You are on page 1of 1

TANGAZO LA MNADA

Baraza la Mitihani la Tanzania linawatangazia wananchi wote kuwa tarehe


04 Februari, 2023 litauza kwa njia ya Mnada wa Hadhara vifaa vifuatavyo

Na. Aina ya kifaa Idadi Hali ya kifaa


1. Magari 14 Hayatembei
2. Pikipiki 01 Haitembei
3. Samani za ofisi 168 Chakavu
4. Vifaa vya Tehama 148 Chakavu

MASHARTI YA MNADA

1. Magari na vifaa vitauzwa kama vilivyo na mahali vilipo.


2. Mnunuzi atalazimika kulipa hapo hapo amana (deposit) isiyopungua asilimia
Ishirini na tano (25%) kwa magari na asilimia Mia moja (100%) kwa vifaa.
Malipo yote ya magari yakamilike katika muda wa siku Kumi na Nne (14)
kuanzia tarehe ya mnada. Mnunuzi akishindwa kutimiza sharti hili atakosa haki
zote za ununuzi wa kifaa husika na amana aliyolipa haitarejeshwa.

3. Mnunuzi atatakiwa kuondoa/kuchukua kifaa alichonunua katika muda wa siku


Saba (07) kuanzia siku ya kukamilisha malipo.

4. Mnunuzi atalazimika kulipa kodi za Serikali kabla ya kukabidhiwa kifaa husika.

5. Ruhusa ya kuangalia magari/vifaa itatolewa siku mbili (2) kabla ya tarehe ya


mnada kuanzia 3 :00 asubuhi mpaka saa 10 : 00 jioni katika ofisi za Baraza la
Mitihani la Tanzania zilizoko Mikocheni, Barabara ya Bagamoyo mkabala na
TBC 1- Dar es Salaam.

KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
S.L.P 2624 AU 32019
DAR ES SALAAM
SIMU: +255-22-27000493-6
NUKUSHI +255-22-2775966
Barua pepe : esnecta@necta.go.tz

You might also like