You are on page 1of 5

PROJECT SUMMARY

Projet Name: My Doctor

Phase 1

DAKTARI WANGU : Ni mfumo wa simu za adroid na iphone yenye lengo la


kuleta utofauti, kuboresha sekta ya afya na kuleta mabadiliko ya kidigital
TATIZO LILILOPO : Upatikanaji wa Huduma kwa mgonjwa kwa haraka na
ufanisi, mapungufu katika uhusiano wa mgonjwa na daktari wake, wingi
wa wagonjwa kulinganisha na uwezo wa madktari na pia muda wa kusubiri
huduma za afya umekuwa ni zaidi ya inavyotarajiwa
LENGO LA DAKTARI WANGU : Ni mfumo utakaomleta Mgonjwa na daktari
wake anaemuamini (yuleyule aliekuwa akimuona kila siku katika taasisi
fulani) mazingira anayoyataka mgonjwa kuhudumiwa, itahusisha daktari
kumfuata mgonjwa popote atakapohitaji huduma yake, kuongeza uhusiano
kati ya Mgonjwa na Daktari wake, kupunguza foleni kusubiri huduma za
afya na kuongeza ufanisi na Thamani ya Daktari.
MAELEZO YA UFANYAJI KAZI WA MFUMO WA DAKTARI WANGU : Mfumo
huu utahusisha phase mbili za utengenezwaji ambapo zitakuwa: Kurasa 4
(nne) katika Phase hii ya kwanza na Kurasa 3(Tatu) katika Phase ya pili
1. Kurasa ya Mgonjwa :
Mgonjwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika kurasa yake kwenye mfumo
baada ya kujisajili na atakuwa na uwezo wa kuedit profile yake ikiwemo
ku-update Location yake na contact adress, kumchagua Daktari wake
anaemtambua kutoka katika eneo lake au hospitali anayoitambua kwa
uhuru wa mgonjwa.
Katika kurasa hio kutakuwa na
Picha ya passport ya daktari, wasifu wake, Jina la Daktari, Sehemu ambazo
Daktari atakuwa ana uwezo wa kuzifikia kwa Muda alionao kwa wakati huo
(Locations on Reach), Uwepo wa Daktari kwa wakati huo (availability),
Gharama za Daktari (Special Price Tag), Sehem fupi ya kujaza Matatizo ya
mgonjwa kwa wakati huo (Complaint Tag), Eneo (Location) ya mgonjwa
kwa wakati huo.
Note: Baada ya mgonjwa kujaza vizuri Kurasa yake Daktari au nurse
atapata notification na Ku-accept ama ku-reject notification.
In acceptance: Notification itarudi kwa mgonjwa kuwa Daktari au nurse
wake atakuja katika mazingira ya mgonjwa na kumuona Baada ya muda
aliouthibitisha. Incase of failure of reach Admin ata-refund kiasi cha pesa
taslim alizotumiwa na mgonjwa wake.
In Reject: Mgonjwa atalazimika kuchagua Daktari mwingine aliyeavailable
ili apate huduma ama kusubiri availability ya Daktari au nurse wake.
Pia mgonjwa atakuwa na uwezo wa kumnotify Admin Kama Huduma
imemfikia na aproceed na malipo kwenda kwa Daktari ama nurse.

2. Kurasa ya Daktari :
Daktari atakapopata Notification ya kumuona mgojwa, Baada ya kuingia
katika kurasa yake atakuwa na uwezo wa Ku-accept au Ku-reject
Notication ya Kumuona mgonjwa kulingana na Muda alionao
In case acceptance: Daktari ata-confirm malipo kufanywa na mgonjwa kwa
ajili ya huduma yake. Malipo atakayolipa mgonjwa yatakuwa withheld na
Admin mpaka Daktari atakapofika katika mazingira ya mgonjwa na mgonjw
ku-confirm uwepo wa daktari wake.
Katika kurasa ya Daktari, Daktari atakuwa na uwezo wa Kutunza
Summary/Hx ndogo ya mgonjwa, Ku-access Nursing service kulingana na
eneo na Price tag ( Nurse Price Tag). Kama kuna Tafiti ataweza kumshauri
mgonjwa wake kuhuduria maabara au vitengo vya radiologia (diagnostic
centres kwaajili ya izo tafiti za ugonjwa) na baada ya tafiti hixo pia
kumshauri manunuzi ya dawa kwenye pharmacies zilizo karibu na
mazingira yake.
Uwezo wa Kurasa ya Daktari:
Edit Profile yake, Edit Price tag yake, Edit Location anayoweza kuhudumia,
Edit availability kulingana na shughuli zake.

3. Kurasa ya Nursing officer na wengineo

Atakuwa na uwezo wa kupokea notifications kutoka kwa daktari ama


mgonjwa ikiwa na Management plan au complaint tag, uwezo wa
kuaccess options za madaktari kama ilivyo kwa mgonjwa, uwezo wa Ku edit
taarifa zake, Price tag, Location na availability (Active / inactive), contact
information
4. Kurasa wa Admin
Atakuwa na uwezo wa Kurecruit madaktari wa wahudumu wa Afya
kulingana na Kada zao husika hata kuwaondoa pia incase Hajalipa
commision au muhudumu hajakidhi vigezo, uwezo wa kuhold malipo
yanayofanywa na mgonjwa kwenda popote pale kabla ya Huduma kwa ajili
ya usalama. Malipo yote yatafanyika kupitia kwa system Admin, kuaccess
system na kurasa zote.

HITIMISHO : Daktari wangu ni mfumo wa mabadiliko utakaomsogeza yule


Daktari anaeaminika na mgonjwa kutoka katika taasisi yake karibu zaidi na
mazingira ya mgonjwa kulingana na matakwa ya mgonjwa.

Daktari wangu
“Niite nikuhudumie”
Phase 2

Hatua hii itahusisha Kutengeneza kurasa mbili(3) ambazo zitakuwa


incooperated kwenye kurasa ya Medical Practitioners na wagonjwa
ambazo ni
(i) Kurasa ya Pharmacy
(ii) Kurasa ya Maabara
(iii) Kurasa ya Radiolojia

PHARMACIA

Kwa upande wa kurasa hii itahusisha Maduka ya dawa yenye mobile services
ambayo yatakuwa na uwezo wa kuleta dawa kwa mgonjwa husika katika
location aliopo mgonjwa.
Pharmacy hizi zitakuwa na uwezo wa kupokea notifications kutoka kwa
daktari juu ya uwepo wa uhitaji wa dawa kwa mgonjwa zikiambatanishwa
dawa zinazohitajika, approval ya uwepo wa daw hizo katika duka hilo
zitafnyw pamoja na price tag ya dawa kutumwa na Kwasababu Duka hizo
zitaonekana katika orodha kwenye Kurasa ya Mgonjwa pia, mgonjwa
ataweza kulipia dawa Hizo kwenye mfumo. Mfumo utatoa malipo kwenye
pharmacy husika pale ambapo mgonjwa atathibitisha kupokea dawa hizo

MAABARA
Ukarasa huu utahusisha maabara zenye mobile service ambazo zitakuwa
na uwezo wa Kuchukua sampuli na Kuzifanyia chunguzi vile ambavyo
daktari wa mgonjwa atakavyoagiza na kisha Daktari kurejesha majibu
kwa mgonjwa.
Maabara hizi zitapokea taarifa katika interface zao baada ya registration
juu ya uwepo wa mgonjwa anaetakiwa kuchukuliwa sampuli na vipimo
vinavyotakiwa kufanyika kutoka kwa daktari. Maabara hizo zitatuma
invoice ya gharama za vipimo na kuviwasilisha ili vilipiwe mgonjwa
atalipia kupitia mfumo huu na maabara zitamfata na kuchukua sampuli
kwaajili ya vipimo, mfumo utalipa gharama za vipimo baada ya huduma
Majibu yatatumwa kwenye mfumo wa daktari wa mgonjwa na majibu
yatatolewa kwa mgonjwa kupitia daktari wake kwa utaratibu ambao
daktari anaona utafaa.

RADIOLOGIA
Ukarasa huu utahusisha usajili wa Radiologia kwenye mfumo ambao daktari wa
mgonjwa atakuwa na uwezo wa kuchagua Diagnostic centre katika
choices zake na Kumshauri mgonjwa Kufika sehem hio kwa vipimo
vikubwa ama kwa vipimo vinavyoweza kufanyika nnje ya eneo hilo
mgonjwa atafuatwa na kufnyiwa vipimo hivyo kwa kipaumbele.

Daktari wangu
“Niite Nikuhudumie”

You might also like