You are on page 1of 16

Sauti ya Waislamu

Inapokuwa heri ya James Mbatia

Ni Msiba mkubwa! Uk. 10

Al Had kujipendekeza mpaka lini?

ISSN 0856 - 3861 Na. 1039 Dhuul-Hijja 1434, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Kadhia ya Ponda, Sheikh Farid:

Vita ya Msalaba yaja kwa nguvu


Washakamata Mombasa Waislamu wanauliwa Ndoto za Wazanzibari kupumua kuyeyuka punde Tusaidie serikali, Afande Mwema kuzuiya mbweha

Polisi waharibu mali Markaz Changombe Mansour yamemkuta Mbagala sawa Mwembechai Alisema kweli Ilunga Jamhuri kukosa uadilifu katika masuala ya kidini
Ataka kuchoma kichaka cha mfumokristo Maalim Seif naye sasa amekalia kuti kavu Waislamu walishambuliwa wakienda Ijumaa Tatizo Polisi kupuuza malalamiko ya Waislamu
BAADHI ya polisi waliovamia Chuo cha Kiislamu Markaz Chang'ombe ambapo baadhi majengo yaliharibiwa na mali kupotea wakiongea na maasa wa Ubalozi wa Misri. Chuo hicho kipo chini ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar Misri,

SHEIKH Ponda Issa Ponda

SHEIKH Farid Hadd

Wavunja madrisha, wapiga wanafunzi Masheikh Azhar waduwaa, wafunga Chuo Bakwata wazika historia ya Changombe Mpemba aliyenunua ajitafutia balaa

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari
AN-NUUR
Sunday Schools hadi kuhitimu kipaimara. Aliyofanya Josephat ni matokeo ya mafundisho hayo. Kwa mkristo, Muislamu ni mfuasi wa shetani, licha ya kwamba huko mitaani wanapokutana na jamaa zao Waislamu, wanamudu kucha hisia na kuonyesha sura za upendo wa kinaki. Haya ndio mazingira wanayoishi Watanzania walio wengi kiimani. Hivi sasa watu wamekamatwa kwa kile kinachoitwa kuharibiwa na kuibwa mali za makanisa huko Mbagala. Viongozi wa juu wa serikali na vyombo vya dola tayari wameshatoa maagizo kuhakikisha waliofanya uharibifu huo wanashikishwa adabu. Viongozi wa Waislamu wanakamatwa na kuswekwa ndani. Katika mchakato wa namna hii, tunaona kwamba kuna udhaifu mkubwa kwa serikali na vyombo vyake vya dola

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012


katika kukabiliana na matatizo ya kiimani kwa watu wake hususan shida inapokuwa ya kidini au ya kisiasa. Badala ya serikali na viongozi wake kupambana na chanzo cha tatizo, wamekuwa na desturi ya kuhangaika na matokeo ya tatizo. Huu umekuwa ugonjwa wa miaka mingi hasa shida yenyewe inapowahusu Waislamu. Tunavyofahamu kila jambo lina chanzo chake. Na dawa sahihi ya kuondoa tatizo ni kushughuhulikia chazo cha tatizo ili kuweza kuliondoa kabisa lisijitokeze tena. Kama ni kuondoa mti, basi ungolewe na mizizi yake, sio kukata matawi yake na kuuacha, utachipua. Sote tunafahamu kuwa chanzo cha tatizo Mbagala kuwa ni kukojolewa Quran kwa makusudi. lakini tukio linalozungumzwa sasa ni kuharibiwa mali za makanisa na kuchukua hatua za kuwadhibiti Waislamu na viongozi wao. Utadhani wanaotuhumiwa kuharibu makanisa hayo walikurupuka tu kama wehu na kufanya uhalifu huo. Ipo haja sasa kwa serikali kutumia busara na uadilifu katika kutanzua mizozo ya kiimani nchini badala ya kutumia mazoea. Siku zote ni vyema kikatizamwa chanzo. Ukiingizwa udini, dharau, kibri na kujipendekeza na ushabiki katika kutatua shida hatarishi kama hizi za kiimani, ni sawa na kuuteketeza mti kwa kukata matawi yake tu. Viongozi wa dini nao wana dhima ya kufundisha waumini wao elimu sahihi ya dini kwa mujibu wa maandiko ya vitabu vyao vya kiimani, badala ya kutoa mafunzo ya dini kwa dhana za chuki za kiimani, kwa kuamini kuwa ndio kumjengea imani muumini na kumlinda asije akaasi dini. Si lazima kumjaza chuki Mkristo juu ya Uislamu ili apate kuwa Mkristo mzuri na adumu katika dini hiyo.

AN-NUUR

MAONI YETU

QURAN Tukufu ni kitabu ambacho ndio muongozi wa Waislamu. Chenyewe na Hadithi za Mtume Muhammad (s.a.w) ndio mihimili ya imani ya Kiislamu. Hivi karibuni kijana Emannuel Josephat, mkazi wa Mbagala anadaiwa makusudi, alitemea mate na kukojolea kitabu kitukufu cha Qur an mbele ya wenzake Waislamu. Kukojolewa Quran ni dharau na tusi kubwa na uchokozi wa makusudi kwa Waislamu popote pale. Lakini zaidi, kitendo hicho kinatafsiri chuki kubwa dhidi ya Waislamu na imani yao. Hatua hiyo imeleta tafrani kubwa ambapo Makanisa yameharibiwa, misikiti imeharibiwa na Waislamu wamepigwa mabomu na kujeruhiwa. Hayo yote ni matokeo ya hasira zilizosababishwa na tendo hilo chafu la kukojolea kitabu cha Mwenyezi Mungu. Baada ya kitendo hicho, zimekuwepo kauli za utetezi kwa baadhi ya watu kwamba utoto ndio uliomsukuma kijana Emannuel Josephat (14) kutenda uhalifu huo. Hata hivyo, wanaotoa kauli hizi hatudhani kwamba watoto wao wa kike wangetokea kubakwa na mtoto mwenye umri kama wa Josephati wangekuja na utetezi wa namna hii. Yaani kwamba mbakaji ni utoto hivyo isieleweke vibaya na huruma ichukue nafasi zaidi. Swali la kujiuliza, mkosaji ni mtoto kwa kiwango gani kiasi kwamba ameshindwa kutambua kwamba kitendo anachokifanya ni kichafu. Je, kwa utoto huo huo, anaweza kukojolea Biblia yake? Yupo msanii anayeitwa Elizabeth Michael (Lulu) ambaye yupo rumande hivi sasa akikabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake Steven Kanumba. Pamoja na kuwepo hoja za utoto dhidi ya mtuhumiwa,

Si lazima kutukana Waislamu kuzuiya Wakristo kuasi Kanisa

bado sheri a i n a c h u k u a mkondo wake ili haki iweze kupatikana. Umri wa Lulu ambao bado una utata (miaka 17 au 18) na umri wa kijana aliyekojolea Qur,an (miaka 14) unaweza kuwa katika kiwango cha kuitwa watoto, lakini si watoto wa kushindwa kutambua zuri na baya. Kwamba miaka 14 aliyo nayo Emannuel Josephat, haiwezi kuhalalisha uhalifu wake wa makusudi dhidi ya imani ya watu wengine, halafu itarajiwe kwamba umri wake mdogo unaweza kuwa kinga ya kushughulikiwa au kupuuza kile alichokifanya. Kutokana na mazingira ya tukio lenyewe, Inaonekana wazi kwamba chuki iliyokithiri dhidi ya Uislamu na Wa i s l a m u , ndio iliyomsukuma kijana Josephat kukojolea Quran. Hakununua wala kuokota kitabu hicho Quran, bali alichukua msahafu kwa mwenzie na kukikojolea huku mwenye kitabu akishuhudia. Kwamba alikusudia kuonyesha chuki aliyo nayo dhidi ya wale wote wanaoamini katika kitabu hicho. Kabla ya kufanya tukio hilo, Josephat alisema kuwa nyumbani kwao wanakijua kitabu cha Quran kuwa ni kitabu cha shetani na kwamba Waislamu wanafuga majini na Qur an yao ni kitabu cha mapepo. Hata hivyo, tunaamini kabisa kwamba kauli za kijana huyo hazikuja tu kwa bahati mbaya. Bali dhana hizi ni matokeo ya mafundisho ya miaka mingi yanayotolewa Makanisani na Mapadri na Maaskofu kwa waumini wao. Pamoja na kuwa ni mafundisho ya uongo na ya kujenga mioyo ya chuki kwa waumini, lakini wenyewe wanaona kuwa ndio njia sahihi ya kulinda imani za waumini wao wasivutwe kuingia katika Uislamu. Wa k r i s t o w e n g i wamepandikizwa dhana hii na viongozi wao tangu

Mansour yamemkuta Alisema kweli Ilunga


Na Mwandishi Wetu kuzungumza kwa dhati, ni wakati wa kuzungumza ukweli, bila ya hofu wala bila woga kwa maana hofu na woga haukupeleki mahali, haswa unapozungumzia mustakabali wa nchi hii. Alisema. Kwa upande mwingine Mansour aliwataka Wazanzibari kuwapuuza viongozi wa serikali na kisiasa wanaotaka kulazimisha muungano wa serikali mbili ambao alisema kuwa umefeli kutatua zinazoitwa kero za muungano. Anaposimama kiongozi wa juu wa nchi aliyepewa imani na watu, akisimama akasema mkitaka msitake, muungano utakuwa hivi hivi (wa serikali mbili), mie huwa najiuliza, kulikoni? Unamlazimisha nani, wakati mwanao mwenyewe ndani ya nyumba zama hizi huwezi kumlazimisha, sasa utoke ukawashurutishe watu, viongozi wa namna hiyo ni waovu, na wamekosa muelekeo. Alisema Mansour na kusisitiza kuwa Zanzibar inahitaji viongozi ambao wana hikima, wana busara (na) wanarai watu.Kiongozi hawezi kushurutisha watu. Alichosema na kusisitiza Mansour katika kongamano hilo ni kuwa mfumo wa muungano uliopo hauwasaidii Wazanzibari na kwamba hata Tume na Kamati zilizowahi kuundwa kuangalia matatizo

AMESEMA kweli Sheikh Ilunga Hassan Kapungu, ukitaka balaa hoji muungano. Mansour alitangaza kutaka Zanzibar huru, yenye kiti Umoja wa Mataifa; yamemkuta. Rais Alli Mohammed Shein amefuta uteuzi wa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi aliokuwa amempa Mansour Yussuf Himid. Badala yake nafasi hiyo amepewa mtu ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa akijipamba kwa kauli za Maskani ya Kisonge za kutaka Zanzibar iendelee kuenzi muungano wa serikali mbili. Huyu ni Shawana Bukheti Hassan ambaye katika uchaguzi mdogo wa hivi karibuni Jimbo la Bububu anatajwa kuwa mmoja wa makada wa CCM waliofanikisha kupatikana ushindi wa kibabe wa chama hicho tawala. Ukiacha aliyokwisha kuyasema huko nyuma kuonyesha kuwa muundo wa muungano uliopo haufai na kwamba Wazanzibari wanataka kupumua, hivi karibuni katika kongamano lililofanyika katika hoteli ya Bwawani, Mansur, aliwataka Wazanzibari kusimama imara kupigania uhuru wa nchi yao. Huu ni wakati wa

ya muungano, zilibaini kuwa mfumo wa serikali mbili haufai. Miaka 48 watu wameshindwa kuzungumza, tutazungumza leo, kwa mfano kuna kamati karibia ya 25, zote hizi zimekia maamuzi mamoja tu, kwamba mfumo tuliokia haufai, hawa wote ni wasomi waliobobea na timu zao ni za wasomi waliobobea, tena nyingine zinaundwa mie bado mi ndogo nipo nje nasoma. Sasa leo msitunyoshee vidole kina Moyo na Mansour, wanataka kuharibu, hawa ndio waliosema kwamba huu mfumo sio. Sasa jamani kamati tumeziunda wenyewe, zimeundwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibra na kila kazi waliyopewa jibu ni moja tu, mfumo siyo. Hata hivyo, pamoja na kusema yale yale ambayo y a l i s h a s e m w a n a Tu m e zilizowahi kuundwa na serikali, ambayo hata hivyo hayakufanyiwa kazi, inaonekana Mansour kagusa eneo lisilotakiwa kama alivyosema Ilunga. Amehoji muungano kitu alichosema kwamba ni sawa na kugusa mfumokristo unaodhibiti Zanzibar kupitia muungano huu wa serikali mbili. Katika makongamano Inaendelea Uk. 4

Habari

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

Ipeni elimu nafasi ya kwanza Maendeleo yatakuja -Sheikh


Na Bakari Mwakangwale
WAISLAMU kote nchini wametakiwa kufanya juhudi katika kuuhisha Uislamu kupitia elimu ili kujiletea maendeleo katika jamii yao kwa ujumla. Akizungumza mwishoni mwa juma lililopita katika haa fupi ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi katika shule ya Almustaqiim iliyopo Mtoni kwa Aziz Ali Temeke Jijini Dar es Salaam, Sheikh Mansour Nassor alisema hakuna jambo kubwa la kuwarithisha watoto kama elimu. Akikariri Aya kutoka ndani ya Quran tukufu pamoja na Hadith za Mtume Muhammad (saw), Sheikh Nassor, alisisitiza suala la elimu na kuongeza kuwa ubora wake mbele ya Mwenyezi Mungu umepewa nafasi ya kwanza kabla ya ibada nyingine yoyote. Alisema, suala hilo licha ya kukokotezwa sana katika mafundisho ya Kiislamu, bado kuna watu wachache wamekuwa wakipuuza wakati ambapo nayo ni faradhi kama alivyopata kusema kiongozi wa Umma huu. Mtume (s a w) amesema, kutafuta elimu ni lazima kwa kila Muislamu mwanaume na Muislamu mwanamke, hivyo hatuwezi kudai tutafanikiwa kuipigania dini hii bila ya kufanya hima kuwapeleka watoto wetu wapate mafunzo yatakayowawezesha kuyakabili vema mazingira yao ya duniani na akhera. Alisema Sheikh Nassor. Kwa upande wake, meneja wa Shule hiyo ambaye pia ni Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Farid Saleh, aliwataka Waislamu kutumia fursa za kuanzisha Shule za Kiislamu kwani shule zilizopo kwa sasa hazitoshi. Nawaomba wazazi na Waislamu popote pale mlipo hapa nchini kuhakikisha mnazitumia vema fursa mnazozipata kwa kuanzisha Shule nyingi ili vijana wetu hawa wasipate kisingizio cha uchache wa Shule, alisema. Akaongeza kuwa, kwa sasa Shule zilizopo ni chache sana ukilinganisha mahitaji halisi ya Waislamu pamoja na mwamko wao kwa kupeleka vijana wao kwenye Shule zinazotoa elimu ya maadili na malezi ya Kiislamu. Mathalan, hapa kwetu Mustaqiim, tayari darasa la kwanza limeshajaa na tumeanza kusimamisha usajili wa wanafunzi, sasa hali itakuwaje itakapoka mwezi Desemba? alisema na kuhoji Shekh Farid. Pamoja na nasaha hizo kiongozi huyo wa Baraza Kuu Wilayani humo aliwataka wazazi kutoa ushirikiano na uongozi wa Shule ambao wanawapeleka watoto wao ili kuleta ufanisi na kupata matarajio mema yaliyokusudiwa. Aidha, Sheikh Farid, aliwanasihi Waislamu kuangalia aina ya shule za Sekondari wanazowapeleka watoto wao mara baada ya kuhitimu elimu ya Msingi. Alisema, ni vyema wazazi kuwaendeleza watoto wao katika shule za Kiislamu, kwa maelezo kuwa ni kupoteza nguvu na kumtoa mtoto katika misingi ya maadili aliyoipata kwa muda wa miaka saba iliyotumika kuwalea vijana hao katika Shule zao ikiwa atapelekwa katika shule za hovyo zisizo na maadili.

Mbagala sawa Mwembechai


za Paroko zilipokewa na serikali kwa uzito mkubwa na kwamba zilitosha kuwa SERIKALI ya Jamhuri agizo kwa serikali kuingia ya Muungano Tanzania kazini kuwashukia Waislamu na Jeshi lake la Polisi, kwa hasira kinyume cha imetuhumiwa kusababisha sheria na utawala bora, kwa vurugu kubwa Mbagala Mbagala Polisi walipuuza wiki iliyopita iliyopelekea malalamiko ya Waislamu na watu kuumizwa na baadhi kwamba kulikuwa na kila ya Misikiti na Makanisa dalili kwamba wanataka kuharibiwa. kulizima kinyemelea suala la K a t i k a t u h u m a h i z o kunajisiwa Quran. imeelezwa kuwa Jeshi la Waislamu hawakuchukua Polisi Wilaya ya Mbagala sheria mkononi, walifuata Kanda Maalum ya Kipolisi taratibu za nchi na za kisheria Mkoa wa Temeke, ndiyo hadi kumkisha mtuhumiwa sababu ya kuzuka kwa vurugu polisi, lakini polisi hawakulipa eneo la Mbagala Jijini Dar es uzito hali iliyowafanya Salaam, baada ya kushindwa Waislamu kwenda kituoni kumchukulia hatua za haraka kutaka maelezo. Anasema kijana aliyekojolea Qur an. mkazi mmoja wa Mbagala. Baadhi ya Waislamu wa Akiongea na mwandishi Mbagala wamekia hatua ya mkazi huyo anasema kuwa kulituhumu Jeshi hilo, wakidai kama Polisi wangekuwa kuwa walishindwa kulipa makini, wakalipokea jambo uzito tukio la kunajisiwa hilo kwa uzito wake, hali Qur an, lililofanywa siku ya isingekia hapo, lakini wao Jumatano wiki iliyopita na utadhani waliona hakuna kijana mmoja aliyetajwa kwa kilichotokea au ilikuwa kana jina la Emanuel Josephat kwamba waliona alichofanya (14). yule kijana ni sawa au kama Shutuma hizo zimetolewa sio sawa basi, ama ni kwa n a w a t u w a l i o k u w a rushwa au vipi ikawa wanataka wakishughulikia suala la kumhami yule kijana, hilo ndio kunajisiwa Quran ambapo lililozua vurugu. Wameumiza wamesema kuwa kilichotokea watu, wameharibu Misikiti, Mbagala ni sawa na yale w a m e s a b a b i s h a v u r u g u yaliyotokea Mwembechai zilizopelekea kushambuliwa ambapo Waislamu waliuwawa m a k a n i s a k u t o k a n a n a wakati serikali ikitekeleza utendaji wao usio wa haki, shinikizo la Paroko wa Kanisa wanaonekana kupendelea Katoliki Mburahati. Wa k r i s t o n a k u d h a r a u Wakifafanua walisema Waislamu. Alisema mama kuwa, wakati katika kadhia mmoja, mkazi wa Chamazi ya Mwembechai shutuma ambaye hata hivyo hakutaka Na Bakari Mwakangwale jina lake kutajwa gazetini. Inaonekana saikolojia iliyojengwa kwa Polisi wetu ni kuwa Mkristo katika nchi hii haguswi inapotokea kuwa mlalamikaji ni Muislamu, ila kwa Mkristo ni kinyume chake, akilalamika Mkristo, Polisi na serikali kwa ujumla hawasubiri wala kushughulika kutafuta ukweli, watawavurumisha Waislamu kama wahalifu na majambazi yaliyokwisha kuhukumiwa, hili ndio lililoleta maafa Mwembechai, ndio pia iliyosababisha kuuliwa Waislamu Pemba Januari 2001 na ndio lililoleta vurugu Mbagala. Aliongeza mama huyo mtu mzima. Akifafanua zaidi akasema kuwa hata kauli za viongozi wa serikali akiwemo Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete, zinaonyesha mwelekeo huo huo. Hakuna aliyeguswa na kitendo cha kunajisiwa Quran wala Misikiti iliyoharibiwa kwa mabomu ya Polisi. Kila mmoja alikimbilia kujisajili kuwa ni mtetezi wa Makanisa, Ukristo na Wakristo. Kwa kweli kitendo cha Rais Kikwete kutokuonyesha kabisa kuguswa na kitendo cha Polisi kupiga mabomu misikiti, inaonyesha Wakristo hawakukosea kuwa yeye ni chaguo la Mungu wao wa Utatu na sasa wanafaidi matunda; ila jambo moja tu linawapa faraja Waislamu kuwa hata washirikina wa

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (kushoto) akionyesha bomu waliolikuta ndani ya Msikiti katika vurugu zilizotokea Mbagala Ijumaa iliyopita.

Kiquraishi walitumia dola kumpiga vita Mtume (s.a.w), lakini hatimaye Makkah ilikombolewa Abu Sufyani akasalimu amri. Alisema mama huyo na kuongeza kuwa hata zile kauli zilizotolewa katika zile vurugu zilizohusishwa na Uamsho, Zanzibar hivi karibuni, zinathibitisha hilo hilo. Ila akasema kuwa wanachotakiwa Waislamu kufahamu ni kuwa kila zama watalazimika kujitoa muhanga kwa namna moja au nyingine kuhami dini yao, Dini ya Haki ambayo hivi sasa nguvu za ukafiri na ushirikina dunia nzima kupitia zinazoitwa jumuiya za kimataifa zimeungana kuupiga vita. Akawapa faraja akiwaambia Waislamu, hasa ambao hivi sasa wanashikiliwa na Polisi wakiwa na kesi ya kujibu kuhusiana na vurugu za Mbagala, akiwataka warejee aya ya Quran inayosema kuwa makari watakusanya pesa, nguvu za kiuchumi na maguvu yao ya kijeshi na kidola kuwapiga vita Waislamu, lakini nguvu na pesa zao zitapotea bure kwa sababu hawataweza kuzima Nuru ya Uislamu huku katika vita yao hiyo wakiwarahisishia Waislamu njia ya kupata Radhi za Mola wao. Mazoea ya Jeshi la Polisi nchini kutokuchukua hatua inapotokea Waislamu Inaendelea Uk. 6

4
Na Mwandishi Wetu kufanana na Al Shabab. Inaelezwa kuwa pamoja na kuwa serikali ya Tanzania na vyombo vyake vya Usalama, imekuwa madhubuti hadi sasa kuweza kuhimili shinikizo la kutumbukizwa katika mtego wa Al Shabab, akina Fazul na usanii wa watoto wa shule za msingi kuvamia Ubalozi wa Marekani, lakini matukio ya Changombe na lile la kukojolea Quran na hatua walizochukua b a a d h i y a Wa i s l a m u ; huenda yakawarahisishia kazi washenga wa inayoitwa vita dhidi ya ugaidi kuitosa nchi ilikozama Pakistan na Yemen. Wachambuzi wa masuala ya inayoitwa Vita dhidi ya ugaidi wanasema kuwa kwa Kenya tukio la kutekwa watalii (ambapo inawezekana pia ilikuwa la kupangwa haikuwa Al Shabab waliohusika); lilitumika vizuri na kwa kasi kuitumbukiza Kenya katika vita na hivi sasa watu wasio na hatia wanauliwa ikidaiwa kuwa ni mashambulizi ya Al Shabab kulipiza kisasi. Hata hivyo wachambuzi hao wanasema kuwa kinachofanyika ni kuhakikisha kuwa mashambulizi ya kuuwa, kutisha na kuwaweka watu katika wasiwasi hayakomi Kenya ili kubakisha kile kisingizio cha jeshi la Kenya kuendelea kuwepo Somalia ambapo mabeberu hawataki kuona Wasomali wakijiamulia mambo yao wenyewe kama

Habari

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

Vita ya Msalaba yaja kwa nguvu


HALI tete inayoendelea Dar es Salaam, Zanzibar na Mombasa kwa wakati mmoja, huenda ikawa na tafsiri na agenda kubwa zaidi kuliko inavyotizamwa. Wasiwasi uliopo ni kuwa ama kwa kupangwa au kwa kutokezea tu, huenda hali hiyo ikatumika kuizamisha Ta n z a n i a k a t i k a t o p e linaloitesa Yemen, Pakistan na Kenya hivi sasa. Wa d a d i s i w a m a m b o wanasema kuwa toka aliyekuwa Rais wa Marekani George W Bush atangaze Vita ya Msalaba na toka Marekani iweke mkakati wake wa kusambaza utando wa kijeshi duniani ili kudhibiti rasilimali za dunia hasa mafuta na masilahi mengine, mbinu ya kuwatangazia watu ugaidi, msimamo mkali na siasa kali, imekuwa ikitumika kujenga uhalali wa taifa hilo kubwa kuingia kwa kisingizio cha kusaidia kuleta amani na kupambana na ugaidi. Kutokana na hali hiyo, yanayojiri hivi sasa Dar es Salaam na Zanzibar ambapo kunaonekana kuwa na mapambano yanayohusisha Waislamu na vyombo vya dola na wakati mwingine kuharibiwa mali na nyumba za ibada; misamiati ya msimamo mkali, ugaidi itaanza kupepewa kama ilivyokwisha kutumika Zanzibar ambapo inalazimishwa Uamsho

Inatoka Uk. 2 yake juu ya madhara ya mfumokristo, Sheikh Ilunga amekuwa akisema kuwa kuvunja au kubadili muundo wa muungano uliopo ni sawa na kuchoma moto kichaka ulikojificha mfumokristo unaoidhibiti Zanzibar ndio maana kila aliyejaribu kuhoji yalimkuta. Katika kusherehesha akatoa mifano ya kuuliwa Mzee Karume, yaliyomkuta Mzee Alhaj Aboud Jumbe, Maalim Seif wakati huo akiwa ndani CCM na SMZ. Kutokana na hoja za Ilunga, yanayomkuta Mansour ni katika mlolongo wa yale yaliyomkuta Alhaj Aboud Jumbe. Wa k a t i h u o h u o , wachambuzi na wadadisi wa

Mansour yamemkuta Alisema kweli Ilunga

siasa za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wanasema kuwa hata Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Shariff Hamad kakalia kuti kavu. Wanasema, msimamo wa Maalim Seif ni sawa na ule wa Mansour wa kutaka Zanzibar huru yenye mamlaka yake kamili ndani ya muungano kwa hiyo hawaoni namna ambavyo atadumu kufanya kazi na Rais ambaye msimamo wake ni kuwaadabisha wanao hoji muungano wa serikali mbili. Habari za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa kanda za mawaidha ya Sheikh Ilunga juu ya mfumokristo Zanzibar, hivi sasa zinatizamwa na kusikilizwa sana Zanzibar watu wakitaka kuona kile alichokisema na hays yanayojiri hivi sasa.

ASKARI wa jeshi la polisi wakiwa katika mitaa ya Unguja (Darajani) kudhibiti ghasia zilizotokea juzi baada ya Waislamu kupata habari za kutoweka kwa Sheikh Farid Had katika mazingira yasiyoeleweka. walivyofanya na kujiletea za nyukilia katika janga uliopo ambao unadaiwa amani wakati wa serikali la serikali kutafuna raia kuwa kichaka cha kujicha iliyoongozwa na Umoja wa wake akidai kupambana na mfumokristo unaofanya kazi Mahakama za Kiislamu. magaidi. Zanzibar. Uganda washaingia kijeshi Kwa upande wa Masheikh Kauli na hatua alizochukua kwa kisingizio cha kusaidia na waumini wao amewataka Rais Shein hivi karibuni kupambana na Joseph Konny, kuwa makini kidogo na ikiwa ni pamoja na kumtoa Kenya tayari washaikamata kuzielewa siasa za kimataifa katika Baraza la Mapinduzi kikachero na kijeshi, drone hivi sasa zinavyokwenda M h e s h i m i w a M a n s o u r, zitaingia Mombasa kupiga ambapo Israel ikiuwa maelfu pamoja na hili la kutekwa madrasa ikisingiziwa kuwa ya Waislamu, ikipiga mabomu Sheikh Farid, yanaunganishwa wanalenga makamanda wa hospitali na shule ikauwa kama ni mlolongo wa matukio Al Shabab, sasa hali hii wagonjwa na watoto wa yaliyoratibiwa ili kutoa ya kutoweka Sheikh Farid skuli, hutasikia ikikemewa kitisho, kubadili agenda na huenda ukawa mpango wa katika Baraza la Usalama la kuzima moto wa kupigania kutaka lizuke zogo lizilo na Umoja wa Mataifa. Zanzibar huru yenye kiti mwisho kipatikane kisingizio U t a k a o s i k i a Umoja wa Mataifa. cha kuikamata na Zanzibar. wakiandamwa ni Omar El Wachambuzi wanasema Alisema mchambuzi mmoja Bashir, Assad, Waislamu kuwa, mahesabu yanaonyesha ambaye hata hivyo hakutaka Gaza, Ahmednajad na watu kuwa huenda waliomteka jina lake kutajwa gazetini. kama hao. wanachotarajia ni kuwa Mimi silitizami suala hili A m e s e m a a k i m a l i z i a zogo litaibuka, itakuwa katika ufinyu wa siasa za n a s a h a z a k e a m b a p o mapambano kati ya wananchi Zanzibar, Polisi wanasema amesisitiza kuwa yeye hapingi na serikali (vyombo vya dola) hawajamkamata, serikali watu kupigania haki zao, ila na kwa njia hiyo, wananchi inasema haihusiki, ni nani watizame wanapigania vipi ili watakuwa washatengana basi anahusika? Hapana wasiwape mabeberu mwanya na viongozi wao katika shaka waliomteka wanajua na sababu ya kuishinikiza kupigania Uzanzibari. nini kitatokezea na hatimaye serikali kupokea misaada yao Aidha wanasema wataitumia vipi fursa hiyo. ya kikachero na kijeshi. kuwa, zogo likizidi kama Aliongeza mchambuzi Kwa upande mwingine inavyohowa kama Sheikh h u y o n a k a t i k a k u t o a wapo wanaodhani kuwa Farid hakupatikana katika nasaha zake akasema kuwa huenda kutekwa Sheikh Farid masaa 24 yajayo, huenda anaisihi serikali ya Jamhuri ni njama za kusha agenda nguvu ya kipolisi na kijeshi ya Muungano na ile ya ya Wazanzibari kutaka ikaongezwa kutoka Bara Zanzibar kuwa makini katika kupumua. na kujenga mazingira kama kulishughulikia suala la Wanaotoa maoni haya yale yaliyokuwa yakitokea Farid kwani huenda kukawa wanasema kuwa hivi karibuni wakati wa uchaguzi mkuu na na mkakati wa kibeberu taarifa kutoka ndani ya Tume hapo halitakuwan tena suala kuifanya Tanzania kuwa ya Warioba zinaonyesha kuwa la Zanzibar na hiyo itakuwa Pakistan ya Afrika na nchi kama itapigwa kura ya maoni namna ya uhakika ya kuzima ikishazamishwa iliko zama leo, basi kama kutakuwa azma ya Wazanzibari kutaka Somalia, si rahisi kutoka. n a w a t u w a t a k a o t a k a kupumua. Mi nawasihi viongozi wa muungano huu wa serikali Mimi nawasihi viongozi serikali na wa kisiasa wawe mbili, hawatazidi asilimia w a U a m s h o , J U M I K I , makini wasije wakawa kama 10 (10%). Masheikh na wananchi Musharraf aliyeitumbukiza H a l i h i i i n a o n e k a n a kwa ujumla wawe makini, nchi yake yenye nguvu kutishia mfumo wa muungano Inaendelea Uk. 8

5
KADUNA Waislamu wasiopungua 20 wameuliwa na watu waliokuwa na silaha baada ya watu hao kushambulia msikiti katika kijiji kimoja cha Kaskazini mwa Nigeria. Mauaji hayo yametokea mwanzoni mwa wiki hii katika kijiji cha Dogo Dawa cha jimbo la Kaduna. Abdullahi Muhammad, Afisa katika eneo hilo amesema kuwa wanashuku kuwa mauaji hayo huenda ni ya kulipiza kisasi na huenda yamefanywa na magenge ya majambazi yenye silaha baada ya kuwapoteza baadhi ya wanachama wake katika ufyatulianaji risasi uliojiri hivi karibuni kijijini hapo kati ya majambazi hao na wanavijiji. Amesema, wakazi wa kijiji hicho wamekuwa wakivamiwa mara kwa

Habari za Kimataifa

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

Waislamu 20 wauliwa Nigeria


mara na watu wenye silaha wanaofanya mashambulizi kutokea kwenye kambi zao zilizoko msituni. Polisi wako katika mchakato wa kutoa taarifa za kina kuhusu shambulizi la wauaji hao. Hatuna hakika iwapo mauaji hayo yameandaliwa na kundi lolote au wanyanganyi. Polisi itatoa taarifa kamili baada ya uchunguzi kukamilia, alisema msemaji wa National Emergency Management Agency Yushau Shuaib. Hata hivyo, baadhi ya wanakijiji wa jamii ya Dogon Dawa wamedai kuwa shambulio hilo limefanywa na kikundi cha majambazi ambao awali walitishia kufanya shambulio baada ya maficho yao kubainiwa na wana usalama, kufuatia uvamizi wa hivi karibuni uliofanywa na majambazi hao.

Mtengenezaji wa lamu kumchafua Mtume kizimbani

LONDON Viongozi wa serikali za Scotland na Uingereza wamekubaliana kuhusu kuitisha kura ya maoni ya kuamua suala la kujitenga Scotland na Uingereza. Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Waziri Kiongozi wa Scotland Alex Salmond, wametia saini mwafaka wa kuitishwa kura ya maoni ya kujitenga Scotland na Uingereza. Lengo la mkutano huo wa leo limetajwa pia kuwa ni kumaliza masuala ya mwisho yaliyobakia kuhusiana na mwafaka huo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, itabidi kura ya maoni ya kuamua kujitenga Scotland na Uingereza ifanyike kwenye msimu wa machipuo wa mwaka 2014. Matini kamili ya mwafaka huo watakabidhiwa Waziri Mkuu wa Uingereza na Waziri Kiongozi wa Scotland kwa ajili ya kujadiliwa na kupasishwa. Miongoni mwa masuala ya mwisho ambayo pande mbili zimekubaliana ni namna ya kudhamini fedha za kuitisha kura hiyo ya maoni. Itakumbukwa kuwa tangu mwaka 1707 wakati ilipoasisiwa nchi inayoitwa Briteni yaani Great Britain, Scotland ilikuwa na serikali ya ndani ya kujiendeshea baadhi ya mambo yake kama vile Wizara ya Elimu, Afya na kujitungia sheria zake za ndani. Mwaka 1999 kuliasisiwa Bunge la Scotland na kuzidi kuifanya kuwa nchi huru, lakini pamoja na hayo bado ilikuwa chini utawala wa kifalme wa Malkia wa Uingereza.

Cameron asaini kura ya maoni Scotland kujitenga na Uingereza


Kwa kweli kuvunja muungano na kujitenga na Uingereza ni ndoto ya miaka mingi ya wananchi wa Scotland na baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa kitakachofanyika kwenye kura ya maoni ya mwaka 2014 ni kupiga muhuri wa mwisho tu wa kujitenga Scotland na Uingereza. Wa c h a m b u z i h a o w a mambo wanaamini kuwa, ni jambo linalowezekana kabisa kwa Scotland kujitenga na Uingereza. Wa s k o c h i w e n y e w e wanaamini kuwa kujitenga Scotland kutawafanya wawe na mwakilishi wao katika Bunge la Ulaya. Vile vile wanaamini kuwa tabia na tamaduni za Uingereza na Scotland hazifanani. Scotland ni nchi inayofuata mfumo wa Social Democrat wakati mfumo wa Uingereza ni wa kihadhina. Weledi wa mambo wanaamni kuwa tofauti hizo kubwa zinalifanya suala la kuendelea kuungana nchi hizo mbili liwe gumu sana. Katika upande mwingine, chama cha taifa cha Scotland kinaamini kuwa ni haki ya kimsingi ya Waskochi kupewa fursa ya kupiga kura ya maoni ya kuamua mustakbali wa nchi yao. Kinaamini kuwa, hilo ni jambo ambalo kwa muda mrefu lilikuwa linapiganiwa na wananchi wa Scotland. Hata hivyo wako watu wanaopinga kuitishwa kura hiyo ya maoni. Jambo hilo linawafanya baadhi ya wafuatiliaji wa

siasa za Uingereza waamini kuwa, kujitenga Scotland na Uingereza si jambo jepesi kama inavyokiriwa. Hivyo kilichobakia ni kusubiri kuona kutatokea nini katika siku za usoni na katika kura hiyo ya maoni ya mwaka 2014. Wakristo wazidi kupungua Marekani Uchunguzi uliofanyika huko Marekani unaonesha kuwa idadi ya Wakristo wa Kiprotestanti imepungua na kukia chini ya asimilia 50 ya watu wote wa jamii ya nchi hiyo. Taasisi ya utati na uchunguzi wa maoni ya Pew, imesema katika ripoti iliyopewa jina la Dini na Maisha ya Kijamii kwamba mtu mmoja kati ya kila Wamarekani watano hujitambua kuwa mtu asiye na itikadi kwa dini yoyote. Ripoti hiyo inasema kuwa kijana mmoja kati ya vijana watatu wenye umri wa miaka chini ya 30, hujitambulisha kuwa hana dini mahususi au anaamini baadhi ya masuala ya kidini na kiroho. Pew imesisitiza kuwa, theluthi moja ya vijana wa Kimarekani kutoka familia za Kikristo, wameachana na Ukristo huku katika kiwango hicho kati ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kimefikia asilimia tisa. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani kwa jamii ya Wakristo wa Kiprotestanti kuwa chini ya asilimia 50 na sasa imekia asimia 48 ya jamii ya nchi hiyo. Kupungua huko kwa jamii ya Wakristio wa kiprotensti kumewatia wasiwasi mkubwa viongozi wa Marekani.

LOS ANGELES Mtengenezaji wa filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw), mapema wiki hii amefikishwa katika mahakama ya Los Angeles akikabiliwa na kesi ya utapeli. To v u t i y a L e m o n d e , imeripoti kuwa Mark Basseley Youssef maarufu kwa jina la Nakoula Basseley Nakoula, amekishwa mahakama kwa mara ya pili chini ya ulinzi mkali wa polisi. Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba mhalifu huyo atahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela. Nakoula Basel Nakoula

ana umri wa miaka 55 na mwaka 2010 alihukumiwa kifungo miaka miwili jela kwa kupatikana na hatia ya utapeli lakini aliachiwa huru kwa masharti. Hata hivyo Disemba 23 mwaka huu jaji wa mahakama moja ya Marekani alimtambua Basseley kuwa ni mtu hatari na akaamuru atiwe mbaroni haraka iwezekanavyo. Mmarekani huyo Myahudi ametengeneza filamu inayomvunjia heshima Mtume (saw) ya Innosence of Muslims, ambayo imewakasirisha Waislamu kote duniani. Filamu hiyo imesababisha maandamano ya Waislamu na hata wasio Waislamu katika maeneo yote ya duniani.

KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERSTanzania COLLEGE S.L.P. 62, Same Kilimanjaro, Mob: 0787 188964

NAFASI ZA KUJIUNGA NA KOZI YA UALIMU WA SHULE ZA AWALI, MSINGI NA MADRASA 2013


Sifa na masharti ya kujiunga Muombaji atimize sifa na masharti yafuatayo: (i) Awe Muislamu aliye tayari kuishi Kiislamu (ii) Awe anajua kusoma Quran kwa ufasaha. (iii) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya Uislamu, Darasa la Watu Wazima kabla ya kujiunga. (iv) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne na awe anafundisha madrasa au kipindi cha dini katika shule za Msingi au Sekondari. Patakuwa na usaili siku ya tarehe 1/12/2012 saa 2:00 asubuhi katika vituo vilivyoainiashwa kwenye fomu ya maombi. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11/2012. Fomu italipiwa shilingi 5,000/- tu. Fomu zinapatikana katika vituo vilivyoorodheshwa ukurasa wa 11 MKUU WA CHUO

6
Inatoka Uk. 3

Makala

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012


Temeke, RPC, RCO pamoja na OCD, wote walikuwepo kituo cha Maturubai, siku hiyo, ambapo amri ya Polisi ilitolewa kuwataka Waislamu waondoke kituoni hapo kwa madai kwamba shauri hilo linashughulikiwa. Maelezo hayo ambayo, umma wa Kiislamu uliokuwepo, walichukulia kama amri hiyo ni muendelezo uleule wa urasimu wa kituo cha Polisi cha Chamazi, kwa maana Waislamu walikosa imani kwa jeshi la Polisi. Alisema. Ponda alisema, Jumuiya na Taaisi zimesikitishwa na hatua ya jeshi la Polisi kuwapiga Waislamu ambao walikuwa Misikitini wakiendelea na Ibada zao. Alisema, vurugu hizo ziliibuka siku ambayo Wa i s l a m u h u k u s a n y i k a katika Misikiti maalum, kwa ajili ya Ibada ya Ijumaa, cha kusikitisha alisema ni pale Polisi walipoa anza kuzingira misikiti hiyo kuanzia majira ya saa nne asubuhi na kuwatia hofu Waislamu. Alisema, ilipofika majira ya saa sita mchana, baadhi ya Misikiti ilianza kushambuliwa kwa mabomu, ukiwemo Masjidi Salama, unaoongozwa na Sheikh Kingo, Sheikh wa Bakwata, Wilaya, ambapo wastani wa mabomu sita yalipigwa na kusababisha madhara kwa Waumini waliokuwemo ndani. Katika hatua nyingine, Jumuiya za Kiislamu zimeshangazwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete, kuyatembelea Makanisa na kulaani uharibifu katika makanisa hayo, huku akipiga kimya kitendo cha Polisi kupiga Waislamu waliokuwa wakiswali Ijumaa. Alisema, hawaungi mkono uharibifu wa Makanisa hayo, sambamba na kukanusha k u w a Wa i s l a m u n d i o waliofanya uharibifu huo, lakini siku tatu kabla ya ziara ya Rais kwa Makanisa hayo, tayari kulikuwa na tukio zito la Mkristo, kukojolea Kitabu Kitakatifu cha Waislamu Duniani, Al-Qur an Kariim, lakini alidai Rais , hili halikumshughulisha. Lakini pia alisema, vurugu hizo zimesababisha uharifu wa Misikiti kwa kupigwa mabomu na Polisi, na kujeruhi Waislamu, akitolea mfano Masjidi Hijra, ulio mita 3 toka lilipo Kanisa alililoka Rais Kikwete, ambapo ndani ya msikiti huo, makapeti yameloa damu na kuungua kwa mabomu yaliyorushwa na polisi.

AN-NUUR

kulalamikia vitendo vya kiudhalilishaji dhidi ya dini yao, yamepelekea kuzuka kwa vurugu kubwa alisema Ust. Ally Yaqub, kwa njia ya simu, akionyesha hatari inayosababishwa na serikali pamoja na vyombo vyake vya dola kushindwa kusimama katika haki na uadilifu katika utendaji wake. Muislamu mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema, baada ya kumkabidhi Emannuel, katika kituo cha Polisi, siku ya Alhamisi, wao (Waislamu) waliendelea kufuatilia kwa karibu suala hilo, lakini alidai waliona dalili za kutaka kupindishwa kwa sheria katika kituo kidogo cha Polisi cha Chamanzi. Imedaiwa kuwa baada ya viongozi wa Kiislamu kulipeleka suala hilo kituo hicho cha Polisi, kwa lengo la kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya kijana huyo, inadaiwa wazazi wa Emmanuel walikuwa wakifanya juhudi za kulisha suala hilo kwa njia za rushwa jambo lililozusha hasira kubwa kwa Waislamu. K u o n a Wa i s l a m u wamebaini njama hizo, Polisi wakamtoa yule mtuhumiwa alfajiri (Ijumaa) na kumpeleka Mbagala katika kituo kikubwa cha Polisi cha Maturubai, alisema Muumini mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Aboubakar Alli, mkazi wa Chamazi. Kuhamishwa kwa kijana huyo kulipelekea Waislamu wa eneo hilo kupeana taarifa na hatimae waliamua kwenda katika kituo hicho ili kujua hatua zitakazoweza kuchukuliwa na Jeshi hilo dhidi ya mtuhumiwa huyo ambaye awali kulikuwa na kila dalili za kutaka kuachiwa. Waumini hao walika kwa wingi kituoni hapo, majira ya asubuhi, siku ya Ijumaa, iliyopita ambapo Polisi walianza kuwatawanya kwa kufyatua mabomu ya machozi kitu kilichopelekea kuamsha hasira za waumini hao huku wakijiuliza sababu za kutawanywa kwa mabomu. Hali ilikuwa mbaya zaidi majira ya saa 8:00 mchana muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa ibada ya swala ya Ijumaa ambapo sasa taarifa zilienea karibu Jiji zima la Dar es Salaam, na miongoni mwao walika kituoni hapo ili kujua hatima ya wenzi wao ambao walianza kukamatwa nyakati za asubuhi pamoja na mtuhumiwa wao. Polisi walikuwa wakipiga watu ovyo, wakikuta watu wanakwenda Msikitini wanawapiga, mahali pengine

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (kushoto) akionyesha kirungu cha polisi kwa waandishi wa habari kilichokutwa ndani ya Msikiti katika vurugu zilizotokea Mbagala Ijumaa iliyopita.

wanaka watu wapo msikitini wanasubiri kuswali Ijumaa, wanawavurumisha kwa mabomu. Anasema shuhuda mmoja ambaye alidai kuwa yeye ni miongoni mwa wale waliokosa Aljumaa baada ya kupigwa mabomu wakati wakielekea msikitini. Vurugu hizo ziliwastua baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu na kulazimika kufika kituoni hapo kwa lengo la kuzungumza na uongozi wa Jeshi la Polisi ili kurejesha hali ya amani katika eneo hilo. Baadhi ya viongozi waliofika kituoni hapo ni Amir wa Baraza Kuu la Taasisi na Jumuiya za Kiislamu (T) Wilaya ya Temeke Sheikh Farid Saleh, Sheikh wa Bakwata Wilaya ya Temeke Mohammed Mshindo Kingo. Baba mzazi wa Zakaria, aliendelea kumwambia mwandishi wa habari hizi kuwa, kutokana na tukio hilo alilazimika kwenda kwa wazazi wa Emmanuel na kisha kwenda kwa mjumbe ambaye aliwaelekeza kwenda kituo cha polisi kuandikisha maelezo. Akiongea na waandishi wa habari, Jumanne wiki hii katika Hoteli ya Lamada, Ilala, Jijini dar es Salaam, kufuatia

Mbagala sawa Mwembechai


kadhia hiyo, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema wanalaani kitendo cha kunajisiwa Qur an Tukufu ambayo ni Kitabu kitakatifu kwa Waislamu wote Duniani. Akizungumzia tukio hilo alisema, lilifanywa kwa makusudi na kijana Emannuel Josephat (14), pamoja na vijana wenzake kumtahadharisha. Sheikh Ponda, alisema Kijana Emannuel aliingilia maongezi ambayo yalikuwa yakimuhusu kijana Deo Novele, na Zakaria Khamisi ambapo (Deo) alikuwa akidadisi kama mwezeke (Zakaria) anaweza kusoma heru za Qur an. Alsema, Emanuel, aliyekuwa kiasi mita 5 toka walipokuwa wenzie, ghaa alifika na kuanza kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Qur an na Waislamu kwa ujumla. Kwa mujibu wa vijana hao, walimnukuu Josephat, akisema Sisi nyumbani kwetu tunakijua kitabu hiki, ni kitabu cha Shetani, Waislamu wanafuga Majini na Qur ana yao ni kitabu cha mapepo. Kufuatia kauli hizo za Josephat, mmoja wa vijana waliokuwepo hapo akiitwa

Tawfiiq, alimuonya kwa maneno yake hayo, huku amkimwabia akifanya mchezo na Qur an atapata madhara. Hata hivyo inadaiwa kuwa, Emanuel alisema kwamba sasa anaitemea mate, kisha ataikojolea, ili aone nini kitatokea, mambo ambayo aliyatekeleza yote mawili kwa pamoja. Zakaria aliporudi nyumba kwa huzuni, mzazi wake wa kike alitumia maji kupunguza athari za mkojo katika Qur an na hatimae baba yake alipeleka suala hilo kwa Mjumbe kisha kuka katika kituo kidogo cha Polisi cha Chamazi. Alisema Shekh Ponda. Alisema, pamoja na Wa i s l a m u k u l i c h u k u l i a kwa uzito, tukio hilo lakini liliendelea kusuasua katika kituo hicho, mpaka Oktoba 12, 2012, lilipohamishiwa katika kituo cha Maturubai, Mbagala. Sheikh Ponda alisema, Waislamu wanawake, vijana na Wazee walilazimika kuka kwa wingi katika kituo cha Polisi cha maturubai, ili kuona haki ya kufikishwa Mahakamani mtuhumiwa inatendeka. Ponda alisema, Wakuu wa Polisi wa mkoa wa Polisi

EWE Allah ifanye historia ya maisha kuwa somo kwa viumbe. Ewe Allah utie nguvu Uislamu kwa mmoja kati ya watu wawili; Amar bin Hisham (Abu Jahl) au Umar bin Khattab. Mtume (s.a.w.) aliomba. (Bakhari na Huslim). Mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini na saba, akiwa na upanga mkononi mwake, mwenye mwili mkubwa wenye nguvu na harara ya ghadhabu, alitoka nje ya nyumba yake kuungamiza Uislamu kwa kummaliza muasisi wa Uislamu, Mtume Mtukufu (s.a.w.). Hata hivyo, haikudhamiriwa kuwa hivyo. Mtume Mtukufu (s.a.w.) aliomba mwongozo kwa mtu huyo huyo. Mtu huyo alikuwa Umar (r.a.) ambaye majaaliwa yake yalikuwa muhimu na uongozi katika kusimamisha Uislamu. Alipokuwa njiani, na upanga usio na ala mikononi mwake akitembea kwa hatua ndefu zenye nguvu, alisimamishwa na Muislamu, Noim bin Abdallah (r.a.) aliye msaili juu ya ghadhabu (hasira) yake. Baada ya kuelezwa dhamira yake, Noim (r.a.) alimshauri Umar (r.a.) badala ya kuwa na matarajio makubwa, aisafishe nyumba yake kwanza, kwani dada na shemejiye walishasilimu. Baada ya kusikia hayo, Umar (r.a.) alielekea nyumbani kwa dada yake, alipofika alisikia Q u r ani ik is o mw a n d an i. Umar alimvaa shemeji yake na akaanza kumshambulia. Dada yake aliingilia kati na alisukumwa pembeni kwa nguvu kiasi cha kujeruhiwa kichwani, na kuvuja damu nyingi. Aliinuka na kumwambia Umar bila wasiwasi, Ewe Umar fanya unyama wako. Hatuto acha Uislamu. Aliposikia hivyo, alilazimisha ayah ile ya Qurani asomewe. Aliposikia Ayah ile; Qurani, TAHA: 14, Hakika mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana Mungu ila mimi tu. Basi niabuduni Mimi, na ushike sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi. Akili zake zilimrejea. Aliomba kumwona Mtume (s.a.w.). Aliongozana na Khabbab (r.a.) kwenda kumwona Mtume (s.a.w.) ambapo alieleza azma yake ya kusilimu. Sauti za Allahu Akbar zilishangilia maneno yale. Hili lilijiri mwaka wa sita wa Utume. Mpaka leo, Uislamu unakabiliwa na uhasama kutoka kwa Maquraish, ulikuwa na wafuasi hamsini na mmoja tu. Walikuwa bado wakichukua tahadhari kiasi cha kusali kwa kicho. Kusilimu kwa Umar kulibadili kabisa hali iliyo kuwepo. Kwa wasifu wa ujasiri wake na ushajaa wake, alitangaza hadharani kusilimu kwake, aliswali ndani ya Kaaba na alipambana na upinzani wa Maquraish. Kwa kutangaza hadharani imani yake, alipewa cheo cha FAROOQ na Mtume

AMIRUL MUMINIIN SAYYIDINA UMAR AL-FAROOQ (R.A.)

Makala/Habari

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

(s.a.w.). Maisha yake ya Mwanzo: Katika maisha yake ya mwanzo, Umar (r.a.) alikuwa akichunga ngamia, alipo baleghe, alitumia muda wake wa mapumziko kujifunza mchezo wa mieleka, kupanda farasi, ufundi wa kushindana kwa vitara, (fencing) ufasaha wa kusema na elimu ya nasaba. Alikuwa maarufu kwa uhodari wake wa mieleka. Aidha alikuwa mpandaji hodari na farasi na aliweza kumpanda farasi bila ya kikuku (cha kupandia farasi) na bila shogi. Alikuwa mmoja wa Maquraish kumi na saba waliojua kusoma na kuandika. Katika ujana wake, Umar (r.a.) alisari sana nchini Syria na Iran kwa ajili ya biashara zake. Kwa sababu hiyo alikuwa mtu maarufu na Maquraish walimteua kuwa Balozi wao kila kulipotokea sintofahamu na makabila mengine. Nimesilimu na ninataka kuweka wazi kuwa kuanzia leo na kuendelea nguvu zangu zote zitatumika kwa ajili ya ufanifu na ushindi. (Umar(r.a.). Kusilimu mpaka Ukhalifa: Jina la Al-Farooq (anaye leta mabadiliko) linaashiria kuwa, kusilimu kwa Umar (r.a.) kulileta mabadiliko makubwa kwenye fikra za Waislamu. Hata hivyo, walikuwapo watu 51 tu waliorejea na wengi wao hawakudhihirisha Uislamu wao. Kitendo cha kwanza cha Umar (r.a.) baada ya kusilimu kilikuwa kwenda na kuswali ndani ya Kaaba bila kificho, akikataa katakata kuzuiwa na yeyote. Hapana aliyethubutu. Alitangaza wazi imani yake, aliwaita Machifu wote wa Makkah na kuwaeleza mabadiliko yaliyo mpitia. Hapana aliyethubutu kusema neno, hata hivyo walikuwa na uchungu wa

Waislamu kuingia ndani ya Kaaba na kusali jamaa. Hii ilikuwa swala ya kipekee ndani ya Kaaba: Alimshauri Mtume (s.a.w.) kuanza njia ya kuwaita waumini kwenye swala ya jamaa kwa kuadhini kwa sauti kubwa. Mtume (s.a.w.) aliridhia. Wa k a t i w a H i j r a , hakuondoka kwa kificho kama watu wengine. Alifanya Tawaaf ya Kaaba na kisha akiwambia mapagani juu ya nia yake ya kuhamia Madina, na aliwakaribisha kupambana naye kama walitaka watoto wao kuwa mayatima na wake zao kuwa wajane. Katika kutetea njia ya Uislamu, hapakuwa na mhanga uliokuwa mkubwa. Katika uhai wa Mtume (s.a.w.) alishiriki kwa ari kwenye vita vyake ambavyo Uislamu ulikabiliwa na alionyesha ushujaa wake. Zaidi ya ushiriki wake wa hali katika vita, pia alitoa mchango mkubwa wa mali yake katika vita. Masoud (r.a.) anasema, Kusilimu kwa Umar ulikuwa ushindi kwa Uislamu; kuhajiri kwake kulieneza ufanisi wake na ukhalifa wake ulikuwa ukarimu. (Al-Hadithi). Ukhalifa: Mnamo mwaka 13 A.H., Abubakar (r.a.) aliugua, na ilipofahamika kuwa maisha yake yalikaribia ukingoni, alikabiliwa na jukumu zito la kumchagua mrithi wake. Alimteua Umar

kumpoteza mtu hodari. Kilichofuatia ni kuwaongoza

(r.a.) kama kiongozi badala yake alisema: Ndugu zangu katika Imani, sijamteua yeyote miongoni mwa ndugu zangu (wa damu) au jamaa zangu kuwa Khalifa. Nimemteua mtu ambaye anafaa miongoni mwenu. Je. Mnamthibtisha? Bila shaka, ndiyo.

Kahalifa. Kuenea kwa Uislamu chini ya Umar Al-Farooq (r.a.): Wakati wa Mtume (s.a.w.) Uislamu ulienea sehemu za mbali ya Arabia. Kabla ya ustawi wake, Mtume (s.a.w.) alifariki dunia. Abubakar (r.a.) Khalifa wa kwanza aliimarisha dola Arabia lakini kabla ya kueneza dola iliyo madhubuti Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uajemi na sehemu ya Ulaya, naye aliondoka kukutana na Muumba wake. Hata hivyo nia ya upanuzi wa baadaye ilikuwa wazi Umar aliachiwa kumalizia utekaji wa shehemu zilizo salia. Syria ilikuwa ya kwanza kushuhudia mapambano ya kijeshi. Yakifanywa na Byzantines. Hawa kufikiria kuwa mpaka sasa jeshi lisilojulikana lingeweza kuwatoa nje ya himaya yao. Chini ya uongozi wa Khalid bin Walid (r.a.), Damascus ilizingirwa na ilibidi isalimu amri baada ya kuzingirwa kwa lengo la kutawaliwa kwa miezi sita. Madhila dhidi ya Waislamu yalikuwa makubwa lakini walifanikiwa kuangusha

Walipiga kelele hadhara iliyokuwepo pale. Huu ulikuwa uchaguzi wa Umar kuwa

utawala wa Damascus, baada ya hapo miji ilianza kuanguka na kisha Syria yote, Palestine na Jordan zilifuata na kuwa chini ya Waislamu. Baada ya mfululizo wa m a p a m b a n o , Wa i s l a m u wakiongozwa na Khalid bin Walid, Mothanna, Abu Abeid na mwisho Saad bin Abi Waqaas (r.a.) jeshi kubwa la Uajemi lilipigwa hapo Cadesiya, mwaka 21 (A.H.) na ardhi yote yenye rutuba ya Iraq Magharibi mwa Tigris ilikuwa chini ya Dola ya Kiislamu. Mfalme wa Uajemi na vikosi vyake walikimbia Jiji lao kuu bila mapigano na Waislamu waliingia kwa ushindi miji mikubwa ya kifalme barani Asia. Kasri nyeupe ilitwaliwa na Waislamu na utajiri wake usio fahamika ulichukuliwa. Hili lilikuwa limekwisha bashiriwa na Mtume (s.a.w.) miaka mingi iliyopita. Kikundi cha Waislamu kitateka Kasri Nyeupe ya Mfalme wa Iran. Kuelekea Kusini, kampeni mahiri ya jeshi la Waislamu chini ya Amr bin Aas (r.a.) waliiteka Misri yote. Walipoiteka Alexandria aliendelea kwenye Pwani ya Kaskazini ya Afrika mpaka ardhi ya Barbers Tripoli. Mafanikio haya ya Waislamu na kutwaa kwa haraka ardhi (nchi) za kistratejia kutoka kwa tawala imara, yaliupa utambuzi Ulimwengu kuwa ilikuwepo nguvu inayojitokeza ya Uislamu. kuwa zingeweza kwa wakati mmoja na kwa ufanifu, nguvu mbili kubwa za dunia kwenye mipaka miwili liliushangaza Ulimwengu. Mfanikio makuu ya majeshi ya Kiislamu yalitokana na ghera yao ya kidini, imani isiyo na mipaka katika njia yao, morali wa juu ya askari Waislamu, ni ujasiri mkubwa wa Makomando, usio na kifani. Juu ya yote kiongozi alikuwa mmoja wa Washindi, aliyepanga kampeni (mashambulizi)_ na mipango thabiti. Huyu ndiye Umar Al-Farooq (r.a.) Amirul Muminin. Kila pahali Waislamu walipopateka, walianzisha mtandao kamili wa Uongozi, Mahakama na Misikiti. Hapana yeyote aliyelazimishwa kuwa Muislamu. Hata hivyo, njia ya maisha ya viongozi wa Kiislamu, kwa mujibu na mafundisho ya Mtume (s.a.w.), yaliwavutia raia ambao sio Waislamu, ambao walisilimu kwa makundi. Sayyidina Umar (r.a.) aliwateua magavana wenye uwezo kutawala nchi alizozitwaa.

Habari/Tangazo

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

Inatoka Uk. 4 watulizane katika kulifuatilia suala la Sheikh Farid wasije wakazua balaa jingine litakaloirejesha Zanzibar miaka 30 nyuma. Alisema mchambuzi mmoja akihoa hatma ya Zanzibar inayoweza kusababishwa na kadhia hii. Uchambuzi na maoni haya umekuja kufuatia ghasia kubwa zilizotokea jijini Dar es Salaam na Zanzibar wiki hii ambapo watu kadhaa walikamatwa na bado wanashikiliwa na polisi huku wengine wakiwa washakishwa mahakamani. Kwa Dar es Salaam ghasia zilianza pale Waislamu walipotuhumu kuwa Polisi walikuwa wakitaka kumwachia kijana aliyedaiwa kukojolea Quran. Katika tukio hilo Ijumaa iliyopita, Polisi waliranda mitaani wakipiga mabomu Mbagala kiasi cha kuzuia watu kuswali Ijumaa. Kwa upande mwingine, ghasia ziliibuka juzi Jumatano baada ya kukamatwa Sheikh Ponda pamoja na Waislamu waliokuwa wamepiga kambi katika kiwanja cha Bakwata kinachodaiwa kuuzwa kwa mfanyabiashara. Baada ya habari za kukamatwa Ponda kuzagaa, b a a d h i y a Wa i s l a m u walikusanyika Polisi kutaka kujua hatma yake ambapo mkusanyiko huo ulitafsiriwa kuwa ni kutaka kumtoa kwa nguvu hali iliyopelekea Polisi kutawanya watu kwa mabomu na maji ya kuwasha. JESHI la Polisi limesema, linamshikilia Sheikh Ponda Issa Ponda kwa ajili ya mahojiano maalum kwa mujibu wa sheria kufuatia m a t u k i o y a Wa i s l a m u yaliyoibuka hivi karibuni Jijini Dar es Salam. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Jumatano wiki hii juu ya kukamatwa kwa Sheikh Ponda, Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Jijini Dar es Salam, Suleima Kova, amesema wamemkamata Ponda kwa mujibu wa sheria. Sisi hatuna ubaya na Sheikh Ponda, yeye anakabiliana na mambo ya kisheria tu, kama itabainika amevunja sheria, baada ya mahojiano na mwanasheria wa Serikali akaona hivyo atapelekwa Mahakamani na kama hakuna kosa ataachiwa. Alisema Kamanda Kova. Alipohojiwa kwamba Ponda, ambaye ni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za

Vita ya Msalaba yaja kwa nguvu


Kiislamu nchini, amekamatwa kwa kosa gani, kamanda Kova, alisema anahojiwa kwa mambo mengi likiwemo suala la Chuo cha Markazi, Changombe. Chanzo cha kukamatwa Sheikh Ponda, ni tukio la kuingia katika kiwanja cha Markazi Changombe, kile kiwanja ni halali kina hati sahihi na huwezi kwenda kuchukua kiwanja wakati wowote ule, ni vizuri ukafuata taratibu. Alifafanua Kamanda Kova. Sheikh Ponda Issa Ponda alikamatwa usiku wa Jumanne, kuamkia Jumatano wiki hii, akiwa katika Msikiti wa Tungi, Temeke Jijini Dar es Salaam. Taarifa za kukamatwa kwa Sheikh Ponda, zilianza kuenea kuanzia usiku huo, ambapo awali taarifa zilisema hajulikani alipo lakini baadaye ilibainika kuwa yupo katika kituo Kikuu cha Polisi. Kwa upande wa Zanzibar, ghasia zilizuka baada ya kuzagaa habari kuwa Sheikh Farid ametekwa na watu wasiojulikana. Awali ilidhaniwa kuwa Sheikh Farid kakamatwa na Polisi, hata hivyo Polisi wamesema wao

VURUGU za Darajani Zanzibar juzi baada ya kupata habari kutoweka kwa Sheikh Farid Hadd. hawajamkamata na wenyewe akaipokea na kuongea na watu atamrudia. Hata hivyo alivyorudi kusema kuwa wanahangaika walioonekana kuwa katika kujua nini kimetokea. gari iliyokuwa imesimama si hakuliona tena lile gari wala Sheikh Farid. Habari zinasema kuwa mbali na pale walipokuwa. Sheikh Farid alitoka Baada ya kuzungumza Toka hiyo siku Jumanne nyumbani kwake na kijana kwa muda mfupi, Sheikh usiku hadi hivi sasa, Sheikh mmoja akiwa dereva kwenda alimwambia kijana wake Farid hajulikani alipo na kununua umeme. anunue umeme auwahishe simu yake aliyokuwa nayo Hata hivyo walipofika n y u m b a n i w a k a t i y e y e ikipigwa haipatikani. akashuka, simu yake iliita akiongea na watu wale halafu

MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO


P.O. BOX 1031 Morogoro, Tanzania. Tel: +255 23 2600256; Fax: +255 23 2600286 E-mail address:mum@mum.ac.tz

FIFTH GRADUATION CEREMONY FOR UNDERGRADUATE DEGREES CONFERMENT 2012


The fth graduation ceremony will be held at the campus of the Muslim University of Morogoro on SATURDAY, 17th November, 2012. The ceremony is expected to start at 2.00 pm and end at 4.30 pm. Students eligible to attend the ceremony are undergraduates who successfully completed their studies in 2012. Parents, relatives and guests of the students as well as interested members of the general public are welcome to attend the graduation ceremony. Guests are expected to dress modestly and decently. Lady guests attending the ceremony are advised to wear the hijab or any dress that does not expose the body other than the face, hands and feet. All eligible students are requested to attend the occasion, regardless of whether or not they bring guests. However, they must inform the ofce of DVC (Academic) of their intent to participate in the ceremony NOT LATER THAN 30th October, 2012. Preferably call or email by a phone call or by electronic mail. Academic costumes (gowns, hoods and caps) are available for hire by the graduands but they must be booked by at least 5th November 2012. The University cashiers ofce must receive from each of the participating students a total of Ts. 35,000 (Ts. 20,000 for hiring the costumes, Ts. 10,000 deposit security which is refundable, and Ts. 5,000 convocation fee). Graduands, who do not have academic costumes on, will not be allowed to participate in the Ceremony. Graduands are required to bear in mind that the hired gowns shall have to be returned after the ceremony. A heavy ne will be imposed in case the costumes are damaged, or not returned and/or in time. A hiring Contract Form will be provided for completion by those intending to hire the costumes. For the safety of all participants and their guests, close-up picture taking and video recording of the graduation ceremony is restricted. Pictures may be taken before and after the ceremony. REHEARSAL Since the rehearsal is an integral part of the ceremony, all graduands who wish to attend the graduation ceremony MUST attend the rehearsal which is scheduled on Saturday morning (17th November, 2012) at 8.30am at the graduation site. Failure to attend all rehearsals by students will result in immediate cancellation of their eligibility to participate in the graduation ceremony. Certicates and transcripts of the graduands will not be given at the ceremony. These can be received at another convenient day from the Ofce of the DVC (Academic) upon signing register books and presenting an ID card. DEPUTY VICE CHANCELLOR (ACADEMIC)

Polisi waharibu mali Markaz Changombe


Na Mwandishi Wetu KWA kuuza kiwanja cha Markaz Changombe, Mufti wa Bakwata amezika historia iliyotukuka ya Waislamu Tanzania. Historia ambayo kwa upande mmoja inawapa heshma Waislamu kwa kuwa watu wa kwanza nchini kutaka kuwa na Chuo Kikuu na kwa upande wa pili eneo hilo kuwa moja ya vielelezo vya hujuma waliyofanyiwa Waislamu na Mwalimu Nyerere. Wakati ukitizama kiwanja cha Markazi Changombe kinakupa kumbukizi kuwa hapo ilikuwa pawe na Chuo Kikuu cha kwanza binafsi nchini kikimilikiwa na Waislamu, kwa kizazi kijacho sasa eneo hilo litanasibishwa tu na Mpemba anayedaiwa kununua eneo hilo. Historia hiyo ya Waislamu itakuwa imekufa na ndio maana mfumokristo kwa kutumia polisi unahakikisha kuwa unatumia nguvu eneo hilo lisirudi mikononi mwa Waislamu maana ni nembo ya uharamia Nyerere aliowafanyia Waislamu. Amesema Mzee mmoja aliyeshiriki kujenga msikiti wa muda kabla ya kufurushwa na polisi. Chuo cha Kiislamu Markaz, ambacho ni kama madrasa tu hivi sasa, awali ilikuwa kiwe Chuo Kikuu cha Waislamu kikisomesha fani zote, lakini Mwalimu Nyerere akavuruga mradi huo uliokuwa chini ya East Africa Muslim Welfare Society (EAMWS) na kufadhiliwa na Rais wa Misri, Abdel Nasser. Baada ya kuhujumu mradi huo, Nyerere aliuwa EAMWS na kuunda Bakwata ambayo ndiyo hivi sasa inakamilisha mradi wa Nyerere wa kuvuruga Changombe ili kurahisisha zoezi la Maaskofu kumtakasa Nyerere na kumpa utakatifu. Baadhi ya taarifa za kuaminika zinasema kuwa hata wazo la kuuza Changombe ukiacha unaoweza kuitwa ufisadi au ulafi katika kuhujumu na kula mali za Waislamu, wazo la kuuza eneo hilo lilipenyezwa Bakwata na mawakala wa mfumokristo ili kufuta historia ya eneo hilo kama ambavyo wameweza kufuta historia ya wazee wa Kiislamu waliopigania Uislamu. Wa z e e w a K i i s l a m u waliozungumza na mwandishi wamemshangaa anayedaiwa kuwa Mpemba aliyenunua eneo hilo wakisema kuwa anajitafutia balaa ya kudumu kwani anaonekana kujali ubinafsi wake badala ya kuangalia masilahi ya Uislamu bila kujali kuwa mali anayojikusanyia anaweza kuiacha muda wowote akaenda Barzakh ambayo itakuwa ama kiwanja cha Pepo kwake au shimo la Jahannam. Wako wapi waliokuwa wakitumia malori ya Bakwata kubeba masanduku ya bia (pombe), yupo wapi Adam Nas s i b , k i m y a a ! wapo makaburini utadhani hawakuwahi kuwepo duniani. Alisema Mzee Juma Mputa. Katika tukio la juzi Jumanne, Polisi walivamia Chuo Cha Kiislamu na Zahanati cha Markazi, Changombe, kisha kuwapiga na kuwakamata Waislamu waliokuwamo humo, baada ya kuvunja nondo za geti na kuingia ndani. Imeelezwa kuwa, maafande hao walianza kurusha mabomu, ndani ya shule hiyo yaliyosababisha kuvunja vioo vya madirisha kisha kuingia katika Msikiti wa Chuo hicho na kuwatoa akinamama huku wakiwapiga. Katika tukio hilo lililofanyika usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki hii, baadhi ya wanafunzi waliofika katika Chuo hicho, mapema asubuhi walitandikwa makofi na Polisi na kuwataka waondoke eneo hilo. Mwafunzi wa Chuo hicho Hamisi Bakari alisema, yeye na mwenzake walikuwa wa mwanzo kuka chuoni hapo na baada ya kuka, walikuta askari Polisi wapatao mia moja na magari mengi katika eneo la Chuo Chao. Tulika mapema chuoni hapa, lakini tulishangaa kuona Polisi wengi sana, tukiwa tukielekea darasani, afande alituita, tulipoka alituuliza tumefuata nini, tukajibu sisi ni wanafunzi wa chuo hiki tumekuja kusoma, alitukebehi kuwa sisi ndio viherehere wa mwanzo, ghaa alitutandika mako na kutuambia haya ondokeni haraka katika eneo hili. Alisema mwanafunzi Hassan. Mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza Chuoni hapo alisema, hali hiyo ni ya kuhuzunisha kwani sasa wanakosa masomo kwa ajili ya uroho wa watu wa kutumia mali za Waislamu kinyemela. Mwanafunzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed H. Mohamed, alisema suala la kiwanja hicho cha Markazi linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu ambao utazingatia kunusuru haki ya Waislamu. Alisema, huko nyuma ni mengi yametokea kuhusu viwanja hivyo, mpaka kukia hapo ni kwamba Waislamu wameamua kunusuru eneo hilo, lakini alidai Serikali

HABARI

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

BALOZI mdogo wa Misri nchini Amri Hussein akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Kiislamu Markaz Chang'ombe baada ya polisi kuvamia chuoani hapo Jumatano ambapo Chuo hicho kimefungwa. inaingilia na kuwakingia watapumzika kuja Marakazi kifua wauzaji. mpaka sherehe za Idd zipite kama Bakwata wanaimani K a m a n d a w a P o l i s i , au hadi hapo amani itakapo haswa kuwa mali hiyo ni aliyetambulika kwa majina patikana kutokana na hali ya kwao, basi wana haki ya kufanya hivyo. Lakini ya P.T. Ngosingosi, aliwataka iliyopo sasa. Alisema, kutokana na kama ni mali ya Waislamu maosa wa Ubalozi wa Misri, walioka Chuoni hapo katika taarifa hiyo ya Mudiru, na Bakwata ni wasimamizi tukio hilo kwenda kituo cha naye aliwafikishia taarifa tu, basi wana makosa na polisi kufungua jalada kama h i y o w a n a f u n z i k u w a watakuwa masulu siku ya kuna uharibifu wowote, w a m e r u h u s i w a k u r e j e a kiama. Alisema. Ijumaa ya wiki iliyopita, makwao mpaka pale taarifa katika Chuo chao. itakapo tolewa rasmi, kwamba Waislamu Jijini Dar es Salaam, Jibu hilo, lilikuja baada waliingia katika Chuo Cha ya osa mmoja wa Ubalozi warudi tena shuleni. Alisema, katika mali zilizo Markazi Changombe, katika kuhoji sababu za Polisi kupiga mabomu, kuvunja vioo vya haribiwa ni madirisha ya eneo ambalo limeuzwa na madirisha ya Chuo, kutoweka vioo, viti kuvunjwa, ambapo BAKWATA. Akiongea mara baada kwa vifaa vya Zahanati na Kompyuta, spika ya Msikiti, emplifaya pamoja na jenereta ya kuingia katika viwanja vifaa vya Msikitini (Spika na hivyo Sheikh Ponda Issa havionekani. Emplifaya). Lakini pia kuna nyaraka ponda, alisema wapo hapo Sisi tupo hapo kwa ajili ya suala lile pale, (akionyesha na baadhi ya vitabu katika kwa ajili ya kutekeleza azma eneo lililouzwa na Bakwata) osi ya Mudiru vimechanwa, ya Waislamu kukomboa mali kama kuna lolote njoo Polisi kwa haraka haraka hiyo ndiyo zilizo uzwa na Bakwata. Wakiwa hapo Waislamu, katoe maelezo kisha utapata hali ya uharibifu tuliyoikuta. waliweza kusimamisha maelezo kamili, hapa siwezi Alisema. A l i s e m a , Wa i s l a m u M s i k i t i k a t i k a k i w a n j a kusema lolote. Alisema waliokuwamo katika kituo hicho, kwa matofali ujenzi Kamanda huo. Afande huyo alisema, hicho usiku wa kuamkia uliokamilika kwa muda t u k i o l i l i l o f a n y i k a n i Jumatano wamekamatwa mchache ambapo majira ya makosa, kwa kuwa lile na kupelekwa katika vituo alasiri, adhana ya swala ya eneo ni la mtu kihalali, na tofauti tofauti vya Polisi, na alasiri iliadhiniwa na kisha w a l i o i n g i a w a m e i n g i a hii ni baada ya kufatilia katika Waislamu kuswali. Waislamu hao waliamua kinyume cha sheria, hivyo kituo cha Polisi Changombe kuuita jina la Masjid Hassan na kuelezwa hivyo. alidai wamewakamata wote Akizungumzia hali ya eneo Bin Amir, huku wakisema waliokuwemo katika eneo hilo kwa ujumla, Amiri huyo wameamua kuupa jina hilo hilo, huku akidai waliwakuta wakiwa na mapanga na wa wanafunzi alisema, eneo Msikiti huo ili kumuenzi hilo lishauzwa na Bakwata Sheikh huyo aliyekuwa Mufti manati. Mubaraka A. Kaisi, Amir ambapo alidai alibaini hivyo wa Waislamu, na kuupigania Mkuu wa wanafunzi Markazi baada ya kufatilia kwa muda Uislamu, kwa dhati. Walisema, Al-marhum, C h a n g o m b e , a m e s e m a mrefu na kujua ukweli Mufti Hassan Bin Amir, ana halisi. kwamba Wanafunzi walikuja A l i s e m a , a l i p o h o j i historia kubwa kwa Waislamu kwa lengo la kuendelea na alielezwa kwamba Bakwata, nchini, kwani moja ya matunda masomo, lakini wakakuta hali si shwari hapa baada ya w a m e u z a k w a k i g e z o yake kwa Waislamu chini ya cha Katiba yao, ambayo Jumuiya ya EAMWS, ni kukuta askari wametanda. U s t . K a i s i a l i s e m a , alidai inawaruhusu kuuza, Chuo na eneo hilo la Markazi, aliitwa na Mudiru akiwa na kubinafsisha, au kupangisha ambapo palikuwa pajengwe Balozi wa Misri na kumpa chochote kilicho katika milki Chuo Kikuu cha kwanza cha Waislamu, mara baada ya taarifa kwamba kuanzia leo ya Bakwata. Kwa mtazamo wangu, Uhuru. (Jumatano wiki hii) wanafunzi

10

Makala

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

Na Khalid S Mtwangi WIKI iliyopita kulitokea fujo kubwa huko Mbagala na makanisa yaliyojirani yalishabuliwa na wananchi waliojawa na hasira. Polisi nao walifanya kazi yao kama ilivyo kawaida na waliweza kuwakamata wananchi takriban mia mbili. Bila shaka kati ya hao wamo waliohusika moja kwa moja na tukio hilo lakini pia inawezekana wamo waliopatwa na bahati mbaya ya kuwepo mahali hapo bila kukusudia. Hayo hutokea mara nyingi tu. Muhimu ni kuwa bila shaka jeshi la Polisi watakuwa makini na kutenda haki. Yaani watakaopelekwa kizimbani wawe wale tu waliohusika sio kuwabambikia kesi wasiohusika. Kutokana na malalamiko ya siku nyingi miongoni mwa jamii, mtu anaweza kusema kuwa haya nayo hutokea. Ili Polisi wasilaumiwe bila hoja za msingi ikubalike kuwa nao ni binadamu, huweza kufanya makosa bila kukusudia. Kufuatana na taarifa rasmi zilizotolewa, kadhia hii ilizuka baada ya kijana mmoja Mkristo kukojolea Kuran ambacho ni kitabu kitakatifu sana kwa Waislamu kisicho na mfano wake katika dini nyingi tofauti. Kwa mfano wakati Biblia iliandikwa na watu ambao wengine inasemekana walikuwa wafuasi wa anayeitwa Yesu Kristo, Kuran iliandikwa kufuatana na Wahayi kutoka kwa Allah Subhana wa Taala kupitia Jibril RA na kumkia Mtume Muhammad SAW. Pia ilipokewa na kuandikwa wakati Mtume mwenyewe, Rasulul-Llah yuko hai. Lakini Injili za huyu ama yule ziliandikwa wakati Yesu hayuko tena duniani. Kwa mfano inasemekana kuwa Injili ya John iliandikwa takriban miaka kati ya themanini na mia moja baada ya Yesu. Hivyo basi ikubalike kuwa Kuran ni kitabu cha aina yake. Ulaya wengi wametambua hivyo. Sasa

hata ilipofikia huyu kijana kukikojolea, hakika hilo si jambo la kawaida ambalo waumini wa Kiislamu wanaweza kulistahamili. Hii haina maana kuwa ilikuwa lazima kuvunja sheria za nchi kwani hata kama watu wasingeweza kustahimili zinaweza kuwepo hatua za kutekeleza katika mikondo ya sheria. Lakini kuna jambo moja ambalo linawakera sana Waislamu wengi pale kadhia kama hii inapotokea. Fujo ilipotokea kule Unguja na makanisa pia yakachomwa moto, Waislamu walilaaniwa na viongozi wengi wa serekali na wa dini zote, yaani Wakristo na Waislamu. Labda hilo ni sawa lakini hakukutokea hata kiongozi mmoja aliyejaribu kukumbusha kuwa labda kunaweza kuwa na sababu za msingi zilizosababisha haya kutokea. Kwa mfano kwa nini kunakuwa na uhasama kati ya dini hizi mbili. Lakini pia ilikuja kutambulika kuwa wengi wa hawa waliokamatwa Unguja kwa kujihusisha na ghasia zile walikuwa ni vijana wahuni tu wavuta bangi waliopata nafasi ya kujichangamsha. Ilitokea kuwa ni jambo la kusikitisha sana kwamba katika wale waliowalaani Waislamu katika kadhia hii walikuwemo masheikh wazito wa Kiislamu hasa wa kutoka Bara. Hivi kweli linaweza kuwa jambo jema kama hawa viongozi wa Kiislamu watatiwa katika kundi moja na viongozi wa Kikristo ambao wao walipata nafasi ya kuwalaani Waislamu sio tu kwa sababu ya kuchoma moto makanisa, bali pia walipata nafasi ya kutoa dukuduku lao lile la chuki waliyonayo juu ya Uislamu na Waislamu. Chuki hii ilijitokeza wazi kabisa katika matamshi ya kiongozi wa Kanisa la Anglikana. Hawa masheikh wangeweza kuwaasa Waislamu kwa njia ambayo wao isingewaweka katika kundi moja na wale maadui wa Uislamu na Waislamu. Uadui ambao unajulikana wazi kabisa katika nchi hii. Kiongozi mmoja niliyewahi kuzungumza naye wakati ule alikubaliana na mimi kuwa baadhi ya laana zilirushwa angani na baadhi ya masheikh hazikufaa kwa sababu the timing was wrong. Haukuwa muda muafaka kuungana na viongozi wa Kikristo

Al Had, kujipendekeza huku mpaka lini?

kuwalaani Waislamu. Sasa hebu itazamwe tena kadhia hii ya Mbagala. Kweli inawezekana kabisa kulikuwepo uvunjaji wa sheria na iliwabidi Polisi wafanye kazi yao kama inavyostahili. Lakini mpaka kuka hapo ni wazi kabisa kuwa hapa pana uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu ambao unataka kutazamwa kwa makini sana. Nampongeza Muheshimwa Mbatia Mb na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ambaye alidokeza kitu kama hicho alipozungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu tarehe 15 Agosti 2012. Mheshimiwa Mbatia alisema kuwa kuna haja kwa serikali kuliangalia suala hili kwa undani kwa sababu inavyoonekana uhusiano kati ya Waislamu na Wakristo sio mzuri. Sasa ni lazima huenda kuna sababu. Itafutwe sababu hiyo ili kuziba ufa tusije tukalazimika kujenga ukuta. Hii ilikuwa ni kinyume kabisa na hayo aliyoyasema Sheikh Al Had Salum, Sheikh Mkuu wa BAKWATA wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alilofanya Sheikh huyu ni kuwalaumu tu Waislamu wala hakukemea kile kitendo cha kukojolea Kuran, kitendo ambacho hata Rais Kikwete alitamka kuwa kilikuwa ni makosa. Sheikh Al Had yeye alipuuza kitendo hicho ati kwa sababu aliyefanya hivyo ni mtoto tu. Kwa vile yeye ni kiongozi kutoka BAKWATA maneno yake hayo hayawezi kustaajabisha hasa kwa vile alikuwa pamoja na Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi wakati alipopewa fursa ya kuwalaani Waislamu. B A K WAT A i n a w e z a kutafsiriwa kama ni jumuia ya Chama Cha Mapinduzi CCM. Hakuna uhakika kama, baada ya kuitwa na Serekali atoe tamko yeye akiwa kiongozi wa BAKWATA, alijaribu kuzungumza na Wa i s l a m u w a s e h e m u kulikotokea mkasa huo na kusikia wao Waislamu wanasema nini. Bila shaka wangeweza kumueleza kwa kirefu mkasa huo. Lau kama alipata nafasi hiyo na akazungumza nao basi hayo aliyoyatoa na kusikika katika television ni ya kusikitisha sana. Kwa sababu kwanza washuhuda walisema kuwa baada ya yule kijana kukojolea Kur an mama yake alishitakiwa kitendo hicho. Majibu ya mama huyo yalikuwa tu kwamba kitabu

SHEIKH Alhad Mussa hicho kinauzwa shilingi ngapi. Hiyo ilikuwa ni dharau ya hali ya juu sana ambayo kweli Waislamu walikuwa na haki ya kukasirika. Sheikh Al Had aliyafahamu hayo? Kwa nini asiulize mengi zaidi? Alijitokeza kijana mmoja aliyedai kuwa ni shuhuda ambaye alieleza maneno aliyoyasema kijana yule kabla hajaikojolea Kuran. Haya ni maneno ya dharau na kashfa ambayo hasa Wakristo kila siku huitukana Kuran. Ilipotokea kadhia huko Arusha hivi karibuni, maneno kama hayo kuhusu Kuran alitupiwa mama mmoja na askari polisi. Itakuwa ni aibu kubwa kama huyu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam hafahamu kiwango cha dharau waliyonayo Wakristo kwa Waislamu na Uislamu. Dharau hiyo sio tu wakubwa wanaizungumza mbele ya watoto, bali hakika ni sehemu ya mafundisho yao kanisani. Jaribu kuzungumza na wale waliokuwa Wakisto waliorejea baada ya kutambua ukweli uko wapi. Kwa hiyo itakuwa ni sahihi kabisa kama Muislamu aliye na upendo wa dini yake atasema kuwa kisa cha huyu kijana kukojolea Kur an kinatokana na ile dharau aliyoionyesha mama yake na ambayo ni sehemu ya mafundisho wanayopewa na mapadiri wao. Ni kweli lazima ikubalike kuwa wale waliochukua sheria mikononi mwao walifanya makosa makubwa. Lakini kweli ilikuwa vigumu kwa Sheikh huyu wa Bakwata, Al Had baada ya kuwalaani Waislamu kutamka kwamba ingekuwa vizuri na wazazi wa Kikristo, hakika Wakristo wote, kuonyesha heshima kwa Uislamu na wafuasi wa dini hiyo? Yeye maonyo yake yote, shutuma na makaripio yake, aliyalenga kwa Waislamu. Hakukuwa hata neno moja la kuwakanya Wakristo kwa kitendo kama alichofanya yule kijana na mama yake. H u y u n d i y e Wa i s l a m u Bakwata wameona anafaa kuwa kiongozi wao wa Mkoa! Ni msiba mkubwa!!! Ni jambo la kawaida kwa baadhi ya masheikh (masheikh maslahi) kujipendekeza sana kwa wale ambao wanaudharau Uislamu na wala hawathamini viongozi wa Kiislamu ila pale tu wanapotaka kuwatumia kufanikisha mambo yao. Masheikh wengi wanaogopa sana kushutumiwa kuwa WANA UDINI kiasi kwamba wako tayari kuwatosa Wa i s l a m u w e n z a o i l i wasishutumiwe kwa huo UDINI. Hivi haiwezekani kuwepo UDINI negative na positive? Kuna ubaya gani kuwa na UDINI POSITIVE ambao haumdhuru mtu yeyote awe Muislamu ama Mkristo. Kuran hairuhusu kuuhami Uislamu kwa njia yeyote ile? Haya ya kujipendekeza yatakwenda hivyo mpaka lini?

11

Tangazo

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Kwanza kwa shule zifuatazo: Mkuzo Islamic High School - (Songea) - BWENI TU. Kirinjiko Islamic Sec. School (Same) BWENI TU Nyasaka Islamic Sec.School (Mwanza) BWENI TU. Ubungo Islamic High School (Dar es Salaam) KUTWA NA BWENI

NAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA 2013

1. Shule hizi ni za Kiislamu, zenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi ya Kiislamu. 2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo: Elimu ya Dini ya Kiislamu, Usomaji Quran na mafunzo yake, Lugha ya Kiarabu, Kiswahili, English, Basic Mathematics, Physics, Chemistry, Biology, Geography, History, Civics, Book keeping na Commerce. 3. Patakuwa na mtihani tarehe 01/12/2012 saa 2:00 asubuhi katika vituo vilivyoorodheshwa kwenye fomu ya maombi. Muombaji anaweza kufanyia mtihani katika kituo chochote. 4. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11 /2012 5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini. 6. Pia, fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa atakayepata fomu kupitia tovuti (download) atatakiwa kulipia wakati wa kurejesha siku ya mtihani. Arusha Kilimanjaro Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni -0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Osi ya Islamic Education Panel - Mwanza -Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni-0714587193 Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA.-0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Osi ya Islamic Ed.Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin-0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Osis ya Islamic Ed. Panel karibu Nuru snack Hotel-0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.ss 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU0715 68 1 701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole-0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul Fallah: 0777125074Osi ya ust.Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627 USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA! MKURUGENZI WABILLAH TAWFIIQ

Dar es Salaam Morogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Maa -

12
SIKU YA ARAFA HIYOO !
ARAFA siku ADHIMU, i njiani yatujia, Twapaswa kuikirimu, kwa FUNGA kukusudia, Kuifunga ni muhimu, sikuyo ikiwadia, ARAFA IKO NJIANI, TUJIANDAE KUFUNGA. Ni letu sote jukumu, sikuyo kukumbushia, Kadhalika tujihimu, FUNGAYE kuipupia, SUNNAH hii ya msimu, si vyema kupuuzia, ARAFA IKO NJIANI, TUJIANDAE KUFUNGA. Haiko mbali fahamu, wikijayo zingatia, ALHAMISI muhimu, kufunga tutie nia, FUNGA hii ni ADHIMU, RASULI katuusia, ARAFA IKO NJIANI, TUJIANDAE KUFUNGA. Tumwa wetu muadhwamu, ashatuonesha njia, Kwa kuifunga SWAUMU, sikuyo lipowadia, Vipi tuone ugumu, kwa tumwa aloridhia, ARAFA IKO NJIANI, TUJIANDAE KUFUNGA. Kwa kweli yatulazimu, SIRAYE kushikilia, Kwa sururi si kwa ghamu, tusije iachilia, Tumtii MUADHWAMU, kwa mwendowe shikilia, ARAFA IKO NJIANI, TUJIANDAE KUFUNGA. Jandae dada Swaumu, nawe kaka Zakaria, Mwifunge hii SWAUMU, ujira kujipatia, Kesho siku ya hukumu, ije mizani jazia, ARAFA IKO NJIANI, TUJIANDAE KUFUNGA. Beti saba zimetimu, ARAFA kukumbushia, Aula na la muhimu, FUNGAYE sije achia, Nimetimiza jukumu, la FUNGA kukumbushia, ARAFA IKO NJIANI, TUJIANDAE KUFUNGA. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

Barua/Tangazo

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

UKWELI HAUFICHIKI

Salamu ya Rahmani,natamka ulimini Kuwasalimu Insani,walinzi wa yetu dini Washikao usukani,kuiimarisha dini Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Waisilamu nchini,nadhani mpo na mimi Sio kwamba hamuoni,yatamkwayo kwa ndimi Waso na haya usoni,wasemavyo kwa maghani Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Kukojolea Qurani,ni kosa kwa wenye dini Vyovyote awe Insani,ukubwani utotoni Sio kuleta utani,ukakuza tafrani Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Shekhe wao kabaini,kamtetea insani Asema yu swaghirani,na hana kosa jamani Hivyo msiwe vitani.alofanya ni utani Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Swali nakutupieni,juu ya hii kalami Ikitokea hadharani,kakojolea chakulani Atasema ni utani,hivyo basi muacheni Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Mfumo upo mwilini,ndo mana hujithamini Haingii akilini,tena kwa mtu msomi Kama jibu hubaini,basi ufunge ulimi Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Kukashifu Qurani,kwa makusudi moyoni Mtu atoa lisani,asema yaso thamani Awaridhishe Insani,wale wanomthamini Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Hivi mliwabaini,walosema TViini Maneno yao jamani,mwaona yanathamani Wamwogope manani,wtajachomwa motoni Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Sababu i machoni,immeminywa chinichini Ila athari hewani,kwa ushabiki wa dini Hivi ninyi hamuoni,kipi kilianza kwani Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Mabomu msikitini,na damu kumwagwa ndani Hilo ninyi hamuoni,kwa chuki zenu za dini Ila moto kanisani,imewadunga moyoni Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Haki basi itendeni,mfarijipo Insani Sio kuwaweka ndani,rumande ka hayawani Ila na ninyi jueni,mtatupwa kaburini Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Ukweli ukija ndani,usingie jazibani Hebu utafakarini,muubaini kwa ndani Kuweka watu mbaroni,hizo ni chuki za dini Uelekezapo kidole,nawe kitakurudia Mimi nipo safarini.naelekea mwishoni Nilipoketi vulini,hili nikalibaini Nikaona na nathamani,kuwapasheni wandani Safari yangu ni ngumu,inahitaji gharama

VIROBA MURUA
Kwa mahitaji ya viroba bora vipya kabisa kwa matumizi mbalimbali sasa unaweza kupata kwa bei ya jumla na rejareja kwa saizi zote kwa bei nafuu zaidi, kwa BANDO. Tupo mtaa wa Likoma na Pemba Kariakoo, Dar es Salaam (nyuma ya Msikiti wa Idrisa). Kwa mawasiliano zaidi wasiliana kwa simu: 0657 800999/0683 800999.

Jina: Rajabu Eliamini Msofe, Aina ya Mtihani ni CSEE, Mwaka wa Mtihani ni 2007 Namba ya mtihani S.24310023 Anwani 42 Utete / Ruji Namba ya Simu: 0759 677734, 0765 404370, 0714546064, 0767 546064 nimepotelewa na vyeti vya

Tangazo la kupotelewa na vyeti vya Shule

shule tarehe 22/08/2012 maeneo ya Stendi ya Mbagala Rangi tatu katika kituo cha Daladala majira ya saa tisa Alasiri vyeti hivyo vilikuwa katika begi la rangi nyeusi katika bengi hilo kulikuwa na Leving Certicate ya Sekondari ya Mabogino, Cheti cha kuzaliwa, Living ya Chuo cha Ualimu Krinjiko na Result Slep ya Ualimu Grade IIIA pamoja na Nguo.

13
Said Rajab HIJA ni miezi maalumu. Na anayekusudia kufanya Hijja katika (miezi) hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija. Na kheri yoyote mnayoifanya, Mwenyezi Mungu huijua. Na chukueni masurufu ya kutumia njiani. Na hakika masurufu bora ni yale yanayamfanya mtu asiombe. Na mcheni Mwenyezi Mungu enyi wenye akili Qur (3:197) Ndugu zangu, hivi sasa tupo katika masiku ya Hijja! Mwenyezi Mungu Mtukufu awalipe malipo mema wenzetu waliojaaliwa kufanya safari hii, na Insha-Allah atuwekee wepesi siye tulioshindwa kuifanya mwaka huu tuifanye kipindi kijacho. Hijja ni wajibu kutoka katika nguzo za Uislamu, ambapo malipo yake Mtume wa Mwenyezi Mungu ameyazungumzia. Abu Huraira (ra) amesimulia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu aliulizwa, Tendo gani ni jema zaidi? Alijibu, Kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Muulizaji akauliza tena, Lipi linafuatia kwa ubora? Akajibu, Kushiriki Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Muulizaji akauliza tena, Lipi linafuatia baada ya hapo? Akajibu, Kufanya Hijja Mabrur.(Bukhari) Abu Huraira (ra) amesimulia tena mahali pengine kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema, Yeyote anayefanya Hijja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na akajiepusha kukutana na mkewe na akaacha kutenda dhambi, basi atarudi kama vile amezaliwa upya (Bukhari). Kupitia makala hii, ningependa kuzungumzia kidogo baadhi ya mafunzo yanayoweza kupatikana kutoka kwenye Ibada ya Hijja kwa lengo la kukumbushana tu: 1- Umoja: Tukiuangalia Uislamu, tutaona kwamba Sheria na Kanuni zake nyingi zinazungumzia dhana ya umoja wa umma. Ibada ya Hijja ni moja ya Sheria na Kanuni hizo. Ni kipindi ambacho Waumini wanakusanyika kwa pamoja kumuabudu Mola wao, wakisoma Talbiya ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu amefundisha: Labbaika Allahumma labbaik, Labbaika la sharika Laka labbaik, Innal-hamda wan-nimata Laka walmulk, La sharika Laka. Tafsiri: Nimeitikia wito wako, Ee Mola wangu, Nimeitikia wito wako, Mimi

Makala

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

Mafunzo kutoka Ibada ya Hijja

ni mtiifu kwa amri zake, Huna Mshirika, Nimeitikia wito wako,Utukufu na Neema zote ni zako, Mamlaka yote ni Yako. Huna Mshirika Hakika katika mambo yanayostaajabisha sana kuhusu Hijja, hata kwa wasio Waislamu, ni ukweli kwamba watu wa rangi zote, Weusi kwa Weupe, watu wa kabila zote - kutoka Ulaya, Uturuki, Indonesia, Afrika; watu wa umri wote - vijana kwa wazee wameungana kumuabudu Mwenyezi Mungu na wote wako sawa mbele yake. Hijja inathibitisha dhana y a U m m a t u n Wa h i d a (Umma Mmoja) kwa vitendo. Waislamu kutoka kila kona ya dunia, ambao wanazungumza lugha tofauti na wana sura na muonekano tofauti, wote wanafanya vitendo vya wajibu kama kuzunguka Kaaba (Tawaf), kukimbia baina ya Safa na Marwa, kupiga vijiwe kwenye Jamarat na kuvaa Ihram. Hakika dhana ya Ummah mmoja uliounganika bila ya tofauti ya ukabila wa mipaka ya kitaifa ni dhana muhimu ya Uislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu wala msifarakane Qur(3:103) Barua iliyoandikwa na Al-Hajj Malik El-Shabazz, ambaye pia alijulikana kama Malcom X, wakati akiwa Makka katika Ibada ya Hijja, inazungumzia uzuri wa umoja na udugu wa Kiislamu. Huyu bwana alikuwa mpigania haki za watu weusi nchini Marekani ambao

walikuwa wakinyanyaswa n a k u d h a r a u l i w a . Ye y e mwenyewe alikuwa Mmarekani mweusi. Aliandika: Sijawahi kushuhudia ukarimu wa dhati na udugu wa kweli kama ulioonyeshwa na watu wa rangi zote na makabila yote hapa kwenye mji huu wa kale, ambao ni nyumbani kwa Ibrahim, Muhammad na Mitume wengine wote waliotajwa kwenye maandiko matakatifu. Kwa kipindi cha wiki nzima, Nimepigwa na butwaa na kukosa kauli kutokana na heshima iliyonizunguka iliyokuwa ikitolewa na watu wa rangi zote. Nimejaaliwa kuzuru mji Mtukufu wa Makkah, Nimezunguka Kaaba mara saba, nikiongozwa na kijana (Mutawaf) anayeitwa Muhammad, Nimekunywa maji kutoka kwenye kisima cha Zam Zam. Nimekimbia mara saba katika vilima vya Safa na Marwa. Nimeswali katika mji wa kale wa Mina, na Nimeswali katika mlima Arafat. Kulikuwa na makumi ya maelfu ya mahujaji, kutoka duniani kote. Walikuwa wa rangi zote, kuanzia wale wenye macho ya bluu na nywele za njano, mpaka Waafrika wenye ngozi nyeusi. Sote tulikuwa tukishiriki katika vitendo vile vile vya Ibada, tukionyesha umoja na udugu ambao uzoefu wangu nchini Marekani, ulinifanya niamini kwamba hauwezekani kuwepo kati ya watu weupe na wasio - weupe. Amerika inahitaji kufahamu Uislamu, kwa

sababu hii ni dini ambayo inafuta katika jamii yake tatizo la ubaguzi wa rangi. Katika kipindi changu chote katika Ulimwengu wa Waislamu, Nimekutana, Nimezungumza na hata kula na watu ambao nchini Marekani wangedhaniwa ni weupe - lakini kasumba ya uweupe imeondolewa kutoka kwenye kra zao na dini ya Uislamu. Sijawahi kuona katika maisha yangu udugu wa kweli ulioonyeshwa na watu wa rangi zote kwa pamoja, bila ya kuzingatia rangi zao. Unaweza kustushwa na maneno haya kutoka kwangu. Lakini katika Hijja hii, kile ambacho nimekiona na kujifunza, kimenilazimisha kupanga upya sehemu kubwa ya fikra nilizokuwa nazo awali, na kutupa baadhi ya mahitimisho yangu ya awali. Hii haikuwa ngumu sana kwangu. Licha ya misimamo yangu madhubuti, mara zote nimekuwa ni mtu anayejaribu kukabiliana na ukweli, na kukubali uhalisia wa maisha, k adr i u nav y ob ain is h w a na uzoefu au mafuhumu mapya. Mara zote nimekuwa nikiwacha kra zangu wazi, jambo ambalo ni muhimu katika kutafuta ukweli. Katika kipindi cha siku kumi na moja hapa kwenye Ulimwengu wa Waislamu, Nimekula kutoka sahani ile ile, kunywa kutoka glasi ile ile na kulala kwenye zulia lile lile - wakati tukiswali mbele ya Mungu yule yule - na ndugu zangu Waislamu, ambao macho yao yalikuwa bluu zaidi kuliko bluu, nywele zao zilikuwa njano zaidi

kuliko njano na ngozi zao zilikuwa nyeupe zaidi kuliko nyeupe. Na katika maneno na vitendo vya Waislamu weupe, Nilihisi uadilifu ule ule niliouhisi miongoni mwa Waislamu Weusi wa Nigeria, Sudan na Ghana. Wote tulikuwa ni ndugu wale wale - kwa sababu imani yao kwa Mungu mmoja imeondoa kabisa kasumba ya uweupe kutoka kwenye kra zao, uweupe kutoka kwenye tabia zao, na uweupe kutoka kwenye mienendo yao. Hiki kipande cha barua iliyoandikwa na Malcom X, kinatoka kwenye kitabu kinachozungumzia maisha yake (The Autobiography of Malcom X). Sheria na Kanuni za dini ya Kiislamu mara zote zinasisitiza umoja na upamoja na siyo utaifa wala ubinafsi. Kanuni za kuwajali majirani zako, kuwatembelea wagonjwa, kuwasaidia waumini na kuendeleza uhusiano baina ya ndugu na jamaa (Silat ar - rahm) inathibitisha ukweli huu. Utaifa ni dhana isiyokubalika katika Uislamu kwa sababu inawaunga watu katika umoja wa kifamilia, kikabila au rangi wakati Uislamu unawaunganisha watu katika misingi ya Aqeedah, yaani kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa maneno mengine, Uislamu unawaunganisha watu kiitikadi. Lakini pamoja na uzuri wote huu wa Uislamu katika kuunganisha watu, maadui wa Uislamu wanafanya kila linalowezekana kuvunja umoja na mshikamano wa Waislamu ulimwenguni kote. Maadui hawa wanafahamu vizuri kwamba umoja wa Waislamu ni tishio kwa maslahi yao. Waislamu hawawezi kutawaliwa, kunyanyaswa wala kukandamizwa iwapo watakuwa na umoja madhubuti wa Kiislamu. Mabeberu wa Magharibi walijua hili mapema na ndiyo maana waliwachochea Waarabu dhidi ya ndugu zao Waturuki kwa kuwatumia mawakala wao maarufu kama Lawrence wa Arabia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, akizungumza na Waziri wake Mkuu, muda mfupi kabla ya Vita Kuu ya Pili ya dunia alisema: We must put an end to anything which brings about Islamic Unity between the sons of the Muslims. As we Inaendelea Uk. 14

14
basi Mwenyezi Mungu ni tajiri hahitaji kwa viumbe ) na amesema vile vile (Natimizeni hija na umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu) na akasema (Kwa hakika safa na marua ni Miongoni mwa dalili za Mwenyezi Mungu na atakayehiji nyumba hii na akafanya umra hapana makosa kuizunguka hiyo safa na Marua. Na atakayeongezea ni bora kwani mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia anayemshukuru na ni mjuzi. Akaja mtume ambaye ni Mwepesi kutilia mkazo juu ya nguzo hii ya hija kwamba ni mara moja tuu katika umri ni pale aliposimama mbele ya watu akiwahutubia akasema:- enyi watu kwa hakika Mwenyezi Mungu amekulazimisheni

Makala

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012


alikuwa ni Mwanamke kwani yeye alikuwa ni Mwanamke mwenye mwendo mdogo na kamruhusu Mtume (S.A.W) kisha akasema mama wa Waumini Aisha (R.A) Kumwambia mtume Umemruhusu uliyemruhusu na hii haionyeshi isipokuwa ni msamaha wa Kiislamu na kuwa hii ni dini ya uwepesi haina uzito pia tukiangalia mawe yanayotupiwa Ibilisi yamesifiwa ukubwa wake uwe kama Changarawe ili itakapotokea Bahati mbaya na kumpiga mtu isimumize. Yote haya yanatafsiri juu ya uwepesi wa Dini ya Kuislamu na msamaha wake. Hakuna makosa wala taabu ni kama alivyosia Mwenyezi Mungu:(Hakufanya kwenu katika dini ugumu) (Hailazimishi Mwenyezi Mungu nafsi isipokuwa inaloliweza tuu) (anataka mwenyezi Mungu kwenu wepesi na wala hataki uzito) Ugumu, hongereni mahujaji katika Nyumba kongwe tukufu kwa Fadhila zake Mwenyezi Mungu kwetu pale mtakapomuomba anakujibuni na Mkitaka jambo anakupeni na Mukiomba msamaha anakubali na anawasameheni auulizwa Mtume (S.A.W) ni kazi gani bora ewe Mtume? Akasema (ni kuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake pakasemwa kisha nini? Akasema jihadi katika Dini ya Mwenyezi Mungu Pakasemwa kisha nini? Akasema:- Ni hija nzuri (iliyokubalika na akauliza mama wa waumini Aisha (R.A) tunaona jihadi ni kazi bora kwa nini sisi hatupigani. Akasema Mtume (S.A.W) (mnayonyinyi jihadi ambayo haina kupigana ndani yake nayo ni hija na Umra) tunamuomba Mwenyezi Mungu kwenda kuhiji katika Nyumba yake tukufu na Mwenyezi Mungu awawepesishie mahujaji wote) Aamini.

AN-NUUR

UWEPESI WA HIJA
Na DR. OSSAMA MAHMOUD ISMAIL HIJA ni nguzo kubwa miongoni mwa nguzo za Kiislamu Nguzo ambayo amelazimisha Mwenyezi Mungu kwa mtu mara moja katika Umri wake. Na mwenye kukanusha nguzo hii huyo ni kafiri. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu (Na amelazimisha M w en y ezi M u n g u w atu kwenda kuhiji katika Nyumba kongwe kwa Mwenye kuweza na kwa njia zake, na atakayekanusha kuhiji. Hivyo nendeni Hija. Wakauliza ni kila mwaka? Ewe mjumbe wa mwenyezi Mungu? Na akasimama Akrau bin Jabir ili amuulize mtume (S.A.W) lau ningesema ndio basi ingewajibishwa na wala msingeweza. Nguzo ya hija ni mara moja tuu katika umri hivyo yatekelezeni yale niliyokuachieni kwani waliangamia watu waliopita kabla yenu kwa wingi wa maswali yao na kuwakanusha mitume yao) basi kile nilichokuamrisheni fanyeni kiasi muwezavyo, na yale, niliyokukatazeni yaacheni) na hii inajulisha juu ya msamaha wa Uislamu na uwepesi wake pale mtume (S.A.W) alipowafundisha umma wake ambao ni mdhaifu wawe ni wakubwa au wadogo na masikini ambao hawamiliki mali ya kwenda hija kila mwaka. Hivyo hai kufaradhishwa hija isipokuwa mara moja juu katika umri. Na laiti tukitazama matendo ya hija na nguzo zake tunaona ni Rehema na upole tuu, kwa hakika hija ni siku ya mwezi tisa mfungo tatu na siku hii ni siku ya arafa wanasimama mahujaji tangu kuchomoza kwa jua hadi kuzama kwake. Kisha wanakwenda muzdalifa na hakuwa waliloamrishwa huko Muzdalifa isipokuwa kutekeleza swala mbili ya magharibi na isha tena kwa njia ya kukusanya na kupunguza. Kisha wameamrishwa baada ya hapo kulala hadi alfajiri na hakuamrisha Mtume (S.A.W) katika usiku huu kuamka na kuswali au kuomba dua au kusoma Qur-ani hii ni kwa ajili ya kuupunguzia Uma taabu. Kwani yeye anajua watu walisimama hii siku ya Arafa. na katika kuondoka toka Arafa kwenda Muzdalifa walipambana na taabu ya mwendo hivyo imependelewa kulala muda mrefu ili kupumzisha miili yao kutokana na taabu na kuchoka. Pia pale alipohama Mtume (S.A.W) toka Muzdalifa kwenda mina walikusanyika watu pembezoni mwake ili wamuulize yale wasiyoyajua na yale yaliyojicha kwao. Hakuna alilosema Mtume isipokuwa alisema (Fanyeni na wala hapana Makosa) na akasema kwa yule aliyetanguliza kutupa mawe kabla ya kuchinja na kwa yule aliyetanguliza kuchinja kabla ya kunyoa. Na pale alipohama Bi Sauda toka Arafa kwenda Muzdalifa na akaomba ruhusa kuondoka Muzdalifa kabla ya Alfajiri kwani yeye

Mafunzo kutoka Ibada ya Hijja


Inatoka Uk. 13

have already succeeded in nishing off the Caliphate, so we must ensure that there will never arise again unity for the Muslims, whether it be intellectual or cultural unity. Tafsiri: Lazima tuzuie kitu chochote kitakacholeta umoja wa Kiislamu kati ya watoto wa Waislamu. Kwa kuwa tumeshaimaliza dola ya Kiislamu, sasa lazima tuhakikishe kwamba hakutatokea tena umoja wa Waislamu, uwe umoja wa kikra au wa kiutamaduni. Mabeberu wa Magharibi, kama Uingereza na Marekani wanapenda kuwaona Waislamu duniani wakiwa wamegawanyika. Watawala vibaraka waliowekwa madarakani na mabeberu hao katika nchi za Waislamu, wanahamasisha zaidi fikra za utaifa, wimbo wa taifa, bendera ya taifa na siku kuu za kitaifa kama siku za uhuru. Kamwe hawaenezi kra za Kiislamu. 2- Kisa cha Nabii Ibrahim na utiifu wa Shariah ya Mwenyezi Mungu. Ningependa pia kutoa mafunzo yanayopatikana kutoka kwenye kisa cha Nabii Ibrahim (as) na mtoto wake Ismael (as). Tunakumbushana kisa hiki maarufu kwa sababu siku kuu ya Eid el Adha iko karibu. Mwenyezi Mungu anatufahamisha kuhusu kisa hiki ndani ya Quran:

Ee Mola wangu! Nipe (mtoto awe) miongoni mwa watenda mema. Ndipo tukampa habari njema ya (kuwa atapata) mtoto mpole. (Basi akapata. Naye ndiye Nabii Ismaili). Basi alipoka (makamu ya) kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ee mwanangu! Hakika nimeona katika ndoto ya kwamba ninakuchinja. Basi kiri, waonaje? Akasema: Ee baba yangu! Fanya unayoamrishwa, utanikuta Inshaallah miongoni mwa wanaosubiri. Basi wote wawili walipojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu), na akamlaza kifudifudi (amchinje).Pale pale tulimwita: Ewe Ibrahim: Umekwishasadikisha ndoto. (Usimchinje mwanao). Kwa yakini hivi ndivyo tunavyowalipa watendao mema Qur(37:100-105). Tukiangalia kisa hiki cha Nabii Ibrahim kwa makini na kutafakari kwa kina, tutaona kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuamrisha mja wake mwaminifu, Ibrahim kumchinja mtoto wake kipenzi wa pekee! Wote baba na mtoto walisalimu kikamilifu amri ya Mwenyezi Mungu bila ya kuhoji. Ibrahim hakutafuta sababu kwa nini Mwenyezi amempa amri ile, wala Ismail hakutaka kujua kwa sababu gani anatolewa kafara! Wote wamekubali maamuzi ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu walitambua kwamba yeye ndiye muumbaji na

lengo la kuumbwa kwao ni kumuabudu yeye tu. Funzo kubwa tunalopata hapa ni kutii amri za Mwenyezi Mungu bila kuhoji. Si lazima Mwenyezi Mungu aeleze sababu ya kutoa amri ile. Wajibu wa kumtii bado uko pale pale. Tunafahamu kwamba Mwenyezi Mungu amekataza mambo mengi tu, ikiwemo riba, uzinifu na kuwageuza makafiri kuwa wasiri wetu. Lazima tutii amri zote za Mwenyezi Mungu bila ya kutafuta vizingizio kwa kutumia akili zetu za kibinadamu. 3 - Idd. Kama Waislamu, tuna dini ya kipekee sana na pia tuna sherehe zetu wenyewe, yaani Idd mbili, Idd el Fitr na Eid el Adha. Hatupaswi kusherehekea siku kuu za makari kwa kuwa ni haramu. Kwa hakika, Siku Kuu ya Idd el Adha ni kipindi cha sherehe kwa Waislamu wa Ulimwengu mzima wanaokadiriwa kufikia bilioni 1.4. Ingawa tutachinja, tutaswali Swala ya Idd na kucheza na watoto wetu katika siku hii, mioyo na kra zetu havitatulia kutokana na mateso tunayopata Waislamu duniani kote. Chakula tunachokula siku hiyo, kitukumbushe pia madhila hayo. Wakati tukichinja wanyama asubuhi, tujenge kwenye akili zetu kwamba, kwa sababu ya Mwenyezi Mungu, ama tunaweza kuchinjwa au kuchinja!

BISMILLAHIR RAHMAN RAHIIM


Jina langu Selemani Mizora,umri wangu miaka sitini na saba (67)Ninawaomba Waislamu - waumini wenzangu wanisaidie mja wa Mungu nimeadhirika, kutokana na umri nilio nao sina nyumba -kiwanja - shamba. Ninaomba mnisaidie angalau nipate kibanda cha vyumba viwili nipate kujihifadhi. INSHAALLAH ALLAH KARIM, Kwa mawasiliano zaidi tumia No. 0653 187282 - 0765-359558 MZEE MIZORA.

15

HABARI

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

Waislamu wamesalitiwa-Ilunga
Inatoka Uk. 16

na Joseph Kasela Bantu, kisha kutambulishwa kwa wazee wa Dar es Salaam, kwa sababu Wazee hao muda huo, tayari walikuwa na Chama chao cha siasa, cha TAA. Viongozi hawa wa TAA, walimpokea kijana Nyerere, aliye Mkristo Mkatoliki, kutoka Butiama, Musoma. Tangu hapo Nyerere akawa mtoto wa Waislamu. Mshume Kiate, mbali ya kumlipa mshahara pia alitoa Nyumba yake nzima ili Nyerere akae. Alisema Ilunga. Alisema, Nyerere mwaka 1985, alikiri moyoni kwamba, alikuwa Mkristo peke yake na hakuwa na nyumba Dar es Salaam, isipokuwa ni zile za Waislamu wa TAA. Dossa Azizi, alinijia akaniambia Julius, wazee wanakuita, nimeenda nyumbani kwa Mzee Jumbe Tambaza, nikakuta kweli wazee wa Kiislamu watupu wananisubiri, wakaniambia tumekuita tufanye dua. Siku ya pili nafatwa tena naambiwa naitwa na Sheikh Ramia Bagamoyo. Alisema Sheikh Ilunga akinukuu maneno ya Julius Nyerere. Alisema, hutuba hiyo ambayo aliitoa Nyerere wakati anangatuka, imefungiwa na wala hakuna chombo cha habari kinairejea hotuba hiyo, kama zinavyorejewa zingine, ikiwa ni njama za kuficha ukweli na kuharibu historia. Sheikh Ilunga alisema kuwa, Mwalimu Nyerere akiwa Tabora, Waislamu wa mkoa huo akina Amina Bint Chande, walimpisha katika nyumba zao, huku akitumia gari ya Mzee Bilali Waikera, katika shughuli za kisiasa mkoani humo. Alisema, maisha yote ya Nyerere na harakati zote za Uhuru, alizifanya akiwa na Waislamu, ambapo kwa Jijini Dar es Salaa, gari ya kwanza ya TANU, ilitolewa na Marehem Dossa Azizi, akimkabidhi Nyerere, kwa ajili ya harakati za Siasa. Muda wote wa kupigania Uhuru usalama wa Nyerere ulikuwa chini ya Waislamu, hata kudiriki kuingia naye Kanisani katika ibada zake ili kumlinda (maana Maaskofu walikuwa wakitumikia wakoloni). Alisema Ilunga. Sheikh Ilunga aliwataja Bw. Yusuph Chembela na Rashid Salum Mpunga, ambao walikuwa walinzi wake katika mikoa ya Kusini, na hata kudiriki kuingia nae Kanisani kumlinda, lakini

alidai baada ya Uhuru, mwaka 1964, Nyerere, aliwatia kizuizini mwaka mmoja na miezi tisa. Alisema, Waislamu walitoa nafsi zao, mali zao yakiwemo majumba, magari kuzifanya k u w a m a l i z a TA N U , wakitegemea haki baada ya utawala wa mkoloni, lakini baada ya Uhuru na Nyerere kutengeneza Serikali, Waislamu wakasalitiwa. Alisema, leo Waislamu hawajulikani hata kama wapo ndani ya nchini hii, kwani hata pale Serikali inapopanga mambo yake pamoja na kudai kuwa yenyewe haina dini, lakini pia haijali kuwa miongoni mwa makundi ya raia wake Waislamu wamo. Waislamu leo wanaishi kama raia wa daraja la nne katika nchi ambayo kwa sehemu kubwa wazee wao wamejitolea mali na nafsi zao, lakini Serikali haijali kama wapo na kuwa ni kikwazo cha kuyaendea mambo yao hususani ya kiibada. Alisema Ilunga. Akirejea hoja ya Askofu Gamanywa aliye ongea na kituo cha TBC 1, siku chache kabla ya sensa, kufuatia msimamo wa Waislamu kutaka kipengele cha dini kiwemo, alidai kuwa barabara zikijengwa watatumia Waislamu na Wakristo, Ilunga alisema hoja sio nani atatumia barabara hizo, bali hoja ni kwamba huduma hizo zimeelekezwa katika maeneo yapi tokea nchi hii ipate Uhuru wake. Alisema, tatizo si barabara za Waislamu au za Wakristo, bali tatizo barabara za lami na huduma bora za miundo mbinu kwa muda mrefu zipo katika mikoa yenye Wakristo wengi na hili lipo wazi halihitaji darubini. Alisema, angalia mikoa ya Kigoma, Tabora na Kusini (Mtwara na Lindi), miaka yote hakuna barabara za uhakika, hakuna huduma bora kwa watu hao ambao wengi wao ni Waislamu, na huko kote, walikuwa bega kwa bega na Nyerere katika kupigania Uhuru, lakini alidai baada ya Uhuru wamesalitiwa. Alisema, hivi sasa miongoni mwa walipa kodi wakubwa nchini, ni Waislamu, lakini kodi hiyo ikishalipwa, sehemu kubwa huenda kuimarisha Taasisi za Kikristo, pamoja na kuimarisha Mfumokristo.

Inatoka Uk. 16 kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa wananchi. Alisema TAMPRO, kwa kushirikiana na taasisi raki ya Helping Hand ya nchini Marekani wamefanikiwa kupata msaada wa vifaa hivyo vya tiba pamoja na madawa. Akaongeza kuwa, mbali ya vifaa hivyo walivyovitoa kwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na taasisi ya mifupa ya MOI, pia wamegawa katika Zahanati ya Sotele iliyopo Mkuranga mkoani Pwani, vikundi vinavyotoa huduma

TAMPRO watoa misaada Muhimbili


za afya katika Wilaya ya Temeke, Kinondoni na Ilala Jijini Dar es Salaam, Tanga na Mwanza. TAMPRO ni taasisi ya wnataaluma wa Kiislamu, iliyoanzishwa na kusajiliwa rasmi na Serikali mwaka 1997 kwa lengo la kuisadia jamii nzima ya Watanzania katika maeneo kadhaa ya kijamii. Mpka sasa TAMPRO, imeanzisha na kuendesha vituo vya Afya na Zahanati iliyopo Jijini Mwanza, Shule ya sekondari Sotele iliyoko Mkuranga mkoani Pwani,

Sheikh Ilunga Hassan Kapungu, akiongea na Waislamu katika Msikiti wa Mtambani, Ijumaa ya wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam.

MSAADA WA UJENZI WA MSIKITI

kituo cha maendeleo ya ufundi kilichopo TemekeTungi ambacho kinaendesha mafunzo anuwai ya Ushonaji na Kompyuta. P i a TA M P R O k w a kushirikiana na Shirika la HEIFA INTARNATIONAL ina mradi wa Ngombe wa maziwa, Mbuzi na Kuku wa kienyeji huko Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, ambapo zaidi ya wananchi 150 wanafaidika na mradi huo unaokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi Milioni 100.

Waislamu wa Mbezi kwa Yufusu jijini Dar es Salaam wanaowaomba Waislamu wenzao kusaidia jitihada zao za ujenzi wa Msikiti. Msaada unaohitajika ni wa vifaa vya ujenzi na fedha. Kwa yeyote atakayetaka kufanya biashara na Mwenyezi Mungu anaweza kuchangia kupitia M-Pesa Namba 0757 375993 M/kiti au Tigo Pesa 0717 649313 au 0657 531367 Katibu . WABILLAH TAWFIIQ

16

AN-NUUR
16

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

AN-NUUR

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA OKTOBA 19 - 25, 2012

Waislamu wamesalitiwa-Ilunga
Na Bakari Mwakangwale WAISLAMU, wametakiwa kujipanga upya na kuendesha darsa za kuamshana kifikra ili kupata njia mbadala ya kujiletea maendeleo yao wenyewe. Hayo yamebainishwa na Sheikh Ilunga Hassan Kapungu, akiongea na Waislamu katika Msikiti wa Mtambani, Ijumaa ya wiki iliyopita, akizungumzia hali ya Waislamu wa Tanzania na changamoto za sasa. Alisema, maendeleo ya Waislamu yapo katika juhudi zao wenyewe, pamoja na kusalitiwa na hata kupata misukosuko ya mara kwa mara ndani na nje ya Uislamu. Sheikh Ilunga alifananisha hali ya Waislamu wa Tanzania na kisa cha Muamerika mmoja aliyepeleka kesi ya binti yake aliyebakwa katika Mahakama ya nchi hiyo,

Kumuenzi Mshume, Dossa, wamuige Amerigo


kisha ikamsaliti. Alisema, kisa hicho kilieza kuwa wabakaji wale walihukumiwa kifungo cha siku 3, ambapo Muamerika huyo, hakuridhika na alihisi kutotendewa haki. Alisema, Muamerika huyo aliyejulikana kwa jina la Amerigo Bonassera, aliiamini mno Serikali yake, Serikali ambayo, baada ya kujitolea mali zake na nafsi yake kuipigania na kuijenga dola yake ya Amerika, alitegemea itamtendea haki lakini badala yake ilimsaliti katika kutenda haki kwa mwanae. Leo Waislamu Tanzania, tunasema kama alivyosema Amerigo Bonasera, Tanzania imewasaliti Waislamu kama Amerika ilivyomsaliti rai wake aliyejitolea, mali na nafsi yake lakini ilimsaliti, na kusababisha Amerigo, kuamua kuitafuta haki kwa njia ingine. Alisema. Ilunga alisema ameleta kisa hicho kisha kuwataka Waislamu kujipanga na kuamshana kifikra kufatia historia yao nchini kuonyesha kuwa wazee wa Kiislamu walipigania Uhuru kwa kutoa mali na nafsi zao, wakitaraji kufaidi matunda ya Uhuru. Lakini badala yake tokea kupatika kwa Uhuru, Serikali zao kuanzia utawala wa awamu ya kwanza hadi sasa imekuwa haiwatendei haki Waislamu na kuonekana kama wao ni tatizo ndani ya nchi. Akimzungumzia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kama kinara wa Serikali ya Tanganyika kisha Tanzania, kwa kuwasaliti Waislamu nchini, pamoja na kujitolea mali zao, muda wao na kumlea (Nyerere) Jijini Dar es Salaam, alisema mwaka 1952, kwa mara ya kwanza Nyerere, anakutana na wazee wa Dar es Salaam, akina Jumbe Tambaza, Haidari Mwinyimvua, Sheikh Suleiman Takadir, akitokea Sekondari ya Pugu. Alisema, Nyerere, wakati huo akisomesha Pugu Sekondari, alichukuliwa
Inaendelea Uk. 15

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akipokea sehemu ya msaada kutoka kwa Amir wa TAMPOR, Ramadhan Mziya, Alhamisi iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Na Bakari Mwakangwale

TAMPRO watoa misaada Muhimbili


Serikali na sekta hizo ni kuzitaka sekta binafsi kuwa na ushirikiano wa karibu na Serikali katika kutoa huduma za afya. Imedhihirika kuwa, Serikali peke yake haina uwezo wa kugharimia mahitaji yote ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vinavyotakiwa katika hospitali hii ya Taifa na nyingine za mikoa, Wilaya, vituo vya afya na Zahanati. Hivyo wanapojitokeza wadau mbalimbali kusaidia utoaji wa huduma bora za afya kwa kuchangia vifaa na rasilimali nyingine, inakuwa ni faraja kubwa kwa Serikali, alisema Dk Mwinyi. Waziri huyo mwenye dhamana ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Serikali ya awamu ya nne, amewaagiza watendaji wa Hospitali ambako vifaa hivyo vitapelekwa kuwa waangalifu ili viweze kutumika muda mrefu. Nawaagiza watendaji wa hospitali kuwa, katika maeneo yote ambako vifaa hivyo vitapelekwa wahakikishe vinatumika kwa uangalifu mkubwa, alisema. Vifaa tiba ambavyo Waziri huyo alivipokea ni pamoja na vya upasuaji, katika Taasisi ya mifupa (MOI), vifaa vya dawa za usingizi, vifaa vya matibabu ya pua, koo, masikio, vifaa vya kuhudumia watoto pamoja na vifaa kwa ajili ya chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU). Naye Amir wa Jumuiya hiyo Ramadhan Mziya aliyekabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya taasisi hiyo alisema kuwa, ingawa TAMPRO siyo asasi inayojiendesha kwa faida (non- proft organization), lakini wameona ni vema wakaitikia wito wa Serikali wa kusaidia sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo hiyo ya afya. Mheshimiwa mgeni rasmi, tunafahamu kwamba, Serikali

JUMUIYA ya wanataaluma wa Kiislamu Tanzania ( TA M P R O ) , i m e t o a msaada wa vifaa vya tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 640, kwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Msaada huo umekabidhiwa kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Alli Mwinyi Alhamisi ya wiki iliyopita, hospitalini hapo na Amir wa TAMPRO, Bw. Ramadhani Mziya, akiambatana na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo. Akizungumza kwa niaba ya Serikali katika haa fupi ya makabidhiano hayo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hussein Alli Mwinyi, amezitaka sekta binafsi kufuata nyayo za TAMPRO, kwa kusaidia sekta ya afya. Alisema, kwa kuwa sera ya ushirikiano kati ya

yetu inajitahidi vilivyo katika kupeleka huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wake, hasa huduma za lazima kama afya na elimu, lakini pia tunafahamu uwezo mdogo wa Serikali yetu katika kugharamia huduma hizo kwa mamilioni ya Watanzania hivyo kuwa vigumu kutoa huduma hizo muhimu kwa wananchi wote. Vilevile tumesikia mara kwa mara viongozi wetu wakihimiza wananchi wenye uwezo na asasi za kijamii na kidini kusaidia juhudi hizi za Serikali kutoa huduma za jamii kwa wananchi, aliema Amir Mziya. Alisema, kwa kulifahamu hilo na kutambua wajibu wao katika kusaidia jamii, TA M P R O i m e k u w a ikijitahidi kila inapoweza na kwa kusaidiana na taasisi raki za ndani na nje ya nchi
Inaendelea Uk. 15

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like