Professional Documents
Culture Documents
tz
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1071 RAJAB 1434, IJUMAA MEI 17-23, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Uk. 6
Wamwandikia barua Mwanasheria Mkuu Wataka Farid, Uamsho watendewe haki Wadai wanadhalilishwa huko korokoroni
Na Mwandishi Wetu
2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Habari
AN-NUUR
AN-NUUR
MAONI YETU
Inatoka Uk. 1 Afisa huyo akasema kuwa wao kama Bakwata wameshangaa na kushtuka sana. Akasema kuwa pamoja na kuwa hawakushirikishwa wanakuja kupewa tu taarifa, lakini wanashangaa pia kwa sababu hata walipopewa taarifa na Kamishna wa Elimu, wameambiwa jambo hilo liwe siri. Ni rai yetu kwamba, Jambo hili linafanywa madhali serikali imeonyesha SIRI, je Serikali inataka nia ya dhati katika kuleta Waislamu wasiambiwe? u m o j a n a u p e n d o k w a Kwanini? Kuna agenda gani? wananchi wake kidini, basi Amehoji asa huyo ambaye fursa hiyo pia itumike kwa hata hivyo hakutaka kutaja kuwaacha Waislamu. Iache jina lake akisema kuwa yeye kurasimisha kuwa msemaji sio msemaji wa Bakwata. Awali taarifa juu ya kikao wa Waislamu ni Bakwata. cha Wakristo na Wizara Kama kuna jambo linahitaji juu ya mitihani ya dini, mawazo ya Waislamu, basi zilianza kuvuja kupitia kwa m a w a z o y a o h a y a w e z i Wakristo waliohudhuria kuwasilishwa na BAKWATA ambao walipokutana na pekee. Lazima taasisi nyingine wadau kutoka upande wa zinazowakilisha Waislamu Waislamu waliwalaumu ni zisikilizwe. kwa nini hawakuhudhuria T u n a y a s e m a h a y a wakasaidiana kupinga uamuzi tukizingatia kauli za baadhi huo wa Serikali. ya Wabunge hivi karibuni Hata hivyo, wadau hao ambao kauli zao zinaonyesha kutoka Islamic Education kuwa hueda Muislamu akiwa Panel waliwafahamisha nje ya Bakwata, anatafsiriwa wadau hao wa Kikristo kuwa kama muhalifu au kavunja sheria za nchi. Lakini tunayasema haya pia tukizingatia kauli za wale waliosema kuwa hatua ya Serikali ya kuwadhibiti Waislamu chini ya Bakwata, na kwa namna moja au nyingine, kuingilia utendaji Inatoka Uk. 1 Muislamu ni ndugu wa Baraza hilo, ikiwa ni pamoja na kuhusika katika yake Muislamu ni haramu kuweka viongozi wa ngazi kumdhulumu na ni haramu kuacha kumnusuru za juu, ni ukandamizaji na akidhulumiwa. kinyume cha sheria kwa Wamenukuu Hadithi hiyo sababu haifanyi hivyo kwa Maimamu na kisha kumkabili taasisi za dini nyingine. Mwanasheria Mkuu kwa Wa k a t a k a Wa i s l a m u kusema kuwa wanamkishia w a a c h w e h u r u k a m a malalamiko yao kwa sababu walivyo huru Wakristo katika ndiye Msimamizi Mkuu madhehebu na taasisi zao. wa Sheria katika Serikali na Lakini kubwa zaidi ni utendaji wake kisheria. W a k a s e m a , kwa Serikali kuhakikisha kuwa kwa kauli na vitendo wanashangazwa sana kuiona h a i o n e k a n i k u p e n d e l e a Serikali ya Umoja wa Kitaifa ( SUT) ikiridhia kwa kukaa upande wowote wa jamii. Kwa hiyo, wakati inataka kimya juu ya dhulma na kukutana na viongozi wa kidini ukiukwaji wa kisheria na huku ikihimiza maelewano, udhalilishaji wanaofanyiwa ijitizame pia katika yale Viongozi wa Taasisi za i n a y o t u h u m i w a k w a y o Kiislamu nchini akiwemo kwamba inawapendelea Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Wakristo. Farid Hadi Ahmed pamoja H a i t a s a i d i a s a n a na viongozi wa Jumuiya ya kuhangaika kuleta maelewano Mihadhara ya Kiislamu na b a i n a y a Wa i s l a m u n a Mashekhe (wengine). Wakristo ikiwa Serikali Jumuiya ya Maimamu yenyewe ndiyo chanzo cha Zanzibar (JUMAZA) inasema utengano kwa kuendesha kuwa Viongozi hao kumi ubaguzi na upendeleo. wa Kiislamu wamezuiliwa
Ufundi, haikuwaita IEP katika kupitisha uamuzi huo mkubwa na wenye athari kubwa kwa vijana wa Kiislamu na vyuo vya Kiislamu. Hivi sasa Vyuo Vikuu kama kile cha Waislamu Morogoro (MUM), pamoja na wanafunzi wa kozi nyingine, huchukua wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kufaulu Somo la Islamic Knowledge kwa ajili ya kuchukua kozi ya Sheria na Sharia kwa pamoja. Aidha, huchukua pia wanafunzi hao kwa ajili ya kozi ya Masomo ya Dini na Ualimu, yaani BA Islamic Studies and Education. Kwa upande mwingine, Chuo Kikuu cha Elimu Zanzibar (Chukwani) na kile cha Tunguu, navyo vinachukua wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kufaulu somo la Maarifa ya Uislamu kwa ajili ya kozi zao mbalimbali. Vi p o p i a v y u o v i k u u vya Mbale Uganda, Sudan, Uturuki, Malaysia na sehemu nyingine ambapo wana kozi zinazohitaji somo la Maarifa ya Uislamu kama vile Islamic Banking. Inaendelea Uk. 5
3
Na Bakari Mwakangwale
SHEIKH Ponda Issa Ponda, amesema kamwe Waislamu hawatorudi nyuma katika kudai haki zao hata kama itabidi kutoa uhai wao au kukabiliana na vifungo na mateso mengine. Sheikh Ponda ametoa msimamo huo, mbele ya maelfu ya Waislamu waliofurika katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni, Jijini Dar es Salaam, akiongea mara baada ya swala ya Ijumaa ya wiki iliyopita. Wakiwa na shauku kubwa kusikia kauli ya kwanza ya Kiongozi huyo wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, baada ya kuwa rumande kwa muda wa miezi saba, katika gereza la Segerea, Umma wa Kiislamu Msikitini hapo ulirindima kwa mvumo wa Takbirii, baada ya kusikia kauli hiyo. Waislamu hatutorudi nyuma, hakuna kurudi nyuma katika kupambana na madhalimu, haki ya Muislamu katika nchi hii lazima ipatikane. Muislamu haogopi jela, yupo tayari kuia dini yake na sisi ni seheme ya Waislamu hao. Alisema Ponda. Ponda alitahadharisha kwamba dhulma dhidi ya Waislamu nchini ni kubwa, kwani alidai matukio yote yanayotokea hivi sasa ni ya kutengeneza kwa lengo la kuuchafua Uislamu na Waislamu. Alisema, jambo ambalo Waislamu wanapaswa kulizingatia muda wote ni umoja wao, kwani alidai kukamatwa kwa viongozi wao lengo lake ni kuvunja umoja wa Waislamu. Ponda alisema hakuna vurugu za kidini nchini, bali Waislamu wanadai haki zao, badala ya kutafuta ufumbuzi wa madai yao, Serikali imekuwa
Habari
AN-NUUR
Sheikh Ponda Issa Ponda inakuja na hoja za kupoteza malengo na kuwatisha Waislamu. Kiongozi huyo wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, alisema yote hayo yanakuja kutokana na Waislamu kuwa na agenda na madai ya msingi kwa Serikali yanayohitaji majibu na kufanyiwa kazi sio kupiga siasa za kuyeshusha mada. Mfano pale NECTA (Baraza la Mitihani) ameajiriwa Mchungaji kwa ajili ya maslahi ya wanafunzi wa Kikristo, swali linakuja kwa nini iwe ni Mchungaji tu, asiwepo na mtaalamu wa Somo la Dini ya Kiislamu, badala ya kujibu hoja hizi, wanasema ni uchochezi, huwezi kuigeuza NECTA kuwa Parokiya, sio nchi ya dini moja
hii, yapo mengi huu ni mfano tu. Alisema Ponda. Kuhusu mauwaji ya Mwembecha alisema kuwa ipo mikanda ya muda mrefu yenye maelezo ya Padri kupitia radio moja ya Kikristo, akiishawishi Serikali ikawashambulie Waislamu, lakini pia ipo CD, ambayo anasikika kiongozi wa Serikali akiliomba radhi Kanisa, na kuahidi kuchukua hatua. Mauaji yale ni mauaji ya kinyama kwa Waislamu, na yalifanyika mbele ya vyombo vya habari kumbukumbu zipo katika vyombo hivyo na mikanda ipo hakuna anayeliona hili kwa kuwa waliouwawa ni Waislamu. Alisema Ponda. Alisema, hivi karibuni zimepelekwa CD, Bungeni wabunge wakichachamaa kwa maneno yaliyomo ndani na kulalamika kuwa huo ndio udini, lakini alidai CD ya mauaji ya Waislamu Msikiti wa Mwembechai ipo tokea mwaka 1998, hakuna aliyestuka na mauaji hayo na kwamba Bunge lilikataa hata kuunda Tume ya Uchunguzi. Sheikh Ponda alisema kama si udini dhidi ya Waislamu na kutokujali haki za raia, basi hiyo CD, ya mauaji ndiyo ingestahili kupelekwa Bungeni na kuishinikiza Serikali ifanye uchunguzi na wahusika wachukuliwe hatua. Ndugu zangu, kipindi tunachopita hivi sasa ni kizito sana, si Tanzania tu, bali duniani kwa ujumla, hali ya Waislamu ni nzito. Alisema, yanayojiri hivi sasa nchini dhidi ya Waislamu ni kutokana na kuitambua dhulma dhidi yao na kuiweka hadharani jambo ambalo
SAFARI YA UMRAH PAMOJA NA KUTEMBELEA JIJI LA ISTAMBUL, UTURUKI KWA DOLA 1850,
KUONDOKA TAREHE 17 JUNE NA KURUDI TAREHE 30 JUNE 2013 GHARAMA INAJUMUISHA: TIKETI YA NDEGE YA KWENDA NA KURUDI DAR-MADINA, JEDDAH- DAR MALAZI SIKU 4 MADINA KATIKA HOTELI YA NYOTA TATU YA AL ANSAAR NEW PALACE MALAZI SIKU 6 MAKKAH KATIKA HOTELI YA NYOTA TATU YA NAWRAT SHAMS ZIYARAH SEHEMU ZA KIHISTORIA MADINA NA MAKKAH MATEMBEZI YA SIKU 3 KATIKA JIJI LA ISTAMBUL, UTURUKI MALAZI HOTELI YA NYOTA TATU KUTEMBELEA SEHEMU ZA KIHISTORIA IKIWEMO: MAKUMBUSHO AMBAMO KUMEHIFADHIWA NGUO, UPANGA NA PETE YA MTUME SAW. KUZURU KABURI LA ABI AYUB ANSAARI, MSIKITI WA MEHMET (BLUE MOSQIE) PAMOJA NA SEHEMU MBALIMBALI KATIKA JIJI LA ISTAMBUL CHAKULA MILO MITATU NA VIZA YA UTURUKI SIKU YA MWISHO YA KUJISAJILI NI TAREHE 29 MAY 2013 SAFARI YA UMRAH YA SIKU 15 KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KWA DOLA 3400 KUONDOKA TAREHE 23 JULY (15 RAMADHAN) NA KURUDI TAREHE 7 AUGUST (29 RAMADHAN) GHARAMA INAJUMUISHA: TIKETI YA NDEGE YA KWENDA NA KURUDI DAR-MADINA, JEDDAH- DAR MALAZI MADINA SIKU 4 KATIKA HOTELI YA NYOTA TATU YA AL ANSAAR NEW PALACE MALAZI MAKKA SIKU 10 KATIKA HOTELI YA NYOTA TATU YA NAWRAT SHAMS ZIYARAH SEHEMU ZA KIHISTORIA MADINA SIKU YA MWISHO YA KUJISAJILI NI TAREHE 20 JUNE 2013. HUDUMA YA UMRAH KWA MTU BINAFSI, FAMILIA NA KIKUNDI INAPATIKANA WAKATI WOWOTE HADI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI. PIA TUNATOA HUDUMA YA KUOMBA VIZA ZA NCHI MBALIMBALI DUNIANI KWA MAWASILIANO ZAIDI NA USAJILI WASILIANA: PEACE TRAVEL, MTAA WA MAFIA INATAZAMANA NA MASJID MANYEMA. NAMBA YA SIMU 0655/0784 411 788, 0777 411 020, 0713 530 036 Barua pepe: peacetraveltz@gmail.com. Tovuti: http// www.peacetraveltz.com
4
Na Kassim I. Chubwa
Makala
AN-NUUR
Kuna maneno mazuri ya Kiingereza husema Every thing has happened there is the reason to be, ukiwa na maana kuwa kila kitu kinachotokea kuna sababu ya kuwa hivyo. Katika hali ya utando na giza iliyotanda katika baadhi ya vichwa vya Watanzania juu ya hali ya hatari inayolinyemelea Taifa, na watu kuzidi kuipalilia mbegu ya chuki ya kimahusiano kati ya Wakristo na Waislamu nchini, kwa kuzingatia msemo huu wa Kiingereza h ay a y an ay o to k ea ip o sababu ya kuwa hivi! Kunahitaji umakini ili kumjua ni nani mhandisi (Architect) wa propaganda na chuki za kidini na hatari inalolinyemelea Taifa letu. Hebu tuitizame historia kidogo baina ya Waislamu na Wakristo nchini, na nani chanzo cha chokochoko zinazoendelea. Ni kianzia na makala maarufu ya mwanahistoria Mohamed Said aliyoipa jina Tusiwalaumu wa Zanzibar kwa kukosa subra turejee Historia, nitamnukuu sehemu ya manneo katika makala hiyo si kweli kuwa Waislamu wana chuki na Wakristo anaetaka kujua ukweli rejea katika histori ya uhuru wa Tanganyika. Ajiulize vipi Mkatoliki Mwalimu Nyerere aliweza kupokelewa na Waislamu Dar es Salaam na wakampa uongozi na baadae kumfanya Waziri Mkuu wa Tanganyika mwaka 1961? Waislamu wangekuwa na chuki na Wakristo Mwalimu Nyerere asingekuwa kama mtoto wa Bi MLUGURU BINT MUSSA akiingia nyumbani kwake Kirki Street akila, kulala na kufuliwa nguo zake pale. Mama zetu wangelikuwa wana chuki na Wakristo, TATU BINT MZEE asingelimwita Nyerere kaka. Waislamu wangelikuwa wana chuki na Wakristo, wasingelikuwa wanakula n a Wa k r i s t o w e n g i n e katika harusi za misiba yao, wangelikuwa na chuki
wasingeliwapangisha Wakristo katika nyumba zao Kariakoo, Ilala, Temeke na kwingineko. Kama hali ilikuwa hivyo, nini kimetokea hadi leo tumekuwa maadui? Jibu ni kuwa ulipopatikana uhuru roho ya Mwl Nyerere ikabadilika akawa si yule aliyeletwa osi ya TAA na Abdulwahid Sykess akawa si Nyerere yule aliyekuwa mkono wa kulia kwake kuna Sheikh Hassan Bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi na wengineo. Kisa ni kirefu sitaki kukuchosha matokeao ya kubadilika roho ya Nyerere na uadui wake si kwa wale tu waliomfadhili kama Abbdulwahid Sykes na Sheikh Hassan Bin Ameir na wengineo bali na Waislamu wote kwa ujumla. Nyerere kaenda mbali zaidi akaja na njama kwanza kudhalilisha Uislamu na pili kufuta historia ya kudai uhuru wa Tanganyika. Laiti watu wangejua historia ya Waislamu na Nyerere huenda hali ingekuwa tofauti kidogo. Mwisho wa kunukuu. Nasikitishwa na kejeli na matusi nisomayo katika mitandao ya kijamii, na magazeti mbali mbali y a k w a m b a Wa i s l a m u hawajasoma, Waislamu ni magaidi, Waislamu wanapeleka nchi pabaya! Najiuliza nini kimetokea, kulikoni. Haya ni matokeo ya mbegu ya chuki iliyopaliliwa na kumea vizuri na sasa kuanza kuchipua vyema. K i u h a l i s i a Wa i s l a m u hawana ugomvi na Wakristo isipokuwa Wakristo na Waislamu ni mithili ya watoto wawili wa mama mmoja na baba mmoja, mtoto mmoja ambaye ni Wakristo amedekezwa na kupendelewa na babaye
Makala
AN-NUUR
Kwa uamuzi huu wa Serikali, ina maana kuwa sasa itakuwa vigumu kwa MUM na Chukwani kupata wanafunzi wenye sifa kwa hiyo huenda vikalazimika kufuta kozi hizo. Hii maana yake ni kuwa uamuzi huu unapunguza idadi ya wanafunzi wa Kiislamu wanaokuwa na sifa za kupata elimu ya juu. Kinachosikitisha ni kuwa Serikali imeamua kukaa na Wakristo pekee kupitisha maamuzi mazito kama haya bila kujali athari yake kwa vijana wa Kiislamu na taasisi za Kiislamu nchini. Amesema mjumbe mmoja wa Islamic Education Panel akizungumzia suala hilo. Hii ni dharau iliyopitiliza kiwango, Serikali inachukuaje maamuzi kama haya bila kujali kuwa kuna shule za Kiislamu na Vyuo vya Ualimu vya Kiislamu pamoja na Vyuo Vikuu ambavyo vinategemea kupata wanafunzi kutokana na wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita wenye somo la Maarifa ya Uislamu? Amesema mjumbe huyo wa Islamic Education Panel ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina lake gazetini. Kama Serikali imeona kuna mantiki kujitoa katika kutahini somo hili, kwa nini ifanye kinyemela? Kwa nini isiwashirikishe wadau husika ili kujua, ni utaratibu gani mwingine utafanyika ili vyuo vya Kiislamu vilivyopo visiathirike? Kwa nini wasikae pamoja na Panel? Mbona waliwaita Wakristo? Kitu gani kiliwafanya wakwepe kuwaita Waislamu, ni dharau, UDINI, au kuna agenda ya siri? Mdau mmoja wa Kikristo aliyekuwa katika kikao hicho cha Machi kati ya Serikali na wadau wa Elimu wa Kikristo alipoulizwa kuwa katika kikao hicho Serikali imetoa
Inatoka Uk. 2
Dk. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani hoja gani ya kufuta mtihani huo alisema kuwa, hakuna jambo lililoelezwa la kujenga hoja madhubuti, lakini yeye binafsi anadhani ni kutokana na masuala ya Waislamu toka walipopinga matokeo ya Islamic mpaka ikabidi Baraza la Mitihani liyabadili. Wajumbe wa Islamic Education Panel wanasema kuwa, wakati Waislamu wametimiza matakwa yote ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya kuwa na Mihutasari na vitabu kwa ngazi zote, Wakristo hawakuwa w ametimiza matakwa hayo, hawakuwa hata na mihutasari, lakini somo lao lilikuwa likitahiniwa. Hata hivyo, akasema, hao hao ambao hawakuwa wametimiza matakwa ya Wizara na Baraza la Mitihani, ndio walioitwa kupitisha uamuzi wa Serikali kujitoa katika kutahini mtihani huo. Waislamu wakilalamika kuwa kuna ubaguzi, udhalilishaji, uonevu na udini, wanaambiwa wanafanya uchochezi, hivi Serikali inaweza kukaa na Waislamu pekee na kufanya maamuzi makubwa yenye kugusa masilahi ya Kanisa Katoliki na Wakristo wote, halafu ifanye tu kuwapelekea taarifa Baraza la Maaskofu juu ya maamuzi hayo? Alihoji. Wachambuzi wa masuala ya kidini na kijamii nchini wanasema kuwa huenda Serikali imeamua kujitoa katika suala hili ili ipate fursa ya kuweka mkakati mwingine wa kuibuka na somo la dini mseto baada ya kukwama huko nyuma. Hata hivyo wengine wanasema kuwa hii ni moja tu ya mikakati ya kupunguza idadi ya vijana wa Kiislamu wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu. Wengine wakakumbusha kuwa zilipoanzishwa shule za kwanza za seminari za Kiislamu, Serikali ilitangaza kuwa shule hizo sio shule zinazotambulika. Ni Madrasa. Kwa hiyo wanafunzi wake wakimaliza kidato cha nne wasingepatiwa nafasi za kusoma kidato cha tano katika shule za Serikali. Na kwamba kwa wale watakaomaliza kidato cha sita, wasingechaguliwa kuingia vyuo vikuu na vyuo vingine vya Serikali. Kwa vile isingewezekana kutangaza kuwa wasiotakiwa ni Waislamu pekee, ilibidi tangazo liguse shule zote pamoja na seminari za Kikristo. Hata hivyo, baadae walilazimka wenyewe kuondoa tena kimya kimya sera hiyo kabla haijafanyiwa kazi, baada ya kuona kuwa watakao athirika zaidi ni vijana wa Kikristo kwa sababu ni taasisi za Kikristo zilizokuwa na shule nyingi za seminari. Ni kwa sababu ya matukio kama hayo, baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa huenda kuna agenda ya siri inayowalenga Waislamu na ndio maana waliitwa Wakristo pekee ili waelimishwe kuwa wawe radhi kutoa muhanga mtihani wa Divinity. Kwa upande mwingine huenda hawakuitwa Waislamu kwa kuhowa kuwa wangehoji mambo ambayo yasingeweza kupatiwa majibu moja likiwa ni utaratibu gani umeandaliwa kuhakikisha kuwa MUM, Chukwani na
vyuo vingine vya Kiislamu vyenye kozi za Islamic Studies, Shariah na Islamic Banking, vitapata wanafunzi kulingana na vigezo vya Mamlaka ya Vyuo VikuuTanzania Commission for Universities (TCU). Habari kutoka ndani ya Bakwata na Islamic Education Panel zinasema kuwa taarifa kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi juu ya suala hilo, imeeleza kuwa nao Wizara wamefanya kupewa maelekezo na Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu. N a k w a m b a Wi z a r a ilitakiwa kukaa na wadau, kwa maana ya taasisi za kidini kuangalia suala hilo. Hata hivyo, haikuweza kufahamika kuwa uamuzi wa kutokuwashirikisha Waislamu na badala yake kukaa na Wakristo pekee, ilikuwa ni maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au ulikuwa uamuzi wa Kamishna wa Elimu. Wa d a d i s i w e n g i n e wanasema kuwa jambo hili limetokea Baraza la Mitihani ( N E C TA ) n a k w a m b a kama ambavyo Baraza hilo liliona umuhimu wa kuajiri Mchungaji wa kutizama masilahi ya wanafunzi wa Kikristo na kugoma kuajiri Muislamu, ndio mtindo huo huo umetumika katika kuita kikao cha Wizarani. Kutokana na hali hiyo, Waislamu kupitia taasisi zao, wamepanga kumuona Katibu Mkuu Kiongozi kupata ufafanuzi juu ya suala hilo. Na kwa kuwa suala hili linagusa masilahi ya Waislamu wote nchini, litafanyiwa taratibu za kujadiliwa na kupitishwa maamuzi ya pamoja. Hadi jana tukienda mitamboni juhudi za kuwapata wahusika Wizara ya Elimu na NECTA kuzungumzia suala hili, hazikuweza kufanikiwa.
ambalo halipo kuwa ni kosa kubwa na la kutisha kinchi. Wa k i m t u p i a l a w a m a Mwanasheria Mkuu, JUMAZA wakamkabili wakisema: We w e n i m w e l e d i zaidi wa mambo ya sheria na hivyo unafahamu fika kuwa dhamana ni haki ya mtuhumiwa kwa kesi kama hiyo, lakini bado Mashekhe wanaendelea kunyimwa dhamana hiyo na kupigwa
danedane. Sheria zinachezewa huku Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikibariki ukiukwaji huo kwa ukimya wake na kupongeza Jeshi la Polisi. Mbali ya kuwa dhamana ni haki yao, kesi yenyewe unafahamu wewe na Serikali kuwa kisheria kesi hiyo ililazimika isikilizwe ndani ya miezi minne na Sheria inaelekeza ikishindikana, basi kesi ifutwe, la kusikitisha leo ni mwezi wa sita udhalilishaji unaendelezwa huku wananchi
wakifanywa waamini kuwa nchi hii ina Utawala Bora na Kuheshimu Sheria. Wakikamilisha maelezo yao JUMAZA wakasema k u w a Wa i s l a m u w a Zanzibar hawajawahi kuona viongozi wa dini ya Kikristo wakidhalilishwa kwa namna yoyote ile kama wanavyofanyiwa viongozi wa Waislamu. Na wakamaliza kwa kuwataka wananchi kuungana na kutoa sauti moja ya
kupinga dhulma, uonevu na udhalilishaji kwa sababu hiyo sio yaliyotarajiwa kuletwa na kufanywa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Jumuiya ya Maimamu inatoa wito kwa Serikali na Wawakilishi wa wananchi kusimamia Utawala wa Haki na Sheria bila ubaguzi na kushirikiana pamoja na wananchi kutanguliza utetezi wa maslahi ya nchi kwanza. Maslahi ya vyama, vikundi vya watu na mtu binafsi
yatafuatia baadae. Walimaliza JUMAZA katika barua yao waliyoinakili kwa Waziri wa Sheria, Baraza la Mapinduzi, Jaji Mkuu, Baraza la Wawakilishi na Mkurugenzi wa Mashitaka. Wengine waliopewa nakala ni Shirika la Kimataifa la Kutetea Wafungwa (Amnesty International), Umoja wa Majaji na Makadhi Zanzibar, East Africa Law Society, Zanzibar Law Society na Waandishi wa Habari.
6
Na Omar Msangi
The Church is now totally dependent on State aid for the administration of these schools. If this aid were withdrawn the church will be forced to close its schools. Hii ni kauli ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) Fr Robbinson, D. W miaka ya 1960. Kauli hiyo inamaanisha kuwa Kanisa limekuwa tegemezi kabisa kwa Serikali katika kutoa pesa za kuendesha shule zake na kwamba ikiwa Serikali itasita kutoa fedha kwa shule hizo, basi Kanisa litalazimika kuzifunga. Hiyo ilikuwa ni mwaka 1965 ambapo inaelezwa kuwa hadi kukia mwaka 1964, kiasi cha asilimia 60 ya bajeti ya Kanisa Katoliki katika kuendesha shule zake ilikuwa inategemewa kutoka Serikalini. Kutoka katika Hazina yenye kuchangiwa na Watanzania wote. Kwa mujibu wa taarifa ya Padiri Robbinson, kufika mwaka huo wa 1965, ndio ikawa kwa asilimia mia moja (100%), ndio kanisa likawa linategemea kuchotewa pesa kutoka Hazina. Kwa upande mwingine, Padiri Dr. John Sivalon anasema kuwa, kutokana na ukweli kuwa wahitimu wengi wa shule za Kanisa za St. Marys Tabora na St. Francis Pugu, ndio walishika serikali, iliwezesha kukua kwa uhusiano kati ya viongozi wa Kanisa na wa Serikali na Chama (TANU/CCM). Na kwamba hali hii imefanya matendo, msimamo na uamuzi wa viongozi wa Serikali ufanane mara kwa mara kwa namna moja au nyingine na mafundisho na mwelekeo wa Kanisa. Na nini ulikuwa mwelekeo, mtizamo na msimamo wa Kanisa? Padri Sivalon anasema kuwa ulikuwa ule wa kupinga kuenea kwa dini ya Kiislamu na kwamba walifanya makusudi kujenga uhusiano na viongozi wa Serikali ili wawe na nafasi nzuri katika kujihami dhidi ya uenezi wa Uislamu. Padiri Sivalon anasema kuwa moja ya mambo ambayo maaskofu hawakupenda kuona, ni kuwepo kwa taasisi madhubuti za Waislamu zinazowajengea umoja na kuwaleta maendeleo. Waliitaja kwa jina Jumuiya ya Maendeleo ya Waislamu ya Afrika Mashariki-East A f r i c a M u s l i m We l f a r e Society (EAMWS). Na baada ya kuonyesha kuwa hawataki kuiona EAMWS, kilichofuatia ni Mwalimu Nyerere kupiga marufuku taasisi hiyo na Serikali kusimamia kuundwa kwa Bakwata kule Iringa. Nikutokana na historia hiyo, ndio maana mpaka leo akina Mheshimiwa Anna Abdallah bado hawaoni vibaya kusimama bungeni kuitaka Serikali iendelee kuwadhibiti Waislamu chini ya Bakwata. Ijumaa wiki iliyopita wakati wa mazishi ya watu waliokufa katika mlipuko wa Bomu
MAKALA
AN-NUUR
Bomu lisiunganishwe na madai ya Waislam Yaliyosemwa Diamond Jubilee haya hapa Na huu ndio Waislam wanaita Mfumokristo
Kanisani Arusha, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa alihusisha tukio la kulipuliwa bomu Kanisani na Waislamu. Katika maelezo yake mbele ya Waziri Mkuu, Askofu Ngalalekumtwa amesema kuwa katika miongo mitatu hali ya usalama nchini imetoweka na hili linafanywa na baadhi ya watu wasiolitakia mema taifa hili na wapinga Ukristo. Akifafanua na kuwataja hao wasiolitakia mema taifa hili na wapinga Ukristo, akasema kuwa ni wale waliofanya vikao vingi na cha mwisho kilikuwa Oktoba 16 mwaka 2011 katika ukumbi wa Diamond Jubilee na kuazimia kuuwa ili kutokomeza Ukristo. Akifafanua zaidi akasema kuwa katika kongamano la Diamond walichochea chuki ya kidini kati ya Waislamu na Wakristo kwa kudai kuwa Serikali ya Tanzania inaongozwa kwa mfumokristo ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Nyerere. Akinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari Askofu Ta r c i s i u s N g a l a l e k u m t w a alisema kuwa katika kongamano hilo, washiriki waliaminishwa kuwa Serikali inatoa fedha za ruzuku kujenga shule na taasisi za Kanisa kutokana na kuwapo mkataba maalum kati ya Kanisa na Serikali, jambo ambalo siyo kweli. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba Serikali haikukanusha madai na uchochezi huo, licha ya mambo hayo kufanyika na kusemwa hadharani kwa wahusika kuzunguka nchi nzima kueneza chuki na uchochezi huo. N i s e m e k u w a , kinachosikitisha ni kuwa Serikali haijajibu wala kutekeleza madai haya ya Waislamu. Sio kuwa haijakanusha kama anavyosema Askofu Ngalalekumtwa. Serikali haiwezi kukanusha kwa sababu ni madai ya kweli. Na kama anavyosema Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Waislamu walikutana Diamond Jubilee. Hawakujicha. Walitembea nchi nzima na kueleza madai yao hadharani. Walifanya hivyo kwa sababu hawakuwa wakitangaza biashara ya bangi wala kusema mambo ya kuzua na kuchochea chuki wala kutangaza ubaya na Wakristo. Waliyosema yote yalikuwa ya kweli. Kwa bahati mbaya Serikali ikaona namna ya kujibu ni kukaa kimya. Labda tumuulize Askofu Ngalalekumtwa, hivi ingekuwa n i k w e l i k u w a Wa i s l a m u waliokutana Oktoba 16 mwaka 2011 katika ukumbi wa Diamond Jubilee waliazimia kuuwa (Wakristo) ili kutokomeza Ukristo na wakatembea nchi nzima kutangaza azma hiyo, leo 2013, bado nchi ingekuwa salama? Kwa wanasiasa kusema mambo ya kuzua kama haya na hata makubwa zaidi, inaweza isiwe ni jambo la kushangaza sana; lakini inapokuwa ni kiongozi wa Kidini, kidogo hapo inaleta maswali mengi na utata mwingi! Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kamati Maalumu iliyoandaa Makongamano ya Waislamu Dhidi ya Mfumokristo na wakaandaa lile kongamano la Ukumbi wa Diamond Jubilee Oktoba 16, 2011, katika mwaka wa fedha wa 2009/10 Serikali ilitumia jumla ya shilingi 85,776,373,200 katika hospitali na taasisi nyingine za huduma ya afya zinazomilikiwa na makanisa na zile zinazomilikiwa na Serikali kwa ajili ya kulipa mishahara wafanyakazi na gharama za uendeshaji. Kati ya fedha hizo, shilingi 46,624, 820, 500 ambazo ni sawa na asilimia 54.4 ya fedha zote, zilipelekwa katika hospitali na taasisi nyingine za huduma za afya zinazomilikiwa na makanisa. Hospitali na taasisi zinazomilikiwa na Serikali zilipatiwa shilingi 39,151,552,700 sawa na asilimia 45.6 Lakini ukiacha taarifa hizi za kiutati, Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake katika Misa ya kusimikwa Askofu wa Jimbo la Dodoma , Gervas Nyaisonga, Machi mwaka 2011 alisema kuwa mwaka 2010 Serikali yake iliwapa Wakristo ruzuku ya shilingi bilioni 61.9 (61,900,000,000). Na kwamba kwa mwaka 2011 ruzuku hiyo ilitarajiwa kukia shilingi bilioni 112. Yote haya yanafanyika kwa sababu toka huko nyuma kama alivyosema Fr. Robbinson, Serikali ilikuwa imejiwekea utaratibu wa kuwapa Wakristo fedha kutoka hazina ya nchi kuendesha shughuli zao na kufika mwaka 1992 ndio
Tangazo
AN-NUUR
Makala
AN-NUUR
Vipi hii inakufaa? Inaonekana inafanana sana na rangi (ya njano) ya kile chama chako. Lakini sasa hivi ni kuchagua mtu siyo mambo ya chama-Askofu Alex Malasusa. Ndugu mhariri naomba unipatie nafasi katika gazeti lako ili niweze kuwatahadharisha wale wanaodhani kwamba vuguvugu la Waislamu la kudai mfumokristo ukomeshwe zinaweza kunyamazishwa na propaganda na uongo na unaoenezwa na baadhi ya Maaskofu na mawakala wao. Tumeearifiwa kupitia katika vyombo vya habari kwamba siku ya maziko ya watu waliouwawa katika mlipuko wa bomu uliotokea kanisani Arusha, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa alinukuliwa akidai kwamba walipuaji wa bomu wana uhusiano na Waislamu waliokutana Diamond Jubilee tarehe 16 Oktoba, 2011 kuzungumzia mfumokristo. Aidha juma hili Dr Kitima ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Saint Agustino (SAUTI) aliiambia Star Television katika kipindi kimoja cha TV hiyo kwamba viko vyuo hapa nchini kimojawapo kikiwa huko Morogoro ambavyo vinatoa magaidi. Huu ndiyo ninaosema ni uongo na propaganda za wale wanaofaidika na mfumokristo. Tuliona jinsi mara baada ya mlipuko wa bomu kutokea Arusha ambavyo haraka haraka ilikimbiliwa kuwakamata Waarabu. Hii ilikuwa ni kuweka taswira kwamba walipuaji walikuwa ni Waislamu. Hatujaambiwa kwamba hakuna Wazungu waliokuwa Arusha siku ile ya tukio. Bila shaka watu wamejengewa dhana potofu kwamba Wazungu ni Wakristo hivyo hawawezi kufanya uovu ule! Kuhusu kongamano la Diamond Jubilee ni kweli kwamba lilifanyika na kufuatiliwa na makongamano ya nchi nzima. Yaliyosemwa pale yamo katika kijitabu na katika CD/DVD. Kijitabu kilisambazwa katika osi zote za serikali. Kwa hiyo kongomano lile halikuwa na siri yoyote na wala maudhui yake kamwe hayawezi kusemwa kwamba ni siri. Viongozi wa serikali, maaskofu wanatambua wazi kwamba maudhui ya kongamano la Diamond ilikuwa ni kujaribu kuwazindua wale wanaodhani kwamba kunaweza kuwepo amani ya kweli na ya kudumu katika taifa ambalo baadhi ya watu wake wanabaguliwa kwa misingi ya dini yao. Kijitabu kile kimesheheni mifano kadha wa kadha ya kuonesha jinsi serikali inavyotumia rasilimali za nchi kuwanufaisha Wakristo huku Waislamu wakibanwa. Mwito ulitolewa kwa serikali kukomesha upendeleo huo ambao ndiyo ulioitwa mfumokristo. Wa i s l a m u h a w a k u k u t a n a Diamond kutangaza vita dhidi ya Wakristo. Wanajua kwamba Wakristo wengi wa kawaida hawajui uwepo wa mfumokristo kwa maana ya ubaguzi dhidi ya Waislamu. Wamezoea kujiona wakiwa wengi katika shule na vyuo vya umma. Wamezoea kuwaona baba zao na shangazi zao wakiwa katika maosi ya umma peke yao. Wengi wa Wakristo wa kawaida wameelewa kwamba Waislamu hawako shuleni, vyuoni na maosini kwa sababu
kama inavyosemwa mara kwa mara na wakuu wa mfumokristo kuwa (eti) Waislamu hawapendi kusoma. Wote tuliokuwa Diamond tunatambua ukweli huu na hivyo hatuna sababu ya kutangaza vita na Wakristo wala nyumba zao za ibada. Na kwa kuwa kijitabu kipo na DVD pia zipo na hilo halimo, ni dhahiri basi kwamba uongo na propaganda za Maaskofu lengo lake ni kuwazuia Waislamu kufahamamishana ukweli kuhusu uwepo wa mfumokristo na kuwataka waupinge kwa nguvu zao zote ili kuihakikishia Tanzania amani ya kweli na ya kudumu. Ifahamike pia kwamba Waislamu wote tuliokuwa Diamond Jubilee tunafahamu wazi kwamba maaskofu wote wanajua uwepo wa mfumokristo na namna ambavyo wao binafsi na makanisa yao yatakavyoathirika kama mfumokristo hautaendelea kuwepo. Lakini pia tunajua wote tuliokwenda Diamond Jubilee kwamba sio wote wanaodai kuwa wanaipenda nchi na kuitakia amani, wanasema kweli. Tazama gazeti la Mwananchi la Oktoba 17, 2010 ambalo liliripoti kwamba MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Alex Malasusa amewataka Watanzania kuchagua kiongozi makini badala ya chama. Ona jinsi alivyowahamasisha waamini wake kuinyima CCM kura mwaka 2010, rejea maneno yafuatayo yaliyonukuliwa kutoka Gazeti la Mwananchi la tarehe niliyoitaja, Wakati akipiga mnada wa khanga, ambayo ilikuwa na rangi ya njano, Askofu Malasusa alimtazama mmoja wa watu waliotaka kununua khanga hiyo na kumuuliza: Vipi hii inakufaa? Inaonekana inafanana sana na rangi ya kile chama chako. Lakini sasa hivi ni kuchagua mtu siyo mambo ya chama. Ifahamike pia kwamba wote tuliokuwa Diamond tunafahamu ka lipi lilikuwa chaguo la Maaskofu katika uchaguzi wa mwaka 2010
na kipi chama kilikuwa chaguo lao na kwa nini. Na kwa bahati nzuri hawakujicha. Wote tuliokuwa Diamond tunaelewa kwamba maana ya udini ambayo sisi tumeiita mfumokristo ambayo in dhana inayoelezea upendeleo unaofanywa na serikali kuwapendelea Wakristo huku ikiwabana Waislamu siyo sawa na dhana ya udini inayotamkwa na maaskofu. Kwa watumishi hawa wa Bwana maana ya udini ni Muislamu kupata haki yake! Rais akimteua Muislamu kuongoza taasisi au kuwa katika cheo fulani huo ni udini. Na neno hili kuwa udini ni kumpa Muislamu nafasi limedhihirika hata katika Bunge linaloendelea hivi sasa. Waziri wa nchi Osi ya Rais Prof. Mark Mwandosya alisimama kumtetea Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete kwamba hana udini na kutoa ushahidi kuwa Osi ya Rais imejaa mawaziri, makatibu na wakurugenzi Wakristo. Kwa mtazamo wa wenzetu hawa kuwepo Wakristo wenyewe katika osi moja ya umma, huo si udini! Lakini huko UDOM kumejaa udini na bunge limeelezwa kwa sababu tu yuko kiongozi mmoja Muislamu tena Profesa! Wote tuliokwenda Diamond Jubilee tunafahamu kwamba maaskofu wanapozungumzia umoja wa kitaifa wanazungumzia maslahi yao serikalini. Kila anayepinga maslahi ya kanisa serikalini anaonekana kuhatarisha amani. Maneno yatatungwa ili kuwapiga vita. Katika tukio la kuchomwa makanisa Mbagala, maaskofu walitumia fursa hiyo kuitaka serikali ifikirie uwezekano wa kupiga marufuku vazi la hijabu katika osi za umma na mashuleni. Katika tamko lao la tarehe 18 Oktoba 2012 wanasema, Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za Watanzania. Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala
katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi? Kwa maaskofu kupinga maadili ya dini za wengine ndio utaifa wenyewe. Maaskofu wanapinga vazi la hijab kwa hoja ya Utanzania. Hata siku moja hawapingi makasisi na watawa kuvaa nguo na misalaba mikubwa inayoashiria dini zao. Kwa maaskofu dini ya Tanzania ni Ukristo na Watanzania wenye haki mbele ya serikali ni Wakristo. Wengine sisi ni kama wapagazi tu au wapangaji. Tunaweza kutakiwa kuondoka wakati wowote. Kwao wao lazima tuwe na adabu! Hili si udini! Kwa sisi tuliokuwa Diamond Jubilee, tungependa kutambuliwa kama Waislamu wa Tanzania badala ya Watanzania Waislamu. Wote tuliokwenda Diamond Jubilee tunatambua dhamira njema tuliyo nayo hata sasa kwa taifa hili. Tuna yakini kwamba Waislamu hawataweza kuendelea kusubiri kwa miaka mingine 50 wakiwa watazamaji tu na wengine wakifaidi maliasili na rasilimali za nchi yetu. Hawatakubali kuendelea kulipa kodi na kuiacha serikali kuendelea kutoa sehemu ya kodi zao kuwapa makanisa kuendeshea taasisi zao za elimu na afya kupitia muafaka wa MoU. Wote tuliokuwa Diamond Jubilee hatuwezi kusema kwamba hatuna wasiwasi kwamba huenda baadhi ya maaskofu hulipwa mishahara yao kupitia pesa za MoU kwa ulaghai wakijifanya kama watumishi wa afya katika hospitali za kanisa wakati hawafanyi kazi hizo. Kwa maaskofu hili la kupewa pesa za serikali kuendeshea mambo yao si udini! Ningependa kuishauri serikali yangu na maaskofu na wale mawakala wa mfumokristo kwamba amani ya Tanzania itakuwa endelevu kwa kuzingatia haki sawa kwa wote. Ingekuwa amani inadumishwa kwa kuwakamata wanaosema dhidi ya maovu na kuwafunga, basi
wangefanikwa Makaburu wa Afrika Kusini. Waislamu waliokwenda Diamond hawawachukii Wakristo japo wasitegemewa kuwapenda maaskofu ambao kila uchao dua yao ni kuona Waislamu wakikwa na mabalaa. Kila linalotakiwa na Waislamu: Iwe Mahakama ya Kadhi, OIC, haki sawa, elimu kwa Waislamu, uteuzi na ajira bila ubaguzi, wao hutoa kauli za kupinga. Japo maaskofu hawategemei siku moja serikali iwaaambie waache kuhubiri hadharani uungu wa Yesu, lakini kila siku wanaichagiza serikali iwazuie Waislamu kuhubiri kuwa Issa bin Mariam (Yesu) si Mungu! Wa i s l a m u w a l i o k w e n d a Diamond Jubilee kuupinga mfumokristo na kuchukua azimio la kukisha ujumbe ule nchi nzima hawakutegemea maaskofu waje na kauli yenye heri nao. Hivyo kama ambavyo hatukushangaa Makaburu na wakoloni wa Kireno walivyowaua akina Steve Biko, Solomoni Mahlangu na Edward Mondlane, hatuwashangai maaskofu wanapoitaka serikali kuwashughulikia walikwenda Diamond kuupinga mfumokristo. Mfumokristo ndiyo lifeline yao! Mwenye kutaka kuingia hapo anatafuta ugomvi. Waislamu waliokwenda Diamond wako tayari kwa ugomvi huo kwa sababu hapo ndiko kwenye salama ya Tanzania ya sasa na ya baadaye. Tutaitwa magaidi, wachochezi, mujahidina, siasa kali n.k., lakini hatuaacha kusema dhidi ya mfumokristo kwa sababu hii ni haki yetu ya kikatiba ya kutoa maoni yetu na pia haki yetu ya kibinaadamu na ya kiungwana ya kujaribu kuiepusha nchi yetu na machafuko. Maneno ya waliokwenda Damond Jubilee hayatofautiani na yale ya Shahid Malcom X aliyepigania haki za watu weusi huko Marekani. Wakati anatafakari hali yake na watu Weusi wenzake kama wahanga wa mfumo wa ubaguzi ulikuwepo kule aliposema: Im one of 22 million black people who are the victims of Americanism. I see America through the eyes of a victim. I do not see American dream, I see American nightmare. Kuhusu nini cha kufanya ili kujikomboa na hali ya Weusi wa Marekani Malcom X alipinga kuwakumbatia wabaguzi na kuwashauri Weusi wenzake hivi: . Everything, anything that you beg other men to set you free you will never be free. Freedom is something that you have to do for yourself. And until the American Negro let the white men know that we are real ready and willing to pay the price necessary for freedom our people will always be walking around here second class citizen which we call 20 century slaves.. The price of freedom is death! Wa i s l a m u w a l i o k w e n d a Diamond Jubilee wanaamini kuwa Waislamu wa nchi hii wanadhulumiwa, wanabaguliwa na kunyimwa haki zao za msingi. Wanaamini kuwa inawabidi kufanya juhudi kubwa na kujitolea muhanga kama walivyofanya kuzunguka nchi nzima kulieza jambo hili, ndio watapata haki zao. Tunatoa mwito kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao tuungane kuuondoa mfumo unaoendeleza ubaguzi na dhulma nchini.
Makala
AN-NUUR
Mwandishi Ibn e Abdul Haq anakamilisha uchambuzi wa ushahidi wa mashirika ya upepelezi ya Marekani kuhusu kuhusika kwa Waislamu, na Al Qaeda, katika shambulio la Septemba 11 mwaka 2001 nchini humo. 7 . Wa s h i r i k a w a A l Q a e d a walikamatwa katika video za usalama katika uwanja wa ndege? Mojawapo ya ushahidi kwa madai kuwa washirika wa Al Qaeda walikuwa katika ndege hizo ni fremu za picha za mikanda ya video, zinazosemekana zilichukuliwa na camera za usalama zinazodaiwa kuonyesha watekaji waliingia katika viwanja vya ndege (ndege hizo zilikotokea). Muda mfupi baada ya mashambulio, kwa mfano picha zinazomwonyesha Mohamed al-Atta na al-Omari katika uwanja wa ndege zilizungushwa duniani kote. Hata hivyo, ingawa ilikuwa inadhaniwa kuwa picha hizo zilipigwakatika uwanja wa ndege wa Boston, ukweli ni kuwa zilipigwa katika uwanja wa ndege wa Portland. Hakuna picha zinazomwonyesha Atta au mwingine kati ya wanaodaiwa kuteka nyara ndege katika uwanja wa ndege wa Logan mjini Boston ziliwahi kutolewa. Sana sana tuna ushahidi wa picha kuwa Atta na al-Omari walikuwa katika uwanja wa ndege wa Portland. Hivyo, uthibitisho wa video kuwa watekaji hao waliingia viwanja vya ndege siku hiyo 9/11 haupo. 8. Majina ya watekaji yalikuwa katika orodha ya abiria? Je, nini kuhusu orodha za walioingia katika ndege, ambazo zinaweka majina ya abiria wote? Kama wanaodaiwa ni watekaji walinunua tiketi na kuingia
ambazo inazitumia kuwanyamazisha raia wa Marekani bila kupitia mkondo wa sheria. Soma: http://www.salem-news.com/ articles/may042013/drones-bostonwh.php Idara ya Usalama wa Ndani ina risasi zaidi ya bilioni moja, vifaru, kikosi maalum cha kijeshi. Kambi za wafungwa zimejengwa. Bunge la Marekani lina fedha za walipakodi kuilipa FBI (Shirika la Upelelezi) kuwabambika wasio na hatia na kuwapeleka jela. Hii ndiyo nchi ambayo Marekani imekuwa. Haya ndiyo mashirika ya usalama iliyo nayo, ikijaza mifuko yao kwa kuteketeza maisha ya wasio na hatia na wanyonge. In God we trust (Katika Mungu tunatumaini) ndiyo nembo ya serikali ya Marekani. Ingefaa isomeke: In Satan we follow. (Katika Shetani tunafuata). (Paul Craig Roberts alikuwa Naibu Waziri wa Fedha na Sera za Uchumi na Mhariri mshiriki wa jarida la Wall Street Journal. Amekuwa mwanasafu wa jarida la kiuchumi la Business Week, mtandao wa habari wa Scripps Howard. na Creators Syndicate (jukwaa la waandishi). Amekuwa na miito mingi kufundisha katika vyuo vikuu, Makala zake katika mtandao zimewavutia wasomaji kote duniani. Kitabu chake kipya Kushindwa kwa ubepari usio na mpaka na kuyeyuka kiuchumi kwa ukanda wa Magharibi (The Failure of Laissez-Faire Capitalism and Economic Dissolution of the West) sasa kinapatikana. Mfasiri kwa Kiswahili Anil Kija)
lazima ni kazi ya ndani. Hitimisho: Baada ya muongo mmoja wa vita vilivyoanzishwa kwa madai ya uwongo kukaribia kumalizika nchini Afghanistan, kuanzia 2014, suala la nani aliyefaidika na 9/11 halipo tena mashakani. Katika miaka 12 iliyopita, dunia imeona faida kubwa waliyopata Marekani, Ulaya Magharibi na Israel kisiasa, kidiplomasia, udhibiti wa maeneo na uchumi kutokana na vita hivyo. Afghanistan, Irak na majirani zao wa Kiislamu, kwa upande mwingine, wamekuwa waathirika wa utumiaji nguvu, umwagaji damu na uharamia uliofanywa na Marekani na washirika wake wa NATO. Mfumo wa kijeshi wa nchi za Magharibi umekuwa ukikanyaga kila mahali duniani miguu yake ikiwa na madoa ya damu ya mamilioni ya Waislamu wasio na hatia. Maelezo rasmi na ushahidi wote uliotoa kuwa Marekani ilishambuliwa na Waislamu mnano Septemba 11, yakiangaliwa kwa undani, yanaelekea kuwa yametengenezwa. Kama hilo litathibitishwa, matokeo yake yatakuwa ya kutisha. Kuwagundua na kuwapeleka mahakamani wahusika halisi wa mashambulio ya Septemba 11 bila shaka kungekuwa na umuhimu mkubwa. Uhakika wa watu katika uadilifu na usahihi kisiasa wa nchi za Magharibi ungeporomoka. Matokeo ya kwanza, hata hivyo, ingekuwa kugeuza mielekeo na sera zilizojengwa juu ya mtazamo kuwa Marekani ilishambuliwa na Waislamu hapo Septemba 11.
10
Sie ni hadithi ya mtoto kulilia wembe Huenda nasi tunataka tuletewe droni Tutafakari ya Umar Farouk Mutallab
Na Omar Msangi
Makala
AN-NUUR
Kuna wasiwasi na uwezekano mkubwa kwamba huenda tukio la bomu Kanisani Arusha, likatumika kujenga hoja kuwa sasa Tanzania inakabiliwa na kitisho cha ugaidi wa Al Shabab, Al Qaidah na magaidi wengine. Na hilo likifanyika, utakuwa ni msiba kwa taifa, lakini kwa wakati mwingine kuwa mafanikio makubwa kwa wale ambao kwa muda mrefu sasa walikuwa wakionyesha hamu ya kuona nchi hii kuwa nayo inasajiliwa kuwa na magaidi. Na hilo likitimia, itahalalisha uwepo wa kudumu wa FBI/CIA na hata vikosi vya kijeshi na droni. Kauli ya hivi karibuni ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Saidi Mwema kwamba katika kuchunguza tukio la Arusha wanashirikiana na makachero wa Kenya kwa sababu wao wana uzoefu wa mambo haya, yaweza kwa upande mmoja isiwe na tatizo. Kwa maana kuwa ikaonekana ni kauli ya kuonyesha tu kusaidiana majirani katika shida kama hii. Hata hivyo, kutokana na kauli za wanasiasa huko nyuma na hata vyombo vya usalama ambazo zimekuwa zikionyesha wazi kuwa kulikuwa na hamu ya kutangaza kuwa tuna ugaidi wa Al Shabab na Al Qaidah, huenda kuwepo k w a m a k a c h e r o wa Kenya kukakamilisha azma hiyo. Wasiwasi ni kwamba iwapo makachero hao watasema kuwa bomu la Arusha linafanana na yale yaliyokuwa yakilipuliwa Kenya ambayo yalidaiwa kuwa ni ya Al Shabab, basi hiyo itatosha kutangaza kuingia kwa Al Shabab Tanzania na mengine kufuatia. Wasiwasi huu unapata nguvu zaidi kwa sababu ni kiasi wiki mbili tu zilizopita, Polisi wetu walisema kuwa wana taarifa za ki-intelijinsia zinazoonyesha kuwa Tanzania inakabiliwa na kitisho cha ugaidi wa al Shabab na al Qaidah. Hoja hapa sio kuwa vyombo vyetu vya usalama visifanye kazi na kutekeleza wajibu wao kutizama kuwa nchini kuna vikundi vyovyote vya kigaidi na kuchukua hatua. Lakini ukiacha propaganda, ukweli uliokwisha dhihirika mpaka sasa ni kuwa kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi imekuwa kama mkakati na mipango ya mabeberu ya kutimiza malengo yao katika nchi mbalimbali duniani. Na
Quran hadi wakati wa kwenda darasani. Wakasema pia kuwa Umar alikuwa akitumia kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani kukaa Itiqaaf Msikitini na kwamba alikuwa akiwapa nasaha vijana wenzake wasiwe na mahusiano na wasichana ya uboy na girl friends, labda kama ni kutaka uchumba. Kwamba madai haya juu ya Uislamu wa Umar ni sahihi au ya uwongo, sio muhimu. Muhimu hapa ni mambo mawili. Moja ni hilo la kuunganisha Uislamu na ugaidi. Na pili, jinsi watu walivyopumbazwa na kuathiriwa katika kukiri kwao kiasi kwamba hawataki tena kujua ukweli. Wanachoshikilia ni propaganda wanayopewa na makachero wa Serikali. Hawana haja ya kuwasikiliza akina Kurt Haskell walioshuhudia tukio. Watu wamepumbazwa kwa propaganda hawaoni, hawahoji wala hawasikii. Mwaka 2005 liliwahi kuandika gazeti moja katika ukurasa wake wa mbele kuwa Waislamu walikuwa wameingiza majambia, mapanga na silaha nyingine kwa ajili ya kupambana na Wakristo. Likasema kuwa silaha hizo zilikuwa zimehifadhiwa katika Misikiti Dar es Salaam na Morogoro. Taarifa kama hizi ambazo zimekuwa zikirejewa kwa namna tofauti tofauti, hazikuwahi kukanushwa wala kukemewa na Serikali hata mara moja. Wakati ule baada ya kuona kuwa Serikali imekaa kimya, gazeti la An nuur liliandika likihoji kuwa mchezo kama huo ukiachwa, je, jamii haioni kuwa kama itatokea tu vurugu, au akatokea kichaa mmoja kupiga mtu jiwe kanisani au kutia moto Kanisa, hatuoni kuwa Wakristo watakimbilia kusema kuwa ni Waislamu kwa sababu walishaambiwa kuwa wameandaa silaha? Mantiki ya hoja ya An nuur ilikuwa kwamba kama madai yale yalikuwa ni kweli, basi wahusika wakamatwe wakishwe mahakamani. Lakini kama ilikuwa ni mambo ya kuzua, yakemewe, yasiachwe yakaathiri ufahamu, uelewa na uoni wa watu wetu. Hilo halikufanyika. Hivi watu waliopiga propaganda chafu kama hizi, wanashindwa kupanga tukio ili kutaka kuthibitisha madai yao? Na hata wakishindwa kupanga na kutekeleza, hivi likitokea tukio lolote la kihalifu kama ilivyotokea Zanzibar au hili la bomu Arusha (na hata kilichodaiwa kuwa ni kuchomwa makanisa Mbagala katika maandamano), watashindwa kutumia tukio hilo kupiga propaganda kujenga uwongo kuwa wahusika ni wale walioingiza majambia mwaka 2005?
11
Makala/Tangazo
AN-NUUR
miaka 20 ijayo, wakati Israel inaendelea na uvamizi wa ardhi bila ya kikwazo. Mwishowe mazungumzo hayatafanikiwa na hakutakuwa na amani tunayotarajia. Tumemaliza zaidi ya nusu karne. Hii ni mara ya kwanza tunaadhimisha Nakba wakati Palestina imetambuliwa kama Dola katika Umoja wa Mataifa. Ingawa tungali tuko chini ya ukoloni wa Israel, tumechukua hatua thabiti kuelekea tunakokusudia. Tutaendelea kuelekea huko ili kushinda haki yetu ya kimsingi kama taifa. Ni lazima tukomeshe miaka 65 ya ufedhuli wa Israel. Ulimwengu hauwezi kuendelea kuadhimisha siku kama hii bila ya kuchukua hatua thabiti. Ni lazima Israel itanabahi kuwa kukataa kuwapa Wapalestina haki yao kutawagharimu sana. Kukubali kuishi kwa amani ni njia pekee waliyo nayo. Hawana njia nyingine. Bahati mbaya, jambo hili halijaingia katika akili za Waisrael na ndio maana wanaendelea kujidanganya. Saeb Erekat ni Mkuu wa Mazungumzo ya amani kwa niaba ya Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO). Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 Email: pict@pal-tz.org Website: www. pal-tz.org
MAWASILIANO Zaidi: Piga Simu: 0789 272 737 Maombi yote yatumwe katika mtandano. Email: fairlandcom@yahoo.com Au kwa Barua S.L.P 4804- DSM MAOMBI YAAMBATANISHWE NA PASSPORT SIZE.
12
AN-NUUR
MAKALA
MAULID!!! MAULID!!!
12
Masjid Allah Karim Kazimzumbwi Kisarawe Inawaalika waislamu wote katika Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) Kazimzumbwi Kisarawe, Tarehe 25/05/2013, siku ya Jumamosi Saa 2:30 Baada ya Swalatul Ishaa , Inshaalah. Wafadhili wa maulidi Hii ni. 1. Sheikh Juma Sadiki Muyenga 2. Mohamed Rak Nurmohamed Satya 3. Ndugu wa Familia ya Madenge
Balozi wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Ujerumani, Av i P r i m o r, a m e k i r i kwamba Shirika la Kijasusi la Israel MOSSAD, ndilo lililopanga na kutekeleza njama za kumuua Emad Mughniya, kamanda wa Hizbullah Februari mwaka 2008 mjini Damascus, Syria. Avi Primor ameyaeleza hayo kwenye mahojiano na televisheni moja nchini Ujerumani na kusisitiza kwamba, utawala wa Israel ndio uliotekeleza shambulio la kumuua kigaidi kamanda Mughniya. Hayo yanajitokeza katika hali ambayo utawala wa Kizayuni wa Israel mara zote umekuwa ukikanusha
yale ya Zanzibar, ili kuondoa hisia zinazoweza kusababisha chuki na kudhaniana vibaya kati ya watu wa dini tofauti hapa nchini. Awali, Wanazuoni hao wametoa kauli ya kulani shambulizi hilo la kihalifu na ukatili. Hay-atul Ulamaa inachukua nafasi hii kulaani vikali kitendo hicho ambacho hakikubaliki kidini na kibinaadamu (na) tunatumia fursa hii kuwapa
pole wale wote walioathirika kwa njia moja au nyengine na tukio hilo na kuwaombea waliojeruhiwa wapate nafuu haraka ili waweze kuendelea na shughuli za kila siku za ujenzi wa Taifa. Imesema taarifa hiyo huku ikivitaka vyombo vya habari kuwa makini pale vinaporipoti matukio kama haya, bila kusindikizwa na mitazamo ya kiitikadi walizo nazo ili kuzuia uwezekano wa kusababisha kutokea machafuko hapa nchini.
Amesema hayo katika mkutano wa Jumuiya hiyo mjini Cairo, ambako pia ametaka kuanza kuchukuliwa hatua za kisiasa na kidiplomasia za kuulazimisha utawala wa Kizayuni kusimamisha hujuma zake dhidi ya Wapalestina. Baraza Kuu la Jumuiya ya Arab League lilihitimisha kikao chake hicho cha saa mili kujadili jinai za kila siku za Israel katika mji wa Quds Tukufu, bila kutoa tamko lolote rasmi juu ya suala hilo. Hayo yanajiri huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukizidisha jinai za kila aina dhidi ya wananchi wa Palestina wasio na ulinzi wowote.
TEHRAN Chombo cha kutegua bomu baharini kilichotengenezwa na wataalamu wa Iran kimezinduliwa. Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibullah Sayyari, amezindua chombo hicho na amesema, Iran ni kati ya nchi chache duniani zenye uwezo wa kutegua na kuondoa mabomu baharini. Kamanda huyo amesema hayo wakati wa mazoezi ya kutegua mabomu baharini, yanayofanyika baharini kusini mwa Iran ambako mfumo huo umezinduliwa. Sayyari amesema Jeshi la Wanamaji la Iran linafuatilia kwa karibu
harakati za vikosi vya kigeni katika eneo la Ghuba ya Uajemi, ili kuhakikisha kuwa hakuna tishio lolote dhidi ya nchi hiyo. Amesema Jamhuri ya Kiislamu imethibitisha kuwa nchi za eneo hilo zinaweza kusimamia usalama wa eneo hilo bila kuwepo vikosi vya kigeni. Hivi karibuni Jeshi la Wanamaji la Iran lilianzisha mazoezi ya kutegua mabomu baharini Mashariki mwa Lango la Bahari la Hormuz na Ghuba ya Oman. Iran mara kwa mara imezihakikishia nchi za eneo hilo kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi si tishio na kwamba lengo lake ni kujihami.
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.