You are on page 1of 8

Get started Open in app

Judith Mwanri

Follow About

JINSI YA KUFANYA MAKADIRIO YA


GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA YAKO
— S1
Judith Mwanri May 10, 2020 · 5 min read

SEHEMU YA KWANZA: MAHESABU YA IDADI YA TOFALI ZINAZO HITAJIKA


KWAAJILI YA UJENZI WA MSINGI NA KUTA (TOFALI ZA BLOCK)

Habari wana Ujenzi!, nimegundua watu wengi wanapata changamoto ya kufahamu


makadilio ya material wanayo hitaji katika ujenzi wa nyumba ama majengo mbalimbali.
Kwasababu hiyo nimeamua kuanza mfululizo wa kutoa elimu hiyo na leo tutaanza na
mahesabu ya idadi ya tofali zinazo hitajika kujenga

Kabla haujaanza kufanya mahesabu lazima uwe na vitu vifuatavyo

1. Uwe na ramani yenye vipimo ili kujua ukubwa wa jengo lako. Ramani inachorwa na
wasanifu majengo wataalamu ambao wanasomea — wataalamu hawa wanahitimu
katika vyuo vinne tu hapa nchi navyo ni Ardhi University (chuo kikuu), na vyuo vya kati
Ardhi Institute — Tabora, Ardhi Insitute — Morogoro, Institute of Lands Dar es Salaam.

2. Ufahamu aina ya material ama tofali utakazo tumia, kama ni hydraform, tofali za
kuchoma ama blocks, hii ni kwasababu tofali zina tofautiana size ama ukubwa hivyo
hata idadi yake itakuwa tofauti. Tofali zipo za aina tatu, ukubwa wake ni (length x width
x thickness/urefu x upana x unene)
HYDRAFORM; 90 mm x 240 mm x 40 mm
Get started Open in app

BLOCK; 450 mm x 230 mm x 130 mm

KUCHOMA; 450 mm x 230 mm x 150 mm

Hapa tuta tumia mfano wa nyumba hii yenye vyumba viwili-kimoja kikiwa na choo/bafu
ndani, sebule, jiko, choo cha wageni na vibaraza viwili; kufanya mahesabu ya tofali zetu.

Hapa kuna hatua mbili za kufuata

1. Tafuta eneo la kuta zote

2. Jumla ya eneo lote la kuta gawanya kwa ukubwa wa tofali


KUTAFUTA ENEO LA KUTA
Get started Open in app

Hapa tuta tumia kanuni ifuatayo

Eneo = Urefu( wa kuta) x kimo (urefu wa ukuta kwenda juu)

Sasa kujua urefu wa kuta zote, utatakiwa kujumlisha urefu wa kuta zote

Kwenye mchoro wetu pale juu nime weka namba kila kuta hivyo itakuwa kama
ifuatavyo {vipimo vipo katika milimita (mm)}.

1 m = 100 cm = 1,000 mm; 1 cm = 10 mm

Ukuta 1= 6,500 mm; ukuta 2 = 9,150 mm; ukuta 3 = 4,000 mm; ukuta 4 = 4,000 mm;
ukuta 5 = 9,450 mm

Ukuta 6=11,046 mm, ukuta 7=6196 mm +3200 mm, ukuta 8=9,101 mm, ukuta 9
=3,060 mm, ukuta 10 = 2,900 mm

Sasa uki jumlisha kuta hizo zote unapata jumla ya = 68,603 mm

Eneo la kuta = urefu wa kuta x kimo cha kuta

Hapa kama utajenga nyumba ya kozi 13 maana yake ni kimo cha 3000 mm

Hivyo eneo litakuwa = 68,603 x 3000= 205,809,000 mm

Sasa kumbuka tuna sehemu za wazi ambazo hizi hazihitaji tofali, mfano milango,
madirisha na sehemu za wazi za vibaraza

Kanuni ni ile ile urefu x kimo:

Tuna madirisha 6 yenye urefu 2,000 mm & kimo 1,800 mm= 2000 x 1800 sawa na
3,600,000 mm

sasa, tuna madirisha sita yenye vipimo sawa hivyo 3,600,000 x 6 = 21,600,000

Tumia dirisha 1 lenye urefu 1,400 na kimo 1,500 = 1,400 x 1500 sawa na 2,100,000
mm
Tuna dirisha 1 lenye urefu 1,000 na kimo 1,800 = 1,000x1, 800 sawa na 1,800,000 mm
Get started Open in app

Tuna madirisha 2 yenye urefu wa 800 na kimo 600 = 800x600 sawa na 480,000 mm

480,000 zidisha kwa 2 sawa na 960,000 mm

Tuna milango 9 yenye urefu wa 900 na kimo 2,400 = 900 x 2,400 sawa na 2,160,000
mm

2,160,000 zidisha kwa 9 sawa na 19,440,000 mm

Uwazi wa vibaraza jumla uref 10,010 kimo 2,400 =10,010 x 2,400 sawa na 24,024,000
mm

Jumla ya wazi = 21,600,000 + 2,100,000 + 1,800,000 + 960,000 +19,440,000 +


24,024,000 = 69,924,000 mm

Eneo kamili linalo hitaji tofali za kuta lita kuwa

ENEO LA KUTA — ENEO LA WAZI0 = 205,809,000–69,924,000= 135,885,000 mm

hivyo basi, IDADI YA TOFALI, itakuwa kama ifuatavyo:

Sasa urefu wa msingi wako utategemea na nature ya eneo lakini tuchukulie utakuwa na
urefu wa 900 mm, ambapo ni sehemu tambarare (isiyo koro )

Kumbuka jumla ya urefu wa kuta zote ni 68,603 mm

Kwahiyo 68,603x900 = 61,742,700 mm

Kwahiyo kupata tofali tutalazimika kuchukua jumla ya ukubwa wa kuta ukiwa umetoa
uwazi na jumla ya eneo la kuta za msingi kisha tuta gawanya kwa eneo la tofali moja

135,885,000+61,742,700= 197,627,700 mm

Kumbuka tofali ya block lina urefu wa 450 mm na kimo cha 230 mm

Hivyo eneo la tofali ni 450 x 230=103,500 mm


Idadi ya tofali itapatikana kwa 197,627,700mm/103,500mm = 1,909 matofali
Get started Open in app

Hapa utahitaji kuongeza asilimia kidogo ya tofali kwaajili ya zile zitakazo vunjika na
ngazi pia, tutatumia 5%, kwahiyo jumla ni tafali 1909+ 0.05(1909) = 2,004.45 ≈
2,000 tofali

MAHESABU YA IDADI YA MIFUKO YA CEMENT NA MCHANGA INAYO HITAJIKA


KUJENGEA NYUMBA YAKO

hapa tunaingia sehemu nyingine ambayo itahusu ukadiliaji wa idadi ya mifuko ya


cement itakayo hitajika kujengea jengo lako.

NB: kumbuka haya huwa ni makadilio, hivyo sio lazima yawe sawa kwa asilimia 100,
lakini mara nyingi yanakaribia ukweli halisi kwa asilimia kubwa sana

Tukichukulia mfano wa TOFALI 2,000

Hapa nazungumzia tofali ambazo wengi wanaziita za block, ambazo kitaalamu zinaitwa
SAND CEMENT BLOCKS

Hapa tuseme idadi ya tofali za Msingi (inch 6) ni tofali 700

Idadi ya tofali za kuta (inch 5) ni tofali 1300

A: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA MSINGI (TOFALI ZA INCH 6)

-Ikumbukwe hapa tofali hizi hujengwa kwa kulazwa

-hivyo tofali hizi zitahitaji cement na mchanga Zaidi kuliko zile za kusimama (inch 5)

KANUNI

Mfuko 1 wa cement unajenga tofali 45 za msingi (inch 6- za kulaza)

Hivyo ukichukulia zile tofali 700 za msingi kwenye ule mfano wetu itakuwa ifuatavyo

Tofali 700 gawanya kwa 45 = 15.5 sawa na mifuko 16 ya cement


NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 50 ama 60
Get started Open in app
za msingi za kulaza). Hii hufanywa ili kupunguza gharama japo kama ni kwenye
kiwanja koro inaweza kuleta shida.

B: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA KUTA (TOFALI ZA INCH 5)

-Tofali hizi mara nyingi hujengwa kwa kusimama hivyo hazili mchanga na cement
nyingi kama zile za msingi

KANUNI

Hapa mfuko 1 wa cement unajenga tofali 60 za kuta (inch 5- za kusimama)

Hivyo ukichukulia tofali 1,300 za kuta kwenye ule mfano wetu, itakuwa kama ifuatavyo

Tofali 1,300 gawanya kwa 60 = 21.6 sawa na mifuko 22 ya cement

NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 70 mpaka
90 za kuta, za kusimama), pia hii ni ili kupunguza gharama.

NB: KIPIMO CHA MCHANGA

Mfuko 1 wa CEMENT una changanywa na NDOO 9 kubwa za MCHANGA

Ama mfuko 1 wa CEMENT unachanganywa na NDOO 18 ndogo za MCHANGA


Get started Open in app

Katika makala ijayo tutaendelea na kujumlisha gharama za usa rishaji, gharama za


maligha ya kumalizia nyumba ( nishing) na nyinginezo.

Tunatoa ushauri wa kitaalam na kufanya ujenzi, usanifu majengo


(ramani) & kukadiria gharama za ujenzi. Tafadhali tuandikie maoni (comment) yako
hapo chini & kisha washirikishe (share) na wengine makala hii.

Karibu!
Get started Open in app
Ujenzi Nyumba Tanzania Makadirio Ya Gharama Construction Costing

About Help Legal

Get the Medium app

You might also like