You are on page 1of 7

KUMB: PPR/2023 - 4/1

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI


KUANZIA JUMATANO, TAREHE 5 APRILI 2023

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za


bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano,
Tarehe 5 Aprili 2023. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-

(a) Kwa Aprili 2023, bei za rejareja za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa
yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa Shilingi
187/Lita, Shilingi 284/Lita na Shilingi 169/Lita, mtawalia, ikilinganishwa na
toleo la tarehe 1 Machi 2023.

(b) Kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara), bei


za rejareja za Aprili 2023 kwa mafuta ya petroli na dizeli zimepungua kwa
Shilingi 158/Lita na Shilingi 231/Lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la
tarehe 1 Machi 2023. Kutokana na kuisha kwa mafuta ya taa kwenye
matanki ya kuhifadhia yaliyopo Tanga, waendeshaji wa vituo vya mafuta
kwenye mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka
katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa
katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa
kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa
husika.

(c) Kwa Mikoa ya Kusini (Mtwara, Lindi, and Ruvuma), bei za rejareja za
Aprili 2023 kwa mafuta ya petroli na dizeli zimepungua kwa Shilingi 220/Lita
na Shilingi 176/Lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 1 Machi 2023.
Kwa kuwa hakuna matanki ya kuhifadhia mafuta ya taa katika bandari ya
Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini
wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es
Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa
kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es
Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

Bei za miji, wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 1.


1
Tofauti ya bei kutoka sehemu moja kwenda nyingine inatokana na tofauti ya
bandari mafuta yanapochukuliwa na gharama ya usafirishaji.

Mabadiliko haya ya bei yanachangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta katika


soko la dunia, gharama za usafirishaji (BPS Premium) na thamani ya Shilingi
ikilinganisha na dola ya Marekani.

Katika kutekeleza bei hizi, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na


rejareja pamoja na jamii kwa ujumla wanatakiwa kuzingatia yafuatayo: -

(a) EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za


mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi
kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni
bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei
za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA
itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa
za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi
stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya
ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (Price Cap) au kushuka
chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama ilivyokokotolewa kwa
mujibu wa Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022
zilizotangazwa kupitia Gazeti la Serikali Na. 57 la tarehe 28 Januari
2022.

(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika
mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo,
vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale
ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za
mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha
ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei
inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika
kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

(e) Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka


kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi
wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la

2
kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa Lita. Stakabadhi hizo
za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo
kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei
kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia,
risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na
mauzo ya mafuta ya petroli.

(f) Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza


mafuta kwa bei inayooneshwa katika Jedwali Na. 1. Hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka
AGIZO hili.

(g) Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza


mafuta kwa bei inayooneshwa katika Jedwali Na. 2 isipokuwa kwa
wateja wenye msamaha wa kodi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.

JEDWALI 1: BEI KIKOMO ZA REJAREJA KWA SHILINGI/LITA


Bei Kikomo
Mji Petroli Dizeli Mafuta Ya Taa
(Shs/Lita) (Shs/Lita) (Shs/Lita)
Dar es Salaam 2,781 2,847 2,929
Arusha 2,813 2,957 3,013
Arumeru (Usa River) 2,813 2,957 3,013
Karatu 2,831 2,975 3,031
Longido 2,824 2,968 3,024
Monduli 2,818 2,962 3,018
Monduli-Makuyuni 2,823 2,967 3,023
Ngorongoro (Loliondo) 2,897 3,041 3,105
Coast (Kibaha) 2,786 2,851 2,933
Bagamoyo 2,792 2,858 2,940
Bagamoyo (Miono) 2,823 2,888 2,971
Bagamoyo (Mbwewe) 2,804 2,869 2,952
Chalinze Junction 2,795 2,861 2,943
Chalinze Township (Msata) 2,800 2,865 2,947
Kibiti 2,802 2,867 2,949
Kisarawe 2,788 2,854 2,936
Mkuranga 2,791 2,856 2,939
Rufiji 2,809 2,874 2,956
Dodoma 2,840 2,905 2,988
Bahi 2,847 2,913 2,995
Chamwino 2,835 2,901 2,983
3
Bei Kikomo
Mji Petroli Dizeli Mafuta Ya Taa
(Shs/Lita) (Shs/Lita) (Shs/Lita)
Chemba 2,866 2,932 3,014
Kondoa 2,873 2,938 3,020
Kongwa 2,837 2,903 2,985
Mpwapwa 2,841 2,907 2,989
Mpwapwa (Chipogoro) 2,853 2,919 3,001
Mtera (Makatopora) 2,859 2,924 3,007
Mvumi 2,846 2,912 2,994
Geita 2,947 3,012 3,094
Bukombe 2,936 3,001 3,083
Chato 2,968 3,033 3,115
Mbogwe 2,985 3,050 3,132
Nyang'hwale 2,962 3,027 3,109
Iringa 2,845 2,911 2,993
Ismani 2,850 2,916 2,998
Kilolo 2,850 2,915 2,997
Mufindi (Mafinga) 2,855 2,921 3,003
Mufindi (Igowole) 2,864 2,929 3,012
Kagera (Bukoba) 2,997 3,062 3,144
Biharamulo 2,971 3,037 3,119
Karagwe (Kayanga) 3,013 3,079 3,161
Kyerwa (Ruberwa) 3,019 3,084 3,167
Muleba 2,997 3,062 3,144
Ngara 2,985 3,050 3,132
Misenyi 3,005 3,071 3,153
Katavi (Mpanda) 2,939 3,004 3,087
Mlele (Inyonga) 2,921 2,986 3,068
Mpimbwe (Majimoto) 2,958 3,024 3,106
Tanganyika (Ikola) 2,957 3,022 3,105
Kigoma 2,944 3,009 3,091
Uvinza (Lugufu) 2,934 2,999 3,081
Muyobozi Village (Uvinza) 2,942 3,008 3,090
Ilagala Village (Uvinza) 2,944 3,010 3,092
Buhigwe 2,942 3,008 3,090
Kakonko 2,944 3,010 3,092
Kasulu 2,953 3,018 3,100
Kibondo 2,950 3,016 3,098
Kilimanjaro (Moshi) 2,802 2,946 3,003
Hai (Bomang'ombe) 2,806 2,950 3,006
Mwanga 2,795 2,939 2,996
Rombo (Mkuu) 2,819 2,963 3,024
Same 2,789 2,933 2,989
Siha (Sanya Juu) 2,809 2,953 3,009
Lindi 2,807 3,013 2,988
Lindi-Mtama 2,811 3,018 3,006
Kilwa Masoko 2,830 3,037 2,963
Liwale 2,842 3,049 3,009
Nachingwea 2,826 3,033 3,017

4
Bei Kikomo
Mji Petroli Dizeli Mafuta Ya Taa
(Shs/Lita) (Shs/Lita) (Shs/Lita)
Ruangwa 2,833 3,040 3,019
Manyara (Babati) 2,847 2,991 3,051
Hanang (Katesh) 2,857 3,001 3,062
Kiteto (Kibaya) 2,862 3,006 3,062
Mbulu 2,860 3,004 3,064
Simanjiro (Orkasumet) 2,879 3,023 3,083
Mara (Musoma) 2,947 3,012 3,095
Musoma Vijijini (Busekela) 2,960 3,025 3,107
Rorya (Ingirijuu) 2,954 3,019 3,102
Rorya (Shirati) 2,962 3,027 3,109
Bunda 2,938 3,004 3,086
Bunda (Kisorya) 2,951 3,016 3,098
Butiama 2,944 3,010 3,092
Serengeti (Mugumu) 2,955 3,021 3,103
Tarime 2,956 3,021 3,103
Tarime (Kewanja/Nyamongo) 2,961 3,027 3,109
Mbeya 2,888 2,954 3,036
Chunya 2,898 2,963 3,046
Chunya (Makongolosi) 2,903 2,969 3,051
Chunya (Lupa Tingatinga) 2,905 2,971 3,053
Kyela 2,904 2,970 3,052
Mbarali (Rujewa) 2,872 2,938 3,020
Rujewa (Madibira) 2,886 2,951 3,033
Rujewa (Kapunga) 2,882 2,948 3,030
Rungwe (Tukuyu) 2,897 2,963 3,045
Morogoro 2,806 2,872 2,954
Mikumi 2,822 2,887 2,970
Kilombero (Ifakara) 2,844 2,910 2,992
Kilombero (Mlimba) 2,866 2,932 3,014
Kilombero (Mngeta) 2,856 2,921 3,003
Ulanga (Mahenge) 2,855 2,920 3,002
Malinyi 2,865 2,930 3,013
Kilosa 2,825 2,890 2,972
Gairo 2,825 2,890 2,972
Mvomero (Wami Sokoine) 2,817 2,882 2,964
Mvomero (Sanga Sanga) 2,806 2,872 2,954
Turian 2,831 2,897 2,979
Mtwara 2,793 3,000 3,001
Nanyumbu (Mangaka) 2,830 3,036 3,050
Masasi 2,809 3,016 3,027
Newala 2,814 3,021 3,033
Tandahimba 2,807 3,014 3,026
Nanyamba 2,807 3,014 3,026
Mwanza 2,931 2,997 3,079
Kwimba 2,949 3,015 3,097
Magu 2,939 3,005 3,087
Misungwi 2,926 2,991 3,073

5
Bei Kikomo
Mji Petroli Dizeli Mafuta Ya Taa
(Shs/Lita) (Shs/Lita) (Shs/Lita)
Sengerema 2,964 3,029 3,111
Ukerewe 2,991 3,056 3,139
Njombe 2,874 2,939 3,021
Njombe (Kidegembye) 2,894 2,960 3,042
Ludewa 2,912 2,977 3,059
Makambako 2,866 2,931 3,014
Makete 2,904 2,970 3,052
Wanging'ombe (Igwachanya) 2,871 2,937 3,019
Rukwa (Sumbawanga) 2,954 3,020 3,102
Sumbawanga Rural (Mtowisa) 2,954 3,020 3,102
Kalambo (Matai) 2,961 3,027 3,109
Nkasi (Namanyele) 2,968 3,033 3,115
Nkasi (Kirando) 2,977 3,043 3,125
Ruvuma (Songea) 2,879 3,085 3,052
Mbinga 2,891 3,098 3,065
Namtumbo 2,870 3,076 3,058
Nyasa (Mbamba Bay) 2,917 3,123 3,075
Tunduru 2,844 3,050 3,032
Shinyanga 2,910 2,976 3,058
Kahama 2,915 2,980 3,062
Kishapu 2,918 2,984 3,066
Ushetu (Nyamilangano) 2,926 2,992 3,074
Ushetu (Kangeme Village) 2,932 2,998 3,080
Salawe 2,924 2,989 3,072
Simiyu (Bariadi) 2,928 2,994 3,076
Busega (Nyashimo) 2,940 3,006 3,088
Itilima (Lagangabilili) 2,928 2,994 3,076
Maswa 2,922 2,987 3,070
Meatu (Mwanhuzi) 2,933 2,999 3,081
Singida 2,872 2,937 3,020
Iramba 2,884 2,950 3,032
Manyoni 2,857 2,922 3,004
Itigi (Mitundu) 2,872 2,938 3,020
Ikungi 2,867 2,933 3,015
Mkalama (Nduguti) 2,896 2,962 3,044
Songwe (Vwawa) 2,898 2,963 3,045
Songwe (Mkwajuni) 2,904 2,970 3,052
Ileje 2,901 2,967 3,049
Momba (Chitete) 2,907 2,972 3,054
Tunduma 2,902 2,967 3,049
Tabora 2,889 2,955 3,037
Igunga 2,889 2,955 3,037
Kaliua 2,902 2,968 3,050
Ulyankulu 2,900 2,965 3,048
Nzega 2,900 2,965 3,047
Sikonge 2,898 2,964 3,046
Urambo 2,899 2,965 3,047

6
Bei Kikomo
Mji Petroli Dizeli Mafuta Ya Taa
(Shs/Lita) (Shs/Lita) (Shs/Lita)
Uyui 2,896 2,961 3,043
Mpyagula 2,921 2,987 3,069
Tanga 2,756 2,900 2,975
Handeni 2,777 2,921 2,954
Kilindi 2,792 2,936 2,989
Korogwe 2,768 2,912 2,968
Lushoto 2,778 2,922 2,978
Mkinga (Maramba) 2,763 2,907 2,989
Muheza 2,761 2,905 2,975
Pangani 2,763 2,907 2,982

JEDWALI 2: BEI KIKOMO ZA JUMLA KWA SHILINGI/LITA

Bandari Petroli Dizeli Mafuta ya Taa


Dar es Salaam 2,650.48 2,715.44 2,798.01
Tanga 2,625.48 2,768.66 -
Mtwara 2,662.38 2,867.94 -

Dkt. James A. Mwainyekule


MKURUGENZI MKUU- EWURA

You might also like