You are on page 1of 10

JINSI YA KUFANYA

MAKADIRIO YA GHARAMA
ZA UJENZI WA NYUMBA
YAKO
Judith Mwanri

May 10·5 min read

SEHEMU YA KWANZA: MAHESABU YA IDADI YA TOFALI


ZINAZO HITAJIKA KWAAJILI YA UJENZI WA MSINGI
NA KUTA (TOFALI ZA BLOCK)

Habari wana Ujenzi!, nimegundua watu wengi wanapata


changamoto ya kufahamu makadilio ya material wanayo hitaji
katika ujenzi wa nyumba ama majengo mbalimbali. Kwasababu
hiyo nimeamua kuanza mfululizo wa kutoa elimu hiyo na leo
tutaanza na mahesabu ya idadi ya tofali zinazo hitajika kujenga

Kabla haujaanza kufanya mahesabu lazima uwe na vitu vifuatavyo

1. Uwe na ramani yenye vipimo ili kujua ukubwa wa jengo lako.


Ramani inachorwa na wasanifu majengo wataalamu ambao
wanasomea — wataalamu hawa wanahitimu katika vyuo vinne tu
hapa nchi navyo ni Ardhi University (chuo kikuu), na vyuo vya
kati Ardhi Institute — Tabora, Ardhi Insitute —
Morogoro, Institute of Lands Dar es Salaam.

2. Ufahamu aina ya material ama tofali utakazo tumia, kama ni


hydraform, tofali za kuchoma ama blocks, hii ni kwasababu tofali
zina tofautiana size ama ukubwa hivyo hata idadi yake itakuwa
tofauti. Tofali zipo za aina tatu, ukubwa wake ni (length x width x
thickness/urefu x upana x unene)

HYDRAFORM; 90 mm x 240 mm x 40 mm

BLOCK; 450 mm x 230 mm x 130 mm

KUCHOMA; 450 mm x 230 mm x 150 mm

Hapa tuta tumia mfano wa nyumba hii yenye vyumba viwili-


kimoja kikiwa na choo/bafu ndani, sebule, jiko, choo cha wageni
na vibaraza viwili; kufanya mahesabu ya tofali zetu.
Hapa kuna hatua mbili za kufuata

1. Tafuta eneo la kuta zote

2. Jumla ya eneo lote la kuta gawanya kwa ukubwa wa tofali

KUTAFUTA ENEO LA KUTA

Hapa tuta tumia kanuni ifuatayo


Eneo = Urefu( wa kuta) x kimo (urefu wa ukuta kwenda juu)

Sasa kujua urefu wa kuta zote, utatakiwa kujumlisha urefu wa kuta


zote

Kwenye mchoro wetu pale juu nime weka namba kila kuta hivyo
itakuwa kama ifuatavyo {vipimo vipo katika milimita (mm)}.

1 m = 100 cm = 1,000 mm; 1 cm = 10 mm

Ukuta 1= 6,500 mm; ukuta 2 = 9,150 mm; ukuta 3 = 4,000 mm;


ukuta 4 = 4,000 mm; ukuta 5 = 9,450 mm

Ukuta 6=11,046 mm, ukuta 7=6196 mm +3200 mm, ukuta


8=9,101 mm, ukuta 9 =3,060 mm, ukuta 10 = 2,900 mm

Sasa uki jumlisha kuta hizo zote unapata jumla ya = 68,603 mm

Eneo la kuta = urefu wa kuta x kimo cha kuta

Hapa kama utajenga nyumba ya kozi 13 maana yake ni kimo cha


3000 mm

Hivyo eneo litakuwa = 68,603 x 3000= 205,809,000 mm

Sasa kumbuka tuna sehemu za wazi ambazo hizi hazihitaji tofali,


mfano milango, madirisha na sehemu za wazi za vibaraza
Kanuni ni ile ile urefu x kimo:

Tuna madirisha 6 yenye urefu 2,000 mm & kimo 1,800 mm=


2000 x 1800 sawa na 3,600,000 mm

sasa, tuna madirisha sita yenye vipimo sawa hivyo 3,600,000 x 6


= 21,600,000

Tumia dirisha 1 lenye urefu 1,400 na kimo 1,500 = 1,400 x 1500


sawa na 2,100,000 mm

Tuna dirisha 1 lenye urefu 1,000 na kimo 1,800 = 1,000x1, 800


sawa na 1,800,000 mm

Tuna madirisha 2 yenye urefu wa 800 na kimo 600 = 800x600


sawa na 480,000 mm

480,000 zidisha kwa 2 sawa na 960,000 mm

Tuna milango 9 yenye urefu wa 900 na kimo 2,400 = 900 x 2,400


sawa na 2,160,000 mm

2,160,000 zidisha kwa 9 sawa na 19,440,000 mm

Uwazi wa vibaraza jumla uref 10,010 kimo 2,400 =10,010 x 2,400


sawa na 24,024,000 mm
Jumla ya wazi = 21,600,000 + 2,100,000 + 1,800,000 + 960,000
+19,440,000 + 24,024,000 = 69,924,000 mm

Eneo kamili linalo hitaji tofali za kuta lita kuwa

ENEO LA KUTA — ENEO LA WAZI0 = 205,809,000–


69,924,000= 135,885,000 mm

hivyo basi, IDADI YA TOFALI, itakuwa kama ifuatavyo:

Sasa urefu wa msingi wako utategemea na nature ya eneo lakini


tuchukulie utakuwa na urefu wa 900 mm, ambapo ni sehemu
tambarare (isiyo korofi)

Kumbuka jumla ya urefu wa kuta zote ni 68,603 mm

Kwahiyo 68,603x900 = 61,742,700 mm

Kwahiyo kupata tofali tutalazimika kuchukua jumla ya ukubwa wa


kuta ukiwa umetoa uwazi na jumla ya eneo la kuta za msingi kisha
tuta gawanya kwa eneo la tofali moja

135,885,000+61,742,700= 197,627,700 mm

Kumbuka tofali ya block lina urefu wa 450 mm na kimo cha 230


mm
Hivyo eneo la tofali ni 450 x 230=103,500 mm

Idadi ya tofali itapatikana kwa 197,627,700mm/103,500mm =


1,909 matofali

Hapa utahitaji kuongeza asilimia kidogo ya tofali kwaajili ya zile


zitakazo vunjika na ngazi pia, tutatumia 5%, kwahiyo jumla ni
tafali 1909+ 0.05(1909) = 2,004.45 ≈ 2,000 tofali

MAHESABU YA IDADI YA MIFUKO YA CEMENT NA


MCHANGA INAYO HITAJIKA KUJENGEA NYUMBA
YAKO

hapa tunaingia sehemu nyingine ambayo itahusu ukadiliaji wa


idadi ya mifuko ya cement itakayo hitajika kujengea jengo lako.

NB: kumbuka haya huwa ni makadilio, hivyo sio lazima yawe sawa
kwa asilimia 100, lakini mara nyingi yanakaribia ukweli halisi kwa
asilimia kubwa sana

Tukichukulia mfano wa TOFALI 2,000

Hapa nazungumzia tofali ambazo wengi wanaziita za block,


ambazo kitaalamu zinaitwa SAND CEMENT BLOCKS

Hapa tuseme idadi ya tofali za Msingi (inch 6) ni tofali 700


Idadi ya tofali za kuta (inch 5) ni tofali 1300

A: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA MSINGI


(TOFALI ZA INCH 6)

-Ikumbukwe hapa tofali hizi hujengwa kwa kulazwa

-hivyo tofali hizi zitahitaji cement na mchanga Zaidi kuliko zile za


kusimama (inch 5)

KANUNI

Mfuko 1 wa cement unajenga tofali 45 za msingi (inch 6- za


kulaza)

Hivyo ukichukulia zile tofali 700 za msingi kwenye ule mfano wetu
itakuwa ifuatavyo

Tofali 700 gawanya kwa 45 = 15.5 sawa na mifuko 16 ya cement

NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement


unajenga tofali 50 ama 60 za msingi za kulaza). Hii hufanywa ili
kupunguza gharama japo kama ni kwenye kiwanja korofi inaweza
kuleta shida.

B: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA KUTA


(TOFALI ZA INCH 5)
-Tofali hizi mara nyingi hujengwa kwa kusimama hivyo hazili
mchanga na cement nyingi kama zile za msingi

KANUNI

Hapa mfuko 1 wa cement unajenga tofali 60 za kuta (inch 5- za


kusimama)

Hivyo ukichukulia tofali 1,300 za kuta kwenye ule mfano wetu,


itakuwa kama ifuatavyo

Tofali 1,300 gawanya kwa 60 = 21.6 sawa na mifuko 22 ya cement

NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement


unajenga tofali 70 mpaka 90 za kuta, za kusimama), pia hii ni ili
kupunguza gharama.

NB: KIPIMO CHA MCHANGA

Mfuko 1 wa CEMENT una changanywa na NDOO 9 kubwa za


MCHANGA

Ama mfuko 1 wa CEMENT unachanganywa na NDOO 18 ndogo za


MCHANGA

You might also like