You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA


MALIPO YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT) KATIKA SHUGHULI ZA
UTALII

Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 (Finance Act 2016) inaelekeza kufutwa kwa
msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye shughuli za Utalii.
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), iliyochukua jukumu
la Usimamizi wa Wanyamapori ambalo lilikuwa chini ya Idara ya Wanyamapori
kwa maeneo yaliyo nje ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kuanzia tarehe 01 Julai 2016, Inawajulisha
wateja wake wote kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2016, itaanza kutoza kodi hiyo
kwa kiwango cha asilimia 18 kwenye tozo zote zitakazolipwa kupitia huduma
mbalimbali.
Imetolewa na:
KAIMU MKURUGENZI MKUU,
MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA
S.L.P. 2658,
MOROGORO
Simu: +255 769 900 909

You might also like