You are on page 1of 12

Walitaka kuniuwa asema Sheikh Farid

ISSN 0856 - 3861 Na. 1022 SHABAN 1433, JUMANNE

JUNI 26-28, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Mwanamke ajitoa kufa akishikilia bendera Amwambia polisi ina jina la Allah nakufa nayo Aumizwa jicho, mguu anyimwa matibabu

Machinjio ya Waislamu Baraza la Mitihani haya

DKT. Joyce Ndalichako.

Ushauri kwa Ndalichako, Serikali Kuchoma kichaka cha wahujumu Vinginevyo ni kudumisha dhulma
miezi miwili baada ya walimu kusahihisha? Katika usahihishaji, wanakuwepo walimu wengi na kunakuwepo na uwazi na uhakiki. Katika hali hii ya watu wachache kujifungia mahali kwa siri, kutakuwa na uhakika gani kwamba majibu wanayokuja kutoka ndio yale yale yanayotokana na makisi walizotoa wasahihishaji? (Soma Uk. 2)

Jussa atoa darsa Yametimia. Askofu hatawanunia tena Polisi: Waislamu washushiwa kipigo kikali muhimu Barazani
Mwadini Suleiman Juma alipigwa na polisi katika eneo la Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja kabla ya kuka Donge kulikoandaliwa mkutano.

KUMKABIDHI mtu mmoja au kikundi cha watu matokeo yote ya nchi nzima kwenda kukaa nayo kwa muda mrefu bila kuyatangaza, ndio chanzo cha hujuma. Kwa nini matokeo hayatangazwi pale pale yanapomalizika kufanyiwa kazi? Baraza linafanya nini na matokeo kwa zaidi ya

Msikiti wavurumishiwa mabomu, wavunjwa vioo Wanawake wavuliwa shungi, wapigwa mabuti Watu Donge wataka kutolewa kifungoni Misri

Irudi Tanganyika, Zanzibar huru Muungano uwe wa kimkataba


Uk. 4

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

TAHARIRI/HABARI
uliopo kama ambavyo wana haki hiyo Watanganyika (Tanzania Bara). Ni kweli pia kuwa wananchi wa Zanzibar wana haki kutaka uhuru wa nchi yao na Dola yao yenye mamlaka kamili ndani ya Muungano. Kwamba Muungano uwe wa nchi mbili kila moja yenye uhuru na mamlaka yake (sovereignty) kamili ndio pawe na ushirikiano unaotowa haki sawa kwa nchi zote mbili. Hata hivyo, tunachosema ni kuwa pamoja na uhuru na haki hiyo, Wazanzibari watambue kuwa mfumo wa serikali mbili uliopo haunganganiwi kwa bahati mbaya tu au sio kwamba una masilahi makubwa ya kisiasa na kiuchumi kwa Zanzibar. Unanganganiwa kwa sababu ndio unaotakiwa na mfumokristo. Wakishatambua hilo, watambue pia nguvu ya mfumo huo. Zanzibar ina Rais wake ambaye huchaguliwa na wananchi wa Zanzibar na huapishwa kuwa ni Rais wa nchi inayoitwa Zanzibar. Lakini Rais huyo huyo wa nchi, huingia katika Baraza la Mawaziri la Tanzania akivaa gwanda la Mawaziri. Hata hivyo, serikali ya Zanzibar, Wazanzibari na Rais anayekuwa madarakani, hahisi tatizo. Anakula kiapo na kuhudhuria vikao. Sisi hatudhani anafanya hivyo kwa kuridhia. Anaangalia nguvu iliyompitisha kule Dodoma kugombea Urais na ikamsimamia hadi kuapishwa. Hiyo ndiyo nguvu na athari ya mfumo ulioshikilia Muungano huu. Labda tutaje mfano mwingine ulio wazi zaidi. Katika suala la OIC ambalo Mheshimiwa Mwakilishi Raza alilikumbusha Barazani hivi karibuni. Waziri wa

AN-NUUR
Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Mheshimiwa Benard Membe alishalitolea ufafanuzi Bungeni Dodoma kuwa halina tatizo. Kwamba baada ya serikali kulifanyia utati ilikuwa tayari kujiunga kwa sababu ya faida zake na kwamba halina tatizo lolote. Lakini mara tu baada ya kutoa msimamo huo rasmi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mheshimiwa aliitwa na Askofu wake Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo na kuambiwa marufuku OIC. Sasa ukitaka kugombana na Mheshimiwa Membe, mkumbushie juu ya ule msimamo wa serikali kwamba haina tatizo kujiunga na OIC! Hiyo ndiyo nguvu ya mfumokristo ulioshikilia Muungano huu ambao Uamsho (na Wazanzibari wengine) wanasema hawautaki.

S.L.P. 55105, Simu: Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

AN-NUUR

Sasa Unguja watafahamu alichosema Ustadh Ilunga


Ukitaka yakuke, uguse Muungano Ni kichaka ulikojicha mfumokristo
KATIKA makongamano juu ya hatari ya m f u m o k r i st o n c h i n i , mhadhiri Ustadh Ilunga Hassan Kapungu alikuwa akisema kuwa kwa Tanzania Bara, mtu akitaka yamke, auguse mfumokristo. Akirejea katika historia akaeleza yaliyomkuta Mufti Hassan Bin Ameir, Mzee Sheikh Suleiman Takadiri, Chifu Abdallah Said Fundikira, Bibi Titi Mohamed, Profesa Kighoma Ali Malima na wengine wengi. Katika ufafanuzi wake akasema kuwa kila aliyetaka kuhoji juu ya nafasi ya Kanisa nchini na kuonyesha jinsi mfumo uliopo unavyowabagua na kuwahujumu Waislamu na Uislamu huku ukilipendelea na kuliimarisha Kanisa; basi aliandamwa na kuangamizwa kwa visingizio mbalimbali. Kwa upande wa Zanzibar akasema kuwa inakuwa vigumu kwa Wazanzibari kuelewa habari ya mfumokristo kwa sababu takriban viongozi wote wa serikali na taasisi za Dola kama Polisi ni Waislamu, ni Wazanzibari, ni Ibn Ami. Hata hivyo akasema kuwa, pamoja na ukweli huo, bado mfumokristo upo Zanzibar unafanya kazi na ndio unaoendesha mambo. Na kwamba mfumo huo hufanya kazi kupitia muundo wa Muungano uliopo. Muungano umekuwa ndio kichaka ulikojificha mfumokristo na ni kwa kupitia Muungano kila Mzanzibari amedhibitiwa na mfumokristo. Akatahadharisha akisema kuwa kama mtu anataka kujua nguvu ya mfumokristo, kama mtu anataka yamfike, basi auguse Muungano. Kwamba mfumokristo hautakuwa tayari kuona Muungano ukitikiswa kwa sababu hiyo ni sawa na kuchoma kichaka ulikojicha mfumo huo. Wakati ule japo Ustadh Ilunga alitaja mfano wa yaliyomkuta Mzee Aboud Jumbe na wanasiasa wengne wa Zanzibar waliohoji mfumo wa Muungano uliopo, lakini darsa ilionekana kuwa ngumu kueleweka kwa wengi. Maadhali mihadhara ile ya Pemba na Unguja juu ya mfumokristo ilikuwa imerekodiwa katika CD na DVD, Wazanzibari wakiitizama na kuisikiliza sasa, wakizingatia haya yaliyotokea Mahonda na Donge, na jinsi Uamsho wanavyoandamwa hivi sasa kwa msimamo wao wa kukataa Muungano; huenda wakaelewa kile alichosema Ilunga. Na pengine wakielewa watajua ukubwa wa jambo wanalozungumzia na hivyo kuweka mikakati yao vizuri na kujiandaa vyema. Wajipime uzuri iwapo ubavu wanao. Suala la kupambana na mfumokristo, sio lele mama. Lisifanywe ngoma ya kitoto ambayo huwa kawaida yake haikeshi. Ni kweli Wazanzibari wana haki kuhoji juu ya mfumo wa Muungano

MAONI YETU

Matatizo makubwa Baraza la Mitihani


Na Ibn Rajab Abu Nasri

KWA mara ya kwanza nilipatwa na mshangao mkubwa kusikia kuwa ati mitihani ya wanafunzi wa shule za Kiislamu na pia za serikali na watu binafsi waliofanya mtihani wa Maarifa ya Uislamu (Islamic Knowledge) takriban wote w a k i w a n i Wa i s l a m u imekosewa. Habari hizi zilinijia wakati nikiwa siamini kuwa madai ya Wakuu wa Shule za Kiislamu kuwa wanapinga matokeo yale ni ya kweli. Imekuwa muda mrefu Wa i s l a m u w a m e k u w a wakilalamika nchi nzima kuwa wamekuwa wakinyimwa haki sawa za elimu na ajira hasa serikalini na kwenye mashirika yake. Kwa hiyo kutokana na ukweli huo, inajenga taswira ya kuamini baadhi ya malalamiko hata kama hayana uhusiano wa karibu. Imenitisha zaidi kusikia kuwa kilichotokea ni kosa la Asa anayeingiza hesabu hizo kwenye Komputa au tuseme mtu anayehusika na IT- (Information Technology) kugawanya matokeo kwa tatu badala ya mbili. Na baada ya hapo kilichofanyika ni kutoa majibu mengine

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa


haraka haraka bila ya kufanya tathmini ya kina kuhusiana na tatizo hili. Hali hii ya kutisha imenipa maswali mengi sana ya kuliuliza Baraza la Mitihani kuanzia usahihishaji wa mitihani husika na hadi utoaji wa matokeo yake. Ili kutaka kujua haswa hili linawezaje kutokea kwa mtu mmoja kuweza kuharibu mitihani yote ya nchi nzima bila Baraza kuhisi na kujua, hadi kutoa majibu yenye Inaendelea Uk. 4

AN-NUUR

Walitaka kuniuwa asema Sheikh Farid


Na Mwandishi Wetu
WASIWASI umetanda kuwa huenda kuna watu wanataka kumuuwa Sheikh Farid. Hiyo ni kutokana na kile kilichojiri hivi karibuni ambapo watu waliokuwa katika gari walifukuza gari yake na kuipiga risasi, lakini kwa bahati nzuri Sheikh alikuwa hayupo ndani ya gari hiyo. Wa k a t i h u o h u o , mwanamke mmoja aliyekuwa akishikilia bendera ya Uamsho yenye maandishi Laaila ha ilallah, ameshushiwa kipigo kikali na polisi alipokataa kuachia bendera hiyo. Huyo polisi mmoja alikuwa akinilazimisha nimpe bendera, nikamwambia mimi hii siitoi hata kama utaniuwa, basi bora nife nayo mkononi mwangu hii ina Lailaha ila llahsikupi akaendelea kunipiga kwa kile kirungu cha polisi alichokuwa nachoakanipiga tena nikaanguka chini na akanivuta bendera yangu tukawa tunanyanganyiana. Amesema Bi Riziki akiongea na mwandishi juzi. Bi Riziki Omar Chande (42) ni mmoja wa wanawake kadhaa waliojitokeza na kueleza jinsi walivyopigwa na kudhalilishwa na polisi. Riziki Omar Chande (42) mkaazi wa Mfenesini anasema kuwa baada ya kusikia kuna mhadhara Donge, yeye alitoka mapema na kwenda kupanda gari kuelekea Donge kama wenzake lakini baada ya kufika Mahonda jeshi la polisi lilisimamisha msafara na kuwataka watu wote warejee mjini. Hata hivyo anasema kuwa viongozi wa msafara waliwataka wasiondoke mpaka viongozi wakuu watakapoka. Ilikuwa ni katika muda huo huo Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake walika katika eneo la Mahonda na kutaka jeshi la polisi kuacha kuhatarisha amani kutokana na kitendo chao cha kuwazuiya watu waliokuwa wakielekea Donge kuhudhuria mkutano uliokuwa ufanyike katika Msikiti wa Donge. Hata hivyo badala ya kuwasikiliza na kujadiliana nao, polisi waliwafukuza kwa mabomu ya machozi

HABARI

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

GARI alilokuwemo Sheikh Farid Had likiwa na matundu ya risasi. na ndipo Masheikh hao walipoingia Msikitini. Taarifa kutoka eneo la tukio zinafahamisha kuwa polisi waliwafuata huko huko Msikitini kuwatawanya kwa mabomu ambapo Sheikh Farid na wenzake waliruka ukuta na kukimbia kwa miguu katika pori kutoka Mahonda kuelekea njia ya Mwangapwani. Huku nyuma, wakidhani Sheikh Farid yupo ndani ya gari alilokuja nalo, watu wasiofahamika walilifukuza gari hilo na kulipiga risasi ambapo lilipinduka na kuharibikia vibaya. Sijui kama walitaka kutuuwa au vipi, lakini bahati mimi sikuwemo katika ile gari ingawa wanadhani kwamba ile gari ni yangu, lakini niseme mimi ile gari sio yangu ila nilipewa kwa kutumia kwa ajili ya shughuli za kuendeleza hizi harakati zetu, alisema Sheikh Farid muda mfupi baada ya kurudi katika hekaheka hizo ambapo walifanya mhadhara wao Mbuyuni baada ya kutokufanikiwa kupenya kwenda Donge. Akielezea juu ya kilichomfika Bi Riziki anasema kuwa kwa vile alikuwa kashikilia bendera, ilikuwa rahisi kwake kufuatwa na polisi. Mimi nilikuwa nimekamata bendera yangu polisi alipokuja kunichukua akanikamata mkono ananipeleka kituoni alipoka mbele kuna polisi mwenzake akawambia unampeleka kituo kama Bi Harusi, mpige virungu, yule polisi akajibu kwa nini tumpige wakati amekubali kutii amri halali? Mwenzake akasema, haiwezekani hao hawana adabu lazima apigwe, yeye ndio akaanza kunipiga huku akinambia nimpe bendera yangu ya Uamsho mimi nikamwambia nipige lakini bedera yangu sikupi ndio akaendelea kunipiga na kunipiga, alisema Bi Riziki. Wakawa wanatuambia maneno ya ovyo kwamba tutakoma, kwa hivyo yule polisi mmoja akawa anaendelea kunipiga alipokuja polisi mwenzake akawambia unampigia nini huyo wakati yeye amekubali umpeleke kituoni ndipo waliponichukua na kunipiga tena. Riziki ambaye aliumia sehemu ya jicho baada ya kupigwa kibao na jicho lote kupiga wekundu, anasema kilichomshangaza ni kwamba kila kituo cha polisi alipokwenda alikataliwa kupewa barua ya kwenda kupata matibabu. Tunafanywa kama sio raia wa nchi hii tulipokwenda kituo walikataa kutupa barua wakati wanajua hatuwezi kutibiwa kama tumeumia mpaka tupate barua ya polisi, tulipotoka Mahonda tukaja mjini tulikwenda Kituo cha Polisi Mkunazini wakakataa kutupa kibali tukenda Malindi pia wakatwambia nyinyi nendeni tu huko huko hospitali wambieni madaktari kuwa mmepigwa na polisi hawakutupa. Bi Riziki ambaye aliumia mkono na jicho anasema hata walipokwenda hospitali walikataliwa kupewa tiba hadi watakapokwenda na barua ya polisi. Naye Hafsa Mohammed Mahfoudh (19) mkaazi wa Kinuni, Magogoni anasema katika zahma hizo watu wengi walikimbilia Msikitini na ndipo walipoona Polisi wakiingia Msikitini na kuwapiga wanawake na wanaume na kuwatoa nje huku wakitaka wanawake wote wavuliwe mashungi yao. Walikuwa wakisema maneno mabaya mabaya huku wakituvuta mashungi yetu wakitwambia tokeni hapa Waislamu, Waislamu, Waislamu nini, wanafiki wakubwa, na kuna askari wa kike alinivuta sana shungi na kunipiga sana kwa

Inaendelea Uk. 7

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

MAKALA

AN-NUUR

Inatoka Uk. 4

Matatizo makubwa Baraza la Mitihani


na wakaguzi wasiopungua wawili na baada ya kuridhika wote, waalimu na wakaguzi hutia saini karatasi ya orodha hii na matokeo yote ya mitihani huwekwa katika ulinzi mkali na kukabidhiwa Msimamizi Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania. Pia Mkuu huyo anakabidhiwa na kuondoka na matokeo yote katika mtandao wa Komputa (Soft copy), ama ni kwenye Flash Disk au kwenye Lap top yake au ya Baraza. Baada ya kumaliza zoezi hili muhimu, majibu hayatangazwi mpaka mkuu huyu apeleke matokeo hayo makao makuu na huko hukaa kwa muda mrefu, miezi miwili kwa uchache. Sikupata maelezo ya kina kwa nini matokeo hayatangazwi pale pale yanapomalizika kufanyiwa kazi, na pia huko makao makuu nini kinaendelea kwa muda wote huo. Hili ni swali linahitaji majibu. Baraza linafanya nini na matokeo kwa zaidi ya miezi miwili baada ya walimu kusahihisha? Na yanapokuwa huko Barazani, yanakuwa mikononi mwa nani? Katika usahihishaji, wanakuwepo walimu wengi na kunakuwepo na uwazi na uhakiki. Huko Barazani, uwazi upo wapi? Uhakiki unahakikishwaje na unafanywa na nani? Katika hali hii ya watu wachache kujifungia mahali kwa siri, kutakuwa na uhakika gani kwamba majibu wanayokuja kutoa ndio yale yale yanayotokana na makisi waliyotoa wasahihishaji? Maelezo yote ya mtiririko wa taratibu hizo hayakunipa shida lakini maelezo haya ya mwisho yaliniacha na mshangao mkubwa ambao kwa mujimu wa yote yaliyojiri ya kukosewa matokeo, hapa ndiko lilikolala tatizo kubwa. Ni jambo la kushangaza sana taratibu hizi zinafanyika katika kipindi hiki ambacho tuko kwenye ulimwengu wa teknologia ya takwimu na program nyingi za kufanya mambo kwa uwazi, ufasaha na kwa haraka zaidi. Kumkabidhi mtu mmoja au kikindi cha watu matokeo yote ya nchi nzima kwenda kukaa nayo kwa muda mrefu bila kuyatangaza, kunaleta tafsiri mbali mbali zisizojibika na ndio chanzo cha matatizo yote yaliyotokea. Mtu mmoja ambaye amekabidhiwa dhamana nzito ya haki za wanafunzi kirahisi tu amefanya kosa linaloweza kuleta maafa makubwa na pia kusababisha Baraza zima kukosa imani na wananchi wote kwa ujumla. Inatisha zaidi kuona kuwa hata Bodi ilishindwa kugundua tatizo hili ambalo hata wachunguzi wa takwimu wamelielezea kuwa lilikuwa wazi mno kutokana na kufeli kwa kiwango kikubwa katika somo hili. Wengine wamehoji pia hata mwaka jana hali ilikuwa kama ya mwaka huu, ikimaanisha kuwa inawezekana kosa kama hili linaweza kuwa lilikuwepo. Mfumo huu wa Baraza ni wa hatari sana na sidhani kuwa Baraza limekosa washauri wa kitakwimu na kiteknologia kiasi ambacho taratibu hizi bado zimepewa nafasi ya kuendelea. Baraza aidha linapenda au la halinabudi kutoenda na teknologia ya sasa ambayo ulimwengu umekia. Hivi sasa kusoma hadi kufanya mtihani kwa njia ya mtandao wa Internet ni jambo la kawaida na kupata matokeo ya mtihani kwa muda wa saa moja sio jambo la kushangaa tena. Baraza halina budi kubadilika na kurekebisha kasoro hii kubwa ambayo inatoa mwanya mkubwa wa uchakachuaji wa matokeo unaoweza kufanywa na baadhi ya watu wake wasiolitakia mema Baraza la Mitihani Tanzania na nchi kwa ujumla. Hapa sio suala la kuliamini Baraza na watendaji wake kuwa watafanya walichotakiwa kufanya, ni suala na hoja ya kuweka kila kitu wazi na kwa ufasaha zaidi. Matokeo yaliyorekebishwa nayo pia yamesikika kuanza kuleta utata, kwani inasemekana yana maswali mengi kuliko majibu. Kwa mfano Mwanafunzi aliyepata alama E sasa amepata B na aliyepata alama D amepata C. Kwa kila utakachojaribu kufanya kimahesabu ya mchanganyiko, Mathmatical or Statistical Combination ya aina yoyote ile, inaleta maswali mengi sana na hata kuhisi kuwa sio tena kugawanya kwa mbili au tatu kuwa ndio tatizo. Kama haya ndio yaliyomo, basi kuna tatizo kubwa sana huko Baraza ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka na wa kina zaidi. Ni muhimu kulisaidia Baraza la Mitihani kwa haya yafuatayo: 1. K u w e k a m f u m o program maalum ya kusahihishia mitihani. Mfumo huo usiruhusu mabadiliko yoyote yale mbali na wale waliosahihisha mtihani huo. 2. Kutumia mfumo wa Tekinologia ya kusahihisha mtihani na kila msahihishaji kuweka alama moja kwa moja kwenye program hiyo ambayo itakuwa na nambari za watahiniwa wote. 3. Iweke mfumo au program itakayowezesha kila msahihishaji anaweka alama/ maksi za swali analosahihisha na pia kila Mkaguzi kukagua na kutumia mtandao huo wa Komputa. 4. A l a m a zote zijumlishwe (automatically) na program husika badala ya kujumlishwa na mtu au watu. 5. Baada ya kila somo kumalizika kusahihishwa alama/maksi zote za mwanafunzi husika zitajijumlisha (automatically) kwenye mtandao wa program husika, na matokeo yake ya masomo yote yatajulikana siku hiyo hiyo. Hili litakuwa pia kwa wanafunzi wote kwa ujumla. 6. Baada ya kumaliza zoezi hilo, Bodi inatakiwa kukaa hapo hapo na kuyapitisha au vinginevyo kurekebisha kama ilivyo sheria. Marekebisho hayo yafanywe na wasahihishaji husika, kwani program hairuhusu mtu mwingine wa pembeni kuingilia matokeo hayo. 7. K a m a k u t a t o k e a suala la kurekebisha matokeo kwa kuzingatia usawia wa kitakwimu standardization na mengineyo, zoezi hili liwe wazi kwa wote wanaosahihisha. 8. G r a d e z a k i l a mtihani ziwe wazi na sisiwe ni siri ya Baraza na watu wachache kwani inasemekana ni moja ya tatizo kubwa sana katika Baraza ambalo muda mfupi litaleta mfarakano mwingine. 9. Iwe ni lazima kuwa masaa 24 baada ya kumaliza kusahihisha mitihani na Bodi kupitia matokeo, matokeo yatolewe kwa wananchi bila kusubiri. Ni muhimu kuzingatia yaliyotajwa hapo juu kwani lengo ni kuwa na utaratibu wa makini kuzuia kinachoitwa makosa ya kibinaadamu human error kwani hata kama yanaweza kujitokeza kwenye program inayowahusisha watu wengi ni kidogo sana (negligible). Natarajia kwamba Baraza la Mitihani litachukulia jambo hili kwa uzito unaostahili ili kulinda heshima ya Baraza na elimu kitaifa kwani kushindwa kwake kuwa makini kunaweza kupoteza heshima ya Baraza hilo kitaifa na hata kimataifa kama kituo makini cha usaili wa wanafunzi duniani.

makosa ya daraja hiyo, nilipata maelezo kutoka kwa mtu mmoja wa Baraza na pia haswa kutoka kwa Mwalimu ambaye miaka mingi amehusika na usahihishaji wa mitihani ya sekondari nchini. Kutokana na maelezo yake ya kina, mitihani husahihishwa kwa makini sana kwani huhusisha waalim takriban 400 na zaidi na kila mmoja anasahihisha swali moja la mtihani wa somo analohusika. Baada ya hapo kuna mkaguzi anayepitia swali hilo na kuhakikisha kuwa mwalimu huyo amesahihisha vizuri na kuweka maksi husika kikamilifu. Baada ya kila mwalimu kusahihisha swali lake na kuweka alama ya maksi na kupitiwa na wakaguzi wote, anachukua mwalimu teule kujumlisha alama zote na kuweka jumla ya alama zote za mwanafunzi. Zoezi hili hupitiwa na waalim wakaguzi wengine wawili kuthibitisha kuwa mweka alama huyo hakufanya makosa na kama yapo hurekebishwa mara moja. Matokeo yote ya alama za kila mwanafunzi yanakusanywa pamoja na waalimu wawili wateule na kuyaweka pamoja kwa orodha ya watahiniwa wote kulingana na mitihani yao iwe ni mmoja miwili au zaidi. Kazi hii ya kuweka pamoja matokeo hayo hukaguliwa

Jussa atoa darsa muhimu Barazani


Na Mwandishi Wetu mrefu kurejea historia, muhimu akionyesha kuwa tunaouenzi sasa haukuwa muungano uliotokana na ridhaa ya wananchi. Kwamba ujaji wa muungano ulizungukwa na mashinikizo ya nchi za nje zilizokuwa na masilahi katika Zanzibar na Tanganyika. Katika uchambuzi wake akahitimisha akisema kuwa ufumbuzi pekee wa kero na matatizo yaliyopo katika muungano, ni kubadili muundo na kuwa wa

ISMAIL Jussa ametaka irudi Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kisha ndio uundwe muungano wa kimkataba. Jussa ameyasema hayo jana Barazani akichangia Hotuba ya Bajeti ya Makamo wa Pili wa Rais, Zanzibar. Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mji Mkongwe, alikuwa kama anatoa darsa kwa Wawakilishi ambapo alitumia muda

kimkataba. Akasema, kinachotakiwa ni kuwa na Tanganyika, Zanzibar, zote zikiwa nchi huru zenye mamlaka yake kamili ya kidola, kisha nchi na serikali hizo mbili ziangalie namna ya kushirikiana kimkataba. Hali Bungeni ilikuwa kama Jussa ndio katoa kauli ya siku iliyoakisi hisia na matakwa ya Wa w a k i l i s h i w e n g i kwa jinsi walivyopokea uchambuzi na maoni yake.

(Haya ni maoni yangu, mwananchi, msamaria mwema wa nchi hii nzuri Tanzania)

AN-NUUR

Makala

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

Wanaotaka kuvua koti la muungano wasipigwe mabomu

Na Na Khalid Said GWIJI

TANZANIA imeamua kuandika upya katiba yake. Mchakato huu wa Katiba na suala la muungano umeanza kwa kupitishwa sheria n o 8 / 2 0 1 1 . Ta y a r i mwanzo mbaya (falsestart) imeonekana katika mchakato unaoundwa na sheria hiyo. Kasoro kubwa ya sheria hii ni kuwa HAITOI FURSA YA WAZI kwa wananchi (wamiliki na wadhamini wa Katiba) kuujadili muungano na ukweli ni kuwa muungano ni nguzo kuu ya katiba yenyewe. Hasa kwa upande wa Zanzibar, ambako wananchi wa Zanzibar uhusiano wao juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kupitia muungano. Yote yaliyo nje ya mambo ya muungano, upande wa Zanzibar hawana haki nayo kama ambavyo Watanzania bara hawana haki na mambo ya Zanzibar (yasiyokuwa ya muungano). Ukisoma vifungu vya 8, 9 na 17 vya sheria hiyo ambavyo vimeainisha hadidu rejea (terms of reference) au mipaka (na kuna umuhimu gani wa kuwekea wananchi mipaka kuhusiana na mjadala wa Katiba yao?) ya kazi za tume ya katiba hamna hadidu rejea yo yote inayaotaja kuangalia suala la muungano. Na baya zaidi vifungu vya 9(1) (C) na 17(1) na 17(2)(d) vimeielekeza tume kutayarisha na kuwasilisha ripoti kwa kuzingatia hadidu za rejea hivyo ni kuwa

WAISLAMU Zanzibar wakiwa katika maandamamo ya kupinga Muungano.

HATA kama wananchi watazungumza sana juu ya suala la muungano, lakini kwa mujibu wa sheria hii, Tume haitoandika cho chote kuhusu mambo haya ya muungano. Tukizingatia ukweli wa kuwa wananchi wa nchi mbili hizi hawajawahi kupata fursa ya kutoa maoni yao juu ya suala la muungano, ilitegemewa muungano uwe ndio hoja kuu ya mjadala wa katiba na kuacha kabisa kuendeleza utamaduni wa muda mrefu wa kulitenga suala la muungano na wananchi wenyewe kulifanya halifikiki, halijadiliki wala haligusiki. Ni busara tusome alama za nyakati. Jambo jengine ni kuwa tatizo lililojitokeza mwaka 1977 kuhusu kukosekanwa kwa uwiano wa wajumbe katika kuunda Bunge la Katiba la wakati ule, linajikoteza tena mwaka 2012 katika kosa hilo hilo la kukosekanwa uwiano wa kuunda Bunge la Katiba la sasa. Yaani hatukujifunza hata baada ya miaka karibu 35 au ndio muendelezo wa ile dhana ya kuwa lengo la Muungano ni nchi moja (Tanganyika) kuitawala nchi nyengine (Zanzibar)? Bunge la Katiba la 1977 lilikuwa na wajumbe 207: ambapo wajumbe 45 tu walitoka Zanzibar na wajumbe 162 walitoka

Tanganyika. Na Bunge la Katiba la sasa kwa mujibu wa Sheria nambari 8 ya 2011 ya mchakato wa marekebisho ya Katiba linaeleza kuwa; kutakuwa na wajumbe takriban 600 wa Bunge la Katiba: ambapo wajumbe kutoka Zanzibar watakuwa kama 200, na wajumbe kutoka Tanganyika watakuwa kama 400. SUALA la kujiuliza: Mbona tunapoingia katika ushirikiano wa kimataifa na nchi nyengine, principle ya equality of membership inafuatwa na kuheshimiwa? Kwa mfano Bunge la Afrika Mashariki lenye nchi wanachama: Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi: kila nchi wanachama imepeleka wajumbe tisa (9) tu katika Bunge la Katiba la Jumuia hii. Haikusemwa kwamba Tanzania kwa sababu tuko wengi kwa idadi ya watu milioni 43 hivyo inabidi tupeleke wajumbe wengi zaidi kulinganisha na Rwanda yenye watu milioni nane? Nchi zote hizo zilipeleka wajumbe tisa bila ya kujali wingi wa idadi ya watu wake au ukubwa wa eneo kwa sababu si demograpy wala geography zinazotumika katika kuzingatia vipimo vya mamlaka (sovereignity) ya nchi. Sasa kwa nini Bunge la Katiba la Tanzania liwe

na wajumbe wachache kutoka Zanzibar; lakini liwe na wajumbe wengi k u t o k a Ta n g a n y i k a ? Mbona Tanzania hiyo hiyo inaifuata principle ya usawa wa uwiano ikiwa nje ya nchi (kimataifa) lakini kwa makusudi inaipuuza ikiwa ndani ya nchi? Tatizo kubwa jengine ambalo linajirudia kama ilivyotokea mwaka 1977: lile Bunge la Katiba la 1977 na hili la sasa kwa mujibu wa sheria nambari 8: YOTE mawili ni mabunge ya kuteuliwa si Mabunge ya kuchaguliwa. Kwa nini Mabunge haya yasichaguliwe na wananchi wenyewe na badala yake Rais ayateue? Je, yataweza ku - reflect wishes za wananchi? Wa s h i r i k i w a k u u wa mchakato huo wa marekebisho ya Katiba ni WANANCHI ambapo mamlaka ya kuendesha nchi yanatokana na wananchi wenyewe. Universal declaration of human rights inasema hivyo. Hiyo Katiba ya Muungano ya 1977 nayo inasema vivyo hivyo. Na Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010 nayo inalitambua hilo pia. Ibara ya tisa inaeleza kuwa uwezo, nguvu na mamlaka yote ya kuendesha nchi yatatoka kwa wananchi wenyewe na si kwengineko. Kama

hivyo ndivyo, iweje Tume ya Katiba iweke hadidu rejea (terms of references) ambayo maana yake ni MIPAKA? Unawawekeaje mipaka wananchi ambao sio tu ndio wamiliki wa Katiba; bali ndio walio na MAMLAKA na HAKI kuhusiana na mustakbal wa taifa lao kama ibara ya 21 (2) ya Katiba ya Zanzibar inavyoeleza? Sheria nambari 8 ya 2011 ya marekebisho ya Katiba haiwezi KUWA JUU YA Katiba ya Zanzibar. Wanaoutetea Muungano kwa madai kuwa ni mzuri na hauna matatizo na kwamba tuendelee nao kama tulivyo - wanaonekana sio tu ni wahafidhina wasiojua mambo (political naives); bali hawajui hata kusoma alama za nyakati na mahitaji na kwamba wanaonekana ni politicians with NO politics. Essence ya marekebisho ya Katiba ya Muungano maana yake nn? Maana ya marekebisho ni kuwa kuna mapungufu na kasoro. Kitu kikiwa kizuri hakihitaji marekebisho. Ila, Muungano una kasoro na kero nyingi ambazo wao wenyewe wamekiri kushindwa kuzipatia ufumbuzi. Kwa wengine, Muungano umekuwa ndio kero yenyewe kutokana na kuonekanwa una dhamira ya nchi mmoja kuitawala nchi nyengine. Kwa mfano, ibara ya 55 (1) ya Katiba ya Muungano inasomeka: Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54, watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu. Sasa tujiulize, nani Rais na nani Waziri Mkuu? Rais ni Kikwete, Waziri Mkuu ni Pinda iko wapi Zanzibar hapo? Eti hiyo ndiyo cabinet inayoamua sera za mambo ya Muungano huu. Kwa nini ibara isiseme kuwa Rais atateua Mawaziri baada ya kushauriana na Makamo wa Rais ambayo ndiyo formula katika Katiba isemayo kwamba - Rais akitoka upande mmoja wa Muungano, Makamu wa Rais anatoka Inaendelea Uk. 8

Waislamu washushiwa kipigo kikali


Na Mwandishi Wetu
K A T I K A k i l e kilichoonekana kama kutekeleza shinikizo la Askofu Vallentino Mokiwa aliyesema haridhishwi na utendaji wa polisi, sasa Polisi wamefanya jambo ambalo huenda litamfanya Askofu Mokiwa awapongeze. Katika kufanya hivyo, hawakujali hata heshma ya wanawake wa Kiislamu na heshma ya Msikiti. Waliwashushia kipigo wanawake waliokuwa Msikitini huku wengine wakiwachania nguo zao. Wala haikuwapitikia kuwa haikustahiki wao kuingia Msikitini na mabuti yao. Mmoja ya Misikiti hiyo, haukuweza kuingilika kwa ajili ya swala kwa siku kadhaa kutokana na hewa kali ya mabomu na uharibifu uliokuwa umefanyika. Hiyo ni ile siku Polisi walipowazuiya wananchi pale Mahonda ambao walikuwa wakielekea Donge kwa ajili ya mkutano uliokuwa ufanyike katika Msikiti wa Donge Pwani. Hiyo ilikuwa ni ile siku Misikiti ya Donge Pwani, Donge Skuli na Mahonda ilipovurumishiwa mabomu ya machozi kuwapiga waliokuwamo ndani. Kati ya watu walioumia sana ni Mwadini Suleiman Juma mkaazi wa Mkwajuni na Mzee Amour Simai Ame mkaazi wa Fukuchani mkoa wa Kaskazini Unguja. Akizungumza na mwandishi, Mzee Mwadini Suleiman amesema yeye ni mkazi wa Mkwajuni lakini alikuja Donge baada ya kusikia kuna mhadhara na akataka kusikiliza na ndipo walipokaa nje ya Msikiti wakisibiri muda wa mkutano. Hata hivyo anasema, ghaa walivamiwa na jeshi la polisi ambapo walirusha mabomu na kuripuka karibu na alipokaa yeye na ndio moja lilipompiga na kumuathiir sana. Kwa hakika ilikuwa kama ile kadhia ya Mwembechai kama ambavyo gazeti hili lilihoa toka awali. Kwamba huenda wananchi wa Zanzibar wakashushiwa kipigo kikali kutokana na shinikizo la maaskofu. Naam, wanawake wamefuatwa ndani ya Msikiti baada ya kuvurumishiwa mabomu na kupigwa virungu na mateke huku wengine wakivuliwa shungi zao. Askari wamefanya

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

HABARI

AN-NUUR

WANANCHI wa Donge wakitawanywa kwa mabomu ya kutoa moshi na Polisi.

MOSHI na moto uliotanda eneo la Donge baada ya polisi kurusha mabomu ya moshi. unyama na uhalifu wa hali ya juu kwa kuunajisi Msikiti wa Ijumaa wa Mahonda kwa kuwahujumu raia wasio na silaha ndani ya Msikiti kwa kuwarushia mabomu ya machozi yasiojulikana idadi yake ambapo hadi hii leo Msikiti huo hausaliki ndani kutokana na harufu kali ya mabomu. Pia askari hao walipiga risasi pamoja na kuingia ndani ya Msikiti na viatu na kuvunja kwa makusudi vyombo ikiwa ni pamoja na Vespa, Pikipiki na Baskeli vilivyoegeshwa eneo la Msikiti huo wa Ijumaa pamoja na kuiba viatu vya waumini kwa kunyanganyiana. Imesema sehemu ya Tamko la Uamsho. Maelezo ya wananchi waliokuwa katika eneo la tukio wanasema kuwa ilikuwa kama wakati ule wa Janjawed maana Polisi walikuwa wakitolea hasira zao mpaka kwenye vyombo vilivyoegeshwa nje ya Msikiti na majumbani mwa watu. Jambo la kushtusha zaidi ni kitendo cha kuwadhililisha wanawake na kufikia hadi kuwakashifu kwa kuwachania nguo zao na kuwavua mashungi yao pia hata watoto wadogo mitaani wako walopata kipigo, kitendo cha kuwatimba wanawake kwa viatu bila ya huruma na kuwapiga marungu na kuwajeruhi vibaya sehemu za usoni na mwilini kwa ujumla, huo wote ni unyama na ukiukwaji wa haki za binaadamu. Imesema taarifa ya Uamsho. Awali mara tu baada ya kutokea vurugu ambapo baadhi ya makanisa yalichomwa, Askofu Mokiwa alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa anataka kuona watuhumiwa (Uamsho)

wakikamatwa wapigwe bakora na polisi na baadaye wakishwe kwenye vyombo vya sheria. (Nipashe, Mei 31 2012) Lakini kabla ya hapo alisema pia kuwa hajaridhika na utendaji wa Polisi kwa sababu hajaona kasi yao kwa vitendo wakiwashughulikia Uamsho. Kwa kukujua nguvu ya mfumokristo na kwa kuzingatia uzoefu wa kadhia ya mauwaji ya Mwembechai, gazeti hili katika toleo lake namba 1015 la Juni 1-7, 2012 lilielezea wasiwasi wake kuwa huenda Polisi Zanzibar wakafanya hujuma kubwa kwa Waislamu ili kuitikia na kutekeleza matakwa na shinikizo la Kanisa. Naam, yametimia. Uamsho, Waislamu na waumini ndani ya Msikiti wa Mahonda, wamepigwa bakora kabla ya kuhukumiwa kama alivyotaka Askofu Vallentino Mokiwa. Baada ya bakora hizo, sasa waliokamatwa ndio watakishwa mahakamani. Kwa upande mwingine, Kule Donge nako, Waislamu waliokuwa wamekusanyika katika Msikiti ulipokuwa ufanyike mkutano, hawakunusika. Walipa mgao wao wa kipigo. Walivamiwa na kupigwa sana. Ilipofikia wakati wa Laasiri Jeshi la Polisi walianza kupiga mabomu ndani ya Msikiti wa Donge Pwani pamoja na kuuhujumu Msikiti na waumini wakiwa wanaswali na kuvunja vioo vya msikiti huo. Inasema taarifa moja. Kwa mujibu wa maelezo ya wananchi walioongea na mwandishi, Polisi walikuwa na hasira na kisirani ambacho hakijulikani sababu yake ilikuwa nini. Wakifafanua walisema kuwa walishangaa kuona baadhi ya polisi wakiharibu vyombo ya usafiri vya waumini waliokuwa ndani ya Msikiti. Japo taarifa ya Polisi inasema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa, lakini mwandishi ameshuhudia na kuongea na watu kadhaa wenye majeraha yaliyotokana na virungu au mabomu ya machozi. Mmoja wa majeruhi Mzee Kassim Sheha aliyepigwa wakati akiswali swala ya Laasir na kujeruhiwa vibaya miguuni kwa mlipuko wa bomu la machozi akiwa ndani ya swala. Inaendelea Uk. 7

AN-NUUR

Waislamu washushiwa kipigo kikali


Inatoka Uk. 6
Baadhi ya wanawake walioongea na mwandishi aliyefika Donge kufuatilia kadhia hii wamesema kuwa, walivamiwa Msikitini, wakavuliwa shungi zao huku wakirushiwa maneno ya kifedhuli. Kuna wengine walikuwa nje mbali na Msikiti, nao wakabururwa hadi ndani na kupigwa sana, ilikuwa kama tumevamiwa na jeshi la adui, alisema mama mmoja. Katika hali hiyo, Wananchi wa Donge wanasema wamechoshwa na ubaguzi na udikteta wanaofanyiwa na baadhi ya viongozi wa serikali. Wananchi hao wanasema kuwa wanataka Serikali itoe ufafanuzi ni kwa nini wananchi wa Donge wananyimwa fursa ya kufaidi uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni pamoja na uhuru wa kuchanganyika na ndugu

HABARI

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

zao Wazanzibari? Jambo hilo limegusiwa pia katika Tamko la Uamsho lililotolewa tarehe 19 Jun, 2012 ambalo pamoja na mambo mengine limesema kuwa: Wananchi wa Donge wanaomba ufafanuzi kutoka Baraza la Wawakilishi kwani kwa miaka yote wanajiona kuwa wanabaguliwa wakati wananchi wenzao wa Mashamba yote mengine katika wilaya tofauti wakipata haki kikamilifu, jee wao si Wazanzibari? Ni dhambi gani waliyotenda hata wakabaguliwa kiasi hicho? Au Donge ni nchi
yenye mfalme kama wafalme wa ki-Misri wakijulikana kwa jina la Firauni? (Soma Tahariri Uk. 2)

Walitaka kuniuwa asema Sheikh Farid


Inatoka Uk. 3 kweli tulipoka nyumbani tulikuwa kama tumepigwa mawe mwili mzima kwa yale marungu maana mimi miguu ilikuwa haiwezi hata kutembea jinsi ya marungu tulopigwa katika magoti na mwilini, anasema Hafsa. Wanawake hao baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa polisi, walipelekwa kituoni na kuwekwa hapo tokea saa 9 hadi saa 4 usiku ambapo walitakiwa kurejea zao majumbani na kufika siku ya pili mapema. Wa n a w a k e h a o waliosomewa mashitaka ya kukusanyika isivyo halali na kukataa kutii amri halali ya jeshi la polisi. Hata hivyo, pamoja na kuwa dhamana ilikuwa wazi, shida kubwa iliwapata baada ya Masheha kukataa kutoa barua za udhamini. Nusura ya kinamama hayo ilipatikana baada ya Wakili wa kujitegemea alipoingilia kati na kusema dhamana ni haki ya mteja hivyo hakuna sababu ya kuendelea kukoseshwa haki zao kwa kuwa hakuna barua za Sheha wakati Masheha wanajulikana hawataki kutoa barua.

Hili ni bomu la moshi lililotupwa ndani ya Msikiti na polisi .

Mwanamke wa Kiiaslamu aliyekuwa akishikilia bendera ya Uamsho yenye maandishi Laaila ha ilallah, aLIshushiwa .

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

MAKALA

AN-NUUR

Wanaotaka kuvua koti la muungano wasipigwe mabomu


Inatoka Uk. 5

upande mwengine? Halafu wahadhina hawa watuambie tusiuzungumze Muungano huu uliojaa viini macho!? (To them politics is just a business; not a mission) ! Vil vile, Sheria nambari 8 ya 2011 ya marekebisho ya Katiba imeweka suala la makosa na adhabu. Sheria ime creates makosa ya jinai kupitia kifungu cha 21 cha sheria ile. Makosa yenyewe ni pamoja na kuzuia Tume isifanye kazi ambapo kufanya hivyo ni kosa la jinai na utashitakiwa. Kuchochea mtu yo yote kuzuia Tume isifanye kazi zake au sekretarieti au mjumbe wa Tume asifanye kazi zake pia ni kosa la jinai na utashitakiwa chini ya kifungu hicho cha 21. Kubwa zaidi, yo yote anaetaka kufanya mikutano au makongamano nk yenye lengo la kuelimisha umma (public awareness programme) - kwa mujibu wa sheria hiyo analazimika afuate taratibu za sheria hiyo zinavyotaka. Hapo maana yake nini? Maana yake ni kuwa; sheria nambari 8 ya 2011 ya marekebisho ya Katiba inakana na kunyima haki ya wananchi ya Kikatiba ya kutoa maoni yao kwa uhuru kwa kuwalazimisha wafuate taratibu za sheria hiyo. Baada ya kuyaona hayo, ukweli ni kuwa sio tu kuwa suala la muungano liwe ni msingi katika mjadala wa katiba; lakini suala la muungano lilistahiki kuamuliwa mwanzo na ndiyo baadae lije suala la katiba. Vipi tusiuzungumze Muungano ambao ndio uliozaa Katiba? Tuliungana kwanza kabla ya kuwa na Katiba. Muungano ndio uliozaa katiba tulizonazo, katiba zote mbili (ya Zanzibar 1984 na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977) ni matokeo ya muundo wa muungano huu. Muundo ambao uliunda mamlaka tatu (three Jurisdictions): ya Tanganyika, ya Zanzibar, na ya Muungano na baada ya hapo mamlaka mbili za Tanganyika na ya Muungano

zikachanganywa (fused) na kuwa chini ya serikali moja na mamlaka ya Zanzibar kuwa chini ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hivyo pakawa na Serikali mbili na katiba mbili. Na huu ndio msingi unaowafanya wengi (Aboud Jumbe, 1994 & Dourado, 1999 nk) wakasisitiza kuwa mkataba wa muungano ulikusudia mamlaka 3 na serikali 3 na ule utaratibu wa mamlaka 3 chini ya serikali 2 na hivyo katiba mbili ulikuwa ni wa muda wa mwaka mmoja tu mpaka utapoundwa mfumo wa katiba mpya ndani ya mwaka mmoja kuanzia siku uliposainiwa mkataba wa muungano. Mkataba wa Muungano unataja kipindi hicho kuwa ni interim period Angalia kifungu (iii) cha Mkataba wa Muungano: During the interim period, the Constitution of United Republic shall be the constitution of Tanganyika so modied as to provide for . Mkataba ulielekeza kuundwa kwa tume ya katiba (kifungu vii) ambayo ingeundwa kwa makubaliano kamili ya Marais wawili wa nchi zilizoungana. La kushangaza ni kuwa hilo lilikwepwa kabisa, tena kwa amri ya upande mmoja tu (Tanganyika chini ya Nyerere) alipoamua kivyake - vyake tu (uniletarally) kupitisha sheria (Act no 18 of 1965) na kuliakhirisha hilo kwa muda usiojulikana mpaka hapo lilipoibuka tena miaka 14 baadae kwa kuunda katiba ya 1977 wakati huo ikiwa ni sawa na kuvuta shuka wakati kumeshakucha kwani mkataba wenyewe ulishajeruhiwa vya kutosha. Sheria hii ndio iliyovuruga kabisa Mkataba wa Muungano na ikafungua milango kwa upande mmoja wa Muungano kuamua watakalo. K. Sasa tujiulize endapo Wa z a n z i b a r i a m b a o wataamua, katika maoni yao, kuwa hawataki muungano na kwamba muungano kwao ndio kero yenyewe ni vipi bunge la katiba litakuwa na wajumbe kutoka Zanzibar? Inakuaje

leo wanaodai kuukataa Muungano waonekana maadui na hata ikie hadi kukamatwa na kupigwa mabomu? Huku si ni kwenda kinyume na Katiba ambazo zinaeleza kuwa mamlaka, uwezo na nguvu zote za Serikali zitatoka kwa wananchi? Na hata Nyerere mwenyewe wakati akiwa Uingereza, tarehe 20 April, 1968 alisema na maneno yake kunukuliwa ndani ya makala ya London Observer akisema: If the mass of the people of Zanzibar should, without external manipulation, and for some reason of their own, decide that the union was prejudicial to their existence, I Nyerere could not BOMB Zanzibaris into submission. The union would have ceased to exist when the consent of its constituent members was with drawn; yaani, Endapo umma wa Wazanzibari wataamua bila ya ushawishi kutoka nje kwa hoja zao wenyewe, wakaamua kukoma kwa Muungano, mimi Nyerere sitoweza kuwapiga mabomu. Muungano utasita pale tu utakapokosa ridhaa ya wananchi. Sasa kama hivyo ndivyo, iweje leo viongozi wa Serikali wawapige MABOMU wananchi halali kwa kuitumia haki yao hiyo Kikatiba na ya right to self - determination kuukataa Muungano uliowagharimu kila kilicho chao? Wanaodai kuwa wao ni watetezi wa Muungano wanadai kuwa tuudumishe Muungano ili kuwaenzi marehemu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume wakiwa ni waasisi wa Muungano huo. Suala: Vipi tuwaenzi marehemutena wawili kwa kuwadhulumu waliohai kwa mamilioni? Je, ni nani alie na maana na thamani zaidi kati ya marehemu na aliehai? Tuwaenzi kwa kuudumisha hata kama unatugharimu kila kilicho chetu? Muhimu si kuwaenzi marehemu; muhimu ni MASLAHI ya waliohai. (The damage is HERE; the damage is NOW).

Na kwa hakika Wazanzibari walio wengi kama ni kumuenzi Karume basi wanamuenzi sio tu kwa maneno matupu; bali wanamuenzi kwa vitendo kwa kuisimamia hoja yake kuwa Muungano ni sawa na kushona koti, ukiona linakubana, UNALIVUA,

hoja ambayo aliizungumza wakati bado Nyerere yuhai! Lakini na Watanganyika nao watamuenzi Nyerere kwa kuwaachia Wazanzibari wajiamulie walitakalo bila ya kuwapiga mabomu kama alivyoeleza Nyerere alipokuwa Uingereza 1968.

VIROBA MURUA
Kwa mahitaji ya viroba bora vipya kabisa kwa matumizi mbalimbali sasa unaweza kupata kwa bei ya jumla na rejareja kwa saizi zote kwa bei nafuu zaidi, kwa BANDO. Tupo mtaa wa Likoma na Pemba Kariakoo, Dar es Salaam (nyuma ya Msikiti wa Idrisa). Kwa mawasiliano zaidi wasiliana kwa simu: 0557 800999/0683 800999.

MSAADA WA UJENZI WA MSIKITI


Waumini wa Al-Masjid Kauthar And Islamic Centre, ulioko Kimara King`ongo jijini Dar es Salaam wanaomba msaada ili kukamilisha Msikiti walionza kujenga. Msikiti wa awali ulikuwa wa Matope sasa wanajenga mpya wa matofali kwa michango ya waumini wa msikiti huo. Vifaa vinavyohitajika:1. Nondo 44 mm 12 2. Nondo 36 mm 16 3. Cement Mifuko 100 4. Tofali 4000 5. Bati 150 6. Mbao Treated 2 by 4, 200 7. Mbao Treated 2 by 2, 150 Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba hizo, Imam 0784 536 664, Katibu, 0713 239 529, Muweka Hazina 0718 537 588 au ka katika msikiti huo ulioko King`ongo. Au unaweza kutuma mchango wako kwa M- pesa 0663 241 288 au Tigo pesa 0713 239 529.

AN-NUUR

MAKALA

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

Kura ya maoni, Muungano wa kimkataba


Muungano kutoka Tanzania Bara. 2. Jaji Mkuu Tanzania Bara 3. Spika wa Bunge Tanzania Bara 4. Naibu Spika, Tanzania Bara 5. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje ni Tanzania Bara 6. Wa z i r i w a F e d h a , Tanzania Bara 7. Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Tanzania Bara 8. Msajili wa Vyama wa Tanzania Bara 9. Mkuu wa Polisi wa Tanzania Bara 10. Mkuu wa Jeshi wa Tanzania Bara 11. Mkuu wa Usalama wa Taifa Tanzania Bara 12. Mkuu wa Uhamiaji wa Tanzania Bara 13. Mkuu wa Necta wa Tanzania Bara 14. Gavana wa Fedha wa Tanzania Bara Katika kuiendeleza mikakati ya kuitawala Zanzibar vikauliwa vyama vyote viwili vya saisa A.S.P cha Zanzibar na TANU kwa upande wa Tanganyika, kikaundwa chama kipya cha CCM yaani Chama Cha Mapinduzi. Watawala na watendaji huibuliwa ndani ya chama hicho. Mfano ulio wazi ni wa Sir John Rankine, Sir Henry Poter na Sir Georg Mooring walitawala Zanzibar kwa niaba ya Uingereza. Hapa visiwani upo muelekeo huo huo wa kiutawala kwa niaba ya Tanganyika. Masikini ndugu zetu hawa hawajuwi wanalolifanya kwa Mama Zanzibar si tunaona, wanapoona maslahi yao yanahatarishwa haraka haraka huletwa Wanajeshi na vifaru ili kulinda maslahi yao. Masikini Zanzibar, tulikua Ta i f a l e n y e k u t a m b u l i w a ulimwenguni kote, leo si lolote mbele ya Mataifa. Hebu litupieni macho Bunge la Muungano. Bunge hilo linafanya kazi sehemu mbili ya Muungano na Tanganyika. Katika Bunge, kimtazamo faida za watu kutoka Tanzania Bara zitapewa kipaumbele zaidi kuliko zile za Wazanzibari katika mambo ya Muungano. Eti hivi sasa walipoona kijungu chapwaga bila ya moto jikoni, ndio wanaanza kukiri namna ya kuidanganya Mama Zanzibar kupitia kwa mawakala wa Serikali ya Muungano. Uhodhi wa upande mmoja wa Tanzania Bara umekuwa na nguvu zaidi katika uendeshaji wa muundo wa Muungano na kisheria. Waswahili wanasema kheri hutokana na shari. Vile vile kuna usemi kwamba, penye mchafuko ndio nidhamu inapozaliwa. Kwa hivyo mchakato wa kuipa nguvu zaidi

Na Ibrahim Mohammed Hussein MAMBO yanataka mipango. Jambo lolote lile linataka mipango. Inawezekana watu wakawa na nguvu, wakawa na mali na wakawa wengi na wakashinda kwa kishindo, lakini wakakosa mipango na hapo mambo yao yote yakaharibika. Tu l i j i n a s i b u t u l i f a n y a Mapinduzi yenye lengo la kuwakomboa Wazanzibari kutokana na hali mbaya ya maisha na kutaka kunyanyua uchumi wa visiwa hivi pamoja na kujiamulia mambo yao. Sio lengo la Mapinduzi kuwafukuza watawala wa Kiarabu ili Waafrika wa Bara watawale Visiwa hivi. Lakini kutokana na mipango na mikakati madhubuti ya majirani zetu ilioanzishwa tokea miaka ya sitini ya kutoiona Zanzibar kama ni nchi walifanya mipango ya kujishirikisha katika siasa za Zanzibar kwa malengo maalum. Ni wao waliopika Mapinduzi na kuyasaidia kwa hali na mali ili kuhakikisha mipango iliyopangwa kwa ustadi inatimia. Wakafanya juu chini kulipora Taifa la Zanzibar kupitia katika mtego wa Muungano, na kuanzia hapo Zanzibar ikawa iko chini ya Serikali moja yenye nguvu ya Muungano yenye kuongozwa na Serikali ya Tanganyika iliyosokomezwa ndani ya Muungano. Inabidi hivi sasa tutafakari na kujiuliza nani alihusika kuuwawa kwa watu kama Marehemu Othman Sharif. Marehemu huyu nae ni miongoni mwa Viongozi walioutumikia mpango maalum wa kupindua Zanzibar. Alipokuja shituka ndipo aliposema: Wa n a n c h i S e r i k a l i ishatwawa, ishakuwa Bara. Tunamnyanganya Muengereza, tunampa Songoro Hereza, kashampa Mjombawe Mali Jeza. Sasa ataka tuangamiza. Wapiii:- Hatamu zote za Uongozi ziko upande wa pili:1. Rais wa Jamhuri ya

MMOJA wa wananchi wa Zanzibar akichangia mada kuhusu muungano.


sehemu moja kwa niaba ya Bara, ndio hivi sasa umeleta msukumo wenye nguvu kuitetea Zanzibar na Uhuru zaidi na madhubuti. Serikali ya Muungano kwa kupitia Chama Cha CCM wanajiona wao ndio walindaji wa mirathi ya mfumo wa Muungano wetu ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere. Kuubadilisha mfumo huo ni vita vikubwa kutoka kwa mawakala na vibaraka wa chama na Serikali yenyewe ya Muungano, ambao wengi wao ni ndugu zetu wa hapa hapa Visiwani Zanzibar. Huko nyuma nimekwisha sema kwamba panapokuwa na mchafuko, ndipo inapozaliwa nidhamu. Leo watu wanataka kura ya maoni. Wazanzibari wamekuwa na matumaini juu ya sheria hiyo. Kweli sheria hiyo ipo ndani ya katiba ya Zanzibar, lakini chanzo chake ni kipi? Uvumilivu wa kisiasa aliouonesha Maalim Seif Sharif Hamad baada ya uchaguzi wa 2010, kukubali kwa Maalim Seif matokeo ya uchaguzi huo ndio sababu moja kubwa ya kupatikana sheria hiyo ya kura ya maoni. Kila chenye thamani, gharama yake inakuwa kubwa. Kwa vile kura ya maoni ni kitu chenye thamani kubwa sana kwa Wazanzibari, kilipatikana kutokana na gharama ya kusamehe kwa Maalim Serif matokeo yaliochezewa na kuchakachuliwa na Tume ya Uchaguzi. Hicho ndio chanzo cha kuundwa kwa Serikali ya Kitaifa ambayo ilimpa fursa muwakilishi wa CUF Bw. Abubakar Khamis kupeleka ombi binafsi mbele ya Baraza la Wawakilishi ili lijadiliwe na kuombwa wajumbe walipitishe. Kwa hivyo chini ya marekebisho ya kumi yaliyofanywa na Baraza la Wawakilishi mwaka 2010 chini ya sheria ya kura ya maoni, sheria na 6 ya mwaka 2010 imeanzisha kura ya maoni. Katika Katiba imesisitizwa kwa kila jambo kubwa au lenye umuhimu wa kipekee ni vyema suala hilo likaamuliwa kwa kuwashirikisha wananchi wote kupitia kura ya maoni. Ndio kilio cha Uamsho kutaka kura ya maoni. Ukiona kinaeleya ujuwe kwamba kimeundwa. Tunawashukuru Wawakilishi wote waliokubali ushauri huo, lakini vile vile tusisahau kwamba uvumilivu wa Mh. Maalim Seif Sharif Hamad ndio sababu kubwa ya kupatikana kitu adhimu kama hicho kutiwa ndani ya Katiba yetu. Na kama inavyoeleweka kwamba Katiba ya Nchi ni matakwa ya Wananchi kwa Serikali yao namna gani wanavyotaka Serikali iendeshe utawala wake. Katiba ni mkataba baina ya watawaliwa na watawala. Sasa leo wakitokezea watu na wakaleta kejeli na matusi kwa kiongozi huyu Maalim Seif, basi juwa hao bado hawajatambua mchango wa mwanasiasa huyo juu ya ukombozi wa Nchi yake na kwa Wazanzibari kwa ujumla wao. K U R A YA M A O N I . KITANZI CHA MUUNGANO unaoshikiliwa kwa mabavu na hila za kikatiba. Nilifurahi, sana niliposikia mada ya vijana wa kitaifa kutaka Muungano lakini uwe wa kimkataba sio wa kikatiba. Vile vile dai la Uamsho la kutaka kura ya maoni sio baya ni haki yao ya kikatiba. Sasa ni kazi ya CCM kuchagua kulia au kushoto. Kura ya maoni ndio kulia katika maana hiyo hiyo ya kulia au kushoto maana Muungano wa mkataba, njia nyengine sioni. Kukataa vyote ni kuwafanya umoja wa vijana kuunga mkono Uamsho katika dai lao la kura ya maoni. Ndio niliposema Kuna kijungu chapwaga bila ya moto jikoni. Moto ni pale wote watakapodai kura ya maoni. Amma kweli kijungu tayari kimeshaiva walaji wengi wapo tayari kula chakula chenye ladha hasa ya mapishi ya Kizanzibari, lakini bado hajapatikana mpakuaji wa chakula hicho. Amma kweli ajabu ya kiroboto kubwaga tembo porini. Hivi kweli Kizanzibari hichi kiduchu kinataka kuibwaga Tanganyika! Kama kiroboto alie mdogo anaweza kumuangusha tembo na kujipiga na miti porini hadi likaanguka, basi yawezekana Tanganyika ikaporomoka chini miguu juu. Ujanja mwingi huondoa maarifa. Kuanzishwa kwa Muungano wa nchi mbili ili kila moja ibakie na utawala na uendeshaji wa mambo yake ya ndani. Wazanzibari walifanya hivyo kwa kuzisalimisha baadhi ya Wizara zake katika Muungano huo, wakidhani Watanganyika nao watafanya hivyo. Kumbe kinyume chake. Watanganyika hawakubali kuzisalimisha baadhi ya Wizara zao. wao waliingiza Serikali yote ya Tanganyika ndani ya Muungano. Kuanzia hapo Tanganyika ikawa ndio Muungano na ndie muongozaji na mpangaji wa kukubali na kukataa jambo lolote lile. Wanaokataa suala la OIC ni wao na suala la Kadhi ni wao viongozi wa Serikali ya Tanganyika. Tanganyika ipo na Baraza lake lipo ndani ya Serikali ya Muungano. Zanzibar My Country, right or wrong. Kwa maoni, maswali kwa mwandishi tumia: 0715-498 363)

10

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

MAKALA

AN-NUUR
Jengo la Kanisa ambalo lina ramani ya ukubwa wa kushinda Kanisa lolote katika Visiwa hivi. Mikusanyiko mikubwa inayoonekana hapo kila Jumapili kwa sasa inawajumuisha takriban watalii wote wa Ukanda wa Pwani ya Mashariki mwa Kisiwa cha Unguja, anzia Paje, Jambiani, Uroa, Chwaka, Matemwe, Pwani Mchangani, Pongwe, hadi Kiwengwa; wote hao hujumuika hapo, kunogesha wimbo wasioujua maana yake wa udumu Muungano. Kwa wimbo huo wananchi wametakiwa waendelee kuwa watulivu na watoto wao watakuwa wakipatiwa huduma ya maziwa na uji kila siku watakayohudhuria ndani ya kituo cha Maandalizi kiliopo Kanisani hapo, na yeyote atakayebisha huyo ataitwa UAMSHO na Adui Nambari Moja wa Muungano, hivyo ndivyo linavyotaka Kanisa. (Abu Hassan Ally Makame)

HAKUNA Muislamu, Mzanzibari, mwenye busara yeyote katika nchi ambaye haelewi kwamba Kanisa na wafuasi wake hawako radhi kuona Zanzibar ikiwa tulivu na yenye kutengamaa. Huenda huo ndio mwelekeo uliompelekea hata Raisi\ Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Benjamin William Mkapa hata akashindwa kucha hisia zake juu ya shaka ya kuviwacha Visiwa hivi vikitanafasi. Msimamo huo ambao ni kama ufuasi wa njia ambayo ilishazoeleka kabla na baada ya Uhuru kwamba isifike wakati Zanzibar ikaishi kwa murua, kutokana na shaka iliyotawala nafsi za waliokereketwa na nuru ya neema ya Visiwa hivi, ulikuwa si mzaha katika hima ya kuimeza na ikibidi kuifutilia mbali jamii ya watu hawa wa Pwani ikibidi na vizazi vyao popote walipo Ulimwenguni. Kama inawezekana natamani kuvikunjakunja vijisiwa hivi na kuvitupilia mbali baharini kutokana na ..............., hiyo ni miongoni mwa dalili za mawingu ya hisia nzito za watawala waliopita dhidi ya visiwa vya Unguja na Pemba na watu wake. Haikuwa mzaha kwani ni muda mfupi wa Miongo isiyozidi Miwili ya Utawala wa Bw Mkapa pekee tuliposhuhudia Zanzibar ikigeuka ghaa kutoka safari ya kuelekea Dubai ndogo kibiashara hadi katika jangwa la idhilali lisilokuwa na hali wala mahali. Mpaka inakuja Serikali ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, chini ya Uongozi wa akina Dr. Shein, Maalim Seif, na Balozi Idd, Biashara

Linavyotaka Kanisa ....

yao. Mbona hakuna kelele kwamba msikiti hadi leo hausaliki, Waislamu wanaswali nje kutokana na harufu ya mabomu na damu iliyotapakaa, ya Waislamu waliopigwa mabomu na risasi ili kuridhisha mlingano wa ile vita ya panzi. Ni lipi ilitakalo Kanisa katika Visiwa hivi... Tafakari: Hebu funga safari mpaka Kijiji kimoja kinachoitwa

ASKOFU Mokiwa kutoka Zanzibar kwenda Bara, hali ambayo haikuwahi kujiri tangu asili ya Nchi hii, ilikuwa ni ya thamani ya Sh. bilioni 2 ukilinganisha na bilioni 60 kutoka Bara kwenda Zanzibar. Tunabaini kwa mujibu wa takwimu sahihi ndani ya takriban kipindi cha mwaka mmoja hali imekuwa ya kujiuliza wakati ambao maagizo ya kibiashara kutoka Bara kwenda Zanzibar yakisalia kwenye bilioni 60, kutoka Zanzibar kwenda Bara yameruka hadi bilioni 70 na kuwacha pengo si dogo; huku ndiko kupumua inakohitaji Zanzibar sasa. Hayo ni ya upande wa uchumi pekee, na mengi memgineyo yapo chini ya azma njema tokea pale watu wa Visiwa vya Unguja na Pemba walipokubali Maridhiano, chini ya Serikali ya sasa ya Umoja wa Kitaifa. Bila shaka hayo yameanza kupiga kengele ya tahadhari kwa Kanisa na kila asiyeitakia mema Nchi hii ya Waislamu, ambayo hayana ubishi yakisikika kwenye hadhara za siri na za dhahiri, kwamba hawa wasije wakaelewana hali itakuwa mbaya. Utashangaa sana visingizio vilivyopo mara vya Uamsho, mara vya Wapemba, na mara vya Waislamu kuchoma m ak an is a , a lm u r ad i nyimbo tu za kuwazuga watu, lakini linalotakiwa halisemwi; hili hili la vita vya panzi neema kwa kunguru. Usishangae kwa nini ni Waislamu waliosimama barabarani Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja wakawajeruhi vibaya vibaya Waislamu wenzao, pamoja na kuuteketeza Msikiti Mkubwa wa gharama uliopo hapo, kisa Uamsho wasiende Donge, ambako tayari umma wa Wakaazi wa huko na wa maeneo ya jirani walishasheheni kiwanjani kungojea tafakari murua ya nchi

Hanyegwa Mchana, k a t i k a Wi l a y a y a Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. Ni eneo mashuhuri kutokana na gereza la muda mrefu, ingawa si wengi wanaopafahamu hapo, miongoni mwa wakaazi wa visiwa vya Unguja na Pemba. Waislamu wachache ambao wanalitumia eneo hilo kwa harakati zao za kujitafutia riziki za halali, hivi karibuni walipigiwa upatu ili wakaelimishwe juu ya matunda ya Muungano. Walichoshuhudizwa hapo ni harakati ya

Kiwanja kikubwa kinauzwa. Kipo katika eneo zuri la kuweza kufanya biashara, makazi au shughuli nyingine yoyote muhimu ya kimaendeleo. Kimepimwa na kupewa Namba Knd/tnd/ktb3/9. Kipo Mtaa kwa Tumbo Kata ya Tandale Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam. Kwa mawasiliano zaidi: 0787 463400

KIWANJA KINAUZWA

AN-NUUR

MASHAIRI/MAKALA

SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012

11

DINI NA SIASA HAVITENGANI


1. Salamu aleykumu, Waislamu jamia, Naja na jambo muhimu, kwenu kulifafanua, Hili ni swala adhimu, juu yenu kulijua, Naja kwenu fafanua, kusu dini na siasa. 2. Kuhusu dini na siasa, huwezi kuviambua, Kila neno yanipasa, fasiri yake kutoa, Kuepuka ububusa, katika kuyaendea, Naja kwenu fafanua, kusu dini na siasa. 3. Kwanza naanza na dini, tafsiri kuwambia, Hili neno la kigeni, la lugha ya Arabia, Kupitia Kur`an, tarjumu naitoa, Naja kwenu fafanua, kusu dini na siasa. 4. Neno dini ni mfumo, wa maisha kwa jamia, Tatu themanina tano, kur`an we fungua, Aya zipo nyingi mno, neno dini zachambua, Naja kwenu fafanua, kusu dini na siasa. 5. Dini zipo nyingi mno, za watu na ya Jalia, Za watu ziso mifano, kama uyoga za kua, Zipo kwenye mashindano, wafuasi kuvutia, Naja kwenu fafanua, kusu dini na siasa. 6. Dini iliyo ya Mungu, hii ya ISLAMIA, Dini ya tangu na tangu, kwa Adamu na Hawia, Yaletwa kwa walimwengu, kufuata yake njia, Naja kwenu fafanua, kusu dini na siasa. 7. Sasa ninahitaji, maana pia kutoa, Mtulie kama maji, mtungini yalopoa, Usemi wawahitaji, haya kuyazingatia, Naja kwenu fafanua, kusu dini na siasa. 8. Siasa uendeshaji, wa mambo kwenye jamia, Bila siasa taraji, mambo kombo kukwendea, Utakuwa ufujaji, malengo kutokia, Naja kwenu fafanua, kusu dini na siasa. 9. Huwezi kutenganisha, dini na siasa jua, Vyote vyahusu maisha, ya watu kwenye dunia, Siasa inaendesha, mambo mlopangilia, Huwezi kutenganisha, dini na siasa jua. 10. Kuna sisa za watu, wao wamejibunia, Hizi ni siasa butu, kinyume na ya jalia, Kwa kweli hazithubutu, vyema kukuendea, Huwezi kutenganisha, dini na siasa jua. 11. Na mengi ya kueleza, ila hapa natulia, Kama mwataka uliza, ili kwa kina kujua, Namba zangu nawajuza, mpate kunipigia, Huwezi kutenganisha, dini na siasa jua. 12. Ziro saba moja tisa, ni namba za kwanza, Nane nne bila kosa, hizi zinajalizia, Nane nane nazitosa, mbili saba yaishia, Huwezi kutenganisha, dini na siasa jua. Abdul-karim Mbunju. Dar es salaam.

Inatoka Uk. 12

MUM yapiga hatua


walimu toka Marekani na Misri. Chuo kina madarasa na kumbi nzuri za kufundishia, library kwa ajili ya kupata vitabu mbalimbali vya rejea, internet ya wire na wireless. Maabara ya sayansi na lugha kwa ajili ya wanafunzi wa masomo ya sayansi na lugha. Chuo Kikuu cha Waislamu kina hosteli za kutosha kwa ajili ya malazi kwa wanafunzi na hasa

Universities (AAU) na na mtandao wa vyuo vikuu vya jumuiya ya madola yaani Commonwealth Universities (CU). Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kina walimu wenye uzoefu na utaalamu wa kutosha kutoka ndani na nje ya nchi. Chuo kina walimu wa sayansi toka nchini Cuba, Australia na pia Chuo kinatarajia kupata

kipaumbele kinatolewa kwa wanafunzi wa kike, walemavu na wanafunzi kutoka nje ya nchi. Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kina mpango wa kuanzisha masomo ya ngazi ya Masters katika eneo la Kigamboni Dar es Salaam, kuanzisha masomo ya cheti na diploma na pia kuanzisha Chuo cha utati wa urithi wa mambo ya kale Kilwa Masoko, Mkoani Lindi.

Moja ya hostel za wanafunzi Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro.

Jengo la Utawala Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro

AN-NUUR
SHABAN 1433, JUMANNE JUNI 26-28, 2012 CHUO Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) kilianzishwa rasmi mwaka 2004, Chuo kinamilikiwa kisheria na Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu nchini (Muslim Development Foundation MDF). Chuo kilianza udahili mwaka 2005 na kilianza na jumla ya wanafunzi 167 kikiwa na degree program tatu ambazo ni Bachelor of Arts (Education), Bachelor of Arts (Mass C o m m u n i c ation) n a Bachelor of Islamic Studies with Education. Miaka minne baadae, Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kiliongeza degree programu nne na kufanya jumla ya program hizo kuwa saba. Programu zilizoongezwa ni pamaja na Bachelor of Science (Education), Bachelor of Law with Shariah, Bachelor of Business Studies na Bachelor of Languages and Interpretation. Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kina jumla ya wanafunzi 3093 ikiwa ni pamoja na wanaume 1196 na wanawake 1897. Ta n g u k u a n z i s h w a Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kimeshatoa wahitimu zaidi ya 900 ambapo wanafanya kazi sehemu mbalimbali serikalini, mashirika ya umma na katika taasisi binafsi. Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro ni mwanachama wa jumuiya mbalimbali zilizopo ndani na nje ya nchi. Jumuiya hizo ni pamoja na Tanzania Commission for Universities (TCU), Tanzania Association for Private Universities (TAPU), Committee of Vice Chancellors and Principals in Tanzania (CVCPT). Jumuiya za nje ni pamoja na Inter University Council for East Africa (IUCEA), Association of African
Inaendelea Uk. 11

Soma AN-NUUR kila Ijumaa na Jumanne

MUM yapiga hatua

Serikali kuwaadhibu Mafanikio kuanzia 2005 2012 wachafuzi wa mazingira


MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali italazimika kutumia ukali na kuondoa muhali kwa watu wanaoendeleza vitendo vya uchafuzi wa mazingira hasa katika vianzio vya maji. Amesema ni hatari kuona vitendo hivyo vikiendelea huku taifa likikabiliwa na uhaba wa maji unaotokana na uharibifu wa mazingira katika vianzio hivyo. Akiwa katika ziara ya kutembelea vianzio vya maji katika chemchem ya Mtopepo, Maalim Seif ametahadharisha kuwa ikiwa vitendo hivyo vitaachiwa kuendelea, kuna hatari ya taifa kuwa na upungufu mkubwa wa maji katika miaka michache ijayo. Inabidi sasa tuwe wakali ili isije ikaka wakati tukawa hatuna maji katika nchi yetu, alitahadharisha Maalim Seif. Amesema katika kudhibiti hali hiyo, serikali itachukua kila aina ya tahadhari kuhakikisha kuwa vianzio vya maji haviendelei kuharibiwa kwa maslahi ya vizazi vijavyo na taifa kwa ujumla. Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Mustafa Ali Garu amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kwa sasa ni uvamizi wa ujenzi karibu na vianzio vya maji, hali inayopelekea mfumo wa uzalishaji wa maji kubadilika na kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha maji katika chemchem. Kwa upande wake Mhandisi wa Mamlaka hiyo injinia Said Saleh amesema baadhi ya chemchem ndogo ndogo zimeanza kutoweka, na kutaka tahadhari zaidi zichukuliwe katika kudhibiti uvamizi wa vianzio hivyo. Amefahamisha kuwa karibu nusu ya kiwango cha maji yamepungua katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kutoka katika chemchem za Mtotopepo na Mwanyanya, huku chemchem ya Mtopepo ikiwa na upungufu mkubwa zaidi. Ziara hiyo pia imemshirikisha Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdallah Shaaban. (Habari kwa hisani ya Ikulu, Zanzibar)

Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu wakiwa katika picha ya pamoja

Ania Margarita (Kutoka Cuba) akiwa na wanafunzi wake

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagaration Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like