You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE

Unapojibu tafadhali taja:


Kumb. Na. RDC/ Tarehe: 23.10.2020

Mkurugenzi Mtendaji (W) Rungwe


S. L. P. 148,
TUKUYU.

YAH: TAARIFA YA UJENZI NA UKARABATI WA NYUMBA ZA HALMASHAURI


NYUMBA ZA AFISA UTUMISHI NA AFISA NYUKI

Ukarabati wa nyumba hizi ulianza kutekelezwa kwa kuanza na nyumba moja


ambayo ni ya DHRO na sasa tumeanza kutekeleza nyumba ya DNRO kutoka na
ukarabati huo na uboreshaji wa nyumba hizo baadhi ya vifa havikuwepo kwenye
makisio ya awali.

Vifaa vya awali ambavyo viliangiwa ni kama ifuatavyo:

1. Ukarabati nyumba ya DHRO Tsh. 9.915,100.00 Kiambata na 1

2. Ukarabati nyumba ya DNRO Tsh. 30,504,210.00 Kiambata na 2

Jumla kuu Tsh. 40,419,310.00

Kupitia barua hiyo uliagiza ofisi ya Afisa Elimu na Mhandisi kukagua na kuleta taarifa
mapendekezo na ushauri.

KILICHOONEKANA KWENYE UJENZI HUO.

Chumba kimoja cha ofisi kimejengwa na kufikia usawa wa kuanza kupiga linta/ ring
beam kilichojengwa kwa matofali ya saruji na mchanga (blocks). Ambacho
kinajengwa kwa fedha za wazazi (nguvu za wananchi).

Vifaa vya kuendeleza jengo ambazo ni mbao za linta 1’’x 8’’x 12’ zipo mbao 20,
mbao za kupauwa jengo ambazo 2’’ x 3’’ x12’=30, 2’’x 4’’ x12’= 74, matofali kwa ajili
ya kujenga juu ya linta na mchanga ambao hauna gharama za kuleta kwani
mchanga wa kazi zote unapatika eneo la shule unachimbwa hapohapo eneo la
shule.

Ujenzi wa ofisi umeanza bila kupigwa jamvi.


USHAURI/MAONI.

Kwa kuwa chumba cha ofisi kinahitaji kukamilishwa kazi hizo ziendelee kwa kufuata
utaratibu wa ukamilishaji wa taratibu za ujenzi kwa fundi kupata ushauri wa ofisi ya
Mhandisi ili kuboresha ofisi hiyo ili kusiwepo na gharama zisizokuwa na lazima.

Kamati ya ujenzi ishirikiane na ofisi ya mhandisi ili kuhakikisha ukamlilishaji huo


unaleta tija.

Chumba hicho cha ofisi kikamilishwa kitatatua upungufu wa ofisi katika shule hiyo.

Kwa kuwa wananchi wa Ilundo wamehamasishana katika kutatua kero iliyokuwepo


kwa muda mrefu ikikuwia naomba uwaunge mkono katika kukamilisha ujenzi huu.
Katika mchanganuo wa ukamilishaji ulioambatanishwa na taarifa hii

Pamoja na taarifa hii ofisi ya mhandisi imefanya makisio ya ukamilishaji wa ofisi hiyo
ili itumike kwa muda muafaka.

Nawasilisha kwa hatua zako muhimu,

Eng. Anosisye A. Mwasege

KAIMU MHANDISI WA UJENZI (W)


RUNGWE.

You might also like