You are on page 1of 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Maaskofu, Serikali watavuruga nchi


Ngoma wanayocheza itatupeleka Kenya Porojo, Propaganda, haiwezi kuleta amani Kiporo cha NECTA, MoU, Mfumokristo bado

ISSN 0856 - 3861 Na. 1051 SAFAR 1434, IJUMAA DES. 28, 2012 - JAN 3, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Madabida atoa changamoto kwa TAMPRO Uk. 3

Wanaomtusi Amani Karume hawaijui siasa ya Zanzibar


Na Ibn Mohammed

Rais mstaafu Amani Abeid Karume.

EFATHA waendelea kuvunja kiwanda cha AFRO PLUS

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Kardinali Polycarp Pengo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wenzake.

Mlinzi akamatwa na kufungwa pingu, kitambaa machoni

HOJA ya kupinga GNU, kumkejeli Rais mstaafu Karume, inapata nguvu wapi ikiwa Gulam na Kermali walizika tofauti zao na kushirikiana katika shughuli ya arusi? Tukae tukijua kuwa jahazi la wapinga mabadiliko linakumbwa na

misukosuko ya bahari. Upepo wa Kaskazi unavuma sijui kama watapona maana tanga lao bovu, foromali chakavu huku hali ya bahari ikichafuka. Na sijui kama papa wenye njaa wanaoranda randa katika upwa wa kisiwa chao kama watawaacha. (Soma Uk. 6, 7)

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Tangazo SAFAR 1434, IJUMAA


AN-NUUR
busara haikutumika, itakuwa ndio mwisho wa amani na utulivu katika nchi. Na mifano hai ipo. Ni kutoka na ukweli huo na kutokana na uzalendo wao, Waislamu wamekuwa wakitahadharisha juu ya dhulma na ubaguzi uliopo nchini kwa misingi ya dini. Kwa kutekeleza wajibu wao katika nchi hii, wameandika na kukusanya takwimu na vielelezo vya kutosha juu ya dhulma iliyopo. Isitoshe, wamechukua taabu ya kupita nchi nzima kufanya makongamano kuzungumzia hatari ya mfumokristo ambao ndio unaoendeleza dhulma nchini, ukiwapendelea Wakristo na kuwahujumu Wa i s l a m u . Yo t e h a y a yamefanyika kwa matarajio kwamba ile dhulma iliyopo itaonekana na jamii kwa ujumla itaona mantiki na ulazima wa kuchukua hatua ya kuondoa ubaguzi na dhulma iliyopo. H a t a h i v y o , inavyoonekana imekuwa kana kwamba yale yaliyosemwa katika makongamano yale yameangukia sikio la uziwi maana watu wanaendelea na kupiga porojo na propaganda zilezile. Labda tuchukue tena fursa hii kuwataka viongozi wa serikali, viongozi wa makanisa na wale wote wanaoendelea kupiga porojo za Tanzania hakuna mfumokristo wachukue kanda za makongamano yaliyofanyika nchi nzima. Humo watakuta hoja za Waislamu, ushahidi, vielelezo na ainisho la mfumokristo na jinsi unavyofanya kazi. Hata hivyo itabidi wanunue CD/ DVD za makongamano hayo kwa sababu Waislamu wamezigharamia. Kinachosisitizwa katika CD hizo ni kuwa mfumokristo upo na ndio uliowabagua na unaoendelea kuwabagua Waislamu katika fursa mbalimbali. Ndio uliosababisha hii leo serikali na taasisi zake za uongozi na utendaji kwa asilimia zaidi ya 80 kushikiliwa na Wakristo. Ndio uliozaa MoU, kupigwa

DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013

AN-NUUR

MAONI YETU

TUNAMALIZA mwaka wa 2012 tukiwa na maswali ambayo bado kupatiwa majibu. Tumekuwa tukijiuliza, ngoma gani inachezwa katika nchi hii? Je, ni ile iliyoitumbukiza Somalia katika janga la vita vya wenyewe kwa wenyewe? Je, ni ile iliyowakokota Kenya mpaka hivi sasa imekuwa kulipuka mabomu, kurushwa maguruneti na kuuwa watu wasio na hatia, linaelekea kuwa sehemu ya maisha ya Wakenya? Inavyoelekea ni kuwa ile hali iliyopo Kenya hivi sasa au ile iliyopo Pakistan na Yemen, wapo watu wanaitamani sana. Ila tu kwa bahati mbaya wamekuwa kama wale watu wanaokimbilia boti inayozama wakati waliomo ndani wakitaharuki kutaka kujinasua kuokoa maisha yao. Uwongo na Propaganda iliyojengwa katika nchi hii ukaonekana kama kweli, ni kuwa nchi hii na serikali yake haina dini ila wananchi wake wana dini. Inaelezwa na wanasiasa kuwa katika uongozi na utendaji ndani ya serikali, suala la dini halitizamwi. Kwa maana kuwa hakuna mtu atakayeteuliwa kushika nafasi fulani kwa kuangalia dini yake na vivyo hivyo kwamba watendaji wa serikali na taasisi za umma hawafanyi kazi zao kwa upendeleo. Hapendelewi wala kubaguliwa Muislamu au Mkristo. Haya ndiyo yamekuwa yakisemwa toka nchi hii ipate uhuru. Ti z a m a M a w a z i r i wapo wangapi kwa

Maaskofu, Serikali watavuruga nchi

dini zao, Makatibu Wakuu, Makamishna na Wakurugenzi katika vitengo mbalimbali wapo wangapi kwa dini zao. Tizama Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Tarafa na Watendai wa Serikali za Mitaa. Tizama pia watendaji katika Wizara wapo wangapi kwa dini zao. Utafiti mdogo utakuonyesha kuwa Wakristo wanahodhi nafasi hizo kwa zaidi ya asilimia 80. Katika hali hiyo wanachoambiwa Waislamu waamini ni kuwa watendaji hao hawakuteuliwa kwa kuangalia Ukristo wao, lakini pia waamini na kuridhika kuwa watendaji hao wanaohodhi serikali kwa asilimia 80, katika kufanya kazi kwao hawatafanya upendeleo wala ubaguzi! Hata hivyo matukio kama lile la mwanafunzi Kopa Abdallah aliyekuwa akiongoza darasani kwake na katika Kata na Tarafa kukatwa jina lake kwenda sekondari na nafasi yake kupewa Antony Samirani, ni ushahidi kuwa watendaji hao hawatendi haki. Kutokana na utafiti na ukweli uliokusanywa kwa muda mrefu, madai yote hayo yameonekana kuwa ni uwongo na propaganda tupu. Na kwamba propaganda hii inazidi kukolezwa ili kuendeleza ubaguzi, hujuma na dhulma dhidi ya Waislamu. Ni ukweli usiopingika kuwa kila penye dhulma na ubaguzi, hapawezi kuwa na amani ya kudumu. Ipo siku wanaodhulumiwa watakuja juu na kama

marufuku EAMWS na k u n a u b a g u z i , k u n a kuanzishwa BAKWATA, mfumokristo, badala ya kufutwa Mahkama ya kuwataka watoe ushahidi Kadhi, kuzuiya Tanzania uangaliwe kama madai kujiunga na OIC huku hayo ni kweli, yanaibuka k u k i w a n a U b a l o z i madai ya kuwasingizia wa Vatican, Mauwaji Wa i s l a m u u o v u n a y a M w e m b e c h a i n a kuwapaka matope. kuwepo kwa Kamati Iliwahi kutangazwa y a K u t u n u k u n d a n i katika moja ya siku kuu za ya Baraza la Mitihani Krismazi zilizopita kwamba ambayo inatuhumiwa Jeshi la Polisi litaimarisha kufanya kazi ya kuzifanya ulinzi kulinda makanisa, baadhi ya shule kutesa kisa ulizambazwa urongo kila mwaka na nyingine k u w a k u n a Wa i s l a m u kuteseka. siasa kali wanataka

Ni kwa sababu ya mfumokristo, yale madai mazito ya Waislamu juu ya utendaji ndani ya Baraza la Mitihani kwamba limekuwa kama Parokia, yamekuwa yakipuuzwa na kuacha Baraza hilo na Kamati yake ya kutunuku likiendelea kufanya kazi katika mazingira na taratibu tata zisizofuata kanuni za kisomi, kitaaluma na kitaalamu katika masuala ya mitihani. Kama ilivyo kwa zile porojo za mtoto wa shule ya msingi kuwashinda nguvu na ujanja walinzi wa ubalozi mmoja wa nchi kubwa na kupenya ngome yao ya ulinzi; badala ya serikali kutizama madai haya ya Waislamu na kufanya uchunguzi kubaini ukweli na kuchukua hatua, imekuwa ikija na mikakati mingine kabisa ambayo kila ukitizama ni kana kwamba ina hamu kuona Tanzania inatumbukia ilikozama Kenya.

iwapo kutakuwa na haki na usawa. Kila mwananchi akaona na kuridhika kuwa serikali inatenda haki. Hakuna Waislamu wanasema ubaguzi wala dhulma.

kushambulia Wakristo. Labda tuulize, hivi Wakristo wanapatikana makanisani tu? Je, jeshi la Polisi litasambaza pia askari wa kuwalinda Wakristo mitaani ambapo Waislamu na Wakristo wamepanga vyumba katika nyumba moja? Tufupishe maoni yetu kwa kusema kuwa mwaka wa 2012 unamalizika na kuingia 2013 na kiporo cha madai ya Waislamu juu ya NECTA, MoU, Mahkama ya Kadhi, OIC na Mfumokristo kwa ujumla. Tusisitize kuwa propaganda za wanasiasa na maaskofu pamoja na zinazodaiwa kuwa dua za kuombea amani nchi, hazitaleta amani na umoja wa kitaifa. Amani ya kweli na ya kudumu, itaku wepo tu

Masjid Muzdalifa Mbezi kwa Yusufu inawashukuru waislamu wote waliofanikisha ujenzi wa msikiti kufikia mahala hapa ulipokia. Lakini pamoja na shukrani hizo bado tunaomba msada kwa waislamu wenye moyo wa kujitolea waendelee kutusaidia ili tukamilishe ulipobakia kwa uwezo wa Allah Inshaalah. Kwa yeyote mwenye kutaka kuchangia chochote ulicho nacho wasiliana nasi kwa namba hizi 0717 649313/ 0713 673216/ 0715 874127 au 0657 531367 au unaweza kuka katika msikitini.

3
Na Shaaban Rajab PAMOJA na kuwepo zuio la mahakama na kesi ikiwa bado ipo mahakamani, waumini wa Kanisa la EFATHA la Mwenge jijini Dar es Salaam wameendelea kukivunja na kuharibu mali za kiwanda cha uchapishaji cha AFRO PLUS kilichopo Mwenge, jirani na kanisa hilo jijini Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa siku ya Jumanne ya Desemba 25, ambayo ilikuwa ni siku ya Sikukuu ya Wakristo ya Christmas, walinzi wa Kanisa hilo walimkamata mlinzi wa kiwanda hicho Bw. Salum Ibrahim, ambaye ni mwajiriwa wa kampuni ya ulinzi ya Kwanza Security na kumnyanganya silaha yake na simu yake ya mkononi, hatimaye walimfunga pingu na kitambaa mdomoni na baadae waliwaamuru waumini wa Kanisa hilo kuvunja kiwanda hicho. Taarifa zimesema kuwa waumini hao waliendelea na kazi hiyo ya kuvunja kiwanda hicho hadi majira ya saa kumi jioni, ambapo ndipo walinzi hao wa EFATHA walipomfungua pingu na kitambaa mlinzi Ibrahim. Baada ya mlinzi huyo kufunguliwa alitoa taarifa Kwa wenzake, ambao walika eneo la tukio na kukuta uharibifu mkubwa umefanyika kiwandani hapo. Kufuatia uhalifu huo, walinzi hao waliamua kwenda kituo kidogo cha polisi Mwenge, kutoa taarifa za juu

Habari
s

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013

AN-NUUR

Na Bakari Mwakangwale

Madabida atoa changamoto kwa TAMPRO


inakuwa rahisi kuwatambua na kuwasaidia. Aliunga mkono mpango na mikakati ya TAMPRO ya kuwakusanya na kuwalea watoto wenye vipaji maalum, jambo ambalo alisema linapaswa kuungwa mkono, na Taasisi zingine, lakini pia aliwataka, kutupia macho na wale vijana wasio na vipaji maalum lakini wanajitambua. Kwa upande mwingine, mshikamano miongoni mwa Taasisi na Jumiya za Kiislamu nchini, umeleezwa kuwa ndiyo njia pekee ambayo italeta tija na maendeleo miongoni mwa jamii ya Kiislamu. Hayo yamebainishwa na waongeaji mbalimbali katika Mkutano Mkuu huo wa Wanachama wa Jumiya ya Wataalum wa Kiislamu nchini (TAMPRO) mwishoni mwa wiki iliyopita, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, Ilala Jijini Dar es Salaam. Akichangia katika Mkutano huo, Amiri wa Baraza Kuu la Jumiya na Taasisi za Kiislamu (T), Alhj Mussa Kundecha aliasa kwamba, kila Taasisi ikibaki inaamini kwamba inaweza kufanya kazi yake vizuri ikiwa yenyewe, si kra sahihi. A l i s e m a , Wa i s l a m u wakiweza kufanya mashirikiano mazuri na Taasisi walizonazo wanaweza kutumia nguvu kazi zilizopo kwa namna nzuri lakini pia kutatuna matatizo ya msingi yanayoonekana kuwa ni matatizo makubwa katika jamii ya Waislamu. Kundecha amesema, kwa ushirikianao mzuri na Tampro, wao kama Baraza Kuu la Jumiya na Taasisi, waliweza kukidhi mahitaji ya elimu, na ilikuwa ni tija nzuri ya mashirikianao kati ya jumuiya ya wanataaluma wa Kiislmu na taasisi nyingine katika kuyaendea mambo ya Waislamu. Alisema, awali utamaduni wa kuwa na shule za awali kwa waislamu ulikuwa haupo na kuonekana ni kitu kigumu, lakini alidai kwa ushauri wa wanatampro, kupitia Shura ya Maimamu, kama ufunguo wa kuingilia Misikitini, ilileta tija na matunda yake yanaonekana,

walinzi hao walikwenda kituo cha polisi Oysterbay, ambako walionana na RCO. Baada ya kutoa maelezo juu ya tukio hilo, waliongozana na RCO huyo na askari wengine kwenda eneo la tukio. Hata hivyo baada ya kuka Afro Plus, walinzi wa Efatha walikataa kufungua lango la kuingilia. RCO, askari wake na walinzi wa Kwanza Security walirejea kituoni Oysterbay. Kesho yake siku ya Jumatano Desemba 26, 20012, OCD wa Kinondoni na OCCID walirudi tena Apro Plus, lakini kama ilivyokuwa awali, walinzi wa Efatha walikataa kufungua geti. Kufuatia hali hiyo, OCD na OC-CID walishauriana na baadae wakasema hawataweza kuvamia na kuwakamata walinzi hao wa Efatha kwasababu wanaogopa kupoteza ajira zao. Wa l i b a i n i s h a k u w a katika tukio la awali ambalo waliwavamia wahalifu hao na kuwakamata, walikaripiwa kwa kuingia nyumba ya ibada na kupiga mabomu. BAADHI ya mashine za kiwanda cha AFROPLUS zilizoharibiwa na waumini wa Kanisa Hata hivyo walinzi hao siku la EFATHA, Mwenge jijini Dar es Salaam. hiyo ya Jumatano mchana, ya tukio hilo. hao wakianza kutoa maelezo Mlinzi mmoja alibainisha walifanikiwa kufungua jalada ata hivyo polisi wa zamu yao kwa askari aliyekuwa kuwa hata baada ya kuingia kituo cha polisi Oysterbay. aliyekuwepo kituoni hapo mezani, askari mwingine katika chumba hicho, askari Aidha kuna taarifa kuwa alidai kuwa hawezi kupokea aliyekuwa pembeni akisikiliza waliyemkuta aliwaambia licha ya kusuasua, polisi maelezo juu ya tukio hilo na alisiwasimamisha walinzi hao kuwa mwenye mali ndiye wamechukua maelezo ya kuwaelekeza kwenda kituo kutoa maelezo na kuwaamuru anayetakiwa kutoa maelezo kuharibiwa mali za kiwanda cha polisi Mabatini. waingie chumba kingine yake na si wao. hicho cha Afro Plus. Hata hivyo wakati walinzi wakazungumze zaidi. Kutokana na hali hiyo,

EFATHA waendelea kuvunja kiwanda cha AFRO PLUS

Mlinzi akamatwa na kufungwa pingu, kitambaa machoni

ALHAJ Ramadhani Madabida ametoa wito kwa TAMPRO na taasisi za Kiislamu kwa ujumla kujishughulisha na mambo yanayoigusa jamii ikiwa ni njia pekee ya kupata uhalali wa kuwepo kwake. Madabida akiwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa TAMPRO amesema kuwa ili Taasisi iweze kuthaminiwa na jamii, ni lazima kusimamia yale mambo ambayo yanawagusa wanajamii, kama vile hospitali, Shule za Sekondari na Msingi. Alisema, kwa kufanya hivyo uhusiano wa Taasis kwa umma utajulikana, kutambuliwa na hatimaye umma utaheshimu na utawapenda na hata kuwaunga mkono. Bw. Madabida, alisema uhusiano na Taasisi za nje ni jambo muhimu sambamba na kuwa mipango mizuri na kuonyesha nini mnachotaka kukifanya ni jambo muhimu, kwani kwa kufanya hivyo

kwani kila Msikiti sasa una shule. Awali, Amir wa TAMPRO, Bw. Mussa Kassim Mziya, akiizungumzai Jumiya hiyo Inaendelea Uk. 4

ALHAJ Ramadhani Madabida akiongea katika Mkutano Mkuu wa TAMPRO uliofanyika wiki hii Lamada Hoteli, jijini Dar es Salaam.

4
Na Mwandishi Maalum

Makala/Habari

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013


wa jemedari Dr. Karume. Umuhimu wa mambo haya mawili unaeleweka sana kwa maslahi ya Zanzibar yetu. Lakini tukumbuke kuwa kuna Dr. Shein ambae kwa sura yake aliyo sasa amewekwa kuyakabidhi haya tuwe tumemaliza kila kitu chetu. Wasi wasi uliopo ni kuwa chini ya Uongozi wa Dr. Sheni haya yote atayapeleka Muungano, kama hajayapeleka hivi sasa. Kinachomsukuma Dr. Shein kukubali haya yote ni yale yale, ya kulipa fadhila na ihsani ya mkono ukulishao. Yeye alipewa Umakamo wa Rais na sasa Rais wa Zanzibar, ambao ni utukufu wa dunia kwa miaka kumi. Kwa jinsi binadamu alivyo, miaka kumi ya Urais mtu huiona mingi sana na kwa hivyo yuko tayari kutoa chochote ili abakie kuwa Rais tu. Mwisho wake atakuja kukaa na sisi atuambie hili na hile, nchi keshaiuza wakati ambao alikuwa na uwezo wa kuitetea. Kwa hali hii tuendayo nayo, itaka pahala Zanzibar isiwe na lolote. Hakutakuwa na Rais wala Baraza la Wawakilishi. Na haya yako njiani. Naamini akiondoka Sheni, yote haya yatakuwa yamekwisha. Labda tutabakiwa na mapendekezo ya CUF, ya kuwepo kwa Gavana wa Zanzibar katika Muungano. Basi! Na hapo tutakuwa tumeshajizika na kujisomea hitma yetu. Natoa hoja. (Maoni haya yamechapishwa kwa mara ya kwanza katika mtandao wa mzalendo)

AN-NUUR

I K I WA n i t a k r i b a n i mwaka mmoja tu, kwa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kutimiza nusu karne, kuna kila dalili kwamba Zanzibar, kama ilivyo Tanganyika imepoteza utaifa na utambulisho wake wote. Kilichobaki ni historia au magofu tu ya masaza ya visiwani hivi ambavyo vilikuwa Jamhuri kamili hapo awali. Zanzibar ndani ya Muungano haina kikubwa ilichovuna zaidi ya kupoteza utaifa na kila kitu chake. Hata hivyo ieleweke kwamba, kumalizika huku na kulisika kwa Zanzibar kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wakuu wa visiwa hivi. Katika sura hii, tuangalie hasa chanzo na mchango wa Wazanzibari wenyewe katika kuimaliza nchi yao wenyewe. Zanzibar inamalizwa na viongozi wasio itakia mema w alio ndani ya serikali ya Muungano na SMZ. Viongozi ambao kwa kutojali maslahi ya nchi yao, utu wao, na utambulisho wao, huweka maslahi binafsi kwanza na kuiingiza nchi hii katika mashaka makubwa ambayo yanaigharimu Zanzibar roho, damu, na nguvu ya watu kuikomboa tena. Dokta Salmin Amour Juma (Komandoo), aliingia madarakani mwaka 1990 hadi 2000. Kabla hajawa Rais wa Zanzibar alikuwa mtoto kipenzi wa Dodoma na katika chama. Akapewa Urais. D r. S a l m i n A m o u r atakumbukwa kama Baba wa siasa za tna, za kimaskani, na Upemba na Uunguja katika vitabu vya historia vya nchi hii na dunia kwa ujumla. Hiki ndicho kikubwa tunachomkubuka Dr. Salmin katika umuri wa Utawala wake. Nje na hayo, Dr. Salmi atakumbukwa kwa mambo matano aliyoyafanya kuizamisha Zanzibar ndani ya kinywa kipana cha Muungano. Ni Dr. Salmin aliyeoandowa uingiaji wa watu Zanzibar kwa kutumia passpoti. Kosa hili lilichukuliwa kuwa dogo sana wakati alipolifanya, lakini mashaka yake yamekuwa ni ya udhia mkubwa kwa visiwa hivi hasa Unguja. Visiwa hivi vidogo vilivyokuwa na watu

Zanzibar yetu ishazikwa inasubiri kusomwa hitma

RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad . wasiozidi laki 6 hadi miaka ya 1988, imekurupuka na kuwa ni nchi yenye idadi ya watu inayoongezeko na msongamano wa watu kwa kasi ya asilimia 3 kwa mwaka (sensa, 2002), idadi ambayo ni kubwa hata kuliko Mkoa wa Dar es Salaam. Zanzibar imejaa watu, wenye haki ya kuishi na wasio na haki. Watu wema na wabaya. Kila mtu anakuja tu na anaachiwa aingie afanye analotaka. Athari ya kuondoa uingiaji kwa passpoti, pia umechangia sana kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu, ukahaba, uingizaji wa madawa ya kulevya, kufa kwa tamaduni za asili na hata wizi wa watoto wachanga kwa mara ya mwazo katika historia ya nchi hii. Dr. Salmin atakumbukwa kwa kufunguwa milango ya uingiaji wa makanisa hapa visiwani sambamba na kutoa viwanja kwa Wakristo bila hisabu wala kujali athari yake baadae. Tunaamini haki ya kuabudu na tunakiri kuwa Zanzibar kuna Wakristo lakini wasiozidi aslimia moja ya watu wote. Sasa idadi hio ndogo inakujaje kuwa ifuatiwe na mkururo wa makanisa ambayo waumini wake ni lazima waletwe kwa boti kila Jumamosi kutoka bara kuja kuabudu Zanzibar ili angalau kila kanisa lipate safu mbili za waumini? Ni Dr. Salmin alienyamaza kimya wakati nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa makamo wa Ris ikiondolewa na kumuweka Rais kuwa ni Waziri tu katika Jamhuri ya Muungano. Ijapokuwa yeye hakukubali hata siku moja kuingia bungeni kama Waziri, lakini ilikuwa tisha toto tu. Hakuweza kulipinga suali hilo na kusema iwapo ni hivi sisi hili hatulitaki. Kwa maana hii tunasema aliridhia kabisa, na hana budi kubeba lawama. Dr. Salmin pia ndie alieikaribisha TRA na kuunganisha mapato ya nchi hii kwenda bara. Na kwa kufanya hivi alikuwa hajui kuwa ndio anaimaliza kukatwa mishipa ya mwisho ya kuvutia pumzi kwa Zanzibar baada ya kuiuwa biashara ya bandari huru. Leo hii bara inajengwa majumba makubwa, barabara viwanja vya ndege vikubwa kwa mapato ya Zanzibar. Huku Zanzibar miundo mbinu na maendeleo kwa ujumla ikisuasua na kudumaa. Leo Mzanzibar analipa kodi mara mbili bara na Zanzibar lakini wa bara analipa kodi mara moja tu. Haya ndio malipo ya hisani yetu kwao. Na walipokwisha kupata maslahi yao Dr. Salmin kasahauliwa kama kwamba hajawafanyia hisani yoyote ile. Licha ya kufanya yote haya na mengine nimeyasahau kwa sasa. Malipo yake fedheha, ndio aliyopata. Pia, hivi karibuni kulivumishwa taarifa kuwa eneo la bahari kuu litakuwa mali ya Muungano. Pia suali la mafuta nalo likaja tena juu hata baada ya kukingiwa kifua wakati

Inatoka Uk. 3 na shughili zake alisema, Tampro, ina madhumuni ya kuwaunganisha wanataaluma Waislamu wote waliopo nchini ili waweze kutumia fursa na taaluma zao mbalimbali hatimaye kusaidia umma, kuweza kujiletea maendeleo. Alisema, katika kufanikisha malengo yake, alisema Tampro inafanya kazi ki-idara ambapo kuna idara za Elimu, Dini, Afya, Miundombinu, Biashara na Maendeleo ya Jamii, Sheria, Habari na Teknolojia ya Habari. Amir. Mziya, akifafanua kwa ufupi mafanikio ya baadhi ya idara hizo mbali ya changamoto wanazokutana

Madabida atoa changamoto kwa TAMPRO

nazo alisema, katika elimu, Jumiya imefanikiwa kumaliza mradi wa upanuzi wa majengo ya Shule yao iliyopo Sotole, Mkuranga, Mkoani Pwani, mradi ambao ulifadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (IDB), kwa thamani ya USD 449,000. Ama katika sekta ya afya, alisema, wamefanikiwa kupata taasisi shirika kutoka nje ya nchi (Helping hand for relief and development) ya kutoka nchini Canada. Alisema, Taasisi hiyo imeweza kusaidia kupata vifaa vya tiba na madawa vyenye thamani ya zaidi ya UDS 400,000, na kwamba bado Jumuiya inaendelea kupokea misaada ya namna hiyo na mingine.

Habari za Kimataifa/Tangazo

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013

AN-NUUR

TEL AVIV Waziri Mkuu wa utawala wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa utawala wake umeanza awamu mpya ya kupambana na wimbi la wahajiri wa Kiafrika wanaoingia Israel, kwa kuwarudisha katika nchi zao walizotoka. Netanyahu amesema kuwa, utawala wake pia unaweka mikakati ya kuweka doria ya kuzuia uingiaji kiholela wahamiaji katika mpaka wenye urefu wa kilomita 240 kati ya utawala huo na Palestina na Misri. Taarifa zinasema kuwa, wengi kati ya wahamiaji hao ni raia kutoka Sudan na Eritrea, ambao hawako tayari kurejea katika nchi zao wakihoa kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashitaka. Wahamiaji hao mara kadhaa wamefanya maandamano wakitaka kukomeshwa vitendo vya unyanyasaji, ukandamizaji na vile vya kibaguzi wanavyofanyiwa na utawala huo. Benyamin Netanyahu aliwahi kusikika akisema kuwa, kuwepo Waafrika huko Israel ni pigo kubwa kwa utambulisho wa Uyahudi. Waafrika wanaoishi Israel wanakabiliwa na wakati mgumu, licha ya kuchomwa visu mara kwa mara na kuteketezwa kwa moto makazi yao na kukumbana na vitendo kadhaa vya kibaguzi. Hivi karibuni gazeti la Haaretz la Israel liliandika kuwa, chuki ya Waisraeli dhidi ya Waafrika na Waarabu inahama kutoka kizazi hadi kizazi kingine huko Israel.

Israel yaanza kufukuza wahamiaji wa Kiafrika

Asilimia 63. 8 Misri waunga mkono rasimu ya Katiba mpya


CAIRO ASILIMIA 63. 8 ya watu waliopiga kura juu ya rasimu ya katiba nchini humo hivi karibuni, wameunga mkono kuidhinishwa katiba mpya ya nchi hiyo. Samir Abu al Matti, Mkuu wa Kamisheni Kuu ya Uchaguzi ya Misri alitangaza matokeo hayo Jumatatu katika mkutano na vyombo vya habari huko Cairo, mji mkuu wa nchi hiyo. Wakati huo huo, Hisham Qandil, Waziri Mkuu wa Misri ametoa taarifa akisema kuwa hakuna aliyeshindwa kwenye kura hiyo ya maoni na kwamba katiba mpya ya Misri itakuwa ya Wamisri wote. Ameyataka pia makundi yote ya kisiasa kushirikiana na serikali ili kuisaidia nchi hiyo kufufua uchumi wake. Katika baadhi ya mikoa kama vile Matruh na al Faiyum, zaidi ya asilimia 90 ya wapiga kura wameunga mkono katiba mpya. Pamoja na hayo suala lililopo ni je, baada ya kupasishwa katiba hiyo mpya utulivu na amani itarejea Misri, na je mchakato wa kisiasa wa nchi hiyo utafuata mkondo wa kawaida au la? Viongozi wa Harakati ya Uokovu wa Kitaifa, Muhammad el Baradei, ambaye ni kiongozi wa chama cha Katiba pamoja na wadau wengine maarufu wanaompinga Rais Muhammad Mursi, wametamka bayana kuwa endapo watapata viti vingi zaidi katika Bunge lijalo,

wataivunja katiba mpya ya nchi hiyo. Mirengo ya kisiasa inayompinga Rais Mursi, imetishia pia kuwa itaendelea na maandamano yao pamoja na msimamo wao wa kuipinga katiba. Misimamo hiyo inatangazwa katika hali ambayo wananchi wengi zaidi wa Misri wameipigia kura ya ndiyo rasimu ya katiba mpya, na kwa maoni yao kupasishwa katiba hiyo ya kwanza baada ya kuangushwa utawala wa Hosni Mubarak, sio tu ni hatua kubwa ya aina yake, lakini ni mwanzo wa harakati ya kuelekea kwenye uthabiti wa kisiasa na hatua moja mbele ya kuongeza kasi ya mchakato wa uundaji utawala wa kidemokrasia katika Misri mpya.

Mkutano wa Ustaarabu wa Kiislamu Mashariki mwa Afrika kufanyika Zanzibar

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, ameikemea vikali Marekani na kuiambia kwamba, haina sifa ya kuzikosoa nchi nyingine kuhusiana na suala la haki za binadamu. Rais Putin amesema ni kichekesho kwa nchi kama Marekani, ambayo ina rekodi mbaya ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu

Marekani haina sifa ya kuzungumzia haki za binadamu-Putin


kujifanya kuwa kinara wa kuzikosoa nchi nyingine na kuzituhumu kwamba, zinakiuka haki za binadamu. Rais Putin ametanabahisha kwamba, ulimwengu haujasahau unyama waliyofanyiwa wafungwa waliohukumiwa na Marekani bila kesi katika gereza la Abu Ghuraib nchini Iraq, na yanayoendelea kufanywa n a Wa s h i n g t o n h u k o Guantanamo Bay, ikiwa ni pamoja na kuwashikilia watu bila ya kuwafungulia mashtaka kwa madai kama ya ugaidi na kadhalika. Aidha Rais Putin amesema nchi yake itatoa jibu la jino kwa jino na jicho kwa jicho kwa Marekani, endapo itataka kuchukua hatua dhidi ya Moscow. Amesema nchi yake haina nia ya kuharibu uhusiano wake na nchi yoyote ile, lakini katu haitokubali kuburuzwa au kushinikizwa kwa visingizo visivyo na kichwa wala miguu. Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amezungumzia suala la ugaidi na kusisitiza kuwa ugaidi ni ugaidi tu.

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin (kushoto) akiwa na Rais Barack Obama wa Marekani

JUMUIYA ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, kupitia kituo chake cha Utafiti wa Historia, Sanaa na Utamaduni wa Kiislamu (IRCICA) kimeandaa kongamano la kimataifa linalohusu Historia na Ustaarabu wa Kiislamu Mashariki mwa Afrika. Kwa mujibu wa tovuti ya ircica.org, kongamano hilo litakalo fanyika Septemba 36 mwaka 2013, linaandaliwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Nyaraka za Kitaifa na Makazi ya Ufalme wa Oman na Chuo Kikuu cha Zanzibar nchini Tanzania. Imeelezwa kuwa kongamano hilo linalenga kuangazia zaidi ustaarabu wa Kiislamu Mashariki mwa Afrika na kuchunguza athari za ustaarabu wa Kiislamu katika eneo. Kati ya maeneo yatakayochunguzwa ni pamoja na athari za ustaarabu wa Kiislamu katika usanifu majengo, jamii, uchumi na siasa. Aidha kongamano hilo litachunguza nyaraka za kale kuhusu utaarabu wa Kiislamu. Itakumbukwa kuwa bara la Afrika lilikuwa sehemu ya kwanza kuka wahajiri wa Kiislamu kutoka Makka. Waislamu hao walika katika eneo la Abyssinia (Ethiopia na Eritrea ya leo). Baadae Waislamu walienea katika maeneo mengine ya pwani ya Mashariki mwa Afrika. Wa s o m i w a n a o t a k a kuwasilisha makala katika kongamano hilo wanaweza kutembelea tovuti ya http:// www.ircica.org, ili kupata maelezo zaidi. Habari na IQNA.

Amesema kuwa hatua ya nchi za Magharibi kuugawa ugaidi huko Syria katika mafungu mawili, yaani ugaidi mzuri na mbaya, inatilia shaka madai ya nchi hizo kuhusu demokrasia. Waziri huyo amesema kuwa ni jambo lisilokubalika kwa nchi za Magharibi kuwaunga mkono magaidi huko Syria.

6
Na Ibn Mohammed

Makala

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013 wa ASP waliingia katika kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika kutaka nguvu, si za kupigana bali za kiuchumi na ndio maana suala la uchumi halikuwa katika orodha ya mambo ya Muungano. Mzee Karume na Sheikh Thabit Kombo walisimama katika nguzo ya nia njema. Tunapoadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi, tuna kila sababu ya kuwaenzi na kudumisha misingi yao. Je, wale wanaodai kuwa CCM imesalitiwa kwa kuwepo GNU iliyozaliwa kutokana na maridhiano ya kisiasa Zanzibar, wana lipi la kusema na kujinasib ikiwa CCM ni zao la vyama vya ASP na TANU? Hivyo basi, wafahamu kuwa sikio siku zote halizidi kichwa. Wahafidhina ni ASP ipi mnayoitetea? Hii iliyoasisiwa na Mzee Karume, Sheikh Thabit Kombo Jecha au nyingine maana wazee wetu hawa walichukia sana ubaguzi. Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiwasingizia baadhi ya viongozi waliotangulia mbele ya haki. Wengi utawasikia kama angekuwepo Mzee Karume, Seif Bakari, Mzee Thabit Kombo, au Said Bavui , wasingekubali mseto au maridhiano haya ! Hii si kweli. Ni kujaribu kuwalisha maneno maiti badala ya kuwarehemu. Mzee Karume alikuwa Waziri wa Afya katika Serikali ya Mseto iliyoundwa na Vyama vya ZNP na ASP kabla ya Mapinduzi. Sasa Karume anayesikingiziwa uzushi huo ni yupi huyu wa sasa au wa zamani? Karume mkubwa na mdogo wote ni waumini wa umoja na maridhiano na ndio maana Baraza la kwanza la Mapinduzi lilijumuisha watu wenye nasaba tofauti. Itakumbukwa pia kuwa mara tu baada ya Mapinduzi mwaka 1964, Mzee Karume huyo huyo kama ilivyo kwa Sullivan na Mwalimu Nyerere, naye alichukia sana ubaguzi na ndio maana aliongoza kampeni ya ndoa za mchanganyiko wa rangi na makabila mbalimbali Zanzibar. Mzee Karume hakulazimisha watu kuoana, bali aliwataka wazazi wawape watoto wao Inaendelea Uk. 7

AN-NUUR

WIKI iliyopita rafiki yangu kutoka Fiji aliniletea jarida moja lenye picha za kihistoria y a k u m b u kumbu ya ubaguzi kule Marekani enzi za ubaguzi wa rangi na ukandamizaji wa mtu mweusi. Jarida lile linasononesha na kuhuzunisha ukitazama p i c h a z a Wa a f r i k a waliokuwa wakiitwa Negro, walifanya kazi kucha kutwa kwenye mashamba ya mabepari wa Kizungu huku wakilipwa ujira mdogo! Sehemu kama Mississippi, Alabama na nyingine Waafrika walinyanyasika sana, lakini si haba juhudi za akina Malcom X, Dk. Martin Luther King Jr, Mchungaji Leon Sullivan na wapigania haki wengine, leo Marekani ni taifa lenye umoja na mshikamano na ndio taifa lenye kupigiwa mfano wa kilele cha demokrasia. Kisa maarufu kilichomtokea Mchungaji Leon Sullivan, Mmarekani mwenye asili ya Afrika ambaye anajulikana kwa msimamo wake wa kuchukia ubaguzi wa rangi siku moja alienda kunywa soda kwenye hoteli moja kule Marekani, alipoingia akanyimwa kiti kwa vile yeye alikuwa mtu mweusi. Kitendo hicho kilimfanya kuuchukia ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa aina yoyote. Tukiwa tunakaribia maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar na hapo baadae miaka 49 ya Muungano ni muhimu kukumbusha dhamira za Afro Shiraz Party (ASP), juu ya msimamo wake katika kupiga vita ubaguzi. 1927, safari yetu leo itaanzia Mzizima jina la asili la Dar es Salaam ya sasa. Huko Waafrika wa mjini Dar es Salaam walianzisha jumuiya yao iliyoitwa African Association kwa ajili ya kupigania haki na maslahi yao ya kijamii. Waafrika wa Zanzibar nao walianzisha African Association yao hiyo ilikuwa 1934, pengine ni kutokana na ushawishi wa ndugu zao wa Dar es Salaam. Nao Waafrika wa Zanzibar wakawashawishi Waafrika wa Dodoma

ambao nao walianzisha ya kwao. Upepo wa mabadiliko ulikuwa ukivuma katika sehemu nyingi za dunia na hasa Afrika wakitaka kuwa huru kutoka kwa wakoloni. Hali hiyo ilifanya 1954 kuzaliwa Ta n g a n y i k a A f r i c a n National Union (TANU), chama kilichoanzishwa Tanganyika kutokana na Tanganyika African Association, kwa ajili ya kudai uhuru kwa upande wa Tanganyika. Zanzibar nako 1957 ilianzishwa Afro Shirazi Party (ASP), kutokana na kuungana kwa African Association na Shirazi Association iliyokuwa imeundwa 1938. Kuundwa kwa ASP kulishuhudiwa n a R a i s w a TA N U , Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pale Mtaa wa Mwembe Kisonge. ASP ilizaliwa katika mazingira yaliyokwisha andaliwa kisiasa na African Association (AA) na Shirazi Association (SA), vyama ambavyo vilikuwa nusu vya siasa na nusu vya kijamii kupigania maslahi ya watumishi wa Kiafrika kazini. Hata baada ya kuundwa kwake, ASP na TANU

Wanaomtusi Amani Karume hawaijui siasa ya Zanzibar


MWALIMU Julius K. Nyerere MZEE Abeid Amani Karume. katika ilani zao zilisisitiza suala zima la ushirikiano, umoja na mshikamano katika dunia ambapo ASP toka enzi za mapambano ya kudai uhuru ilikuwa na vipengele vya kutaka umoja wa Afrika. Inastaajabisha leo kuna watu Zanzibar wamejivika joho la U Afro Shirazi kupinga maridhiano, kubeza Serikali ya Umoja wa Kitaifa na wengine kumfuja, kumkejeli na hata kumtusi mama yake mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Sita Dk. Amani Abeid Karume, kwa maoni yake aliyoyatoa mbele ya mkutano mkuu wa CCM Dodoma na hatua yake kuasisi maridhiano na umoja Zanzibar. Sijui ni ASP ipi inayoelezwa kuwa haikutaka umoja, mshikamano, kwani wakati wa harakari za kutafuta uhuru, ASP pamoja na vyama vingine vya ukombozi Afrika vilishiriki kikamilifu katika majukwaa yote yaliyowaunganisha Waafrika wa nchi mbali mbali katika kudai uhuru kwa lengo la kuja kuziunganisha nchi hizo baada ya uhuru. Kwa mfano, TANU na ASP zilikuwa wanachama wa PAFMECA na baadae

PAFMECSA, vyombo ambavyo viliviweka pamoja vyama vilivyokuwa vikidai uhuru kutoka nchi mbali mbali za eneo la Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika. Mwasisi wa Taifa la Zanzibar, Abeid Amani Karume na Jamal Ramadhan Nasib ambao wote sasa ni marehemu, waliwahi kushiriki mikutano mara kadhaa katika nchi za Ghana, Misri na Ethiopia. Je, tuwahukumu kwa suala hilo? Watu wenye busara kamwe tutawakumbuka kwa mchango wao kutaka umoja na mshikamano. Katibu Mkuu wa kwanza wa ASP, Sheikh Thabiti Kombo Jecha katika kitabu cha Masimulizi ya Shekikh Thabit Kombo Jecha, kilichoandikwa na Minael-Hosanna Mdundo (DUP 1999), Sheikh Thabit Kombo ananukuliwa kusema k w a m b a Wa z o l a Muungano ni wazo la AfroShirazi tokea mwanzo, katika Manifesto yetu tulisema kuwa tukipata Uhuru azma ya ASP ni kuona kuwa Afrika yote inakuwa moja yenye nguvu Akiamini katika Umoja wa usawa, Sheikh Thabit Kombo na waasisi wengine

7
Inatoka Uk. 6

uhuru wa kuoa na kuolewa na wawapendao. Waarabu hawakutaka mabinti wao waolewe na Waafrika ilhali wanawapenda na kinyume chake baadhi ya Waafrika nao walikataa watoto wao kuoa Waarabu. Shafi Adam Shafi ameeleza katika kitabu chake cha vuta nikuvute suala la ndoa za aina hiyo, akapeleka posa kwa Gulam. Gulam alipojidai kumtilia nakshi Kermali akibwata na kufoka kuikataa posa ya golo, Kermali akamwambia ho! Mbona wewe unaye golo umemcha Vikokotoni Mwenyewe Karume akaanza kuoa Waarabu akifuatiwa na Wajumbe wengine wa Baraza la Mapinduzi (MBM) ambao walioa wake wa makabila mbalimbali, Ramadhan Haji Faki, Brigedia Yussuf Himid, Khamis Darwesh, Ibrahim Amani, Thabit Kombo Jecha na wengine ambao vizazi vyao ndio leo wanachama wa CCM na wengine ni viongozi. Je, unambagua mtoto au mjukuu wa Mzee Thabit Kombo Jecha kwa misingi ipi? kwasababu Mahmoud Thabit Kombo mama yake ni Mzanzibari mwenye asili ya kihindi au Mahfoud Ali Mahfoudh ambaye mamake Bi Naila Jidawi ana asili ya Kiarabu? Ambao leo ni makamanda wa mstari wa mbele ndani ya Jeshi kubwa la CCM katika kutafuta ushindi kwenye uchaguzi. Mzee Karume alishawishi watu kuwa wamoja na kwa kweli baadhi ya wazazi wakashawishika na kuanza kuunga mkono dhana ya ndoa za mchanganyiko ambapo faida yake baada ya miaka takriban 49 sasa tunaiona matunda ya ndoa hizo wengine ni viongozi na raia wa kawaida wasiojigamba kwa rangi na nasaba zao, bali kwa uzalendo wa Uzanzibari. Ndoa hizo hazikuwa za kulazimishana kama inavyodaiwa na baadhi ya watu wapinga umoja na maelewano. Katika kuthibitisha hilo soma kitabu cha Vuta ni nkuvute katika ukurasa wa 275, Shafi Adam Shafi ameeleza kwa kina suala

Wanaomtusi Amani Karume hawaijui siasa ya Zanzibar

Makala

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013 kuwashawishi watu katika njia za ukabila na ujimbo kama utambuzi mkuu katika kuungwa mkono ili kulinda maslahi yao ya kuweko kwenye nafasi bila kujali athari za baadae wanafaa kusikilizwa au kupuuzwa? Ni muhimu pia kuuliza Viongozi wa CCM na hata wale waliomo ndani ya SMZ kuwa ushupavu wa kutetea uamuzi uliofanywa na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Zanzibar kuhusu kumalizika kwa mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Bila shaka Amani Karume ni Kiongozi shupavu ambaye hakuchukua ubinafsi kama dira na mwelekeo wake katika maisha yake ya siasa. Kwa wale wataalam wa Tasnia ya Manajimenti wanaelewa vyema msamiati wa The Courage of Leadership. Ushupavu wa Uongozi. Tuwe wepesi kutambua maslahi yetu katika mabadiliko hayo, na tuwe wepesi kubuni mikakati ya kutetea maslahi hayo. Tuwe shupavu kama Chama kuwaiga raki zetu Wachina. Uchumi wa dunia ya leo ni uchumi wa soko. Ni kujidanganya kufikiri tunaweza kuukwepa Bila shaka Karume ni aina ya Kiongozi katika jamii ambaye hakutaka kubeba mizigo yenye harufu mbaya na kuifanya ni mwelekeo mbadala katika siasa na maendeleo kwani katika duania ya utandawazi inayoendelea kwa kasi majadiliano na kufikia maafikiano ndio nguzo na silaha madhubuti. Pengine tuwauliza Viongozi waliokuwamo katika GNU kutoka CCM, wana ushupavu unaohitajika au walitaka uongozi kwa maslahi binafsi, lakini je CCM kinao ushupavu wa uongozi unaohitajika katika mazingira ya sasa ya Serikali ya GNU? Mbona hatuwasikii kuelezea umuhimu wa maridhiano katika siasa za ushindani wa vyama vingi? (Makala hii imetolewa kwa hisani ya Ibni Mohammed na wanamtandao wa Mzalendo)

AN-NUUR

MAMA Fatma Karume (kushoto) hilo akihusisha ndoa ya Bukheti Madoriani na Yasmin. Kwa kuwa ndani ya CCM hivi sasa wapo watoto, wajukuu na vitukuu vya waasisi wa ASP na hata CCM yenyewe, hoja ya kupinga GNU, kumkejeli Rais mstaafu Karume, inapata nguvu wapi ikiwa Gulam na Kermali walizika tofauti zao na kushirikiana katika shughuli ya arusi? ASP iliungwa mkono na Waarabu, Wahidi na watu wengine. TANU nayo ilikuwa na watu kama hao kina Alnoor Cassum, Derek Bryson, Amir Habib Jamal, Habib Punja na wengineo. Kuna baya lipi lililofanywa na CCM kushirikiana katika kuendesha nchi na Chama cha CUF ambacho cha Wazalendo wenzao? Mawaziri wote ni Wazanzibari ambao naamini wanafanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria kuwatumikia wananchi wenzao. Wakati Tanga la jahazi la wataka mabadiliko katika mfumo wa muundo wa Muungano limeshiba upepo wa Kaskazi, hivi sasa na kusi hapo baadae, komamanga imelala upande mmoja inakata maji kama papa, huku wanamageuzi wa kweli wakiwa wamesimama te z i w a k ia n g al ia M j i wa uhasama, chuki na ubaguzi ukitoweka ambapo katika upeo wa macho yao nuru ya matumaini kutapa mabadiliko katika Muungano ikianza kujichomoza, tuna kila sababu ya kutetea hoja ya mabadiliko. Jahazi la wapinga mabadiliko linakumbwa na misukosuko ya bahari, upepo wa Kaskazi unavuma sijui kama watapona maana tanga lao bovu, foromali chakavu huku hali ya bahari ikichafuka sijui kama papa wenye njaa wanaoranda randa katika upwa wa kisiwa chao kama watawaacha. Hakuna ubishi kwamba katika dunia ya sasa mambo yote hadharani, Msondo Ngoma wameimba katika wimbo wao wa mambo hadharani. Tumeshuhudia mchakato wa utoaji maoni mambo yakiwa hadharani, wanaotaka mabadiliko ya muundo wa Muungano wanasema na wale wanaopinga nao wanaeleza hoja zao, mwisho wa siku tutakumbana kwenye kura ya maoni. Rais Jakaya Kikwete aliwahi kusema kuwa Wazanzibari ni wamoja hakuna haja ya kugombana. Sasa wewe unaeshabikia siasa za chuki na uhasama, unapingana na Mwenyekiti wako wa CCM na Halmashauri Kuu yako ya Taifa iliyoamua kule Butiama kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa? Bila shaka katika maneno hayo kuna mafundisho makubwa yanapatikana kwa muumin wa kweli wa Kiislamu ambapo naamini genge la Wahafidhina asilimia kubwa kama si yote ni Waislamu. Mwenyezi Mungu anasema na hawakumbuki ila wenye akili. Marekani, ilikuwa ndoto kwa Mmarekani mwenye asili ya Afrika kutawala katika nchi hiyo, lakini tumeshuhudia mwiko huo ukivunjwa Januari 20, 2009, pale Barack Obama alipoapishwa kuwa rais wa 44 wa Marekani na hivi karibuni ameshinda tena Uchaguzi. Hivi leo dhambi kuu ya baadhi ya wanasiasa hasa Zanzibar wanaopenda

8
Imetafsiriwa na AbdunNaaswir Hikmany WAKATI wa zama za kale, siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za Kusini kulisherehekewa mfano wa usiku, ambao mungu wa Mama Watakatifu alijifungua mtoto akijulikana kuwa ni mungu wa Jua. Pia (siku hii) inaitwa Yule, siku ambayo inasherehekewa zaidi kwa kurushwa pashpashi. Ambapo kila mtu atacheza na kuimba ili kuliamsha jua kutokana na usingizi wake mnono wa majira ya baridi. Wa k a t i w a Wa r u m i , iliadhimishwa kwa kumsifu Satunusi (mungu wa mavuno) na Mithrasi (mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia jua ambao umekuja ukitokea Syria hadi Urumi. Karne kabla ya madhehebu ya Sol Invictus, ilitangazwa ya kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele na kwamba, maisha yanasonga mbele, na ni mualiko wa kubaki kwenye nguvu nzuri. Siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za mviringo za Kusini ni baina ya siku ya 20 au 22 Desemba. Wa r u m i w a l i a d h i m i s h a Saturnalia baina ya tarehe 17 na 24 Desemba. Wa k r i s t o w a k a l e : Nao Wakristo wa kale ili kuepuka kuchunguzwa wakati wa sherehe ambazo ni za wapagani, Wakristo wa kale walikaa majumbani mwao pamoja na mtakatifu Saturnalia. Kwa vile idadi ya Wakristo iliongezeka na mila zao zikaenea, sherehe zikachukua shuruti za Kikristo. Lakini, Makanisa ya kale hakika hayakusherehekea mwezi wa Desemba kwa kuzaliwa Kristo hadi a l i p o k u j a Te l e s p h o r u s , ambaye alikuwa askofu wa pili wa Roma kutoka mwaka 125 hadi 136 M. Askofu huyo ndiye aliyetangaza kwamba huduma za Kanisa zifanywe wakati huu ili kuadhimisha Kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mwokozi. Hata hivyo, kwa vile hakuna mtu hata mmoja aliye na uhakika wa mwezi ambao amezaliwa Kristo, kawaida ya uzawa ulikumbukwa Septemba, ambapo ulikuwa ni wakati wa sherehe za Kiyahudi za Trumpetsi (kwa sasa ni Rosh Hashanah). Ukweli ni kuwa, kwa zaidi ya miaka 300, watu walielewa kuzaliwa kwa Yesu katika tarehe tofauti. Katika mwaka 274 M, kikomo cha jua kiliangukia tarehe 25 Desemba. Mfalme wa Roma aitwaye Aurelian,

Makala/Tangazo

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013


wa ki-Rumi wa kale kwa kuadhimisha kurudi kwa jua. Hivyo, hakuna mshangao wowote kwamba Wakristo waliosafi (puritans) au Wa k r i s t o w a s i o t a k a mabadiliko (conservative) watahamaki kwa Krismasi kuwa sio ya kidini kama ilivyotakikana kuwa, Wakisahau kwamba Krismasi h aik u s h er eh ek ew a h ata kidogo hadi siku za hivi karibuni. Mti ulio bora wa Krismasi unanunuliwa. Ukipambwa kwa madoido yenye kungara pamoja na kumetameta, unasimamishwa karibu na dirisha. Maduka yanajazana wanunuzi wakisaka zawadi na vile viduchu, vinasubiri kwa hamu kubwa zawadi ya Baba Krismasi Santa Claus. Ni mshughuliko na homa ya Krismasi. Lakini Je, umewahi kukiri kabla? Je, Biblia au Yesu aliwahi kusababisha homa ya Krismasi? Tafakari juu ya mchanganuo ufuatao kuhusu Krismasi, na ukweli utakuja kuwa wazi zaidi na zaidi. Je, Krismasi ina ushahidi wa Biblia? Neno Krismasi halipo ndani ya Biblia. Biblia Inaendelea Uk. 9

AN-NUUR

Inasherehekewa Christmas ipi?


alitangaza tarehe hiyo kama ni Natalis Solis Invicti, Sherehe ya kuzaliwa jua lisiloshindikana. Katika mwaka 320 M, Papa Julius I, aliitangaza tarehe 25 Desemba kuwa ni tarehe rasmi ya kuzaliwa Yesu Kristo. Mnamo mwaka 325 M, Krismasi ilitangazwa rasmi, lakini kiujumla haikutiliwa maanani. Mtakatifu Constantine, ambaye ni Mfalme wa mwanzo wa dhehebu la Ukristo la Kirumi, aliitanguliza Krismasi kama sherehe isiyohamishika kwa tarehe 25 Desemba. Pia aliitanguliza Jumapili kama ni siku kuu ndani ya siku saba za wiki na aliitanguliza (Pasaka) kama ni sherehe yenye kuhamishika. Mnamo mwaka 354 M, Askofu Liberius wa Rumi, alitoa amri rasmi kwa wafuasi wake kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu ndani ya tarehe 25 Desemba. Hata hivyo, ingawa Constantine, aliifanya rasmi tarehe 25 Desemba kama ni sherehe ya kuzaliwa Kristo, Wa k r i s t o w a k i i t a m b u a kama ni tarehe ya sherehe iliyofanana na mapagani, hawakushiriki katika mambo mazuri (kwa siku hii) iliyopangwa na Askofu. Krismasi ilishindwa kupata utambulisho wa kilimwengu miongoni mwa Wakristo hadi kipindi cha hivi karibuni. Huko Uingereza England, Oliver Cromwell, alizipiga marufuku sherehe za Krismasi baina ya miaka ya 1649 na 1660 kupitia kwa inayoitwa Sheria ya Rangi Samawati (Blue Laws), akiamini kwamba iwe ni siku ya kumuabudu mungu tu. Hamu ya kuifurahia sherehe ya Krismasi ilikirimiwa pale Waprotestanto (Wakristo wasiokubali baadhi ya mafundisho ya Kanisa la Kirumi), walipokimbia uchunguzi dhidi yao kwa kutorokea sehemu za makoloni yote duniani. Hata hivyo, Krismasi bado haikuwa ni sikukuu halali hadi miaka ya 1800. Wala hakukuwa na picha ya Baba Krismasi (Santa Claus) kwa wakati huo. Krismasi inaanza kuwa maarufu Umaarufu wa Krismasi ulianza ghafla mwaka 1820, kutokana na kitabu cha Washington Irving, kiitwacho The Keeping of Christmas at Bracebridge Hall (Kuiadhimisha Krismasi kwenye ukumbi wa Bracebridge). Mnamo mwaka 1834, Malkia wa Uingereza aliyeitwa Victoria, alimkaribisha mumewe wa Kijerumani Prince Albert, ndani ya ngome ya Windsor Castle, akimuonesha tamaduni za mti wa Krismasi (Christmas tree) na nyimbo za kumsifu Yesu Kristo (carols), ambazo ziliadhimishwa Uingereza kwa Mfalme wa Uingereza. Mwaka 1834, wiki moja kabla ya Krismasi, Charles Dickens, alichapisha nyimbo za kumsifu Yesu za Krismasi, yaani Christmas Carols. Christmas ilikuja kuwa ni maarufu sana hadi kufikia kwamba sio makanisa wala serikali kukana umuhimu wa sherehe za Krismasi. Mwaka 1836, Alabama ilikuja kuwa ni taifa la mwanzo ndani ya Marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mwaka

Historia ya Christmas, kusherehekea na kupongezana


1860, mchoraji (illustrator) wa Marekani aitwaye Thomas Nast, alichukua kutoka hadithi za Kiingereza kuhusu Mtakatifu Nicholas, muangalizi mtakatifu wa watoto, kumtengeneza Baba Krismasi (Father Christmas). Mwaka 1907, Oklahoma ilikuwa ni ya mwisho miongoni mwa mataifa ya Marekani kutangaza Krismasi kama ni sikukuu halali. Mwaka baada ya mwaka, nchi za dunia nzima zilianza kuitambua Krismasi kama ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu. Leo, mambo mengi yasiyokuwa ya Kikristo yananasibishwa ndani ya Krismasi. Yesu alizaliwa mwezi wa Machi, bado siku yake ya kuzaliwa inasherehekewa Desemba ya 25, wakati wa solstice. Sherehe za Krismasi zinamalizikia siku kumi na mbili za Krismasi (Desemba 25 hadi Januari 6), ni idadi hiyo hiyo ya siku ambazo zilisherehekewa na wapagani

Uongozi wa Shule ya Answaar Islamic Model School inawatangazia waislamu wote nafasi za masomo kwa mwaka 2013, kama ifuatavyo. Shule ya awali ( Nursery School) Kg - 1 and Kg 11 Umri kuanzia miaka mitatu na nusu na kuendelea. 2. Shule ya msingi ( Primary School) Darasa la kwanza hadi la Sita, kwa wale wanaotaka kuhamia nafasi pia zipo. ADA: shule ya awali ( Nursery school) 550,000/= kwa mwaka. Shule ya msingi (Primary school). i) Darasa la kwanza hadi la tano ni Tsh. 650,000/= ii) Darasa la sita na la saba Tsh. 750,000/= ada inalipwa kwa awamu tatu. - Shule ipo kinondoni Studio/ karibu na vijana Social Hall au nyuma ya vijana. - fomu zinapatikana shuleni Kinondoni studio Masjid Answaar. - Tarehe ya USAILI ni Tarehe 6/01/2013, usaili utafanyika shuleni Answaar Islamic Model School, Siku ya Kufungua shule ni Tarehe 14/01/2013. Kwa mawasiliano zaidi piga simu. 0767- 121555,0777-790283, 0712 790283. Au Email answaarislami@yahoo.com au tembelea Tovuti yetu: www.answaarislamic.co.tz Mlete mwanao apate elimu na malezi bora ya Kiislamu 1.

ANSWAAR ISLAMIC MODEL SCHOOL

Krisimasi inatuharibia Uzanzibar (Maoni)


Na Mwandishi Maalum

Makala/Tangazo

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013

AN-NUUR

KILAtarehe 25 December 2012 ndani ya Zanzibar kumekuwa na dhana kwamba ni sikukuu. Vijana wengi wako tayari kuchukuwa day off katika shughuli zao eti wanasherehekea sikukuu hii. Wengine wamekosa hata kuhudhuria madrasa kwenye vyuo na taasisi nyengine, nao wajumuike. Dhana hii bila ya shaka itakuwa na kichocheo chake, licha ya Zanzibar kuwa na misingi ya utamaduni wake iliyotokana na urithi wa wazee karne nyingi zilizopita. Iweje leo kuwe na dhana na hoja kama hizi zisizokuwa na mashiko? Iweje leo Wazanzibar wapoteze muelekeo na kushusha utamaduni wao waliorithi dahar baada ya dahar. Hakuna budi kwa wazalendo kulitafakari hili kwa kina, badala ya kulaumu itafutiwe ufumbuzi wa kudumu. Dhana ya kusema Inatoka Uk. 8 ilifunga midomo ya sherehe yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kitu kimoja; upambaji wa mti. Biblia wenyewe inashutumu upambaji wa miti (ya Krismasi). Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu, wanaugandanisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika (Jeremia 10-3,4). Wazungu wa ki-Pagani kabla ya Ukristo, waliamini miujiza kwamba miti ya kijani ina nguvu maalum za ulinzi. Hakika, matumizi ya miti ya krismasi yameanza hivi karibuni tu, katika karne ya 17 huko Strasbourg, Ufaransa na kutoka huko yakaenea hadi Ujerumani, Uingereza na baadaye Marekani. Ibada ya miti ilikuwa ni jambo la kawaida kwa dini miongoni mwa watu wa Teutonic na Scandinavia

Ni moja ya kero za muungano

RAIS Barack Obama wa Marekani (kushoto) akiwa na Papa Benedict (katikati) kulia ni mke wa Rais Barak Obama. serikali haina dini, wakati inafahamika Zanzibar ni nchi ya Waislamu, ikiwa na asilimia 99 ya watu wake wote wakiwa Waislamu, huko ni kuvunja heshma ya watu wako. Huko ni kupotea kunakohitaji kuonyeshwa njia. Huko ni kuwadhulumu raia hawa wengi haki zao. Angalia, leo na kesho siyo siku ya kazi Zanzibar. Kwa kigenzo gani? Pia mwezi wa nne ziko siku 2 kama hizi. Kigenzo kikuu ni kwa ile asilimia 1 iliyobakia ikiwa na mchanganyiko wa dini nyengine. Lakini iweje siku zote nne wapewe dini moja tu? Linganisha na siku nne walizopewa kundi la asilimia 99, usawa uko wapi hapo? Shetani wa hili si mwengine isipokuwa

Inasherehekewa Christmas ipi?


wa Ulaya ya Kaskazini, kabla ya kuingia kwenye UkristoWalowezi wa ki-Jerumani walileta mila za mti wa Krismasi kwenye makoloni ya Kimarekani mnamo karne ya 17. Kukia karne ya 19, matumizi yake yalienea sehemu tofauti. (Angalia Encyclopedia ya Compton, Toleo la 1998) Je, Yesu alizaliwa Desemba ya 25? Si tarehe ya Desemba 25 wala tarehe nyengine yoyote iliyotajwa ndani ya Biblia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Ilikuwa ni hivyo hadi kukia mwaka 530 C.E kwamba mtawa aitwaye Dionysus Exigus, aliweka tarehe isiyobadilika ya kuzaliwa kwa Yesu kuwa ni Desemba 25. Kulingana na taratibu za ki-Roma, alikosea kuipanga tarehe ya kuzaliwa kwa Kristo (yaani, miaka 754 baada ya kupatikana nchi ya Rumi) kama ni Desemba 25, mwaka 753. (Angalia: Encyclopedia Britannica, toleo la mwaka 1998) Tarehe hii ilichaguliwa ili iendane pamoja na sikukuu ambazo zimeshagandana na imani za kipagani. Mapagani wa Kirumi walisherehekea Desemba 25 kama ni ya kuzaliwa kwa mungu wao wa nuru, aitwaye Mithra. Mnamo karne ya pili M, hiyo sherehe ya Mithra ilikuwa ni ya kawaida zaidi ndani ya Ufalme wa Rumi kuliko Ukristo, ambayo ilizaa mifanano iliyo mingi (The Concise Columbia Encyclopedia, toleo la mwaka 1995). Waungu wengine wa kipagani waliozaliwa Desemba ya 25 ni: Hercules, mtoto wa Zeuz (Wagiriki); Bacchus, mungu wa mvinyo (Warumi); Adonis, mungu wa Kigiriki, na

ni yuleyule JINI MUUNGANO. Lengo ni kuuwa kila kitu cha Kizanzibar, tokea jina lenyewe, historia, mamlaka, utamaduni, mila na silka zake. Hii ni kama ile tabia ya mchwa kuumega mti akiwa yeye kajicha humo humo ndani. Kuubaini unahitaji tafakur ya hali ya juu. Tu e n d e l e e k u e n z i utamaduni, mila na silka zetu kutolikubali hili liendelee nchini kwetu. Haiyumkini serikali nzima isitishe kazi kwa muda wa siku mbili hali ya kuwa hakuna anayefaidika na hilo. Tujifunze kutoka nchi nyingi dunia, mfano Uingereza, wao wanasema kabisa hakuna sherehe ya dini nyengine, isipokuwa sherehe ya ni kristo. Yule anayetaka kusherehekea dini yake ni khiari yake. Kwa nini vitu vingi tunajifunza kwao, lakini hili hatulitaki? (Maana haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza Desemba 25, 2012 katika mtandaoMzalendo) Je, Yesu au wafuasi wake waliwahi kusherehekea Krismasi? Kama Yesu alimaanisha kwa wafuasi wake kusherehekea Krismasi, angeliifanyia kazi yeye mwenyewe na kujikusanya pamoja na wafuasi wake. Hakuna sehemu iliyotajwa ndani ya Biblia kwamba kuna mfuasi yeyote aliyewahi kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kama Wakristo wanavyofanya leo. Kanisa halikupata kuweka sikukuu kwa ajili ya sherehe za tukio la Krismasi hadi ilipofika karne ya 4 (Angalia: Encyclopedia ya Grolier) Hivyo, tunaona kwamba sio Biblia wala Yesu na wafuasi wake waliosema kitu kuhusu sherehe za Krismasi, ambazo sasa zinahusisha viingilio vya sherehe, biashara, na matumizi yaliyochupa mpaka. Zaidi kuna maandiko ya Yesu kula Pasaka, sio Christmas. (Alhidaaya.com)

mungu Freyr wa Ugirikimapagani wa Roma. Je, Vipi Kuhusu Baba Krismasi Santa Claus? Majina ya Santa Claus, hayamo popote ndani ya Biblia. Hata hivyo, Mtakatifu Nikolas Saint Nicholas (Baba Krismasi Santa Claus) alikuwa ni mtu halisi, Askofu, ambaye alizaliwa miaka 300 baada ya Yesu. Kwa mujibu wa hekaya za kale, alikuwa ni mtu mwenye huruma mno na alitenga nyakati za usiku kwenda kutoa zawadi kwa mafukara. Baada y a k i f o c h a k e Desemba ya 6, watoto wa shule huko Ulaya walianza kusherehekea siku hiyo kwa karamu kila mwaka. Baadaye Malkia Victoria, aliibadilisha sherehe hiyo kutoka Desemba ya 6 kuwa ni Desemba ya 24 kuamkia Krismasi.

10

Makala/Tangazo

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013


vitandani, mito na foronya zake. Mtu alipaswa kuchukuwa dawa zake na hata chakula chake mwenyewe. Huduma pekee, ambayo hospitali hiyo ilitowa ilikuwa ni wale madaktari mafedhuli wasio hisia hata chembe kwa kuchanganyikiwa na maisha. Dokta Abokor, akiwa na mawazo ya kimaendeleo na kimabadiliko, akaamua kushirikiana na wenzake kuleta matumaini mapya katika Hargesia. Yeye na wenzake wakaamuwa kuanzisha kampeni ya makusudi ya kuwasaidia watu wa eneo hili. Na kwa kuwa tokea hapo watu hawakuwa wavivu walishirikiana vizuri na kujenga ustawi wa Hargesia mpya, wakaamuwa kuwashajiisha wasomi wazawa ambao walikuwa sehemu mbali mbali za ulimwengu kurudi kwao kuja kuwasaidia watu wao. Mwito huu ukaitikiwa kwa kishindo. Ndani ya mwaka mmoja tu, wasomi wa kila fani wa kisomali wakawa wanamiminika kila siku. Wengine walikuwa ni walimu, madaktari, wahandishi, wachumi, wafanyabiashara na wengi wengineo. Kila mmoja akijitolea kuisaidia Hargesia ikaanza kunawiri na kupendeza. Wahisani nao, kwa kuona kuwa watu wa hapa walikuwa na moyo wa kujisaidia wenyewe, wakaamuwa kuwaletea misaada yao moja kwa moja. Kundi la madaktari wa kijerumani likaleta vitanda vipya, mashuka, vyakula gari la wagonjwa, madawa na vifaa vyengine vya hospitali. Hata zile dawa ambazo zilikuwa hazipatikani kwa raia wa Somalia ila kwa wale waliokuwa na jamaa zao katika nchi za Kiarabu, sasa zikawa zinapatikana hapa hapa na wagonjwa wakawa wanatoka miji ya jirani kufuatia huduma za matibabu hapa. Kuna kujitolea na kuwa mzalendo kama huku? Kumbe jambo hili lilikuwa linawakera sana wakubwa

AN-NUUR

Na Ibrahim Mohammed Hussein


MAELEZO machache kuhusiana na masaibu yawapatayo wanaharakati walio na fikra tofauti wa watawala wao. Imenilazimu kutoa mifano michache ili tuweze kuelewa vyema habari hiyo kwa manufaa ya kuwepo misukosuko iliyowakabili watu wa aina hiyo. Ni jambo la kawaida jamii inapokua chini ya utawala ulioziba masikio, na macho na nyoyo, watawala hupenda waachiwe tu wafanye watakavyo. Wao huamini kwamba nchi na raia kuwa ni milki yao. Anapotokezea mtu kuwasahihisha, basi humchukulia kuwa ni adui yao nambari moja, na hivyo hujihalalishia kumuadhibu kwa namna yoyote waionayo wao inafaa. Amma mimi, ukosoaji nauona kuwa ni nyenzo moja muhimu sana katika kuleta mabadiliko na maendeleo, mimi mkosoaji namuhesabu ni miongoni mwa wanaharakati. Sioni kwamba ni jambo sahihi kuwageuza wanaharakati kuwa wahanga wa watawala wasiotaka mawazo tofauti, badala yake ninadhani ni wajibu wa watawala hawa kubadilika kwa mujibu wa matakwa ya umma, ambao mara nyingi huwasilishwa na wanaharakati hawa. Ukweli watu hawa si maadui kwa utawala unaokubali kubadilika kwa mujibu wa wakati ulivyo. Hawa huwa ni muhimili mkuu wa usaidizi. Kosa moja kubwa la watawala wetu ni kuamini kuwa msaidizi wao ni Yule tu anaewaitikia Ndiyo Mzee na kwamba Yule anaesema hapana Mzee ni adui yao. Hii ni dhambi kubwa. Hii ndio tabia ya watawala wakaidi wa mabadiliko, kwa bahati mbaya sana, ni kuwa tabia hii ya kuwatawala watu kwa kutumia mkono wa chuma, haibadili tabia ya mwanaadamu ya kupinga walionalo silo. Na ndio maana kote ulimwenguni tawala za aina hii zimepata kuweko upinzani dhidi yake huzidi kukuwa kila dakika. Ukweli kila watawala wakaapo, hawawezi kutanafasi nafsi zao, maana macho yote ya umma huwakodolea wao na vinywa vyao huhanikiza sauti muundo huo hatuutaki,hatuutaki. Mwangwi wa sauti hizi na miono yao ni vitu vinavyoudhi sana mbele ya hadhara ya mtawala, lakini si vitu vinavyoweza kuepukika ikiwa

mtawala huyo hakubali mwito wa mabadiliko, kila mtawala akizidi kuwa muimla, ndipo anapozidi kuzalisha sauti zinazomsuta na macho yanayomkodolea. Hizi ni sauti na macho ya watu waliojitolea kumwambia mtawala wao makosefu yake na kumwonesha njia. Na kwa kuwa aina hii ya utawala huambatana pia na ujigambo na majivuno, mtawala hujihisi kupadwa na kichaa ikiwa ataambiwa kuwa ana makosefu Fulani na Fulani. Maana kwa kila hali, huwa kilevi cha madaraka kishamlevya na zile andasa zake humdanganya kwamba yeye yu mkamilifu sahihi kabisa, hawezi kuwa na mapungufu yoyote yale. Basi hapo hucharukwa na kuanza kumuadhibu kila anayehoji hadharani hoja hiyo iwe na nguvu ya hoja kiasi gani. Na kila anavyoadhibu kwa ulimi wake, kwa mikono yake, kwa jela, kwa risasi, kwa vurugu na kwa kila kitu, lakini bado wanaharakati huendelea tu. Dunia imejaa mifano ya visa na mikasa kama hii, vitabu vya historia na fasihi vimejaa hekaya za tanbihi, sasa ni juu yetu kufundishika, ikiwa kweli tu watu wa kuzingatia kutokana na maandiko. Yaliyomtokezea Socrates, mmoja kati ya wanaharakati wa kale, kilichomchongea Socrates ni uthubutu wake wa kuwapa changamoto watukufu na watendaji wa Serikali ya Athens juu ya uadilifu na elimu yao. Socrates alikuwa akitumia mbinu ya uandishi na uchambuzi wa mambo yaliyoonekana ya kuwaida tu, lakini muhimu sana kwa maisha ya watu, kama vile imani juu ya Mungu, ururi wa matendo, uadilifu, ilimu, maumbile na kadhalika. Mbinu hii ilivuta umma wa watu, wengi wao wakiwa vijana, ambao walimchukulia kuwa kigezo chao, kama ilivyo hapa petu sasa. Wanaharakati wanavyochambua masuala muhimu kwa maisha yao, kama vile Muungano, Mafuta, Sarafu, kiti cha Zanzibar katika umoja wa Mataifa na kadhalika. Kupitia uchambuzi na uadishi huu, huwa inatowa changamoto kwa watawala na kuuhoji udhaifu wao. Hilo hawalipendi hata kidogo. Katika Phaedo, kitabu kilichoandikwa na plato, aliyekuwa mwanafunzi wa Socrates, tunamsikia mwenyewe akijitetea mahakamani wao (watawala) hukereka mno na hili, nasi kuwa wanakerwa na udhaifu wao walionao, bali kwa kuwa udhaifu wao umedhihirishwa na kubainika, basi hushika kunilaumu na kunichukia mimi Khatima ya kukereka huku kwa wakubwa ikiwa ni kumtoa muhanga Socrates, ambaye tunaweza kumwita kuwa ni aalim mkubwa wa wakati wake na mwanaharakati jasiri. Alishitakiwa kwa makosa wawili la kwanza kusambaza mafundisho ya kumkana

Wako wapi leo wateswa na watesaji?


Muungu, na la pili ni kupandikiza mbegu ya udadisi kwa vijana ambayo uthubutu wa kuukosea hishima utawal wao Makosa haya mawili yalimhalalishia adhabu ya kifo. Naye licha ya kupewa fursa na watawala ya kujitetea ili asalimishe roho yake na mauti, kwa kuahidi kuwa angeliwacha kabisa kazi hii, mwanaharakati Socrates alikataa kwa kusema:Waheshimiwa waungwana, licha ya kuwa mimi ni mtumishi niliyejitolea kwenu, lakini nina jukumu la kuonesha utiifu wangu wa kiwango cha juu zaidi kwa Mungu wangu na sio kwenu nyinyi, na madhali ninaendelea kuvuta pumzi na kuendelea kubarikiwa vipawa hivi nilivyonavyo, basi kamwe sitaacha kuifanya kazi hii ya kuufunuwa ukweli kwa kila mtu nimkutayena sitaliacha hili, hata kama itabidi nife mara mia moja! Masikini Socrates, akafa kwa kuamriwa na Mahkama anywe sumu. Maisha yake yalizimwa, lakini ukweli ni kuwa ameendelea kutukuzwa hadi leo hii ulimwenguni. Hayo ndio malipo wayalipayo watawala wasiopenda kubadilika.Heri afe mtu mmoja lakini lisiangamie taifa zima Watawala wa aina hii hawahitaji sababu kubwa ili wapate kumvamia raia wake wanayemuhisi kuwa ni hatari kwao. Vile kuwa tafauti na wao tu, ni sababu inayotosha kabisa kukupambanisha na ghadhabu ya dola. Kama unahitaji kuishi salama usalimini chini ya tawala kama hizi, basi ni kukubali kuwa kama vile wakutakiavyo wao. Uitikie wimbo waimbao, ucheze ngoma waipigayo, usioneshe tofauti yeyote ile hata vile ukiimba basi ukighani vizuri kuliko wao watalihesabu ni tendo la kiadui.

Kuna kisa kilichoelezewa na Dokta Adam Yussuf Abokor kinachoelezea:- kwa nini tulikamatwa kisa hicho kimo katika kitabu kiitwacho The Cost of the Dictatorship Lilian Barber press, Inc., 1995 cha Jama Mohamed Ghalib, Dokta Abokor anasema kosa kubwa lilosababisha yeye na wenzake wakamatwe na kufungwa jela zaidi ya miaka sita, wakipewa mateso makali ya kimwili na kiakili, lilikuwa ni kujaribu kuleta maendeleo katika mji wa kwao wa Hargeisa, ambao ulikuwa umetupwa miaka nenda miaka rudi na utawala wa kidikteta wa Said Barre. Yeye binafsi akiwa daktari kwa taaluma na fani, alichangia sana kuifufua hospitali kuu ya Hargesia, ambayo licha ya kuwa kwake hospitali kuu na iliyotegemewa na watu wa eneo hilo, Serikali ilikuwa imeikana na kuinyima huduma yoyote ile. Alipopelekwa kuwa Mkurugenzi wa Hospitali hiyo katika mwaka 1980, alikutwa kila kitu kikiwa kimeshasambaratika. Maabara ilikuwa inafanyakazi kwa taabu sana kutokana na ukosefu wa vifaa na kemikali. Benki ya damu, idara za wagonjwa wa dharura na wagojwa wa nje zilikuwa zimefungwa. Mashine ya X-ray ilikuwa haifanyikazi kwa miaka miwili sasa kutokana na ukosefu wa filamu na pia uchakavu wa baadhii ya vifaa vyake. Makaro yalikuwa yameziba kabisa kabisa kiasi ya kwamba wagonjwa walilazimika kuvizia usiku uingie wakamalize haja zao nje. Alimuradi hali ilikuwa mbaya sana kiasi ya kwamba ili wagonjwa wapatiwe kitanda, walilazimika kuja na magodoro yao wenyewe, mashuka ya

Inaendelea Uk. 11

MWENGE EVENING SECONDARY SCHOOL (MESS) KWA KUSHIRIKIANA NA SMS MICROSOFT INTERNATIONAL COMPUTER, LANGUAGES AND ACADEMIC SOLUTIONS
Tunatangaza kuanza kutoa fomu za kujiunga na masomo kwa mwaka 2013 katika kozi zifuatazo: Sekondari ya jioni (Miaka mitatu) Wanaorudia mitihani (Re-sitters) Lugha za kimataifa - Kiingereza, Kiarabu na Kifaransa Kompyuta (Computer studies) Masomo ya Chekechea (Nursery School) WALENGWA: Wafanyabiashara, Wafanyakazi katika sekta binafsi na serikali, wanafunzi waliomaliza darasa la saba , wenye kipato kidogo, wake kwa waume na watoto wadogo kwa kozi ya chekechea. MASOMO: Basic mathematics, English, Civics, Physics, Geography, Kiswahili, History, Maarifa ya Uislam na Computer (kwa wale wa Sekondari) Fomu zinapatikana bure katika vituo vifuatavyo; Shuleni Mwananyamala; Kituo cha njiapanda ya Makumbusho, ndani ya majengo ya Islamic Club (Jirani na Msikiti wa gorofa). Msikiti wa Ijumaa Mwenge Osi za Vijana Osi za TAMPRO (Magomeni Mapipa) Masjid N-nuur, Sinza, Palestina (Muone Dada Aisha) Osi za gazeti la An nuur (Manzese, Tip Top) Osi za gazeti la Kisiwa (Kariakoo, jirani na shule ya Al-Haramain) Pia fomu zinapatikana katika tovuti zifuatazo; www.zidamaafoundation.org, www.eamuslim. com na www.lulunewspaper.com mwengevening@gmail.com/barsett@yahoo.com 0788 307 607, 0713 459 470, 0787 533 123, 0654 533 123 CHAGUA KUSOMA KWETU HUTAJUTIA UAMUZI WAKO NYOTE MNAKARIBISHWA!

NAFASI ZA MASOMO 2013

JUMUIYA ya Ukombozi ya Palestina imethibitisha kutowezekana kufumbia macho kiwango cha madhara na athari zitokanazo na mradi wa makazi wa E1, katika kuanzisha taifa la Palestina lenye faida na uwepo wa kijografia, huku mji mkuu wake ukiwa ni Jerusalemu ya Mashariki. Jumuiya imeongeza kuwa endapo mradi huo wa (E1) ukitekelezwa kikamilifu, utaikosesha Jerusalemu Mashariki maeneo yaliyobaki yanayo hakikisha ukuaji wa uchumi na maendeleo katika siku zijazo. Vilevile eneo la (E1) na ukubwa wake litahakikisha udhibiti wa barabara kwa Israeli, kwenye makutano ya barabara kuu inayo unganisha Kaskazini na Kusini mwa Ukingo wa Magharibi. Idara ya mapatano katika Jumuiya ya Ukombozi ya Palestina imesema kuwa hata kama mradi huu haukutekelezwa, hakika ukuta wa Adumim unaojumuisha maeneo haya hadi Israeli, utatenganisha kabisa Jerusalem Mashariki na Magharibi. Hatimae kuugawa pia Ukingo pande mbili juu ya msingi wa faida, huku ukivuruga kabisa utatuzi wa kuwepo dola mbili chini ya mji mkuu wake Jerusalem Mashariki. Jumuiya ya kimataifa inauona mradi huu kama ni msumari wa mwisho katika jeneza la ufumbuzi wa kuwepo dola mbili, ambao bado dunia inaona kuwa ndio ufumbuzi wa kumaliza mzozo uliopo kati ya Palestina na Israeli. Idara pia imesema kuwa mradi wa Adumim na matawi yake ukiwemo pia mpango wa upanuzi wa maeneo ujulikanao kama E-1, unazingatiwa kuwa

Palestina - mradi wa makazi ya Israel, kikwazo cha dola mbili


ni hatari mno katika mipango ya Israeli mjini Jerusalem Mashariki, kwani unatishia mshikamano wa maeneo ya Palestina. Mradi wa makazi wa Adumim upo katika miinuko iliyoanzia Mashariki mwa Jerusalem Mashariki inayokaliwa kimabavu, ambao ni mojawapo ya maeneo muhimu sana na yenye nguvu kimaendeleo na ukuaji wa kiasili wa Palestina unaotarajiwa. Hili ni eneo muhimu sana kimkakati, kutokana na uwepo wake kijograa Ukingoni mwa Magharibi na ukaribu wake na mji mtukufu na bonde la Jordan. Idara ya mapatano imesema kuwa, Israeli imejenga makazi mengi katika eneo hilo kinyume na sheria kama vile Adumim, Almon, Kifar, Alon, Kedari na sehemu ya viwanda iitwayo Mishor Adumim. Huku idadi ya walowezi wa Kiisraeli wanaoishi humo wakikia 41,700. Aidha idara imeongeza kusema kuwa makazi ya Adumim ni makubwa zaidi, kwani yana wakazi wapatao 36,000, huku eneo lake likiwa ni kilometa 50 za mraba, sawa na eneo la Telaviv, huku wakazi wa Adumim wakiwa hawavuki asilimia 10 ya wakazi wa Telaviv. Hata hivyo makazi haya yanaongezeka na kupanuka, kwani Israeli tayari imejenga nyumba zisizopungua 8,000 tokea mwaka 2001. Israeli toka mwaka 1975 imeweka msingi wa makazi ya Adumim kupitia misafara mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha udhibiti wa Jerusalem Mashariki na bonde la Jordan, huku ikijenga uhusiano wa kijograa na kikoloni kati ya maeneo hayo mawili ya mikakati. Israeli ilianzisha mtandao mkubwa wa barabara unaounganisha makazi ya Adumim na mengine, pia Jerusalemu Magharibi. Kama ilivyojenga barabara kuu (namba 1), kupitia Adumim upande wa Mashariki kuelekea bonde la Jordan. Kwa mujibu wa ripoti, Israeli inakamilisha ujenzi ukuta wa makazi ya Adumim na mengineyo, ili kutia nguvu na kupata wepesi wa kuyapanua zaidi hapo baadae. Ukuta huu unaomega ardhi ya Palestina kwa kilometa 14 za mipaka ya 1967, utapelekea pia kutaisha kilometa 58 za mraba za Palestina, huku ukikamilisha kugawa pande mbili Jerusalem Mashariki na sehemu ya Ukingo wa Magharibi. Kama Israeli ilivyoboresha mpango wake wa E1 kwa lengo la kuwepo uhusiano kati ya Adumim na Jerusalem Magharibi, itajenga pia eneo la ukubwa wa hekta 12,442 ya Palestina, kwenye maeneo ya Atana, Tur, Asawiya, Abudis na Aziziza. Huku ukitarajiwa ujenzi huo kutovuka makazi 3,500 yanayotosha walowezi 15,000. Vilevile watatenga eneo rasmi kwa ajili ya viwanda na biashara, maofisi, michezo, burudani, mahoteli na makaburi. Waziri Mkuu wa zamani wa Israeli Izhak Rabin ndio wa kwanza aliyetaka kuandaa mpango wa E1 mnamo mwaka 1994, pale ulipo pambamoto mchakato wa amani, huku ukitangazwa rasmi mpango huo mwaka 1999 ikiwa katika utawala wa Waziri Mkuu Netanyahu wa kwanza. Israeli iliwanyanganya Wapalestina ambao ndio wamiliki wa ardhi hiyo kwa miaka mingi iliyopita. Mnamo mwaka 2002 Wizara ya Jeshi ya Israeli iliridhia kutekeleza mpango huo wa E1, kisha Waziri wa Jeshi wa wakati ule Ben-Eliezer aliiahidi Marekani kutotekelezwa kwa mpango huo, huku ikitilia mkazo kuhakikishiwa usawa ifikapo mwaka 2005 na 2009. Idara ya mapatano imesema kuwa pamoja na hayo, Wizara ya Nyumba na Ujenzi ya Israeli ilianza kujenga mwaka 2004 katika eneo la E1, tayari imejenga vituo viwili vya polisi, kimoja kipo kati ya eneo la Zaimu na Anata, huku cha pili kikiwepo Mashariki ya Mbali ya eneo la E1, katika barabara namba 1 inayoelekea makazi ya Adumim. Serikali ya Israeli imewekeza zaidi ya Shekeli milioni 200 ambazo ni sawa na dola milioni 52 za Marekani, ili kuandaa miundo mbinu katika eneo la E1, ikiwa ni andao la ujenzi wa makazi ya walowezi na miradi mingine. Idara imeongeza kuwa, limewekwa tangazo katika njia namba 1 ya E1, linasema Karibuni katika makazi ya Masit Adumim, hii inajulisha kuwepo makazi mengine mapya katika eneo hili hivi karibuni. Septemba mwaka 2007, jeshi la Israeli limepanga kutaisha eneo la ukubwa wa dunum 1,128 kutoka ardhi ya Palestina iliyopo kati ya Jerusalem Mashariki na Adumim, kwa lengo la kupasua barabara mbadala kwa Wapalestina, itokayo Ukingo wa Magharibi hadi maeneo ya Mashariki na Kaskazini. Huku maeneo pekee litalobaki kwa Wapalestina ni Abu Dis, Sawareh, Nabii Musa na Khan Nyekundu. Barabara hii imepangwa kupita maeneo ya Kusini na Mashariki ya ukuta wa

11

Makala

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013

AN-NUUR

Inaendelea Uk. 10
wa Mogadishu, lilikuwa linahatarisha utukufu wa ulwa wao. Lilikuwa linawadhalilisha kwa kuonekana kuwa wao hawafai kitu, maana jambo lililowashinda watawala kwa miaka 34, sasa lilikuwa limefanywa na raia kwa mwaka mmoja tu. Kwao hilo lilikuwa tusi Novemba 2,1981 mtu wa kwanza miongoni mwa wale wasomi waliojitolea akaanza kukamatwa, November 19, ikiwa ni zamu ya Dokta Abokor mwenyewe kuwekwa kizuizini. Tena ukamataji ukaendelea hadi wakakia 29, wote watu muhimu katika jamii wote wanaharakati waliojaribu kuleta mabadiliko kwao. Mashitaka walioshitakiwa ni kuunda kundi la kupinga Serikali na kupanga njama za kupindua Serikali ya Said Barre. Miongoni mwao wakahukumiwa vifungo vya maisha kama Ahmed Mohamed Yussuf, aliyekuwa mwalimu bingwa

wa FIZIKIA na Mohammed Barrood Ali, aliyekuwa mkemia wa viwanda. We n g i n e 2 2 w a k a p e w a kifungo cha miaka 30 kila mmoja, na adhabu nyengine za vifungo tafauti kwa watu kadhaa wa kadhaa. Hilo ndilo lililokuwa lipo la wanaharakati hawa, ambao hakuna msamiati wowote unaotosha kuzitaja sifa zao kwa ukamilifu. Watu hawa baadae waliachiliwa wakiwa wameshatumika zaidi ya miaka sita jela, kutokana na shinikizo la vijana na wanafunzi, ambao walikuwa wakiandamana kila siku ya February 20 kuwakumbuka wanaharakati hawa na kupinga kukamatwa kwao. Hata hivyo, maandamano haya hayakumalizika bure tu, maana inakisiwa kuwa zaidi ya wanafunzi hamsini waliuwawa kwa mumiminiwa risasi na askari

Wako wapi leo wateswa na watesaji?


wa Said Barre. Lengo langu ni kuonesha kwamba kazi ya mwanaharakati ni ngumu. Hata hapa Zanzibar wanaharakati wengine wamekumbwa na khabari nzito nzito ambazo zinataka wakati wa kuzungumzia habari hizo mfano wa Kassim Hanga, Twala Mdungi, Othman Shariff, Babu na makumi kwa mamia yawengine. Wengine walipotea kiajabu ajabu, kuna waliopaswa kuihama nchi yao, kuna waliodhalilishwa na kuteswa kwa mateso mabaya mabaya na wengine wao yaliwafika kwa kusema hivi sivyo, hilo silo, kwa kuhoji hoji kwao kusiko kwisha. Lakini dunia shimo la sahau, leo hii wa wapi wateswaji na watesaji? Wote hao watapokea hukumu yao mbele ya Mwenyezi Mungu. Qur-ani juzuu ya 3 Surat AlImran aya ya 21 inasema:Wale watu wanaowauwa watu waamrishao haki wabashirie adhabu kali. Sio kuwauwa hata kuwatesa kwa sababu ya yale waliyoyasema yalikuwa ni ya haki, basi utapokea adhabu yake kuanzia hapa hapa duniani na huko unakoelekea ambapo muda sio mrefu akhera ndipo utaipata vizuri picha ya matendo yako. Wala tusidanganyane kwa kufikiri kwamba tunawapa wapenzi wetu tiketi za bure za kwenda kuhiji kwamba wataweza kukuombea watapoka kwenye sehemu takatifu ya msikiti wa Makkah. Kur ani surat Al munafiqun ni sura ya 63 aya sita inamwelezea Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba:Sawasawa kwao, ukiwatakia maghfira au hukuwatakia maghra (msamaha) Mwenyezi Mungu hatawaghufuria (hatawasamehe). Sasa hebu angalia ikiwa Mtume wa

Adumium nje ya makazi ya Adumim, mwishowe itawazuia Wapalestina kutumia barabara namba 1 inayopitia eneo la E1, pia barabara namba 60 inayoka Jerusalem Mashariki, hatua itayowazuia pia kuingia eneo hilo. Hatua hii inafanana na mojawapo ya barabara za manispaa ya Maale Adumim mnamo Aprili 2005, yote haya yanalenga kuwabana Wapalestina na kuwapa nafasi walowezi waishio kinyume na sheria. Kwa mantiki hii raia wa Palestina wapatao zaidi ya 3,000 wa kabila la Jahalin waliopo tokea miaka ya hamsini katika karne iliyopita, katika maeneo kati ya Jerusalem Mashariki na bonde la Jordan. Hatari ya kuhamishwa na kutolewa kutoka katika maeneo yao, ni jambo linalowapata Waarabu wa kabila la Jahalin kwa mara ya tatu, baada ya kufukuzwa mwaka 1948 kutoka maeneo ya Nakib, pia Adumim mwaka 1998 na leo wanataka wahamishwe kutoka maeneo ya E1, ili kupisha upanuzi wa makazi hayo. Idara ya mapatano inasema tena kuwa harakati za upanuzi wa makazi ya walowezi unaofanywa na Israeli ni kinyume na sheria, kwani unapingana na kanuni ya 49 ya makubaliano ya nne ya Geneva, kinachozuia uvamizi wa ardhi kwa nguvu. Hatua hii pia inakiuka haki ya Wapalestina ya kujitawala na kujiamulia mambo yao, huku ikienda kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 242 na 338, pia Mahakama ya haki ya kimataifa, vilevile inapinga mtazamo wa nchi nyingi duniani katika rai hii.

Mwenyezi Mungu anaelezwa maneno hayo, wewe mwenzangu uliyezijaza chuki dhidi ya Muislamu mwenzako hiyo tiketi uliyopewa wende Makkah kwa kuwaombea wakubwa ambao kazi zao ni kupanga ubaya dhidi ya binaadanu wenzake ambao husema yaliyo ya haki, itasaidia nini jamani? Haya viongozi wetu lazima wayazingatie. Sisi sote ni Waislamu tumezaliwa katika nchi moja haifai kutendeana maovu na hasa pale yule unayemfanyia anayosema ni ya haki. Ukifanya ubaya basi ujuwe mahkama ya mwanzo itakayokusumbua ni mahkama ya nafsi yako. Nafsi yako itakukosesha raha itakapokunongoneza kwamba umefanya ubaya dhidi ya mwenzako, nafsi haitoacha kukulaumu hadi dakika ya mwisho wa uhai wako. Sasa unakwenda kwenda kwenye mahkama ya Mwenyezi Mungu kusomewa uovu wako uliokuwa ukiupanga usiku na mchana dhidi ya viumbe wa Mwenyezi Mungu.

AN-NUUR
12
Na Bakari Mwakangwale

SAFAR 1434, IJUMAA DESEMBA 28, 2012 - JANUARI 3, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

Maaskofu waikana Krismasi


IMEELEZWA kuwa si sahihi kwa Wakristo kusheherekea sikukuu ya kuzaliwa Yesu Kristo, kila ifikapo Desemba, 25, kwa kuwa siku hiyo haipo katika maandiko. Hayo yamebainishwa na baadhi ya Maaskofu Jumanne wiki hii, Desemba 25, siku ambayo Wakristo, waliadhimisha kuzaliwa kwa Yesu. Wa k i o n g e a k a t i k a kipindi maalum na kurushwa hewani na Shirika la utangazaji la BBC, Maaskofu hao wamewataka Wakristo kutumia siku hiyo kutafakari na kutafuta siku sahihi aliyozaliwa, Yesu (Nabii Issa) huku wakilinganisha na usemi wa mtaani kuwa kwa kusherehekea Krismasi, Desemba 25, ni sawa na kuingizwa Chaka. Kama alivyotangulia kusema, mchungaji mwezangu, hii ni kama siku ya mapumziko, watu hawaendi kazini kwa hiyo ni vizuri zaidi ikawa ni siku ya familia, lakini kusema kwamba ndiyo Yesu kaziliwa, kwa kweli kama ingekuwa nazungumza kwa lugha ya mjini ningesema tunaingia chaka. Alisema Mchungaji Carlos Kilimbai. Mchungaji Kilimbai, alisema tarehe sahihi ya kuzaliwa Yesu haijulikani, hivyo ni vyema kutumia siku hiyo kutafakari juu ya kuzaliwa kwake kwa kufanya hivyo alidai itakuwa ni jambo jema zaidi. Alisema mpaka sasa kuna makundi mawili ya Makanisa yaliyopo Jijini Dar es Saalam, tayari hayasheherekei sikukuu hiyo ya Krismasi, Desemba 25, hii alidai huenda baada ya kuona ukweli kuwa siku hiyo haipo katika maandishi. Akianisha makundi hayo ambayo tayari yamejipapatua na kujiepusha na Sikukuu hiyo, alisema kundi moja ni la muda mrefu na kwamba wao hawana Krismasi kabisa, huku akilitaja Kanisa la Seventh Day Adventist. Mchungaji huyo alisema, kutokana na hali hiyo, hawezi kuwahukumu wale ambao hawaadhimishi na vilevile alidai hawezi kuwahukumu wanaoadhimisha pamoja na kuwa wanaadhimisha siku isiyo sahihi. Lakini kuna kundi la pili jipya ambalo limetokea hivi karibuni hilo kundi limebadilisha siku, sasa hiyo nayo ni ajenda nyingine itabidi nayo ifanyiwe kazi, mimi kama mwalimu walinifuata wakanieleza kuhusua suala hilo kwamba hii siku wao wameibadilisha, wanaadhimisha siku yao nyingine lakini siyo hii ya Desemba 25. Alisema Mchungaji huyo. Alisema, yeye kama Mchungaji (Kilimbai) kilichomfanya kutaka kujua uhalali wa siku hiyo ya kuzaliwa Yesu, ni baada ya kuikosa katika Biblia na hata katika Injili kwamba Yesu hakusheherekea katika Kanisa la Matendo, na katika nyaraka za Mtume Paulo, pia hakuona tarehe hiyo. Akijibu swali la mtangazaji ni vipi anaongoza watu wanaoka Kanisani kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo, huku akijua kwamba haipo, Mchungaji Ngonyani, alisema kuwa huwezi kubadilisha kra ya mtu kwa siku moja, hususani kwa mambo ambayo yamekuwepo karne na karne. Kumbuka ni toka karne ya tatu haya mambo ndiyo yameanza rasmi na kuwepo hadi hivi sasa, na kumbuka kihistoria Kanisa lilikuwa moja toka Karne ya kwanza mpaka karne ya kumi na tano, sasa kama Kanisa lilikuwa moja nakumbuka mamlaka ya Kanisa ilikuwa imetangaza kwamba ni siku ambayo itaazimishwa kuzaliwa kwa Yesu. Sasa siku hiyo, ipo katika nyoyo za watu imo katika kra za watu na ipo katika Ulimwengu mzima. Alisema Mchungaji Kilimbai. Alisema, kutokana na hali hiyo anaweza asiwe na mamlaka ya kubatilisha hilo na hata kama angekuwa nayo, alisema bado huwezi kubadilisha utamaduni ambao umekwenda kwa miaka mingi. Kutokana na ugumu huo, Askofu Kilimbai, alisema ushauri wake na ombi kwa Wachungaji na Maaskofu, wenzake popote walipo ikiwa ndani ya Tanzania au nje, ni kuanza kuwafundisha watu (Wakristo) ukweli kwamba hii tarehe siyo ambayo Yesu amezaliwa. Tuangalie uhalisia wa kuzaliwa kwa Yesu, kwamba (Yesu) anapaswa kuzaliwa ndani ya nyoyo za watu, waache matendo maovu, ili Yesu akija aweze kuwanyakua waweze kwenda Mbinguni, hilo litakuwa ni jambo la maana zaidi, kuliko kuwaaminisha kuwa Desemba 25 ni siku ya kuzaliwa Yesu. Alisema

USTADH Habib Othman Mazinge na kuasa. Akiongea na An nuur, kufuatia kauli za Maaskofu hao, Mhadhiri maarufu wa mihadhara ya kidini nchini na nje ya nchi, Ustadhi Habib Othman Mazinge, alisema kutokana na kukiri kwa Maaskofu hao juu ya Sikuku ya Krismas kuwa ni uzushi Serikali, iifute sikukuu hiyo. Alisema, kama viongozi wenye dini yao wamekiri, kile ambacho yeye na Waislamu kwa ujumla wamekuwa siku zote wakikisema kuwa sikukuu hiyo ni uzushi, ni vyema ikafutwa ili Watanzania wakawa wanaendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa. Alipoulizwa tarehe halisi ya kuzaliwa Yesu (Nabii Issa) kwa mujibu wa maadiko, alisema kiukweli siku halisi haijulikani, kwani kwa upande wa Quran, imesema kwamba Nabii Issa (Yesu) alizaliwa katika mji wa Bethelehem, lakini haikutajwa tarehe. Ust. Mazinge, alisema kwa upande wa Biblia, anaungana na Maaskofu hao kwani hakuna sehemu ilitajwa tarehe ya kuzaliwa Nabii Issa (Yesu), lakini alidai mara nyingi anapokuwa katika mihadhara, linapokuja swala hilo, wao (Wakristo) hutoa ushahidi wa Yeremia 52:31. Tarehe hiyo, imetajwa katika Biblia, kama siku ya kutowa wafungwa gerezani, ikisema katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi., mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani. Hukuti mahala tarehe hiyo ikisema ndiyo alizawa Yesu. Alisema Ust. Mzinge. Mara nyingi Ustadhi Mazinge, akiwa jukwani katika Mihadahara yake ya Biblia, hunadi kwa kutoa changamoto kuwa ajitokeze Mkristo, Mchungaji, Padri au Askofu, aonyeshe katika Biblia au Qur an, tarehe ambayo Yesu.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like