You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA




PRESS RELEASE
22/07/2014

WATU WANANE WAKIWEMO MADAKTARI WASHIKILIWA NA
KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPWA VIUNGO
VYA BINADAMU MAENEO YA BONDE LA MBWENI MPIJI ENEO LA
BUNJU
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watu wanane
na kuwahoji kuhusu tukio la kupatina kwa viungo vya binadamu
vilivyogundulika katika maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji ambapo mifuko ya
plastiki ipatayo 85 yenye mabaki ya viungo vya binadamu yaligundulika. Polisi
walipata taarifa 21/07/2014 jioni kutoka kwa wasamaria wema na ndipo jopo la
wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP.
Camilius Wambura walifika hapo majira ya saa 1.00 usiku.
Walipofika katika tukio waligundua mifuko ipatayo 85 mieusi yenye viungo vya
aina mbali mbali vya binadamu kama vile Vichwa, Miguu, Mikono, Mioyo,
mapafu, vifua na mifupa ya aina mbali mbali ya binadamu. Viungo hivyo
havikuwa na uvundo au harufu ya aina yoyote na vilionekana kwamba
vimekaushwa na kukakamaa. Katika eneo hilo pia vilikutwa vifaa
vinavyotumika hospitali kama vile mipira ya kuvaa mikononi (gloves) mifuko
miwili iliyotumika ,nguo maalum (apron) zipatazo 20 na karatasi mbili zenye
maswali ya kujibu.
Wananchi wasiopungua 1,000 walifika katika eneo hilo la tukio lakini hakuna
aliyekuwa na taarifa sahihi. Viungo hivyo vilichukuliwa na kupelekwa hospitali
ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi. Aidha jopo la Wapelelezi chini ya Mkuu wa
Upelelezi Kanda Maalum ACP. Japhari Mohamed walianza uchunguzi mara
moja kwa kusaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi anayehusika na uchunguzi wa
miili ya binadamu (Forensic Doctor) ambaye kwa pamoja walishirikiana na
madaktari wengine kutoka hospitali wa Taifa Muhimbili.

Hatimaye uchunguzi wa kina ulibaini kwamba viungo hivyo kwa mara ya
mwisho vilikuwa katika Maabara ya Chuo Kikuu Madaktari IMTU jijini
DSalaam. Baada ya kugundulika hivyo Polisi wamewakamata na sasa
wanaendelea kuwahoji watu wanane ambao wanasadikiwa kuhusika na miili
hiyo ikiwa ni pamoja na baadhi ya madaktari wa IMTU. IMTU (International
Medical and Technolegical University) ni chuo Kikuu cha Madaktari ambacho
pia hufanya mafunzo ya udakitari kwa vitendo (practical). Jeshi la Polisi Kanda
Maalum litamuhusisha Mkemia Mkuu wa Serikali na hatimaye mara baada ya
kukamilika kwa uchunguzi jalada litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kwa hatua zake ili sheria ichukue mkondo wake.



S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

You might also like