You are on page 1of 134

Published & Designed by Matra Media

Dar es Salaam, Tanzania.


+255 742 270 551, +255 699 354779

Mauzo na Masoko kupitia:-


1. Whatsapp 0758 255 255 au 0742 270 551
2. Instagram:- GIF Bakery/ Jackline Machoke.

Copyright (c)2022, Zacharia Machoke. All Rights Reserved. No part of this


ebook may be printed, reproduced, distributed, or transimitted in any form or
by any means or stored in a database or retriveal system , without the prior
written permission of the publisher.
Utangulizi

Hiki ni kitabu cha vitafunio, lakini sio meno, tukiongelea vitafunio


tunamaanisha vitafunwa. Wakati tunatafuta suluhu ya neno sahihi
kati ya kitafunio na kitafunwa kitabu hiki kitakufundisha kuten-
geneza aina zaidi ya 20 za vitafunio au vitafunwa pamoja na snacks
nyepesi.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 1


Kwanini Kitabu Hiki

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 2


Maandalizi ya awali:- Baadhi ya Vifaa Utakavyotumia

Lazima utahitaji jiko, kika-


angio na Oven. jiko linaweza
kuwa deep fryer, jiko la mkaa
au gesi na kikaangio au sufu-
ria tu. Hivi sio shida sababu
inawezekana unavyo tayari
jikoni kwako.

Utahitaji mizani, zinauzwa


kuanzia 10,000 lakini pia
kuna mbadala wake yani
measuring cups & spoons.
Ni vya kupimia recipes na
vinapatikana supermakert.
Unapopika vitafunwa
utahitaji kuchanganya na
kusukuma mchanganyiko
na kazi hiyo hufanywa na
wewe kwa mikono, na mix-
er na kusukuma kwa msu-
kumio na kibao au meza.

Utahitaji kuwa na vifaa mbalim-


bali vya jikoni kama vile
sahani, bakuli, visu, vikaan-
gio, miiko, vijiko, cutter, na
vinginevyo. Vingi unavyo
tayari jikoni kwako
Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 3
Maelezo kuhusu Mahitaji (Ingredients za Muhimu)
Ni muhimu kufahamau kuwa

1. Kila kitafunio kina recipe yake na taratibu zake, kwa hiyo


hamna mahitaji (ingredients) ya namna moja ambayo yata-
pika vitafunio vyote. Lazima ufanye manunuzi tofauti kwa
mapishi tofauti. lakini hata hivyo vifuatavyo utavikuta mahali
pengi kama vile:-

Unga wa Ngano:-
Karibu vitafunio vyote vina-
tumia unga wa ngano kwahi-
yo hakikisha una unga sahihi
kwa matumizi sahihi sababu
sio kila Unga wa ngano unafaa
kwa vitafunio. Mfano Unga wa
mkate unaweza usifae kwenye
maandazi. Kwahiyo soma lebo
na ulizia kabla hujanunua

Mafuta ya Kupikia:-
unahitaji kuwa nayo
wakati wote sababu
utatumia sehemu nyingi.

mahitaji mengine ni kama Chumvi, Hamira, Maji, Ajinamoto,


Kalipoda, Sukari etc ambayo ni madogo madogo na yanabadi-
lika kutokana na kinachopikwa.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 4


SAMBUSA

5
Utangulizi

Ma born town wahenga wa miaka ya nyuma sana walikuwa


wanaziita “watch mosquito watch” yaani ‘sa mbu sa’. Hiki ni
kitafunio chenye asili ya India ingawa kinalika sana uswahil-
ini na ni ajira kubwa sana kwa vijana wanaotembeza mitaani
hasa katika mji wa Dar es salaam. Kwahiyo somo utakalolipa-
ta hapa linaweza kuwa ajira tosha kwa baadhi ya watu. Kwa
ufahamu tu ni kuwa kuna sambusa na samosa. Sambusa ni
kile kitafunio chenye nyama ndani na samosa ni kile chenye
mboga mboga kama karoti etc.

Hapa tunajifunza sambusa na Recipe yake ni:-

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 6


Awamu ya Kwanza...Andaa nyama ya ndani ya sambusa. chan-
ganya

Zipike recipe mpaka zibadilike


Zimimine recipe zote rangi upate rangi hii ya brown.
kwenye sufuria au ki- onja ili ujihakikishie ladha yake
ni nzuli. Ongezea vitunguu
kaango na uzipike. usi- vilivyokatwakatwa gram 500 na
weke maji changanya

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 7


Awamu ya pili...Kutengeneza Manda

Manda ni lile gamba la nje kavu la Sambusa ambalo ndani


yake kunakuwa na nyama au mbogamboga kama vitunguu
na karoti. Manda ndio inaipa Sambusa shape ya pembe tatu.
Utengenezaji wake ni kwa hatua zifuatazo:-

Kwanza weka unga wa nga- Pili Ongezea Maji nusu lita


no kilo moja na chumvi
gram 10 kwenye chombo
kama dish

Tatu kanda kwa mikono au


Nne:- kanda mpaka upate donge
mixer itakurahisishia kazi.
lililoshikamana na lililojichang-
anya vizuri kabisa.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 8


Tano:- Litoe donge kwenye Sita;- Viviringishe vipande vya
dish na uliweke mezani hala- donge ulivyokata kwenye vi-
fu kata vipande vidogo vya ganja vya mkono wako ili viwe
wastan wa gram 80 vya mviringo au round

Saba:-Visukume kama una- Utapata kitu kama chapati, tafadha-


sukuma chapati li ona picha . Kila moja ipake mafu-
ta pande zote 2.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 9


Kumi;-Zipange zote pamo-
ja. moja juu ya nyingine na
Tisa:-Paka mafuta kila moja
zigandamize kama unavyoona
mbele na nyuma halafu
kwenye picha.

kumi na 1;- Chukua msuku- Kumi na Mbili:-


mio na uzisukume zote kwa • Washa Oven na weka nyuzi
pamoja kama chapati kwa joto 220
mara ya pili tena. • Iache ipate moto kwanza
• Halafu weka manda kwa da-
kika 15 oven ikiwa tayari ya
moto sana

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 10


kumi na Tatu:- Baada ya daki-
ka 15 itoe manda kwenye Oven
na acha ipoe kidogo halafu ikate
katikati vipande 4. kutoka kush-
oto kwenda kulia na kutoka juu
kwenda chini.

Kumi na Nne angalia picha


kushoto:- Ondoa sehemu ya
chini ya manda ambayo itaku-
wa kavu.

Unaweza kuitumia kutengene-


za kaukau baadae.

Utabakiwa na sehemu hiyo ya


pembe tatu ambayo utaikunja
kupata umbo la sambusa.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 11


Jinsi ya kukunja Sambusa na Kuweka Nyama Ndani Yake

Kwanza:- Anza kwa Kutengeneza Gundi ya Nga-

weka ngano kido- Ongezea Maji Koroga na


go kwenye bakuli utapata mchan-
ganyiko unao-
Pili:-Kunja Manda ya Sambusa nata

1.Kunja ku- 2. Paka gundi


3. kunja ku- 5. paka gundi
toka kulia ya ngano na 4. weka
toka kushoto kwa juu alafu
kwenda kush- maji sehemu nyama
kwenda kulia Ikunje kufu-
oto ya maungio
nika

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 12


weka mafuta kwenye jiko
utakalotumia kukaangia ili
yapate moto. unaweza kutumia
kikaangio, sufuria au deep fryer
ya umeme.

Ziweke sambusa kwenye


mafuta zijipike au kujik-
aanga. uwe unageuza geuza
mara kwa mara ili pande
zote zipate mafuta. Zikiba-
dirika rangi sawa pande zote
na kuwa brown au rangi ya
dhahabu zitakuwa tayari zi-
meiva.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 13


Kabab

14
Kabab

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 15


Anza kwa kupima recipe ifuatayo:-

• Changanya na mkono
mimina recipe yako yote • Ongezea mafuta ya
kwenye dish kasoro mayai. Sle- kupikia kijiko kimoja
si za mikate ziloweke kwenye
maji kidogo ili zilainike.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 16


Ikishikamana nyunyuzia unga wa
ngano kidogo kama grama 20 tu
kwa juu na endelea kukanda.

utapata donge kubwa la nyama nam-


na hii tayari kwa kutengenezea kabab
na egg chop pia

ili kupata kababu kata kipande cha


donge hilo kama unavyokata tonge
la ugali na lifinye finye kutengeneza
umbo dogo la kabab, kama kibomba
cha duara.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 17


finyanga mpaka upate umbo
hili.

Vipake unga wa ngano

Bandika mafuta kwenye kikaan-


gio yapate moto halafu ziweke
kababu zijikaange kwa dakika
kama tano mpaka zikauke

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 18


zikibadilika rangi na kuiva zitoe
kwenye mafuta

• Yapasue yale mayai matano ya


kwenye recipe kwenye chombo
na uyakoroge

• Yatumie kuzipaka kabab zote kwa


nje

• Halafu zirudishe jikoni zikiwa


zimepakwa mayai na baada
ya dakika mbili au tatu zitoe
kwenye mafuta.

• Zipake tena mayai yaleyale na


zirudishe tena kikaangoni kwa
mara ya pili kwa dakika mbili
au tatu.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 19


Unaweza kurudia zoezi la
kupaka mayai na kukaanga
hata mara tatu mpaka uridhike
na mwonekano wa kabab

Kababu zipo tayari

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 20


Egg Chop

21
Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 22
Anza kwa kupima recipe ifuatayo:-

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 23


mimina kwenye dish kama ulivy-
ofanya kwenye kabab

Kanda na ongezea:-

• mafuta kijiko kimoja

• Nyunyuzia ngano
kama gram 20

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 24


Utapata donge kama lile la
kwenye kabab

Mega kipande cha donge la nyama


na bonyeza katikati kupata tundu
pana tu la kutosha kuweka yai.

Weka yai moja ulilochemsha ka-


tika tundu ulilotengeneza

Lifunike yai pande zote na donge


la nyama

Nyunyuzia na zungushia
unga wa ngano kwa nje.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 25


bandika mafuta jikoni kwenye kikaangio
na uziweke egg chop zianze kujikaanga.

Acha zijikaange kwa dakika chache sana


mpaka zibadilike rangi na kukauka. Ta-
fadhali ona picha kushoto.

Zitoe jikoni na zipake mayai kwa nje kama


ulivyofanya kwenye kabab.

Zirudishe tena jikon kwa dakika 2 au


tatu

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 26


Zitakuwa namna hii, ona picha kushoto.

Zipake tena mayai

Rudisha tena jikoni kwa mda mfupi


tu. na zitakuwa zipo tayari.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 27


Half Cake

28
Anza kwa kupima recipe ifuatayo:-

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


Zimwage recipe kwenye
meza ya kukandia na anza
kuzichanganya zenyewe
kwanza bila kuongeza kitu

Recipe zikisha jichanganya zi-


kusanye vizuri halafu weka
shimo katikati na weka maji ya
moto kiasi au ya uvuguvugu ka-
tikati, ona picha kushoto.

Endelea kukanda mpaka


upate donge zito kabisa na
gumu

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 30


Chukua msukumio wa
chapati na anza kusuku-
ma donge lote kwa pamoja
mpaka upate saizi ya half
cake unayoitaka.
Half cake ina saizi kubwa
kwahiyo hakikisha donge
lako sio jembamba sana.

Ukimaliza kulisikuma chukua


kisu na kata kwa urefu kuondoa
kona na mzunguko halafu likate
kupata vipande vidogo vidogo.

Angalia picha kushoto kuona


wastan wa kipande cha kukata
cha half cake.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 31


bandika sufuria au kikaangio
chenye mafuta jikoni na yakishapa-
ta moto weka vipande vya half cake
ili vijikaange.

Geuza geuza mpaka


upate rangi kama ya
dhahabu au brown
hiyo.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 32


Maandazi

33
Anza kwa kupima recipe ifuatayo:-

mimina recipe yote kwenye Anza kukanda mpaka recipe


dish la kukandia na ongezea yote ijichanganye na upate
maji nusu lita. donge laini

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 34


Donge likiwa tayari litoe
kwenye dish na kuliweka
mahali pa kusukumia.

Lisukume kwa msukumio wa


chapati mpaka upate size unayoi-
taka ya andazi.

Likate kwa urefu

halafu kata vipande vya


maandazi

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 35


Ukishapata vipande vya maan-
dazi viache vi umuke kwa Weka jikoni yajikaange. uwe
takriban dakika 15 unageuza geuza mpaka upate
rangi ya maandazi.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 36


Donati

37
Donati

Tofauti ya donati na maandazi ni majina na namna viwili hivi


vinavyokatwa. Donati ni neno la kiingereza linalomaanisha
andazi kwa hiyo donati na maandazi ni kitu kimoja isipoku-
wa tu wazungu maandazi yao huyakata kwa shape ya duara
wakati sie maandazi yetu huweza kuwa na pembe nne.

Recipe yake ni kama ya


maandazi hapo juu.

• Unga kilo 1
• Sukari gram 100
• Baking powder gram 10
• Hamira gram 15
• Blueband/ margarine
gram 100
• Unaweza kuweka yai 1
pia

mimina kwenye dish la ku-


kandia na ongeza ongezea
maji nusu lita

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


38
Kanda mpaka lishikamane
vizuri

Donge likiwa tayari

Hamishia mezani na sukuma kama


chapati mpaka upate size ya maan-
dazi

Tumia donati cutter ili kukata donati.


kama huna donati cutter tumia ujan-
ja wowote tu kupata shape ya donati.
mfano unaweza kutumia bakuli au bi-
lauri kubwa kukata kipande cha nje na
ndogo kupata upande wa ndani

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 39


Tenga kikaangio au sufuria
Donati zikiwa zime4katwa. ziache
yenye mafuta na kaanga
ziumuke.

baada ya dakika chache donati zitabalika rangi na kuwa


tayari

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 40


Chapati

41
Chapati

Vitafunio vya asili vya waafrika ni kama mihogo, viazi,


magimbi, mahindi ya kuchemsha na vinguinevyo vya
jamii ya mizizi lakini kwa miaka ya hivi karibuni chapati
imevishusha vyote hivyo na zimekuwa kitafunio cha taifa.
Kuna watu wanaishi kwa kutengeneza na kuuza chapati tu.
Recipe yake ni:-

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 42


Hatua Ya Kwanza
Chapati mara nyingi hazihitaji mixer, lakini unaweza kutumia
ukiwa na haraka na unataka kazi nzuri. anza kwa kupima in-
gredients hizi chini:-

mimina recipe zote kwenye Ongezea maji ya uvuguvugu


dish

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 43


Anza kukanda

Donge likishikamana
ongezea mafuta ya kupikia
kijiko kimoja na endelea
kukanda mpaka liwe tayari

Donge likiwa tayari hamishia


mezani na uanze kukata
vipande vya wastan wa gram
100. Ukiwa mzoefu unanyo-
foa tu.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 44


Hatua ya Pili

Vi roll vipande kwenye viganja vikisha kuwa round una vi-


vya mkano wako ili viwe vya sukuma na msukumio wa
mviringo au round. chapati kupata chapati. Kwa
wazoefu wanaweza kwenda
kukaanga moja kwa moja. la-
kini kwa chapati yenye ubora
endelea...

yeyusha blue band ndani Ipake kwenye chapati upande


ya kikaango mmoja wa ndani

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 45


Iviringishe chapati kupata round tena. Unaweza kuikata chapa-
ti kuanzia kati (angalia picha)halafu izungushe mpaka mwisho.
ukimaliza ibonyeze juu na chini kupata round

Round za donge utakazopata uziache zit-


ulie kidogo kama dakika tano

halafu sukuma tena

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 46


Hatua ya Tatu

Weka kikaango ulichokipaka mafuta


kidogo jikoni

Weka chapati kwenye kikaango mafuta


yakishapata moto

endelea kuongeza mafuta kwa


pembeni kidogo kidogo na kui-
geuza geuza chapati mpaka iive.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 47


Chapati Tayari

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 48


Bagia

49
RECIPE YA BAGIA

mimina vyote kwenye Dish la Ongezea maji ya uvuguvugu


kukandia au mixer kama ipo wastan wa kikombe kimoja

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 50


koroga mpaka upate uji
mzito

Acha uumuke ( Kama huja-


tumia hamira hamna haja ya
kuacha uumuke)

Baada ya dakika chache


(kama 10 tu) mchanganyiko
wa bagia utakuwa umeumu-
ka

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 51


Chota kwa mkono (Ona pi-
cha)

Weka kwenye mafuta ya moto

Geuza geuza mpaka vyote


mpaka bagia zote zibadilike
rangi na kuwa ya dhahabu

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 52


Baada ya dakika
chache bagia zitakuwa
tayari

Kama hujatumia hamira na hujaacha iumuke utapata bagia


nyembamba na nyepesi kama zile zinazopatikana kwa wau-
za urojo na mitaa mingine ya uswailini..kwa wale tutunao-
ishi ushwailini.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 53


ONION
BAGIA

54
Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery
Ongezea maji kikombe kimoja
kwenye mchanganyiko wa Rec-
ipe

Changanya Recipe

Changanya mpaka upate donge


zito la njano (kama uji mzito, ona
picha kushoto))

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 57


Mega donge kwa viganja au
vidole vya mkono(hamna haja
ya ku roll) na weka pembeni,
ona picha kushoto)

Pasha mafuta kwenye ki-


kaango, sufuria au deep
fryer mpaka yawe ya moto
kabisa halafu dumbukiza
donge la bagia lijipike kwa
sekunde chache

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 59


Baada ya Donge la Onion bagia
kubadilika rangi na kuiva ndani ya
dakika moja au 2 ipua jikoni

Ziweke bagia kwenye kibao au


sahani au chombo chochote bapa
na Zigandamize bagia na chom-
bo kilicho bapa ili ziwe flat (ona
picha kushoto)

Onion Bagia zikiwa flat

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 60


Zirudishe jikoni tena ziki-
wa flat kwa sekunde kad-
haa tena

Zikibadilika rangi na
kuwa mchanganyiko wa
rangi ya dhahabu na nja-
no zinakuwa zimeiva.
Bon Apetit

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 61


Kalimati

62
Anza kwa kupima recipe ifuatayo:-

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


Mimina kwenye dish

Weka maji kikombe kimoja

Kanda ili kupata donge la ka-


limati. ongeza maji inapobidi
kwani donge la kalimati ni
tepetepe kama uji mzito sana.
(thick)

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 64


Donge likisha jichangan-
ya vizuri ongezea mafuta
ya kupikia vijiko 2

Ukishapata mchanganyiko
mzuri uweke pembeni ili uu-
muke kwa angalau nusu saa.

Donge likishaumuke chota


kwenye kuganja cha mkono

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 65


katia na kuweka ma donge ya
kalimati kwenye mafuta ya
moto. Wakati yanachemka
uwe unageuza geuza na uki-
ona yamebadilika rangi na
brown au rangi ya dhahabu
hivi basi kalimati zitakuwa
zimeiva

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 66


KACHORI

67
RECIPE YA KACHORI

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


mimina Recipe yote kwenye su- Viazi vikiwa tayari vitoe
furia na ichemshe mpaka viazi kwenye sufuria na viweke
vilainike kabisa kwenye dish na mimina vi-
tunguu vilivyokatwa punje
ndogo ndogo gram 500

Ponda ponda viazi na vitunguu Ukisha pondaponda mega na fin-


pamoja mpaka upate donge yanga kama unavyomega tonge
mfano wa ugali mlaini au la ugali.. Roll mkononi mwako ili
mashed potato tonge liwe round. (Ona picha juu)

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 69


Kutengeneza Uji wa Bagia

Weka unga wa ngano nusu kikombe


kwenye bakuli

Ongezea maji nusu kikombe

Ongezea rangi ya chakula (food col-


or ya njano) kama mls 5

Koroga mchanganyiko wote na


utapata uji wa kachori wa njano. Un-
aweza kuongeza ngano kidogo kama
ukiona ni mwepesi sana.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 70


Chukua ma donge ya viazi uliy-
ofinyanga mwanzoni na ya weke
kwenye mchuzi wa kachori.
paka mchuzi kuzunguka donge
lote.

Donge lote lipate mchuzi

Weka mafuta jikoni na haki-


kisha yanapata moto halafu
ndio uweke kachori zijik-
aange

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 71


Katlesi za
Nyama na
Mayai

72
RECIPE YA KATLESI

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


Viazi vikiwa tayari mimina
mimina Recipe yote kwenye su- vitunguu vilivyokatwa punje
furia na ichemshe mpaka viazi ndogo ndogo gram 500
vilainike kabisa

Ponda ponda viazi na vitunguu Ukisha pondaponda mega na fin-


pamoja mpaka upate donge yanga kama unavyomega tonge
mfano wa ugali mlaini au la ugali.. Roll mkononi mwako ili
mashed potato tonge liwe round. (Ona picha juu)

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 74


Kuandaa nyama ya Katlesi ya nyama

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


Iweke recipe yote ya nyama jikoni
iive yenyewe. ongeza maji ya limao-
vijiko viwili.

Nyama ipo tayari

Gandamiza madonge mawili ya


donge la viazi mpaka yawe flat
au bapa, moja litakuwa la chini
jingine la juu

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


76
Kadiria nyama na weka katikati katika
donge la chini

Chukua donge bapa jingine na


funika kwa juu

Yaunganisjhe yote pamoja na yaviring-


ishe ili upate donge moja kubwa la
mviringo

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 77


Kupata Katlasi ya mayai gandam-
iza tena donge la viazi kwenye ki-
ganja upate madonge mawili flat

Weka yai lililochmeshwa na ku-


menywa katikati ya donge moja la
chini.

Funika na donge bapa jingine kwa


juu

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 78


Funika yai lote kwa kuun-
ganisha donge la chini na
juu

Liviringishe kabisa

Zungushia unga wa ngano


kwenye katilesi ushike sehemu
zote.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 79


Pasua mayai manne kwenye bakuli
na ongezea ngqano kijiko kimoja.

Koroga ngano ichanganyike na yai

Zipake katilesi (donge) zote aina 2


(ya nyama na ya yai) kwa mchuzi
wa yai na ngano

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 80


Pasha mafuta yachemke sana
halafu weka katilas mpaka ziba-
dilike rangi (Tumia utashi wako
kujua kama zimeiva)

Zikisha badilika rangi zitoe na


zidumbukize au paka tena ule
mchanganyiko wa mayai na
ngano.

Rudisha tena jikoni zijikaange


huku ukigeuza geuza kwa mda
kidogo mpaka ukiona zimeba-
dilika rangi na kuwa brown

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


katilas ya nyama ipo ta-
yari

Katilas ya yai ipo tayari

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 81


VIKOKOTO

82
RECIPE YA VIKOKO-

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


Changanya ngano na sukari,kisha
weka maji na uanze kukanda.

Unaweza kutumia nixer ukita-


ka lakini unaweza kukanda kwa
mkono tu.

Hakikisha umepata donge soft lakini


liwe gumu kiasi

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 84


Nyunyuizia unga juu baada
Nyunyuzia unga mezani ,sukuma
ya kusukuma na uanze ku-
kama chapati nzito kiasi .
kata vipande vidogo vidogo
kama pichani.

• Andaa mafuta yako kisha yaki-


pata moto weka uanze kukaan-
ga kokoto zako.

• Geuza geuza vipate rangi ya


brown kote viive vizuri.

• Kisha epua uvichuje mafuta


..vipoe tayari kwa kuliwa.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 85


VISHETI

86
RECIPE YA VISHETI....INAFANANA NA YA MAAN-

Ongezea maji kama kanda kama ulivyofanya Sukuma kama ulivy-


ulivyofanya kwenye kwenye maandazi ofanya kwenye
maandazi maandazi

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 87


Wakati Donge la Visheti Linaumuka

• kata kama ulivyokata kwenye vishet

• Acha donge liumuke kwa dakika 10


mpaka 15

Wakati donge la visheti linaumuka weka


mafuta ya kupikia kwenye kikaango
au deep fryer etc na yakishapata moto
mkali mimina vipande vya donge la
visheti na uanze kukaanga. uwe unageuza
geuza.

Visheti viklibadilika rangi na kuwa


na rangi ya maandazi au ya dhaha-
bu basi jua visheti vimeiva. hatua
inayofuatia ni kupaka Sukari juu.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 88


KUPAKA SUKARI KATIKA VISHETI

Bandika jikoni Sukari iliyochang- Wacha ichemke mpaka itoe


anywa na maji povu na iwe nzito kama asali

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 89


Mimina visheti vyako kwenye
povu la mchanganyiko wa Su-
kari na maji

Geuza geuza visheti ili vyote


vijichanganye na mchangan-
yiko wa sukari na vitaanza
kung’aa. Adjust moto kulin-
gana na mazingira

Visheti vikipoa utaanza kuo-


na Sukari inaonekana juu ya
visheti.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 90


BURGER

91
Utangulizi

Burger inahitaji utangulizi wake sababu ina sehemu mbili


ambazo ni

1. Buns au zile scons zinazokatwa kati

2. Nyama zinazowekwa katikati pamoja na “greens’ kama


nyanya vitunguu, lettuce etc

Unaweza kununua Burger buns au scons zile halafu nyama ya


ndani ile ukatengeneza mwenyewe. Lakini katika somo hili
tutaanza na kutengeneza burger buns halafu tutatengeneza
nyama ya ndani.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 92


Hatua ya Kwanza:- Kutengeneza Burger Bun
Tutaanza na kutengeneza burger buns. na recipe yake ni hiyo
hapo chini lakini kumbuka kuwa unaweza kuboresha recipe na
vitu kama maziwa na chochote kile kitakachoweza kukupa rec-
ipe yako ya kipekee.

Utahitaji pia na:-

Ufuta kidogo ingawa sio lazima sana

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


93
Anza Kukanda kwa mkono au
Mimina recipe katika dish na
unaweza kutumia mixer. Ende-
Ongezea Maji Kidogo kikombe
lea kuongeza maji kidogo kido-
kimoja
go lakini usizidishe nusu lita.

Kanda mpaka upate donge Likate donge katika size ndogo


lililochanganyika vizuri kama ngumi hivi

Liviringishe liwe duara


Chovya kwenye Ufuta

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 94


Paka tray mafuta halafu
weka kwenye joto kwa zaidi
ya nusu saa donge liumuke

Baada ya nusu saa mpaka da-


kika 40 litakua limeumuka

Seti moto nyuzi 200 na bake


kwa dakika 20

Bugger bun ipo Tayari

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 95


Hatua ya Pili

Kutengeneza Nyama ya Ndani ya Burger

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


Loweka slesi za mikate kwenye
maji na zikatie katie kwenye dish
lenye recipe

Anza kuchanganya vyote pamoja

Endelea kukanda

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 97


Vyote vikijichanganya vizuri
kabisa utapata donge kama hilo
pichani kushoto. kata donge
moja linalojaa kwenye kiganja
cha mkono

kama una cutter, tumia cutter,


kama huna basi liviringishe liwe
duara halafu lipige pige na kulib-
inya kwa mkono liwe flat kama pi-
cha inavyoonyesha

Donge likishakuwa flat nyunyuzia


au paka unga wa ngano kidogo tu
kwa juu na chini....sio lazima lakini
kupaka unga huo, unaweza ukaz-
ichoma zenyewe tu

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 98


halafu pasha mafuta kwenye
kikaangio na weka nyama ya
burger ianze kujikaanga.

AU

Weka mafuta kidogo tu kwenye


kikaango na ukaange (ona picha
kushoto)

AU

Choma kama unavyochoma mi-


shikaki

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 99


Utajuaje Nyama ya Burger
ipo tayari?

• Itabadilika rangi kutoka


pink na kuwa na rangi
kama ya dhahabu kwa
nje

• Ukikata kwa ndani ita-


kuwa na rangi ya kama
nyama ya kuchoma iliy-
oiva, yani gray

Kutengeneza Burger

Ikate burger Bun katikati


igawanyike vipande 2

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 100


Panga katikati ya
burger Bun uliyoi-
kata

• Vitunguu
• Nyanya
• Cheese
• Nyama
• Lettuce
• Mayonaise
etc nakadhalika

Burger ipo Tayali kuliwa,


kuuzwa, kupostiwa etc

Bon Apetit

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


101
Piza

102
Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery
RECIPE YA KUPATA DONGE/DOUGH LA PIZZA

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


Mimina recipe yote ndani ya dish

Weka maji kikombe kimoja

Anza kukanda huku ukiongeza maji


kidogo kidogo lakini usizidishe nusu
lita

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 105


endelea kukanda mpaka up-
ate donge lililochanganyika
vizuri namna hii.

kata gram 2oo na isukume


kama chapati mpaka upate size
ya piza unayoitaka

Donge la Pizza likiwa tayari li-


natakiwa liwe na mviringo huu

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 106


Baada ya kupata donge

1.katakata 2. Kaanga vi- 3. Ongezea nyanya Utapata rost


nyanya 3 na tunguu kwenye ajinamoto na viun- nzito
vitunguu2 mafuta jikoni go vingine

Isambaze Rost kwenye donge la


piza

Katia katia cheese juu yake

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 107


Ongezea vitunguu juu yake.
unaweza pia:-

1. kuchemsha nyama ya
kuku na kuikatkata na
kuongezea kupata chicken
Piza

2. kuchemsha nyama na
kuisaga au kuikatakata
kupata beef pizza

3. Kuweka vipande vya sau-


sage etc

Set moto wa Oven


kwenye 200 na iweke Piza
ndani ya Oven na ioke
kwa dakika 10

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 108


Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 109
CROIS-
SANT/
MEAT PIES/
SAUSAGE

110
RECIPE YA CROISSANT, MEAT PIE NA SAU-
SAGE ROLL

Utahitaji Pia kuwa na:-


1. Blue Band au Margarine Robo kilo

2. Mayai Matatu

3. Nyama ya Kusaga Nusu kilo

4. Vitunguu,

5. Sausages
Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery
Weka recipe kwenye dish na Onge-
za maji kidogo kidogo wakati un-
akanda
• Kanda mpaka upate Donge zito
kabisa na litakuwa gumu gumu
kiasi.

Lisukume lote kwa pamoja


kama chapati

Weka wastan wa gram 50 za


margarine au blue band au puff
paste kama utakuwa nayo.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 112


Ipake na kuisambaza blue band
kwenye sehemu zote za donge hala-
fu likunje donge kama ifuatavyo:-

Ukimaliza kulikunja
• lisukume tena lote kama chapa-
ti na litarudi kuwa kubwa tena

• Likunje tena (bila kupaka cho-


chote) na lisukume tena kwa
mara ya 2

• Ukimaliza kusukuma mara ya


pili likunje tena na kulisukuma
mara ya 3

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 113


Funika, sukuma na kukunja
mara 3 na ukikunja mara ya 4
usisukume

Ukikunja mara ya 4 utapata


donge kama hilo pichani kush-
oto

Liweke kwenye fridge au freezer


lipoe kidogo tu kama dakika 20
zinatosha

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 114


Ukilitoa kwenye freezer lisukume tena na lirudi
kuwa pana . Jaribu kulipa shape ya mraba au pembe
nne yoyote tu. Tutalitumia donge hili kutengeneza:-

1. Croissant

2. Meat Pie (andaa nyama ya kusaga)

3. Sausage Roll

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 115


1.Croissant

116
Ili kupata croissant anza na
kulikata donge katika pem-
be 3 za namna hiyo katika
picha kushoto

Jaribu kuinyoosha pem-


be tatu kadri unavyowe-
za

Weka chochote un-


achotaka kiliwe na
croissant kwenye seh-
emu pana mwanzoni
mwa pembe 3 halafu
anza kuikunja kama
picha chini inavyoo-
nyesha

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 117


Ukishaikunja croissant
kwa hatua kama zina-
vyoonekana katika picha
iliyotangulia basi kin-
achofuatia ni kuipaka
mayai kwa juu.

Ukimaliza kupaka mayai


washa Oven kwenye joto
200 juu na chini na iache
ipate moto kwanza kwa da-
kika 10 halafu ingiza crois-
sant zi bake kwa dakika 10.
Lakini uwe unaangalia zis-
iungue.

UIkiona zimebadilika rangi


vizuri basi zitakuwa zimeiva
. Zitoe.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery


118
2. Meat Pie

119
Tunatumia donge lililoto-
ka kwenye freezer amba-
lo tulilitumia kutengeza
Crouissant hapo juu au
page zilizotangulia

Tafadhali ona picha ku-


shoto...anza kwa kukata
shape ya vipande vya mra-
ba wastan wa inchi 3 kila
upande

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 120


• Weka nyama ya kusaga am-
bayo tayari ulishaiandaa. Un-
aweza ukachanganya na may-
onaisse halafu ndio uiweke
• Ukishaweka nyama paka
mayai sehemu zote pembeni
ya nyama

Kwa kuwa nyama itakuwa


katikati basi likunje donge
ili uipate pembe tatu kama
unavyoona kwenye picha
huku nyama ikiwa katikati

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 121


shikizia au kandamizia
kwa vidole pembeni

Tumia upande wa nyuma


wa umma kugandamizia
na itaacha urembo wa mis-
tri mistari

zoezi la kufunika likikami-


lika paka ute wa mayai juu
yake.

Washa Oven ianze kupa-


ta moto wa nyuzi 200 kwa
dakika 10 kabla hujaanza
kubake

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 122


Ziingize kwenye oven yenye
moto tayari wa nyuzi 200
juu na chini na iache iji bake
kwa dakika 10.

Ukiona zimebadilika ran-


gi na kuiva vizuri zitoe
kwenye oven. Meat Pie zipo
tayari.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 123


3. Sausage
Roll

124
Tunatumia donge ambalo tulilitoa kwenye
freezer na kulitumia kutengenezea Crois-
sant na Meat Pie hapo juu’

• Hatua ya kwanza ni kulishape donge


liwe katika shape ya pembe nne

• Hatua ya Pili :-Kata kwa urefu vipande


vyenye upana mdogo kuliko Urefu wa
Sausage (robo tatu ya Sausage) kiasi
ukiweka sausage basi pande zake 2 ziwe
zinachomoza nje ya donge

Picha moja ni zaidi ya kuandika maneno


elfu moja. Tafadhali ona picha ya 2 kulia na
picha ukurasa unaofatia.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 125


Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 126
Ukishamaliza kuzungushia
donge kwenye sausage

• lipake tray la ku bake ma-


futa na zipange
• Washa Oven na weka joto
200 juu na chini. wacha
Oven ipate moto kwanza

chana kidogo na kisu kwa juu


kama unavyoona katika picha
kushoto

Zipake rolls mayai kwa juu

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 127


Ziingize katika Oven am-
bayo tayari ina moto nyuzi
200 na Rolls zi bake kwa
kama dakika 10. uwe un-
aangalia zisiungue

Ukisha jihakikishia zi-


meiva zitoe kwenye
Oven. Zipo tayari.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 128


Hitimisho
Hongera sana kwa kuupata ujuzi kwani nizaidi ya degree wapatazo wengi
mavyuoni.

Ni zaidi ya diploma na vyeti vilivyotunzwa makabatini na wengi kusub-


iria kuajiriwa ambapo ajira imekua mtihani na ujuzi ndio ujanja na mahali
penye wigo mkubwa wa kufanikiwa nakutajirika.

Niwewe tu kuamua saa na muda wakutengeneza pesa kupitia ujuzi huu.

Kwani biashara ya chakula hususani vitafunio haijawahi kutosheleza,uhitaji


ni mkubwa wakati wote ,niwewe tu kuutumia ujuzi huu kwa viwango na
utaalam wakujiongeza kukabiliana na uhitaji na soko kwa ujumla.

Kwa mtakaoonza biashara kupitia ujuzi huu hakikisha unatumia vizuri


mitandao ya kijamii kufikia soko kubwa zaidi,usitegemee tu wanaokuzungu-
ka.

Mara nyingi unapoanza biashara wanaokuzunguka hawawezi kuwa wateja


wako kwa mwanzo,ni kama hawaaamini unachofanya mpaka baadae sana
ndio utawaona tena wachache,sapoti yao hawa watu huwa haipo au ni ndogo
sana.

Jitahidi kutumia mitandao ya kijamii ,soko lipo tena kubwa ,usichoke


kupost,kuwekea bei bidhaa yako na kueleza unapopatikana,kuwa mbunifu
zaidi. hata ukipata like 1 tena kutoka kwa mama yako wewe usikate tamaa,
endelea ku post.

Huitaji ofisi wakati unaanza,nyumbani ni ofisi tosha kwa kuanzia hata


nakuendelea nikukubalika tu na kuaminika nawatu au wateja wako kwani
watakufata popote ulipo.

vifaa hivyo hivyo ulivyonavyo nyumbani ,utaongezea vichache tu,hakika hii


ni fursa kubwa kwako wewe uliepata bahati yakuwa na hiki kitabu itumie
ipasavyo.

Copyright(c): 2022 by Machoke & GIF Bakery 129

You might also like