You are on page 1of 16

Sauti ya Waislamu

Wanafunzi waliofukuzwa Ndanda kurejeshwa shuleni


Waliokiuka maadili ya uongozi kuchukuliwa hatua Wanafunzi wahoji, wampa Waziri kitabu cha utati
Na Waandishi wetu, Zanzibar

ISSN 0856 - 3861 Na. 996 RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JAN. 27 - FEB. 2, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Uhalali wa muungano kwanza katiba baadae Uk. 2

Waziri Shamhuna atakiwa kujiuzulu


Adaiwa kula njama kupeleka mafuta ya Zanzibar Bara Prof. Tibaijuka azidi kuwakoroga Wazanzibari

HALI si shwari k w a Wa z i r i A l i Juma Shamhuna ambaye wajumbe wenzake wa Baraza l a Wa w a k i l i s h i Inaendelea Uk. 4

Polisi wapewa bangi kuchukia Waislamu


Na Mwandishi Wetu

Waziri Ali Juma Shamhuna

Hofu: Mtaala huo kutua CCP, Moshi, Kurasini Dar

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Shukuru Kawambwa (pichani juu) akiingia katika viwanja wa Kidongo Chekundu jini Dar es Salaam kupokea maandamano ya wanafunzi wa Kiislamu wa Shule mbalimbali, Ijumaa iliyopita. Picha chini ni baadhi ya wanafunzi hao.

H A B A R I z i l i z o v u j a kutoka vyombo vya usalama vya Marekani vinaonyesha kuwa


Inaendelea Uk. 4
IGP Said Mwema

2 AN-NUUR

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012


wameshakula bila jasho na bado zoezi la kubomoa litafuata. Tunajiuliza, siku z o t e wa t u m i s h i h a wa wanakuwa wapi wakati wa n a n c h i wa n a n u n u a viamba vyao na kujenga makazi pasipo kupimwa? Katika nchi zenye watendaji makini wa sekta ya ardhi, huwa unakuwa ni wajibu wa serikali kupima v i wa n j a k u l i n g a n a n a mahitaji na matumizi, na huuziwa watu wanaohitaji ilimradi wanafuata taratibu na sheria. Katika nchi hizo, anayehitaji kiwanja huenda tu Idara husika na kupewa ramani ya maeneo yenye viwanja vilivyopimwa na kuwekwa miundo mbinu tayari. Huchagua kiwanja anachohitaji kulingana na mahitaji yake, uwezo wake na matumizi ya kiwanja husika. Akipata anachohitaji huuziwa na kumilikishwa kwa makubaliano au u t a r a t i b u u l i o w e k wa . Mfano mzuri ni katika nchi kama Zimbabwe, Botswana, Namibia, n.k. Huo ndio utaratibu. Haiwi

AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

TAHARIRI/HABARI
kazi ya wananchi kumtafuta mpimaji osini kwake, kwa wakati wake, kumhonga, kumpatia usari ndipo aje kupima au kutathimini kiwanja chako. Lakini Kwa kuwa utaratibu wa huduma hiyo haupo hapa jini, anayeweza kuipata huduma hiyo ni yule mwenye uwezo, ambaye atalazimika kutoa rushwa na kumaliziwa shida yake mara moja. Akina kabwela wao watalazimika kumfuatilia ofisa ardhi ofisini kwake, awapige kwanza kalenda za hapa na pale kwa kuwa mchuzi wao wa kuhonga ni haba ndipo baadae watimiziwe shida yao. Kwa mtindo huu hakuna jinsi, watu wataendelea kujinunulia maeneo na kujijengea watakavyo, si kwa sababu wanapenda, ila ni matokeo ya kukosekana v i wa n j a v i l i v yo p i m wa kwa ajili ya kuuzia watu wanaohitaji. Wa z i r i wa A r d h i n a Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibauka analazimika kuweka utaratibu wa kiutendaji ambao utawalazimu maasa wake wa ardhi kutoka maosini na kuwafuata wananchi walipo kuwapimia viwanja vyao na kuwamilikisha. Uwepo utaratibu wa malipo ambao wananchi wa kati na chini watamudu kulipia gharama za upimaji wa maeneo yao na umilikishwaji. Ni aibu kwa serikali katika karne hii kusubiri gharika za mafuriko ndipo uanzishwe mchaka m c h a k a wa z i m a m o t o kuwapimia wananchi viwanja na kuweka miundombinu mfano wa Mabwepande. Huduma ya upimaji na umilikshaji si hatimiliki ya wenye uwezo pekee, bali ni huduma kwa jamii na ni jukumu la serikali kutekeleza kazi hiyo. Kama imewezekana kuipima Mabwepande kwa muda mfupi tu, basi inawezekana zoezi la upimaji viwanja likawa endelevu na kuwa dawa ya kudumu ya migogoro ya ardhi na ujenzi holela jini Dar es Salaam.

MAONI YETU

Upimaji viwanja usiishie Mabwepande


HIVI sasa serikali ipo katika zoezi la kupima na kugawa viwanja kwa waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha jini Dar es Salaam mwishomi mwa mwaka jana. Mpaka sasa tayari zaidi ya viwanja 600 vimeshapimwa kwa jili ya kuwagawia waathirika hao na zoezi la upimaji tunaambiwa kwamba bado linaendelea. Tayari visima saba vya maji vimeshachimbwa. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman K o va n a ye a m e t a a r i f u kwamba jeshi la polisi linajenga kituo cha Polisi eneo hilo la Mabwepande ili kuweka usalama na kuwalinda waathirika na mali zao katika kipindi hiki cha zoezi la kuwahamisha. Zoezi linalofanyika Mabwepande linadhihirisha kwamba kumbe serikali ikiamua na watumishi wake wakiwajibika ipasavyo katika nafasi zao za kazi, inaweza kutatua tatizo sugu jini Dar es Salaam la ujenzi holela na uhaba wa viwanja vilivyopimwa kwa ajili ya makazi ya wananchi. Kwamba iwapo wahusika wataamua kuacha usingizi maofisini na kufanya kazi kama walivyofanya Mabwepande, kuna uwezekano mkubwa wa k u p i m wa v i wa n j a v ya kutosha na kuwauzia wakazi wa ji la Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi, na zoezi likawa e n d e l e v u i l i k u u we k a mji katika mandhari na mpangilio mzuri na kuepuka misongamano na mogogoro ya viwanja isiyokuwa ya lazima. Lakini kwasababu ya kile kinachoonekana kuwa ni uvivu tu, na uzembe, serikali pamoja na watumishi katika sekta za ardhi, mipango mi na makazi wameshindwa kutimiza wajibu wao kwa umma, hivyo kuruhusu wananchi hasa wa uwezo wa kati na wa chini kuendeleza ujenzi holela katika maeneo mbalimbali ya ji, kwasababu wamekosa huduma ya v i wa n j a v i l i v yo p i m wa kutoka katika serikali yao. Kama wiki tatu zimetosha kupima viwanja 600 Mabwepande, mwaka mmoja vingepimwa viwanja vingapi na watu wakauziwa na kujenga makazi yao kwa mpangilio mzuri?. Kuna Idara ya Ardhi katika Manispaa na Halmashauri zote jiji la Dar es Salaam, kwa miaka mingi wamekupo maasa ardhi walioajiriwa kwa kazi hiyo, kwa miaka mingi wamekuwepo maasa ardhi katika Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi, hawa ni watumishi walioajiriwa k wa a j i l i ya k u p i m a , kutathmini na kuthaminisha viwanja kwa ajili ya wananchi. Wameajiriwa ili kuwahudumia wananchi na kuboresha makazi ya watu. Kila mwezi wanalipwa mishahara kupitia kodi za wananchi, kila siku wanaamka asubuhi kwenda kazini na kurejea majumbani mwao jioni, wanachofanya ni nini kama hakuna viwanja vilivyopimwa jini? U k i a c h a m a e n e o ya katikati ya jiji kama Kariakoo, Posta, Upanga, Masaki, Oysterbay, Mbezi Beach, baadhi ya maeneo ya Magomeni, Ilala na b a a d h i ya m a e n e o ya Temeke, Si Kimara, Mbezi, Pugu, Mbagala, Boko, Bunju, Kitunda, Kibamba, Kiluvya, Mpigi, Bonyokwa na kwingineko kando ya jiji ambako kumepimwa viwanja kwa ajili ya makazi. Kote huko watu wamekuwa wakinunua viamba na kujijengea, alimradi papatikane mahali pa kujisitiri. Kama ni kupima, kila mmoja anajipimia kivyake, sio kwa kufuata Mipango Mi. Lakini pamoja na jitihada z a wa n a n c h i k u j e n g a vibanda vyao kujihifadhi, ndipo baadae watu wa ardhi kutoka Manispaa, Halmashauri za miji na Wizarani wanatoka huko wanakoshida kila siku na kuja kuwabughudhi wananchi na porojo za kusimamisha ujenzi, kuvunja haparuhusiwi kujengwa, hapajapimwa, eneo ni kwa ajili ya miundo mbinu n.k. Wa k a t i m w i n g i n e hayo hufanyika bila hata f i d i a . H a t a i k i t o l e wa , basi itachotwa njiani na itakapomfikia mlengwa inakuwa imebakia kiduchu. Kikubwa walafi

Uhalali wa muungano kwanza katiba baadae


Na Waandishi wetu, Zanzibar

Ni kauli ya Masheikh Zanzibar

IMEELEZWA kuwa ili kuimarisha muungano, pana haja kujadili misingi na kuhakiki uhalali wake kwanza kabla ya kujadili katiba mpya. Hayo yamesemwa na baadhi ya Masheikh katika kikao kinachoendelea visiwani hapa. Azma ya mkusanyiko huo ulioandaliwa na Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, ilikuwa ni kujadili nafasi ya Waislamu katika Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Ta n z a n i a ; a m b a p o walisema ni vyema kwanza kuangalia hali za kuthibiti kwa fungamano hilo katika medani za kisheria. Masheikh hao wamesema kabla ya kujadili mambo gani ya msingi ya kufanyia marekebisho ipo haja ya kubaini mazingira yaliyokuja kuasisi Muungano huo na iwapo unayo mashiko ya kisheria. Kwanza hebu jamani tuangalie kabla kuka mbali upande wa mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jee huo Muungano wenyewe upo kihalali, alihoji Sheikh Msellem Aliy Msellem alipokuwa akaribu kupitia sehemu ya ajenda za kikao hicho. Hoja hiyo ya Sheikh

Msellem ambayo ilipokelewa na kuungwa mkono na sehemu kubwa ya wajumbe wa kikao hicho cha pamoja, inatokana na kile walichotaja ni kuwapo kwa manunguniko ya kila upande, Tanzania Bara na Zanzibar, ya kwamba muungano huo haukuweka misingi yake ya kisheria na haupo kwa mujibu wa mikataba inayoeleweka. B a a d h i ya M a s h e i k h walisikika katika kikao hicho hata wakadili maelezo ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar , Bw. Iddi Pandu Hassan, ambaye aliwahi kuiambia Mahakama Kuu ya Zanzibar , kwamba Osi yake haikuwahi kuona kile kilichoitwa Mkataba wa Muungano, uliounganisha Jamhuri mbili huru za Zanzibar na Tanganyika mwaka 1964. Bw. Pandu alitoa jawabu h i yo p a l e a l i p o t a k i wa na Mahakama kujibu hoja ya Wazanzibari 10 waliowasilisha dai hilo kutaka ufafanuzi. Juu ya nani anayefaa kumrithi Rais Kikwete katika Kiti cha Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , M a s h e i k h wa l i s i k i k a wakisema siyo hoja kwamba lazima akiondoka Kiongozi Muislamu ampishe Mkristo. Walisema la msingi ni kuangalia nani mwenye sifa za kuliongoza Taifa hasa

katika wakati huu ambao nchi imeanza kukabiliwa na changamoto za siasa za makundi kwa misingi ya udini na ukabila. M a s h e i k h wa l i s i k i k a wakisema huu ni wakati ambao Zanzibar inalazimika kuchukua nafasi yake ya wadhifa wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, h a s a b a a d a ya a wa m u zilizopita kuongozwa na Tanzania Bara mfululizo. Pamoja na mengi yaliyoendelea kujadiliwa katika mfululizo wa mikusanyiko, Masheikh wameendelea kutafakari juu ya hatua za kumezwa kwa Zanzibar kupitia Muungano na pia Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Wa m e s e m a Z a n z i b a r imepoteza nafasi na heshima ya k e k wa u j u m l a h a l i iliyodhoosha nyanja zote za maisha. Walichoendelea kutafakari Masheikh ni juu ya njia muafaka ya kuirejesha nafasi na heshima ya Z a n z i b a r , a m b a p o wamesema iwe iwavyo sasa wakati umewadia wa kukia hatua hiyo. Mikusanyiko hiyo ambayo mwishoni mwa wiki hii itawakusanya pia wasomi, wanataaluma, wanasiasa na viongozi mbali mbali, imeahidi kwamba hatimaye watatoa msimamo imara juu ya kile jamii na umma kwa ujumla wanachokihitaji katika kuamua mustakbali na hatma ya Taifa.

HABARI

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

AN-NUUR

Wanafunzi waliofukuzwa Ndanda kurejeshwa shuleni


Na Bakari Mwakangwale

SERIKALI imeahidi kuwarejesha wanafunzi 20 wa Shule ya Sekondari Ndanda waliofukuzwa baada ya kutokea mtafaruku wa kidini. Serikali pia imeahidi kulifuatilia suala hilo kwa undani na kuwachukulia hatua watakaobainika k u k iu k a maa dil i o ya uongozi. Waziri wa Elimu na M a f u n z o ya U f u n d i , Mheshimiwa Shukuru Kawambwa ametoa msimamo huo wa mbele ya umati wa wanafunzi wa Kiislamu wa Shule m b a l i m b a l i n a Vy u o baada ya kuhitimisha maandamano yao katika viwanja vya Kidongo Chekundu Jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita. Mbali ya kupokea ahadi hiyo ya serikali, wanafunzi walimuuliza maswali Waziri huyo wakitaka ufafanuzi, kwamba inakuwaje Wakuu wa Shule, takribani zote za Sokondari nchini ni Wakristo. Hali hiyo ilijiri mara baada ya Mheshimiwa Waziri, kumaliza kujibu r i s a l a ya wa n a f u n z i ambapo mamia ya wanafunzi walinyoosha mikono juu wakiashiria kuwa na maswali yaliyohitaji majibu na ufafanuzi kutoka kwa Waziri. Mmoja wa wanafunzi hao akiwa na kitabu cha Mfumo Kristo na Dhulma Dhidi ya Haki za Waislamu Nchini, aliuliza kwa nini hakuna uwiano sawa kwa Wakuu wa Shule za Sekondari. Mheshimiwa Waziri suala hili limefanyiwa uchunguzi na data tunazo, hakuna uwiano sawa kati ya Waislamu na Wakristo kwa walimu wakuu katika shule za serikali, na katika idara zingine za elimu. Alisema mwanafunzi huyo huku akinukuu data hizo kutoka katika kitabu hicho, ambapo alipomaliza kunukuu, mwanafunzi huyo alimkabidhi Waziri kitabu hicho. Mwanafunzi mwingine aliuliza, kwa nini viongozi Wa i s l a m u w a l i o p o

madarakani yanapoibuka masuala yanayowahusu Waislamu wanakuwa wazito kuyatolea ufumbuzi, tofauti na wenzao Wakristo waliopo serikalini. Mwanafunzi huyo alitoa mfano sakata la serikali kufuta misamaha ya kodi kwa asasi za kidini ambapo Maaskofu waliijia juu serikali na kupelekea Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Mkristo) kutoa kauli na kusimamia msimamo na matakwa ya Maaskofu. Awa l i , Wa z i r i Kawambwa akiongea na wanafunzi hao akiwa amezunguukwa na maasa wa jeshi laPolisi, wakiongozwa Kamanda wa Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema wanafunzi waliofukuzwa katika shule ya Sekondari Ndanda, watarudishwa shuleni na watafanya mtihani bila mashariti yoyote. Alisema kwamba, serikali imekerwa kuona taifa limewasomesha kuanzia darasa la kwanza, l e o wa n a k wa m i s h wa wakiwa wameka katika ngazi ya juu ya elimu wakitarajiwa kuwa wataalamu katika fani mbalimbali. Kazi kubwa iliyopo sasa si tu kuwarejesha wanafunzi wa Ndanda, b a l i i n a k a z i k u b wa k u wa c h u k u l i a h a t u a za kisheria wahusika ili kuhakikisha tukio kama hili halijirudii tena. Alisema Waziri Kawambwa. Alisema, serikali italinda usawa, haki na amani kwa wanafunzi wote, wa dini zote na makabila yote kwa kuhakikisha wanapata haki sawa katika shule za serikali. Wa z i r i K a w a m b a amesema kuwa, serikali haitakubali kuona wanafunzi wakiandamana tena wakilalamikia k u o n e wa k i i m a n i a u kikabila. Akitolea maelezo kipengele cha risala ya wanafunzi hao waliotaka ufafanuzi juu ya madai ya kauli ya Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ndanda, aliyenukuliwa

RAIS wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu (TAMSYA), Bw. Jafar Mneke akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya Kidongo Chekundu.

akiwatambia wanafunzi wa Kiislamu shuleni hapo, kuwa Shule hii (Ndanda) ilikuwa ni ya Kanisa kabla ya kutaishwa na serikali, hivyo ardhi na mamlaka ya matumizi bado ni mali ya Kanisa na serikali inachomiliki hapa ni majengo tu. Waziri Kawambwa, alisema kauli hiyo si ya kweli pamoja na kwamba ni kweli serikali ya awamu ya kwanza ilitaifisha mashule ya taasisi zingine kwa asilimia mia moja, majengo na kila kitu, itabaki kuwa hivyo na serikali inawajibika kwa kila kitu. Katika risala yao mbele ya Waziri wa Elimu na M a f u n z o ya U f u n d i , iliyosomwa na Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA), Jaffar Said Mneke, waliiomba serikali kuwarejesha wanafunzi 20, waliofukuzwa katika shule ya sekondari Ndanda pamoja na kutengua mashariti waliyowekewa wanafunzi walionusurika kufukuzwa kwani mashariti hayo yanawatoa katika imani yao. Wanafunzi hao pia waliiomba serikali kuunda tume huru ya kuyatati matatizo ya wanafunzi wa Kiislamu mashuleni

na vyuoni ili kuyapatia suluhisho la kudumu. Wa n a f u n z i h a o wa l i m u e l e z a Wa z i r i Kawambwa, kuwa hawatakuwa tayari kuanzia sasa kuona wananyanyasika na kwamba mwisho wa hayo yote ni baada ya kukisha kilio chao kwa Wizara husika. Mheshimiwa Waziri, hatutakuwa tayari k u a n z i a wa k a t i h u u kuona tunadhulumiwa haki zetu, kwani mwisho wa unyonge, dhulma, unyanyasaji na ubaguzi umeka tamati leo. Alisema Rais wa TAMSYA. M a a n d a m a n o h a yo yaliyoanza katika misikiti mbalimbali ya Ijumaa ya Jijini Dar es Salaam, yalipata upinzani mkali k u t o k a k wa J e s h i l a Polisi, kwa kuwazuia kuka Wizara ya Elimu wa k i wa t a k a k we n d a Kidongo Chekundu. Maafande hao wa Polisi, walilazimika kuongea na Rais wa TAMSYA, Jaar Mneke, wakimsihi kuwa maandamano hayo yaelekee viwanja vya Kidongo Chekundu, kwani Mheshimiwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi atafika hapo kuwasikiliza. M a a n d a m a n o h a yo

makubwa ya Wanafunzi kutoka shule na vyuo mbalimbali yamekuja kwa anuani ya kupinga na kukithiri kwa dhulma, uonevu, ubaguzi na madhila wanayofanyiwa wanafunzi wa Kiislamu. M a a n d a m a n o h a yo yamechagizwa zaidi na tukio la hivi karibuni lililotokea katika Shule ya Sekondari Ndanda, Mikoani Mtwara, baada ya uongozi wa Shule hiyo kuwafukuza wanafunzi wa Kiislamu 20. Imedaiwa kuwa Wanafunzi hao walifukuzwa baada ya kudai eneo la kufanyia ibada, kama ambavyo we z a o Wa k r i s t o walivyotengewa. Aidha walikuwa wakipinga Kanisa kuingilia uchaguzi wa serikali ya wanafunzi, pamoja na kulalamikia lugha za kashfa dhidi yao na dini yao zinazotolewa na mkuu wa shule hiyo (Bw. Joseph Sowani). Na wale waliopewa onyo, walitakiwa kurudi shuleni hapo kwa mashariti ya kutojihusisha na Uislamu kwa muda wote watakao kuwapo shuleni hapo, sharti ambalo linawapora haki ya kikatiba ya kuabudu.

Waziri Shamhuna atakiwa kujiuzulu


wanataka ajiuzulu. S h a m h u n a anadaiwa kuisaliti Zanzibar kutokana na hatua yake ya kushiriki mpango wa kuongeza mpaka wa baharini wa Ta n z a n i a a m b a o unadaiwa kuwa iwapo utafanikiwa utafanya rasilimali ambazo kwa sasa ni za Zanzibar kuwa za Tanzania.
Inatoka Uk. 1
kutoka nafasi ya Uwaziri wa Serikali ya Zanzibar , kutokana na kile walichokifafanua kuwa ni kutumia vibaya madaraka na kukiuka taratibu za uongozi. Mheshimiwa Spika, naona kwa hatua hii ya mheshimiwa Waziri ya kuisaliti na kutaka kuiuza Zanzibar na pia kutumia vibaya mamlaka ya k e s e r i k a l i n i h a p a n a budi akajiuzulu, alisema Muwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Bw. Hamza Hassan Juma alipokuwa akichangia hoja hiyo. Hoja hiyo ya Mwakilishi Hamza ilisogea katika u f a f a n u z i wa M a m l a k a waliyonayo Wajumbe wa Baraza hilo ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na yeyote mwenye mamlaka ya juu serikalini kuanzia Rais, Makamu wake wa Rais, na hata Waziri yeyote, pindipo akishindwa kuwajibika au kushindwa kumwajibisha aliyetumia vibaya madaraka kama ilivyokuwa kwa Mheshimiwa Shamhuna. Waliounga mkono haja ya Alhaj Shamhuna ambaye ni Waziri wa Maji, Nishati, Ardhi na Makaazi wa Serikali ya Zanzibar , kujiuzulu, ni pamoja na Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Bi Asha Bakari Makame. Bi Asha ambaye amewahi pia kutumikia nafasi mbali mbali za uongozi serikalini, alisema licha ya kwamba mheshimiwa Shamhuna ni mwenzake kutoka CCM, lakini kwa hili alilolitenda dhidi ya nchi ya Zanzibar, hapana budi ajiuzulu kwa maslahi ya umma. Ukumbi ulizizima na wananchi walihamasishana kutegea sikio yale yaliyokuwa yakisikika ambapo wajumbe waliweza kufafanua kila ambacho walibaini kutoka ofisi ya Mheshimiwa Shamhuna, pamoja na shinikizo la kutaka ajiuzulu. Yalikuwa ni maji shingoni kwa Bw. Shamhuna pale Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Mji Mkongwe, mheshimiwa Ismail Jussa Ladhu alipowasilisha hoja juu ya hatua ya Waziri Shamhuna kuisaliti nchi na kusaidia juhudi za kuidhoofisha Zanzibar kihaiba na kiuchumi kupitia mipaka na raslimali yake ya baharini. T u m e m u o n a Mheshimiwa leo ameingia baridi kabisa haya mambo si mchezo bwana, walisikika baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo wakitoa maneno ya utani juu ya mjadala wa kikao hicho ulioonekana kuwa moto wa kuotea mbali.

4 AN-NUUR

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012


Wengi miongoni mwa Wa j u m b e wa B a r a z a l a Wawakilishi na hata wananchi kwa ujumla walionekana kuiwafiki hoja hiyo baada ya kile walichoeleza kubaini usaliti ndani ya Wizara ya Mheshimiwa Shamhuna dhidi ya maslahi ya watu wa Visiwa vya Unguja na Pemba . Ni pale Wawakilishi hao wa Wananchi waliposema vyovyote iwavyo Mheshimiwa Shamhuna na baadhi ya watendaji wake wameshiriki kusaidia hila za kutaka kuinyima Zanzibar raslimali zake zikiwamo za mafuta na mipaka ya Bahari Kuu. Wa j u m b e wa B a r a z a l a Wa w a k i l i s h i k a b l a ya tishio lao la kutaka kupiga kura kuyapitisha maamuzi magumu dhidi ya mheshimiwa Shamhuna na Mamlaka yake, walipendekeza kulituma suala hilo katika Baraza la Mapinduzi la Zanzibar ili liingilie kati na kuzuiya lile zoezi la Tanzania Bara kuwasilisha ombi mbele ya Jamii ya Kimataifa kuomba kuongezewa mipaka ya eneo la bahari kuu. Wanachoamini Wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi na pia Wananchi wa Zanzibar ni kwamba Ombi hili la Tanzania Bara linaambatana na hila ya kutaka kuyamega mafuta yaliyobainika kuwapo upande wa Pwani ya Visiwa vya Unguja na Pemba, hasa baada ya utati ulioendelea hivi karibuni kuthibitisha u w e z e k a n o wa m a f u t a hayo kuinamia upande wa Visiwani na siyo Mwambao wa Pwani ya Tanzania Bara, kama ilivyodaiwa hapo kabla. Wa n a n c h i wa l i s i k i k a wakisema ama kweli akumulikaye mchana usiku akuchoma pale walipokumbuka hatua ya mheshimiwa Shamhuna kushawishi matumizi makubwa ya nguvu za dola na mabomu ya machozi kuzuia mkutano wa hadhara wa Chama cha CUF usifanyike katika Jimbo lake la Donge mwaka 2005, hatua iliyoleta hamasa ya mtafaruku mkubwa wa hali ya kisiasa nchini. Upande mwingine uliozidi kumpa fadhaa mheshimiwa Shamhuna wiki hii ni pale makundi ya wananchi wa jimbo lake kuibuka kumlaani kiongozi huyo chachu wa siasa za Zanzibar na pia Tanzania . Wananchi wa Jimbo la Donge kutoka maeneo ya Mahonda na Shehia za Mkataleni wamejitokeza katika vyombo mbali mbali vya habari nchini kulaani hatua za mheshimiwa wao

HABARI
huyo za kuwatelekeza. Siye hatumuoni M u wa k i l i s h i wa l a n a n i tunadhalilika na sasa iwe iwavyo hatukubali tena tutapambana kupigania haki zetu wenyewe, alisema Mzee Juma Said Saleh aliyeongozana na msafara wa wananchi wenzake kuja serikalini kuwasilisha kilio chao. Hii ni kutokana na hatua ya mtu aliyeelezwa kuwa muwekezaji kuyachukua mashamba ya wananchi wa Jimbo hilo , hali inayoendelea kuwapo mivutano na misuguano mikubwa. Kufuatia hali hiyo, baadhi ya wananchi waliwekwa kizuizini hivi karibuni, na hatimaye kupelekwa mahakamani, kabla ya juhudi za makusudi za Mwakilishi wa Jimbo la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja, Haji Makame Mshimba, kama alivyoliambia Baraza la Wawakilishi, kulazimika kwenda kuwakomboa, wananchi hao wanaoteseka. B a a d h i ya wa n a n c h i hao kwa ukali walisikika wakisema pamoja na mabomu ya akina Shamhuna wamekosa imani moja kwa moja na viongozi wao wa Jimbo la Donge kwa kile walichotaja kitendo cha kuwatelekeza wakiendelea kudhalilishwa.

Wakati moto ukimuwakia Shamhuna, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Tanzania (Bara), Prof. Anna Tibauka amesema Zanzibar ilishirikishwa katika mradi wa kuongeza eneo la ziada nje ya ukanda wa uchumi wa baharini. Tibauka anasema kuwa i n a yo o m b a k u o n g e z wa eneo ni Tanzania (Zanzibar ikiwemo) kwa hiyo hapakuwa na sababu kwa Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa kulalamika. Amesema, mipaka inayoongezwa ni ya Tanzania, sio Tanzania Bara, kwa hiyo Zanzibar kulalamika ni sawa na kugombania to wakati nyumba inayojengwa ni moja (ya Bara na Zanzibar). Hata hivyo, ufafanuzi huo umezidi kuwakoroga Wazanzibari wakidai kuwa maelezo yake yanathibitisha k u wa Ta n z a n i a i n a t a k a ipanue ili kile ambacho ni cha Zanzibar sasa ionekane kuwa ni cha Tanzania. Katika hali hiyo, Zanzibar itakuwa haina nguvu tena ya kudai haki ya kumiliki rasilimali zilizo katika bahari kuu ambazo awali zikulikana kuwa zipo Zanzibar. Kubwa linalotajwa ni lile la mafuta ambayo inasemekana yamegundulika kuwepo katika baadhi ya maeneo ya visiwani. Wajumbe kutoka pande zote za Baraza, Chama cha Mapinduzi CCM na Chama cha Wananchi CUF, pamoja na wa pembezoni backbenchers wamemchachafya mjumbe huyo wa Jimbo la Donge, Alhaj Ali Juma Shamhuna, wakisema ni lazima ajiuzulu kwa kuhini amana ya uongozi aliopewa. Wajumbe hao walimtaka Alhaj Shamhuna, mbele ya Kikao cha Baraza, ajiuzulu

Polisi wapewa bangi kuchukia Waislamu


polisi wamekuwa wakivutishwa bangi la kuwachukia Waislamu. Bangi hilo kisirani lililopewa jina la The Third Jihad, linapewa maosa wa ngazi za juu wa polisi lengo likiwa kuwajenga kisaikolojia na mtizamo w a w a o n e Wa i s l a m u kuwa ni mazimwi hatari katika jamii na kwamba kupambana nao kikatili bila kuwaonea huruma ni stahiki yao. Kwa mujibu wa taarifa zilizonukuliwa na vyombo vya habari vya Marekani, zaidi ya maosa 1500 wa polisi washavutishwa bangi hilo ambalo limekuwa kama mtaala maalum wa kuandaa vikosi vya kuhujumu Waislamu. Ominous music plays as images appear on the screen: Muslim terrorists shoot Christians in the head, car bombs explode, executed children lie covered by sheets and a doctored photograph shows an Islamic ag ying over the White House. Anaeleza mwandishi Michael Powell (January 24, 2012 NY Times) akionesha yaliyomo kwenye mtaala huo ambao umezusha mtafaruku
Inatoka Uk. 1

mkubwa kati ya polisi n a Wa i s l a m u n c h i n i Marekani. Ufupi anasema kuwa mkanda huo huonyesha magaidi (wanaodaiwa k u wa Wa i s l a m u ) wakiwapiga risasi Wakristo kichwani, kisha yanalipuka mabomu na kulipua magari, zinaonekana maiti za watoto waliouliwa na mabomu hayo zikiwa zimefunikwa mashuka. Ukisonga mbele mkanda unaonesha picha ya benderea ya Kiislamu iliyofanyiwa usanii ikipepea katika Ikulu ya Marekani. This is the true agenda of much of Islam in America. A strategy to inltrate and dominate America. ... This is the war you dont know about. Baada ya kuonyeshwa picha hiyo, msimuliaji anasema, hii ndiyo a g e n d a ya Wa i s l a m u Marekani. Mkakati wa kujipenyeza na kuitawala Amerikahii ndiyo vita usiyoua. Pengine unaweza kujiuliza nini lengo la kuwaonesha maofisa wa polisi lamu hii ya kubuni ikiwaonyesha Waislamu wakichinja na kuwalipua

kwa mabomu watoto wa Kikristo! Filamu hii ya dakika 72 iliyopewa jina la Jihad ya Tatu (The Third Jihad), zaidi ya kujenga chuki baina ya Waislamu na Wakristo, hapana shaka imelenga zaidi kuwafanya polisi na maofisa wa usalama wawe katili kwa Waislamu. Filamu hiyo Jihad ya Tatu iliyotengenezwa na kufadhiliwa na taasisi iitwayo Clarion Fund, ni ya pili kutengenezwa na taasisi hiyo baada ya ile ya awali iliyopewa jina la Obsession: Radical Islams War Against the West. ambapo huoneshwa Waislamu kuwa ni hatari kwa Marekani. Taarifa zinaonyesha kuwa pamoja na kuwa na wajumbe katika Bodi yake ambayo ni maofisa wastaafu wa CIA, Clarion Fund ina uhusiano wa karibu na taasisi nyingine ya Aish HaTorah, zote zikiwa na uhusiano na Mayahudi wenye siasa kali na wenye ushawishi mkubwa katika siasa za Marekani.
Utaratibu huo wa kuwavutisha bangi polisi kuwachukia na kuwashukia

Inaendelea Uk.6

HABARI ZA KIMATAIFA

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

AN-NUUR

Walibya waandamana kutaka Shariah itawale


TRIPOL Mamia ya wananchi wa Libya wameandamana wakiwataka viongozi wa nchi hiyo kutekeleza sheria za Kiislamu. M a a n d a m a n o yamefanyika katika mji mkuu Tripoli na miji ya mashariki mwa nchi hiyo ya Benghazi na Sabha. Wa k i wa wa m e i n u a j u u Q u r a n i Tu k u f u , waandamamaji wametoa kauli za kuitaka serikali ya mpito nchini humo kutegemea sheria za K i i s l a m u wa k a t i wa kuandika katiba mpya. Aidha wametaka kuwepo kipengele katika katiba kinachotambua Uislamu kama dini rasmi ya serikali. Wa n a h a r a k a t i w a Kiislamu Libya wanasema wameamua kuandamana baada ya kubainika kuwa v ya m a v ya K i s e k u l a vinavyoungwa mkono na Wamagharibi vimeundwa nchini humo. Itakumbukwa kuwa Waziri Mkuu wa Muda wa Libya Abdel Rahim al-Kib, alipoingia madarakani mwezi Novemba mwaka jana alisema serikali mpya ya Libya itazingatia sheria za Kiislamu. Hali inaonyesha k wa m b a u s h i n d i wa wanaharakati wa Kiislamu katika chaguzi za Misri, Tu n i s i a n a M o r o c c o umedhihirisha wazi kuwa wimbi la mwamko wa Kiislamu katika Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika haliwezi kuzuilika

JESHI la Marekani likkingia nchini Libya hivi karibuni

Rais Saleh aikimbia Yemen Rushdie afuta safari ya India


Yuko Oman njiani kuelekea Marekani
SANAA VIONGOZI wa Yemen wametangaza kuwa, Rais wa Yemen, Ali Abdallah Saleh ameondoka katika uwanja wa ndege wa Sanaa akielekea Marekani. Baadhi ya duru za Yemen zimetangaza kwamba, dikiteta Ali Abdallah Saleh atakuwa nchini Oman kwa siku kadhaa kabla ya kuelekea Marekani. Taarifa zaidi zinadai kwamba, dikiteta huyo anakwenda Marekani kwa ajili ya matibabu na kwamba, atarejea Yemen baada ya kumaliza matibabu kwa ajili ya kukiongoza chama chake. Ali Abdallah Saleh, aliondoka Yemen Jumapili wakati maandamano ya kupinga kupewa kinga ya kutoshitakiwa yeye pamoja na viongozi wenzake yakishika kasi. Maelefu ya wananchi wa Yemen waliandamana m w i s h o n i m wa w i k i katika miji mbalimbali nchini humo wakitaka kunyongwa Rais huyo. Wananchi hao walisikika wakipiga kauli mbiu za kutoa wito wa kunyongwa Ali Abdallah Saleh waliyemtaja kuwa ni muuaji. CAIRO M U R TA D I S a l m a n Rushdie amefuta safari yake ya India kutokana na maandamano makubwa ya Waislamu wa India wanaopinga safari hiyo na kuogopa uwezekano wa Waislamu wa India kutekeleza fatwa ya kumuuwa. M a a n d a m a n o yaliyofanywa kwa siku kadhaa na Waislamu wa India dhidi ya mwandishi h u yo wa k i t a b u c h a Ay a z a K i s h e t a n i , yamemlazimisha murtadi huyo kufuta safari ya kuzuru nchi hiyo. Makundi mbalimbali ya Kiislamu ya India yamewashukuru Waislamu kwa kufanikisha suala la kuzuia safari ya murtadi Rushdie nchini humo na kusema kuwa, k u f u t wa s a f a r i ya k e huko India ni ushindi mkubwa. Salman Rushdie mwenye umri wa miaka 65 alizaliwa katika mji wa Mumbai nchini India na mwaka 1988 alichapisha kitabu cha Aya za Shetani kunachomdhalilisha na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na Quran, suala ambalo liliwakasirisha Waislamu kote duniani. Murtadi Rushdie

Rais Saleh

Ali Abdallah

Thailand yaitambua Palestina


IQNA THAILAND imekuwa taifa la kwanza kuitambua rasmi nchi huru ya Palestina mwaka huu wa 2012. Ujumbe wa Palestina katika Umoja wa Mataifa umesema umepokea barua kutoka kwa serikali ya Thailand inayosema kuwa, nchi hiyo ya kusini mashariki mwa bara Asia imeitambua rasmi nchi ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967. Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameipongeza Thailand kwa hatua hiyo aliyoitaja kuwa ni ya kutia moyo na yenye nafasi ya kipekee katika medani ya kidiplomasia Palestina. Riyad al Maliki, ameongeza kuwa Thailand

imekuwa nchi ya 131 kuitambua rasmi nchi huru ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967. Oktoba mwaka 2011, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, liliipatia Palestina uanachama kamili. Hata hivyo Marekani na Israel zilipinga hatua hiyo.

MURTADI Salman Rushdie alitazamiwa kuhutubia katika siku ya ufunguzi wa Tamasha ya Fasihi Jaitapur mjini New Delhi lakini amelazimika kufuta safari ya kwenda India kushiriki katika tamasha hiyo kutokana na malalamiko ya makundi mbalimbali ya Waislamu nchini humo na kuhoa kifo. Nchi nyingi duniani ikiwemo India zimepiga marufuku kitabu cha Aya za Shetani. Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya I r a n h a ya t i I m a m Khomeini, alitoa fatwa akiwaamuru Waislamu kote duniani kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya Salman Rushdie popote pale atakapokuwa.

Wasomi wa Kiislamu wazindua Kitabu Unguja


Na Mwandishi wetu, Zanzibar WASOMI, wanataaluma, na masheikh mbali mbali walumuika katika haa maalumu ya uzinduzi wa Kitabu cha Kuyakumbuka Mauti. Hafla hiyo ilifanyika m wa n z o n i m wa w i k i katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Alfalah, maeneo ya Mombasa , Zanzibar .

6 AN-NUUR

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

Habari/Tangazo

Inatoka Uk. 4 kwa hasira na ukatili Waislamu, unakuja wakati hivi sasa serikali ya Marekani imesambaza makachero katika misikiti na taasisi za Kiislamu kuifanya hujuma na kuweka mitego ya kuwakamatisha na unaoitwa ugaidi. Habari za kipolisi zinaonyesha kuwa maofisa wote wanaokwenda kozi za muda mfupi huonyeshwa lamu hiyo ikiwa ni sehemu ya muhutasari wa mafunzo. Katika mafunzo hayo polisi wanaambiwa wasimwamini Muislamu yeyote kwa sababu hata wale wanaojifanya siasa poa (hapa kwetu tunaweza kusema akina Al Had na Bakwata), si watu wema. Wanajicha tu lakini magaidi hatari. Polisi hao wanaambiwa kwamba Jihad ya kwanza ilikuwa wakati wa Mutume Muhammad (s.aw), kisha ikaja ile ya wakati wa zama za Kati (mpaka wakati wa Vita ya Msalaba). Na ya tatu ni sasa ambapo Waislamu wanataka kuteka Ulya na Marekani kupitia ugaidi. Kwa ujumla uhai wote wa Uislamu toka Mtume Muhammad (s.a.w) kuhamia Madina, umeitwa ni muda wa Vita. The 1,400-year war , kwamba ni vita iliyodumu kwa miaka 1400 na bado Waislamu wanaendelea nayo katika mtindo wa kigaidi. Aw a l i h a b a r i h i z o zilipovuja, uongozi wa polisi New York (Police Academy) ulikanusha kutumia lamu hiyo na kusema kwamba kama kuna maosa walioitizama, basi ni kama watu binafsi. Hata hivyo, baadae walikiri kwamba huitumia lamu hiyo iliyotengenezwa na Mayahudi siasa kali (Jewish extremists) katika kile walichokiita terrorism awareness training program. Hofu iliyopo ni kuwa huenda mafunzo kama hayo yakawafikia pia polisi na

Polisi wapewa bangi kuchukia Waislamu


wana usalama wetu. Ukichukua uzoefu wa ile Patriot Act ambapo serikali yetu ilishinikizwa mpaka nayo ikaweka Patriot Act yake, kuna kila sababu ya kuwa na wasiwasi kuwa mkakati huu wa kuhujumu Waislamu utafika CCP na Kurasini. Au hata kama haukuja huku, lakini tunafahamu kwamba kila uchao maosa wetu wa vyombo ya dola wamekuwa wakipaa kwenda Marekani (School of Americans?) kunolewa. Lakini pia tunafahamu pia kwamba kwa kisingizio cha kushirikiana katika suala la kupambana na ugaidi, ya m e k u wa ya k i f a n y i k a mazoezi ya pamoja kati ya wanajeshi wetu na wale wa Marekani. Hatujui ni kwa kiwango gani mitaala hii ya Dark Film on Muslims imekuwa ikitumika. Lakini pia tunajua kuwa kabla hata ngoma haapigwa, ni kwa namna gani vyombo vyetu vya usalama vimekuwa vikicheza ngoma hii ya kuwahujumu Waislamu kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Tu n a w e z a k u r e j e a aliyofanyiwa Sheikh Said Abri wa Iringa, Abu Hudhaifah na kufungwa kwa taasisi ya Alharamain. M wa k a 2 0 0 5 l i l i wa h i kuandika gazeti la MsemaKweli habari iliyodai kuwa Waislamu Tanzania wameingiza silaha z a k u w a u l i a Wa k r i s t o na kwamba silaha hizo zimefichwa katika Misikiti igamboni na Morogoro. Zaidi ya kujenga chuki miongoni mwa Waislamu na Wakristo, habari hiyo ni kana kwamba inavichochea vyombo vya dola ni kwa nini haviwabamizi Waislamu. Japo mwandishi wa habari hii aliwahi kuongea na mmoja wa viongozi wa WAPO wanaomiliki gazeti hilo na kukiri kwamba habari

Katika uzinduzi huo walihudhuria pia viongozi mbalimbali wa Taasisi za Kiislamu, serikali, za Kijamii, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Mui Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi. Sheikh Mahmoud aliwahimiza Waislamu kushikamana na kupaza sauti ili kuhamasisha maarifa sahihi ya Dini ya Kiislamu.

Alisema, suala la kuandika vitabu vya Dini ya Kiislamu ni muhimu sana ingawa linahitaji juhudi ya makusudi hivyo ni vyema kwa wasomi kuongoza harakati hiyo ya kheri. Akitoa ufafanuzi wa aya mbali mbali za Qur-an Tukufu za Suurat Zumar, K a t i b u M t e n d a j i wa Kamisheni ya Waqfu na Mali ya Amana Zanzibar, Sheikh Abdalla Talib

hiyo ilikuwa ya kuzua. Hata hivyo, jambo la kushtua ni kuwa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na vyombo vya dola juu ya uzushi huo. Badala yake gazeti hili lilipoandika kuonyesha hatari ya habari kama hiyo katika nchi, ndio likaitwa kukemewa na kuonywa na Msajili wa Magazeti. Unachoweza kuona ni kuwa iwapo polisi wetu watapewa dozi hiyo ya The Third Jihad,, hawatasubiri tena kuchochewa na MsemaKweli. Wakati wakuu wa White House wakiweka mtaala wa kuwatia polisi wao chuki dhidi ya Waislamu kwa kuwapaka matope kuwa n i ma g a i d i , m wa n d i s h i wa historia wa Marekani William Blum amechapisha muhtasari ulioboreshwa wa sera za nje za Marekani tangu viishe Vita Vikuu vya Pili Duniani. Katika muhutasari huo kama ulivyonukuliwa na John Pilger katika makala yake The World War on Democracy, Marekani imejaribu kupindua zaidi ya serikali 50, nyingi zikiwa zimechaguliwa kidemokrasia. Imejaribu kunyamazisha harakati za kizalendo katika nchi takriban 20. Imeingilia kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi wa kidemokrasia katika nchi walau 30. Imeangusha mabomu juu ya watu wa nchi zaidi ya 30. Imejaribu kuwaua zaidi ya viongozi 50 wa nchi za nje. Anasema, ni Marekani iliyounda na kufadhili Al Qaidah kupitia ile Operesheni Kimbunga ambapo Waislamu wamekuwa ndio waathirika wakubwa. Kwamba katika siasa hizo, adui amekuwa akibadilika

Abdalla, alisema hima katika ibada duniani ni jambo muhimu ili kumuandaa mja na maisha ya Akhera. Alisema wenye kufaulu ni wale ambao wanatumia hali na mali katika kile alichowajaalia Allah (SW) ili kuieneza Dini ya Kiislamu na hatimaye kujitolea kwa ajili ya maisha ya kudumu Akhera. Akitoa wasifu wa Mtunzi wa Kitabu hicho, Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, SUZA, Dokta Issa Haji Zidy, alisema kifo ni jambo la kukumbuka na hakuna atakayeweza kukiepuka, la msingi ni kujiandaa vyema ili kuweza kukabiliana nacho katika hali njema. Alisema katika kujali hayo, ndiyo miongoni mwa mambo yaliyopelekea Mtunzi wa Kitabu hicho, M wa n a c h u o n i D o k t a Hamed Rashid Hikmany, kuutanabahisha umma juu ya safari hiyo adhimu. Katika kitabu hicho, Mtunzi Dokta Hikmany ametumia falsafa kubwa ya kujiandaa na k u ya k u m b u k a m a u t i , pamoja na changamoto za

hoja za wale wasioamini juu ya hali za kifo na maisha ya Akhera baada ya kufa. Dokta Hikmany ambaye ni miongoni mwa wanataaluma mashuhuri nchini katika fani mbali z a e l i m u , n a a m b a ye amehudumu katika Taasisi na Mamlaka mbali mbali za Elimu, Uchumi, Dini, na Maendeleo, ndani na nje ya nchi, amejumuika pia kuandaa Miswada mbali mbali ya Vitabu, kikiwamo cha Mirathi, Haki na Wito kwa Majirani, vilivyotolewa na Mwanachuoni Sheikh Habib Ali Kombo, ambaye ni Kadhi Mkuu Mstaafu wa Zanzibar. K i t a b u c h a Kuyakumbuka Mauti, K i l i c h o c h a p i s h wa n a Chuo Kikuu cha Elimu C h u k wa n i , Z a n z i b a r, kimesambazwa na Umoja wa Kiislamu wa Elimu, Uchumi, na Maendeleo, UKUEM, na pia kupitiwa na Wanachuoni Mashuhuri akiwamo Katibu Mkuu Mstaafu wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, Zanzibar, Sheikh Khamis Abdulhamid.

LUQMAN ISLAMIC SEMINARY


INAWATANGAZIA WAISLAMU WOTE KUWA NAFASI ZA MASOMO BADO ZIPO KATIKA SHULE ZETU ZA: SEKONDARI (KUJIUNGA FORM ONE) PRIMARY (KUJIUNGA GRADE ONE) CHEKECHEA USAILI KWA WANAFUNZI UNAFANYIKA KILA JUMAMOSI PIA WANAOTAKA KUHAMIA NAFASI BADO ZIPO SHULE IPO MASJID NNUUR SINZA USAFIRI UPO KWA WANAFUNZI WA NURSERY NA PRIMARY. KWA MAWASILIANO: 0713-819391 AU 0713-220567 WABILLAHT TAWFIIQ UONGOZI

jina, kutoka ukomunisti kuwa ugaidi na Uislamu.

Vita ya Dunia kuhusu demokrasiaa


Na John Pilger
JANUARI 20, 2012 (Wakala wa Habari, Washington) LISETTE Talate alikufa hivi karibuni. Namkumbuka kama mwanamke mwerevu, mdadisi aliyekuwa ameficha majonzi yake kwa udhati wake uliokuwa ukionekana dhahiri. Alikuwa kielelezo cha wananchi wanaopambana dhidi ya wale wanaovunja demokrasia. Nilimwona mara ya kwanza kwa mbali katika sinema ya Idara ya Makoloni ya miaka ya 1950 kuhusu wakazi wa visiwa vya Chagos, taifa dogo la watu wa rangi mchanganyiko wanaoishi katikati ya Afrika na Asia, katika Bahari ya Hindi. Kamera ilionyesha vijiji vyenye uchangamfu wa maisha, kanisa, shule, kituo cha afya, vikiwa katika mazingira ya uzuri wa asili na amani. Listte anakumbuka mtengenezaji wa filamu hiyo akimwambia yeye na marafiki zake, Endelea kutabasamu, mabinti! Akiwa ameketi jikoni kwake nchini Mauritius miaka mingi baadaye, alisema sikuhitaji k u a m b i wa n i t a b a s a m u . Nilikuwa mtoto mwenye furaha, kwa sababu mizizi yangu ilikuwa imechimbika katika visiwa hivyo, paradiso yangu. Bibi yangu mzaa bibi alizaliwa pale; nilipata watoto sita pale. Ndiyo maana hawakuweza kutuondoa kisheria kututupa nje ya nyumba zetu; ilibidi watutishe tuondoke au watutoe kwa nguvu. Kwanza walaribu kuleta njaa. Meli za kuleta vyakula ziliacha kuka, halafu wakaanzisha uvumi kuwa tutapigwa mabomu, halafu ndipo wakawageukia mbwa zetu. Katika miaka ya awali ya 1960, serikali ya Uingereza ya Harold Wilson ilikubaliana kwa siri na hitaji la Marekani kuwa visiwa vya Chagos, koloni la Uingereza, kifagiliwe na kusashwa kiondolewe wakazi wake 2,500 ili kituo cha kijeshi kengwe katika kisiwa kikuu, Diego Garcia. Wa l i k u w a w a n a j u a hatuwezi kutenganishwa n a wa n ya m a w e t u wa kufugwa,alisema Lisette. Wakati askari wa Marekani walipowasili kujenga kituo hicho, waliegesha magari ya keshi makubwa kando ya uzio wa matofali wa e n e o a m b a l o t u l i k u wa tunatengenezea nazi; m a m i a ya m b wa w e t u walikuwa wamekusanywa na kufungiwa hapo. Halafu wakawaua kwa gesi kwa mipira iliyounganishwa katika bomba za kutolea moshi za magari hayo. Ulikuwa unawasikia mbwa wakilia. Lisette na familia yake na mamia ya wakazi wa kisiwa hicho walilazimishwa kupanda meli iliyochoka kwenda Mauritius, umbali wa maili 2,500. Walilazimika kulala juu ya mzigo wa mbolea: madondosheo ya ndege. Hali ya hewa ilikuwa mbaya; kila mtu alikuwa anaumwa, wanawake wawili wakaharibikiwa mimba. Wa l i v y o t u p w a k a t i k a b a n d a r i ya Po r t L o u i s , watoto wawili wa mwisho wa Lisee, Jollice na Regis, walikufa ndani ya wiki moja wakifuatana. Walikufa kwa majonzi, alisema. Walikuwa wamesikia na kuona mkasa uliowapata wa l e m b wa . Wa l i k u wa wanajua wanaondoka milele n y u m b a n i . D a k t a r i wa

Makala

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

AN-NUUR

The World War on Democracy


By John Pilger
January 20, 2012 Information Clearing House --LISETTE Talate died the other day. I remember a wiry, fiercely intelligent woman who masked her grief with a determination that was a presence. She was the embodiment of peoples resistance to the war on democracy. I first glimpsed her in a 1950s Colonial Office film about the Chagos islanders, a tiny creole nation living midway between Africa and Asia in the Indian Ocean. The camera panned across thriving villages, a church, a school, a hospital, set in a phenomenon of natural beauty and peace. Lisette remembers the producer saying to her and her teenage friends, Keep smiling girls! Sitting in her kitchen in Mauritius many years later, she said, I didnt have to be told to smile. I was a happy child, because my roots were deep in the islands, my paradise. My greatgrandmother was born there; I made six children there. Thats why they couldnt legally throw us out of our own homes; they had to terrify us into leaving or force us out. At first, they tried to starve us. The food ships stopped arriving [then] they spread rumors we would be bombed, then they turned on our dogs. In the early 1960s, the Labor government of Harold Wilson secretly agreed to a demand from Washington that the Chagos archipelago, a British colony, be swept and sanitized of its 2,500 inhabitants so that a military base could be built on the principal island, Diego Garcia. They knew we were inseparable from our pets, said Lisee, When the American soldiers arrived to build the base, they backed their big trucks against the brick shed where we prepared the coconuts; hundreds of our dogs had been rounded up and imprisoned there. Then they gassed them through tubes from the trucks exhausts. You could hear them crying. Lisette and her family and hundreds of islanders were forced on to a rusting steamer bound for Mauritius, a distance of 2,500 miles. They were made to sleep in the hold on a cargo of fertilizer: bird shit. The weather was rough; everyone was ill; two women miscarried. Dumped on the docks at Port Louis, Lisees youngest children, Jollice, and Regis, died within a week of each other. They died of sadness, she said. They had heard all the talk and seen the horror of what had happened to the dogs. They knew they were leaving their home forever. The doctor in Mauritius said he could not treat sadness. This act of mass kidnapping was carried out in high secrecy. In one ocial le, under the

heading, Maintaining the fiction, the Foreign Office legal adviser exhorts his colleagues to cover their actions by re-classifying the population as oating and to make up the rules as we go along. Article 7 of the statute of the International Criminal Court says the deportation or forcible transfer of population is a crime against humanity. That Britain had commied such a crime in exchange for a $14 million discount o an American Polaris nuclear submarine was not on the agenda of a group of British defense correspondents own to the Chagos by the Ministry of Defense when the US base was completed. There is nothing in our les, said a ministry ocial, about inhabitants or an evacuation. Today, Diego Garcia is crucial to Americas and Britains war on democracy. The heaviest bombing of Iraq and Afghanistan was l a u n c h e d f r o m i t s va s t airstrips, beyond which the islanders abandoned cemetery and church stand like archaeological ruins. The terraced garden where Lisee laughed for the camera is now a fortress housing the bunker-busting bombs carried by bat-shaped B-2 aircraft to targets in two continents; an attack on Iran will start here. As if to complete the emblem of rampant, criminal power, the

Mauritius alisema hawezi kutibu majonzi. Kitendo hiki cha kuteka n ya r a h a l a i k i ya wa t u kilifanywa kwa siri kubwa. Katika jalada moja la kiosi, chini ya kichwa chwa habari Kusitiri uzushi, mshauri wa kisheria wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza anawahimiza washirika wake kufunika vitendo vyao kwa kubadilisha kutambuliwa kwa watu hao kama ambao wapo hati hati na kuunda kanuni mbele ya safari. Kipengere cha 7 cha kanuni za Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (The Hague) kinasema kuhamishwa au kuondolewa kwa nguvu kwa wakazi ni uhalifu dhidi ya binadamu. Kuwa Uingereza ilitenda kosa hilo ili kubadilishana na dola milioni 14 za ununuzi wa nyambizi (submarine) ya nuklia halikuwa katika agenda ya kundi la waandishi wa habari za ulinzi wa Uingereza waliopelekwa Chagos na Wizara ya Ulinzi wakati kituo hicho cha Marekani kilipokamilika. Hakuna chochote katika majalada yetu, alisema osa mmoja wa wizara, kuhusu wakazi au uhamishaji. Leo hii, Diego Garcia ni muhimu sana kwa vita vya Marekani na Uingereza dhidi ya demokrasia. Upigaji mabomu wa nguvu zaidi wa Irak na Afghanistan ulitokea katika viwanja vipana vya ndege, ambako ukivivuka maeneo ya makaburi ya wenyeji na kanisa vinaonekana kama mabaki ya watu wa kale. Bustani yenye matuta ambako Lisee alicheka akipigwa picha, sasa ni ngome ya kuhifadhi mabomu ya kuvunja ngome yanayobebwa na ndege bundi za B-2 dhidi ya kinacholengwa katika mabara mawili; ushambuliaji wa Iran utaanzia hapa. Kana kwamba ni kukamilisha muhuri wa ubabe, mamlaka jinai ya shirika la ujasusi la Marekani (CIA) liliongeza jela ya aina ya Guantanamo kwa wafungwa wanaohamishiwa kutoka kwingine na hatimaye kupelekwa kwingine kwa m a t e s o , i i t wa yo C a m p Justice. Kilichofanywa kwa paradiso ya Lisee kina maana ya haraka na inayohusu watu wote, kwani inawakilisha utumiaji nguvu na kutojali haki za watu ambako ni msingi wa mfumo mzima wa sura ya demokrasia ambayo hutangulizwa, na kiwango cha kujazwa dhana potofu kuona kinachofanyika kuwa ni chema tu kwa binadamu wote, ambako Harold Pinter alisema ni kitendo cha kulalisha

Cont. Pg. 8

Inaendelea Uk. 8

8 AN-NUUR
Inatoka Uk. 7

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

u s i n g i z i k i l i c h o f a n y wa kwa ustadi mkubwa, hata kwa kufurahisha. Ikiwa ndefu zaidi na yenye kuleta madhara makubwa zaidi kuliko vita yoyote tangu 1945, vikipiganwa kwa silaha za kishetani na uharamia unaojificha kama sera za uchumi ambazo mara nyingine huitwa utandawazi, vita dhidi ya demokrasia haitajwi miongoni mwa wasomi na watendaji nchi za magharibi. Kama Pinter alivyoandika, haikuwahi kutokea hata ilipokuwa inatokea. Julai mwaka jana, mwandishi wa historia wa Marekani William Blum alichapisha muhtasari ulioboreshwa wa sera za nje za Marekani. Tangu viishe Vita Vikuu vya Pili Duniani, Marekani: 1. Imejaribu kupindua zaidi ya serikali 50, nyingi zikiwa zimechaguliwa kidemokrasia. 2. Imejaribu kunyamazisha harakati za kizalendo katika nchi takriban 20. 3. Imeingilia kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi wa kidemokrasia katika nchi walau 30. 4. Imeangusha mabomu juu ya watu wa nchi zaidi ya 30. 5. Imejaribu kuwaua zaidi ya viongozi 50 wa nchi za nje. Kwa jumla, Marekani imefanya kitendo kimoja au viwili kati ya vitendo hivyo katika nchi 69, na katika vitendo karibu vyote, Uingereza imekuwa mshirika wake. Adui anabadilika jina, kutoka ukomunisti kuwa Uislamu lakini zaidi ni kuzuka kwa demokrasia isiyoambatana na mataifa ya m a g h a r i b i a u j a m i i inayoshikilia eneo ambalo linafaa kwa mikakati ya kijeshi, ambayo inaweza kuondolewa, kama visiwa vya Chagos. Kiwango cha kushangaza cha mateso kinafahamika kidogo sana katika nchi za magharibi, pamoja na kuwepo kwa njia bora zaidi za mawasiliano, vyombo vya habari vilivyo huru kimsingi kuliko vyote, na uwepo wa kiwango kikubwa cha usomi. Kuwa waathirika wengi zaidi wa ugaidi wa nchi za magharibi ni Waislamu haisemeki, kama inafahamika. Kuwa watoto wachanga nusu milioni wa Irak walikufa katika miaka ya 1990 kutokana na vikwazo vilivyowekwa na Uingereza na Marekani si jambo la maana kwao. Kuwa u-jihad wa kupindukia uliopelekea Septemba 11 (2001) ulengwa kama silaha ya mikakati ya nchi za magharibi (Operesheni Kimbunga) inafahamika kwa wataalamu lakini imenyamazishwa.

Wakati hulka za kitamaduni za Uingereza na Marekani zinafunika Vita Vikuu vya Pili duniani katika bwalo la kuongelea la kimaadili kwa washindi, mauaji ya halaiki yanayotokana na ukiritimba

Vita ya Dunia kuhusu demokrasiaa


wa Uingereza na Marekani katika maeneo yenye raslimali nyingi yanatupwa yasahaulike. Chini ya Suharto, dikteta wa Indonesia aliyetiwa mafuta kuitwa mtu wetu na

Makala
moja ya watu wa Timor ya Mashariki waliouawa kwa njaa au risasi huku nchi za magharibi zikiangalia, kwa kutumia ndege za kivita za Uingereza, na bunduki za risasi za kumimina. H a b a r i h i z i z a k we l i zinaonekana katika majalada ya Public Records Office (baada ya muda wa kuzuiliwa kupita), na hata hivyo zinawakilisha upande mmoja wa siasa na kutumia mamlaka ambako ni nje ya kuhusishwa wananchi. Hii imefanikiwa katika mfumo wa usimamizi wa habari usio wa kulazimisha, ukitawaliwa na liturgia ya matangazo ya kuteka walaji na uangalifu kuhusu nukta zinazotumiwa katika habari za BBC, na s a s a k a t i k a u l i m we n g u maridhawa ya mawasiliano ya kompyuta. Ni kama vile waandishi kama waangalizi wameshapotea duniani, au wako katika mduwaza wa ari ya kizazi-usomi cha kupuuza kabisa jamii, wakiamini kuwa ni wajanja mno hawawezi kudanganywa. Angalia kupigana vikumbo kwa watafuta mshiko wanaojitahidi kukabiliana na (hayati) Christopher Hitchens, mpenda vita aliyetaka sana kuruhusiwa kuhalalisha uhalifu wa taifa kubwa lenye tamaa. Kwa mara ya kwanza katika karne mbili, aliandika Terry Eagleton, hakuna mwandishi wa mashairi, maigizo au riwaya aliye tayari kuhoji mfumo wa maisha wa nchi za magharibi. Hakuna (George) Orwell (1984 na Animal Farm, mzaha wa udikteta wa Ujamaa) kuonya kuwa hatuhitaji kuishi katika nchi ya kidikteta kuharibiwa na udikiteta wenyewe. Hakuna Shelley anayewasemea maskini, hakuna (William) Blake anayetoa taseira, hakuna (Oscar) Wilde kutukumbusha kuwa kutotii, katika macho ya yeyote aliyesoma historia, ndiyo tunu ya awali ya binadamu. Na mbaya zaidi hakuna Pinter wa kughadhibika kuhusu mfumo-vita, kama katika American Football: Hallelujah. Tu m s i f u B wa n a k wa mambo yote mazuri. Tulilipua mipira yao kuwa vipande vya vumbi Vipande vya vumbi habithi Kuwa vipande vya vumbi habithi ndiyo yalikokwenda maisha yote yaliyolipuliwa huko na Barack Obama, mdau wa tumaini-mabadiliko wa udhalimu wa magharibi. Wakati wowote moja ya madege yasiyo na rubani ya Obama yanapofyeka familia nzima katika eneo la mbali la kikabila la Pakistan, au Somalia, au Yemen, waongozaji ndege wakiwa mbele ya screen zao za michezo ya kompyuta wanagonga Bugsplat. Obama anapenda madege

(Margreth) Thatcher, zaidi ya watu nusu milioni waliuawa (1967). Ikiwa imeitwa na CIA mauaji makubwa zaidi katika sehemu ya pili ya karne ya 20, makisio hayo hayajumuishi theluthi

From Pg 7 CIA added a Guantnamostyle prison for its rendition victims and called it Camp Justice. What was done to Lisees paradise has an urgent and universal meaning, for it represents the violent, ruthless nature of a whole system behind its democratic faade, and the scale of our own indoctrination to its messianic assumptions, described by Harold Pinter as a brilliant, even wiy, highly successful act of hypnosis. Longer and bloodier than any war since 1945, waged with demonic weapons and a gangsterism dressed as economic policy and sometimes known as globalization, the war on democracy is unmentionable in western elite circles. As Pinter wrote, it never happened even while it was happening. Last July, American historian William Blum published his updated summary of the record of US foreign policy. Since the Second World War, the US has: 1. Attempted to overthrow more than 50 governments, most of them democratically-elected. 2. Attempted to suppress a populist or national movement in 20 countries. 3. Grossly interfered in democratic elections in at least 30 countries. 4. Dropped bombs on the people of more than 30 countries. 5. Attempted to assassinate more than 50 foreign leaders.

The World War on Democracy


In total, the United States has carried out one or more of these actions in 69 countries. In almost all cases, Britain has been a collaborator. The enemy changes in name from communism to Islamism but mostly it is the rise of democracy independent of western power or a society occupying strategically useful territory, deemed expendable, like the Chagos Islands. The sheer scale of suering, let alone criminality, is lile known in the west, despite the presence of the worlds most advanced communications, nominally freest journalism, and most admired academy. That the most numerous victims of terrorism western terrorism are Muslims is unsayable, if it is known. That half a million Iraqi infants died in the 1990s as a result of the embargo imposed by Britain and America is of no interest. That extreme jihadism, which led to 9/11, was nurtured as a weapon of western policy (Operation Cyclone) is known to specialists but otherwise suppressed. While popular culture in Britain and America immerses the Second World War in an ethical bath for the victors, the holocausts arising from Anglo-American dominance of resource-rich regions are consigned to oblivion. Under the Indonesian tyrant Suharto, anointed our man by Thatcher, more than a million people were slaughtered. Described by the CIA as the worst mass murder of the second half of the 20th century, the estimate

does not include a third of the population of East Timor who were starved or murdered with western connivance, British ghter-bombers, and machine guns. These true stories are told in declassified files in the Public Record Office, yet represent an entire dimension of politics and the exercise of power excluded from public consideration. This has been achieved by a regime of uncoercive information control, from the evangelical mantra of consumer advertising to sound-bites on BBC news and now the ephemera of social media. It is as if writers as watchdogs are extinct, or in thrall to a sociopathic zeitgeist, convinced they are too clever to be duped. Witness the stampede of sycophants eager to deify Christopher Hitchens, a war lover who longed to be allowed to justify the crimes of rapacious power. For almost the rst time in two centuries, wrote Terry Eagleton, there is no eminent British poet, playwright, or novelist prepared to question the foundations of the western way of life. No Orwell warns that we do not need to live in a totalitarian society to be corrupted by totalitarianism. No Shelley speaks for the poor, no Blake proffers a vision, no Wilde reminds us that disobedience, in the eyes of anyone who has read history, is mans original virtue. And grievously no Pinter rages at the war

Cont. Pg. 9

Inaendelea Uk. 9

Makala
Inatoka Uk. 9 yasiyo na rubani na amekuwa akifanya mizaha na waandishi wa habari kuhusu madege hayo. Moja ya hatua zake za kwanza kama rais ilikuwa ni kutoa amri ya kutumia madege ya Predator (mnyama mwindaji) yasiyo na rubani k u s h a m b u l i a Pa k i s t a n , ambako yaliua watu 74. Kuanzia hapo ameua maelfu, zaidi ni raia wa kawaida; madege hayo yanatoa makombora ya Hellfire (moto wa Jehanam) ambayo yakilipuka yananyoya hewa kutoka mapafu ya watoto wadodo na kuacha sehemu za mwili zimetwanyika katika ardhi kame. Kumbuka vichwa vya habari vilivyowatoa watu machozi wakati Bidhaa Obama ilipochaguliwa: tukio muhimu, linainua ashki uti wa mgogo, kwa mujibu wa The Guardia (ya Uingereza). Hali ya baadaye ya Marekani, aliandika Simon Schama, ni taswira, mwanga, bila umbo, rahisi kubeba kichwani. Mwanasafu katika jarida la San Francisco Chronicle aliona mwelekezaji wa kiroho anayeweza kuleta njia mpya ya kuishi katika sayari hii. Nje ya upuuzi huo, kama mtoa tahadhari makini Daniel Ellsberg alivyokwisha tabiri, mapinduzi ya keshi yalikuwa yanatokea Washington, na Obama ndiye mtu wao. Baada ya kuibembeleza harakati ya kupinga vita karibu kunyamaza kabisa, amelipatia tabaka fisadi la wakuu wa majeshi Marekani mamlaka yasiyo ya kawaida ya kupanga na kuendesha vita. Hii ni pamoja na mipango ya vita Afrika na nafasi za kuichokoza China, mkopeshaji mkuu wa Marekani na adui mpya barani Asia. Chini ya Obama mlengwa wa zamani wa utaka-vita nchini Marekani, Russia amezungukwa na makombora ya masafa marefu na upinzani nchini Russia kupenywa. Timu za mauaji za kijeshi na CIA zimeelekezwa cha kufanya katika nchi 120; mashambulio yaliyopangwa muda mrefu dhidi ya Syria na Iran zinaashiria vita vya dunia. Israel, mwendeshaji wa ukandamizaji na uharamia wa Marekani kwa uwakala, amepokea hivi karibuni kile kinachoitwa pesa ya mfukoni dola bilioni 3. Ni pamoja na rukhsa ya Obama kuiba ardhi zaidi ya Wapalestina. Alichokifanya cha kihistoria Obama ni kuleta vita dhidi ya demokrasia nchini Amerika k we n ye we . M k e s h a wa Mwaka Mpya, alitia saini Sheria ya Uratibishaji wa Ulinzi wa Taifa ya 2012, sheria ambayo inayapa haki ya kisheria makao makuu ya Jeshi la Marekani kukamata raia wa kigeni na wa Marekani na kuwafungia kwa kipindi c h o c h o t e , k u wa h o j i n a kuwatesa, na hata kuwaua.

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

AN-NUUR

Wanahitaji tu kuwahusisha n a wa n a o p a m b a n a n a Marekani. Hapatakuwa na ulinzi wa kisheria, kujibu mashitaka, uwakili. Hii ndiyo sheria ya kwanza ya wazi ya kufuta habeas corpus (hali ya kushitakiwa kwa mwenendo wa kawaida wa sheria) na hivyo inatengua Rasimu ya Haki za Raia ya mwaka 1789. Hapo Januari 5, katika hotuba isiyo ya kawaida makao makuu ya Jeshi, Obama alisema jeshi halitakuwa tu tayari kulinda eneo na wakazi nchi za nje

Vita ya Dunia kuhusu demokrasiaa


lakini pia litapigana ndani ya nchi na kutoa msaada kwa mamlaka za kiraia. Kwa maneno mengine, askari wa Marekani watasambazwa katika barabara za mi yake pale machafuko ya ndani yasiyozuilika yakianza. Marekani sasa ni nchi ya umaskini uliokithiri na jela za kutisha: matokeo ya usoko huria wa kupindukia ambako chini ya Obama imewezesha kupelekwa kwa dola 14 triliioni fedha za walipa kodi kwa makampuni jangili ya soko la hisa (Wall Street). Waathirika zaidi

ni vijana wasio na kazi, watu wasio na makazi, Wamarekani Weusi walioko magerezani, waliosalitiwa na rais wa kwanza mweusi nchini humo. Taswira ya kihistoria ya mwelekeo wa kudumu wa vita, huu siyo ufashisti, bado, lakini hata hivyo siyo demokrasia katika hali yoyote inayotambulika, licha ya nafasi ambayo siasa za kupangwa zitakavyokula muda wa habari hadi N o ve m b a . K a m p e n i z a urais, linasema gazeti la kila siku la Washington Post,

From Pg 8 machine, as in American Football: Hallelujah. Praise the Lord for all good things We blew their balls into shards of dust, Into shards of fucking dust Into shards of fucking dust go all the lives blown there by Barack Obama, the Hopey Changey of western violence. Whenever one of Obamas drones wipes out an entire family in a faraway tribal region of Pakistan, or Somalia, or Yemen, the American controllers in front of their computer-game screens type in Bugsplat. Obama likes drones and has joked about them with journalists. One of his rst actions as president was to order a wave of Predator drone aacks on Pakistan that killed 74 people. He has since killed thousands, mostly civilians; drones re Hellre missiles that suck the air out of the lungs of children and leave body parts festooned across scrubland. Remember the tear-stained headlines when Brand Obama was elected: momentous,

The World War on Democracy


spine-tingling: the Guardian. The American future, wrote Simon Schama, is all vision, numinous, unformed, lightheaded The San Francisco Chronicles columnist saw a spiritual lightworker [who can] usher in a new way of being on the planet. Beyond the drivel, as the great whistleblower Daniel Ellsberg had predicted, a military coup was taking place in Washington, and O b a m a wa s t h e i r m a n . Having seduced the antiwar movement into virtual silence, he has given Americas corrupt military ocer class unprecedented powers of state and engagement. These include the prospect of wars in Africa and opportunities for provocations against China, Americas largest creditor and new enemy in Asia. Under Obama, the old source of ocial paranoia Russia, has been encircled with ballistic missiles and t he Russian opposition inltrated. Military and CIA assassination teams have been assigned to 120 countries; long planned aacks on Syria and Iran beckon a world war. Israel, the exemplar of US violence and lawlessness by proxy, has just received

its annual pocket money of $3bn together with Obamas permission to steal more Palestinian land. Obamas most historic achievement is to bring the war on democracy home to America. On New Years Eve, he signed the 2012 National Defense Authorization Act (NDAA), a law that grants the Pentagon the legal right to kidnap both foreigners and US citizens and indenitely detain, interrogate and torture, or even kill them. They need only associate with those belligerent to the United States. There will be no protection of law, no trial, no legal representation. This is the rst explicit legislation to abolish habeas corpus (the right to due process of law) and eectively repeal the Bill of Rights of 1789. O n 5 J a n u a r y, i n a n extraordinary speech at the Pentagon, Obama said the military would not only be ready to secure territory and populations overseas but to ght in the homeland and provide support to the civil authorities. In other words, US troops will be deployed on the streets of American cities when the inevitable Cont. Pg 12

utashindanisha falsafa zinazotofautiana kimsingi kuhusu uchumi. Hii siyo kweli kabisa. Kazi ambayo imepangiwa waandishi wa habari pande zote mbili za Atlantiki ni kuunda dhana ya kuwepo kwa uhuru wa kuchagua kisisa wakati ambapo haupo. Kivuli hicho pia kinaonekana Uingereza na sehemu kubwa ya Ulaya a m b a k o d e m o k r a s i a ya kamii, kipengere muhimu cha imani vizazi viwili v i l i v yo p i t a , i m e a n g u k a mikononi mwa madikteta wa benki kuu. Katika jamii kubwa ya David Cameron, wizi wa pauni bilioni 84 za kazi na huduma unazidi kiasi cha fedha za kodi kilichoacha kihalali bila kulipwa na makampuni haramia. Kosa haliko upande wa uhadhina wa k u p i n d u k i a , l a k i n i utamaduni wa kiliberali (sera holela) wa kisiasa ambao umeruhusu hali hii kutokea ambayo, aliandika H y we l Wi l l i a m s b a a d a ya mashambulizi ya 9/11, kuwa yenyewe inaweza kuwa aina ya siasa kali inayojihalalisha. Tony Blair ni mtu wa s i a s a k a l i h i yo . K a t i k a utawala uchumi usiojali uhuru inaodai kuwa ni muhimu kwake, utawala wa kibwanywenye aliousimamia Blair umeunda dola pelelezi yenye makosa 3,000 mapya ya jinai na sheria zake: zaidi ya zilizotungwa katika karne yote iliyopita. Polisi ni wazi wanaamini wanaweza kuua bila kuzongwa na sheria. Kwa matakwa ya CIA, matukio kama lile la Binyam Mohamed, mkazi wa U i n g e r e z a a s i ye n a k o s a a l i ye t e s wa h a l a f u akafungiwa miaka mitano jela ya Guantanamo, atashughulikuwa katika mahakama za siri Uingereza ili kulinda taasisi za kasusi watesaji wake. Serikali hii isiyoonekana imewezesha utawala wa Blair kupigana na wakazi wa v i s i wa v ya C h a g o s walipoinuka katika kukata tamaa uhamishoni na kutaka haki itendeke katika mitaa ya Port Louis na London. Ni pale tu unapochukua hatua za moja kwa moja, ana kwa ana, hata kuvunja sheria, ndipo unapoweza angalau kuonekana, alisema Lisette. Na ulivyo mdogo zaidi, ndiyo mfano wako kwa wengine unakuwa mkubwa zaidi. Ni jibu fasaha kabisa k wa wa l e a m b a o b a d o wanauliza, naweza kufanya nini? Niliona kiwiliwili kidogo cha Lisette kimesimama katika mvua kubwa pamoja na wanaharakati wenzake nje ya malango ya Bunge. Kilichonishangaza ilikuwa ni ujasiri unaodumu wa mapambano yao. Ni huku kukataa kukata tamaa ambako mamlaka zilizooza zinaogopa, zaidi ya yote, wakua ndiyo mbegu iliyo chini ya barafu. (www.johnpilger.com)

10 AN-NUUR

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

Na Khalid S Mtwangi KILA Muislamu wa nchi hii ni lazima awe amefadhaishwa na kichwa cha habari kilichochapishwa ukurasa wa kwanza wa gazeti hili wiki iliyopita. Zanzibar kuingiliwa na Kanisa Katoliki kwa kiasi hicho ni msiba mkubwa sana. Huko nyuma kulikuwa kikielezwa kisa kimoja kilichomuhusu Al Marhum Mzee Abeid Amani Karume akiwa ndiye Rais wa kwanza wa Zanzibar akiliongoza Baraza la Mapinduzi. Ilikuwa ikielezwa kuwa kuna wakati mmishionari mmoja ama wa Kizungu au Marekani alimuomba Mzee Karume ampe huyu mmishionari kipande cha ardhi pamoja na rukhsa ya kujenga kanisa. Mzee Karume hakumpa jibu la kumkatalia maombi yake wala kumkubalia bali alimualika waonane siku ya Jumapili. Siku hiyo ya ahadi Mzee Karume alimtembeza mgeni wake kupitia makanisa takriban yote yaliyomo Zanzibar mjini. Inaelezwa kuwa takriban makanisa yote yalikuwa ama tupu au yakiwa na waiumini wa chache sana. Baada ya hapo Mzee Karume alimuomba mgeni wake awe na subra asiwe na haraka ya kurudi kwao. Hivyo alimualika tena mgeni huyo wakutane siku ya Ijumaa. Siku hiyo ilipoka Mzee Karume alimtembeza mgeni wake kupitia misikiti takriban yote ya Zanzibar Mjini. Misikiti yote siku hiyo ilikuwa imefurika, na hiyo ndiyo ilikuwa ni kawaida; yaani misikiti hiyo haikufurika kwa sababu Mzee Karume alitoa amri ama kuwajulusha Waislamu kuwa wahudhurie swala ya Aljumaa kwa sababu atakuwa na mgeni. La, haikuwa hivyo bali ni kawaida tu ya waumuni kuhudhuria kwa wingi swala hiyo muhimu. Baada ya kuona hivyo Mzee Karume alimuuliza mgeni wake kuwa kufuatana na hali aliyoiona ya miskitini akilinganisha na makanisa, kipi kinatakikana zaidi, Misikiti au Makanisa. Inasemekana kuwa mmishionari yule Mzungu (ama Marekani) akawa hana jibu. Alifunga virago vyake na kuondoka bila kulizusha tena

suala la kujenga makanisa. Story hii ilikuwa i k i s i m u l i wa s a n a h u k o nyuma, lakini mwandishi huyu hakuweza kupata usahihi wake; hasa kutambua kama mkasa huu ulitokea ama ilikuwa ni mazungumzo tu ya waumini wa Kiislamu. Lakini iwe ni kweli au la, hapa tunajifunza kiasi gani waumini wa dini ya Kiislamu wasivyopendezwa na kuingiliwa na makanisa. Wa k a t i h u o i l i k u w a ikifahamika kiasi gani Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ilivyokuwa ikigamba kuwa ni ya kisekula. Itakumbukwa kiasi gani wengi wa wanataaluma, wakiwemo masheikh wakubwa wakubwa, walivyoikimbia Zanzibar. Kama mkasa huu ni kweli, inaonyesha kiasi gani viongozi walikuwa bado wakiali dini wanayoiamini kuwa ndiyo ya kweli. Msomaji yeyote anayeweza kuwahakikishia wasomaji wenziwe, akiwemo mwandishi huyu, kuwa mkasa huu kweli ulitokea na ni wa kweli, tafadhali atupashe tushushe mioyo yetu. Sasa iweje leo hii Kanisa Katoliki limepata f u r s a p a n a ya k u w e z a kuvamia Zanzibar kiasi hicho kilichoelezwa katika toleo la wiki iliyopita? Imetokea sehemu nyingi sana nchini humu viongozi wa Makanisa ya kila aina wameweza kupata ardhi kwa ulaghai mkubwa sana. Huwakurubia Wananchi vijijini na kuahidi kujenga shule na zahanati kwa minajili ya wanaki hao. Hawataji kamwe kama pia watajenga makanisa kwa sababu wanafahamu wakitoa ukweli huo unaweza kuwaamsha hawa wanaki na pengine wa k a k a t a a k u i n g i l i wa . Hata wanapojenga shule kwa mfano wanafunzi wa Kiislamu hulazimishwa kuhudhuria misa. Haatokea hata siku moja vijana wa Kikristo waliomo katika shule za Kiislamu kulazimishwa k u t a wa d h a n a k u i n g i a m s i k i t i n i k u s wa l i . N a o viongozi wa Serekali huwa mstari wa mbele kusaidia makanisa kupata ardhi. Bila shaka baadhi ya wasomaji watakumbuka jinsi gani ardhi ya makaburi ya Waislamu huko Kyela ilivyoporwa kwa shinikizo la Mkuu wa Wilaya na kupewa kanisa. Wazee wa Kiislamu wa hapo Kyela walilalamika sana, lakini kelele zao na jitihada zao hazikufua dafu, ardhi yao ikaporwa. Haijulikani kama viongozi wa Serekali huko Zanzibar wanaweza nao kuwasaidia mapadri na wachungaji kiasi hicho. Ushahidi uliopo mpaka sasa nikuwa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Vatican yavamia Zanzibar

MAKALA

inajivunia sana ule USEKULA wa k e . H i v y o n i r a h i s i kwa makanisa kutamba na kujitanua watakavyo wakielewa kuwa wanalindwa na Serekali. Kama ule mkasa ulioelezwa hapo nyuma wa Al Marhum Mzee karume ni kweli, basi viongozi wa leo wa Zanzibar wamepotoka sana na huo USEKULA WAO. Watambue kwamba h u k o U l a ya M a g h a r i b i ambako ndiko wanadai wanautekeleza sana huo USEKULA, wao ni manaq. Wasomaji watakumbuka kwamba Uturuki imekuwa ikijaribu sana kujiunga na Umoja wa Ulaya (European Union) kwa muda mrefu. Tangu kuingia kuiongoza Turkey Waziri Mkuu Tayipp Erdogan kafanya mabadiliko mengi sana kuifanya nchi hiyo kweli iwe ya kidemokrasia. Hayo ni yale waliyokuwa wakisema ndiyo yanazuia Turkey kukubaliwa kjiunga na Umoja huo. Lakini ukweli ni kwamba Ulaya hawaitaki Uturuki kuwa mmoja wao kwa vile ni nchi ya Kiislamu. Ukweli ni kwamba huyu Baba Papa wa sasa Papa Benedictine XII amekuwa anawaongoza watu wa kabila lake la Bavaria, Ujeremani, kupinga kabisa Uturuki kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Chama cha Chancellor wa sasa wa Ujeremani, Angela Markus kina pata nguvu yake kutoka huko. Papa huyu kasema wazi kuwa Ulaya ni ya Wakristo na ametamka kutaka katiba ya Umoja Wa Ulaya na zile za nchi zingine zitamke hivyo. Msimamo wake huyu Papa Benedict XII ni mkali sana dhidi ya Waislamu na Uislamu. Itakumbukwa jinsi gani alivyomkashifu Rasl-ul-Llah Muhammad SAW na akakataa kuomba

radhi. Askofu Kilaini wa nchini humu alimuunga mkono kwa hilo. Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafakari kwa makini kabisa msimamo huu wa Kanisa Katoliki. Wasisahau kuwa wao ni Waislamu. Wenzao hao wa Kanisa Katoliki wanaongoza kuivamia Zanzibar wanakumbuka kila dakika kuwa wanatakikana kulitumikia kanisa leo na wa k a t i wot e. K u ivamia Zanzibar ni katika njia za kutimiza ahadi na maazimio k a m a ya l e ya N a i r o b i , Kenya. Inajulikan wazi hapa d u n i a n i k u wa M f a l m e aliyebaki mwenye kauli ya mwisho (Abnsolute Monarch) ni Papa aliye Vatican. Papa Leo XIII aliyetawala kuanzia 1878 mpaka 1903 aliamuru hivi:It is always urgent indeed the chief preoccupation to think best how to serve the interests of Catholicism. .which is the only true religion (p 150, Vicars of Christ by Peter de Rosa). Hapa anamaanisha kwamba ni wajibu wa kila Mkatoliki kuutumikia Ukatoliki ambayo ndio dini pekee (duniani). Kanisa halikuishia hapo. Wasomaji bila shaka wanakifahamu kitengo cha Kanisa hilo watawa wake wa kiume wakiitwa THE JESUITS. Hawa ni kikosi cha sakari wa miguu (foot soldiers) ambao wao husasha njia Ukatoliki upite kwa urahisi. Bila shaka wamo tele Zanzibar. Aliyekianzisha kikosi hicho anajulikana kama Ignatius de Loyola (ana historia ya kutisha). Inasemekana alianzisha kikosi hicho kwa madhumuni mawili (i) universal political power and (ii) universal church; yaani kutawala ulimwengu. Wengi

wa wanataaluma wa Agano Jipya wanasema haulikani nani aliandika INJILI UFUNUO (REVELATIONS) lakini dhamira ya huyu Ignatius de Loyala ilikuwa ni kufanikisha ama kutimiza utabiri uliomo katika Injili hiyo, 6, 13, 17 na 18. Hakuishia hapo tu. Kaamrisha kuwa We must see black as white if the Church says so (THE SECRET HISTORY OF THE JESUITS). Kama ni haya kweli, basi Zanzibar kweli wamevamiwa. Wa s o m a j i b i l a s h a k a watakumbuka ule mkutano mkubwa uliowakutanisha Maaskofu kutoka Afrika uliofanyika Nairobi mwaka 1994. Labda bila kujua hayati Cardinal Otunga wa Kenya alichua mbinu walizopanga kuupiga vita Uislamu Afrika na Tanzania. Sijui ni kiasi gani viongozi wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar walivyo na msimamo kuhusu U i s l a m u i n g a wa k we l i takriban wote ni waumini wa dini hiyo ya kweli na haki. Lakini wakumbuke kuwa ni khulka ya Kanisa Katoliki kwamba kila wanapokuwepo wao, ni lazima washike hatamu ya utawala. Uzoefu walionao Waislamu wa Tanganyika (DANGANYIKA?) unatosha kuwa fundisho zuri kwao. Kwa msaada wa Serekali, Waislamu wa Tanganyika (DANGANYIKA?) wamebanwa koo hata hawawezi kufurukuta kukohowa. Jee, viongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar wanataka wakumbukwe na historia kama wao ndio Waislamu walioupiga ama waliofanikisha kuumaliza Uislamu Zanzibar?

MAKALA

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

AN-NUUR

11

Uhuru wa Tanganyika haukuletwa na Nyerere peke yake


Na Mohamed Said (19 Januari, 2012) KAMA kawaida ya makala z a M z e e w a n g u Yu s u f Halimoja huwa ni mchuzi wenye viungo vingi, hiliki, giligilani, abdalasini, binzari nyembamba na kadhalika. Mzee Halimoja kazungumza kuhusu historia ya TANU na nafasi ya Nyerere, kazungumza kuhusu Mihadhara ya Uchochezi ya Waislamu, kazungumza kuhusu Elimu ya Waislamu na Chuo Kikuu, kama ada yake hakuweza kuacha kuzungumza kuhusu Waarabu na Utumwa, nk. (Jamhuri 17 23, 2012). Insha Allah nitajitahidi kugusa kote. Pili ningependa kumfahamisha Mzee Halimoja kuwa hicho kichwa kilichopamba makala yangu aliyoijibu, Halimoja ana Chuki na Waislamu, si kichwa nilichoandika mimi. Nadhani kichwa hiki ndicho kilichomfanya Mzee Halimoja aseme kuhusu uchochezi wangu. Sasa ikiwa mimi sikuweka kichwa hicho hapo awali ni wazi kuwa shutuma ya uchochezi itakuwa i m e n i e p u k a i s i p o k u wa nitabakia na lile la kuwaenzi Waislamu na mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Hata hivyo hilo halinitoi katika kujibu baadhi ya shutuma kuhusu Waislamu kuwa ni wachokozi. Napenda kumfahamisha Mzee wangu Yusuf Halimoja kuwa katika maandiko yangu yote na katika mihadhara niliyopata kutoa ndani na nje ya nchi, sapata kusema kuwa Waislamu walitoa mchango mkubwa kuliko mchango aliotoa Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Saona haja ya kupima nani kasaidia zaidi harakati za kudai uhuru labda kwa kuwa hata kama leo nitataka kufanya hivyo tatizo litakuwa ni vigezo gani nitumie ili kujua nani kamzidi nani. Hii bila shaka itakuwa kazi kubwa kwa kuwa waliopigania uhuru wa Tanganyika walikuwa wengi. Kuna wale waliokuwa pale Makao Makuu ya TAA na kisha TANU pale New Street, Dar es Salaam na kuna wale waliokuwa majimboni. Jingine ni kuwa hadi TANU inaanzishwa, TAA ilikuwa tayari ishakuwapo kwa miaka 21 na viongozi wakiingia na kutoka na kila mtu alikuwa na mchango wake. Mzee Halimoja akitaka kujua mchango wa viongozi hawa ambae yeye hawaoni kuwa ni wanasiasa na asome tahariri alizokuwa akiandika Erika Fiah katika miaka ya 1930 ndani ya gazeti lake Kwetu alilokuwa akilihariri yeye mwenyewe. Nakala za gazeti hili zinapatikana Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. F i a h a l i k u wa m f u a s i wa Marx na alijaribu kuhamasisha tabaka la wafanyakazi na wakulima kuwaunganisha dhidi ya ukoloni. Kuanzia mwaka wa 1950 kulikuwa na kamati ya ndani ya TAA iliyokuja kuasisi TANU. Pamoja na haya kuna viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika waliokujatoa uongozi katika TANU. Sasa vipi mtu atasema harakati kazianza Nyerere wakati haya yalipokuwa yakitendeka Nyerere hakuwapo? Kuna wazalendo kama Kleist Sykes, Ali Jumbe Kiro, Ali Mwinyi Tambwe, Salum Abdallah, Ibrahim Hamisi, Hassan Machakaomo, Maalim Popo Saleh na wengine, hawa waliitumikia African Association, kisha TAA na baadae TANU. Wengi wao walishughulika sana katika miaka ya 1940 hadi kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili. Kuna watu kama Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz (wanakamati ya ndani ya TAA) waliokuja kupokea kijiti kutoka kwa wazee wao. Dossa alikuwa hapandi j u k wa a n i l a k i n i n d i yo ilikuwa benki ya TANU. Inasemekana hakuna wa kumkia Dossa kwa fedha alizotoa katika kupigania uhuru. Ikutoshe tu kuwa gari la kwanza TANU kuwanalo kumsaidia Nyerere kwenda huku na kule alilitoa Dossa. Abdulwahid Sykes hakuwa anapanda jukwaani lakini na yeye alikuwa sanduku l a f e d h a l a TA N U , halikadhalika mdogo wake Ally Sykes. Kalamu ya Abdulwahid Sykes na mipango alokuwa akiipanga akishirikiana na Mufti wa Tanganyika na Zanzibar Sheikh Hassan bin Amir, Hamza Mwapachu, Dk. Vedasto Kyaruzi, Stephen Mhando na wanakamati wa TAA Political Sub Commiee ndiyo iliyosababisha uhuru upatikane mwaka 1961. Kamati hii iliundwa 1950 ndani ya TAA na wakati ule Nyerere hakuwapo. Vana hawa waliungwa mkono na wazee waliounda Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa na Waislamu watupu. Katika hawa wazee wapo waliokuwa wanapanda majukwaani na kusafiri na Nyerere vijijini kuitangaza TANU kama Sheikh Suleiman Takadir, Rajab Diwani na wengineo na walikuwapo wengine hawakuwa wapanda majukwaa lakini wakichangia juhudi zile kwa njia nyingine. Katika hawa mchango wa Mshume Kiyate ni wa kupigiwa mfano. Harakati za kudai uhuru hazikuanza na Nyerere m wa k a 1 9 5 4 v u g u v u g u lilianza toka miaka ya mwisho ya 1920 African Association ilipoasisiwa. Chama hiki kina historia yake na kina mashujaa wake waliofanya makubwa katika wakati wao kama Kleist Sykes, Erika Fiah, Ali Juma Ponda, Hassan Tawafiq Suleiman, Edward M wa n g o s i n a w e n g i n e wengi. Wazalendo hawa walikuwa na mchango wao wa kuwaamsha wananchi wajue. Naamini Mzee wa n g u H a l i m o j a l a b d a h a k u wa a n a ya j u a h a ya kama Watanzania wengi walivyokuwa gizani katika historia hii ya kutukuka. Mzee Halimoja yeye anaamini hapakuwa na siasa katika TAA lakini Waingereza wakijua fika kuwa TAA ingawa haikuwa na katiba ya siasa lakini kilikuwa chama cha siasa kamili. Moja ya masikitiko yangu ni kuwa hadi leo watoto wa marehemu Abdulwahid Sykes hawajaamua kuzifungua na kuziweka wazi shajara za baba yao alizokuwa akiziandika kabla na baada ya kuunda TANU kwa hiyo mengi hayajulikani kama ambavyo tungelipenda kufahamu. Ningependa kumwekea msomaji hapa machache kutoka nyaraka za Sykes: ...it is reported that the Secretary of the Association, A b d u l Wa h i d S y k e s h a s dispatched leers to all branches asking members for suggestions under the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal Commission... ...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as reported in last months summary (paragraph 20) was going on safari up country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then visited Kampala alone.....on 8th March, a secret meeting was held, aended by leading members of the Mwanza B r a n c h . . . ( Ta n g a n y i k a Political Intelligence Summary March, 1952). Tukija katika TAA hasa kuanzia mwaka wa 1950 kuna wengi waliopambana na ukitaka kujua hali ya siasa ilivyokuwa wakati ule pitia nyaraka za marehemu Abdulwahid Sykes. Utakayosoma katika nyaraka hizi zitakudhihirishia bila hofu wala wasiwasi kuwa TAA kilikuwa chama cha siasa. Kutokana na nyaraka hizi mwandishi ameandika kitabu cha maisha ya Abdulwahid Sykes na ndani yake kawataja wale wote walioondolewa aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya katika historia ya kudai uhuru. Inawezekana watu kama Halimoja hawataki tu kusikia upande mwingine wa historia. Hili ni jambo la kusikitisha kwani kwa kuifunga akili yao kuhusu historia hii watapitwa na mengi. Halimoja anasema Nyerere ndiye aliyepeleka harakati vijijini. Halimoja anasema hivyo kwa kuwa labda kama ni mkweli kuna asiyoyajua kuhusu kuipeleka TANU kwa wananchi. Ushahidi wa kihistoria haukubaliani na msimamo wa Mzee Halimoja. Ningependa kumkumbusha Mzee Halimoja majina ya waasisi wa African Asociation kwa kuwa yeye kanasa na Cecil Motola peke yake mtu wa Masasi mwenzake. Kleist Sykes ndiye aliyeasisi Africa Association baada ya kuifanyia kazi fikra aliyopewa na Dr. Aggrey mwaka 1924. Kleist aliasisi African Association mwaka 1929 akiwa na rafiki zake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake wa l i k u wa Wa m a n y e m a kutoka Belgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Was na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi, Kleist akiwa katibu muasisi wa African Association. Napenda tena kumjuvya Mzee Halimoja kuwa wanachama wa kwanza wa TANU walitoka Rufiji mwaka 1954 na aliyekwenda kuwatafuta wanachama hao ni Said Chamwenyewe baada ya kuagizwa na Abdulwahid Sykes ili TANU ipate tasjila kwa kuwa wakoloni walikataa kuisajili TANU ati chama hakina watu. Katika kipindi hicho majuma machache tu tangu TANU iasisiwe Zuberi Mtemvu akachukua kadi za TANU kutoka kwa Ally Sykes akifuatana na Nyerere wakenda Morogoro kukitangaza chama. Mwaka 1956 katika vi vya Dodoma TANU iliingizwa vini na Haruna Taratibu na Omar Suleiman. Mwaka huo huo katika vijiji vya Jimbo la Kusini, TANU iliingizwa vijijini na Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Suleiman Masudi Mnonji, Sharia bint

Mwalimu Julius K. Nyerere Mzee, Said Alley Mwalimu, Mohamed Ali Abdallah na wanaharakati wengine. Huko Kilimanjaro TANU ilienezwa na akina Yusuf Olotu, Mama bint Maalim, Halima Selengia, Melkezedek Saimon, Gabrieli Malaika, Eikaeli Mbowe, Juma Ngoma na wengine wengi. Mifano naweza kuitoa mingi sana. Halimoja anasema labda kwa kuegemea historia ya Nyerere kama auavyo yeye kuwa tawi la Dar es Salaam la TANU ndilo lilikuwa dhaifu. Sui anakusudia tawi lipi kwa kuwa matawi ya TANU Dar es Salaam yalikuwa lukuki na yote hayo yalikuwa na nguvu sana kuanzia Makao Makuu New Street hadi uje Tawi la Kisutu ambalo baadae lilikuja kuhamia Mtaa wa Mvita. Hili tawi la Mvita lilikuwa chini ya uongozi wa Mtoro Kibwana kama katibu na Sheikh Haidar Mwinyimvua kama Mwenyekiti na baadae uenyekiti ukashikwa na Yahya Saleh. Inasemekana tawi hili ndilo lililokuwa na nguvu kushinda matawi yote Tanganyika. Huu ndiyo ukweli na picha na nyaraka k u t h i b i t i s h a h a ya yo t e zipo na mwandishi katika kutati historia ya uhuru wa Tanganyika kapata bahati ya kuzisoma nyaraka za wakati huo na kuzifanyia uchambuzi. Sasa kama Mzee Halimoja bado kaelemewa na ile propaganda kuwa TAA kilikuwa chama cha starehe hakuna wa kumzuia katika fikra zake hizo. Kwa mukhtasari hii ndiyo ilikuwa michango ya baadhi ya wazalendo ambao hadi l e o t a i f a l i m e wa s a h a u . Katika hali kama hii vipi Mzee Halimoja atadai kuwa Nyerere alikuwa na mchango wa pekee? Hiyo pekee kama ipo na atufahamishe tupo tayari kumwazima masikio yetu. Itaendelea toleo lalo

12 AN-NUUR

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

Barua/Shairi/Makala

Hitajio la Katiba
Kalamu imkononi, ikiwa Mwanza jini Namhimidi Manani, na kumuomba auni Yailahi niauni, nitoe yangu maoni Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Wazalendo sikilizeni, wa bara na visiwani Awali ni wajuzeni, hoja kuu ya shairi Katiba ndio kiini, cha yangu hasa maoni Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Katiba yetu nchini, dosari imesheheni Hilo mtalibaini, mkiidurusu kwa ndani Mtatambua kiini, cha hoja ilo mezani Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Dosariye namba wani, ni uhuru ibadani, Wang`ara wa kanisani, uhuru wa yao dini Jambo hili kulikoni, liminywe kwa yetu dini Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Ubaguzi wa kidini, utadumu hadi lini Unalelewa kwa nini, kwa maslahi ya nani Kama nchi si ya dini, ubaguzi ni wa nini Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Jambo hili kwa makini, ladiliwe nchini Jukwaa tushirikini, kutoa yetu maoni Tusibaki mkiani, mfumo ukatuwini Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Tume huru pa nchini itabaki kuwa njozi, Mteuziwe ni nani, si Rais wa hi nchi Hapo mwataraji nini, mwananchi nambieni Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Ni muajiriwa gani, bosiwe anomukhini Ni muhali abadani, nyote hilo tambueni Hiki hasa ndo kiini, cha Tume mbovu nchini Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Na ule mfumo duni, utoweke katibani Mtu mmoja bungeni, huyo huyo wazarani Mbunge kwake jimboni, waziri serikalini Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Ujamaa ni wanini, hadi leo katibani Siku nyingi mautini, ushazikwa kaburini Hadi leo ni kwa nini, wanadiwa katibani Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Mjamaa leo nani, ajinadi hadharani Si kiongozi wa nchini, wala raia sioni Kama si hadaa nini, kumtaja katibani Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Wasomi wenye uoni, ebu nanyi tujuzeni Mlo Dar Mlimani, na Moro MUM chuoni Mambo haya katibani, yatadumu hadi lini Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Maoni yapokeeni, kwa kina tafakarini Na kisha yapembueni, mnuze nuksani Jamii iaunini, msiiache kizani Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Mheshimiwa Kombani, na wenzo serikalini Kwa kweli nakusihini, kwa nia njema moyoni Maoni yaheshimuni, ya wananchi nchini Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Kwa heri nakuageni, ni yenu sasa mizani Khamsa shara jamani, kuzidisha sitamani Tamatini ikalamu, naweka chini jamani Twataka katiba mpya, kwa maendeleo yetu. Na Abuu Nyamkomogi Mwanza

Mwelekeo wa kujitia hasira kama wa Mtwangi hautusaidii sana


Bwana Mhariri, Assalaam Aleikuum, NINGEPENDA kutoa maoni kuhusu makala ya Bwana Khalid Mtwangi iliyochapishwa kwenye toleo la Januari 20, 2012. Bwana Mtwangi amegusa jambo muhimu ambalo lipo katika jamii yetu ya wasomi wa Kiislamu, nalo ni kutoshiriki kikamilifu katika juhudi za kijamii za kuinua hali ya maisha ya Waislamu wenzetu, hususan katika elimu. Mfano ujenzi wa shule unawezekana kabisa, watu wakijitolea kuchangia kwa hali na mali kufanikisha ujenzi huo. Wi k i i l i yo p i t a , Jumapili tarehe 22; wanawake wasomi wa Kiislaamu wa l i k u s a n y i k a n a mojawapo ya mambo mazuri waliyoazimia ni kujenga mabweni na kituo cha elimu kitakacho jumuisha wa t o t o ya t i m a n a wale waishio katika mazingira magumu; wanaokosa fursa za elimu kwasababu ya kutokua na uwezo. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanawake takriban 350 kutoka taaluma mbalimbali. Palepale tuliweza kuchanga fedha nzuri tuu kwa ajili ya maandalizi ya kituo hicho. Njia mmojawapo i l i y o t u m i k a kutuhamasisha tuone umuhimu wa k u wa k wa m u a Waislamu wenzetu ni takwimu na hadithi zilizotolewa ambazo ziliashiria hali ngumu na duni iliyokua inawakabili watoto wengi hususan hapa mji mkubwa wa Dar es Salaam. V i l e v i l e tulipewa takwimu zinazoashiria hali duni ya asilimia kubwa ya wanawake wa Dar es Salaam wengi wao wakiwa ni wanawake wa Kiislamu wanaoishi na kulea familia zao kwenye makazi duni na hatarishi. TA K W I M U , DOCUMENTARIES, HALI HALISI; HATA KAMA NDOGO NI NJIA NZURI NA E N D E L E V U YA KUHAMASISHA W A S O M I KUCHANGIA K A T I K A MAENDELEO. MFUMO HUU NI BADALA YA K U T U M I A MAENDELEO YA W E N Z E T U WAKRISTO KAMA BENCHMARK AU NDIO KAMA KICHOCHEO CHA SISI KUJENGA SHULE AU VITUO VYA AFYA N.K.

Taasisi gani bora kwa safari za Hijja


Ndugu Mhariri, I n s h a A l l a h nakusudia kwenda hija msimu ujao. Mnanishauri nitumie taasisi gani yenye kutoa huduma bora? Najua zipo taasisi
From Pg. 9

N J I A H I I YA TA K W I M U N A HALI HALISI NI ENDELEVU ZAIDI K WA S A B A B U INAHAMASISHA HISIA AMBAZO NI ZA KIMIKAKATI NA ZA KUTENDA ZAIDI (PRO-ACTIVE); KULIKO HISIA ZINAZOPELEKEA HASIRA NA KUJIHURUMIA KAMA ZILE ZA MZEE KHALID MTWANGI. Tu s a i d i a n e n a tuinuane kwa s a b a b u n i wa j i b u w e t u s i s i t u k i wa Wa i s l a m u . I b a d a zetu hazijakamilika bila kusaidia na kutoa sadaka kwa njia mbalimbali kama Qurani Tukufu inavyotueleza kwenye Surat-il-Baqara Aya 177 ( Quran 2 : 177). Wabillah Tawq, Ta t u Z u b e d a Mtwangi (Dr)

The World War on Democracy


rooted in distinctly different views of the economy. This is patently false. The circumscribed task of journalism on both sides of the Atlantic is to create the pretence of political choice where there is none. The same shadow is across Britain and much of Europe where social democracy, an article of faith two generations ago, has fallen to the central bank dictators. In David Camerons b i g s o c i e t y, t h e theft of 84bn pounds in jobs and services even exceeds the amount of tax legally avoided by piratical corporations. Blame rests not with the far right, but a cowardly liberal political culture that has allowed this to happen, which, wrote Hywel Williams in the wake of the aacks on 9/11, can itself be a form of self righteous fanaticism. Tony Blair is one such fanatic. In its managerial indifference to the freedoms that it claims to hold dear, bourgeois Blairite Britain has created a surveillance state with 3,000 new criminal oences and laws: more than for the whole of the previous century. The police clearly believe they have an impunity to kill. At the demand of the CIA, cases like that of Binyam Mohamed, an innocent British resident tortured and then held for ve years in Guantanamo Bay, will be dealt with in secret courts in Britain in order to protect the intelligence agencies the torturers. This invisible state allowed the Blair government to fight the Chagos islanders as they rose from their

nyingi zenye kufanya shughuli hii. Lakini inakuwa tabu kujua nani bora kwa kufuata matangazo yao kwenye magazeti na redio kwani haulikani wanakusudia

kuwasaidia waumini kufanya ibada yao hii kwa ufanisi au ni wao wanafanya biashara ya kupeleka watu ha. Karibuni tujadili, tusaidiane ili kuboresha ha zetu na kupata malipo ya ha

kama inavyotarajiwa. Mliowahi kwenda ha mtatusaidia sana kwa kutupa uzoefu wenu. Saidiane kwa ajili ya Allah. Mohammed Said Tanga

civil unrest takes hold. America is now a land of epidemic poverty and barbaric prisons: the consequence of a market extremism which, under Obama, has prompted the transfer of $14 trillion in public money to criminal enterprises in Wall Street. The victims are mostly young jobless, homeless, incarcerated AfricanAmericans, betrayed by the first black president. The historic corollary of a perpetual war state, this is not fascism, not yet, but neither is it democracy in any recognizable form, regardless of the placebo politics that will consume the news until November. The presidential campaign, says the Washington Post, will feature a clash of philosophies

despair in exile and demanded justice in the streets of Port Louis and London. Only when you take direct action, face to face, even break laws, are you ever noticed, said Lisee. And the smaller you are, the greater your example to others. Such an eloquent answer to those who still ask, What can I do? I last saw Lisettes tiny figure standing in driving rain alongside her comrades outside the Houses of Parliament. What struck me was the enduring courage of their resistance. It is this refusal to give up that roen power fears, above all, knowing it is the seed beneath the snow. www.johnpilger. com

Makala

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

AN-NUUR 13

Wajibu wa wazazi kwa watoto


Na Azza Ally Ahmed WAZAZI wanawajibu mkubwa kwa watoto w a o . Wa j i b u h u o n i kuwapa malezi bora yatakayowawezesha kuinukia kuwa watu wema katika jamii. Malezi yanahusu yale yote anayofanyiwa mtoto tangu akiwa tumboni mwa mama yake mpaka kukia umri wa kujitegemea mwenyewe. Wazazi wote wawili wanahusika kwa ukamilifu na malezi haya. Malezi ya mtoto tunaweza kuyagawa katika sehemu mbili - Malezi ya kimwili na malezi ya kiroho. Malezi ya kimwili ni yale yote anayofanyiwa mtoto ili akue katika afya njema. Malezi haya huanza mara tu mama anapoanza ujauzito. Baba ana wajibu wa kumtunza mkewe na kumpatia vyakula maalum ili mama na mtoto wake tumboni wawe na afya nzuri. Jukumu la mama ni kufuata masharti ya kulea mimba anayopewa na Daktari. Baada ya mtoto kuzaliwa wajibu wa baba na mama kwa mtoto wao u n a b a i n i s h wa k a t i k a Quran: Na wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha; na ni juu ya baba chakula chao (mama na mtoto wake) na nguo zao kwa sheria. Wala haikalishwi nafsi yoyote ila kwa kadri ya wasaa wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake, wala baba (asitiwe taabuni) kwa ajili ya mtoto wake. Na juu ya mrithi ni kama hivyo. Na wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa (kabla ya miaka miwili) kwa kuridhiana na kushauriana, basi si kosa juu yao. Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha ( we n g i n e wa s i o k u wa mama zao), basi haitakuwa dhambi juu yenu kama m k i t o a ( k u wa p a h a o wanyonyeshaji) mlicho waahidi kwa sharia. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayoyatenda. (2:233). Aya hii inatubainishia wazi kuwa hata katika umri wa kunyonya mtoto, wazazi wote wawili wanawajibika, kila mmoja katika nafasi yake. Katika kipindi chote cha kumlea mtoto jukumu kubwa la baba ni kuilisha familia, kuivisha na kuiweka katika makazi mazuri kwa kadiri ya wasaa wake. Mama naye ana jukumu la kuwatunza watoto kwa kuhakikisha kuwa wanakula vilivyo, wanakuwa wasa wa mwili na nguo na wanaishi katika mazingira masafi. Haya ndiyo malezi ya kimwili ambayo humuwezesha mtoto kuwa na afya mzuri na kukua vyema. Malezi ya kimwili ni muhimu sana, lakini yenyewe tu hayatoshelezi kumuinua mtoto atakayekuwa raia mwema mwenye kuwajibika ipasavyo kwa wazazi wake na kwa jamii yake kwa ujumla. Uislamu haumtizami mwanaadamu kama mnyama, bali unamtazama kama Khalifa wa Mwenyezi Mungu (s.w.) ambaye asili yake ni mwili unaotokana na udongo na Roho takatifu, inayotokana na Mwenyezi Mung u (s.w.) kama tunavyojifunza katika Quran: Na (kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo mkavu unaotoa sauti, wenye kutokana na matope meusi yaliyovunda! Basi nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayotokana na Mimi, basi muangukieni kwa kumtii (15:28-29). Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa kilichomfanya mwanaadamu kuwa na hadhi juu ya viumbe vyote hata malaika ambao waliamrishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.) kumuangukia kwa utii, si uzuri wa sura yake au umbile lake, bali ni ile Roho takatifu inayotokana na Mwenyezi Mungu (s.w.). Lakini si kila mwanaadamu atakaye stahiki heshima hii ya kuangukiwa kwa utii na malaika. Anayestahiki heshima hii ni yule tu atakayeishi kwa kufuata tabia na mwenendo anaoridhia Mwenyezi Mungu (s.w.) au kwa kufuata maadili mema anayoyaridhia Mwenyezi Mungu (s.w.).

USTAADH Rashid Jumaa akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi wa Al Jumaa mbele ya mwalimu wake. Atakayeishi kwa kufuata wa kufundisha watoto asiyezaliwa katika (dini msukumo wa matashi U i s l a m u n a k u wa l e a ya) asili (Uislamu). Kisha ya mwili (unyama) wake k a t i k a m we n e n d o n a wazazi wake humfanya na kuukataa mwongozo tabia ya Kiislamu, tangu kuwa Myahudi au Mkristo wa Mwenyezi Mungu wanapokuwa na umri a u M m a j u s i . K i s h a ( s . w. ) , h a d h i y a k e wa miaka mitano mpaka akasema: Umbile la Asili itashuka na kuwa duni kufikia umri wa miaka ndilo umbile Mwenyezi Mungu aliloumbia watu. kuliko vilivyo duni kama 15. M z a z i a h a k i k i s h e Hakuna mabadiliko katika Mwenyezi Mungu (s.w.) kuwa watoto wa umri wa maumbile ya viumbe vyote anavyhotufahamisha: B i l a s h a k a miaka saba na kuendelea vya Mwenyezi Mungu. t u m e m u u m b a wanatekeleza ipasavyo (Bukhari na Muslim). Hadithi hii iliyomalizia mwanaadamu kwa umbo i b a d a m a a l u m k a m a na aya ya Quran (30:30) lililo bora kabisa. Halafu v i l e s wa l a , s wa u m u , tukamrudisha chini kuliko na kadhalika. Watoto inatukumbusha kuwa walio chini. Ila wale wenye wa umri wa miaka 10 U i s l a m u n d i o d i n i kuamini na kutenda mema, na kuendelea ni lazima inayolingana na umbile watakuwa na ujira usio watekeleze maamrisho la mwanaadamu na kwa yote ya Mwenyezi Mungu hiyo kila mtoto huzaliwa kwisha. (95:4-6). Hivyo, wazazi pamoja ( s . w. ) k wa k a d i r i ya M u i s l a m u . H i v y o n i n a k u w a l e a w a t o t o uwezo wao. Wakiacha wajibu wa kila mzazi wao kimwili, hawana makusudi kufanya hivyo Muislamu kumlea mtoto budi kuhakikisha kuwa wazazi au walezi wao wake katika dini yake ya wa n a wa l e a k i m a a d i l i wawaadhibu. Pia mzazi asili kwa jitihada zake zote kwa kuwafunza tabia anatakiwa ampeleke mtoto mpaka amkishe kwenye wake shuleni anapofikia na mwenendo mwema umri wa kwenda shule utu-uzima wake. Hapana anaoridhia Mwenyezi na kufuatilia masomo shaka kutekeleza wajibu huu wa kuwalea watoto M u n g u ( s . w. ) . M t o t o aanze kufunzwa tabia ya y a k e i l i k u m u a n d a a wetu katika maadili ya Kiislamu tangu mwanzo, m wa n a we k u wa r a i a Kiislamu ni jambo gumu h a s a p a l e a n a p o a n z a hodari atakayeweza kutoa linalohitajia msaada wa kuongea na kuelewa lile mchango wake katika Mwenyezi Mungu (s.w.). analoelekezwa. kuiendeleza jamii kwa M u u m i n i w a k w e l i Mtoto afikapo umri kadiri ya ujuzi wake. pamoja na jitihada zake wa miaka mitano, Huu ndio utaratibu katika kutekeleza wajibu ahudhurishwe pamoja na unaosisitizwa na Uislamu huu hana budi kuomba watoto wenzake katika katika kumlea mtoto ili msaada wa Mwenyezi kituo cha malezi ya watoto ainukie katika Dini ya Mungu (s.w.) kwa dua (madrasa) ambapo watoto Uislamu, ambayo ndio ambayo Yeye mwenyewe wanalelewa Kiislamu. Dini yake ya asili kama ametufundisha katika Wazazi wa Kiislamu tunavyojifunza katika Quran: hawana budi kujumuika hadithi ifuatayo: Mola wetu! Tupe katika pamoja katika mtaa wao Abu H u r a i r a h wake zetu na watoto wetu na kuhakikisha kuwa amesimulia kuwa Mtume yaburudishayo macho panakuwa na madrasa wa Mwenyezi Mungu Inaendelea Uk. 15 yenye utaratibu mzuri amesema: Hapana mtoto

14 AN-NUUR

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

TRIPOL HALI si shwari nchini Libya baada ya Marekani kupeleka wanajeshi wake 12,000 nchini humo, ambao lengo lao ni kwenda kudhibiti visima vya mafuta na bandari za kistratejia. Maandamano ya wananchi yameendelea huku mji wa Bani Walid, ulioko umbali wa kilomita 170 kutoka mji mkuu Tripoli ukitekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa marehemu Kanali Muammar Gaddafi, mji ambao ulikuwa mmoja wa miji ya mwisho kabisa k u t e k wa n a wa p i n z a n i wa G a d d a f i wa k a t i wa mapinduzi. Kupelekwa askari hao wa Marekani nchini Libya kumeelezwa kuwa kuna m a l e n g o ya k i s i a s a n a kiuchumi, hususan ikitiliwa maanani kwamba tangu awali, majeshi ya nchi za Magharibi yalivamia nchi hiyo kwa shabaha ya kudhibiti maliasili ya mafuta na gesi ya nchi hiyo na si kwa sababu za kibinadamu kama inavyopigiwa debe katika vyombo vya habari vinavyomilikiwa na mataifa ya kibeberu ya Magharibi. Imefahamika kwamba askari hao wa Marekani wamepelekwa katika mji wenye utajiri mkubwa wa m a f u t a wa B r e g a h u k o mashariki mwa Libya. Mji huo ndio wenye visima vikubwa zaidi vya mafuta nchini Libya na bandari yake ni miongoni mwa vituo muhimu zaidi vya kusarisha nje mafuta gha ya Libya. Inaonekana kuwa kuchaguliwa mji wa bandarini wa Brega kama kituo cha majeshi hayo ya Marekani, kumefanyika kwa mahesabu maalumu ikitiliwa maanani umuhimu wake kutokana na utajiri wa mafuta. Viongozi wa serikali ya Washington wamehalalisha uamuzi huo wa kutuma majeshi nchini Libya, kuwa ni kwa shabaha ya kulinda visima vya mafuta na bandari za kusarishia bidhaa hiyo. Hata hivyo ukweli wa mambo ni kinyume kabisa na madai hayo. Moja ya malengo ya hatua hiyo ni kutaka kupata mafuta kwa bei ya chini zaidi kuliko ile ya bidhaa hiyo katika masoko ya kimataifa. Mwaka 2003 hadi 2007 Marekani ilitekeleza mpango kama huo baada ya kuivamia na kuikalia kwa mabavu Iraq, ambapo inapora mafuta ya nchi hiyo kwa kununua pipa moja la mafuta kwa bei ya dola moja tu! Inaonekana kuwa Washington inataka tena kukariri mwenendo huo. Wataalamu wa masuala ya mafuta wanakadiria kwamba akiba ya maliasili ya mafuta ya Libya inakaribia mapipa bilioni 43 na milioni 600, kiwango ambacho ni cha pili kwa ukubwa duniani baada ya akiba ya mafuta ya Saudi Arabia. Ukweli huo ndio unaotegua kitendawili na kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na watu wengi kwamba ni kwa nini nchi za Magharibi, chini ya mwavuli wa majeshi ya NATO, ziliamua kuingia katika vita vyenye gharama k u b wa v ya L i b ya k wa kisingizio cha kuwalinda

Libya kwisha kazi


Wafuasi wa Gadda wapambana na kuuteka Bani Walid Marekani yatuma majeshi Libya Yaweka kambi Mji wenye utajiri wa mafuta, bandari
Hivi karibuni wananchi wa B e n g a z i wa l i va m i a ofisi za NTC mjini humo wakilalamikia kutofikiwa malengo ya mapinduzi yao. Hata hivyo Fauzi Abdul Aal, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya amekanusha habari za wafuasi wa Gadda kuhusika katika matukio ya mji wa Bani Walid na kusema kuwa, kilichotokea mjini humo ni ugomvi baina ya makundi hasimu na hakuna mfuasi yeyote wa Gaddafi au bendera ya kani iliyoonekana ikipepea hewani. Katika mikakati mingine ya mabeberu kunyakua uchumi wa Libya baada ya kuanguka utawala wa Gadda, Waziri M k u u wa I t a l i a M a r i o Monti, tayari ameshazuru L i b ya t a n g u J u m a m o s i iliyopita akiongozana na ujumbe wa ngazi za juu wa wa n a d i p l o m a s i a n a wafanyabiashara wa nchi yake. Monti alitazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake wa Libya Abdurrahim al-Keib. Lengo kuu la safari hiyo limetajwa kuwa ni kuimarisha uhusiano wa masuala ya keshi na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili. Katika safari ya sasa ya Waziri Mkuu wa Italia nchini Libya, Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Italia Eni itatiliana saini na shirika la mafuta la Libya mkataba wenye thamani ya dola milioni 380. Pande hizo mbili pia zitatiliana saini mikataba mingine kadhaa ikiwemo ya k u t o a m a f u n z o k wa jeshi la Libya, kujenga upya kikosi cha polisi cha nchi hiyo, masuala ya uvuvi na forodha. Miongoni mwa ajenda za safari ya Mario Monti huko Libya ni kuhuisha mkataba wa uraki kati ya Roma na Tripoli. Mkataba huo ulitiwa saini mwaka 2008 wakati wa utawala wa Kanali Muammar Gadda. Kwa mujibu wa mkataba huo, Italia inalazimika kuilipa Libya fidia ya dola bilioni tano kutokana na kuifanya koloni nchi hiyo kwa kipindi cha kati ya mwaka 1911 hadi 1947. Fidia hiyo inapaswa kulipwa katika kipindi cha miaka 20. Katika upande wa pili Libya nayo iliahidi kuzuia wahamiaji haramu wanaoelekea Italia kupitia mpaka wa nchi hiyo. Mkataba huo wa urafiki ulisitishwa kwa muda mwaka 2011 baada ya kuanza vita vya ndani nchini Libya. Baada ya kukomeshwa uhusiano wa kikoloni kati ya Italia na Libya kufuatia kumalizika Vita vya Pili vya raia wa nchi hiyo. Yapata mwezi mmoja uliopita, Waziri wa Ulinzi wa Marekani alitembelea Libya na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Mazungumzo hayo yamefanyika katika hali ambayo tangu zama za uongozi wa Rais Thomas Jefferson huko Marekani, hadi kiongozi wa sasa wa nchi hiyo Barack Obama, serikali zote za Marekani zimekuwa katika vita au zikifikiria kuanzisha vita dhidi ya Libya. Hata hivyo tangu kuporomoka kwa utawala wa G a d d a f i , n c h i h i yo kumetayarisha uwanja mzuri wa Marekani kwa ajili ya kulazimisha siasa na sera zake za kiuchumi na kisaisa huko Libya. Marekani ni miongoni mwa nchi chache sana ambazo baada tu ya kufutwa vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ilitangaza kuwa imeachia huru mali na milki zote za Libya isipokuwa katika kesi maalum. Hatua hiyo ilichukuliwa i l i k u t a n g a z a k wa m b a Wa s h i n g t o n i m e f u n g u a ukurasa mpya katika uhusiano wake na Tripoli. Hali inaonyesha kwamba h a k u n a s h a k a k wa m b a Marekani ina ndoto kuhusu Libya. Kupelekwa maelfu ya majeshi ya Marekani nchini Libya, tena katika mji wenye visima vya mafuta na bandari za kusafirishia mafuta za nchi hiyo, kumeweka wazi ramani ya njama ya Marekani kuhusu Libya mpya. Hata hivyo kuna taarifa kwamba kiongozi wa wa n a m a p i n d u z i wa Libya, Abdullah Nakir, amelitahadharisha Baraza la Taifa la Mpito la nchi hiyo na kusema kuwa uingiliaji wa aina yoyote wa Marekani katika masuala ya ndani ya Libya, utawafanya askari wa Marekani waliopo nchini humo wakabiliwe na moto wa Jahannam kuliko ule wa Iraq. Wakati hali ikiwa hivyo, serikali kwa upande wake imeshindwa kupitisha sheria mpya ya uchaguzi nchini humo. Abdur Razzaq al Iradi, mjumbe mwandamizi wa Baraza la Mpito la Libya amenukuliwa na mtandao wa al Arab Online akisema kuwa, kazi ya kutunga sheria ya uchaguzi Libya imeahirishwa kwa wiki moja nyingine. Wa k a t i h u o h u o wanachuo wanaokia 4,000 wameandamana mjini Benghazi, wakitaka wanachuo wenzao waachiliwe huru baada ya kutiwa mbaroni kufuatia kushiriki kwenye maandamano ya kupinga Baraza la Mpito la Libya NTC. Dunia, Italia ilikuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Libya. Serikali ya Roma inanunua sehemu kubwa ya mahitaji yake ya mafuta kutoka kwa koloni lake la zamani na shirika la mafuta la Italia Eni ndio muwekezaji mkubwa zaidi katika sekta ya mafuta ya Libya. Uhusiano wa pande hizo mbili ulidorora kwa kiwango kikubwa wakati wa vita vya ndani vya Libya kutokana na hatua ya Italia ya kuruhusu ndege za keshi za shirika la NATO kutumia vituo vyake kwa ajili ya kufanya mashambulizi dhidi

Habari
ya utawala wa Muammar Gaddafi. Uhusiano huo u l i h u i s h wa t e n a b a a d a ya k u u a wa G a d d a f i n a kuhitimishwa utawala wake uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya miongo minne. Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti, amekwenda Libya wakati ambao serikali yake inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi. Italia ambayo inahesabiwa kuwa nguvu kubwa ya tatu ya kiuchumi katika eneo la Euro, inadaiwa deni la Euro bilioni 1900. Hata Taasisi ya Viwango ya Standard and Poors ilishusha chini daraja la ubabe wa kiuchumi la Italia. Monti ambaye alishika madaraka nchini Italia baada ya kujiuzulu Silvio Berlusconi, anafanya jitihada za kukarabati uchumi ulioathirika wa nchi hiyo kwa kutekeleza sera za kubana matumizi na kupanua zaidi ushirikiano wake na nchi za kigeni ili kuhuisha uchumi wa nchi hiyo. Kwa msingi huo safari ya Mario Monti Libya inapewa umuhimu mkubwa na viongozi wa serikali ya Roma.

Saad wa Ikhwanul Muslimin Spika Bunge jipya la Misri


CAIRO SAAD Katatni wa chama cha Kiislamu cha Ikhwanul Muslimiin, amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge jipya la Misri, hatua ambayo imeelezwa kuwa ni ya kihistoria katika siasa za nchi hiyo. Katatni alipata kura 399 kati ya kura 496 zilizopigwa bungeni ikiwa zimesalia siku mbili tu, kufikia maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu kuanza harakati za mapinduzi ya wananchi nchini Misri Januari 25 mwaka jana. Bunge jipya la Misri limeanza shughuli zake Jumatatu wiki hii, ikiwa ni kikao cha kwanza cha Bunge hilo tangu utawala wa Hosni Mubarak kuangushwa takribani mwaka mmoja uliopita. Chama cha Ikhwanul Muslimin, ndicho chama kilichojipatia viti vingi k a t i k a b u n g e j i p ya l a Misri kufuatia kufanyika uchaguzi wa kwanza huru

Msaada wa Ujenzi wa Msikiti

nchini humo. Chama hicho kimepata asilimia 47.18 ya viti bungeni. Chama cha Uhuru na Uadilifu (FJP) ambacho ni tawi la kisiasa la Ikhwanul Muslimiin, kimeshinda viti 235 vya Bunge, sawa na asilimia 47.18 ya kura zilizopigwa katika duru zote tatu za uchaguzi wa Bunge. Awali Ikhwanul Muslimiin kilikuwa kimepigwa marufuku nchini humo wa k a t i wa u t a wa l a wa Hosni Mubarak, lakini hilo halikupunguza umashuhuri wa chama hicho miongoni mwa wananchi wa Misri. Kwa miezi kadhaa sasa wananchi wa M i s r i wa m e e n d e l e a n a maandamano yao wakilitaka baraza la keshi linaloshikilia madaraka nchini humo, kukabidhi uongozi mikononi mwa wananchi ambapo wananchi hao wanalituhumu baraza hilo kwa kukwamisha kufikiwa malengo ya mapinduzi ya wananchi katika Taifa hilo.

UONGOZI wa Msikiti wa Nangando, Liwale mkoani Lindi chini ya Imamu Sheikh Abeid Makokora wanaomba msaada kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Msikiti. Msaada unaohitajika ni pesa taslimu, vifaa vya ujenzi, ikiwamo simenti, nondo na mchanga ili kufanikisha ujenzi wa Msikiti huo. Uongozi unawaomba Waislamu kujitolea kwa ajili ya Allah katika kuwekeza kwenye mambo ya kheri na swadaka yenye kundelea. Ukitoa kwa ajili ya Allah hupotezi, unajiwekea akiba yako ya kesho Akhera. Changia kupitia A/C ya Al Jihadil Masjid Na. 703200486 NMB au unaweza kuchangia kwa kutumia Tigo pesa au kupiga kwa namba hiyo hiyo 0718 414850. IMAMU

Makala
Inatoka Uk. 13

RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

AN-NUUR

15

(yetu) (nyoyo zetu), na utujaalie kuwa waongozi wa wamchao (Mungu). (25:74). Na tumemuusia mwadamu afanye mema kwa wazazi wake, mama yake amechukua mimba yake kwa taabu na akamzaa kwa taabu, na kubeba mimba yake hata kumwachisha ziwa; (uchache wake) ni miezi thalathini. Hata anapokia balehe yake na akawa mwenye umri wa miaka arubaini, ( mtoto mwema) Husema, Ee Mola wangu! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na niwezeshe nifanye vitendo vizuri unavyovipenda, na unitengenezee watoto wangu; kwa yakini n i n a t u b u k wa k o ; n a hakika mimi ni miongoni mwa waliosilimu (walionyenyekea). (46:15). Wa t o t o we t u wanapokuwa wakubwa tuwaozeshe mapema kwa wanaume au wanawake wenye mwenendo na tabia ya Kiislamu na daima tusiache kuwapa nasaha njema. Hebu turejee Quran tuone nasaha ya Luqman kwa mwanawe: Na (wakumbushe) Luqman alipomwambia mwanawe; na hali ya kuwa anampa nasaha. Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu, maana kushirikisha ndiyo dhulma kubwa. Ewe mwanagu! Kwa

Wajibu wa wazazi kwa watoto


hakika jambo lolote l i j a p o k u wa n a u z i t o wa chembe ya hardali, likawa ndani ya jabali au mbinguni, au katika ardhi, Mwenyezi Mungu atalileta (ampe anayehusika) bila shaka Mwenyezi Mungu ni Latifu (Mpole), Mjuzi wa kila jambo. Ewe Mwanangu! S i m a m i s h a s wa l a , n a uamrishe mema, na ukataze mabaya, na usubiri juu ya yale yatakayokusibu. Hakika hayo ni katika mambo yanayostahiki k u a z i m i wa . Wa l a usiwatazame (watu kwa jeuri) kwa upande mmoja wa uso, wala usiende katika ardhi kwa maringo; hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunae, ajifaharishaye. Na ushike mwenendo wa katikati, na uteremshe sauti yako, bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote (mbele ya Mwenyezi Mungu s.w.). Jambo jengine muhimu kwa wazazi katika kuwalea watoto wao ni kuwa na upendo na huruma juu yao. Ukali wa kupindukia na ukaripiaji wa mara kwa mara watoto si malezi mazuri na kamwe mtoto haleleki vyema katika mazingira kama hayo, Mtume (s.a.w.) aliye kiigizo chetu pekee, alikuwa ni mlezi mwema mno. Alikuwa na huruma na upendo mkubwa mno kwa watoto wake na wajukuu zake kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo: Ay s h a ( r. a . ) amesimulia: Sijamuona mtu aliyeshabihiana kitabia na mwenendo na Mtume (s.a.w.) kuliko Fatma. Alipokuja kwa Mtume, Mtume (s.a.w.) alimsimamia, kisha alimchukua kwa mkono wake na kumbusu na kisha kumkalisha karibu yake. Na Mtume (s.a.w.) alipokwenda kwake, Fatma alikuwa akimsimamia, k i s h a a k i m t wa a k wa mkono wake na kumbusu, na kumkalisha karibu naye. (Abu Daud). P i a M t u m e ( s . a . w. ) amesisitiza kuwapenda na kuwahurumia watoto kwa kuwabusu kama hadithi zifuatazo zinavyotufahamisha: Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa mwenyezi Mungu alimbusu mjukuu wake, Hassan bin Ali, mbele ya Aqra bin Habis ambaye alisema: Nina watoto kumi na sambusu hata mmoja wao. Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwangalia na kusema: Yule asiye na huruma hatahurumiwa. (Bukhari na Muslim). Aysha (r.a.) ameeleza kuwa Mwarabu wa jangwani (Bedui) alikuja k wa M t u m e ( s . a . w. ) , akasema: Nini! Unabusu watoto? Sisi hatuwabusu. Mtume (s.a.w.) akasema: S i n a l a k u wa s a i d i a , kwani Mwenyezi Mungu (s.w.) ameondoa huruma nyoyoni mwenu. (Bukhari na Muslim). Hadithi hizi mbili

zinatusisitiza tuwalee watoto wetu kwa huruma na upendo. Kuwabusu watoto ni kielelezo cha upendo wetu kwao. Pamoja na kuwalea watoto wetu ipasavyo, hatuna budi kuchunga mipaka ya Mwenyezi M u n g u ( s . w. ) k a t i k a kufanya kazi hiyo. Huruma na upendo kwa wa t o t o w e t u k a m w e kusitupelekee kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (s.w.) na Mtume wake. Muislamu anatakiwa ampende Mwenyezi Mungu (s.w.) na Mtume wake kuliko hata anavyoipenda nafsi ya k e , s e m b u s e n a f s i nyingine. Mara nyingine, baadhi ya wazazi, kwa ajili ya kuwapenda na kuwahurumia watoto wao, huwaachia huru kwenda kinyume na maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu (s.w.) ili kuwaridhisha watoto wao hili ni kinyume na mafundisho ya Mtume (s.a.w). Aidha Katika harakati za kuchuma mali husahau jukumu la kuwalea watoto wao. Kuhusu jambo hili Waislamu hawana budi kila mara kukumbuka n a s a h a ya M we n ye z i Mungu (s.w.) katika aya zifuatazo: Enyi mlioamini! Yasikusahaulisheni mali yenu wala watoto wenu kumkumbuka Mwenyezi Mungu! Na wafanyayo hayo, hao ndio wenye kuhasirika. (63:9).

Enyi mlioamini! Kwa yakini baadhi ya wake zenu na watoto wenu ni maadui zenu, basi jihadharini nao... (64:14). Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni mtihani. Na kwa Mwenyezi Mungu kuna ujira mkubwa kabisa. (64:15). Mali na watoto ni p a m b o l a m a i s h a ya dunia. Na vitendo vizuri vibakiavyo ndivyo bora mbele ya Mola wako kwa malipo na tumaini bora (kuliko hayo mali na watoto). (18:46). Aya hizi kwa ujumla zinatukumbusha kuwa pamoja na kuwapenda na kuwahurumia wake zetu na watoto wetu na pamoja na kuipenda mali na vyote vingine vinavyopendeka, hatuna budi kuhakikisha kuwa upendo wetu juu ya Mwenyezi Mungu (s.w.) na Mtume wake unakuwa juu ya kitu chochote kile kama Mwenyezi Mungu (s.w.) anavyotutanabahisha tena katika aya zifuatazo: Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi (vyenu) ikiwa wanastahabu (wanapenda) ukari kuliko Uislamu. Na katika nyinyi atakayewafanya hao kuwa ndio vipenzi vyake, basi hao ndio madhalimu. Jambo lingine muhimu la kuzingatia zaidi katika kuwalea watoto ni kutokuwa na upendeleo au ubaguzi kati ya watoto. Wazazi wanawajibika sawa kwa watoto wao wote na kila mtoto anahaki sawa na mwingine katika kupendwa, kuthaminiwa na kuhurumiwa na wazazi wake.

Waandalizi Mihadhara wa Masjid Qiblatein wanawaalika Waislamu wote kuhudhuria Mihadhara ya kumbukumbu ya Mazazi ya Mtume Muhammad ( S.a.w) katika Misikiti Mbalimbali mkoani DSM chini ya uenyekiti wa Maalimu Sheikh Ali Basalleh, kila siku Baada ya Sala ya Magharib kwa Mpango ufuatao.
Siku Ijumaa Tarehe 27/01/2012 Msikiti Lindi Mtambani- kinondoni Istiqama- Ilala Boma Ibadhi Mjini Mtoro Mtoro Makonde Madina Ndugumbi Magomeni - Kondoa Islaah Kigogo kati Idrisa Idrisa Idrisa Mada Fadhila za Kutoa Sababu za mfumuko wa Bei na mafundisho ya mtume Muhammad s.a.w kupambana na mfumko wa bei Mtume (s.a.w) na mafanikio Mtume ambaye ni rehema Mimi nimetumwa kuwa Mwalim Jina la mtume s.a.w katika Kur-an na madhumuni yake Mtume Muhammad na mwongozo wa Umma Wajibu na Msingi ya Daawa Mimi ni mwito wa Baba yangu Ibrahim na Bushra ya ndugu yangu Issa E unajuwa nafasi ya Mtume Muhammad s.a.w katika kukia lengo la kuumbwa kwako? Utamaduni wa Kiislam Kumfuata mtume Muhammad s.a.w ni kielelezo cha kumpenda yeye Hukmu ya Eda ya Kupotelewa na Mume Mhadhiri Sheikh Musa Ngala Sheikh Ramadhani Kwangaya Sheikh Walidy Alhadi Omar Sheikh Ibrahim Ghulam Sheikh Nassor Moh`d Majid Sheikh Suleiman Amran Kilemile Sheikh Musa Kundecha Sheikh Abdala Mohamed Sheikh Muutamid Juma Sheikh Yusuf Salim Sheikh Mohamed Issa Sheikh Taha Suleiman Bane Sheikh Hashim Ahmad Rusaganya

Mihadhara

Jumamosi 28/01/2012 Jumapili Jumatatu Jumanne Jumatano Alhamis Ijumaa Jumapili Jumatatu Jumanne Jumatano 29/01/2012 30/01/2012 31/01/2012 01/02/2012 02/02/2012 03/02/2012 05/02/2012 06/02/2012 07/02/2012 08/02/2012

Jumamosi 04/02/2012

16 AN-NUUR

16

Bassaleh awahimiza wanafunzi Waislamu kusoma kwa juhudi


Bi Asha Sururu ataka wazazi wasimamie maadili, Hijab
Na Bakari Mwakangwale

AN-NUUR
RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012 RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA JANUARI 27 - FEB. 2, 2012

USIKOSE KUSOMA AN-NUUR KILA IJUMAA

MAALIM Ally Bassaleh amewataka wanafunzi Waislamu kusoma kwa bidii kwani hiyo ndiyo amri ya Uislamu. Aidha, amesema kuwa kusoma hakuna mwisho na kila mtu anavyosoma ndio anatakiwa kuweka m i p a n g o ya k u s o m a zaidi. Maalim Bassaleh ametoa nasaha hizo katika mahafali ya wanafunzi Wa i s l a m u w a s h u l e ya B e n j a m i n M k a p a wanaomaliza kidato cha sita. Mbali ya kuwapongeza kwa juhudi zao za kusimamia Uislamu shuleni hapo, mgeni rasmi katika mahafali hayo, Maalim Ally Bassaleh, aliwahimiza kujiendeleza kielimu zaidi wamalizapo hapo. Alisema, Muislamu siku zote anatakiwa awe ni mwenye kusoma, kutokana na kuwa kwa Waislamu suala la kusoma huanza tokea utotoni mpaka unapofikwa na umauti. Alisema, asiwe mmoja miongoni mwao (wahitimu hao) akawa na mawazo kuwa elimu aliyopata ya kidato cha sita ndio amemaliza, na kumfanya asitake tena kusoma au kujiendeleza kwa chochote kitaaluma, huo alidai utakuwa ni ujinga. A k i wa n a s i h i h u k u akimnukuu Imam AlGhazali, Maalim Bassaleh, a l i s e m a k wa m u j i b u wa mwanazuoni huyo anaeleza kwamba yule aliyesoma na amejua kwamba amesoma lakini, ikiwa ameleta mawazo kwamba sasa amemaliza na hakuna tena cha kusoma na wala hakuna

Bi Aisha Sururu akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu watarajiwa wa kidato cha Sita katika mahafali ya wanafunzi Waislamu wa shule ya Benjamin Mkapa mwishoni mwa wiki. wazazi husika. mwanadaamu. wa kumsomesha, anasema Alisema, kumekuwa Wa i s l a m u w a l i p o (Imam Ghazal), kama shikamana na kitabu chao na kero nyingi za vazi la ujinga ni nyumba basi waliweza kupata na kuleta Hijab mashuleni, lakini ndiyo kwanza anafungua maendeleo katika nyanja ikiwa wazazi hawana mlango kuingia ujingani. Nyinyi mnaomaliza ya sayansi katika zama msimamo wa kisawasawa hapa leo kidato cha sita, kuchukizwa hizo. Mengi ya kisayansi n a ni wazi mlianza safari yanayovuma nakusikika n a u n y a n y a s a j i yenu ya masomo nasari leo yameanzishwa na wanaofanyiwa mabinti (chekechea), kisha Wa i s l a m u . A l i s e m a w a o w a t a e n d e l e a mkaingia msingi (shule k u c h e z e wa n a k u t o a Maalim Bassaleh. ya msingi) mkamaliza Kwa upande wake, Bi. m w a n y a k w a w a l e kidato cha nne na sasa Aisha Sururu, aliwataka wa c h u k i a o va z i h i l o kidato cha sita, muelewe wa z a z i wa K i i s l a m u k u wa n ya n ya m a b i n t i hapa bado hamjamaliza, kusimamia vazi la Hijab watakavyo. Uislamu ni elimu siku Ikitokea kadhia ya kwa mabinti wao, kuanzia zote ujione bado unahitaji H i j a b u wa z a z i w o t e nyumbani mpaka shuleni, elimu. Alisema Maalim k w a k u w a e l i m i s h a tusimame kidete kupinga Bassaleh. umuhimu wa stara kwa d h u l m a h i i , v i t a h i i Aliwataka wahitimu hao mwanamke. tutashinda ikiwa tu wazazi kushikamana na Qur ana A l i s e m a , w a z a z i watakuwa mstari wa katika safari yao ya kutafua kama hawatakuwa na mbele kusimamia vazi la elimu kwani alisema, msimamo hata watoto stara toka majumbani hadi kila watakachokisoma nao watapuuza vazi hilo, shuleni. Wazazi hakuna kipya kwao Qur an ilisha jambo ambalo halitakuwa kumruhusu mtoto kwenda kielezea kwa mapana na maana wanapotokea shuleni mpaka amevaa siku nyingi, kwani Qur watu wengine kutetea na Hab ya kisawasawa, sio an haijaacha kitu katika kusimamia vazi hilo nje ya ilimradi habu. Alisema mfumo wa maisha ya

Bi. Sururu. K wa u p a n d e wa o , wanafunzi wa Kiislamu katika Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa ya Jijini Dar es Salaam, wamewataka wadau wa Dini ya Kiislamu kuwakwamua kiuchumi katika mikakati yao ya kuanzisha mradi maalum ili kuongeza akiba na kipato cha Jumuiya yao Shuleni hapo. Vijana hao wametoa o m b i h i l o k wa j a m i i ya Wa i s l a m u k a t i k a mahafali ya kuwaaga na kuwaombea dua wanajumuiya wanafunzi wa Kiislamu wa kidato cha sita, mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya shule hiyo. A k i s o m a r i s a l a ya wanajumuiya hao, mmoja wa viongozi wa jumuiya hiyo alisema, ili kufikia malengo na kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo shuleni hapo, ni vyema wakawa na mradi wao ambao utawaongezea kipato na kuweza kukakabiliana na changamoto hizo. Alisema, Jumuiya yao i p o m i k o n o n i m wa o h a d i s a s a k wa k u wa hawana mdhamini h i v y o wa n a l a z i m i k a kuchangishana ili kuweza kusaidiana katika matatizo mbalimbali yanayowakumba vijana wa Kiislamu wakiwa shuleni. Alisema, wamebuni mradi wa steshenari, ambao kuanza kwake kazi utakua ni ukombozi wa kiuchumi na kuwaepusha na kuomba misaada ya k u t a t u a m a t a t i z o yao madogomado yanayowakabili. Wanafuzi wa kidato cha sita kote nchini wanatarajiwa kufanya mtihani wao wa kumaliza elimu ya juu ya sekondari (A level) ikapo Februari 8, mwaka huu.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like