Nimepitia dokezo la uanzishwaji na uendeshaji wa mradi wa mafuta na kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kuwasilisha mchango wangu kwa maandishi kama ifuatayo; 1. Eneo la mradi limewekewa TZS;360,000,000=, kuonyeshwe mchanganuo kwamba kitajumisha ununuzi wa eneo lenyewe, gharama za ufutiliaji, gharama za uhaulishaji kutoka katika jina la muuzaji kuja katika jina la UTAHIZA, gharama za Sheha, mwanasheria na kwa kuwa katika dokezo hakuna kipengere cha usafishaji/ ushindiliaji wa eneo, nashauri kijumuishwe katika gharama hii kama kikihitajika. 2. Ujenzi wa ofisi imewekewa TZS;107,591,000=, mchanganuo uboreshwe kuonyesha idadi ya vyumba vya ofisi na ukubwa, flour itakuwa ya saruji, terazo au tiles, kama ni tiles zitakuwa za ceramic, porcelain au granite, madirisha yatakuwa PVC, aluminium au mbao, kama ni mbao basi tuseme ya mninga, mkongo na kadhalika, katika paa tusema kama bati za kawaida, slab tukitegemea kuongeza kitu kingine juu, na kadhalika. Muhimu kila kipengere katika ofisi kiguswe wajumbe wawe na taswila ya ofisi wanayotarajia kumiliki. 3. Samani (Furniture and fittings) kimewekewa TZS;2,000,000= kwa tano na kupata jumla TZS;10,000,000=, mchanganuo uwepo kuonyesha samani zinazotarajiwa aina na idadi ya viti, meza, makabati, fittings, na kadhalika, zitakuwa mbao au fibreboard au chuma na kadhalika. 4. Ujenzi wa uzio umewekewa TZS;35,000,000= mchanganuo unahitajika kuonyesha urefu wa ukuta, idadi ya tofali, lovers, na kadhalika zitakazohitajika na kutumika katika ujenzi wa uzio. 5. Uwekaji wa interlock umewekewa TZS; 25,000,000=, mchanganuo unahitajika kuonyesha idadi ya squire meters zitakawekewa na gharama kwa kila squire meter. 6. Uchimbaji na uwekaji wa matank umewekewa TZS; 10,000,000= kwa kila moja na kwa matatu kutagharimu TZS; 30,000,000=, kunatakiwa maelezo kuonyesha kama kwamba bila kujali ukubwa wa tank za gharama za uchimbaji na uwekaji wa matank ziko sawa. 7. Usimamizi wa mradi umewekewa TZS;10,000,000=, kunahijika mchanganuo kuonyesha matumizi yatakavyokuwa yanafanywa kwa kila week na kila mwezi, hatimae kupata ya mwaka mzima. 8. Matumizi; a) Kumeonyoshwa mishahara jumla ya TZS; 7,000,000=, kunatakiwa mchanganuo kuonyesha gharama kwa mwezi hatimae kupata ya mwaka, kwa kuwa TZS;7,000,000=, ukigawa kwa miezi kumi na mbili, TZS;583,333=, hivyo, kumaanisha kwamba muundo wetu wa mishahara haiko constant throughout the year. b) Kumeonyeshwa michango ya ZSSF asilimia 10% ya TZS;700,000= kunahitajika mchanganuo kuonyesha gharama kwa mwezi na hatimae kupata ya mwaka, hata mishahara yetu haiku constant throughout the year. c) Kumeonyeshwa malipo ya umeme ya TZS;500,000=, kunahitajika mchanganuo kuonyesha gharama kwa mwezi na hatimae kupata ya mwaka, hata hivyo, kiasi hicho ni sawa na TZS;41,667=, kwa matumizi ya kituo cha mafuta ni kidogo sana. d) Kumeonyeshwa malipo ya ZRB ya dola 1000 kuzidisha exchange rate ya TZS;2,300, utapata TZS;2,300,000=, lakini katika matumizi kumewekwa TZS;191,666.67, kunahitajika maelezo. e) Kumeonyeshwa malipo ya ZURA ya dola 500 kuzidisha exchange rate TZS;2,300=, utapata TZS;1,150,000=, lakini katika matumizi kumewekwa TZS;95,833.33, kunahitajika maelezo. f) Haukupunguza gharama za usimamizi wa mradi, ambazo umeweka TZS;10,000,000=, ni sehemu ya gharama za uendeshaji zitapunguza faida tarajiwa. g) Haukuonyesha gharama za maji, kwa mwezi na hatimae mwaka, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. h) Haukuonyesha gharama za BIMA, kwa mwezi na hatimae mwaka, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. i) Haukuonyesha gharama za SDL, ambazo ni asilimia 5% kwa kila mwezi kwa jumla mishahara yote kwa mwajiri mwenye wafanyakazi kuanzia wanne, hivyo, 5% ya TZS;7,000,000= na kupata TZS;350,000=, jumla TZS;4,200,000= kwa mwaka, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. j) Haukuonyesha gharama za ulinzi, haukusema kwamba katika mishahara kuna sehemu ya malipo ya mishahara ya ulinzi, kama haipo ionyeshwe, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. k) Hakuonyesha depreciation formula na rates zitakazotumika, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. l) Haukuonyesha gharama za auditors, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. m) Haukuonyesha gharama za simu, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. n) Haukuonyesha gharama za stationary, wino, kalamu na kadhalika, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. o) Haukuonyesha gharama za viburudisho katika vikao vya wawekezaji au wafanyakazi, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. p) Haukuonyesha gharama ya vifaa usafi, cleaning materials, ni sehemu ya gharama za uendeshaji, zinapunguza faida tarajiwa. 9. Haukuonyesha baada ya kupunguza matumizi na kupata faida, malipo yatakayofanywa TRA kama kodi, income tax katika biashara ya mradi wa mafuta ambayo ni asilimia 30% ya faida yote. 10. Haukuonyesha mgawanyiko wa faida baada ya kodi, asilimia ya kubaki katika mradi, kuwa sehemu ya mtaji wa kuendeshea mradi na asilimia itakayogawanywa kwa wawekezaji, ambao utawakata kila mmoja 10% katika malipo yao ya kuwasilisha TRA, kama interest on dividends. 11. Haukuonyesha mchanganuo wa mishahara kurahisisha kutambua wanaowajibika kukatwa PAYE na kuwasilisha TRA, kwa kuwa kisheria, mwajiri yeyote anaelipa mshahara kupindukia TZS;180,000= kwa Zanzibar, lazima akate kwa kiwango kilichobainishwa katika jedwali na kuwasilisha TRA, lakini sio sehemu ya gharama za uendeshaji, hivyo, halipunguzi faida tarajiwa. 12. Dokezo lionyeshe mchanganuo wa mradi kikamilifu katika kila kipengere pamoja na haki, mipaka, wajibu na yawepo makubaliano ya uwekezaji, yawepo maandishi kabla ya uchangiaji watu wajipime na waamue kuwekeza, liwe specific liondoshe maelezo ya jumla jumla. 13. Nashauri kila kipengere kijadiliwe kwa kina, kieleweke, penye mapungufu/ utata pajazwe/ patatuliwe, kurahisisha utekelezaji kulingana na makisio, kuepusha kuvuruga makisio tuliopitisha, tuzingatie kwamba tukishindwa kupanga tumepanga kushindwa.