You are on page 1of 4

Maombi yote yaanze kwanza kwa ushirika na Roho Mtakatifu katika sifa na kuabudu pamoja na

kushukuru, hakikisha umeunganika na Mbingu kabla ya kuanza kuomba.

Zingatia
Hakikisha umesoma andiko unalosimamia kabla ya kuanza kuomba, kumbuka Mungu analiangalia
neno lake apate kulitimiza.

SIKU YA 11.
A) Kumiliki Malango Ya Mtaa
1. Kumbu 12:2-3. Baba katika jina la Yesu, ninaamuru moto wa Mungu juu ya miungu, sanamu,
matambiko, maashera na madhabahu ya uovu Kimara, tunaamuru malango ya Kimara kuifungukia
Redeemers Assembly katika jina la Yesu.
2. 1 Wafalme13:2.Kwa Damu ya Yesu ninatabiri kinyume cha madhabahu ya wachawi na kila mahali
pa juu katika mtaa wa Kimara, Ee madhabahu na kiti cha wachawi teketea kwa moto na kuwa majivu
katika jina la Yesu.
3. Waamuzi 7:18.Baba katika jina la Yesu tunatangaza upanga wa Bwana na upan ga wa Redeemers
Assembly juu ya makuhani wa giza Kimara wanaoshindana na mafanikio ya Redeemers Assembly
katika jina la Yesu.

B) Kuombea Mwaka Wa 8 Wa Redeemers Assembly


1. Waefeso 5:16.Kwa Damu ya Yesu tunakomboa kila sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi na
mwaka wa nane wa Redeemers Assembly tunatangaza kwamba viumbe vyote na majira vitaitumikia
Redeemers Assembly katika jina la Yesu.
2. Isaya 54:3. Ee Baba katika jina la Yesu, sababisha huduma hii kuenea bila vizuizi pande zote za Dar
es salaam na Tanzania mwaka huu wa nane kwa kibali chako katika jina la Yesu.
3. Hesabu 11:31. Ee Baba kwa upepo wa Roho Mtakatifu peperusha na kukusanya rasilimali zote,
Fedha, watu, fursa na wakati vinavyohitajika kutimiza maono haya katika mwaka wa nane wa
Redeemers Assembly katika jina la Yesu.

SIKU YA 12.
A) Kongamano La Mwanzo Mpya Tarehe 15 Hadi 20 Mwezi Wa Nane.
1. 1 Samweli 3:21.Ee Baba katika jina la Yesu jifunue tena kwetu kwa viwango vipya, tuonyeshe
utukufu wako katika kongamano letu la mwanzo mpya mwaka huu katika jina la Yesu.
2. Isaya 45:8.Ee Baba katika jina la Yesu fungua mbingu zako juu ya kongamano letu la New
Beginning, sababisha kamba zetu kutuangukia mahali pema katika mipango yote katika jina la Yesu.
3. Isaya 41:15. Ee Baba mwandae mtumishi wako Emanuel kupita kawaida kwa ajili ya hili
kongamano, mfanye chombo kipya kikali cha kupuria na ukombozi katika jina la Yesu.

B) Ubatizo Wa Pendo La Mungu Juu Ya Kila Mshirika Redeemers Assembly.


1. Warumi 5:5.Ee Baba mbatize kila mshirika wa Redeemers Assembly na upendo wa Mungu
usiozimika katika jina la Yesu.
2. 2 Wafalme 10:16.Ee Baba mbatize kila mshirika wa Redeemers Assembly na wivu wa nyumba
yako utakaosababisha kuwavutia watu wengine kumfuata Yesu katika jina la Yesu.
3. Ufunuo 3:16. Baba katika jina la Yesu tunakemea kila roho za uvuguvugu na ubaridi katika
kukutumikia Redeemers Assembly, Ee Baba washa moto wako ndani ya kila mshirika usizimikekwa
ajili ya ufalme wako katika jina la Yesu.

SIKU YA 13.
A) Kuombea Tanzania.
1. Mathayo 6:9.Ee Baba katika jina la Yesu, tunaomba ufalme wako uje Tanzania ndani ya Bunge,
Mahakama, Serikali, Vyuo vikuu, Mashuleni, Mikoani katika jina la Yesu.
2. Kumbu 12:1-3.Ee Baba inuka tuma malaika wako wavunje madhabahu ya uchawi na uganga
iliyolishilia Taifa la Tanzania na watu wake katika umasikini katika jina la Yesu.
3. 1 Wafalme 3:12.Ee Baba mpe Raisi Joseph Magufuli na Mawaziri wake hekima na akili ya
kulitawala na kiliongoza Taifa hili katika njia zako katika jina la Yesu.

B) Kuombea Uchaguzi wa Kenya Mwezi wa 8 Tarehe 8.


1. Zaburi 16:5-6.Ee Baba inuka kwa ajili ya Taifa la Kenya, ishike kura yake na kusababisha uongozi
wa hili Taifa kuangukia mikononi mwa watu sahihi katika jina la Yesu.
2. Ayubu 34:22. Ee Baba achilia nuru yako ya haki imulike kwenye uchaguzi wa Taifa la Kenya,
kusiwe na chochote kitakachofanywa gizani kuhatarisha amani ya Taifa katika jina la Yesu.
3. Mwanzo 11:1,7.Ee Baba katika jina la Yesu, tunakemea roho ya babeli inayozuia mshikamano na
umoja katika uchaguzi wa Kenya, ninaamuru amani na umoja Kenya katika jina la Yesu.

SIKU YA 14.
A) Kuangusha Madhabahu Ya Uovu Katika Familia Yako.
1. 1 Wafalme 13:1-2. Ee Baba katika jina la Yesu, inuka kwa mfungo huu kwa ajili ya familia yangu,
ninalaani madhabahu ya uovu iliyotushikilia mateka katika ulevi, uzinzi, mitala, umasikini, uchawi,
teketea kwa moto na kuwa majivu katika jina la Yesu.
2. Isaya 49:24-26.Wewe kuhani muovu wa madhabahu ya ukoo wangu, unayenuiza na kutoa kafara
kinyume cha mafanikio yetu, Bwana Yesu anakupokonya familia yangu leo na wewe utalishwa nyama
yako na kunywa damu yako katika jina la Yesu.
3. Zekaria 9:11-12.Kwa Damu ya Yesu ninamuamuru kila mmoja katika familia yangu kutoka katika
gereza na shimo la mateso siku ya leo katika jina la Yesu.

B) Kuitiisha na Kuitawala Dar es salaam.


1. Kumbu 2:36. Baba katika jina la Yesu, inuka kwa ajili ya Redeemers Assembly, Dar es salaam,
tunateka anga, ardhi na maji kwa ajili ya ufalme wako katika jina la Yesu.
2. Isaya 45:1-2. Ee Baba inuka kwa ajili ya Redeemers Assembly na watu wake, legeza viuno vya
wafalme na kutufungulia mlango kwa kila wizara na taasisi na mitaa ya Dar es salaam katika jina la
Yesu.
3. Ee Baba tupe ufunguo wa Dar es salaam kwa ajili ya jina lako katika jina la Yesu.

SIKU YA 15.
A) Kuombea Kanisa la Kristo Dar es salaam.
1. Yoshua 5:9. Ee Baba inuka viringishia mbali aibu ya kanisa lako Dar es salaam majengo mabovu,
watu wachache, umasikini wa washirika na wachungaji, geuza umateka wetu katika jina la Yesu.
2. Isaya 2:2-3. Ee Baba inua mlima wa nyumba yako Dar es salaam, uweke imara juu ya madhabahu
za uchawi na uganga, acha watu walijilie kanisa lako Dar es salaam makundi makundi katika jina la
Yesu.
3. Mambo ya walawi6:12. Ee Baba katika jina la Yesu, washa moto wako juu ya madhabahu ya
kanisa lako Dar es salaam, usababishe uwake daima wala usizimike.

B) Kuombea Mafanikio ya Washirika wa Redeemers Assembly.


1. Isaya 60:22. Ee Baba inuka mfanye kila mshirika wa Redeemers Assembly mara elfu pande zote
katika jina la Yesu.
2. Zaburi 146:16. Ee Baba mfumbulie kila mwanabishara na mwanataaluma mkono wako wa utajiri
katika jina la Yesu.
3. Malaki 3:10-11. Ee Bwana kwa wote wanaolipa zaka Redeemers Assembly, fungua madirisha ya
Mbinguni juu ya kazi ya mikono yao na kuwamwagia Baraka zisizo na kipimo, kwa ajili yao kemea
yeye alaye asiharibu kazi yao wala mitaji yao isipunguke katika jina la Yesu.

You might also like