Professional Documents
Culture Documents
TAARIFA KWA UMMA (Kima Cha Chini Cha Mafao Ya Wastaafu)
TAARIFA KWA UMMA (Kima Cha Chini Cha Mafao Ya Wastaafu)
1.0.
Mnamo mwezi Julai mwaka 2015, Wizara ya Fedha kupitia Tangazo la Serikali Na. 285 la
tarehe 30/6/2015 (the Public Services Retirement Benefits (Minimum Pensions)
Order, 2015 (Government Notice No GN N. 285 of 30/06/2015) baada ya kuridhiwa na
Bunge, ilipandisha kima cha chini cha malipo ya mafao kwa wastaafu chini ya kifungu cha
30 cha Sheria ya PSPF. Kwa mujibu wa Tangazo hilo, kima cha chini kwa malipo ya
pensheni ya kila mwezi kiliongezeka kwa kiasi cha shilingi 45,000/- pamoja na asilimia 10
ya mafao ya zamani na hivyo kufanya kima cha chini kupanda kufikia kiasi cha takribani
Shilingi laki moja (100,000/=).
2.0.
3.0.
Aidha, ni muhimu ikaeleweka kwamba, utaratibu wa kuweka kima cha chini cha mafao
kwa wanachama wa Mifuko ya Msingi (Mandatory Schemes) yaani NSSF, PPF, LAPF,
PSPF, GEPF, NHIF & WCF umeainishwa katika kifungu cha 25 cha Sheria ya Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 kikisomwa pamoja
na kifungu cha 36 cha Sheria hiyo. Kwa mujibu wa vifungu hivyo, kima cha chini cha
malipo ya mafao ya wastaafu hupangwa na Mamlaka baada ya kufanya tathimini
(Actuarial Valuation) na kushirikisha wadau. Lengo la kufanya tathimini kabla ya
kupandisha kima cha chini cha malipo ya mafao ni kujiridhisha juu ya uwezo wa Mfuko
husika kubeba ongezeko linalopendekezwa. Kwa kupitia utaratibu huu, mwaka 2014
Mamlaka ilitengeneza na kutoa Kanuni za Uwianishaji wa Mafao (Pensheni Benefit
Harmonisation Rules). Kanuni hizi pamoja na mambo mengine zinaainisha kima cha chini
cha malipo ya mafao kwa wastaafu kuwa ni asilimia 40 ya kima cha chini cha mshahara
wa Sekta husika. Kununi hizi zinatumika kwa Mifuko ya Msingi ambayo ni NSSF, PPF,
LAPF, PSPF & GEPF.
4.0.
Vile vile katika jitihada za kuendelea kuimarisha Sekta, Mamlaka imekamilisha zoezi la
kufanya tathimini ya Mifuko na Taarifa ya Mtathmini hiyo ipo katika hatua ya majadiliano
na wadau wakiwemo wawakilishi wa wanachama. Pamoja na mambo mengine, taarifa
hiyo itakuja na mapendekezo mahsusi ya namna bora ya kuboresha mafao ya
wanachama. Hivyo, Mamlaka inawasihi wanachama na wadau wengine wote wawe na
subira wakati huu ambao taarifa ya Mtathimini inafanyiwa kazi.
Imetolewa na
Kitengo Cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar Es Salaam