You are on page 1of 17

AFRICAN UNION UNION AFRICAINE

UNIÃO AFRICANA

UMOJA WA AFRIKA UNIÓN AFRICANA

Addis Ababa, Ethiopia P. O. Box 3243 Telephone: +251 115 517 700 Fax: +251 115 517 844
Website: www.au.int

BARAZA KUU
Mkutano wa Kawaida wa Arobaini na Nne
15 Januari - 15 Februari 2024
Addis Ababa, ETHIOPIA

EX.CL/1476(XLIV)
Matini chanzi: Kingereza

ANDIKO DHANA JUU YA ELIMU KAMA KAULIMBIU YA UMOJA WA


AFRIKA YA MWAKA 2024

KAULIMBIU:
Mwelimishe Mwafrika Amudu Karne ya 21: Kujenga mifumo thabiti ya
elimu, kuongeza upatikanaji wa ujifunzaji jumuishi, endelevu, bora, na
unaoendana na mazingira ya Afrika.
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 1

1. Dhumuni la Andiko dhana la Elimu kama Kaulimbiu ya Umoja wa


Afrika ya Mwaka 2024

1. Ni muhimu kusema kuwa hapo awali, Elimu haikuwahi kuchukuliwa kama


Kaulimbiu ya Mwaka ya Umoja wa Afrika.
2. Kuanzia Septemba 17 mpaka 19, 2022, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, M.
Antonio Guterres aliitisha Mkutano wa dunia wa Mageuzi ya Elimu. Katikati ya
mambo mengine ya muhimu ya kidunia, mkutano huu ulionekana kuwa wa lazima
na kupewa kipaumbele, kwa kigezo kwamba, duniani, elimu ipo katika hali mbaya,
na maendeleo katika kufikia Lengo la 4 la Maendeleo Endelevu (SDG4), yalikosa
mwelekeo kabisa.1 Hii ndio sababu SG ilitaka kuanzisha fursa ya “kipekee katika
kizazi hiki” kushughulikia janga hili la elimu kwa kufufua juhudi za pamoja na
utendaji kazi wa pamoja.
3. Afrika inaelemewa kuliko mabara mengine kwa pengo lililopo katika kufikia
malengo ya SDG4, ambayo yanaakisiwa pia kwenye Mkakati wetu wa Elimu wa
.Kibara CESA (16-25).
4. Katika muktadha huu, Idara ya ESTI, kwa kushirikiana na washirika wake wa
Umoja wa Mataifa na washirika wengine, kama UNESCO, UNICEF, na WFP kwa
umakini mkubwa waliandaa na kuratibu maandalizi ya hafla ya ziada ya Umoja wa
Afrika yenye Hadhi ya Juu, ambayo ilifanyika tarehe 20 September 2022 mjini New
York.
5. Mchakato wa maandalizi ulianza mapema mwezi Juni 2022. Mhe. Kamishna wa
ESTI, aliunda kikosi kazi ambacho kilikuwa jumuishi kwa kiasi kikubwa, kikileta
pamoja makundi ya Elimu ya Umoja wa Afrika, utaalamu wa kiufundi kutoka
kwenye Bara na ughaibuni, washirika wa maendeleo, vyama vya kijamii, sekta
binafsi na wawakilishi wa vijana. Kikosi kazi kilijishughulisha na matukio
yanayojirudiarudia kikiwa na lengo la kupata mtiririko halisi, mapendekezo yenye
uhalisia ambayo yalitumika kama msingi wa tamko rasmi lililowasilishwa kwenye
hafla ya ziada ya Umoja wa Afrika yenye Hadhi ya Juu na kutoa ramani kwa Nchi
Wanachama na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kutafsiri mapendekezo ya Mkutano
wa Mageuzi ya Elimu kwa vitendo, kwa kuzingatia muktadha wa Kiafrika.
6. Rasimu ya tamko ilipitiwa na kukubaliwa na mkutano wa 4 wa Kamati Maalumu ya
Kiufundi kwenye Elimu, Sayansi na Teknolojia (STC-EST4).
7. Tarehe 20 Septemba 2022, hafla ya ziada ya Umoja wa Afrika yenye Hadhi ya Juu
ya Kubadili Elimu kwa muktadha mahususi wa Afrika ilifanyika kwenye viunga vya
Umoja wa Afrika mjini New York. Iliongozwa na Mhe. Rais Macky Sall, kwa nafasi

1
Repoti ya Taasisi ya Takwimu ya UNESCO (UIS) na Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani (GEM) kuhusu
“Kufikia Malengo: Je, Nchi Zinajishughulisha Kufanikisha SDG4?”
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 2

yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, mbele ya uwepo wa Mhe. Moussa


Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC).
8. Wakuu kadhaa wa Nchi za Kiafrika, Mawaziri Wakuu, Mawaziri wa Elimu
walihudhuria hafla hiyo na kutoa matamko mazito, yakitilia mkazo maendeleo
yaliyofikiwa kwenye elimu, lakini vilevile changamoto na mianya ya kuziba,
hususani baada ya janga la Uviko-19 ambalo liliunganisha kwa pamoja hali ya
mifumo ya elimu katika bara.
9. Katibu Mkuu wa UNESCO, Wakurugenzi Wakuu wa UNICEF na WFP, EU, GPE
na wawakilishi wa washirika wengine, wakiwemo wawakilishi wa vijana, sekta
binafsi, Asasi zisizo za Kiserikali, walishiriki kwenye mkutano. Walikubaliana na
maandalizi ya hafla hiyo na kuthibitisha kujitoa kwao kufanya kazi na AUC na Nchi
Wanachama kuongeza nguvu kwa lengo la kuziba mianya kuelekea kufikia
malengo yanayohusu elimu katika Afrika.
10. Mhe. Moussa Faki Mahamat alipendekeza, katika hotuba yake, kwamba, ili
kuendana na kasi na msukumo unaotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
na uongozi wa Umoja wa Afrika na Nchi Wanachama ambao walihudhuria hafla
ya ziada, Elimu lazima ichukuliwe kama Kaulimbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka
2024.
“Kuifanya Elimu kama kaulimbiu ya Umoja wa Afrika kwa mwaka 2024,
ninauhakika, itahifadhi makubaliano yaliyofanywa hapa New York
kuwa muongozo sahihi wa uhamasishaji wa elimu katika Afrika”,
alisema.
11. Karibu nchi zote zilizohudhuria kwa kiasi kikubwa zilipaza sauti na kuunga mkono
pendekezo hilo, kuanzia Wakuu wa Nchi mpaka Washirika hadi wawakilishi wa
Vijana wa Afrika.
12. Baada ya mjadala jopo, tamko la mwisho liliwasilishwa na kupitishwa kwa kura ya
siri.
Katika “muktadha wa aya” yake, tamko lilirejea kuwa “Elimu inabaki kuwa haki ya
msingi ya binadamu kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 26 cha Tamko la Dunia
la Haki za Binadamu, kifungu cha 28 cha Sheria ya haki za watoto na kifungu cha 11
cha mkataba wa Afrika wa haki na ustawi wa mtoto, hayo yote yakisisitiza haja ya
kuwepo kwa wajibu wa Nchi kutoa elimu msingi ya bure na ya lazima.” Aya mbili za
kwanza, chini ya sehemu ya “Makubaliano” inasomeka kama ifuatavyo:
“Tunasisitiza makubaliano yetu na wito wetu kwa nchi zote wanachama wa Umoja
wa Afrika:
1. Kufanya kazi kufikia mafanikio ya Mkakati wa Kibara wa Elimu wa Afrika
2016 mpaka 2025 na shabaha zihusuzo elimu za Malengo ya Maendeleo
Endelevu, hususani SDG 4.
2. Kuifanya Elimu kuwa Kaulimbiu ya Umoja wa Afrika kwa mwaka 2024
na kwa utekelezaji wa wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa
kuleta mageuzi ya elimu duniani.”
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 3

13. Ni kwa mantiki hiyo kwamba pendekezo hili la kuchagua Elimu kuwa kaulimbiu ya
Mwaka 2024 liliwasilishwa kwa kujadiliwa na kupitishwa na Mkutano mkuu kwenye
mkutano wake wa 36 wa kawaida wa Februari 2023.

2. Sura ya Sekta ya Elimu Afrika kwa Ufupi

Mapitio ya hivi karibuni ya CESA (16-25) na Mpango Kazi wa Elimu 2030, ripoti ya kibara
kati ya Umoja wa Afrika na UNESCO ya CESA na SDG42 na ripoti ya pamoja kati ya
Umoja wa Afrika na UNICEF juu ya Mageuzi ya Elimu Afrika, yanaonesha ukweli kuwa
kwa miaka kumi iliyopita, Serikali za Kiafrika zimefanya programu nyingi na juhudi kwa
ngazi ya kisera kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anabaki nyuma katika kupata elimu.
Kumekuwa na juhudi kubwa katika bara kuhakikisha, upatikanaji, uhitimishaji na elimu
msingi bora kwa wote.
Kwa ujumla, kiwango cha watoto wasiodahiliwa shule kilipungua mpaka kufikia mwaka
2010. Kiwango cha kuhitimu kiliongezeka kwa ngazi ya msingi na ngazi ya chini ya elimu
ya sekondari, pamoja na upatikanaji na ushiriki katika TVET. Vilevile maendeleo
yalionekana kwenye upatikanaji wa elimu ya awali na elimu ya watu wazima na elimu
endelevu. Kwa upande wa Chakula Shuleni, nchi za kipato cha chini zimeongeza
maradufu matumizi ya bajeti zao za kitaifa kwenye HGSF kutoka asilimia 17 mpaka
asilimia 33 kati ya mwaka 2013 na 2020. Katika nchi zenye kipato cha kati cha chini,
bajeti za kitaifa kwa sasa zimefikia asilimia 88 zaidi ya ufadhili wa fedha kwenye chakula
shuleni, kutoka asilimia mia 55 mwaka 2013.
Walakini, mbali na juhudi na maendeleo yaliyofikiwa, viashiria vikuu vitatu vinagonga
kengele ya tahadhari:
− Ingawa kiwango cha Wasiodahiliwa, yaani “idadi ya watoto na vijana wadogo
walio katika umri rasmi kwa ngazi husika ya elimu ambao hawajadahiliwa katika
ngazi ya awali, msingi, sekondari au ngazi za juu za elimu” inaendelea kushuka
mfululizo, hususani kwa ngazi ya msingi, idadi kamili imefikia kiwango cha hatari
cha dunia kinachokadiriwa kuwa milioni 98 katika Afrika3 (tazama kielelezo cha 1
hapo chini).
− Kiwango cha umasikini wa ujifunzaji, yaani “idadi ya watoto ambao hawawezi
kusoma kifungu rahisi cha maneno na kuelewa katika umri wa miaka 10 ilikuwa
ni kubwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kabla ya janga la UVIKO-19,
kikiwa asilimia 86. Kiwango hiki kilikadiriwa kuwa kibaya baada ya janga,
kikikadiriwa kwa sasa kuwa asilimia 90. Hii humaanisha kuwa watoto tisa kati
watoto kumi hawaaezi kusoma kifungu rahisi cha maneno na kuelewa katika
umri wa miaka 10.4 (tazama kielelezo cha 2 hapo chini)

2
Elimu Afrika- Kuleta usawa kwenye kiini cha sera: https://unesdoc.unesco.org/ark:/48223/pf0000384479
3
UIS 2022 : https://unesdoc.unesco.org/ark:/48223/pf0000382577
4
Benki ya Dunia: The State of Global Learning Poverty: 2022 Update
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 4

− Afrika itahitaji nyongeza ya walimu milioni 175 ili kufanikisha elimu ya msingi na
sekondari kwa wote ifikaapo mwaka 2030.

Kwakutazama kwa ukaribu kwenye kila lengo mahususi kwenye CESA 16-25 au kwenye
SDG4, mtu anaweza kuona ulazima wa kufanya mageuzi na kuhuisha mfumo mzima wa
elimu katika bara, wakati huo akiweka umakini mkubwa kwenye makundi yaliosahaulika
wakiwemo wasichana, watoto maeneo ya vijijini, wale wanaoishi na ulemavu, na wale
wanaohamahama, wakiwemo wale walio kwenye nchi zenye hali na mazingira tete.

Kwa ngazi ya dunia, na katika muundo wa Mchakato wa Uratibu wa Elimu ya Dunia,


unaosimamiwa na UNESCO, Umoja wa Afrika umekuwa mshiriki muhimu kwenye uratibu
wa kanda na uungaji mkono wa CESA na SDG4 na ushirikiano miongoni mwa nchi. Hii
ni kwa kupitia Nchi Wanachama zilizohudhuria na washirika na kutoa michango mikubwa
kuendeleza matumizi ya ushahidi, kuweka vipaumbele, kujifunza kwa kundi rika na mbinu
za ufuatiliaji.
Kadhalika, kwenye Kamati Maalum ya Kiufundi ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Uvumbuzi iliyokaa tarehe 1 na 2 Septemba 2022, Mawaziri kwenye Tamko lao juu ya
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi6 waliiomba Kamisheni kuwezesha uingizaji wa
kaulimbiu ya mwaka inayohusiana na Elimu kupitia Umoja wa Afrika kwa mwaka 2023,
kushughulikia mzigo na usumbufu uliosababishwa na UVIKO-19 kwenye Mifumo ya
Elimu, kukuza utekelezaji yakinifu wa kuleta madadiliko ya elimu katika Afrika na
kuongeza msukumo kwenye utekelezaji wa CESA 2016-2025 na SDG 4.

Kielelezo cha 1

5
UIS 2016: http://uis.unesco.org/en/files/fs39-world-needs-almost-69-million-new-teachers-reach-2030-education-
goals-2016-en-pdf
6
Tamko juu ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi iliyokubaliwa na STC-EST 4 ikifanyika Septemba 2022
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 5

Upper secondary
Total number: 98 million
Total: 98
Lower secondary

Primary

Kielelezo cha 2
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 6

Kwa ufupi,
Mbali na maendeleo makubwa yaliyofikiwa katika Afrika kwa miongo miwili iliyopita kwa
maana ya upatikanaji, uhitimishaji na ubora wa elimu msingi, tofauti zinaendelea kuwepo
kati ya nchi. Mafanikio katika kujifunza bado ni ya chini maeneo mengi ya Afrika.
Wasichana, watoto wanaotoka kwenye historia ya umasikini mkubwa, watoto wenye
ulemavu, na watoto wanaohama kama vile wanaohamishwa kwa nguvu, wanapata
changamoto ya kuipata haki yao ya elimu. Vilevile vikwazo bado vipo kwenye
kumwendeleza mwalimu katika Afrika pamoja na upungufu wa mara kwa mara wa walimu
ikitokea pamoja ukosefu wa fursa za kujiendeleza kitaalamu na hadhi na mazingira duni
ya kufanyia kazi. Dharura nyingi na za muda mrefu zimeathiri kwa kiasi kikubwa utoaji wa
elimu, ikiwemo ongezeko la mashambulizi ya shule. Kuna ulazima wa kuimarisha elimu
ya amani na kutengeneza utamaduni wa amani na uvumilivu katika ngazi zote za elimu-
inayofuata mfumo rasmi, isiyofuata mfumo na isiyo rasmi.
Changamoto hizi za kimfumo zinaanzia kwenye elimu ya awali ya utotoni, na kuendelea
elimu ya msingi na sekondari, elimu ya ujuzi na ufundi, na mafunzo kwenye ngazi ya vyuo
vya kati na elimu ya juu.
Janga la UVIKO-19 lilichochea vikwazo vya utekelezaji wa mbinu zilizopo za elimu kwa
ngazi zote, likizidisha kutokuwa na usawa katika elimu na moja kwa moja kutishia
kurudisha nyuma mendeleo yaliyopatikana kwa miongo kadhaa, ingawaje ni kidogo,
katika Afrika.
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 7

Katika muktadha huu, lisipofanyika jambo katika kuleta mageuzi na kuhuisha elimu katika
Afrika, mafanikio ya Mkakati wa Kibara wa Elimu kwa Afrika (CESA7 2016-2025), SDG
2030 na Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika hayatafikiwa. Pasipokuwa na suluhisho la ziada
la haraka, lilioratibiwa vizuri, shabaha za kupunguza umasikini wa ujifunzaji katika Afrika
hazitafikiwa. Matokeo yake kwa watoto na na jamii yatakuwa makubwa, na athari hasi za
muda mrefu kwenye matokeo ya maisha ya mtoto, ikiwemo kujifunza kwao, afya (kimwili
na kiakili), lishe na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Dhana ya biashara kama siku zote
kwa ufupi haina mashiko.
Maendeleo katika Elimu yana athari inayofika mbali katika nyanja nyingine zote za
maendeleo ya raslimali watu. Idadi kubwa ya vijana wadogo katika Afrika ni chanzo
kikubwa cha ukuaji na maendeleo ya kiuchumi, endapo watapewa elimu bora na ujuzi
kwa fursa za ajira za karne ya 21.Hivyo kuwekeza kwenye elimu, ni uwekezaji mzuri
wenye tija katika kupambana na umasikini, kupunguza ukosefu wa usawa wa kijinsia,
kuwawezesha watu kujikimu kimaisha na kusitawi na kuendelea kusaidia kuboresha
maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Vilevile elimu inahusishwa na jamii zenye amani,
ushiriki mkubwa wa kiraia, na demokrasia imara.

3. Mustakabali wa Elimu kama Kaulimbiu ya Mwaka ya Umoja wa Afrika


kwa Mwaka 2024

Mwaka 2024 kutolewa kwaajili ya Elimu Afrika itakuwa ni fursa ya kipekee kwa Umoja wa
Afrika kuwaamsha Nchi Wanachama kuelekea kufanikisha shabaha za CESA na SDG4.
Muhimu, hii itakuja kama namna ya kufuatilia Matamko ya STC-EST4, AU-HLSE, Wito
wa Haraka wa Kuchukua Hatua wa Kamati ya Utendaji ya Ngazi ya Juu8 ya SDG4 na
Kauli ya Dira ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya Kuleta Mageuzi ya Elimu9.
Itahusisha Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuwaweka pamoja Serikali na washirika wa
Maendeleo kutafakati mbinu za elimu na maendeleo ya ujuzi yanayohitajika kwa Afrika
tunayoitaka kwa karne ya 21.

Mkazo utakuwa kwenye maendeleo na utekelezaji wenye ufanisi, wa kudumu, mikakati


ya mageuzi ya kimfumo ya elimu katika Afrika, na kurudi katika hali ya kawaida baada ya
UVIKO-19, kujenga uthabiti na mageuzi, kuendana na kasi ya dunia. Vilevile inatarajiwa
kuchochea utekelezaji wa matamko yatokanayo na nyakati muhimu za elimu kwa ngazi
ya bara na dunia ikiwemo kikao cha nne cha kawaida cha Kamati Maalumu ya Kiufundi
kwenye Elimu, Sayansi na Teknolojia (STC-EST4), matamko kutoka kwenye Mkutano wa
Umoja wa Mataifa wa Mageuzi ya Elimu, Hafla ya Ziada yenye Hadhi ya Juu juu ya

7
CESA inakusudia “Kuunda upya mifumo ya elimu na mafunzo Afrika kufikia maaarifa, uwezo, ujuzi, uvumbuzi na ubunifu
vinavyohitajika kutunza mila zetu za msingi za Kiafrika na kukuza maendeleo endelevu katika ngazi za kitaifa, kanda ndogo na
kibara”
8
Kamati ya Utendaji ya Ngazi ya Juu ni chombo cha juu cha uratibu na ufuatiliaji wa dunia wa SDG 4
9
Kauli ya Dira ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ilijawa na michakato ya kina na jumuishi ya maandalizi
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 8

Mageuzi ya Elimu katika Afrika pamoja na Ilani ya Vijana juu ya Mageuzi ya Elimu katika
Afrika ambayo ilitokana na mashauriano ya vijana mwaka 2023 ambayo yaliwasilishwa
HLSE mjini New York.

4. Kaulimbiu Iliyopendekezwa

Mwelimisha Mwafrika afae kwa Karne ya 21-Kujenga mifumo thabiti ya elimu


kuongeza upatikanaji wa ujifunzaji jumuishi, endelevu, bora, na unaoendana na
mazingira katika Afrika.

Iliyopo hapo juu ni kaulimbiu pendekezwa ya mwaka 2024. Itaundwa kutokana na


kaulimbiu ndogo ndogo zinazobeba mwonekano mzima wa maendeleo ya elimu na ujuzi
kuanzia elimu ya awali ya utotoni na kuendelea mpaka elimu ya vyuo vya kati na vyuo
vya ufundi na elimu endelevu. Mkazo utakuwa kwenye maendeleo na utekelezaji wa
mikakati ya mageuzi ya kimfumo ya elimu katika Afrika, na kushughulikia vikwazo kwenye
mwenendo wa ufadhili wa kifedha katika elimu. Nafasi ya walimu kama vichocheo
muhimu vya mageuzi itapewa msisitizo, kwani walimu wanahitaji kuungwa mkono na
kuwezeshwa kikamilifu ili kuwezesha mageuzi haya kutokea.

Kusheherekea kaulimbiu ya mwaka, inapendekezwa shughuli mbalimbali kufanyika


katika ngazi ya taifa, kanda, bara na dunia. Shughuli hizo zinatarajiwa kuchochea
utekelezaji wa Tamko la STC-EST4, Tamko la hafla ya ziada yenye Hadhi ya Juu kuhusu
Mageuzi ya Elimu Afrika na maeneo ya vipaumbele ya Mageuzi ya Elimu ya Umoja wa
Mataifa katika kuelekea kwenye kujenga mfumo wa elimu thabiti na wenye matokeo
katika Afrika.Utekelezaji utakuwa chini ya uongozi wa kiufundi na uratibu wa Idara ya
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa
kushirikiana kwa karibu na Kamati ya Wakuu wa Nchi Kumi (C10) kwenye Elimu katika
Afrika. Idara itafanya kazi kwa ukaribu na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (ikiwemo
kupitia STC), RECs, Washirika wa Maendeleo, Wakala wa Umoja wa Mataifa na Wadau
wote wa Elimu ikiwemo sekta binafsi na vijana.

Kuwa na Elimu kama kaulimbiu ya mwaka 2024 itaongeza kasi kwenye msukumo
uliotokana na Mkutano wa Mageuzi ya Elimu (TES) na, kuendelea kufanya kazi na Nchi
Wanachama na washirika, kuangazia katika bara kwenye kurudi katika hali ya kawaida
baada ya UVIKO-19 na kujenga mifumo thabiti ili kuongeza upatikanaji wa Elimu jumuishi,
bora na inayoendana na mazingira katika Afrika. Hii itafanyika kwa njia hatua halisi na
zenye matokeo zinazochukuliwa na Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika
kuelekea kwenye mageuzi ya elimu Afrika.
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 9

Kiambatisho 1. Muongozo wa Umoja wa Afrika wa Kaulimbiu ya Mwaka 2024

Shughuli za kitaifa, kanda, na bara zitatekelezwa mwaka mzima katika kumbukizi ya kaulimbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2024.
Matukio haya ya kumbukizi itakuwa kama fursa ya kuthibitisha juhudi ya kisiasa kwa Serikali za Afrika kwenye Elimu. Miongoni mwa
mambo hayo ni pamoja na:

Namba Malengo Maeneo ya Kipaumbele/matokeo yanayotarajiwa Muhusika / washirika

Kujitolea katika Kutekeleza Nyenzo za Uendelezaji wa Mwalimu.

Sera za kuchochea maendeleo zimeanzishwa na kutekelezwa.


Kuchochea mageuzi ya AFTRA, ATUPA, VVOB, Ashoka, AfECN, AUC,
fani ya ufundishaji kwa Majukwaa ya ujifunzaji wa Rika na Rika ya kuwaendeleza UNESCO-IICBA, RUFORUM, UNICEF, Plan
1 njia ya programu za kina walimu yamewezeshwa, ikiwemeo utekelezaji wa Tuzo ya Bara Intertnational, IRC, ADEA, Ripoti ya GEM, FAWE,
na bora za ya Mwalimu. ANCEFA, GPE, AfDB and CESA Teacher
kuwaendeleza walimu. Shughuli za kujenga uwezo kwa walimu na taasisi zinafanyika Development Cluster, EU, Benki ya Dunia.
kusaidia ufundishaji na ujifunzaji bora katika ngazi zote.

Matokeo na ushahidi wa maarifa na ujifunzaji kusaidia


ufundishaji yametengenezwa.

Vitendea kazi kwa elimu ya STEM iliyoboreshwa na Vigezo vya


Ufundishaji vimeanzishwa na kutekelezwa.
Mbinu za Ufundishaji ikiwemo kuimarisha elimu ya STEM
inayojikita kwenye michezo katika ngazi ya msingi ya ujifunzaji
Kusisitiza uwekezaji Afrika.
kwenye STEM na Miundombinu ya shule imeendelezwa kwa kusaidiwa mahitaji Chama cha Mitaala cha Afrika, AUC, UNICEF,
Ujifunzaji wa Msingi stahiki kufanikisha STEM/ raslimali za kufundishia na kujifunzia. African Early Childhood Network, UNESCO- IICBA,
kupitia, pamoja na BMGF, AFTRA, ADEA, ICQN on Mathematics and
2
mambo mengine, Mkakati wa kibara wa “Kumaliza Umasikini wa Ujifunzaji” lengo Science Education, VVOB, TaRL Africa, GEM
uunganishaji wa likiwa kuzielimisha serikali na wadau wa elimu kuwekeza Report, CESA Curriculum Development, ECED, and
teknolojia na shughuli kwenye Ujifunzaji wa Msingi umetengenezwa na kusambazwa. STEM Clusters, Benki ya Dunia.
za pamoja za mitaala.
Sera na miundo stahiki ya kisheria ikiwemo njia ya pamoja ya
kibara ya kufanya tathmini imeanzishwa na kutekelezwa.
Matokeo na ushahidi wa Ujifunzaji kusaidia STEM na Ujifunzaji
wa Msingi yametengenezwa.
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 10

Kuwezesha/kujenga
uwezo wa walimu Historia Kuu ya Afrika (GHA) Programu za Kimkakati
kufundisha Historia ya zimeanzishwa na kutekelezwa UNESCO (ED, IBE, IICBA, PAX), Umoja wa Afrika,
Afrika, na kusaidia
Kamisheni za Kitaifa za UNESCO, ATUPA,
3 kuujumuisha mkataba
Mkakati wa Umoja wa Afrika wa ujumuishaji na matumizi ya ANCEFA, PAPS, ACERWC, AU ECOSOCC, and
wa Umoja wa Afrika wa
Mkataba wa Afrika wa Demokrasia, chaguzi na uongozi kwenye Save the Children
demokrasia, chaguzi na
uongozi kwenye mtaala mtaala wa shule umetekelezwa.
wa shule.

Sera na miundo ya Kisheria kwa Elimu ya Juu inaanzishwa na


kutekelezwa

Mtandao wa Kimataifa wa Elimu ya Juu Afrika


Kasi ya utekelezaji wa mikakati ya Elimu na Mafunzo ya Ujuzi (INHEA) na Chama cha Vyuo Vikuu vya Afrika
na Ufundi (TVET) kuhakikisha uchumi jumuishi na endelevu (AAU), ACBF, AUC, AUDA-NEPAD, UNIDO,
Elimu na Mafunzo ya
UNECA, ATUPA, CAFOR, UNESCO (ED), Taasisi
Ujuzi na Ufundi (TVET)
Mawasiliano yaliyoimarishwa na kujito katika utekelezaji wa wa ya Teknolojia ya Maji Ethiopia & Grundfos, ADEA,
na nafasi ya elimu ya juu
Mkakati na Mpangokazi wa TVET UNICEF; ETF, GIZ, UNICEF, AU CIEFFA; GAN,
inaimarika kwa
4 ILO, GIZ, Higher Education and TVET Clusters,
kuongeza kasi kwenye
ANCEFA, VVOB, UNAIDS, UNESCO (ED, PAX),
utekelezaji wa TVET na Uchakataji wa Ushahidi na Matokeo ya Ujifunzaji kuwezesha
UNESCO National Commissions, AfDB, UNESCO
Mikakati ya Elimu ya maendeleo ya ujuzi kwa ajili ya ajira
UNEVOC, EU, Benki ya Dunia.
Juu.
Kuimarisha uwezo wan chi wanachama kutekeleza TVET na
sera za maendeleo ya ujuzi

Ubora wa utoaji wa TVET kwa njia ya uboreshaji wa kisasa wa


Miundombinu na Raslimali za Ufundishaji na Ujifunzaji
unawezeshwa

Suluhisho la elimu kwenye maeneo ya dharura na yaliyo tete ADEA, AU ESTI/ AfECN and National Advocacy
Utekelezaji wa uvumbuzi linapatikana na kuimarishwa, kuwezesha usawa na upatikanaji partners, AfECN/ WHO/UNICEF/EVAC/PLH, IED/
uliojikita kwenye wake. EU+ITU, UNICEF kwa kushirikiana na Airtel, EU,
5 ushahidi, suluhisho la Microsoft, Google, AUDA-NEPAD, SIFA FC & TC,
kidijitali yakinifu na Matokeo ya ujifunzaji yanaendelezwa na kujikita kwenye Save the Children, UNESCO-IICBA, UNESCO,
endelevu unaongezeka. ushahidi wa suluhisho la kidijitali la kiuvumbuzi na endelevu AfDB, Microsoft Philanthropies, AOSTI, ATUPA
kiuvumbuzi na endelevu AfroChampions Initiative, AfCFTA Secretariat,
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 11

Africa CDC, UNESCO (ED)/ IFEF, IDEP, EU, Benki


Majukwaa ya utafiti na maendeleo na ubadilishanaji wa maarifa ya Dunia.
kwa suluhisho la kidijitali la elimu linaanzishwa.

Maendeleo ya suluhisho la kidijitali yanakuzwa; kufahamika,


malezi, na shughuli za ujifunzaji rika zinawezeshwa.

Mikakati ya Kujenga Uwezo kwenye elimu ya dijitali kwa ngazi


zote inaimarishwa

Kampeni ya kujenga uelewa Afrika: Siku ya Intaneti Salama kwa


Wanawake, Vijana na Watoto kulingana na Sera ya Umoja wa
Afrika ya Mtoto ya Usalama wa Mtandao na Uwezeshaji

Utekelezaji wa program za chakula shuleni za gharama nafuu


na yakinifu kwa kuzingatia Mazingira ya Wenyeji kwa kufanya
ufuatiliaji, uchakataji wa ushahidi na ujifunzaji wa umeimarishwa

Mawasiliano na Kujitoa kwa ajili ya kazi za afya na mazingira


rafiki ya ujifunzaji yameimarishwa
Mazingira salama na
rafiki ya ujifunzaji kwa Matokeo ya maarifa juu ya huduma ya chakula shuleni kwenye WFP, Plan International, AU/HHS, WHO , FAO,
matokeo bora ya mazingira ya wenyeji, elimu ya amani na elimu kwa afya na Nutritional International, GPE, AfECN, WHO,
ujifunzaji yanajengwa maisha yameandaliwa na kusambazwa UNICEF, UNESCO/ UNFPA, UNAIDS, IPPF,
6 kwa kuimarisha Huduma ANCEFA, Save the Children, UNESCO-IICBA/JET
ya Chakula Shuleni kwa Mkakati wa Kibara wa Elimu kwa Afya na Maisha umetolewa na Ed. & School Feeding Cluster, Peace Education
Mazingira Yaliyopo, kutekelezwa. Cluster, Health & Well being and Career Guidance
Elimu ya Amani na Cluster
Elimu ya Afya
Uendeshaji wa Kitengo cha Afya ya Vijana balehe cha Kampeni
ya Uharakishaji wa Kupunguza Vifo vya Mama Wajawazito
Afrika unaungwa mkono

Utekelezaji wa Tamko la Shule Salama na toleo lililoboreshwa la


mwaka 1974 la Pendekezo la Elimu kwa Maridhiano ya
Kimataifa, Ushirikiano, na Amani na Elimu vinakuzwa
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 12

Kujitoa na majadiliano ya ana kwa ana kuhusu matokeo ya


mabadiliko ya tabia nchi kwenye Elimu na Uharakishaji wa hatua
za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia na
kupitia Elimu zinakuzwa

Usawa wa Kijinsia kwenye Elimu unazingatiwa. Ulinzi wa


wasichana, vijana na watoto kwenye maeneo ya dharura na
migogoro kwa kuzingatia Mkataba wa Afrika wa haki na usalama
wa mtoto unawezeshwa.

Jumbe za kuhamasisha utekelezaji wa kampeni ya


#AfrikaMuelimisheMwanamke kwa ngazi ya taifa, kuhakikisha
ujifunzaji kwa watoto walioathiriwa na migogoro na katika
kujenga utayari na uthabiti wa mifumo ya elimu kwa mitikisiko ya
Kuwezesha upatikanaji wakati ujao zinaandaliwa
wenye usawa wa elimu ANCEFA, AU/CIEFFA, UNICEF, IGAD, SCI,
bora kwa wasichana na ACERWC, Joining Forces Alliance, CSO Forum,
Uendelezaji na utekelezaji wa Muongozo wa Umoja wa Afrika
wanawake, vijana, watu UNAIDS, UNESCO, Save the Children, UNGEI,
7 wa Ilani ya Vijana unaungwa mkono.
wenye ulemavu na ECED Cluster, IED/ITU/EU/WB, Plan International
Matokeo ya kujumuisha kwenye Nyenzo za Uwezeshaji wa
watoto hususani kwenye UNHCR, Council of Europe, Norway, Italy, AUC
Vijana ya Umoja wa Afrika kutumika kwenye Mafunzo ya
maeneo ya dharura na Youth Division, UNESCO-IICBA, JICA
Kujenga Uwezo imeanzishwa/imeratibiwa.
migogoro wanalindwa.
Majadiliano ya ana kwa ana, ikiwemo kuhodhi Bunge la
Umajumui wa Afrika la Watoto kwa watoto kukutana na
kujadiliana kaulimbiu ya mwaka yanawezeshwa

Kampeni za kujenga uelewa katika Afrika: Siku ya Intaneti


Salama kwa Wanawake, Vijana na Watoto kwa mujibu wa Sera
ya Umoja wa Afrika ya Mtoto ya Usalama wa Mtandao na
Uwezeshaji

Uzalishaji na ADEA, UNICEF, SADC/RUFORUM, AUDA-NEPAD,


Muingiliano kati ya mifumo ya taarifa ya usimamizi wa elimu na
muingiliano kati ya ILO, UNESCO, AUC-IPED, GEM Report,
8 ukusanyaji wa taarifa katika soko la ajira, usimamizi,
mifumo ya taarifa za Education.org, ANCEFA, UNICEF, AfECN,
uchanganuzi na utumiaji unaboreshwa.
usimamizi wa elimu na UNESCO, IF, AfDB, UNECA, AU
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 13

taarifa za soko la ajira AU and GPE (inviting heads of UN Agencies, donor


inaboreshwa. Uwezo wa MS katika mbinu za Utambuzi wa Ujuzi kwaajili ya missions, regional orgs/banks), WFP, UNAIDS,
Biashara, uanzishaji Uchumi Mseto, uanzishaji Viwanda AUC-CIEFFA, Save the Children, ATUPA,
kufahamu mustakabali wa ajira zilizotengenezwa kwa kutumia UNESCO-IICBA, ADEA and GEM Report
AFCTFA kuimarishwa/kuendelezwa. CESA Education Planning Cluster, IPED, UIS

Kusaidia awamu ya kwanza ya Nchi Wanachama wa Umoja wa


Afrika kuongeza uzalishaji, utoaji taarifa, na matumizi ya taarifa
bora za elimu na ujuzi katika kupanga, kufuatilia na kutathmini.

Makundi ya CESA kutekeleza malengo ya CESA yamefanya


kazi ya ziada na kuimarishwa

Juhudi za kujenga uwezo zimefanyika kuimarisha sauti ya jamii


ya kiraia na nguvu ya pamoja kama nguzo muhimu katika All CESA Clusters, ADEA and GEM Report
Ushirikiano wa sekta ushirikiano wa sekta mtambuka na wadau mtambuka wa elimu, MoE/VVOB, AfDB, UNAIDS, AUC-CIEFFA, GPE,
mtambuka na wadau kwa ngazi ya nchi, kanda, na bara. ASHOKA, AU/UNICEF/EU and partners, UNICEF,
9 mtambuka kwenye elimu ANCEFA, UNESCO, GPE, EU, AfECN/National
umeanzishwa na Advocacy Partners, ECCAS, EAC, ECOWAS,
kuimarishwa. Tija ya Waafrika waishio ughaibuni kwenye maendeleo ya Elimu UNESCO, IF, Benki ya Dunia.
Afrika inatumika

Kuimarisha uhamasishaji wa ushirikiano wa sekta mtambuka na


wadau mtambuka kwenye elimu.

Uletaji pamoja wa raslimali umefanyika kwa kupitia ushirikishwaji ANCEFA, UNICEF, AfECN, UNESCO, IF, AfDB,
Ongezeko la ufadhili
wa wafadhili na uhamasishaji, ikiwemo hafla za meza duara na UNECA, AU and GPE (inviting heads of UN
endelevu wa kifedha na
10 hafla za Hadhi ya Juu katika kufadhili kifedha mageuzi ya elimu Agencies, donor missions, regional orgs/banks),
uwekezaji wa kimkakati
katika Afrika na katika kuimarisha uongozi wa kibara kwenye WFP, UNAIDS, AUC-CIEFFA, Save the Children,
kwenye Elimu.
elimu. ATUPA, UNESCO-IICBA, ADEA and GEM Report,
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 14

Plan International, CESA Education Planning


Cluster, IPED, UIS, Benki ya Dunia.
Uanzishaji na uendeshaji wa Mfuko wa Afrika wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi (AESTIF)

Uchanganuzi wa ushindani wa mshahara wa mwalimu


ikilinganishwa na fani zingine, ngazi za kuridhika na kazi
kulingana na kiwango cha malipo, na matumizi ya umma
kwenye sekta ya elimu, vimeandaliwa kutokana na taarifa
zilizojikita kwenye ushahidi, kuwezesha vipaumbele vya sera..

Uungaji mkono wa upangaji na matumizi ya bajeti yenye usawa,


inayojali jinsia, jumuishi na yenye ufanisi, ikipelekea kauli za
Wakuu wa Nchi wakifungua Mwaka wa Elimu ikiwemo
makubaliano mapya ya kutenga asilimia 20 ya bajeti kwenye
elimu.

Uwekezaji wa Nchi kukuza upatikanaji wa elimu kwa wasichana


hadi sekondari kwa kupitia Mkakati wa Education Plus
umeanzishwa na kuzinduliwa

Mkutano wa UNECA wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na


Maendeleo ya Uchumi: mjadala wa meza duara na MoF na MoE
umeitishwa, kuhusu namna ya kufadhili kifedha mifumo ya elimu
na ujuzi kwa kipindi cha mpito tu na kuleta uthabiti kipindi cha
misukosuko ya dunia.

Mifumo ya ufuatiliaji/kuchunguza upangaji wa bajeti kwenye


elimu/ECE na mjadala wa matokeo kwenye mikutano wa hadhi
ya juu ikiwemo Mkutano wa Umoja wa Afrika, inaanzishwa
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 15

Kiambatisho 2.Kategoria za Shughuli Zinazotazamiwa za Mwaka wa Elimu (YOE 2024) Uliopendekezwa

Uzalishaji wa Mazao
Mkutano wa ya Maarifa na
Kiufundi na Machapisho
Kongamano

Inapendelewa
(Programu za ➢ Pamoja
Mazungumzo ya ana Kubadilishana) Kibara,kanda au
kwa ana ya Sera kwa nchi kadha
(Kati ya Nchi/Mabara)
Ngazi ya Juu (Ngazi ya kadhaa.
Rais na Mawaziri) Uratibu na ➢ Miradi ya
Ufuatiliaji majaribio yenye
tija kwa kwa
matokeo
makubwa,
yanayojirudia, na
kwa kwa ukubwa

Hatua kwa Ngazi


Mafunzo/Kujenga ya Nchi/Jamii
Uwezo (Warsha na Kuimarisha Miundo
Semina za Mtandaoni) na Majukwaa
EX.CL/1476(XLIV)
Ukurasa wa 16

Kiambatisho 3. Matukio ya Kumbukizi Ngazi ya Bara na Dunia

Kichwa/Jina la tukio MUHUSIKA JAN FEB MAR APR MAY JUN JUL AUG SEP OCT NOV DEC

Siku ya Kimataifa ya Elimu UNESCO


Mkutano wa Umoja wa Afrika AUC
Siku ya Kimataifa ya Wanawake na UNESCO & UN
Wasichana katika Sayansi WOMEN
Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni AU & WFP
Mkutano wa Mawaziri Afrika wa Fedha,
Mipango na Maendeleo ya Kiuchumi UNECA
Jukwaa la Afrika la Kanda la Maendeleo
Endelevu UNECA
Siku ya Wasichana kwenye ICT ITU
Siku ya Afrika AU
Siku ya Mtoto wa Afrika AUC
Mkutano wa Kimataifa wa Kazi ILO
Siku ya Vijana ya Ujuzi Duniani UNESCO
Siku ya Kimataifa ya Vijana UN
WorldSkills International Lyon WSI
Siku ya Kimataifa ya Kuilinda Elimu dhidi ya
Mashambulizi UNESCO/UNICEF
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Wakati
Ujao UN
Siku ya Kimataifa ya Kusoma na Kuandika UNESCO
Siku ya Walimu Duniani UNESCO
Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike UN & AUC
Siku ya Vijana Afrika AUC

You might also like