You are on page 1of 5

DONDOO ZA KIKAO CHA WIKI - IDARA YA UTAFITI

KIKAO CHA 39 WIKI YA 49 CHUMBA NAMBA A 819


TAREHE: 01/12/2015

A. MAHUDHURIO

Na. Jina Kifupi Maelezo


1 Sabina Daati SPD Mwenyekiti
2 Samwel Kessy SAM Udhuru nje ya ofisi - Safarini
3 Gwalusako Mwaipopo GM Mjumbe - Likizo
4 Aurea K. Bigirwamungu AB Mjumbe
5 Ahmed Mwenda AM Katibu
6 Baraka Kanyika BK Udhuru nje ya ofisi – Likizo
7 Josephat Marandu JM Mjumbe
8 Jesca Samwel JS Udhuru nje ya ofisi - Likizo
9 Seleman Mayanjo SM Mjumbe
10 Stewartness Makiko SSM Mjumbe

B. AGENDA

1. Kufunguliwa kikao.
2. Kupitia muhtasari wa kikao kilichopita
3. Mpango kazi wa idara ya utafiti kwa wiki ya 49.
4. Mengineyo.
5. Kufunga kikao.

1
DONDOO ZA KIKAO CHA WIKI - IDARA YA UTAFITI
KIKAO CHA 39 WIKI YA 49 CHUMBA NAMBA A 819
TAREHE: 01/12/2015

Na Yaliyojadiliwa na Mpango Kazi


1. Kufunguliwa kikao:
Mwenyekiti SPD alifungua kikao rasmi saa 03.15 asubuhi na kumteua AM kuwa Katibu
wa kikao. Mwenyekiti alianza kwa kuwakaribisha wajumbe katika kikao na kumuomba
mjumbe AB kupitia dondoo za kikao kilchopita.
2. Yatokanayo na kikao cha 37:
 Mjumbe AM bado anaendela na kuandaa “Management Paper” kwa ajili ya pendekezo
la matumizi bora ya umeme kupitia mfumo wa “Smart grid" na pia ataendelea na
zoezi la kuwasilisha mapendekezo kwa ajili ya bajeto ya 2015/2016
 Mjumbe AB ataendelea kukusanya na kujumuisha pamoja maoni na mapendekezo ya
Bajeti ya 2016/2017 kutoka kwa kila mmoja wa idara ya Utafiti.
Ataendelea na zoezi la uandaajai wa pendekezo la kuweka mifumo mchanganyiko ya
umeme katika kisiwa cha Mafia kwa kusoma jinsi nchi nyingine zilivyofanya na
kufanikiwa katika hili pendekezo. Mwenyekiti SPD aliongezea kwamba zoezi la
utafutaji wa eneo la mradi huu bado linaendela na kuna matumaini makubwa kwa
eneo kupatikana.
 Mjumbe AB na mjumbe SSM bado wanaendelea na zoezi la ufatiliaji wa kibali cha
kupata ardhi kwa ajili ya umeme mbadala wa upepo katika mkoa wa shingyanga.
 Mjumbe JM ataendelea kuandaa mapendekezo kwa ajili ya bajeti ya 2015/2016 na
pia atamalizia uandaaji na uwasilishaji wa ripoti ya mzunguko wa manjinia mikoani.
 Wajumbe JM na SM waliwasilisha ripoti ya Kigoma kwa meneja utafiti kuhusu
kupunguza matumizi ya mafuta katika uzalishaji wa umeme.
 Mjumbe SM anaendelea kuandaa ripoti ya ERB na kwa sasa yupo katika sehemu ya
kwanza.
 Mjumbe SSM,AM,JM,SM walikua na zoezi la kufuatilia usomaji wa mita za AMR katika
kanda ya Dar es salaam ambazo hazitoi hazisomi na kutoa ripoti kwenye mtando wa

2
DONDOO ZA KIKAO CHA WIKI - IDARA YA UTAFITI
KIKAO CHA 39 WIKI YA 49 CHUMBA NAMBA A 819
TAREHE: 01/12/2015

TANESCO. Zoezi bado linaendelea na mwenyekiti aliwashauri waandike ripoti kwa


ajili ya zoezi hili
 Mjumbe SSM bado yupo kwenye mchakato wa kufuatili eneo kwa ajili ya kujenga
plant ya umeme jua kutoka kutoka mkoa wa Dodoma,Singinda na wilaya ya Same.
 Kwa upande wa Dodoma bado anasubiria mrejesho kutoka kwa muhusika(Afisa
manispaa ya Dodoma) ambae amesafiri kwa sasa.
 Kwa mkoa wa Singida ni kwamba bado TANESCO hawajatuma barua ya kuomba eneo
husika. Mwenyekiti alipendekeza kwa sasa tuombe eneo la Manyoni.
na kubaini ya kuwa kulitokea tofauti kati ya manispaa ya dodoma na waadhirika
kwani Manispaa walitathmini mita ya mraba moja kufanyiwa malipo ya TZS 1000
tofauti na TANESCO ambao walitathmini ya ardhi kuwa na gharama ya TZS 5000 kwa
mita ya mraba moja.
3. Mpango kazi wa idara ya utafiti kwa wiki ya 48:
 Mwenyekiti SPD aliagiza wajumbe wote chini ya kitengo cha utaafiti kuandaa bajeti
ya 2016/2017 wakizingatia zile kazi wanazopanga kuzifanya ili kila mmoja awe na
vitendeakazi ili kukamilisha malengo aliyojipangia. Pia alitoa mchango wa miradi
mbalimbali ambayo inahitaji kujumuishwa kwenye bajeti.
AM:
 Ataanda “Management Paper” kwa ajili ya pendekezo la matumizi bora ya umeme
kupitia mfumo wa “Smart grid".
 Atawasilisha mapendekezo kwa ajili ya bajeti ya 2015/2016
 Ataendelea kutoa huduma ya mawasiliano ya komputa kwa idara ya utafiti na
mazingira.
AB:
 Ataendelea na uandaji wa pendekezo la kuweka mifumo mchanganyiko ya umeme
katika kisiwa cha Mafia.
 Ataendelea na kukusanya data kwa ajili ya kukamilisha pendekezo la kubadilisha taa
zenye kutumia nishati ndogo mkoa wa Ruvuma.
 Atamalizia uandaaji wa bajeti a mwaka 2015/2016

3
DONDOO ZA KIKAO CHA WIKI - IDARA YA UTAFITI
KIKAO CHA 39 WIKI YA 49 CHUMBA NAMBA A 819
TAREHE: 01/12/2015

GM:
 Kukusanya maoni na kuandaa bajeti ya idara.
 Kuandaa riport ya ERB
JM:
 Atawasilisha mapendekezo kwa ajili ya bajeti ya 2015/2016
 Atamalizia uandaaji na uwasilishaji wa ripoti ya mzunguko wa manjinia mikoani.
SM:
 Ataendelea na uandaji wa ripoti ya ERB sehemu ya kwanza.
 Ataendelea kusoma na kupembua zaidi ripoti za utafiti.
SSM:
 Atafuatilia na kutembelea meter ambazo hazitoa ripoti.
 Atafutalia kupata jumla ya wateja wote(Total list) wenye mashine za kusaga
 Atafuatilia kibali cha kufanya kazi kwenye live line
 Atafuatilia mchakato wa kupata maeneo kwa ajili ya kujenga plant ya umeme
4. Mengineyo:
 Mwenyekiti alielezea kuwa bado wanafuatilia suala la container
 Mwenyekiti alikumbushia kuhusu kukamilisha ripoti ya CFL.
 Mjumbe GM aliomba kufahamishwa vizuri kuhusu swala la kuzisoma na kusaini
maelezo ya kazi yake (Job description). Mwenyekiti SPD alimfahamishwa kwamba
kila mmoja wetu anatakiwa kusoma vizuri maelekezo ya kazi yake aliyoajiriwa ili
apate kuelewa mpango kazi wake na kama kuna sehemu ya kurekebisha amueleze ili
wairekebishe.
 Mjumbe GM aliongezea kwamba atamtumia mjumbe AB dokezo la mifumo
mchanganyiko ya umeme katika kisiwa cha Mafia kutoka kwa tafiti zilizofanywa
awali na Christopher Ruud

4
DONDOO ZA KIKAO CHA WIKI - IDARA YA UTAFITI
KIKAO CHA 39 WIKI YA 49 CHUMBA NAMBA A 819
TAREHE: 01/12/2015

7. Kufunga kikao
Kikao kilifungwa rasmi na Mwenyekiti SPD majira ya saa 10.15 asubuhi. Na aliwatakia
wajumbe kazi njema na kuwasilisha mipango kazi yao kwa Katibu ili kwa ajili ya
kumbukumbu.

…………………………….. …………………………………
Mha. Sabina Daati Ahmed Mwenda
Kaimu Mwenyekiti Katibu

TAREHE:…………………………….

You might also like