Professional Documents
Culture Documents
ANIMATION OF WEDDING
MASS FOR
2015.
“Siondoki Kando
Yako Na Usiondoke Kando Yangu Hadi Kifo
Kitutenganishe.
1
PROCESSION.
NALIFURAHI SANA
Nalifurahi sana waliponiambia na twende nyumbani ,
Nyumbani mwake ee Bwana x2
1. Miguu yetu imesimama katika malango ya Yerusalemu oh
2. Yerusalemu mji uliyojengwa kama ule mji ulioshikamana oh
3. Makabila yote ya Israel, walishukuru jina lake bwana oh
4. Mmewekwa hukumu ya haki katika ukoo wa mfalme Daudi oh
5. Utakieni Yerusalemu amani , na wafanikiwe wakupendao oh
6. Kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu ninakuomba upate fanaka oh.
MWIMBIENI BWANA
2
UTUHURUMIE (Mitume mass)
Bwana utuhurumie
Sisi wakosefu Bwana – Bwana utuhurumie x2
Ee kristu (ee kristu) kristu utuhurumie-ie
Bwana utuhurumie
Sisi wakosefu Bwana – bwana utuhurumie x2.
UTUKUFU(MITUME MASS)
MASOMO
NASIKIA SAUTI.
Umeniita, nimeitika wito, nakuja kwako leo Najongea mbele zako Bwana
nipokee mimi Niko tayari, nimeyaacha yote, najikabidhi kwako Unitume
popote na mi nitakwenda haraka
3
2. Ninaenda mimi naenda, ninaenda mwenyewe, Ninaenda mbele za Bwana,
sitarudi nyuma
Ndugu zangu na marafiki, mniache niende, Nikafanye kazi ya Bwana,
nitakapotumwa
3. Nilitazama moyo wako, moyo wako mwanangu, Hata kabla hujazaliwa,
nilikutambua
Nilikuteua mapema kati ya ndugu zako, Uwe kuhani wangu mimi, kuhani
mkuu
4. Shamba lake Bwana ni kubwa na mavuno ni mengi, Wavunaji ndio
wachache nitakwenda mimi
Nakuomba sana ee Bwana, nipeleke shambani, Nikavune mavuno yote
yaliyo tayari.
5. Uwe nami siku kwa siku, Bwana usiniache, Unikinge na majaribu nilinde
daima
Nipeleke habari njema, ulimwenguni mwote, Watu wote wakutambue,
wakugeukie
1. Neno hili la bwana ndilo njia ya wokovu wetu, (yatupasa nasi sote
tulipokee)X2
2. Neno hili la bwana ni faraja ya watesekao, (yatupasa nasi sote
tulipokee)X2
3. Neno hili la bwana nit ulizo la moioyo yetu, (yatupasa nasi sote
tulipokee)X2
4.Neno hili la bwana ndilo taa la maisha yetu, (yatupasa nasi sote
tulipokee)X2
UNINYUNYIZIE MAJI
1. Uninyunyizie maji (Bwana) *2
Unioshe nitakate (kweli) Niwe mweupe kabisa *2
2. Mimi ni mwenye dhambi (Bwana) *2
Unioshe nitakate (kweli) Niwe mweupe kabisa *2
3. Natamani nije kwako (Bwana) *2
Unioshe nitakate (kweli) Niwe mweupe kabisa *2
4
4. Naingia nyumba yako (Bwana) *2
Unioshe nitakate (kweli) Niwe mweupe kabisa *2
5. Niuone uso wako (Bwana) *2
Unioshe nitakate (kweli) Niwe mweupe kabisa *2
6. Nifurahi milele (Bwana) *2
Unioshe nitakate (kweli) Niwe mweupe kabisa *2
WEDDING SONGS
HARUSI KIDEDEDEDE
1. Bwana harusi na bibi harusi , leo mmefunga ndoa ya maisha kaeni kwa
amani kidededede.
Tenor: upendo wenu umethihirika - Uyani kwenu bamba ishini
tototo
Uzuri wenu hakuna kifani……………….
Na nyumba yenu imebarikiwa……………
2. Jitulizeni mjizikie sukari, siku ya leoni yenu furahini mmepambwa maua
mnapendeza.
3. Bwana harusi pagawa changamka, Bibi harusi chachawa, chezacheza,
penzi lenu leo limekamilika.
4. Mapenzi yenu kweli yatasitawi, haiku yatasitawi yatamea kama ule
mwerezi wa Lebanoni.
5. Baraka zake Mungu ziwashukie, kaeni pasipo shida siku zote nyumba
yenu iwe hekalu la Mungu.
5
1. Pokea hii pete ee mwenzangu, iwe ishara ya pendo langu, na uaminifu
wangu kwako.
Nakupenda hakikaNakupenda ajabu Wewe wangu daima mimi wako
wewe
Tutahishi pamojaTutakula pamoja- hadi kifo kifike kitutenganishe
X2.
2. Jukumu langu ni kukupenda, wakati war aha na shida, na wewe kwangu
weka heshima.
3. Safari hii ndefu ya maisha,imeanza leo siogope tutatembea bila kuchoka.
4. Milima na mabonde ya maisha, tutapanda tena tutashuka tukiwa pamoja
siku zote.
HERI YENU
Heri yenu ninyi msitengane oh mkavunje ile agano x2
Mungu amewaonganisha binadamu asiwatenganishe x2
1. Na mwanamke atawacha wazazi wake, ataungana na yule mume wake x2
2. Na mwanamme atawacha wazazi wake , ataungana na yule mke wake x2
3. Na bwana Mungu alimuumba Adamu, akampa Hawa awemsaidizi wake
x2
4. Alicho unganisha Mungu baba mwenyezi hakuna atayeitenganisha x2
5. Mue na upendo mkaishi kwa amani, na Mungu baba ataibariki ndoa yenu.
TEMBEA POLEPOLE
1. Tembea polepole, tembea baba tembea kwa madaha, tembea mama
ingia hekaluni mwa mungu wetu mpate kutimiza ahadi zenu
2. Harusi hii ya leo ni yako bwana, mapambo haya yote ni yako bibi,
upendo uzidishe kwa bibi yako heshima uongeze kwa bwana wako.
6
5.Mkeo atakuwa kama zabibu ,uzaao matunda nyumbani mwako
,watoto muwapende na kuwalinda,muwafundishe yale ya uwinguni.
SADAKA
WE DO GIVE TO GOD
We do give to God, the splendid Lord; we do pray you Lord, our grand
joyous gifts, then Lord we shall sing of your gracious life.
1. Bread and wine we offer to the living Lord,
Together in joyful tide praise him God of love
2. Our hearts we offer to the living Lord
Together in joyful tide praise him Lord of love
3. Our joy we offer to the living Lord
Together in joyful tide praise him Lord of love
4. Our world …………………………………..
5. Our wealth …………………………………..
6. Our love ……………………………………….
7. Our lives …………………………………….
ACHENI VISINGIZIO
Bass: (Acheni visingizio wanadamu)X2
Wote:(Acheni visingizio kwamba hali ngumu)X2 (Nendeni mkatoe )X2
Nendeni mkatoe sadaka kwa bwana}X2
7
ANAMIYIANG’O
Anamiyiang’o nyasae wuora madimo riga, inmichiwo ngima mane Adamu
wuora noseko gawito x2
(Abiro giilo (duto), Abiro ging’uono (bende)Abiro gimor (koro) akilo mich
mawangolo )x2
1. Pesa mawagole ofuke wan wakelogi gimor ye igweth gi jalamo
wanwakelogi giera
2. Cham mawagolo e pwothe…………………………..
3. Mwandu mawagolo e miere……………………………
4. Rombe mawagolo e kunde ……………………………..
5. Thok mawagolo e kunde …………………………………
(TN: kwa kutukomboa) asante asante (BS: kutuweka huru) asante asante
MTAKATIFU(MITUME MASS)
Mtakatifu bwanaX3 Mungu wa majeshi, Mbingu na dunia( kweli zimejaa)X2
Utukufu wako.
8
AMINA
Amina x5
AMANI
MAK’ TINGA
1. Bass; makting’a tingi, teyong’ x2
Ee rwoth’ rubang’ maktinga tingi teyong’
Menyut rwoth rubang’ moru wadutu x2
2. Makting’a ting’i aduong’ x2
3. Makting’a ting’i amin x2
KUPOKEA
AMETUALIKA
Ametualika kwenye karamu yake bwana tule mwili wake bwana tunye
damu yake, tumejaaliwa sote chakula cha roho zetu bwana anatuita kutushibisha
roho zetu.
i. Mwili wake bwana yesu ni chakula cha roho zetu, damu yake
bwana yesu ni kinywaji cha roho zetu, kilichoshuka kutoka kwa
baba waumini wote tujongee meza ya bwana tukale chakula cha
mbinguni.
ii. Njoni maskini maskini, viwete, vipovu na wagonjwa meza
imeandaliwa na bwana wetu yesu kristu kwa heshima kubwa kwa
upole na kwa unyenyekevu tujongee wote tupate chakula cha roho
ni mwili wake yesu kristu.
9
i. Tazama yesu wangu ninajongea karamu yako, pengine
kwako sikustahili kuijongea –unihurumie ee yesu wangu
unisamehe.
ii. Hakika kwako bwana makosa mengi nimeyatenda,
ubinadamu wangu siwezi kuficha kwako bwana-
unihurumie………….
iii. Ni wazi yesu wangu unaujua udhaifu wangu, sina cha
kujitolea mbele yako ee yesu wangu-
unihurumie………………
TWENDENI MEZANI
I. Angalieni wenyewe tazameni pendo la bwana,
(kweli) Amejitoa mwenyewe awe chakula, anatuita
twendeni tule mwili na tunywe damu, (kweli) ni cha
mbinguni che uzima.
10
V. Milele tutafurahi tutaishi na bwana yesu, tukishinda
majaribu ya ulimwengu, tunapata nguvu nyingi
tunapokula mwili wake , tunashinda majaribu
tukinywa damu.
SHUKURANI
TUNAKUSHUKURU
(Ee bwana mungu baba wetu tunakushukuru kweli{hakika} kwa kutulinda wiki
nzima ee baba asante sana)X2
MWISHO
1) Mungu awajalie , maisha mazuri, muishi kwa amani, siku zenu zoteX2
2) Mkumbukeni mungu, siku zenu zote, ili azibariki, kazi zenu zoteX2
3) Uzao wenu wote, uwe na Baraka, mjaliwe watoto wenye afya njemaX2
4) Palipo na vikwazo, muiteni mungu, atawasaidia, siku zenu zoteX2
CHOIRMISTRESS
EDITOR P. LOKS
11