You are on page 1of 1

ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA

TAARIFA KWA UMMA

Dar es Salaam, 04 Mei, 2023

UTEKELEZAJI WA UKUSANYAJI WA KODI YA MAJENGO KWA KUTUMIA NJIA YA


UNUNUZI WA UMEME KWA WAMILIKI WA MAJENGO YA GHOROFA

Serikali ilianza utekelezaji wa kukusanya Kodi ya Majengo kwa kutumia mfumo mpya wa
ukusanyaji kwa njia ya ununuzi wa umeme. Hii ni kufuatia mabadiliko ya kifungu cha 56 cha
Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438, ambacho kimeongeza njia ya ulipaji wa Kodi ya
Majengo kupitia ununuzi wa umeme. Utekelezaji huu ulianza tarehe 1 Julai, 2021 na
unafanyika chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Maapato Tanzania TRA kwa kushirikiana na
Shirika la Umeme TANESCO ukihusisha mita za iana zote za Umeme.

Viwango vya utozaji Kodi ya Majengo kwa sasa ni Viwango Mfuto kwa mujibu wa mabadiliko
ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Kodi ya Mamlaka ya Serikali ya Mtaa (Ukadiriaji), SURA 289
yaliyofanyika kupitia Sheria ya Fedha Namba 3 ya mwaka 2021 kama ifuatavyo:
❑ Nyumba ya kawaida ni shilingi 12,000 kwa mwaka
❑ Nyumba ya Ghorofa katika maeneo ya Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji ni
shilingi 60,000/= kwa kila sakafu ya nyumba ya ghorofa kwa mwaka.
❑ Nyumba ya Ghorofa katika maeneo ya Halmashauri za Wilaya ni shilingi 60,000/=
kwa nyumba ya ghorofa kwa mwaka.

Zoezi hili lilipoanza wateja wetu waliwekewa viwango mfuto (flat rate) yaani 12,000 wote
bila kujali kama nyumba ni ya kawaida au ya ghorofa kwa sababu kulihitajika uhakiki wa
kina kabla ya kumwekea mteja viwango stahiki kwa mujibu wa Sheria. Zoezi la uhakiki
lilianza katika mwaka wa fedha 2021/2022. Aidha kwa sasa uhakiki wa majengo ya ghorofa
unaendelea na mita husika kuwekewa kiwango stahiki kulingana na aina ya jengo kwa
kipindi cha mwaka huu wa fedha 2022/2023 ambao ulianzia Julai, 2022.

Aidha, Tunaomba wamiliki wote wa Majengo ya Ghorofa ambao watakuwa na changamoto


ya kununua umeme kufika katika Ofisi ya TRA/TANESCO iliyokaribu nao.

Kwa maelezo Zaidi wasiliana nasi katika namba zifuatazo 0800110016/0800750075 (TRA)
au 0748550000 (TANESCO)

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”

Imetolewa na

TRA na TANESCO

You might also like