You are on page 1of 1

Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limetoa wito kwa wateule

wa JPM wakuu wa mikoa wakiwemo wakuu wa Wilaya kupatiwa


semina elekezi ili wajifunze mifumo na utendaji wa utumishi wa
umma kwa madai kuwa wengi wao hutumia vibaya madaraka
waliyopewa.
Hayo yamesemwa na Katibu wa baraza hilo, Julius Mwita
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam, amesema kuwa baraza hilo limefikia hatua hiyo mara
baada ya viongozi wake kukamatwa mara kwa mara kwa amri ya
wakuu wa Wilaya na Mikoa.
Kwa upande wake Wakili wa kujitegemea, Juma Nassoro
amesema kuwa Sheria ya Tawala za Mikoa namba 19 ya mwaka
1997 vifungu vya 7(9) na 15(9) vinatoa maelekezo kuwa endapo
kiongozi husika atabainika kutumia vibaya madaraka yake
anaweza kushtakiwa chini ya Sheria ya Makosa ya Jinai.
Kiongozi hana mamlaka ya kumweka mtu ndani kama adhabu,
bali anakamatwa ili afikishwe mahakamani ndani ya saa 48,
hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kumwazibu mtu
mwingine isipokuwa Mahakama,amesema Nassoro
Hata hivyo, siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la
ukamatwaji wa viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo
mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee, Meya wa Ubu8ngo,
Jacobo Steven, mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea na
Ester Bulaya wa Bunda mjini.

You might also like