You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

Anuani ya Simu MKUUPOLISI


Simu : (022) 2110734
Fax Na. (022) 2135556
Unapojibu tafadhali taja:

Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,


Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.

20 /11/ 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWAVYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo
maafisa 77 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).
Miongoni mwa maafisa waliopandishwa vyeo kutoka cheo cha Kamishina
Msaidizi wa Polisi kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ni pamoja na
Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishina msaidizi wa
Polisi ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke Kamishina
Msaidizi wa Polisi (ACP) Engelbert Kiondo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala
ACP. Marietha Minangi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ACP. Diwani
Athumani na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Geofrey Kamwela.
Wengine ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP. Frasser Kashai, Kamanda
wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP. Faustine Shilogile, Kamanda wa Polisi mkoa
wa Dodoma ACP. David Misime, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ACP.
Ferdinand Mtui, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP. Costantine Massawe,
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita ACP. Leornad Paul, Kamanda wa Polisi mkoa
wa Pwani ACP. Ulrich Matei na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ACP. George
Mwakajinga.
Zaidi ya hao wengine ni, Kamanada wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Evarist
Mangala, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Deusedit Nsimeke, Kamanada wa
Polisi mkoa wa Njombe ACP. Fulugence Ngonjani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Katavi Dhahiri Kidavashari na baadhi ya Makamanda wa vikosi, Wakuu wa
vitengo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi na Mkuu wa Chuo cha
Taaluma ya Polisi Dar Es salaam.

Kufuatia kupandishwa vyeo kwa Maafisa hao wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini IGP Said Mwema, amemshukuru Rais wa Jamuhuru ya Muungano
wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika
kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Aidha, IGP Mwema amewapongeza wale wote waliopandishwa vyeo, na kuwataka
kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika kuimarisha Usalama wa raia
na mali zao kwa kuwa cheo ni dhamana.

Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

You might also like