You are on page 1of 1

MHUBIRI 7:2

"Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea


nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho
wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake"

Binadamu wote tumewekewa kanuni moja ya kuondoka katika dunia hii, nayo ni mauti.
Ijapokuwa tunafunikwa na majonzi na huzuni nyingi linapotokea tukio la mtu au watu kututoka
kimwili lakini bado kanuni inabaki pale pale...... mauti.

Hii ndio sababu kila mtu mwenye uelewa wa masuala ya kijamii, hujitahidi kuonyesha
ushirikiano kwa namna yoyote ile katika kuomboleza kwa sababu ya tukio la kuondokewa na
mwanajamii mwenzake awe wa karibu au mbali naye.

Kwetu sisi watanzania, kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere; huu ni wakati wa
kuonyesha umoja na ushirikiano pasipo kujali tofauti za namna yoyote ile (kama zipo) kwa
sababu kifo hakichagui mtu.

Pasipo kujali sababu za mazingira ya ajali, kwa sababu kibinadamu hiyo ni ajali kama ajali
zingine, basi mioyo yetu sisi sote inaungana kwa namna moja na kwa dhati kabisa kuugua
pamoja na wale wote wafiwa; wote walioondokewa na ndugu na jamaa wa karibu.

Tunasikitika kuondokewa na wanajamii wenzetu, tunawapa pole ndugu wa karibu kabisa


(wafiwa), na Mwenyezi Mungu awape nguvu ya kuvumilia hali ya majonzi mazito wanayopitia
wakati huu, nasi sote tumeguswa sana hivyo tunaungana na mheshimiwa raisi wetu Dr. JPM na
serikali kwa ujumla katika kuomboleza na kuumia kwa hisia zetu kutokana na tukio hilo.
Tunaomba kwa Mwenyezi Mungu roho za marehemu hao zipumzike kwa amani.

Na mwisho kabisa ni matumaini yetu kwamba Serikali yetu kupitia mamlaka husika itaendelea
kutengeneza mazingira rafiki katika kuimarisha vyombo vya usafiri (maji na nchi kavu) hasa
katika kusimamia sheria za usafiri ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa majanga ya namna
hiyo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU

You might also like