l a m u u n a i l a man adhina lahur rahmaanu waqaala swawaaba. Hiyo ndiyo siku ambayo Quran imeisifu ikisema siku watu watakapoiona kila mwanamke anyonyeshaye atamsahau amnyonyeshaye (mwanawe) na kila mwenye mimba ataiharibu. Utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa, lakini ni adhabu ya Mwenyezi Mungu kali mno. Niseme kuwa ilikuwa ni msiba juu ya msiba pale polisi walipowavamia Waislamu wakiswali Swala ya Maiti Ghaibu na kuwapiga mabomu ya machozi. Binafsi nilibahatika kuwepo katika swala ile. Nilishuka bandarini kiasi saa tisa kasoro na kuelekea moja kwa moja katika Msikiti wa Mbuyuni. Nilipoka nilikuta Waislamu wakiendelea na Adhkari mbalimbali. Hasbunallah waniimal wakil, ndiyo adhkari niliyoikuta ikafuatiwa na kusoma kipande cha aya ya surat tiin inayosema: Alaisallahu biahkamil haakimiin. Baada kumaliza adhkari, mshereheshaji (MC) alitangaza ratiba ambapo

WANAOSWALIA maiti kupigwa mabomu. Wa n a o s o m a K h i t m a kusambaratishwa. Wa l i o t o k a k u h a n i , wanakimbizwa mitaani. Huu unaonekana kuwa ndio ubani wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa wafiwa Zanzibar. Ilikuwa Emmanuel Nchimbi aliyeokoa jahazi. Ni Waziri huyu wa Mambo ya Ndani ambaye aliokoa heshma ya Bunge pale alipotoa hoja ya kusitishwa Bunge ili kushughulikia suala la dharura la msiba mkubwa wa kuzama meli Mv Skagit. Wakati M h e s h i m i w a Emmanuel Nchimbi akitoa hoja hiyo, Bungeni kulikuwa

Ubani wa Emmanuel kwa wawa Zanzibar


kumesalia Wabunge wapato 46 tu baada ya Wabunge wengine kutoka na kususia kikao hicho. Walifanya hivyo kuonesha hisia zao kuwa hawakubaliani na uamuzi wa Spika Mheshimiwa Anne Makinda ambaye kwa busara zake aliona kuwa kuzama meli huku watu kwa mamia wakihowa kufa, halikuwa jambo la dharura la kustahiki kusitisha shughuli za Bunge lake tukufu. Hata alipofika Zanzibar, Mheshimiwa Nchimbi alionekana shujaa na mtu muungwana kinyume na hali ilivyokuwa kwa Spika ambaye bado jina lake lilikuwa likitajwa vibaya. Hata hivyo ambalo wananchi wa Zanzibar hawakufahamu ni kile ambacho kilikuwa kinawasubiri wakati wakijiandaa kumaliza kuwakafini na kuwaombea Dua maiti wao. Ilikuwa siku ya Ijumaa ambapo Masheikh waliamua kuwa iswaliwe swala ya pamoja ya maiti (Swalat Ghaib) pamoja na kuwaombea Dua wote. Baada ya swala ya Ijumaa minalhadhirina walileta Adhkari mbalimbali kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mola wao. Baada ya Adhkari kilichofanyika ni Swala ya Maiti. Ilipigwa adhana watu wakaswali Aswri na kutolewa tangazo kuwa baada ya swala kutakuwa na maelezo mapufi kisha Dua watu watawanyike. Ilikuwa wakati Masheikh wanatoa nasaha ili isomwe Inaendelea Uk. 11

9
Inatoka Uk. 8 Wakristo. Akasema, katika dua hiyo ya watu wa imani tofauti, kuna wanaoanza kwa kumkufuru Mungu. Akatoa mfano kwa Wakristo ambao huomba kwa jina la Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Katika ufafanuzi wake akanukuu aya ya Quran isemayo: Na (makafiri) husema: (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehma amejifanyia mtoto. Bila shaka mumeleta jambo lichukizalo kabisa (kwa kusema hivyo). Zinakaribia mbingu kutatuka kwa (tamko) hilo na ardhi kupasuka na milima kuanguka (ikakatika)

Makala/Tangazo

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012


vya uokozi vilikw enda takriban masaa matatu baada ya tukio. Akasema kuwa hata pale walipokuja watu binafsi wazamiaji wakataka wapelekwe kwenye tukio, wakasaidie kuokoa watu, waliambiwa vyombo havina mafuta. Na hili limesemwa na kuthibitishwa na waokoaji wenyewe. Ndio alipoka hapo akasema, hivi wangeambiwa kuna meli inaondoka imebeba karafuu za magendo, wangesema vyombo havina mafuta? Na mbona magari ya kuwavamia Uamsho hayakosi mafuta hata siku moja! Mbona magari yao (wakubwa) hatujaambiwa kuwa yanakosa mafuta? Ila mafuta ya vyombo vya kuokoa watu, ndiyo kila wakati hakuna mafuta. Lakini pia akasema kuwa katika jambo linalozua maswali mengi yasiyo na majibu ni pamoja na hili: Kwamba meli imezama eneo la Tanzania Bara, kwa nini havikuja vyombo vya uokozi kutoka Tanzania Bara? Na hili alilisema akinunukuu katika yale wanayozungumza na kuhoji watu mitaani na watu waliohusika na uzamiaji kuokoa watu na kuopoa maiti. Lakini akasema pia kuwa hakubaliani na hoja ya serikali kwamba haina fedha za kununua meli kubwa na mpya ambayo ingesaidia kuondoa tatizo la usari kwa Wazanzibari. Kwa msisitizo kabisa akamuelekea Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dr. Shein akiwakumbusha kuwa kwa mujibu wa Dini wanayoifuata, yaani Uislamu, mtu akiuwa mtu mmoja ni sawa na kuuwa watu wote. Kwa hiyo, waone umuhimu wa kuwawajibisha wale wanaofanya uzembe na wale wasiowajibika katika nafasi zao hadi kusababisha vifo kama hivi vya ajali ya meli. Msiwafanye watu dagaa tonge, alisema msemaji akimaanisha kuizindua serikali kujali maisha ya watu. Akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa kwa jinsi hali inavyokwenda, itakia mahali watu watachoka. Watatoka mitaani kama serikali inataka iwauwe wote. Wabaki wao wenyewe viongozi wa serikali na wake zao asibakie mtu wa kuwabughudhi. Binafsi naamini kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesikia kilio cha Ustadh Suleiman na Waislamu wote ndio maana amekubali ombi la Waziri Masoud kujiuzulu. Ingekuwa alichofanya Ustadh Suleiman Inaendelea Uk. 11

AN-NUUR

vipandevipande. Kwa kule kudai kuwa (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema ana mtoto.) (19:88-91). Ndio akasema, itakuwaje tukae mahali ambapo yanasemwa maneno ambayo mbingu zinakaribia kuanguka kwa uzito wa dhambi inayotokana na maneno hayo, kisha tunanyanyua mikono

Afande Azizi mche Mola Zalzala ya Kiama nzito


tunamwomba Mwenyezi Mungu awarehemu maiti wetu. Akatoa mfano wa kibinadamu, kwamba jaaliya mtu kaja nyumbani kwako akakunasa kibao au akakupiga bakora sa, kisha anakuomba maji ya kunywa. Ni katika kuzingatia hayo akasema kuwa wao waliona ni bora Waislamu kufanya dua ya

peke yao. Na hili ndilo alilofanya pia Rais Dr. Ali Mohamed Shein katika swala ile iliyoongozwa na Mufti Sheikh Swaleh Omar Kabi pale Masjid Mushawwara, Muembe Shauri. Hapana shaka katika waliokufa wapo pia Wakristo, lakini mara hii serikali haikufanya Dua ya mseto w a Wa i s l a m u n a Wa k r i s t o . Walifuata nyayo z a Wa i s l a m u waliokusanyika Masjid Mbuyuni Ijumaa iliyopita. Jambo la pili alilozungumza ni kuonyesha jinsi viongozi wa serikali wanavyohusika na majanga haya ya kuzama meli na watu kupoteza maisha. Alisema, watu wasikimbile katika Qadari ya Mwenyezi M u n g u . Wa s i p e l e k e lawama kwa Allah, bali w a t i z a m e kwanza, iwapo hawana mchango katika janga hilo? Alitoa mfano wa mtu kuacha mlango wazi halafu unatawakal. K a t i k a uchambuzi wake mdogo akasema kuwa anaona kuna uzembe. Kwamba taasisi za serikali haziwajibiki ipasavyo. Akatoa mifano ya meli mbovu ambazo huruhusiwa kufanya kazi wakati vyombo vya usimamizi vipo. Lakini pia akazungumzia uzembe kwamba baada ya ajali kutokea hapakuwa na uharaka wa vyombo husika k u p e l e k a huduma za uokozi. Vyombo

10

Makala

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

AN-NUUR

Kipengele cha Dini Sensa kitakuwepo maaskofu watakapotaka


Kwa wale wanaochunguza kwa karibu mwenendo wa nchi kuhusu suala la dini wanaombwa walitazame tena kwa macho manne. Waanzie katika suala la elimu. Imelezwa katika makala hii kuwa yule Bwana Mkubwa wa TBC aliyetoa takwimu zake za idadi ya Wakristo nchini alizuzuka kwa kuwa kila alipogeuka anayemuona ni Mkristo mwenzie. Haya wasomaji waliambiwa na Padri Dr John Sivalon kuwa ndio ulikuwa na umekuwa mkakati maalum katika nchi hii. Hivyo hivyo kuna baadhi ya wananchi wanaosema kuwa sera nzima ya vijiji vya ujamaa ilikuwa ni kurahisidha kuenea kwa Ukristo nchini. Hakika si mara moja Hayati Mwalimu Julius Nyerere alisikika akiwashauri viongozi wa Kikristo kujenga makanisa yao miongoni mwa wakazi wa kila mahali. Aliwaambia kuwa hivyo ndivyo Waislamu wafanyavyo kwani unakuta misikiti katikati ya makazi ya watu. Makanisa kweli yalijengwa vijijini na katika kila kitongoji mijini. Wameweza kuwaghilibu wananchi wengi wasio na dini kubatizwa. Kumbuka kuwa Makanisa wanauwezo mkubwa kwa kila hali. Serekalini ni wao waliofurika na mapesa wanayo mengi sana tu. Mfumo mzima wa uendeshaji nchi ni M F U M O K R I S TO k a m a wanavyosema Waislamu wenyewe kila siku. Kwa hali hii Waislamu, pale wenyewe watapokuwa na uhakika kabisa kuwa sasa nchi hii kweli ni y a K i k r i s t o , YA A N I IDADI YA WAKRISTO ITKAPOJULIKANA BILA WASI WASI WOWOTE KUWA WAO NI WENGI KUZIDI WAISLAMU, BASI KIDODOSHO HICHO CHA D I N I K I TA K U W E M O KATIKA SENSA!! BAKWATA!! Inakuwaje vigumu kwa viongozi wa BAKWATA kuelewa mbinu hizi zinazotumiwa na wale wasioupenda Uislamu? Kweli hawa BAKWATA wanautumikia Uislamu na Waislamu? Hata kama kweli wao ni kitengo cha CCM/ Serekali lakini mengine kweli wangetafakari na kujaribu kutambua ukweli uko wapi. TUWAONEE HURUMA!!

Na Khalid S Mtwangi HAKUNA ubishi kuwa sensa ni muhimu sana kwa nchi yeyote ile duniani kiasi kwamba hata zile nchi zilizoendelea ambako wao wanaweka rekodi ya kila tukio, ikiwa ni pamoja na kila panapozaliwa BinAdam na kila panapotokea kifo cha huyo BinAdam. Hivyo kila siku wanaweza kujua wako watu wangapi nchini wakati wowote hesabu hiyo inapotakikana. Kadri ilivyo takwimu zao haziachi suala lolote lile linalohusiana na wananchi wa nchi hiyo bila kujibiwa kutokana na takwimu zinazopatikana katokana na sensa. Huko nyuma Tanzania nayo ilikuwa ikifuata mtindo huo kiasi kwamba kulikuwa ikijulikana idadi ya waumini wa dini zote na wale wasiokuwa na dini ama wanafuata dini za asili. Mara ya mwiso sensa ya mtido huo ilifanyika mwaka 1967. Tangu hapo inaelekea kuwa Serekali haikutaka kujua idadi ya wananchi wake walio wafuasi wa dini hii ama ile. Baba Askofu Kilaini na Takwimu Zake Kule Marekani kila mwaka kunatolewa kitabu chenye takwimu za kila aina kinachoitwa THE WORLD ALMANAC, And The Book of Facts; na kule Uingereza pia wanatoa kitabu kama hicho kinachoitwa WHITAKERS ALMANACK, To Days World in One Volume. Bahati nzuri mimi ninavyo vya mwaka 2010 cha Marekani na cha 2008 cha Uingereza. Ingawa sio kila mwaka, lakini nimekuwa nikipata hasa nakala ya kile cha Marekani kwa muda mrefu sana. Kile cha mwaka 1974 kilitoa hesabu ya Waislamu Tanzania kuwa ni 40% na Wakristo wakiwa 29%. Hiki cha 2010 kinaandika kuwa Waislamu Tanzania ni 35% na Wakristo ni 30%. Whitakers ya Uingereza inatoa hesabu zake kuwa Waislamu ni 30% na Wakristo pia 30%; hesabu

JOPO la Masheikh wakisoma tamko la Waislamu kutoshiriki sensa iwapo kipengele cha Dini hakitakuwepo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. kidogo ndipo dereva anaweza kutafuta idadi ya Wakristo zote zikiwa ni estimate. Wale Marekani wanatoa kuwa Athumani. Hapo ndipo ama Waislamu wako wangapi hesabu ya Zanzibar baki anapata fursa ya kuzungumza Tanzania kwa sababu katika kuwa huko ni 99% Waislamu. na Athuman na kujua kumbe vidodoshi vilivyokuwemo katika kutafuta idadi ya Wasomaji watakumbuka kuwa hata Athuman nao wapo. Katika hali kama hiyo watu nchini pia kulikuwemo Muhasham Baba Askofu Methodius Kilaini yeye katoa mtu yeyote mwenye mawazo kidodoshi cha kumuuliza takwimu zake kuwa Wakristo finyu, tena kama ilivyo a n a y e h i s a b i w a y e y e n i Tanzania ni 35% na Waislamu yanakuwa finyu sana; hata muumini wa dini gani. Kwa 30%. Hakika katika maandiko kubali kuwa kweli Wakristo hiyo baada ya zoezi hilo yao yote Kanisa Katoliki s io w en g i zaid i n ch in i kumalizika kabisa Serekali hutoa takwimu kuonyesha humu. Wakati huo huo ni ilikuwa na hesabu kamili na kujigamba kuwa Wakristo bora sana kukumbuka kuwa ya waumini wa dini hii ama Tanzania ni wengi kuliko mafundisho wanayoyatoa ile kwa Tanzania nzima Waislamu. Hesabu hizo mapadri na wachungaji ni ikiwa ni pamoja na Zanzibar. wanazipata wapi haijulikani. makali sana kwa kuweza Katika maandishi ya Serekali Itakumbukwa kuwa Shirika la kumghilibu mtu mpaka asiwe ama mwingine yeyote yule Utangazaji la Taifa (Tanzania na uwezo wa kuweza kukiri anayetafiti ama kuandika Broadcasting Corporation na kupata majawabu tofauti tu taarifa juu ya Tanzania TBC) walitangaza kuwa idadi na yale aliyoambiwa na huyo angeweza kunukuu takwimu ya Wakristo Tanzania ni 54% mchungaji ama padri. Hivyo hizo za 1967 na kuzitumia ingawa walikiri baadae kuwa kwa huyu Bwana mkubwa wa vizuri katika maandiko yake. walifanya makosa kutoa TBC yeye takwimu alizotoa Takwimu za Muhasham takwimu hizo. kwake ni sahihi kabisa na Baba Askofu Mthodius Lakini kosa hilo linaweza bila shaka alipoambiwa Kilaini, kwa mfano, kamwe kabisa kueleweka na kwamba kuwa inawezekana sio hivyo hazikutaja kwamba sensa ya bila kukiri sana mtu yeyote alikuja juu na kuwalaumu 1967 ilikuwa ndicho chanzo aliyomo katika nafasi ama h a w a Wa i s l a m u w e n y e chake. Wala vijitabu vingi hali aliyekuwemo kijana siasa kali ama kitu kama vinavyotolewa na makanisa aliyetoa takwimu hizo, hicho. Hakuweza kujioa havitaji vyanzo kuwa ni sensa naye anaweza kutenda kosa kuwa labda yeye kakosea. ya 1967. Hilo inasemekana kuwa kama hilo. Hebu msomaji Pia zikumbukwe zile hisia fikiria; anapokuwa kazini ziliopo nzito kuwadharau linakuwa gumu kwa sababu huyu bwana kila anapogeuka Waislamu. Si jambo geni rekodi zote za sensa ya osini kwake anamkuta na kwa wasomaji kuwa huko mwaka 1967 hazionekani kuzungumza na Fortunatus katika maofisi ya Serekali a m a s i r a h i s i k u z i p a t a juu ya mambo ya kazi. kuwepo ofisa Muislamu ni hata kwa kazi muhimu na Akisogea osi nyingine pia jambo linaloonekana lisilo la zinazotambuliwa kama vile utati wa kina wa aina yeyote anajadili mambo ya kazi na kawaida. ile. MAKARATASI YAKE John huku bosi wake akiwa YOTE YAMEKWENDA Magdalena. Ni mpaka pale Sensa ya 1967 Iko Wapi? WAPI?? anapotaka huduma za tarishi ndipo anakutana na Abdallah Hakika kusingekuwa Dodosho la Dini Litakuja ama anapotaka kwenda mbali na haja ya kubabaika sana

11
Inatoka Uk. 8

Makala

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

AN-NUUR

Dua ya kuhitimisha, hapo ndipo vijana wa Nchimbi walipovamia. Ghafla zilionekana gari za FFU zikivamia eneo hilo na kuanza kuvurumisha mabomu. Kutokana na kizaa zaa hicho, watu walianguka na kukanyagana wakiwemo wanawake na watoto. Wachache waliobaki kutaka kujinusuru hapo hapo ndani ya msikiti walikuta kuwa napo hakukaliki kwa sababu ya moshi wa mabomu. Kutoka eneo la Msikiti wa Mbuyuni, polisi walianza kuranda mitaani na kupiga mabomu ovyo, hali iliyowatia mori na kuwachemsha vijana mitaani nao wengine wakaanza kuchoma moto matairi barabarani. Nikitokea eneo la Mbuyuni, nilipita vichochoroni hadi kutokea eneo la Masjid Salam nakutembea kando kando ya barabara kuelekea Michenzani. Hapo nikakuta FFU wakipita na gari zao huku wakipiga mabomu ovyo. Kwa hakika ilikuwa vigumu mtu kujua nini kilikuwa kikiendelea. Watu wanapita mitaani, wengine wapo katika sehemu zao za biashara na katika makazi yao wanaendelea na shughguli zao, mara zinapita gari za FFU Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Jamhuri wanarusha mabomu. Hali ya Muungano ya Tanzania . hiyo iliendelea mpaka usiku wa manane hali iliyosababisha watu wengine kushindwa kabisa kutekeleza ibada yao ya Tarawehe na Qiyamul laili. Wakati napita mitaani, nakutana na watu wanalaani. Tumewafanya nini? Tumepotelewa na ndugu zetu na mpaka hivi sasa maiti hawajapatikana, tunapigwa mabomu. Tumekosa nini? Msiba haujamalizika w a n a t u p i g a . Tu m e f i w a , tuna majonzi, wengine hata maiti hatujapata, tunapigwa. Haya ndiyo (Rais) Kikwete aliyokuja kutuletea! Haya ndiyo Waziri wake Emmanuel Nchi aliyokuja kutuletea! Kumbe zile salamu na masikitiko ilikuwa sawa machozi ya mamba. Hatutaki chochote, tunasema hivi sasa hatutaki chama chochote, sisi sote tunakimbilia Uamsho, tumechoka. WAOKOAJI katika ajali ya Meli ya Skagit iliyozama hivi karibuni Zanzibar. Hiyo ilikuwa kauli ya msari mmoja katika boti ya wamechoka. Hawathaminiwi. wawa Zanzibar pale Masjid maiti na kuwaombea Dua, ndio Kilimanjaro 2 iliyoondoka Mbuyuni. unayowakisha Wazanzibari Zanzibar Jumamosi saa moja W a n a d a n g a n y w a . I p o k a u l i y a Q u r a n kuwaona viongozi wa Serikali asubuhi kwenda Dar es Salaam. Wanaonewa. Wanahujumiwa kwamba mengi ya majanga ya Muungano Tanzania kama Na kwa hakika haya ndiyo na kudhalilishwa. yalikuwa mazungumzo katika Haya ndiyo aliyovuna yanayowakumba wanadamu, maadui wa Wazanzibari. Na boti hiyo kila mmoja akieleza M h e s h i m i w a W a z i r i wanayachuma kwa mikono hii huzidi kupandisha lile joto kwa namna yake lakini ujumbe Emmanuel Nchimbi kwa yao. Ubani huu wa mabomu la kutaka nchi huru yenye ukiwa mmoja: kuwa watu ule ubani wa mabomu kwa kwa Waislamu wanaoswalia mamlaka kamili.

Ubani wa Emmanuel kwa wawa Zanzibar

Inatoka Uk. 9 ni kutukana na kukashifu, hapana shaka ujumbe huu usingemfikia Mheshimiwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad hadi kuamua kujiuzulu wadhifa wake tofauti na msimamo wake wa awali. Lakini pia serikali imetangaza kupiga marufuku baadhi ya meli zinazoonekana kuwa ni mbovu. Jambo la tatu, alitoa nasaha kwa polisi. Hawa aliwaambia kuwa wachunge heshima ya Msikiti. Yale waliyofanya katika Msikiti wa Mahonda basi wasiyarudie tena maana wanajitafutia laana kwa Mungu. Wasinajisi nyumba za Allah kwa kuingia na mabuti yao. Katika kutilia mkazo nukta hii akasema kuwa iwapo polisi hawatakoma kunajisi misikiti, itafikia mahali Waislamu nao watachukua hatua. Kwamba polisi atakeyekuwa mtovu wa adabu, akaingia msikitini na mabuti yake, basi vitakavyotoka ni viatu. Haya ndiyo yaliyosemwa Mbuyuni. Swali ni je, haya ndiyo hukumu yake imekuwa Waislamu kuvamiwa na kupigwa? Hata kama haya waliyosema Masheikh pengine hayakuwa yakiwafurahisha baadhi ya viongozi wa serikali. Kwa nini wasingesubiri tu na kuwakamata baadae au kuwataka viongozi hao kuripoti kituo cha polisi? Kwa kuvamia Waislamu pale msikitini, polisi walisababisha vurugu kubwa lililodumu hadi usiku wa manane. Watu wameumizwa. Watu wamepoteza mali. Watu wamevuruga ratiba zao za ibada na kazi muhimu za kifamilia na kijamii. Na baya zaidi mabomu hayo ya polisi, yanazidi kujenga hali ya uhasama kati ya serikali na raia. Hayo aliyosema Kamanda Azizi kuwa wafuasi wa Uamsho wakiwa na bendera walianza vurugu, kupanga mawe barabarani na kuchoma moto matairi. Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi likaamua kutumia nguvu kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na maji yenye kemikali za kuwasha, nadhani anazungumzia matokeo ya polisi kupiga watu Msikitini. Polisi wamepiga watu Msikitini waliokuwa wametulia tulii, kama kuna mawe yalipangwa barabarani au matairi yalichomwa, basi hayo yametokana na jazba na mori wa vijana na watu mitaani na hata wahalifu waliotaka kutumia tukio hilo kupora.

Afande Azizi mche Mola

12
HII NI QADAR YA ALLAH (S.W)
1. Salamu yenye thamani, nakupeni waumini Mlio bara na Pwani, naomba ipokeeni Shambani hadi mijini, salamu hii shikeni Apangalo Rahmani, ni Qadariye jamani ! 2. Ni donda jipya jamani, la kovu bichi mwilini Katutahini Manani, kupima zetu imani Tukapoteza wandani, tulowapenda myoyoni Apangalo Rahmani, ni Qadariye jamani ! Tukarudi majumbani, zimetujaa huzuni Wajane,Yatima ndani, tukawapata kundini Kwa zetu nyingi hisani, wote tukawathamini Apangalo Rahmani, ni Qadariye jamani ! Bado tukiwa njozini, yetu mikono shavuni Watujia mtihani, kama ule wa zamani Meli memwaga majini, wametutoka insani Apangalo Rahmani, ni Qadariye jamani ! Tujue huu Mtihani, ameuweka Manani Atupime kwa yaqini, nafsi na zetu imani Ameshatwambia kwani, ndani ya hii Qyrani Apangalo Rahmani, ni Qadariye jamani ! Alolipanga manani, hutokea kwa yaqini Tusikufuru jamani, kuwalaumu insani Wengi aliwatahini, kwa shida na tafrani Apangalo Rahmani, ni Qadariye jamani ! Mwisho namwomba Manani, awaingize peponi Wote waloa ndani, ya maji wawe kherini Nasi tulobaki pwani, tukaze yetu huzuni Sote viumbewe manani, nakwake tu safarini Mwl. Mohammed Makimu Ubungo Islamic Teachers College (UITC) DAR ES SALAAM 0715 465158

Mashairi/Barua

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

AN-NUUR

3.

4.

5.

6.

7.

Hi Everyone, I hope you are well. I am writing this email because of an incident that happened to my dear friend on 6th July 2012 at Mlimani City, Dar-es-salaam.TZ. Mtu asiemjua alimsimamisha kwa kumuita kwa jina lake Mlimani City wakati amemaliza shopping (muda wa saa mbili kasoro usiku baada ya kutoka kazini). Yule kaka akajaribu kumkumbusha matukio mbalimbali ya huko nyuma (kama mtu anayemfahamu). Anasema alisogea restaurant kununua maji na hilo ndio tukio la mwisho analolikumbuka. Saa saba usiku amerudishwa nyumbani kwake na gari yake akiwa bado hana fahamu. Wamemchukulia simu, hela na baadhi ya hela zimetolewa kwenye ATM machines. Thank God hawakudhuru kabisa. Ila kinachoogopesha

Style ya kwanza
ni kwamba huyu mtu alikuwa anajua historia yake (ndugu zake na marafiki zake) na anajua anapoishi. It is very disturbing. Naomba mufahamishe ndugu na maraki zenu kuhusu tukio hili. Ubinaadamu haupo tena kwa hivyo tuwe makini tukiwa tunatembea huko mitaani...I hope this email will help others to avoid such tragedies!! Shufaa Dar es Salaam

From Andrew Peter Kato Kuna utapeli wa aina nyingi sana hasa parking ya Mlimani City! Wenye magari kuweni makini sana! Juzi naingia kwa gari naondoka jamaa akanifuata ati anataka

STYLE YA PILI

AN-NUUR nakupongeza, kwa uloinena kweli, Kadhia ulodokeza, si ya puya ni ya kweli, Hukutaka kuchagiza, kwa kuipamba kwa kweli, AN-NUUR menena KWELI, huyo ni KADHI wa SENSA. Ni haki uloeleza, kwa kila mpenda kweli, Kwa hilo anokubeza, si mwingine mcha kweli, Aso na njema ruwaza, ila ya kupinga kweli, AN-NUUR menena KWELI, huyo ni KADHI wa SENSA. Urongo kuueneza, mwiko kwako ila kweli, Dhuluma kutokomeza, ndo dhatiyo ya kweli, Adharusi endeleza, dhidi ya wakana kweli, AN-NUUR menena KWELI, huyo ni KADHI wa SENSA. Hutafuti kwao izza, kwa kukengeusha kweli, Wala kujipendekeza, kwa wapinzani wa kweli, Kuwarudi waongoza, lengo isimame kweli, AN-NUUR menena KWELI, huyo ni KADHI wa SENSA. Si adayo kwokoteza, habari ziso za kweli, Au umma kuukwaza, kwa kuipindua kweli, Ama dira kupoteza, kwa kuikiuka kweli, AN-NUUR menena KWELI, huyo ni KADHI wa SENSA. Kwa wano dini iuza, kwa thamani duni kweli, Japo watoke BARAZA, la BATILI au KWELI, Huchelei kuwajuza, wafanyacho sicho kweli, AN-NUUR menena KWELI, huyo ni KADHI wa SENSA. Wasaka tonge na feza, na vyeo viso vya kweli, Hawafai kuongoza, kwa kuwa sio wa kweli, Hata wakikupuuza, ALLAH shahidi wa KWELI, AN-NUUR menena KWELI, huyo ni KADHI wa SENSA. Akudumishe MUWEZA, katika kunena kweli, Kwa MWANGAO kuangaza, kwa NURU ya kweli kweli, Beti nane namaliza, kukupongeza kwa kweli, AN-NUUR menena KWELI, huyo ni KADHI wa SENSA. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

SWADAKTA, AN-NUUR !

Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie: Mhariri AN-NUUR, S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk

msaada nikamwona mapema kabisa anavyobadilisha sura ili aoenekana mhitaji msaada! Nikamuwahi nikafunga vioo! Nikashusha kidogo nikamhoji akadai ati anaomba japo nauli arudi gerezani! (Just imagine the way he confused himself kwani nilimchenjia ni balaa). Sasa gerezani umetorokaje, kwanza huna uniform, then umefanikiwa kutoroka bado unataka urudi, LOL! Nilipotafakari na kumsimulia jamaa yangu akadai ndiyo janja yao, anakuomba msaada na ukishampatia anakushukuru kwa kukupa mkono, hapo ndipo inakuwa imekula kwako kwani wana kitu cha nja kali kama kisindano kidogo wanakuchoma nacho mnapopeana mkono then from there unapoteza fahamu, na ndipo wenzake wanatokea. Unapakiwa kwa gari wakidai ndugu yao kazidiwa, unapelekwa kusikojulikana, wazee wanasepa na gari! BEWARE tupunguze ukarimu waTZ, wema usizidi uwezo! Andrew Peter Kato Dar es Salaam

Ndugu Mhariri, MIMI najiuliza, hivi kweli kwa madaraka aliyonayo rais wetu (kwa mujibu wa katiba), anashindwa kutoa maamuzi juu ya suala la OIC? Hata kama mfumokristo umemshika, ndio kiasi hicho mpaka anasahau haki za Waislamu? Nafikiri uoga wake unamfanya ajirundikie kapu la maswali ya kujibu siku ya mwisho juu ya Ummat Mohammed (SAW) uliopo Tanzania. Pili, kuna na hili la Mahakama ya Kadhi. Hivi kweli suala la msingi kama hili mheshimiwa rais analikwepa, anashindwa kutoa maamuzi hadharani (badala yake anamtumia Waziri Mkuu) ambaye anatupa majibu yaliyojaa utata na maswali badala ya kutoa majibu. Uoga huu pia bado ni kiwango cha juu sana kwani mimi naamini kuwa mfumokristo hauna DIVINE POWERS kiasi cha rais kuuogopa kama vile utamhukumu na kumyonga papo hapo akitumia madaraka na mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa katiba ya Tanzania. Tatu kuna hili suala la wakuu wa vitengo mbalimbali katika taasisi na mashirika mbalimbali ya kiserikali. Waislamu nchi hii wako wengi sana (tena wasomi hasa). Mimi bado hainiingii

Uoga dhidi ya Mfumokristo


akilini kuona vitengo nyeti vyote kutopewa Waislamu kwani nchi hii si ya Wakristo peke yao. Hivi kuogopa hata kwenye vitu ambavyo vinatumia vigezo vya elimu ambayo Wislamu tunayo, maana yake nini? Mimi napata shaka kwa Mh. Rais kuogopa kwa kiwango hiki, siku mfumokristo unaweza kutoa amri Waislamu wote wakatupiwe baharini ikatekelezwa kisa mfumokristo umetamka. Nne kuna hii kadhia ya huyu DKT. Ndalichako. Kwanza mimi naona anajishushia hadhi yake. Hivi kweli mtu unaitwa DKT halafu unachakachua matokeo ya watu (kisa dini) huoni aibu kweli jamani? Msomi Dokta Joyce, hata kama ingekuwa tatizo ni program ya kompyuta, bado suala la kuwajibika kwa uzembe lipo pale pale. Haya sasa ona Wasomi (wa kweli wa Kiislamu) wamengamua kuwa ulikuwa ni uchakachuaji na wala si program ya kompyuta. Labda mtuambie kuwa program ya kompyuta ya kuchakachua matokeo ya Waislamu. Katibu Joyce Ndalichako, unaogopa kuzugumza unamwachia huyu Waziri ambaye anatamka na kuandika vitu ambavyo hajavifanyia uchunguzi. Au ndio anatoa Shukrani za uwaziri? Hapa pia mfumokristo unaogopwa. Tano kuna hili la UAMSHO na KATIBA. Mimi sioni sababu ya rais kushindwa na kuogopa kuwaruhusu Wazanzibar kutoa maoni juu ya Muungano. Hivi unambeba mtu, yule mtu anasema kachoka kubebwamshushe, hutaki; kwa nini? Haya umekataa nieleze sababu (makubaliano ya muungano) za kuningangania hutaki. Basi anakwambia nibebe kwa staili hii (aina ya muungano-idadi ya serikali), hutaki. Mheshimiwa rais toa tamko (madaraka unayo). Sita kuna kadhia ya sensa. Mheshimiwa rais suala hili nalo linagusa maslahi ya umma wa Kiislamu. Hivi kweli mfumokristo uchakachue mpaka idadi ya viumbe walioumbwa na Mwenyezi Mungu (SW) (eti kwa kusema kuwa Waislamu ni wachache kuliko Wakristo)? Hivi kwani nani anasimamia zoezi hili? Ni kuogopa kiasi gani Mh. Rais mpaka kushindwa kuzungumza na Waislamu juu ya kadhia hii? Hata kama sio wote ongea na wawakilishi. YUSUPH ABDALLAH KOKOLE CHAMAZI ISLAMIC SEMINARY) 0763 971709/0783 419659

13
Na shaaban Rajab
AMESEMA Mtume (Saw) kuwa: Mwenye kufunga Ramadhani kwa imani na kutarajia malipo (toka kwa Allah (sw) husamehewa madhambi yaliyoyatangulia. (Bukhari na Muslim). Kama inavyoelezwa, Kumi la kwanza katika mwezi wa Ramadhani ni la rehma, Waislamu wanaofunga hurehemewa na Allah (sw) kwa saumu zao za kumi la kwanza. Kumi la pili ni la toba (maghrah) kuomba msamaha kwa Allah (sw) na kutubia. Hapa Waislamu wanapata nafasi pana na maalum kwa ajili ya kutubia makosa yao na kusamehemwa na Mwenyezi Mungu. Kumi la mwisho ni la kuwekwa mbali na moto. Kwa mazingira haya kwa nini Ramadhani usiwe mwezi wa raha kwa Waislamu kutoka kwa Mola wao? Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu. Mwezi huu hupatikana kwa kukamilika siku thelathini za mwezi wa Shaaban au kwa kuonekana mwezi mwandamo siku ya 29 ya mwezi wa Shaaban. Waislamu wameamrishwa na Mwenyezi Mungu kufunga kama inavyoonyeshwa katika Quran tukufu aya ya 2:183 inayosema: Enyi mlioamini, mmeamrishwa kufunga kama walivyoamriwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mwenyezi Mungu. Kabla ya ummat Muhammad (saw) waliotangulia pia nao waliamriwa kufunga. Hata baada ya kuja umma huu, nao ufaradhishwa kufunga katika Ramadhan. Swaum ni neno ambalo linaanisha funga. Kilugha katika lugha ya Kiswahili, lina maana ya kujizuia. Mtu kujizuia kula, kunywa kuvuta sigara, kuingiza chochote puani au masikioni pamoja na kujizuia kufanya mambo maovu kuanzia alfajir hadi magharibi. Kujizuia na kusema mameno machafu au kusengenya nk. Kisheria funga (swaumu) ni kumuabudu Mwenyezi Mungu (sw) kwa kujizuia na vyenye kufuturisha kuanzia kuanza kwa alfajiri mpaka kuzama kwa jua, kwa kutia nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (SWT). Kufunga katika mwezi wa Ramadhani ni nguzo ya tano katika nguzo za Uislamu. Kwa maana hiyo ni wajibu kwa mujibu wa Qur-an na Sunnah kufunga kwa Muislamu Waislamu wanafunga kama ilivyokuwa umma zilizotangulia kabla yao, wanafunga katika miezi ya Rajab, Shaaban, swaumu za sunna za siku za Jumatatu na Alhamisi n.k. Lakini wamelazimishwa kufunga mwezi wa Ramadhani, mwezi ambao ambao imeteremshwa Qurani ili iwe mwongozo kwa watu, kupambanua baina ya haki na batili. Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano; ya kwanza ikiwa ni kushuhudia ya kwamba hakuna

Makala

Ramadhan ni raha kwa Waislamu

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012


Amesema Mtume (saw), Mwenye kusimama (kwa ibada) katika mwezi wa Ramadhani kwa imani (thabiti) huku akitaraji malipo toka kwa Allah (Sw) husamehewa yale aliyoyafanya katika madhambi yake. (Bukhari na Muslim). Kusoma sana Qur-an. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Quran na ndio mwezi ulioteremshwa ndani yake Qur-an. , Amesema Mwenyezi Mungu Hakika tumeiteremsha (Quran) katika laylatul-Qadr (usiku wenye heshima kubwa), katika usiku wa mwezi wa Ramadhani). (Qur 97:1). Kutoa sadaka kwa wingi. Pamoja na kwamba sadaka ina fadhila nyingi, lakini fadhila na thawabu zinazopatikana mwezi wa Ramadhani ni kubwa zaidi. Na miongoni mwa sadaka zinazotiliwa mkazo katika mwezi wa Ramadhani ni kuwafuturisha waliofunga. Kufanya Umrah, amesema Mtume (s.a.w) kwamba Umrah katika mwezi wa Ramadhani ina malipo sawa na ya Hijah (Muslim). Itikafu (kubaki msikitini ukijishughulisha na ibada mbalimbali bila ya kutoka), ni suna kufanya itikafu na hasa katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani. Kuutafuta usiku wa cheo (laylatul-qadr), hasa katika kumi la mwisho la Ramadhani. Imepokewa hadithi kutoka kwa Bi. Aishah (ra) amesema: Amesema Mtume (Saw), Utafuteni usiku wa cheo (laylatul-qadri) katika siku kumi za mwisho za Ramadhani. (Bukhari na Muslim) Amepokea Abu Hurayrah (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema: Mwenye kusimama katika usiku wa cheo (laylatulqadri) kwa imani thabiti na kwa kutarajia malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (SWT) husamehewa dhambi alizofanya nyuma. (Bukhari na Muslim). Kutubu. Yaani kurudi kwa Allah (s.a.w) kutokana na makosa aliyoyatenda kwa kuomba msamaha kutoka kwake, kujuta na kuazimia kutokuyarudia tena makosa hayo. Mwanaadamu si mkamilifu, ni dhaifu na anakuwa katika hatari ya kufanya makosa. Ikiwa ameguswa au kutoguswa na makosa hayo wakati akiyatenda, toba ndio njia ya kujikosha na madhambi ya makosa hayo, mwezi wa Ramadhani ni fursa muhimu ya kutubia. Kama makosa hayo kuna haki za watu umedhulumu, inamlazimu kuzirejesha kwa wenyewe haki hizo kwanza. Amesema Mtume (Saw) kuwa: Mwenye kufunga Ramadhani kwa imani na kutarajia malipo (toka kwa Allah husamehewa madhambi aliyoyatanguliza. (Bukhari na Muslim).

AN-NUUR

Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (Sw) na kwamba Muhammad (s.a.w) ni Mtume wa Allah (Sw). Ya pili ni kutoa Zakah na ya tatu ikiwa ni kuhiji katika nyumba tukufu ya al-Kaaba na ya tano ni kufunga mwezi wa Ramadhani. Waislamu wote hulazimika kufunga mwezi wa Ramadhani. Watoto wakikia umri wa miaka saba waanze kuzoeshwa kufunga na wakifikia umri wa miaka kumi walazimishwe kufunga. Lakini kwa kuzingatia afya na uzima wa mtoto. Funga ya Ramadhani ni wajibu kwa Muislamu yeyote baleghe, mwenye akili, aliye katika mji wake (asiwe msari), mwenye afya na asiwe na mambo yanayozuia swaumu (kama hedhi na nifasi kwa wanawake). Udhuru zinazosababisha Muislamu kuacha kufunga zinatofautiana na kila udhuru una hukumu yake. Hedhi (damu ya mwezi) na nifasi (damu ya uzazi) kwa wanawake. Huu ni udhuru ambao humlazimisha mwanamke kuacha kufunga na inakuwa haramu kwake funga. Iwapo atafunga haitokubaliwa funga yake na atalazimika kulipa funga hiyo. Wenye maradhi wanaruhusiwa kutofunga lakini wanawajibika kulipa funga pindi imalizikapo Ramadhani. Kama maradhi yatazidi au kumletea madhara iwapo atafunga, basi itakuwa lazima kwake kutokufunga. Msari kadhalika anaruhusiwa kutofunga awapo safarini lakini naye akiwajibika kulipa funga alizoacha. Amesema Mwenyezi Mungu: Atakayekuwa katika

mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizoacha kufunga) katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito (Qur 2:185). Wazee (vikongwe) na wenye maradhi sugu (yasiotarajiwa kupona). Iwapo haya yanamsababishia madhara mfungaji, basi ni katika udhuru na ruhusa ya kuacha kufunga. Lakini itamlazimu atoe dia kwa kumlisha masikini kibaba cha chakula (ambacho ni sawa na uzito wa gramu takribani 600) au chakula kinacho mshibisha masikini mmoja kwa kila siku aliyoacha kufunga. Wa j a wazito na wanyonyeshaji. Hawa nao ni katika walioruhusiwa kutokufunga lakini inawabidi kulipa siku walizoshindwa kufunga kwa sababu ya udhuru huo. Funga ya Ramadhani ina nguzo zake. Nazo ni kutia nia, nayo huwekwa usiku wa kuamkia funga kwamba unakusudia kufunga funga ya faradhi. Kujizuilia na vyenye kufunguza (kufuturisha), kula kunywa, n.k. katika muda wa kufunga, yaani mchana kuanzia alfajiri mpaka kutwa (kuzama) kwa jua. Ya n a y o b a t i l i s h a f u n g a . Mwenye kufunga akifanya mojawapo katika haya swaumu yake itakuwa imeharibika. Kula au kunywa kwa kukusudia, kuvuta sigara, kuingiza kitu puani au maskioni kwa maksudi. Kila kinachoingia tumboni au

kooni kwa kukusudia. Kukutana kimwili (kuingiliana) kati ya mume na mke kabla ya kufuturu. Kujitoa manii (mbegu za uzazi) au kusababisha kutokwa na manii (kwa kujichezea sehemu za siri, kujitapisha kwa makusudi. Kutokwa na damu ya mwezi (hedhi) au damu ya uzazi (nifasi). Kusema uongo, kusengenya au kufanya uovu wowote makusudi. Yasiyobatilisha funga. Kula au kunywa kwa kusahau. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Hurayrah amesema, amesema Mtume (Saw) Mwenye kusahau nae amefunga, basi akala au akanywa na aikamilishe funga yake. ( Al Bukhariy na Muslim). Kusukutua au kupandisha maji puani wakati wa udhu. (Lakini maji yasiingie ndani) Kuoga au kujiburudisha kwa kujimwagia maji katika kiwiliwili (hasa katika maeneo yenye joto kali). Kuonja chakula kwa mpishi (kwa sharti ya kutokumeza alichokionja). Kutokwa na mbegu za uzazi (manii) katika usingizi (ndoto) au bila ya kukusudia. Kuamka na janaba. Imepokewa hadithi kutoka kwa Mamama `Aishah na Ummu Salamah (ra) kwamba Mtume (Saw) alikuwa akiamka na janaba kutokana na kukutana kimwili na wake zake, kisha anaoga na kufunga (Al Bukhariy na Muslim). Kupiga mswaki (wakati wowote). Kuchoma sindano ya kawaida ya tiba. Kung`oa jino na mfano wake. Mwanamke kuamka kabla ya kuoga kwa hedhi au nifasi. Baadhi ya mambo yaliyo suna kwa mfungaji: Kula daku. Imepokewa hadithi kutoka kwa Anas ibn Maalik (ra) amesema: amesema Mtume (Saw): Kuleni daku kwani hakika chakula cha daku kina baraka ndani yake (Al Bukhariy na Muslim). Na ni suna kuchelewa kula daku mpaka kukaribia alfajiri. Kuharakisha kufutari (mara tu jua linapozama). Imepokewa hadithi kutoka kwa Sahl ibn Saad (ra), Hakika Mtume (saw) amesema: Watu watakuwa bado wapo katika kheri muda wa kuwa wanaharakisha futari.( Al Bukhariy na Muslim). Na ni suna (kuanza) kufutari kwa tende au maji. Katika siku thelathini au ishirini na tisa za kufunga, Waislamu wanaofunga wana faida kubwa wanazoipata kutoka kwa Allah (sw). Ndio maana ukaitwa ni mwenzi wa kuchuma. Yapo baadhi ya mambo ambayo Muislamu akiyafanya kwa wingi katika mwezi wa Ramadhani anakuwa ni mwenye kuchuma zaidi.

14
Na Said Rajab
WAKATI wa uongozi wa Nyerere (1961- mpaka sasa), Wakristo wamekuwa na uhuru mkubwa wa dini yao, ambao umelindwa vizuri na Katiba ya nchi. Uhuru wao ni pamoja na kuwabatiza Waislamu na kuwahubiria Injili. Lakini Waislamu, walio wahanga wa kubatizwa, hawakuwa na ruhusa wala uhuru wa kupanga na kuendesha mambo yao wenyewe, bila ya kuingiliwa na mamlaka kuu ya nchi. Masuala yote yanayowahusu Waislamu wa Tanzania, yakawekwa mikononi mwa Bakwata lililoundwa kwa minajili ya kuwahujumu Waislamu wa Tanzania, baada ya Nyerere kuvunja chombo kilichoundwa n a Wa i s l a m u w e n y e w e , kwa lengo la kusimamia maendeleo yao eneo zima la Afrika Mashariki. Bakwata linafanyakazi chini ya ulinzi na maelekezo ya serikali inayoendeshwa kwa misingi ya Mfumo Kristo. Kukosekana kwa chombo huru cha kuwasemea Waislamu wa Tanzania, kuliunda ombwe la kiitikadi hapa nchini. Kwa kipindi cha miongo mitatu (19611990), Waislamu wa Tanzania hawakuweza kufanya mambo ya maana kimaendeleo katika jamii yao, kama mafundisho ya dini yao yanavyoelekeza. Katika jitihada za kuziba ombwe hilo, Waislamu walijaribu kuunda taasisi mbalimbali, zikiwemo zile za mlingano wa dini kama Umoja wa Wahubiri wa Mlingano wa Dini (UWAMDI). Hawa UWAMDI, nakumbuka walikuwa wakimiliki gazeti likiitwa Mizani, ambalo lilikuwa likizungumzia sana uongozi wa Waislamu wa Tanzania. Tangu lilipoanza miaka ya 1990, gazeti la Mizani lilionyesha kukerwa mno na kwa nini Bakwata, taasisi iliyoasisiwa na Serikali ya Nyerere mwaka 1968, iwe ndiyo msemaji na msimamizi pekee wa masuala ya Waislamu wa Tanzania! Gazeti la Mizani, toleo la April, mwaka 1990 lilichapisha Khutba ya Ijumaa ya marehemu Sheikh Kassim bin Juma, aliyekuwa Imamu wa Msikiti wa Mtoro jijini Dar es Salaam, ambaye alitoa wito kwa Waislamu nchini Kuwaondoa viongozi wa kitaifa wa Bakwata. Sheikh Kassim bin Juma pia alisema: Waislamu wachoshwa na uongozi wa Bakwata. Hata hivyo, wataalamu na wasomi Waislamu, wakipingwa vikali na Bakwata, walifanikiwa kuunda chombo chao huru, Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, mwezi Novemba mwaka 1992. Kama tunavyofahamu, wakati wa utawala wa N y e r e r e , Wa m i s s i o n a r i wa Kikristo walikuwa huru kuendesha shughuli zao

namna walivyopenda, ikiwa ni pamoja na kuwabatiza Waislamu wanaokandamizwa. Mwaka 1982, kundi linalojiita Crusaders lilizuru mikoa yote ya Tanzania kuhubiri Ukristo katika mikutano ya hadhara, lakini Abubakar Mwilima, Othman Matata, Ngariba Fundi Mussa na Mohammed Ali Kawemba walizuiwa mwaka 1987. Vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na dola, ambavyo vimejaa Wakristo katika nafasi za uongozi, viliwatuhumu akina Ngariba kwa kupanda mbegu ya chuki na vurugu nchini Tanzania. Rais Ali Hassan Mwinyi, ambaye ni Muislamu kutoka Zanzibar alishambuliwa waziwazi na kambi za Wakristo. Mtu aliyeendesha kampeni ya kuwahamasisha Wakristo kupinga uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi, ili kukabiliana na kitisho cha Waislamu alikuwa Mchungaji Christopher Mtikila, Mkristo mwenye itikadi kali. Huyu bwana ni kigogo katika makanisa yenye mrengo wa Kilutheri, ambapo mwaka 1982 kanisa hili lilisimamia matangazo ya moja kwa moja ya Ibada ya Krismas kwenye vyombo vya habari vya Zanzibar, ikiwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya Zanzibar. Akiwa kiongozi mkuu wa Full Salvation Church, Mchungaji Mtikila pia ni kiongozi wa batalioni ya kanisa hilo ya kupambana na Uislamu, ambapo alishawahi kutangaza wazi kwamba Crusade yake ni kulinda Ukristo dhidi ya Uislamu. Mchungaji Christopher Mtikila alipata umaarufu zaidi mwaka 1988 katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanyika Kizota mjini Dodoma, wakati alipomuandikia barua Nyerere, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM kwa niaba ya Wakristo, akipinga Urais wa Ali Hassan Mwinyi kwa kosa la kujaribu kuimarisha Uislamu kwa gharama ya Ukristo. Barua yake hiyo ya uchochezi ilisambazwa kwa wajumbe wote wa mkutano huo uliofunguliwa na Joseph Warioba, aliyekuwa Waziri Mkuu wakati ule. Barua ilitaka ufanyike uchunguzi wa haraka na kurekebisha kile alichoita Dangerous Government Stand (msimamo hatari wa Serikali) chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi. Katika hatua ya kushangaza, Mchungaji Mtikila alisisitiza katika barua yake kwamba, eti TANU ilipokuwa chini ya Nyerere, kiongozi huyo alipigania uhuru, umoja na usawa miongoni mwa raia kwa kuondoa ubaguzi wa kidini! Huo ni uongo ulio wazi na unaweza kuaminiwa na watu

Mavuno ya Crusade ya Nyerere

Makala/Tangazo

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012


kuwaelewesha Waislamu wenzao kwamba baada ya Uhuru, upogo katika elimu hautarekebishwa na nafasi za Waislamu katika maeneo mengine ya kijamii hazitaboreshwa pia. Waislamu hawakuelewa kabisa, ingawa nasaha za akina Sheikh Suleiman Takadir na Hassan bin Amir zilitoka ndani ya Quran Tukufu! Bangi ya Nyerere ilipofua kabisa akili zao. Kutokana na msimamo wao, Sheikh Suleiman Takadir alifukuzwa kutoka kwenye nafasi yake ya Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, Sheikh Hassan bin Ameir alifukuzwa Tanganyika na kurejeshwa Zanzibar na Zubeir Mtemvu alianzisha chama kingine African National Union(ANC), akiipinga TANU chini ya uongozi wa Mkristo, Julius Nyerere. Ukweli ambao wapiganaji wa Mfumo Kristo Tanzania, iwe waandishi wa habari, wanasiasa, wasomi, wakurugenzi, maaskofu, Bakwata na wengineo hawathubutu kuusema ni huu hapa. Makanisa nchini Tanganyika yaliikataa TANU; mara mbili mwaka 1958 mjini Sumbawanga na mwaka 1965 mjini Mbulu. Makanisa yalikuwa yakifanyakazi kwa karibu sana na Serikali ya kikoloni, ambayo ndiyo iliyomlea Nyerere ili aje kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya Waingereza kuondoka. Baada ya uhuru kupatikana, nchi ikiwa chini ya uongozi wa Nyerere, Wakristo wa Tanzania sasa wanavuna kile ambacho hawakupanda. Wanafurahia matunda ya uhuru kila sekta kutokana na Mfumo Kristo ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere, akiungwa mkono na mataifa ya Magharibi.

AN-NUUR

HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wenye akili za Mtikila tu! Anajua ukweli ulivyo, lakini anajaribu kuucha kwa maneno ya uongo. Ni sawa na mtu anayejaribu kupinga kwamba mama yake siyo mwanamke, halafu akawataka watu wamuone anasema kweli! Nyerere alimteua Rev. Mushendwa kuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Elimu ya siasa ya TANU kwa sababu tu ya imani yake madhubuti ya Kikristo, kama inavyonukuliwa katika kitabu cha Jan P. Van Bergen, Development and Religion in Tanzania kilichochapishwa na kanisa Katoliki. Kwa kipindi cha miongo mitatu ya uongozi w ake, Nyerere hakuwahi kumteua Muislamu hata mmoja kuwa

Inawatangazia Waislamu wote kuwa imeandaa safari ya Hijja na Umra mwaka 2012 kwa dola (US) $ 3375 tu. Mambo yatakayogharamiwa. Semina za Hijja, Huduma za Afya, Airport charge na Tiketi za ndege, Nyumba za kulala Makka na Madina, Ihram na Kuchinja kwa ajili ya Tamaa-tuu, Chakula wakati wote, Usari na ziara Makka na Madina, Mahema Mina na Arafa. KUHIJIWA ni DOLA US $ 1450. Fomu zinapatikana. 1 Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam- Magomeni Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba namba 26 Mkabala na Show Room ya Magari Tel: 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930 444 au 0773 930 444. 2. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar RahaLeo Tel: 0777 484982, 0777 413987. 3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar Es salaam Tel: 0784 453838. 4. Abdallah Salehe Mazrui ( Hoko) Dar es salaam Tell. 0715 72 4444. 5. Salim Is-haq Dar es Salaam Tell: 0754 286010, 0774 786101. 6. Dukani kwa Mohamed Hadh Mazrui Wete Pemba Tel: 0777 482665. 7. Sheikh Daudi Khamis Sheha Tel: 07776 79692. 8. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel: 0777 417736. Wahi mapema kulipia ili ushughulikiwe mapema, kama utalipia kwa Account No 048101000030 NBC piga simu kwanza 0774 412975. Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa ni cha Bei nafuu zaidi na huduma zake ni bora zaidi ya vikundi vingine.

Ahlul Daawa Hajj and Travel Agency

Wa z i r i w a E l i m u , l a k i n i Waislamu hawakulalamika wizara hiyo kugeuzwa himaya ya Wakristo. Tuhuma za Mtikila na Wanadhimu wengine wa Mfumo Kristo zilikuwa, eti Rais Ali Hassan Mwinyi alikuwa na lengo la kuisilimisha Tanzania nzima. Kosa lake Mwinyi lilikuwa kuteua wakurugenzi wanne Waislamu katika Wizara ya Elimu. Bila ya kutambua, masikini Mwinyi alikuwa amegusa mshipa wa fahamu wa Mfumo Kristo! Makamanda wa Mfumo Kristo wanaeneza propaganda za sumu kwamba Waislamu wanahatarisha amani na umoja wa Watanzania, licha ya ukweli kwamba amani na umoja huo imekuwa ikitunzwa na Waislamu, tangu kipindi cha harakati za kupigania uhuru na baada ya uhuru kupatikana. Inajulikana vizuri kwamba, ukiwaondoa marehemu Hassan bin Amir na Sheikh Zubeir Mtemvu, Waislamu wa Tanganyika walikataa kukiunga mkono chama chao wenyewe cha All-Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT), ili kulinda umoja wa kitaifa chini ya TANU, ambacho Rais wake alikuwa Nyerere. Waislamu hawa walijaribu kuwanasihi ndugu zao katika imani kwamba Wakristo, ingawa ni Watanganyika wenzao, lakini wana chuki ya ndani na uadui mkubwa dhidi ya Waislamu. Kamwe hawatawatendea haki Waislamu watakapodhibiti nguvu za kisiasa.Walijaribu

15
Na Mujahid Mwinyimvua KATIKA makala iliyopita tulijifunza faida ya kufuturu kwa tende na tende ilivyo msingi wa kuandaa futari. Tuliona kuwa Mtume Muhammad (rehma na amani zimkie) ametuhimiza tufuturu kwa tende. Pia, tukafafanua faida za tenda kiafya. Tulisema tende ina sukari aina ya glucose na fructose ambazo huyeyushwa mwilini kwa haraka na kumpa faraja na nguvu mfungaji. Pia tuliona kuwa tende zina aina mbali mbali za madini na vitamini ambazo ni muhimu kwa kuboresha afya ya mfungaji. Kufuturu awamu ya kwanza ambayo ni kabla ya kuswali Magharibi tutumie t ende au maji. Ndivyo alivyotufundisha Mtume wetu (rehma na amani zimkie). Kama utakosa kabisa vitu hivyo, ni bora ukafuturu kwa kutumia juisi halisi (sio zenye madawa) au asali au maziwa au matunda matamu kama vile ndizi, machungwa, mananasi, matikiti, n.k. Vilevile, mlo wa futari baada ya kuswali Magharibi uwe laini na wenye vitu vitamu vitamu kama vile viliotengenezwa kwa kutumia ndizi, mihogo, viazi vitamu, magimbi, maboga, n.k. Zaidi ya hayo, kwa watu ambao wakila daku wanasumbuliwa kuumwa tumbo mchana (mfano kujaa gesi), kwa hiyo hawali daku. Ni vema mlo wao wa usiku kabla ya kulala uwe ulioandaliwa kwa vyakula vinavyokaa tumboni kwa muda mrefu. Vyakula hivyo ni kama vile mahindi yasiyokobolewa (pika kande), maharage, ngano (usiikobowe sana), mpunga (usikobowe sana), ugali wa muhogo, ugali wa matama. Mlo pia uwe na matunda na mboga za majani, ambazo hazikupikwa sana na zisizo kuwa na mafuta mengi. Katika makala hii tutajifunza mlo unaofafaa kwa daku. Kwanza tujikumbushe maana ya neno daku na tujifunze msisitizo wake katika Dini ya Kiislamu. Kwa makusudio ya makala hii, daku ni chakula kinacholiwa usiku wa manane kwa ajili ya kujiandaa kufunga siku inayofuata. Kula daku ni jambo lililokokotezwa sana na Uislamu kama tunavyojifunza katika aya na hadithi za Mtume Muhammad (rehma na amani zimkie) zifuatazo: Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. (Quran: 2:187). Aya hii inatuhimiza kula daku mpaka karibu na alfajiri. Muhimu kula daku na iwe

Mlo bora wa daku

LISHE

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012


mtu kunywa kwa wingi chai au kahawa au soda ya coca cola/pepsi wakati wa kula mlo wa daku. Hii ni kwa sababu chai au kahawa au soda (ya coka cola na pepsi cola) hutengeneza mkojo mwingi, hivyo maji na madini yatapotea kwa njia ya mkojo kunapo kucha. Vilivile, milo yote wakati wa Ramadhani isiwe na chumvi au sukari nyingi kwa sababu mchana utakuwa na kiu sana na utapoteza maji kwa njia ya mkojo. Ni vizuri kunywa tangawizi au mchai chai au maji ya moto kama mtu hawezi kula daku bila chai au kahawa nyingi. Kawaha au chai au soda (kina coka) ukinywa kabla ya usiku wa manane hakuna shida sana. Kuhusu sukari watu wenye miaka arobaini au zaidi wanashauriwa watumia asali badala ya sukari katika chai sio tu wakati wa mfungo bali maisha yao yote yaliyobaki. Huko India wenzetu ndio kawaida yao asali katika chai, juisi, n.k. wagonjwa wa kisukari wapate ushauri kutoka kwa madaktari. Tuimalizie makala hii kwa nukta mbili. Mosi, tunawaomba wasomaji kujenga tabia ya kutafuta elimu ya maswala ya chakula na lishe. Katika Uislamu Muumini mwenye afya imara ni bora kuliko Muumini mwenye afya dhaifu. Afya nzuri inajengwa kwa kuwa na elimu ya mambo ya afya ikiwemo suala la vyakula na lishe. Pili, funga ya Ramadhani ni chuo cha kutunoa kila mwaka, kwa hiyo tumuombe Mwenyezi Mungu atukubalie funga zetu na tuwe Waislamu wazuri zaidi wa tabia baada ya kumaliza mfungo huu wa Mwezi wa Ramadhani, Aamin.

AN-NUUR

karibu na alfajiri. Mtume Muhammad (rehma na amani zimfikie) alikuwa anakula daku baada ya kiasi cha kusoma aya hamsini za Quran anaswali swala ya alfajiri (makisio ni sawa na dakika 30 kabla ya swala ya alfajiri). Mtume Muhamad (rehma na amani zimkie) amesisitiza sana kula daku. Tuone hadithi moja ifuatayo: Kuleni daku, kwani ipo baraka katika kula daku. Na tofauti ya fadhila ya funga zetu sisi na Ahlul Kitabu (Wayahudi na Wakristo) ni huko kula daku. Ili mtu awe na nguvu na afya katika mwezi wa Ramadhani (au miezi mingine) lazima ale chakula kutoka mafungu makuu yafuatayo: Kundi la kwanza vyakula vya nafaka na mizizi. Kundi la pili - maziwa, nyama, samaki, kuku, maharage. Kundi la tatu - matunda na mboga za majani. Kula matunda baada ya mlo ni muhimu sana kwa afya. Vy a k u l a v i n a w e z a kugawanywa katika makundi makuu mawili kwa kigezo cha muda wake wa kukaa tumboni. Kundi la kwanza ni vyakula vinavyo chukua muda mfupi, saa 3 mpaka 4 kusagwa. Mfano wa vyakula hivyo ni vile laini kama ndizi, viazi na vile vitamu (tende, matunda). Kundi la pili la vyakula ni vyakula vinavyokaa tumboni kwa muda mrefu (kiasi cha saa 8). Mfano wa vyakula hivyo ni nafaka na mbegu ngano, shahiri, mtama, mahindi, mchele na maharage.

Inashauriwa na wataalamu wa vyakula wa Kiislamu kuwa vyakula kama hivi viliwe kama daku au usiku sana kwa wale wanaoshindwa kuamka na kula daku. Vyakula hivi vitawapa nguvu ya kuhimili mikiki mikiki ya saumu mchana na pia wataweza kumudu majukumu mengine ya kazi za mchana. Kwa hiyo, vyakula hivi ndio vizuri zaidi kuliwa kama daku. Katika funga nia kubwa ya Mwenyezi Mungu ni kupima utii wetu kwake, sio kutukomoa. Ndio maana funga ya Kiislamu inahimiza kula daku karibu na alfajiri na kutufuru mara tu jua linapo zama. Maana yake hizo ni takriban saa 14 (kati ya saa 24 za siku nzima) (pale ambapo mchana sio mrefu) zinatosha kupima utii wetu kwa Mola. Hii maana yake ni kuwa Uislamu unazingatia namna Allah alivyo uumba mwili. Swaumu ya muda fulani ni tiba katika mwili, lakini ukizidisha muda sana bila mwili kuupa chakula, utakidhuru kiwiliwili (hasa ubongo) na akili. Ingawa baadhi ya w a s i o k u w a Wa i s l a m u wanabeza na kudai kuwa sisi tunakula alfajiri, halafu ndio tunafunga. Wajaribu na wao kufunga japo kwa saa 12 tu wataona ugumu wa swaumu, hasa kwa asiefunga kwa imani ya kumkubali Mola. Tunakumbuka Mwalimu Julius K. Nyerere alivyofunga na Waislamu enzi za kudai uhuru, kabla ya jua kuzama alisema kichwa kinamuuma na apewe asproo.

Masheikh wakamhamasisha asubiri mpaka muda wa kufuturu ulipoka. Hii ndio swaumu haina mchezo kwa mtu anaependa dunia tu. Kwa hakika kula na kufanya jimai ndio furaha kubwa katika maisha ya kidunia, na wengi wanamuasi Mola kwa hayo mawili, yaani tumbo na utupu (rejea mafundisho ya Uislamu na uzoefu katika maisha ya kila siku. Wakati mwingi wa usiku wa Ramadhani ni muhimu sana mfungaji kunywa maji ili kupunguza hatari ya mwili kukaa muda mrefu bila maji ya kutosha mchana wa mfungo. Maji na juisi huondoa sumu kutoka katika mwili. Hata hivyo, tukumbushe kama makala za nyuma, sio vizuri

Kwa mahitaji ya viroba bora vipya kabisa kwa matumizi mbalimbali sasa unaweza kupata kwa bei ya jumla na rejareja kwa saizi zote kwa bei nafuu zaidi, kwa BANDO. Tupo mtaa wa Likoma na Pemba Kariakoo, Dar es Salaam (nyuma ya Msikiti wa Idrisa). Kwa mawasiliano zaidi wasiliana kwa simu: 0657 800999/0683 800999.

VIROBA MURUA

16

AN-NUUR
16

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

RAMADHAN 1433, IJUMAA JULAI 27 - AGOSTI 2, 2012

Gazeti la An-nuur na watendaji wake wanawatakia Waislamu wote Ramadhani Kareem, Ramadhani Mubaraka.

AN-NUUR

Waliomvua hijab DC Fatma hatiani


Na Mwandishi Wetu

Zidisheni Ibada kupata uchamungu-Amirat Fatma


Na Pendo Masasa

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi Fatma Kimaro akikokotwa na wafuasi wa CHADEMA. Nyuma akionekana Mbunge Maswa Mashariki Christopher Kasulumbai (CHADEMA) aliyeshiriki katika kumdhalilisha Mkuu huyo.

MBUNGE wa Maswa Mashariki (CHADEMA) Christopher Kasulumbai (62) amenusurika kwenda jela miezi minne baada ya mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora kumtia hatiani kwa kutenda kosa la kumshambulia aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario wakati wa kampeni za uchag u z i m d o g o w a Igunga mwaka jana. Pamoja na Mbunge Kasulumbai, pia mahakama hiyo ilimtia hatiani mwanachama wa CHADEMA Robert Magilani (30), ambaye naye alipatikana na hatia ya kumshambulia DC Kimario. Akisoma hukumu hiyo kwa dakika 30, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora Thomas Simba, alisema mahakama imewatia hatiani

WA U M I N I w a dini Kiislamu wametakiwa kuzidisha ibada ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ili pindi Mwenyezi Mungu atakapokuwa amejaalia kumaliza funga zao salama, basi wawe wamezidisha kiwango chao cha u ch a Mu ngu

ikiwa ndio lengo la kuumbwa. Wito huo umetolewa na Amira wa Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania Bi. Fatuma Juma, kwenye mhadhara wa wanawake wa Kiislamu uliofanyika katika msikiti wa Ansar Sunna Mailimoja Kibaha hivi karibuni. Ni vyema mkafahamu kuwa Muislamu hawezi

kufunga bila kutia nia, na nia mahala pake ni moyoni, funga ni nguzo ya nne Uislamu na ni ibada tukufu kwetu hivyo ni vyema kujizuia kufanya kila lililokatazwa kisheria katika Uislamu na kufanya lililoamrishwa na kisheria kulifanya, alisema Bi. Fatma wakati akizungmza na akina mama wa Kiislamu wa Kibaha. Aliwafahamisha

akina mama hao wa Kiislamu kuwa katika mwezi huu Ramadhani Muislamu akifunga anapata faida nyingi. Alizitaja baadhi kuwa ni hukubaliwa moja kwa moja kwa maombi na ibada zao hivyo wazidishe kuomba msamaha kwa Mola wao. Pia alisema kuwa anayefunga anapata siha nzuri na kujihakikishia uzima kiafya.

washitakiwa hao kwa kutenda makosa mawili ambayo ni kushambulia na kutumia lugha chafu na ya matusi dhidi ya DC Kimario. Kasulumbai alinusurika kwenda jela baada ya kulipa shilingi 100,000 kwa kosa la shambulio na shilingi 50,000 badala ya kifungo miezi mitatu jela kwa kumtukana Mkuu huyo wa Wilaya. Hakim Thomas Simba, alisema wakati akisoma hukumu hiyo, kuwa pamoja na kuwapa adhabu hiyo, pia washitakiwa watatakiwa kutoa dia ya shilingi milioni moja kila mmoja kwa DC Kimario. Hata hivyo Mahakama iliwaachia huru washitakiwa wengine wawili ambao ni mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Suzan Kiwanga na Katibu wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Igunga Bw. Anuar Kashaga. H a t u a h i y o imechukuliwa baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yao. Mashitaka ambayo hayakuthibitika mbele ya Mahakama kwa watuhumiwa hao ni lile la kumweka chini ya ulinzi Bi. Kimario na kumwibia simu mbili za mkononi aina ya Nokia. Bi. Fatma Kimario kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, baada ya kuomba kuhamishwa kufuatia kuvunjiwa heshma yake wilayani Igunga. Aliomba uhamisho huo kwa kuwa asingeweza kutekeleza majukumu yake barabara kufuatia tukio hilo.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like