You are on page 1of 15

SKRAM

Mfumo kwa kutatua matatizo changamano


Lengo la jalada
Mimi Abdulsamad Alawi Abdalla, nimeandika jalada hili kwa sababu ya kutaka kulielezea
(scrum guide) iliyopo katika https://www.scrum.org/ kwa lugha ya Kiswahili. Ieleweke kwamba
hii sio tafsiri yake ni maelezo kutokana na uelewa wangu. Lengo kuu ni kuengeza muamko wa
watu kuielewa skram. Baada ya kusoma hili jalada nakusihi ukasome scrum guide halisi katika
linki hii hapa chini

https://www.scrum.org/resources/scrum-guide

i
Lengo la Scrum Guide
Katika miaka ya 90 Ken Schwaber na Jeff Sutherland walitengeneza skram. Mnamo mwaka
2010 wakaandika Scrum Guide ya mwanzo ili kusaidia watu kuielewa skram. Ilikuepo tangu
hapo huku ikibadilishwa badilishwa, na wote kwa pamoja wanasimama nayo kama mawazo yao
thabiti.

Katika scrum guide mmeelezewa maana ya skram na vitu vyake vyote vya kutumia. Muundo na
sheria za skram hazitaki kutumiwa nusu nusu au kubadilishwa. Ukiamua kufanya hivyo,
maanake hutumii skram na hutopata lengo la skram. Hivyo skram haitakua na maana kwako.

ii
Yaliyomo
Lengo la jalada ............................................................................................................................................... i
Lengo la Scrum Guide .................................................................................................................................. ii
Maana ya skram ............................................................................................................................................ 1
Nadharia ya skram ........................................................................................................................................ 1
Uwazi ........................................................................................................................................................ 2
Uchunguzi ................................................................................................................................................. 2
Kukabiliana ............................................................................................................................................... 2
Maadili ya Skram .......................................................................................................................................... 2
Timu ya skram .............................................................................................................................................. 3
Developa ................................................................................................................................................... 4
Prodak ona ................................................................................................................................................ 4
Skram masta .............................................................................................................................................. 5
Matukio ya skram ......................................................................................................................................... 6
Sprint ......................................................................................................................................................... 6
Mpango wa Sprint ..................................................................................................................................... 7
Mada Ya Mwanzo: kuna umuhimu gani wa kua na hii sprint?............................................................. 7
Mada Ya Pili: Nini kinaweza kufanyika katika hii sprint? ................................................................... 7
Mada Ya Tatu: Vipi kazi tulochagua zitaenda kufanywa? ................................................................... 7
Skram ya kila siku ..................................................................................................................................... 7
Uhakiki wa skram ..................................................................................................................................... 8
Marebisho ya skram .................................................................................................................................. 8
Vielelezo vya Sprint ...................................................................................................................................... 9
Prodakt baklog .......................................................................................................................................... 9
Kipimo: Prodakt Gol ............................................................................................................................. 9
Sprint baklog ........................................................................................................................................... 10
Kipimo: Sprint Gol ............................................................................................................................. 10
Inkriment ................................................................................................................................................. 10
Kipimo: Difinishen of Dan ................................................................................................................. 10
Mwisho ....................................................................................................................................................... 11
Marejeleo. ................................................................................................................................................... 11

iii
Maana ya skram
Skram ni mfumo mwepesi unaowasaidia watu, vikundi au mashirika kutengeneza thamani kwa
kutumia njia ya kujihusisha na jambo ili kapata suluhisho la matatizo changamano.

Kiurahisi skram inamtaka skram masta atengeneza mazingira ambayo:-

1. Prodakt ona apange kazi za tatizo changamano katika prodakt baklog.


2. Timu ya skram, ibadilishe kazi zilizochaguliwa kufikia Increment katika sprint.
3. Timu ya skram na wadau wengine, iweze kukagua increment na kauirekebisha palipo
kosewa ili ijianda na sprint ijayo.
4. Irudie hayo ya juu.

Skram ni rahisi, ikitumiwa itasababisha kazi kuengezeka thamani. Skram imeelezea sehemu zote
ambazo zinatakiwa zitekelezwe, lakini haijelezea upite nijia gani kuzitekeleza, ili wenye
kuitumia weweze kuchagua njia sahihi kwa wao. Sheria za skram ndo zinoweka mipaka kua
usitoke ndani ya skram.

Njia zozote zile nzuri zinaweza zikatumiwa katika skram, ili kuengeza ufanisi skram huyaweka
matatizo ya mwanzo wazi na kuyarekebisha.

Nadharia ya skram
Skram hupima matokeo yaliopita, ili kuchanganua kati ya jambo lenye maana na lisilokua na
maana. Lenye maana huendelezwa lisilo maana huachwa.

Skram inatumia njia ya kurudiarudia, ili kuboresha kinachohitajika na kupunguza kutokea


yasiohitajika. Skram inakusanya pamoja watu ambao kwa umoja wao wana taaluma yote
inayohitajika kutimiza kazi walopangiwa.

Katika skram kuna matukio manne, ambayo yamo katika tukio moja kubwa sprint. Matukio haya
huchunguza yaliojiri kwa kutumia njia ya kupima matokeo yaliopita. Njia hii ina nguzo tatu
uwazi, uchunguzi na kukabiliana.

1
Uwazi
Kazi zinazofanywa lazima ziwe na uwazi, kwa wanaofanya na watakaokuja kutumia, katika
skram kuna vielelezo vitatu tu vya kuonesha yanayofanywa na yaliomaliza, vielelezo hivi lazima
viwe na uwazi. Vielelezo hivi vikiwa havina uwazi husababisha maamuzi ya hovyo.

Uwazi hurahisisha uchunguzi, Uchunguzi ulofanyika bila uwazi hupotosha na kupoteza muda.

Uchunguzi
Maendeleo ya kazi na vielelezo vya skram, huchunguzwa ili kufikia malengo, huchunguzwa kwa
makini tena mara kwa mara ili kugundua yasiohitajika na matatizo yaliotokea.

Ukichunguza ndo utaweza kukabiliana na jambo vizuri, ukichunguza bila kukabiliana na


uliyaona, itakua haina maana. Matokeo ya skram yametengezwa ili yasababishe mabadiliko.

Kukabiliana
Ikiwa nijia zilizotumiwa hazifikii malengo au bidhaa haitakubalika kwa watumiaji basi lazima
njia ibadilishwe mara moja ili tupate bidhaa mbadala, na sio lazima mpaka bidhaa imalize, pale
tuu inapogundulika malengo hayatofikiwa au hayatatokea, basi haraka timu ya skram inatakiwa
ibadilike na kutafuta njia nzuri.

Hili halitoweza kua kama timu ya skram haitoweza kukabiliana na matatizo yenyewe. Hivyo
timu ya skram lazima iweze kujisimamia yenyewe.

Maadili ya Skram
Ili skram ifanikiwe lazima wanaoifanya waishi na tabia tano hizi:-

I. Kujitolea
II. Kuzingatia
III. Uwazi
IV. Heshima
V. Ujasiri

Timu ya skram inatakiwa ijitolee, Kuyafikia malengo kwa hali ya kusaidiana. Jambo
wanalotakiwa kuzingatia haswa ni kazi iliyopangwa, ili kufikia malengo ya sprint. Wadau wote
pamoja na timu wanatakiwa wawe wawazi katika kutatua changamoto zinazowakabili. Uwazi
lazima uambatane na heshima, Katika huu mchakato kuheshimana ni jambo la msingi,

2
kuheshimiana ndio kunaleta kuaminiana na kufanya kazi kwa kusaidiana. Ili kuyatimiza haya,
watu wote wanatakiwa wawe majasiri kwa sababu si mchakato rahisi kuutekeleza.

Maadili hayo ndo yanowapa timu ya skram nguvu za kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa.
Katika matukio ya skramu na vielelezo vyake yakiwepo maadili haya ndo nguzo za skramu
zinaweza kusimama.

Timu ya skram
Msingi wa skramu ni timu ndogo, ambayo inahusisha skram masta mmoja, prodakt ona mmoja,
pamoja na madevelopa. Ni timu ya wataalamu iloshikamana na inazingatia kitu kimoja (Prodakt
gol), bila ya madaraja wala timu ndogo ndogo ndani yake.

Timu ya skram ina wataalamu wa aina zote. Maana ni kwamba washiriki wa timu ya skramu
wanataaluma yote inayohitajika kutimiza lengo la sprint. Pia wanaweza kujiongoza wenyewe,
kama kuchagua nini wafanye, lini waanze na vipi watafanya.

Timu ya skram ni mahiri na ni kubwa ambayo inaweza kufanya kazi zote za sprint. Inakua na
watu 10 au chini ya hapo. Wanakua na prodakt gol moja, prodakt baklog moja, na prodakt ona
mmoja. Timu hii uongozi unaiamini na imeipa mamlaka yote ya kutimiza kazi bila kutaka ridhaa
ya mtu yeyote nje ya timu. Timu hii haivunjwivunjwi ovyo labda sababu ya kuvunjwa au
kubadilishwa mshiriki iko nje ya uwezo wa uongozi. Katika timu hii hakuna mtu mwenye wajibu
fulani wote wanawajibika na kazi zote kwa pamoja.

3
Developa
Ni watu katika timu ya skram ambao wamejitolea kutengeneza kila kipengele kinchotakiwa ili
kufikia inkriment.

Utaalamu wanaotakiwa kua nao ni wowote ule ambao utawafanya watimize lengo lao.

Developa wanawajibika:-

I. Kutengeneza mpango wa sprint (Sprint baklog).


II. Kutengeneza bidhaa inayofikia difinshen of dan
III. Kukabiliana na changamoto za mpango wao ili kufikia sprint gol
IV. Kuwajibishana kitaalamu wao kwa wao.

Prodak ona
Ni mtu mwenye wajibu wa kuengeza thamani ya kazi ya madevelopa. Anavyofanya kazi
inategemea uongozi, timu ya skramu, pamoja na yeye mweyewe.

Pia prodakt ona anawajibu wa kulishughulikia prodakt baklog kwa ufanisi kwa kufanya:-

I. Kutengeneza prodakt baklog lenye uwazi.


II. Kuzifanya kazi zilokuemo katika prodakt baklog zinafahamika.
III. Kuzieka katika mpangilio wa kazi, kazi zilokuemo katika prodakt baklog
IV. Kuhakikisha prodakt baklog liapatikana kwa urahisi, lina ukweli wote tena linafahamika.

Kazi za hapo juu anaweza kumruhusu mtu azifanye lakini yeye atakua anawajibika nazo na si
yule alomchagua kufanya.

Ili prodakt ona afanikiwe lazima uongozi uheshimu maamuzi yake, haya maamuzi siku zote hua
yapo na yanaonekana kwa uwazi katika prodakt backlog, ili uongozi uwe unajua na kuona kila
kitu kinachotokea katika timu ya skram.

Prodakt ona ni mtu mmoja, wala sio kikundi cha watu. Hua anawakilisha wadau wengine katika
prodakt baklog. Mabadiliko katika prodakt baklog lazima afanye yeye, wadau wengine
wanaweza kumshawishi yeye kufanya mabadiliko katika prodakt baklog.

4
Skram masta
Skram masta ni mtu mwenye wajibu wa kuianzisha skram kama iliyvoelezewa kwenye scrum
guide.

Skram masta anawajibika na ufanisi wa timu ya skram, anafanya hivyo kwa kuiwezesha timu ya
skram kukua katika kufanya kazi kwa mfumo wa skram.

Skram masta ni kiongozi mhudumu, ambaye anahudumia timu ya skram na shirika kwa ujumla
wake.

Skram masta anaihudumia timu ya skramu katika Nyanja nyingi pamoja na:-

I. Kufundisha washiriki kujiongoza wenyewe katika kufanya kazi.


II. Kuwasaidia kuzingatia inkriment katika ufanyaji kazi wao.
III. Kusababisha kuondolewa kwa vikwazo ili timu ya skramu ikue.
IV. Kuhakikisha matukio ya skram yanatokea, na kua na matokeo chanya tena katika muda
wake.

Skram masta anamhudumia prodakt ona katika mambo mengi pamoja na:-

I. Kusaidia kutafuta njia yenye ufanisi ya kuelezea prodakt gol na kupanga prodakt
baklog.
II. Kusaidia timu ya skram kufahamu umuhimu wa kua na kazi zilizoelezewa vizuri
katika prodakt baklog.
III. Kusaidia wadau wengine kumuunga mkono prodakt ona kama inavotakiwa katika
skram.
IV. Kusaidia kupanga mara kwa mara prodakt baklog.

Skram masta analihudumia shirika katika njia nyingi pamoja na:-

I. Kutoa mafunzo katika shirika kuhusu skram.


II. Kupanga na kushauri katika kufanya skram.
III. Kusaidia viongozi na waajiriwa wengine kutumia na kuielewa skram.
IV. Kuondoa vikwazo baina ya wadau wengine na timu ya skram.

5
Matukio ya skram
Sprint ndo tukio linalobeba matukio yote ya skram, kila tukio la skram ni fursa maalumu
kuchunguza na kukabiliana na yalioyotokea, ambayo huandikwa katika vielelezo vya skram.
Matukio haya yametengenezwa mahasusi ili kuonesha uwazi wa mchakato wa skram. Matukio
haya yanalengo la kutengeneza utaratibu ambao unapunguza mikutano yasio na msingi. Matukio
yote yanafanywa muda mmoja, sehemu moja ili kupunguza uchangamano.

Sprint
Sprint ndio moyo wa skram, tukio ambalo linabadilisha mawazo kua kitu chenye thamani.

Tukio hili lina muda maalum mwezi mmoja au chini ya hapo ili kuengeza uthabiti. Tukio la
sprint jipya linaanza mara tuu tukio la mwanzo likiisha.

Kazi na matukio yote yanayofanya tufikie prodakt gol, kama tukio la mpango wa skram. skram
ya kila siku, uhakiki wa skram, na marebisho ya skram hutokea katika sprint.

Katika Sprint:-

 Hamna marekebisho yatayofanyika yakasababisha lengo la sprint lisitimizwe.


 Ubora haupunguzwi
 Prodakt baklog hubadilishwa kila iwezekanapo.
 Ukubwa wa kazi unaweza ukaelezewa vizuri kila watu wanaposoma kitu kipya.

Kuchunguza na kukabiliana na yaliotokea ili kufika lengo kunasababisha utabiri uwe sahihi kwa
sababu unarudia rudia kila wakati kuchunguza, unachunguza kwa muda mdogo usiozidi mwezi,
ili kujua kama ulichotabiri ni sawa au ubadilishe.

Sprint ikiwa ina muda mkubwa. lengo la sprint linakua halina maana kwa sababu uchangamano
hua mkubwa. mfano vitu vilivyoosewa hua vingi.

Sprint inaweza itakatishwa kama lengo la sprint litapitwa na wakati. Prodakt ona peke yake ndo
anaweza kuikatisha sprint.

6
Mpango wa Sprint
Hili ndo tukio linaloianzisha sprint kwa kuchagua kazi za kufanya katika kipindi cha sprint, kazi
hapa huchaguliwa kwa timu nzima kukubaliana.

Mada tatu huzungumza katika tukio hili:-

Mada Ya Mwanzo: kuna umuhimu gani wa kua na hii sprint?


Prodakt ona atapendekeza kipi kifanyike ili bidhaa tunaoitengeneza iongezeke ubora. Kisha timu
nzima itachangia katika kutengeneza lengo la sprint (sprint gol). Lengo la sprint ndilo
litaloelezea kwa wadau wengine umuhimu wa sprint hii. Lengo la sprint lazima liwe
limeshaandikwa baada ya tukio hili kwa sababu hamna tukio lolote katika sprint linaweza
likalibadilisha labda kulielezea vizuri.

Mada Ya Pili: Nini kinaweza kufanyika katika hii sprint?


Developa wanachagua vitu vya kazi kutoka katika prodakt baklog na kuzihamisha katika sprint
baklog. Timu nzima inaweza ikaziengezea maelezo ili zieleweke vizuri zaidi.

Kuchagua kwa usahihi, kuna changamoto nyingi lakini kila developa wakiingia kwenye sprint,
sprint ijayo wanakua wazuri wa kuchagua kazi.

Mada Ya Tatu: Vipi kazi tulochagua zitaenda kufanywa?


Kila kazi ilochaguliwa, developa wanaipangia mpango wake wa kuitekeleza. Mpango huu ni
lazima uoneshe vipi wataifikia difinishen of dan, katika hio kazi husika. Kwa kawaida kazi
huvunjwa huvunjwa kua ndogo ili ziweze kutimia kwa muda usiozidi siku moja. Kupanga kazi
ifanyike vipi ni jukumu la developa na wengine huwa wachangiaji tuu.

Sprint gol, kazi zilochaguliwa kutoka katika prodakt baklog pamoja na mpango wa kuzitekeleza
kwa pamoja ndio huitwa sprint baklog.

Mpango wa sprint ni masaa yasiozidi nane kwa sprint ya mwezi mmoja, na sprint ikiwa ina
muda mdogo, na muda wa mpango wa sprint hua mdogo.

Skram ya kila siku


Lengo la tukio hili ni kuchunguza maendeleo ya sprint, baada ya kuchunguza kama kuna vya
kurekebisha kwenye mpango wa kazi kurekebishwa kabisa, hapa inawezekana mpango katika

7
sprint baklog ukabadilishwa ila sio lengo la sprint. Lengo la sprint haliwezi kubadilishwa katikati
ya sprint.

Tukio hili hua si zaidi ya dakika 15. Ili kupunguza uchangamano hufanyika sehemu moja na
wakati mmoja katika kipindi chote cha sprint. Kama prodakt ona na skram masta ni madevelopa
kwenye timu ya skram basi watalazimika kushiri, ikiwa si hivyo si lazima kushiriki.

Developa watachagua njia yoyote katika kulifanya tukio hili, muhimu ni kuzingattia Sprint gol.

Tukio hili hukuza mawasiliano baina ya developa, hurahisisha utambuaji wa vikwazo pia
hupandisha uwezo wa madevelopa kujiongoza wenyewe.

Developa wanaweza kurekebisha mpango wa kazi zao wakati wowote. Kawaida hua wanakutana
na kuzungumza kuhusu mpango wao, kwa kina, mara tuu baada ya tukio hili, hapo pia
hurekebisha mpango wao wa kazi.

Uhakiki wa skram
Lengo la tukio hili, ni kuchunguza matokeo ya sprint iliopita, na kuamua vipi tutafanya sprint
mpya. Timu ya skram inaonesha matokeo ya sprint iliopita pamoja na kueleza maendeleo katika
kulifikia prodakt gol. Kisha hivi vyote vitajadiliwa.

Katika tukio hili wadau huchunguza kipi kimekamilika na kipi kitawasaidia katika mazingira yao
ya kazi. Kutokana na mawazo yao prodakt baklog linaweza kurekebishwa.

Tukio hili ni la kazi sio la maonesho tuu, hiyo basi, madevelopa wasilichkulie kama ni la
maonesho ili waweze kulirekebisha prodakt baklog kutokana na mchango wa wadau walioutoa.

Tukio hili ni la muda usiozidi masaa manne, kwa sprint ya mwezi mmoja, au chini ya hapo kwa
sprint ndogo

Marebisho ya skram
Lengo la tukio hili, ni kupanga njia mpya ili kuengeza ubora na ufanisi wa kazi na bidhaa.

Pamoja na madevelopa kujichunguza wenyewe pia huchunguza mawasiliano yao, njia, na vifaa
walivoytumia. Kisha wanajadili kipi walipatia na kipi walikosea, na je makosa yalirekebishwa au
bado hayajarekebishwa

8
Baada ya hapo timu ya skram haelezea mabadiliko wanotakiwa kuyafanya katika sprint zijazo
inawezekana wakaanza katika sprint inayoafuata.

Tukio hili ndo linaloifunga sprint. Tena lina masaa yasiozidi matatu kwa sprint ya mwezi. Sprint
ikiwa ndogo na muda hupungua. Mara tu baada ya sprint kufungwa nyengine huanza.

Vielelezo vya Sprint


Vielelezo huelezea kazi na thamani, vimetengenezwa viwe na uwazi ili kila mdau aweze
kuvichunguza.

Kila kielelezo kina kipimo chake, na kipimo kina uwazi wa hali ya juu ili kila mdau aweze
kukichunguza

 Prodakt baklog ni prodakt gol.


 Sprint baklog ni sprint gol.
 Increment ni difinishen of dan.

Malengo haya yanawezesha uchunguzi ili kundesha skram vizuri.

Prodakt baklog
Ni listi ya kazi zilopangwa kwa mpangilio maalum zikifanywa bidhaa itaengezeka ubora. Ni
sehemu pekee ambayo timu ya skram inachukua kazi za kuzifanya.

Vitu katika prodakt baklog, vinaweza kufanywa katika sprint moja au vikabakia na kufanywa
katika sprint ijayo. Vinakua na uwazi wa hali ya juu.

Vitu katika prodakt baklog vinaweza kuvunjwavunjwa au kelezewa zaidi, ili viwe vinaeleweka
zaidi wakati wowote ule.

Developa ndio wenye jukumu la kuzipa muda utkaotumiwa kazi zote katika prodakt baklog.
Prodakt ona ana kazi ya kuzipanga ipi ianze mwanzo tu, na labda kushawishi muda wa kumaliza
kwa kazi husika.

Kipimo: Prodakt Gol


Prodakt gol linaelezea bidhaa baadae inatakiwa iweje, na hili linakua ndio lengo la muda mrefu
la timu ya skram. Vitu vingine vyote katika prodakt baklog vinaelezea hili litafikiwaje.

9
Prodakt gol ni lengo la muda mrefu, ambalo timu ya skram lazima lilitimize au liliache kabla ya
kua na lengo jengine. Haiwezekeni timu ya skram ikawa na malengo kama haya zaidi ya moja
kwa wakati mmoja.

Sprint baklog
Sprint baklog lina sprint gol (Kwanini tunafanya sprint?). kazi zilochaguliwa kwenye prodakt
baklog (nini kitafanyika katika sprint?) na mpango wa utekelezaji kazi hizo(vipi zitafanyika?)

Ni mpango wa madevelopa unao onesha vipi developa wataifanya kazi katika sprint,
hurekebishwa wakati wowote sprint inapokuepo na lazima ue na maelezo yanayotosheleza
kufanyiwa kuchunguzi katika skram ya kila siku.

Kipimo: Sprint Gol


Ni lengo pekee la sprint . Hili ndilo lengo linalowafanya madevelopa wazingatie kazi za
kuzifanya. Na hili ndilo jukumu la madevelopa kwa pamoja na silo la developa mmoja mmoja.

Hili lengo hutengenezwa kwenye mpango wa sprint halibadilishwi tena. Kama developa
wameona kazi kwenye sprint baklog haziwezi kuisha, wakati wowote ule watarekebisha sprint
baklog kwa kushauriana na prodakt ona pasipo kuliharibu lengo la sprint.

Inkriment
Ni maendeleo kufikia prodakt gol. Kila inkriment inaongezwa katika inkriment ilokuepo zamani
na kuichunguza ili kuihakiki kama inafanya kazi kwa umoja.

Lazima inkriment ifanye kazi kwa pamoja ili kuongeza thamani ya bidhaa.

Kipimo: Difinishen of Dan


Na maelezo rasmi, yanayoelezea vipi bidhaa hua imefikia ubora unaotakiwa.

Wakati kazi inapofikia difinishen of dan ndipo inkriment inapozaliwa.

Maelezo haya husababiisha uwazi kwa kua kila mtu kua na ufahamu mmoja, vipi bidhaa inaitwa
imemaliza.

Ikiwa kazi haikufikia difinishen of dan haiwezi kuoneshwa katika uhakiki wa skram, ila
hurudishwa kwenye prodakt baklog kwa kufanyiwa kazi tena.

10
Kama shirika ishaiandika difinishen of dan, timu ya skram inalazimika kua ndio difinishen of
dan yake ya chini kabisa. Inaweza ikaiengeza kwa lengo la kuongeza ubora.

Kama timu za skramu zitakua nyingi, basi zote zinatakiwa zifate definishen of dan moja
waliokubaliana kwa pamoja.

Mwisho
Skram ni bure na imeelezewa katika scrum guide. Huezi kubadilisha mfumo wa skram. Ukifanya
skram nusu matokeo yake si skram

Marejeleo.
The Scrum Guide. The Definitive Guide to Scrum: The Rules of the Game
https://www.scrum.org/resources/scrum-guide

11

You might also like