You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA




PRESS RELEASE
22/07/2014

WATU WANANE WAKIWEMO MADAKTARI WASHIKILIWA NA
KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPWA VIUNGO
VYA BINADAMU MAENEO YA BONDE LA MBWENI MPIJI ENEO LA
BUNJU
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watu wanane
na kuwahoji kuhusu tukio la kupatina kwa viungo vya binadamu
vilivyogundulika katika maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji ambapo mifuko ya
plastiki ipatayo 85 yenye mabaki ya viungo vya binadamu yaligundulika.
Polisi walipata taarifa 21/07/2014 jioni kutoka kwa wasamaria wema na
ndipo jopo la wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni ACP. Camilius Wambura walifika hapo majira ya saa 1.00 usiku.
Walipofika katika tukio waligundua mifuko ipatayo 85 mieusi yenye viungo vya
aina mbalimbali vya binadamu kama vile Vichwa, Miguu, Mikono, Mioyo,
mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu.
Viungo hivyo havikuwa na uvundo au harufu ya aina yoyote na vilionekana
kwamba vimekaushwa na kukakamaa.
Katika eneo hilo pia vilikutwa vifaa vinavyotumika hospitali kama vile mipira ya
kuvaa mikononi (gloves) mifuko miwili iliyotumika, nguo maalum (apron)
zipatazo 20 na karatasi mbili zenye maswali ya kujibu.
Wananchi wasiopungua 1,000 walifika katika eneo hilo la tukio lakini hakuna
aliyekuwa na taarifa sahihi. Viungo hivyo vilichukuliwa na kupelekwa hospitali
ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi. Aidha jopo la Wapelelezi chini ya Mkuu wa
Upelelezi Kanda Maalum ACP. Japhari Mohamed walianza uchunguzi mara
moja kwa kusaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi anayehusika na uchunguzi wa
miili ya binadamu (Forensic Doctor) ambaye kwa pamoja walishirikiana na
madaktari wengine kutoka hospitali wa Taifa Muhimbili.
Hatimaye uchunguzi wa kina ulibaini kwamba viungo hivyo kwa mara ya
mwisho vilikuwa katika Maabara ya Chuo Kikuu Madaktari IMTU jijini Dar es
Salaam.
Baada ya kugundulika hivyo Polisi wamewakamata na sasa wanaendelea
kuwahoji watu wanane ambao wanasadikiwa kuhusika na miilihi yo ikiwa ni
pamoja na baadhi ya madaktari wa IMTU. IMTU (International Medical and
Technolegical University) ni chuo Kikuu cha Madaktari ambacho pia hufanya
mafunzo ya udakitari kwa vitendo (practical). Jeshi la Polisi Kanda Maalum
litamuhusisha Mkemia Mkuu wa Serikali na hatimaye mara baada ya
kukamilika kwa uchunguzi jalada litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kwa hatua za keilisheria ichukue mkondo wake.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

You might also like