You are on page 1of 2

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425

PRESIDENTS OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM.

Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Abdulrahaman Kinana kuomboleza kifo cha msanii maarufu nchini ambaye pia alikuwa kada na kiongozi wa CCM, Ndugu Salum Shomvi Tambalizeni. Ndugu Tambalizeni ambaye alifariki dunia juzi, Jumamosi, Oktoba 12, 2013 kwa matatizo ya moyo, alizikwa jana, Jumapili, Oktoba 13, 2013, kijijini kwao Marumbo, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amesema kuwa kifo cha Ndugu Tambalizeni kimelinyanganya Taifa la Tanzania msanii hodari na mzalendo wa kweli kweli ambaye alitumia vipaji vyake vya sanaa kuijenga, kuitetea na kuilinda nchi yake. Kwa hakika, nchi yetu na chama chetu, Chama cha Mapinduzi, kimepoteza hazina kubwa ya kipaji cha usanii. Kifo cha Ndugu Tambalizeni kimetuacha masikini zaidi kwa sababu ya vipaji vya msanii huyo na uzalendo wake ulimsukuma kuvitumia vipaji vyake ipasavyo na kwa manufaa ya kuijenga, kuitetea na kuilinda nchi yetu. Kupitia mashairi yake na tenzi zake zenye busara, mvuto na umahiri mkubwa wa utunzi, Ndugu Tambalizeni alitoa mafunzo makubwa kwa jamii yetu, alitoa mchango mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu na dhahiri alikuwa kada wa kujivunia na kutegemewa wa Chama chetu cha Mapinduzi, amesema Rais Kikwete na kusisitiza: Nakutumia wewe Katibu Mkuu wa Chama Chetu, Mheshimiwa Kinana salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza

kifo cha mtumishi wa Chama chetu kwa miaka 14 hadi alipoomba kustaafu mwenyewe na kiongozi wa CCM kwa nafasi alizowahi kuzishikilia katika Baraza Kuu la Wazazi na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama chetu kwa miaka 10 kuanzia 1992. Aidha, kupitia kwako, nakuomba unifikishie salamu zangu za pole kwa viongozi, wanachama, makanda na wapenzi wa CCM ambao wameondokewa na mwenzao na ambaye wanajua fika pengo lake litakuwa gumu sana kuzibika. Nakuomba pia ufikishe pole zangu nyingi kwa wanafamilia ambao wameondokewa na mhimili wa familia. Wajulishe wanafamilia kuwa naungana nao katika kuomboleza, niko nao katika msiba huu mkubwa na pamoja nao namwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema roho ya Marehemu Salum Shomvi Tambalizeni. Amin. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.

14 Oktoba, 2013

You might also like