You are on page 1of 7

KUMB: PPR/2022 - 03/1

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI


KUANZIA JUMATANO, TAREHE 2 MACHI 2022

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo


za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia
Jumatano, Tarehe 2 Machi 2022. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia
yafuatayo:-

(a) Bei za rejareja na jumla za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa


yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimebadilika
ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 2 Februari 2022. Kwa Mwezi
Machi 2022, bei za rejareja za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa shilingi
60/Lita (sawa na asilimia 2.42) na shilingi 65/Lita (sawa na asilimia 2.77)
mtawalia. Bei ya rejareja ya Mafuta ya Taa imepungua kwa shilingi 83/Lita
(sawa na asilimia 3.63). Vilevile, ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita,
bei za jumla za Petroli na dizeli zimeongezeka kwa shilingi 59.65/Lita
(sawa na asilimia 2.54) na shilingi 64.45/Lita (sawa na asilimia 2.92),
mtawalia. Bei ya jumla ya Mafuta ya Taa imeshuka kwa shilingi 82.67/Lita
(sawa na asilimia 3.82).

(b) Kwa Machi 2022, bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya Petroli na Dizeli
kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara)
zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa tarehe 2 Februari 2022.
Kwa Machi 2022, bei za rejareja za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa
shilingi 165/lita (sawa na asilimia 6.88) na shilingi 207/lita (sawa na asilimia
9.09), mtawalia. Vilevile, ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita, bei za
jumla za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa shilingi 164.76/Lita (sawa na
asilimia 7.26) na shilingi 206.62/lita (sawa na asilimia 9.62), mtawalia.
Kutokana na kuisha kwa mafuta ya taa kwenye matanki ya kuhifadhia
yaliyopo Tanga, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya
Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya Taa Dar es Salaam na hivyo
bei za rejareja za Mafuta ya Taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na
gharama za kupokelea Mafuta ya Taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam

1|Page
na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

(c) Kwa Machi 2022, bei za rejareja na jumla kwa bidhaa za mafuta ya Petroli
na Dizeli kwa Mikoa ya Kusini (Mtwara, Lindi, and Ruvuma)
zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa tarehe 2 Februari 2022.
Kwa Machi 2022, bei za rejareja za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa
shilingi 43/lita (sawa na asilimia 1.70 na shilingi 105/lita (sawa na asilimia
4.35), mtawalia. Vilevile, ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita, bei za
jumla za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa shilingi 43.27/Lita (sawa na
asilimia 1.80) na shilingi 105.57/lita (sawa na asilimia 4.60), mtawalia. Kwa
kuwa hakuna matanki ya kuhifadhi mafuta ya taa Mtwara, waendeshaji wa
vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta
ya Taa Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za Mafuta ya Taa katika
mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea Mafuta ya Taa
kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa
husika

(d) Mabadiliko haya ya bei yanachangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta


katika soko la dunia, gharama za usafirishaji (BPS Premium) na thamani
ya shilingi ukilinganisha na dola ya kimarekani.

(e) Bei hizi zingeweza kuwa juu zaidi kama Serikali isingechukua hatua
ya kuahirisha ukusanyaji wa tozo ya Shilingi 100 kwa lita kwenye
bidhaa za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa.

(f) EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za


mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za
mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.
Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za
mkononi hapa nchini.

(g) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166,
bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA
itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za
bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya
maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(h) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya
ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (Price cap) au kushuka
chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama ilivyokokotolewa kwa
kutumia fomula na Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za
Mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia Magazeti ya Serikali Na. 2A na 57
ya tarehe 3 Januari 2022 na 28 Januari 2022, sawia.

(i) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta
2|Page
katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta,
punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo
husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa
kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu
zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka
mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali
itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa
mujibu wa kanuni husika.

(j) Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka


kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi
wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la
kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi
hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo
kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei
kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na
pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali
zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.

JEDWALI A: BEI ZA REJAREJA (SHILINGI/LITA)

Bei Kikomo
Mji Petroli Dizeli Mafuta Ya Taa
(Shs/Lita) (Shs/Lita) (Shs/Lita)
Dar es Salaam 2,540 2,403 2,208
Arusha 2,620 2,541 2,292
Arumeru (Usa River) 2,620 2,541 2,292
Karatu 2,638 2,559 2,310
Longido 2,631 2,552 2,303
Monduli 2,625 2,546 2,297
Monduli-Makuyuni 2,630 2,551 2,302
Ngorongoro (Loliondo) 2,704 2,625 2,384
Coast (Kibaha) 2,545 2,407 2,212
Bagamoyo 2,551 2,414 2,219
Bagamoyo (Miono) 2,582 2,445 2,250
Chalinze Junction 2,554 2,417 2,222
Chalinze Township (Msata) 2,558 2,421 2,226
Kibiti 2,561 2,423 2,228
Kisarawe 2,547 2,410 2,215
Mkuranga 2,550 2,413 2,218
Rufiji 2,568 2,430 2,235
Dodoma 2,599 2,462 2,267
Bahi 2,606 2,469 2,274
Chamwino 2,594 2,457 2,262
Chemba 2,625 2,488 2,293
3|Page
Kondoa 2,632 2,494 2,299
Kongwa 2,596 2,459 2,264
Mpwapwa 2,600 2,463 2,268
Mpwapwa (Chipogoro) 2,612 2,475 2,280
Mtera (Makatopora) 2,618 2,481 2,285
Mvumi 2,605 2,468 2,273
Geita 2,706 2,568 2,373
Bukombe 2,695 2,557 2,362
Chato 2,727 2,589 2,394
Mbogwe 2,744 2,606 2,411
Nyang'hwale 2,721 2,583 2,388
Iringa 2,604 2,467 2,272
Ismani 2,609 2,472 2,277
Kilolo 2,609 2,471 2,276
Mufindi (Mafinga) 2,614 2,477 2,282
Mufindi (Igowole) 2,623 2,486 2,291
Kagera (Bukoba) 2,756 2,618 2,423
Biharamulo 2,730 2,593 2,398
Karagwe (Kayanga) 2,772 2,635 2,440
Kyerwa (Ruberwa) 2,778 2,641 2,445
Muleba 2,756 2,618 2,423
Ngara 2,744 2,606 2,411
Misenyi 2,764 2,627 2,432
Katavi (Mpanda) 2,748 2,611 2,416
Mlele (Inyonga) 2,767 2,630 2,435
Mpimbwe (Majimoto) 2,741 2,604 2,409
Tanganyika (Ikola) 2,766 2,629 2,434
Kigoma 2,772 2,634 2,439
Uvinza (Lugufu) 2,784 2,647 2,451
Buhigwe 2,761 2,624 2,428
Kakonko 2,729 2,591 2,396
Kasulu 2,758 2,620 2,425
Kibondo 2,736 2,599 2,403
Kilimanjaro (Moshi) 2,609 2,530 2,282
Hai (Bomang'ombe) 2,613 2,533 2,285
Mwanga 2,602 2,523 2,275
Rombo (Mkuu) 2,626 2,547 2,303
Same 2,596 2,517 2,268
Siha (Sanya Juu) 2,616 2,537 2,288
Lindi 2,591 2,544 2,267
Lindi-Mtama 2,595 2,549 2,285
Kilwa Masoko 2,614 2,568 2,242
Liwale 2,626 2,580 2,288
Nachingwea 2,611 2,564 2,296
Ruangwa 2,617 2,570 2,298
Manyara (Babati) 2,654 2,575 2,330
Hanang (Katesh) 2,664 2,585 2,341
Kiteto (Kibaya) 2,669 2,590 2,341
Mbulu 2,667 2,587 2,343
Simanjiro (Orkasumet) 2,686 2,607 2,362

4|Page
Mara (Musoma) 2,719 2,581 2,386
Musoma Vijijini (Busekela) 2,760 2,622 2,427
Rorya (Ingirijuu) 2,728 2,590 2,395
Rorya (Shirati) 2,762 2,625 2,430
Bunda 2,710 2,573 2,378
Bunda (Kisorya) 2,720 2,582 2,387
Butiama 2,716 2,578 2,383
Serengeti (Mugumu) 2,764 2,627 2,432
Tarime 2,730 2,593 2,397
Tarime (Kewanja/Nyamongo) 2,734 2,597 2,402
Mbeya 2,647 2,510 2,315
Chunya 2,657 2,520 2,324
Chunya (Makongolosi) 2,662 2,525 2,330
Chunya (Lupa Tingatinga) 2,664 2,527 2,332
Kyela 2,663 2,526 2,331
Mbarali (Rujewa) 2,631 2,494 2,299
Rujewa (Madibira) 2,645 2,507 2,312
Rujewa (Kapunga) 2,641 2,504 2,309
Rungwe (Tukuyu) 2,656 2,519 2,324
Morogoro 2,565 2,428 2,233
Mikumi 2,581 2,444 2,248
Kilombero (Ifakara) 2,603 2,466 2,271
Kilombero (Mlimba) 2,625 2,488 2,293
Kilombero (Mngeta) 2,615 2,477 2,282
Ulanga (Mahenge) 2,614 2,476 2,281
Malinyi 2,624 2,487 2,292
Kilosa 2,584 2,446 2,251
Gairo 2,584 2,446 2,251
Mvomero (Wami Sokoine) 2,576 2,438 2,243
Mvomero (Sanga Sanga) 2,565 2,428 2,233
Turian 2,590 2,453 2,258
Mtwara 2,577 2,530 2,280
Nanyumbu (Mangaka) 2,613 2,567 2,329
Masasi 2,593 2,547 2,306
Newala 2,598 2,551 2,312
Tandahimba 2,591 2,544 2,305
Nanyamba 2,591 2,544 2,305
Mwanza 2,690 2,553 2,358
Kwimba 2,708 2,571 2,376
Magu 2,698 2,561 2,366
Misungwi 2,685 2,547 2,352
Sengerema 2,723 2,585 2,390
Ukerewe 2,750 2,613 2,417
Njombe 2,633 2,495 2,300
Njombe (Kidegembye) 2,653 2,516 2,321
Ludewa 2,671 2,533 2,338
Makambako 2,625 2,488 2,293
Makete 2,663 2,526 2,331
Wanging'ombe (Igwachanya) 2,630 2,493 2,298
Rukwa (Sumbawanga) 2,713 2,576 2,381

5|Page
Sumbawanga Rural (Mtowisa) 2,713 2,576 2,381
Kalambo (Matai) 2,720 2,583 2,388
Nkasi (Namanyele) 2,727 2,589 2,394
Ruvuma (Songea) 2,663 2,616 2,331
Mbinga 2,675 2,629 2,365
Namtumbo 2,654 2,607 2,361
Nyasa (Mbamba Bay) 2,701 2,654 2,375
Tunduru 2,628 2,581 2,390
Shinyanga 2,669 2,532 2,337
Kahama 2,683 2,545 2,350
Kishapu 2,698 2,560 2,365
Ushetu (Nyamilangano) 2,700 2,563 2,368
Ushetu (Kangeme Village) 2,691 2,554 2,359
Salawe 2,684 2,546 2,351
Simiyu (Bariadi) 2,711 2,573 2,378
Busega (Nyashimo) 2,704 2,566 2,371
Itilima (Lagangabilili) 2,714 2,576 2,381
Maswa 2,702 2,565 2,370
Meatu (Mwanhuzi) 2,709 2,572 2,377
Singida 2,631 2,494 2,299
Iramba 2,643 2,506 2,311
Manyoni 2,616 2,478 2,283
Itigi (Mitundu) 2,631 2,494 2,299
Ikungi 2,626 2,489 2,294
Mkalama (Nduguti) 2,655 2,518 2,323
Songwe (Vwawa) 2,657 2,519 2,324
Songwe (Mkwajuni) 2,663 2,526 2,331
Ileje 2,660 2,523 2,328
Momba (Chitete) 2,666 2,528 2,333
Tunduma 2,661 2,523 2,328
Tabora 2,648 2,511 2,316
Igunga 2,648 2,511 2,316
Kaliua 2,661 2,524 2,329
Ulyankulu 2,659 2,522 2,326
Nzega 2,659 2,522 2,326
Sikonge 2,657 2,520 2,325
Urambo 2,658 2,521 2,326
Uyui 2,655 2,517 2,322
Mpyagula 2,680 2,543 2,348
Tanga 2,563 2,484 2,254
Handeni 2,584 2,505 2,233
Kilindi 2,599 2,520 2,268
Korogwe 2,575 2,496 2,247
Lushoto 2,585 2,505 2,257
Mkinga (Maramba) 2,570 2,491 2,268
Muheza 2,568 2,489 2,254
Pangani 2,570 2,491 2,261

6|Page
JEDWALI B: BEI ZA JUMLA (SHILINGI /LITA)

Bandari Mafuta ya Taa


Petroli (Shs/Lita) Dizeli (Shs/Lita) (Shs/Lita)
DAR ES SALAAM 2,410.18 2,272.96 2,079.08
TANGA 2,433.03 2,353.80 -
MTWARA 2,446.97 2,400.13 -

Mha. Godfrey H. Chibulunje


KAIMU MKURUGENZI MKUU- EWURA

7|Page

You might also like