You are on page 1of 236

MAPISHI YA VITAFUNWA

MBALIMBALI
YALIYOMO

1. Mapishi ya chapati
2. Mapishi ya chapati za maji
3. Mapishi ya Maandazi ya kawaida
4. Mapishi ya Maandazi ya kuoka
5. Mapishi ya Half Keki
6. Mapishi ya Kachori
7.Mapishi ya skonsi
8. Mapishi ya
vitumbua 9.Mapishi ya
sambusa za nyama
10.Mapishi ya
sambusa za viazi
11.Mapishi ya bagia
dengu
12. Mapishi ya mikate ya
mchele/mikate ya kumimina
13. Mapishi ya bagia za kunde
14. Mapishi ya mkate wa ndizi mbivu
15. Mapishi ya kababu
16. Mapishi ya Egg chop
17. Mapishi ya Donuts

18. Mapishi ya ubuyu wa Zanzibar


19. Mapishi ya chocolate
20. Mapishi ya katlesi za samaki
21. Mapishi ya biskuti
22. Mapishi ya kashata
za chocolate 23.Mapishi
ya kalimati
24. Mapishi ya kashata nzima

25.Mapishi ya keki za
vikombe 26.Mapishi ya
keki za kuganda
27.Mapishi ya
shawarma
28.Mapishi ya
chauro 29.Mapishi
ya jalebi
30.Mapishi ya pizza za Zanzibar – Mikate

ya nyama
31. Mapishi ya vitumbua vya
maembe 32. Mapishi ya
biskuti za tangawizi
1.MAPISHI YA CHAPATI (NJIA YA

KWANZA)

MAHITAJI
1. Ngano kilo moja
2. Mafuta ya kupikia kwa ajili ya
kukandia robo tatu ya kikombe kidogo
(yaani kikombe kijae na kuacha nafasi
kidogo) au siagi (blueband au
margarine) vijiko vitatu vya chakula au
samli nusu kikombe
3. Chumvi kijiko kimoja na nusu
cha chai 4.Sukari kijiko kimoja
cha chakula 5.Maji ya
uvuguvugu
6.Mafuta ya kupaka chapati na ya
kuchomea chapati.
Kikombe kinachozungumziwa hapa ni
kikombe cha robo lita – 250 mls
*Kama unatumia siagi au samli pasha
moto kwanza ili ziyeyuke.

MAPISHI
KUKANDA CHAPATI NA KUKUNJA
1. Mimina ngano katika
beseni,mimina humo chumvi na
sukari kisha changanya
2. Mwagia mafuta ya kukandia pande
zote za ngano kisha changanya vizuri
3. Anzakumwagia maji ya uvugu
vugu huku ukichanganya unga na
maji taratibu,hakikisha huzidishi
maji.
4. Ngano ikishalowa maji anza
kukanda, kanda ngano kwa dakika
chache kama 15 kisha iache na ifunike
kwa muda wa dakika 15
5. Funuangano kisha kanda tena kwa
dakika 10, ifunike tena kwa muda wa
dakika 10
6. Funuangano kisha tengeneza
madonge madonge ya kiasi cha chapati
unachohitaji – Kwa ngano kilo moja
unaweza kutengeneza madonge 5 hadi
20 inategemea unahitaji chapati za kula
nyumbani au biashara.
7. Andaamafuta katika kibakuli na kijiko
cha kuchotea mafuta, sukuma donge
moja kutengeneza chapati kisha kwa
kutumia tumbo la kijiko pakaa mafuta
kwa juu hadi mafuta yaenee, kisha kunja
chapati kama unavyokunja mkeka, kisha
zungusha hiyo chapati kama
unavyozungusha kamba ili kutengeneza
kama kiota cha kutagia kuku au ndege,
mwisho wa kuzungusha pachika ile
ngano kwa chini ili isijifungue, kisha
weka katika sinia,
8. Endelea kuzungusha madonge yaliyobaki.
9. Anzakusukuma hayo madonge
ulozungusha katika kibao cha chapati,
kumbuka kunyunyuzia unga na kupaka
msukumio unga endapo chapati
itanata katika kibao.Hakikisha
unasukuma chapati
kuanzia pembeni kuja kati ili kupata
duara zuri,pia usisukume sana kati ili
chapati isiwe nyembamba katikati na
kusababisha iwe ngumu wakati wa
kuchoma.

KUCHOMA CHAPATI
1. Moto wakuchomea chapati
unatakiwa usiwe mkali sana wala
mdogo sana, yaani iwe kati na kati
kuelekea kwenye ukali.
2. Wekakikaango cha chapati jikoni
kisha weka chapati uliyosukuma, iache
ipate moto hadi utakapoona inaanza
kuinuka kwa kutoa vipulizo pulizo,
hapo iegeuze upande wa pili, paka
mafuta pande zote kwa tumbo la kijiko
upande uliogeuza kisha pindua tena
choma upande uliopaka mafuta, huku
ukipaka mafuta upande usio na mafuta,
hakikisha unaizungusha zunguusha
chapati kwa kijiko na unaifunua funua
kuona kama imeiva.
Ukiona upande wa chini umebadirika
rangi na kuwa kahawia, geuza chapati
upande huu ambao nao umeupaka
mafuta, kisha choma kwa kuzunguusha
zunguusha na kwa kufunua funua hadi
uone nao umebadirika rangi na kuwa
kahawia.

3. Toa
chapati hifadhi katika sahani au
hotpot na funika ili zilainike zaidi.
4. Endelea kuchoma chapati nyingine.
MAPISHI YA CHAPATI (NJIA YA
PILI) – NJIA NYEPESI/NJIA YA
BIASHARA
Njia hii ni njia nyepesi na inafaa kwa
wafanya biashara wa chakula
wanaohitaji kupika chapati nyingi
kwa wakati mmoja, kwa maana
hauhitaji kukunja chapati zako.
Tofauti hapa ni kwamba mafuta ya
kukandia ni mengi, pia utaikanda
ngano kidogo na utaifunika kwa muda
wa saa 1 ili ilainike, na utaikanda tena
kidogo kama dakika 10 ili kuiweka
vizuri.

MAHITAJI
1. Ngano kilo moja
2. Mafuta ya kupikia kwa ajili ya
kukandia kikombe kimoja na nusu au
siagi (blueband au margarine) vijiko
vinne vya chakula au samli kikombe
kimoja.
3. Chumvi kijiko kimoja na nusu
cha chai 4.Sukari kijiko kimoja
cha chakula 5.Maji ya
uvuguvugu
6.Mafuta ya kupaka chapati na ya
kuchomea chapati.
*Kama unatumia siagi au samli pasha
moto kwanza ili ziyeyuke.

MAPISHI
KUKANDA CHAPATI NA KUSUKUMA
1. Mimina ngano katika
beseni,mimina humo chumvi na
sukari kisha changanya
2. Mwagia mafuta ya kukandia pande
zote za ngano kisha changanya vizuri
3. Anzakumwagia maji ya uvugu
vugu huku ukichanganya unga na
maji taratibu,hakikisha huzidishi
maji.
4. Ngano ikishalowa maji anza
kukanda, kanda ngano kwa dakika
chache kama 15 kisha iache na ifunike
kwa muda wa saa nzima.
5. Funuangano kisha kanda tena kwa
dakika 10.
6. Funuangano kisha tengeneza
madonge madonge ya kiasi cha chapati
unachohitaji – Kwa ngano kilo moja
unaweza kutengeneza madonge 5 hadi
20 inategemea unahitaji chapati za kula
nyumbani au biashara.
7. Sukumachapati moja kwa moja bila
kukunja na anza kuchoma.
Utaratibu wa kuchoma ni ule ule.
*Tumia kikaango kizito au non-stick
pan ili kupata matokeo mazuri ya
chapati.
2.MAPISHI YA CHAPATI ZA MAJI

MAHITAJI
1.Unga wa ngano
nusu kilo 2.Mayai
mawili
3.Maziwa robo kikombe
cha chai 4.Hiriki ya unga
nusu kijiko cha chai
5.Blueband au margarine kijiko kimoja
cha chakula 6.Sukari kijiko kimoja cha
chai
7. Chumvi kijiko kimoja na nusu cha chakula
8. Karoti saizi ya kati
moja 9.Hoho saizi
ya kati moja
10.Kitunguu maji
kimoja 11.Maji
12.Mafuta ya kupikia

MAPISHI

1. Katakatakitunguu maji na hoho


katika vipande vidogo dogo sana kisha
saga karoti
2. Katika
bakuli kubwa mimina unga wa
ngano kisha mimina viungo vyote
3. Mimina maziwa
4.Mimina ute wa
mayai 5.Mimina
chumvi na sukari
6. Yeyusha
blueband au margarine
kwa kuipasha kisha mimina humo
7. Anza
kumimina maji huku
unachanganya na mixer ya mkono au ya
umeme
8. Mchanganyiko wako unatakiwa uwe
mzito kiasi na usiwe na mabuja buja ya
unga
9. Weka kikaango cha chapati jikoni
katika moto wa wastani kisha acha
kikaango kipate moto kiasi.

10. Mimina mafuta ya kupikia kiasi cha


nusu kijiko cha chakula kisha
yatandaze
11. Chota
uji uji wa chapati kwa kikombe
au upawa kisha tandaza katika
kikaango
12. Acha chapati ikauke kisha igeuze
upande wa pili,upande wa juu
miminia mafuta kidogo na tandaza na
pembeni ya kikaango mimina mafuta
kiasi, ikandamize kandamize chapati
yako huku unasambaza mafuta kwa
tumbo la kijiko.
13. Pinduatena chapati acha kwa
sekunde chache kisha itoe, hakikisha
chapati imekuwa na rangi ya brown
(kahawia)
14. Endelea hivi kwa uji wa chapati uliobakia.

*6* Kama hauna margarine au


blueband mimina mafuta kijiko
kimoja cha chakula katika bakuli
wakati wa kuchanganya
*9* Tumia non-stick frying pan kwa
matokeo bora ya chapati zako
*Unaweza usiweke
maziwa,karoti,hoho,na blueband
kama hauna vitu hivyo
*Unaweza ukatumia tui la nazi kama
hauna maziwa kutengeneza chapati
zako kwa ladha bora zaidi
3.MAPISHI YA MAANDAZI –
(MAANDAZI YA NAZI NA KAWAIDA)

MAHITAJI
1.Unga wa ngano
kilo mbili 2.Nazi
kubwa moja
3.Hamira kijiko kimoja cha
chakula 4.Sukari nusu
5. Hiriki kijiko kimoja cha chai
6. Baking powder kijiko kimoja cha
chakula 7.Mafuta ya kupikia kikombe
kimoja cha robo lita

MAPISHI
1. Weka
unga wa ngano katika sufuria
kubwa au beseni
2. Miminasukari,hiriki,hamira na
baking powder kisha changanya
kwa pamoja na unga wa ngano.
3. Chemsha mafuta ya kupikia katika
sufuria ndogo hadi yawe ya moto.
4. Kwauangalifu miminia mafuta ya
moto katika unga wa ngano huku
unachanganya na unga wa ngano kwa
mwiko.
5. Chukuatui la nazi miminia kwenye
ngano ukiwa unakanda hiyo ngano,
unamimina kidogo kidogo hadi
utakapoona ngano ni laini
6. Ukimaliza
kukanda funika ngano yako
na ungo au kitambaa kisha weka
sehemu yenye joto kidogo acha kwa
muda wa kama saa mbili hivi hadi
ngano yako iumuke.
7. Funua
ngano yako kisha fanya
kama unaikandamiza na ngumi ili
upepo utoke kisha ikusanye vizuri
kama duara.Ikate kate kisha
tengeneza maduara kadhaa (mfano
maduara 10) ili usipate shida wakati wa
kukata vipande
8. Sukuma hayo maduara kama
chapati nene na katakata vipande
vipande kisha anza kuchoma
maandazi yako kwa kuanzia vile
vipande vya mwanzo kukatwa
9. Hakikisha
moto si mkali sana ili
maandazi yaive vizuri.

10. Hakikishamaandazi yanakuwa na


rangi ya kahawia kwa nje (Choma
upande moja kwa dakika 3 hadi 4 kabla
ya kumalizia kuchoma upande
mwingine)
4.MAPISHI YA MAANDAZI YA KUOKA

Mahitaji na hatua za kukanda maandazi


ya kuoka ni kama vile maandazi ya
kawaida, tofauti hapa ni kwamba
maandazi hauyakaangi katika mafuta
bali unayaoka katika oven au jiko la
mkaa
NAMNA YA KUOKA
MAANDAZI A.KWA
KUTUMIA OVEN
1. Washaoven nusu saa kabla set joto la
oven katika digrii 120 C au 248 F
2. Pakamafuta trei la kuokea vitu,
kisha panga maandazi katika trei kisha
weka trei humo katika
oven na acha maandazi kwa muda
wa nusu saa hakikisha yamebadirika
rangi
3. Fungua
oven kisha toa trei na acha
maandazi yapoe.

B.KWA KUTUMIA JIKO LA MKAA


1. Chukua sufuria kubwa, kisha tandika
foil ndani yake, kisha paka mafuta foil
kisha panga maandazi humo
2. Washa jiko kisha punguza makaa ya
moto yabaki kidogo sana, kisha weka
sufuria yenye maandazi ifunike na
mfuniko wa bati kisha weka makaa ya
moto kwa juu kiasi kisha acha kwa
muda wa nusu saa.
3. Funua sufuria, toa mandazi.
5.MAPISHI YA HALF KEKI

MAHITAJI
1.Unga wa ngano
kilo moja 2.Sukari
kikombe kimoja
3.Baking powder kijiko kimoja na
nusu cha chai 4.Baking soda nusu
kijiko cha chai
5.Hiriki ya unga robo kijiko cha
chai 6.Maziwa fresh kikombe
kimoja (ukihitaji)
7. Siagi vijiko 3 vya chakula au mafuta ya

kupikia

vijiko vitatu vya chakula


8. Vanilla kijiko kimoja cha chai (ukihitaji)
9. Mayai mawili (ukihitaji)

10. Chumvi kijiko kimoja na nusu


cha chai 11.Maji ya uvuguvugu
12.Mafuta ya kupikia

*Vitu kama maziwa,mayai hivyo ni vya


kuongezea, unaweza usiweke kutokana
na bajeti yako.

MAPISHI

1. Katikabeseni au bakuli kubwa


mimina unga wa
ngano,sukari,chumvi,hiriki,baking
powder,baking soda, kisha changanya
vizuri.
2. Tengeneza kama shimo katika unga
wa ngano kisha mimina siagi,mimina
maziwa mimina vanilla na mimina ute
wa yai kisha changanya vizuri na unga.
3. Anzakukanda unga wa ngano kwa
maji ya uvuguvugu hadi uwe mgumu
mgumu lakini sio sana
na usinate kwenye chombo wala
kwenye mikono.Ngano ya half keki
haitakiwi kuwa laini kama ya
maandazi
4. Tengenezaduara kubwa kisha lipake
mafuta na paka mafuta kwa pembeni
katika chombo cha kukandia.
5. Funika
ngano kwa muda wa dakika 40
hadi saa 1

6. Funuangano kisha ikate katika


madonge makubwa kiasi kama
kabichi dogo
7. Sukuma madonge hayo kama chapati
nene kiasi kisha anza kukata vipande
vya half cake.
8. Weka kikaango katika moto wa
wastani kisha kaanga half keki zako hadi
ziwe na rangi ya kahawia kwa nje, na
geuza upande wa pili.
9. Toa
half keki katika kikaango kisha
ziweke katika chujio au tissue ili zichuje
mafuta.
10. Half keki zipo tayari
6.MAPISHI YA KACHORI ZA NGANO

MAHITAJI
1.Viazi mbatata sado moja
na nusu 2.Vitunguu thomu
punje tano kubwa
3.Kitunguu maji kikubwa
kimoja 4.Pilipili moja kubwa
5.Limao kubwa moja na
kipande 6.Ngano nusu kilo
7.Chumvi kiasi
Ongeza vitu hivi katika viazi wakati
unavichemsha ukihitaji kutokana na
bajeti yako:-
-Manjano:- nusu kijiko cha chai
-Tangawizi iliyopondwa:- Kijiko kimoja cha
chai
-Pilipilimanga ya unga:- nusu
kijiko cha chai huwekwa viazi
vikishaiva
-Binzari nyembamba ya unga nusu kijiko
cha chai
-Karoti ya kusaga huwekwa wakati wa
kuponda viazi
-Garam masala:- Kijiko kimoja cha chai
MAPISHI
1. Menyaviazi kisha kata vipande
vipande vya nusu kwa nusu
2. Menya vitunguu saum na vitunguu
maji kisha vikate katika vipande vidogo
vidogo kisha
pasua pilipili na toa mbegu zake na
katakata pilipili katika vipande vipande
Pilipili tunaiweka kwa ajili ya ladha tu
na si kwa ajili ya kuwasha, ndio maana
tunaitoa mbegu zake.Hivyo usihofu
kuwa kachori zitawasha.
3. Wekaviazi katika sufuria mwagia
chumvi ya kutosha kisha chemsha hadi
mvuke uanze kutokea
4. Mwagia vipande vya kitunguu maji
na vitunguu saum na pilipili humo
kwenye viazi kisha funika.

5. Viazivikishaiva funua kisha mwaga


viazi katika beseni pamoja na viungo
vyote ulivyoweka na anza kuponda
ponda vizuri.
Viazi visiive sana, yaani viive lakini
viwe vigumu kama vina kiini kwa
mbali.
Kama viazi vimeshaiva na bado sufuria
ina maji, hakikisha unabana sufuria kwa
mfuniko kwa mikono miwili kisha mwaga
maji yaliyobaki, usitoe kiazi kimoja
kimoja kwa sababu vitapondeka
pondeka.

6. Tengeneza vidonge donge vya duara


7. Chukua sufuria ya wastani weka maji
kidogo mwagia rangi ya manjano katika
maji kisha mwagia ngano humo na
chumvi kiasi na tengeneza rojo la ngano
zito, ongeza maji kiasi kama rojo la
ngano ni zito sana, rojo la ngano
linatakiwa liwe zito ili wakati wa
kukaanga kachori zisipasuke
pasuke.Tumia blenda au mixer
kutengeneneza rojo la ngano, kama
huna tumia mwiko au kijiko,ongeza rangi
kama utahitaji

8. Weka kikaango chenye mafuta jikoni


kisha acha mafuta yapate moto sana
9. Unatakiwa
uwe na upawa wa
kuchanganyia madonge katika rojo la
ngano ambao pia utatumia
kutumbukiza madonge yako katika
mafuta yanayochemka,pia unatakiwa
uwe na jaro kwa ajili ya kugeuzia
kachori katika mafuta, pia uwe na
mwiko wa kusupport wakati unageuza
kwa sababu kachori huwa
zinagandana.Kama kachori
zimegandana usizitenganishe wakati
unazichoma zichome hivyo hivyo na
uzigeuze kwa pamoja.
(Chovya madonge ya viazi katika ngano
kisha yachome katika mafuta upande wa
kwanza hadi yakauke,pindua upande wa
pili kisha choma upande huo hadi
ukauke)

Kachori zikiiva zitoe katika mafuta na


ziweke katika chujio ili zichuje mafuta.
7.MAPISHI YA SKONZI

MAHITAJI

1.Unga wa ngano nusu kilo


2.Sukari kijiko kimoja cha
chakula 3.Chumvi kijiko
kimoja cha chai
4. Maziwa fresh kikombe kimoja cha chai
5. Hamira kijiko kimoja
cha chai 6.Siagi vijiko
vitatu vya chakula
7.Maji ya uvuguvugu

MAPISHI
1. Chukuabakuli kubwa changanya
sukari,chumvi,hamira, na maji kiasi ya
uvuguvugu kisha funika acha kwa
dakika 5

2. Pasha siagi kidogo ilainike


3. Katika
bakuli lenye mchanganyiko
wa namba 1, mimina ngano,siagi,na
maziwa kisha changanya vizuri.
4. Endeleakukanda ngano huku
unamimina maji ya uvuguvugu na
kuongezea ngano kidogo taratibu
taratibu hadi ngano iwe laini na hainati
mikononi.
5. Funika
kwa kitambaa ngano yako
acha iumuke kwa dakika 30
6. Funua ngano yako kisha ibinye kwa
ngumi ili itoe upepo, kata madonge ya
saizi unayotaka
7. Chukuasufuria nyepesi pana ya
kuokea kisha ipake siagi au mafuta
sehemu zote na panga madonge
yako uyaachie nafasi kidogo
8. Funika
madonge yako kisha acha
yaumuke tena kwa dakika 15.
9. Funua madonge yaki kisha yapake siagi
au mafuta kwa juu kwa kutumia brush
maalum ya kupakia au kwa kiganja
chako kwa taratibu bila kuzibinya.

10. Washa oven kisha ingiza sufuria yako


au chombo cha kuokea weka moto wa
digrii 200, kisha oka skonsi zako kwa
dakika 25
AU:- Kwa jiko la mkaa chukua sufuria
kubwa ijaze michanga kiasi kisha weka
sufuria yako yenye madonge ya skonsi
humo kisha funika hiyo
sufuria kubwa kwa sinia gumu, kwa juu
weka makaa ya moto ya kutosha na kwa
chini weka makaa ya moto
kiasi, acha kwa nusu saa. AU Chukua
sufuria kubwa iweke foil ndani yake,
paka mafuta na panga skonsi kwa ndani
kisha weka sufuria jikoni makaa yawe
machache kisha funika na weka makaa
kwa juu ya kutosha.

11. Skonsi zipo tayari kwa kula


9.MAPISHI YA VITUMBUA

MAHITAJI
1. Mchele vikombe vitano vya robo lita
2. Unga wa ngano kikombe kimoja
cha robo lita 3.Tui la nazi vikombe
viwili vya robo lita 4.Mayai matano
5.Hamira kijiko kimoja cha
chakula 6.Sukari vikombe
viwili vya robo lita
7.Hiriki vijiko viwili
vya chai 8.Mafuta ya
kupikia.

MAPISHI
1.Loweka mchele usiku kucha
au saa 8 2.Changanya hamira
na tui la nazi.

3. Mimina mchele,ngano,ute wa
mayai,hiriki, tui la nazi katika blenda
kisha saga hadi vitu vyote
vichanganyike vizuri
AU:- Mchele ulioloweka anika juani
kisha saga unga wa kutosha kwa ajili ya
vitumbua, hivyo badala ya kusaga
mchele katika blenda utakuwa
unatumia huo unga unachanganya na
vitu vingine.

4. Chukua maji ya uvuguvugu au ya


baridi kiasi kidogo kisha changanya
na sukari hadi iyeyuke kidogo.
5. Mimina ute wa sukari ndani ya
mchanganyiko kisha saga tena ili
sukari ichanganyike.
6. Miminamchanganyiko katika
chombo kikubwa funika na weka
mahali penye joto kisha acha
mchanganyiko uumuke.
7. Baadaya mchanganyiko kuumuka
weka kikaango cha vitumbua kwenye
moto.

8Mimina mafuta kiasi kwenye


kikaango cha vitumbua kisha
mimina rojo la vitumbua.
9. Vitumbua
vikiiva upande mmoja geuza
upande wa pili pia mwagia mafuta hadi
kiive.

10. Vitumbua tayari kwa kula.


10.MAPISHI YA SAMBUSA ZA NYAMA

NA VIAZI
Utengenezaji wa sambusa unahitaji
ujuzi tu wa kutengeneza manda
Hivyo angalia namna ya kutengeneza
manda
NAMNA YA KUTENGENEZA MANDA ZA

SAMBUSA MAHITAJI

1.Ngano nusu kilo:- ½ Kg.


Wheat flour 2.Maji ya uvugu
vugu:- Warm water
3. Mafuta ya kupikia kijiko kimoja cha
chakula:- 1 tbsp cooking oil
4. Hiriki
ya unga theluthi ya kijiko cha
chai:- ⅓ tsp cardamom powder
5. Chumvi kiasi:- A pinch of salt
MAANDALIZI

1. Kwenye chombo kikubwa mimina unga


wa ngano kisha mimina maji
kiasi,hiriki,mafuta kiasi na chumvi
kiasi kisha kanda hadi ngano iwe laini
kisha ifunike endelea na hatua
zinazofuata.

2. Chukua
ngano yako uliyokanda kisha
igawanye katika madonge kumi kisha
sukuma kutengeneza chapati ndogo
ndogo,
chukua chapati moja ipake mafuta juu
kisha nyunyuzia ngano kidogo na
sambaza kisha weka chapati nyingine
juu yake nayo ipake mafuta na
nyunyuzia ngano kidogo na sambaza
kisha weka chapati nyingine juu,endelea
hadi zifike chapati tano zisukume kwa
pamoja kutengeneza chapati moja
kubwa, kandamiza kidogo kwa kiganja
kwa juu kisha
3. Weka chuma cha kukaangia chapati
jikoni bila kuweka mafuta kisha weka
chapati hizo na
zibabue pande zote mbili hadi ziive bila
kubadirika rangi wala kukauka. Endelea
hivi kwa madonge matano mengine.
4. Banduahizo chapati kisha chukua
chapati moja moja weka kwenye
kibao cha chapati kisha kata sehemu
nne sawa

5. Tengeneza uji wa kugandishia kwa


kuchanganya vijiko vitatu vya chakula
na maji kiasi

6. Katikakila kipande tengeneza umbo


la koni kwa kufunga upande mmoja
kwa ute wa ngano.

MAHITAJI YA UTENGENEZAJI WA
SAMBUSA ZA NYAMA
MAHITAJI
1. Nyama ya kusaga nusu kilo
2. Kitunguu maji
kilichokatwa katika
vipande vidogo vidogo mfano wa
voboxi
3. Karoti iliyosagwa
4. Majani ya giligilani yaliyosagwa kiasi
5. Kitunguu saum nusu kijiko cha chai

mbichi iliyopondwa kiasi – itoe


6. Pilipili
mbegu na kata kipande tu ndio usage
kutokana na wingi wa nyama.
7. Garam masala au beef masala nusu
kijiko cha chai 8.Manda za sambusa
9.Mafuta ya kuchomea sambusa

MAPISHI
1. Chukuanyama mbichi ya kusaga kisha
weka katika sufuria, kamulia limao weka
na tangawizi iliyosagwa na pilipilimanga
ya unga kidogo na chumvi na maji kiasi
kisha chemsha hadi iive.
2. Weka
sufuria au kikaango jikoni kisha
mimina mafuta ya kupikia kiasi acha
yapate moto na mimina vipande vya
kitunguu maji,kaanga hadi vianze
kulainika kisha mimina thomu
iliyosagwa endelea kukoroga kisha
mimina majani ya giligilani
yaliyopondwa kiasi kidogo sana kisha
mimina nyama na changanya vyema
kisha mimina pilipili iliyosagwa
changanya, nyunyuzia garam masala
kisha changanya vyema, hakikisha
moto ni wa wastani, kamulia tena
limao kiasi kidogo weka chumvi kiasi
changanya na funika.

3. Funua epua acha ipoe.


4. Chukuamanda za sambusa jaza
nyama uliyopika humo na anza
kuchoma sambusa.
5. Katika
kuchoma hakikiasha sambusa
zimekuwa brown zitoe na zichuje
mafuta.
6. Sambusa zipo tayari.

Ukihitaji kutengeneza sambusa za viazi,


unachofanya ni kukata kata viazi katika
vipande vidogo vidogo kisha
utavichemsha ndani yake utaweka
viungo mbalimbali kama vile vitunguu
maji kidogo,thomu,pilipili na vinginevyo.
Vikiiva utajaza viazi hivyo katika manda
za sambusa na utachoma.
11.MAPISHI YA BAGIA DENGU

MAHITAJI
1.Unga wa dengu kikombe kimoja au
robo kilo 2.Manjano robo kijiko cha
chai
3.Binzari nyembamba ya unga nusu
kijiko cha chai 4.Kitunguu saum
kilichosagwa robo kijiko cha chai
5.Baking powder nusu kijiko cha chai
6. Kitunguu maji kimoja
7. Hoho moja

dogo 8.Pilipili
mbichi kiasi
9.Pilipilimanga robo kijiko
cha chai 10.Chumvi kiasi
11.Mafuta ya kupikia

MAPISHI

1. Katakata
pilipili mbichi na kitunguu
maji na hoho katika vipande vidogo
vidogo sana.
2. Katika bakuli kubwa mimina unga
wa
dengu,manjano,pilipilimanga,chumvi
na baking powder na maji kiasi kisha
changanya
3. Mimina viungo vyote vilivyobaki
katika bakuli kisha changanya vizuri
4. Miminamaji kidogo kidogo huku
unachanganya mchanganyiko (Tumia
mwiko au kipekecho cha mkono au
kipekecho cha umeme (mixer) au
blenda)

5. Hakikisha mchanganyiko unakuwa uji


uji mzito
na si mwepesi sana ambao hauna
madonge.

6. Funika uji uji na acha kwa dakika 20

7. Wekakikaango jikoni kisha mimina


mafuta ya kupikia na acha yapate
moto wa wastani

8. Chukua kijiko cha chakula kisha chota


uji uji wa bagia dengu na mimina katika
kikaango, chota michoto kadhaa
kutokana na ukubwa wa kikaango
chako.
9. Chomabagia zako na hadi ziwe
kahawia upande mmoja na uzigeuze
upande wa pili
10. Ziweke bagia zako katika chujio
lililo juu ya sufuria au juu ya tissue
ili zichuje mafuta
11. Bajia za dengu zipo tayari
12.MAPISHI YA MKATE WA
MCHELE/MKATE WA KUMIMINA

MAHITAJI

1. Unga wa mchele vikombe


vitatu vya chai (Kikombe cha
robo lita - 250 mls)
2. Sukari kikombe kimoja
na nusu 3.Hamira kijiko
kimoja cha chai 4.Yai
moja
6. Tuila nazi vikombe viwili vya chai
(Tui zito na jepesi)
7. Hiriki kijiko kimoja cha chai

MAPISHI

1. Kama hauna unga wa mchele,


chukua mchele vikombe vitatu vya
chai kisha loweka katika maji usiku
kucha.
2. Wekahamira katika tui zito kisha
koroga hadi hamira upate
mchanganyiko mzito
3. Chukua blenda kisha weka mchele
(unga wa mchele),hiriki,hamira na tui
la nazi kisha saga hadi vichanganyike
vizuri, lakini zibakie chenga chenga
kidogo za mchele.
Kama hauna blenda weka unga katika
chombo kikubwa kisha changanya na
vitu vingine humo na koroga na
mwiko.

4. Mimina
mchanganyiko katika
chombo kikubwa kisha funika na acha
uumuke kwa dakika 40.

5. Funuachombo chako kisha mimina


sukari na ute wa yai kisha koroga vizuri.

6. Chukuasufuria au chombo cha kuokea


kisha pake mafuta pande zote.
7. Mimina mchanganyiko katika
chombo cha kuokea.

8. Washa oven kisha set moto wa oven


katika digrii 350 C au 572 F
9. Achamkate kwa dakika 40 hadi uwe
na rangi ya kahawia kwa juu.
10. Toachombo cha kuokea katika oven
kisha acha mkate upoe halafu
ukatekate vipande.
Kama unaoka kwa jiko la gesi au mkaa,
unahitajika uwe na sufuria kubwa
ambayo ndani yake utaweka chombo
chako cha kuokea, kisha washa moto
uwe mkali na funika kwa juu weka
makaa ya moto kidogo kwa muda wa
dakika 40.
Mkate wa kumimina tayari kwa kula.
13.MAPISHI YA BAGIA ZA KUNDE

MAHITAJI
1.Kunde vikombe viwili vya
robo lita 2.Kitunguu maji
kimoja
3. Pilipili mbichi kiasi

4. Juisi ya limao vijiko viwili vya


chakula 5.Baking powder
kijiko kimoja cha chai
6. Kitunguu saum kilichosagwa kijiko kimoja

cha chai
7. Tangawizi iliyosagwa kijiko
kimoja cha chai 8.Curry powder
kijiko kimoja cha chai 9.Chumvi
kiasi
10.Mafuta ya kupikia

MAPISHI

1. Osha
na loweka kunde kwenye maji ya
moto kwa masaa 8 au usiku mzima
2. Katakatakitunguu maji na pilipili
mbichi katika vipande vidogo vidogo
3. Chuja maji katika kunde
4. Miminakunde tangawizi,kitunguu
saum,curry powder,pilipili, na maji ya
limao kwenye
mashine
ya kusagia chakula au blender kisha
saga na zisilainike sana au twanga vitu
vyote kwenye kinu.
5. Kunde zikilainika ongeza vipande
vya kitunguu maji kisha saga kiasi na
vitunguu visisagike sana.

6. Weka
mchanganyiko kwenye bakuli
kubwa.

7. Ongeza
chumvi na baking powder,
changanya vizuri

8. Tengeneza bagia katika maumbo ya


duara
9. Wekakikaango jikoni kisha mimina
mafuta na acha yapate moto kiasi

10. Anza kukaanga bagia zako hadi


zibadirike rangi na kuwa kahawia.
11. Wekabagia zilizoiva katika chombo
chenye tishu au chujio ili kuchuja
mafuta.
12. Bagia za kunde zipo tayari kwa kula
14.MAPISHI YA MKATE WA NDIZI

MAHITAJI
1.Unga wa ngano nusu kilo:- ½ Kg
Wheat flour 2.Sukari robo kilo:- ¼
Kg. sugar
3. Mayai mawili:- Two eggs

4. Siagi vijiko viwili vya chakula:- 2


tbsp butter 5.Ndizi mbivu tatu:- 3
banana
6.Karanga au korosho za
kukaanga 7.Chumvi nusu kijiko
cha chai:- 1 tsp salt
8. Bakingsoda kijiko kimoja cha chai:- 1
tsp baking soda
9. Bakingpowder robo kijiko cha
chai:- ¼ baking powder

MAPISHI

1. Pasha siagi moto hadi iyeyuke


2. Katikachombo kikubwa mimina
sukari,mimina siagi kisha changanya
vizuri hadi sukari iwe rojo rojo
3. Pasulia mayai humo kisha koroga vizuri
4. Kwenye chombo hicho hicho
mimina unga wa ngano,baking
powder na baking soda kisha
changanya vizuri.
5. Saga ndizi kwa maji kiasi katika blenda
6. Mimina rojo la ndizi mbivu kwenye
bakuli yenye mchanganyiko wa vitu
vyote kisha koroga vizuri

7. Funika
mchanganyiko wako na acha
uumuke kwa muda wa dakika 30

8. Paka
mafuta au siagi chombo cha kuokea
mkate

9. Mimina mchanganyiko wako katika


chombo cha kuokea mkate tupia
karanga au korosho za kukaanga kwa
juu kisha ingiza katika oven

10. Joto la
oven linatakiwa liwe 180 C au
350 F, kama unatumia mkaa weka
chombo cha kuokea katika sufuria
kubwa funika kisha weka jikoni katika
moto wa wastani.
11. Oka mkate wako kwa muda wa
dakika 30 hadi saa 1, choma kijiti katika
mkate na kikitoka kikiwa kikavu mkate
unakuwa umeiva.
12. Mkate wa ndizi mbivu upo tayari
15.MAPISHI YA KABABU

MAHITAJI
1.Nyama ya kusaga
kilo moja 2.Vipande
vya mkate vitatu
3.Mayai matatu
4. Ungawa binzari nyembamba kijiko
kimoja cha chai au binzari ya kababu
nusu paketi
5. Binzari ya manjano kijiko kimoja cha chai
6. Kitunguu saum kilichosagwa kijiko
kimoja cha chai 7.Tangawizi iliyosagwa
kijiko kimoja cha chai 8.Pilipili mbichi
iliyosagwa kijiko kimoja cha chai 9.Pilipili
manga nusu kijiko cha chai
10.Ndimu kipande kimoja au juisi ya
limao kidogo 11.Chumvi kiasi
12.Mafuta ya kupikia

MAPISHI
1. Chukuabakuli kubwa weka nyama
ya kusaga iliyochemshwa.
2. Loweka vipande vya mkate katika maji
kisha fanya kama una vikamua kisha
vikatekate vipande vipande na
changanya na nyama ya kusaga.
3. Miminaviungo vyote na mayai
mabichi katika bakuli,kamulia ndimu
na changanya vizuri.
4. Lowekachumvi kwenye maji kidogo
kisha mimina kwenye mchanganyiko na
changanya vizuri.

5. Tengeneza
kababu zako katika
maumbo ya viduara au maumbo
ya karoti.
6. Weka kababu zako katika sinia kisha
ziache kwa muda kama saa moja
iliviungo vikolee vizuri.
7. Miminamafuta ya kupikia katika
kikaango acha yapate moto vizuri.
8. Anzakukaanga kababu zako hadi
ziive upande mmoja kisha zipindue
upande wa pili.
9. Toa kababu zako na ziweke
kwenye chujio ili zichuje mafuta.
10. Kababu zako zipo tayari kwa kula.
16.MAPISHI YA EGG CHOP

Ili kutengeneza egg chop, utafuata hatua


zile zile za utengenezaji wa kababu, cha
kuongeza ni mayai ya kuchemshwa
ambayo utayapasua na utayafunika na
nyama ya kusaga ambayo
umeichanganya kwa viungo na
utatengeneza duara kisha utachoma
katika mafuta.
17.MAPISHI YA DONUTS

MAHITAJI
1.Unga wa ngano
kilo moja 2.Mayai
matatu
3.Mayai mawili ya
kutengenezea kastadi
4.Maziwa fresh lita moja
5.Siagi (blueband) vijiko vinne vya
chakula 6.Sukari robo kilo
7.Sukari robo kilo ya
kutengenezea kastadi 8.Hamira
vijiko viwili vya chai
9.Hiriki ya unga kijiko kimoja
cha chai 10.Baking powder
kijiko kimoja cha chai
11.Vanilla vijiko viwili vya chai
12.Chumvi kijiko kimoja cha
chai

13.Maziwa ya unga
robo 14.Mafuta ya
kupikia
MAPISHI
1. Chemsha maziwa fresh nusu lita
kisha yahifadhi kwenye chombo
yapate uvugu vugu
2. Miminahamira katika maziwa ya
uvuguvugu kisha changanya vizuri acha
mchanganyiko kwa dakika 5 hadi
yatokee mapovu.
3. Yeyusha siagi yako hadi iwe kimiminika

4. Chukua blenda kisha mimina


maziwa yenye hamira,mimina siagi
iliyoyeyushwa,mimina
sukari,chumvi,mayai,hamira,vanilla
na baking powder kisha saga hadi
vichanganyike kama una mixer
utaweka ngano yako kisha utamimina
hivi vitu vyote humo na utakanda
ngano yako kwa mixer.

5. Weka ngano katika bakuli kubwa kisha


minina huo mchanganyiko wa kwenye
blenda katika ngano kisha anza kukanda
hadi ilainike na isinate mikononi
utakuwa unaongezea unga wa ngano
kidogo ili ngano yako iweze kubalance
kati ya ugumu kidogo na ulaini kidogo na
isinate mikononi.

6. Ipake mafuta ngano yako kwa juu na


chini pia paka mafuta chombo cha
kuumulia kisha funika ngano yako na
iache kwa saa 1 hadi iumuke
7. Funuangano yako kisha ikandamize
kwa ngumi ili itoe upepo kisha anza
kukata madonge madogo kama 6

8. Sukumahayo madonge kupata chapati


nene kiasi kisha kwa kutumia chombo
chenye shepu ya donati kandamiza
kwenye chapati ili kutoa donati zako.

9. Ziache ziumuke tena kwa muda wa dakika


45

10. Weka mafuta kwenye kikaango


hakikisha moto ni wa wastani acha
mafuta yapate joto kisha anza
kukaanga donati zako hadi ziwe
kahawia.

11. Andaa kastadi kwa kuchemsha


maziwa fresh kisha mimina sukari robo
lita,kisha mimina viini vya
mayai mawili kisha utachemsha huku
unakoroga hadi mchanganyiko uwe
mzito kiasi kama uji.

12. Achakastadi ipoe kisha chukua


donati zako tumbukiza katika kastadi
kisha tumbukiza katika maziwa ya
unga kwa pande zote ili kupata donati
zenye utando mweupe kwa nje.

13. Donati zako zipo tayari


18.MAPISHI YA UBUYU WA ZANZIBAR

MAHITAJI
1.Ubuyu wa mbegu
vikombe vinne 2.Sukari
vikombe 2
3. Maji vikombe 2

4. Unga wa ubuyu nusu


kikombe 5.Pilipili ya unga
robo kijiko cha chai
6. Pilipilimanga ya unga nusu kijiko cha chai
7. Chumvi robo kijiko
cha chai 8.Hiriki robo
kijiko cha chai
9. Ranginyekundu ya chakula au rangi
yoyote ya chakula - kiasi (Anza na
nusu kijiko cha chai)
10. Ladha ya vanilla au vimto kijiko cha chai
kisijae

MATAYARISHO

1. Katika
sufuria,weka maji,sukari,hiriki,
chumvi,pilipilimanga,pili pili ya unga na
rangi. Moto uwe juu kiasi na changanya
vyote hivyo vichanganye vizuri hadi
sukari iyeyuke.

2. Acha
mchanganyiko uchemke
hadi mapovu yaanze kutokea kwa
juu.
3. Anza kukoroga na endelea
kukoroga hadi mchanganyiko
(shira) uwe mzito na mapovu
kupungua

4. Gusamabaki ya shira katika mwiko


kuona kama yananata, ikiwa shira
inanata inakuwa tayari imeshaiva.

5. Epua shira kutoka jikoni acha ipoe kiasi

6. Weka ubuyu wa mbegu katika beseni


au sufuria kubwa kisha mimina shira
kwa kunyunyuzia sehemu zote na
changanya kwa mikono (Unaweza
kuvaa gloves ili kujikinga na joto la
shira)

7. Chukua
unga wa ubuyu anza
kunyunyuzia juu ya mbegu za ubuyu
ambazo umezimwagia shira - Hakikisha
unga wa ubuyu unaenea sehemu zote
na
kuwa makini unga wa ubuyu usimeze
shira katika mbegu za ubuyu -
Hakikisha rangi inaonekana.

8. Anika ubuyu juani ili uwe mkavu

9. Hifadhi
ubuyu katika chombo chenye
mfuniko au weka ubuyu katika
vifungasha vilivyozibwa tayari kwa
kuuza au kwa kula

*Kikombe kinachotumika ni cha kipimo


cha robo lita (250 mls)
19.MAPISHI YA CHOCOLATE

(Vipande 20)

MAHITAJI
1.Cocoa powder:- vijiko 10
vya chakula 2.Sukari:-
vikombe 3
3.Maziwa fresh:- kikombe
kimoja na nusu 4.Siagi (Butter):-
vijiko vinne vya chakula
5. Vanilla:- kijiko kimoja cha chai

tray ya kuwekea chocolate –


6. Silicon
Inapatikana supermarket

MAPISHI
1. Andaa bakuli la bati la umbo la mstatiri
(ikiwa ni bakuli la bati ni vizuri zaidi)
kisha lipake mafuta - Au chukua bakuli la
plastiki kisha weka foil humo iweze
kukaa katika umbo la mstatiri (box) au
tumia silicon tray special kwa ajili ya
kutengenezea chocolate.

2. Mimina unga wa cocoa katika


sufuria, kisha mimina sukari,kisha
mimina maziwa kisha anza
kuchemsha katika moto wa wastani
huku unakoroga hadi malighafi
(ingridients) zichanganyike vizuri.

3. Baadaya vitu vyote kuchanganyika


acha kukoroga na acha mchanganyiko
uchemke na uwe kama uji mzito
4. Epua
sufuria kutoka jikoni kisha
weka siagi na vanilla katika
mchanganyiko bila kuchanganya.

5. Acha
mchanganyiko upoe kiasi na uwe
vuguvugu
6. Chukua kifaa cha kuchanganyia
(mixer) kisha changanya
mchanganyiko hadi uwe mzito.

7. Mimina mchanganyiko katika


chombo ulichokipaka mafuta kisha
acha mchanganyiko ugande kabisa au
hifadhi katika fridge au freezer kwa
saa 1 au 2.
8. Katakata
vipande vidogo vidogo vya
mraba vya chocolate.
9. Chocolate ipo tayari.
10. Hifadhi chocolate katika fridge
Chocolate inaweza kukaa hadi miezi
mitatu bila kuharibika
20.MAPISHI YA KATLESI ZA SAMAKI

MAHITAJI
1. Viazi mbatata robo kilo
2. Samaki
vibua au samaki yoyote
mwenye minofu nusu kilo:- Samaki
mbichi
3. Ngano nusu
kikombe 4.Mayai
matatu 5.Ndimu
moja
6. Kitunguu saum kilichopondwa nusu kijiko

cha chai
7. Kitunguu maji

kidogo 8.Pilipili
mbichi moja
9.Karoti moja
ndogo 10.Chumvi
11. Mafuta ya kupikia

12. Pilipilimanga
ya unga kijiko
kimoja cha chai kisijae sana
MAPISHI
1. Chukua pilipili mbichi ikate nusu na
ondoa mbegu zake zote, chukua nusu
yake ikate kate vipande vidogo dogo
sana
2. Menyaviazi mbatat kisha vikate vipande
vipande

3. Safisha
samaki vyema, kisha kamulia
ndimu,weka kitunguu thomu na
tangawizi na chumvi kiasi anza
kuchemsha hadi maji yakauke, waive
lakini wasilainike sana.
4. Weka viazi katika sufuria kisha
mimina vipande vya kitunguu maji na
vipande vya pilipili mbichi kisha
chemsha kwa maji kiasi hadi viazi viive
lakini visiive sana.

5. Epuaviazi na viponde ponde ndani ya


beseni kwa kutumia chupa au mchi hadi
vipondeke vyote.

6. Chambua miba na mifupa katika


samaki kupata minofu (hakikisha miba
na mifupa yote imeisha) kisha
chambua nyama ya samaki tena
kupata vipande vipande vidogo
vidogo.
7. Mimina vipande vya samaki katika
bakuli lenye viazi
vilivyopondwa,mimina karoti
zilizosagwa na nyunyuzia pilipilimanga
kisha changanya vizuri kwa mwiko.
8. Miminangano katika bakuli,mimina
maji koroga kupata rojo zito

9. Pasua mayai kisha koroga yachanganyike

10. Changanya rojo la mayai na ngano


kwa pamoja kisha koroga vizuri weka
chumvi kiasi.

11. Weka kikaango jikoni,mimina mafuta


ya kupikia na acha yapate moto vizuri

12. Chukua mchanganyiko wa samaki na


viazi kisha tengeneza viduara kama vya
kachori kisha toweza katika rojo la mayai
na ngano na anza kuchoma katika
mafuta, hakikisha upande wa chini
umekauka kabla ya kugeuza upande
mwingine.

13. Hakikisha
katlesi zimekuwa na
rangi ya hudhurungi au kahawia
au brown
21.MAPISHI YA BISKUTI

Idadi:-
Biskuti 12
MAHITAJI
1. Unga
wa ngano aina ya (Plain flour)
gramu 150 au kikombe kimoja
2. Bicarbonate of soda au baking powder
nusu kijiko cha chai
3. Corn flour vijiko 3 na robo vya chakula
4. Sukari
kikombe kimoja (ukipata sukari
ya unga ni vizuri zaidi)
5. Siagi
Vijiko 10 na nusu vya chakula -
(Yeyusha siagi na ipoe)
6. Vanilla nusu kijiko cha chai
7. Yai moja lililopasuliwa na
kuchanganywa 8.Chumvi kiasi

*Siagi unaweza kutumia blueband au


margarine
*Kikombe cha vipimo ni kikombe
kidogo cha robo lita ( 250 mls)

MAPISHI
1. Washaoven katika joto la digrii 180 (C)
au 350 (F)
2. Paka
mafuta vifaa vya kuokea kisha
weka karatasi ya kuokea
3. Pasua yai katika bakuli na lichanganye
kiasi
4. Weka
ngano katika bakuli kubwa kisha
changanya na bicarbonate of soda
5. Mimina sukari,mimina siagi au
margarine iliyoyeyushwa,ute wa yai na
vanilla kisha changanya vyema.

6. Kanda ngano hadi iwe laini kiasi na


isinate mikononi, ifunike katika bakuli
katika muda wa saa 1

7. Baadaya saa 1 ikande ngano tena


kidogo kisha kwa kutumia msukumio
wa ngano (roller) sukuma ngano iwe
kama chapati, mwagia unga kidogo juu
ya ngano na weka unga kidogo kwenye
sehemu ya kusukumia ili ngano isinate.
8. Chukuakisu kisha kata ngano
vipande vipande kisha weka katika
chombo cha kuokea

9. Weka chombo cha kuokea katika oven

10. Oka kwa dakika 12 hadi 15 mpaka


biskuti ziwe kahawia

11. Zitoe
biskuti na ziache zipoe kisha
zihifadhi katika chombo chenye
mfuniko zitumie ndani ya wiki mbili

12. Kumbuka kuzima oven


22.MAPISHI YA KASHATA ZA

CHOCOLATE

MAHITAJI
1.Unga wa Cocoa (Cocoa powder) -
nusu kikombe 3.Maziwa fresh vikombe
viwili
4. Sukari nusu kikombe

5. Corn flour kijiko kimoja cha chai


6. Blueband,margarine au siagi yoyote
vijiko viwili vya chakula
6. Karanga
za kukaanga zilizotolewa
maganda kikombe kimoja
7. Chumvi kijiko kimoja
cha chai 8.Vanilla nusu
kijiko cha chai

MAPISHI
1. Weka sufuria jikoni kisha mimina
maziwa na anza kuyachemsha,
yakiaanza kuchemka mimina
sukari,cocoa na siagi kisha koroga hadi
vitu hivyo viyeyuke.
2. Miminacorn flour humo kisha
endelea kukoroga hadi upate uji uji
mzito.
3. Mimina
karanga humo kisha
changanya vyema kwa kutumia
mwiko
4. Chukua trei ya pembe nne ya kuokea
vitu au kifaa chochote kipana kisha paka
mafuta na mwagia
humo mchanganyiko na sambaza
vizuri katika unene unaohitaji
5. Acha huo mchanganyiko upoe na
uwe mgumu, unaweza ukahifadhi
katika freezer au fridge
6. Toa
trei yako kisha bandua sheet ya
kashata ya chocolate na anza kukata
vipande kwa kutumia kisu au kifaa
maalumu cha kukatia
7. Kashata za chocolate zipo tayari.
23.MAPISHI YA KALIMATI

MAHITAJI
1. Unga wa ngano robo kilo
2. Hamira kijiko kimoja na nusu cha chai
3. Mtindi
nusu kikombe au tui la nazi
au maziwa fresh.
4. Blueband kijiko kimoja cha
chakula 5.Maji
6.Mafuta ya
kupikia 7.Sukari
vikombe vitatu
8. Hiriki robo kijiko cha chai

9. Vanilla
au ladha yoyoye kidogo
kama robo ya kijiko cha chai

MAPISHI

1. Yeyusha blueband
2. Chukua bakuli kisha mimina unga wa
ngano,mimina blueband,mtindi, mafuta
kijiko kimoja cha chakula na hamira
kisha mimina maji kiasi na koroga hadi
uji uwe mzito kiasi na usiwe na mabuja
buja
3. Funika
unga kwa muda wa nusu saa ili
uumuke
4. Weka kikaango jikoni kisha mafuta
ya kupikia yaache yapate moto kiasi.
5. Chota uji wa kalimati kwa kijiko cha
chakula na mimina katika mafuta kisha
choma kalimati zako hadi upande
mmoja uwe kahawia na geuza upande
wa pili nao uwe kahawia kisha toa
kalimati zako ziweke katika chujio au
tissue ili zichuje mafuta.
6. Andaa shira kwa kuweka sufuria
jikoni mimina maji kikombe kimoja,
mimina sukari koroga hadi sukari iwe
nzito na inayonata ukiishika kwa vidole
viwili.

7. Mimina hiriki na rose essense au


vanilla kisha koroga
8. Epua sufuria ya shira acha ipoe kiasi
9. Wekakalimati katika bakuli kubwa
kisha miminia shira humo na
changanya na kalimati zote kwa mwiko
au kupeta kama mchele.
10. Kalimati zipo tayari
24.MAPISHI YA KASHATA ZA KARANGA

NZIMA
MAHITAJI
1.Karanga kilo moja
na nusu 2.Sukari kilo
moja
MAPISHI

1. Chambua karanga kutoa uchafu


2. Osha
karanga vizuri na zianike juani
zikauke maji
3. Zikaange
karanga kwa moto wa
wastani hakikisha haziungui
4. Acha zipoe
5. Pukuchua karanga kutoa maganda
6. Weka sufuria jikoni katika moto
mkali, mimina sukari humo kisha
koroga hadi iyeyuke kisha mimina
karanga humo na koroga
kuchanganya karanga na shira

7. Pakamafuta meza au sinia kubwa


kisha mimina mchanganyiko wa
karanga na shira hapo na sambaza
msukumio wa chapati.

8. Anza kukata kashata zako katika umbo

unalohitaji 9.Kashata zipo tayari


25.MAPISHI YA KEKI ZA VIKOMBE - CUP

CAKES

MAHITAJI
1.Unga wa ngano
nusu kilo 2.Mayai
sita
3.Maziwa kikombe
kimoja 4.Sukari
kikombe kimoja
5. Siagi
(Blueband) kikombe kimoja au
kopo dogo moja
6. Baking powder vijiko viwili vya chai
7. Vanilla kijiko kimoja cha
chai 8.Rose essence robo
kijiko cha chai 9.Chumvi
nusu kijiko cha chai

MAPISHI

1. Kwa kutumia mixer ya chakula au


kipekecho mimina sukari na chumvi
katika chombo kikubwa kisha yeyusha
siagi na mimina katika chombo
chenye sukari kisha changanya vizuri.
2. Pasulia
mayai kwenye hicho chombo
kisha mimina vanilla na rose essence na
changanya vizuri
3. Mimina unga wa ngano
changanya vizuri na mchanganyiko
4. Mimina maziwa kisha changaya
vizuri upate uji mzito
5. Uji usipokuwa mzito mimina maji kiasi

6. Mimina baking powder na


changanya vizuri 7.Acha
mchanganyiko kwa dakika 20
8. Washa oven katika joto la 350 F kwa

dakika 3

9. Chukua trey maalum la kuokea keki


hizi kisha weka karatasi za kuokea keki
hizi humo na chota uji wa keki mimina
humo hadi karibia na kujaa
10. Ingiza trey lako katika oven kisha
oka keki zako kwa muda wa dakika 25
11. Zitoe
keki zako zipange katika sahani
tayari kwa kula.
Kama hauna oven tumia panga
vikaratasi vya kuokea katika sinia
mimina uji wa keki humo kisha weka
sinia katika sufuria kubwa, weka sufuria
katika jiko la mkaa, kwa chini makaa
yawe kidogo na funika kwa mfuniko wa
chuma au bati kwa juu kisha
weka makaa kiasi na endelea kuoka
kwa dakika 25 hadi 30.
26.MAPISHI YA KEKI YA KUGANDA

MAHITAJI
1. Vipandevya biskuti
vilivyovunjwa vunjwa vikombe
vitatu
2. Siagi (Margarine au Blueband) -
Vijiko 10 3.Vipande vya chocolate
vikombe vitatu 4.Zabibu za
kukaushwa - Vijiko 5 vya chakula
5. Asali vijiko viwili vya chakula

6. Almond au korosho za kukaangwa


(zikatwe katwe nusu vipande) - Vijiko 6
vya chakula

MAANDALIZI
1. Weka vipande vya biskuti ndani ya
mfuko wa plastiki kisha pondaponda na
msukumio wa chapati au kitu chochote
kizito, hakikisha hazipondeki sana
2. Weka chocolate,siagi na asali katika
bakuli ya glass au ya plastiki kisha weka
bakuli juu ya sufuria yenye maji makali
ya moto kisha acha viyeyuke na
kutengeneza ujiuji na changanya vizuri
3. Baada
ya mchanganyiko kupoa,
mimina vipande vya biskuti,vipande vya
korosho na zabibu zilizokaushwa kisha
kwa kutumia mwiko changanya vizuri
4. Chukua bakuli kubwa la umbo la
mstatiri weka foil kwa ndani iendane na
umbo la hiyo bakuli kisha mimina huo
mchanganyiko humo chukua mfuniko
wa bapa au kifaa maalum cha
kukandamizia kisha kandamiza kwa juu
ili ipatikane msawazo.

5. Weka hiyo bakuli katika fridge kwa saa


1 hadi 2 na zaidi ili mchanganyiko
ugande vizuri

6. Baada ya kuganda toa bakuli kisha


toa keki yako na ikate katika vipande
vipande

Keki ya baridi ipo tayari


*Ukiwa na chocolate ya kutosha
iyeyushe na mwagia juu ya
mchanganyiko kabla ya kuweka
katika fridge
27.MAPISHI YA SHAWARMA

MAHITAJI
1.Minofu ya kuku isiyo na mifupa:-
Chicken fillets 2.Karoti moja:- Carrot
3. Hoho moja:- Capsium
4. Kitunguu maji kimoja:- Onion

5. Kitunguu
saumu kilichosagwa kijiko
kimoja cha chai:- 1 tsp garlic paste 1
6. Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha
chai:- 1 tsp ginger paste
7. Pilipili
manga ya unga kijiko kimoja cha
chai:- 1 tsp blackpepper powder
8. Pilipili
mbichi au ya unga:- Chilli or
chilli powder :- Ukihitaji (Optional)

9. Ndimu au limao kipande au


unaweza kutumia vinegar kiasi:- Lime
or vinegar
10. Chicken masala kijiko kimoja
cha chakula 11.Mafuta ya
kupikia:- Cooking oil 12.Chumvi:-
Salt
13.Tortilla au chapati

MAPISHI
****Andaa tortilla
((MAPISHI YA
TORTILLA

MAHITAJI

1. Ngano vikombe vitatu


2. Baking powder kijiko kimoja cha
chai 3.Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya
chakula (Tumia
mafuta ya maituni au sunflower kwa
matokeo bora zaidi)

4. Siagi
(Blueband au Margarine)
iliyoyeyushwa kijiko kimoja cha
chakula
5. Maji ya moto kikombe kimoja
6. Chumvi kijiko kimoja cha chai

MAPISHI

1. Changanya unga na baking powder


katika bakuli kwa kutumia mwiko

2. Changanya chumvi na maji ya moto

3. Tengenezashimo katikati ya unga kisha


mimina mafuta na maji ya moto yenye
chumvi kisha changanya na unga kisha
kanda hadi ngano iwe laini
4. Hamishiakatika sehemu ya kukandia
ngano iliyowekwa unga kiasi kisha
kanda ngano hadi iwe laini
5. Funika ngano kwa nusu saa hadi saa moja

6. Katakata ngano katika madonge


inayofanana kiasi kama tonge linalojaa
katika kiganja cha mkono

7. Chukua
msukimio wa chapati kisha
sukuma donge mojawapo katika mduara
mwembamba

8. Wekakikaango jikoni katika moto wa


wastani acha kipate moto kiasi, tumia
kikaango kizito ambacho ni non-stick au
kama hauna hicho kikaango weka
mafuta kiasi, ila hakuna ulazima wa
kutumia mafuta katika kuchoma tortilla
9. Weka tortilla yako katika kikaango
kisha choma kwa sekunde kama 30 hadi
45 hadi uone kama inajaa kwa juu na
imekuwa kahawia kwa chini, pindua
upande wa pili choma kwa sekunde 15
hadi iwe kahawia
10. Sukuma tortilla nyingine kisha choma

11. Hifadhi
tortilla katika hotpot yenye
mfuniko ili ziwe laini

12. Kumbuka kupunguza au kuzidisha


moto kila unapoona inahitajika
kufanya hivyo, moto unatakiwa
kuwa wa wastani.

***Tumia non stick pan kwa matokeo bora


zaidi

***Hatutumii mafuta katika kuchoma


tortilla

***Unaweza kuzihifadhi tortilla katika


friji kwa matumizi ya baadae, na
zinaweza kuhifadhiwa hadi wiki moja
***Tortilla hutumika kutengeneza
Shawarma au unaweza kula kama
chapati)))

ENDELEA NA HATUA ZINAZOFUATA

1. Muoshe kuku kisha kata vipande


vidogo vidogo sana.
2. Weka vipande vya nyama katika
bakuli kisha mimina kitunguu
saum,tangawizi,pilipili manga,pilipili
iliyosagwa au pilipili ya unga,mtindi,
kamulia limao changanya, nyunyuzia
chumvi kisha changanya tena
3. Andaa pilipili hoho, kitunguu maji na
karoti. Menya kisha kata vipande vidogo
vya karoti na kitunguu,pilipili hoho kata
vipande virefu na vipana.

4. Bandika kikaango jikoni, acha kipate


moto kiasi,weka mafuta kiasi. Acha
hadi yapate moto. Weka nyama,
tandaza vizuri. Acha iive kisha geuza ili
iive vizuri upande wa pili. Endelea
kugeuza mara
kwa mara hadi nyama ikauke kiasi na
kubadirika rangi.
5. Weka kikaango jikoni, kikipata moto
weka mafuta ya kupikia kisha weka
kitunguu maji. Kaanga vizuri hadi kianze
kubadilika rangi. Weka pilipili hoho na
karoti, koroga vizuri. Baada ya dakika 3
weka nyama ya kuku. Koroga pamoja
vizuri. Vikichanganyika vizuri, weka
chicken masala koroga vizuri, kisha epua
weka pembeni.
6. Weka tortilla katika kibao au sinia kisha
kwa kutumia kijiko chota mchanganyiko
wa kuku na mboga mboga weka katika
tortilla, mimina sosi ya jibini au tomato
sauce au sosi yoyote, mimina majani ya
giligilani au ya mnanaa, majani ya saladi
(letuce),weka kwa juu vipande vya
nyanya, kisha funga kunja tortilla vizuri
kama unavyokunja chapati
7. Shawarma ipo tayari kwa kula
28. MAPISHI YA CHAURO

MAHITAJI

1. Vimchele (Poha/Pawa):- Kilo 1


2. Crips
za viazi (Za kununua au za
kutengeneza):- Kiasi chochote kuanzia
bakuli au sufuria
kubwa la lita 3
3. Karanga kavu:- robo kilo

4.Korosho zilizokaangwa:-

robo kilo 5.Zabibu kavu:-

Kikombe kimoja

6.Dengu za vipande za manjano:-

Nusu kilo 7.Ndimu ya unga vijiko

viwili vya chai 8.Pilipili ya unga

kiasi kidogo
9.Majani ya mchuzi (Curry

leaves):- Kiasi 10.Manjano

kijiko kimoja cha chai

11.Sukari:- Robo kikombe


12.Chumvi kiasi

13.Mafuta ya

kupikia

MAPISHI

1. Osha na roweka dengu hadi siku ya pili


2. Weka kikaango jikoni mimina mafuta
ya kupikia ya kutosha acha yapate moto

3. Mimina dengu kaanga hadi ziive na


zikauke zitoe na zikaushe mafuta katika
chujio
4. Kaanga karanga hadi ziive na zikauke,
zitoe zichuje mafuta katika chujio

5. Kaanga vimchele kwa muda kidogo


tu vitoe na vichuje mafuta

6. Kaanga zabibu kavu kidogo

7. Wekamafuta kidogo katika frying


pan, mimina majani ya mchuzi
yakaange hadi yatoe harufu na
yakauke kisha mimina manjano na
koroga vizuri hadi usikie harufu ya
manjano.

8. Vunja
vunja crips ziwe katika
vipande vidogo vidogo
9. Chukua bakuli kubwa kisha mimina
vitu vyote humo, kisha mimina
chumvi,sukari, ndimu ya unga
na pilipili ya unga na changanya kwa
pamoja hadi vitu vyote vichanganyike
kwa pamoja.

10. Chauro ipo tayari.

*Mahitaji yote yanapatikana sokoni


29. MAPISHI YA JALEBI

MAHITAJI

1. Ngano vikombe vitatu


2. Unga wa dengu nusu

kikombe 3.Baking soda

nusu kijiko cha chai


4.Sukari vikombe

vitatu 5.Maji

vikombe vitatu

6.Hiriki ya unga nusu kijiko

cha chai 7.Manjano nusu

kijiko cha chai 8.Limao

moja au ndimu
9.Mafuta ya kupikia

MAPISHI
1. Chukuabakuli kubwa mimina unga wa
ngano, unga wa dengu, baking soda
kisha changanya vizuri kwa kutumia
mwiko

2. Mimina maji katika mchanganyiko na


changanya kwa kukoroga vizuri hadi
rojo liwe zito kiasi na jepesi kiasi,
hakikisha rojo halina madonge.

3. Funika
bakuli kisha hifadhi sehemu
yenye joto kwa saa 8, na kama upo
sehemu yenye baridi hifadhi
mchanganyiko kwa siku nzima.

4. Tengeneza shira kwa kufuata hatua hizi:-


5. Chukua
sufuria kisha mimina sukari
vikombe vitatu,hiriki na manjano kisha
mimina maji vikombe vitatu na weka
jikoni
6. Koroga mchanganyiko hadi sukari
iyeyuke, endelea kukoroga hadi yatokee
mapovu na rojo la sukari liwe zito kiasi
na linalonata ukishika kati ya vidole
viwili, kabla ya kushika rojo hakikisha
unatoa kiasi kidogo unapoza ndipo
unashika.Kamulia limao kidogo kisha
koroga.

7. Funua mchanganyiko wa
kutengenezea jalebi na andaa chupa
yenye kizibo ambacho kina kitobo,
mimina mchanganyiko kwenye chupa

8. Weka kikaango jikoni kisha mimina


mafuta ya kupikia acha yapate moto
kiasi, kisha minya chupa yenye rojo la
jalebi katika mafuta ya moto na
tengeneza miduara michache ya jalebi
kwa kuanzia ndani kwenda nje

9. Chomaupande mmoja wa jalebi hadi


uwe kahawia na mkavu kisha geuza na
choma upande mwingine
10. Toajalebi kadhaa katika mafuta
kisha ziingize katika shira acha kwa
dakika 3 kisha zitoe na weka katika
sinia au sahani
30. MAPISHI YA PIZZA ZA ZANZIBAR
(MIKATE YA NYAMA)

MAHITAJI

1.Ngano nusu
kilo 2.Nyanya
tatu 3.Karoti
moja kubwa
4.Hoho moja
kubwa
5.Nyama ya kusaga iliyochemshwa
nusu kilo 6.Mayai matano
7. Manjano kijiko kimoja cha chai

8. Kitunguu
saum kilichopondwa kijiko
kimoja cha chai
9. Vitunguu maji
10. Majani ya giligilani kiasi

MAPISHI

1. Katakata
kitunguu
maji,nyanya,karoti,na hoho katika
vipande vidogo vidogo sana

2. Wekakikaango jikoni kisha mimina


mafuta ya kupikia kiasi kisha acha
yapate moto kiasi

3. Pasua
mayai weka chumvi kiasi kisha
changanya vizuri kupata rojo
4. Mimina vipande vya kitunguu maji
koroga hadi viwe kahawia,mimina
vitunguu saum koroga hadi vibadirike
rangi kiasi,mimina karoti,hoho na
vipande vya nyanya kisha endelea
kukoroga kiasi,mimina manjano, mimina
chumvi kidogo koroga, mimina majani ya
giligilani kisha changanya tena, epua
mchanganyiko na acha upoe kidogo.

5. Mimina
rojo la mayai katika
mchanganyiko na koroga vizuri

6. Kanda
ngano kama unavyokanda
ngano ya kupika chapati, kisha ifunike
kwa nusu saa
7. Andaa madonge kadhaa

8. Chukua
madonge kisha sukuma na
tengeneza chapati nyepesi sana
9. Kwakutumia kijiko chota
mchanganyiko wa mayai na viungo kisha
weka katika chapati na fungasha chapati
kama vile box lenye unene kiasi,
tengeneza rojo la ngano zito kaisi kwa
kuchanganya ngano na maji kiasi kisha
tumia kama gundi katika kufunga hiko
kibox cha ngano

10. Weka kikaango cha chapati jikoni


kisha weka mafuta kiasi acha yapate
moto, beba kibox chenye
mchanganyiko wa nyama na viungo
kwa kutumia mshikio bapa wa
kupindulia chapati kibox kisha kiweke
kwenye kikaango na kichome kama
chapati pande zote mbili hadi kiwe
kahawia
11. Epua kibox weka katika tissue au
chujio ili kichuje mafuta

12. Andaa sosi ya pilipili na juisi au chai


ya maziwa na hizi piza, kula na
ufurahie.
31. MAPISHI YA VITUMBUA VYA

MAEMBE

MAHITAJI
1.Unga wa mchele kikombe

kimoja 2.Unga wa ngano vijiko

viwili vya chakula

3. Rojo la
embe mbivu zilizosagwa
kikombe kimoja na nusu
4. Maziwa nusu

kikombe 5.Sukari

nusu kikombe

6. Hiriki ya unga nusu kijiko cha chai

7. Baking soda kiasi kidogo kama robo

kijiko cha chai 8.Chumvi kijiko kimoja

cha chai
9.Mafuta ya kupikia au siagi au samli

MAANDALIZI NA MAPISHI

1. Chukuasufuria kisha pasha rojo la


maembe kwa kukoroga hadi mvuke
uanze kutoka
2. Katikabakuli kubwa mimina maziwa
changanya na sukari kisha koroga
vizuri hadi sukari iyeyuke kisha mimina
unga wa mchele na unga wa ngano
changanya kupata ujiuji au rojo

3. Ongeza hiriki ya unga na baking


soda kisha changanya vizuri hadi
vitu vyote vichanganyike vizuri

4. Mimina chumvi kiasi kisha koroga

tena 5.Funika mchanganyiko kwa

muda wa nusu saa


6. Katika moto wawastani weka
kikaango cha vitumbua jikoni kisha
mwagia mafuta kiasi katika kila tundu
na acha yachemke kiasi.
7. Kwa kutumia upawa mwagia rojo
katika kila tundu, kaanga vitumbua hadi
upande wa chini uwe kahawia na
kukauka kidogo kisha kwa kutumia kitu
cha ncha kali pindua vitumbua upande
wa pili taratibu kisha kaanga tena hadi
viwe kahawia na vikavu kiasi.

8. Vitumbua vya maembe vipo tayari


32. NAMNA YA KUTENGENEZA
BISKUTI ZA TANGAWIZI

MAHITAJI

1.Unga wa ngano aina ya (Plain flour)


vikombe viwili 2.Tangawizi ya unga vijiko

viwili vya chai


3. Bicarbonateof soda au baking
powder kijiko kimoja cha chai

4. Siagivijiko nane na nusu vya chakula


(Siagi kama blueband au magarine)

5. Sukari nusu kikombe na vijiko vinne

vya chakula 6.Asali vijiko vinne vya

chakula au golden syrup 7.Yai moja

8.Chumvi kiasi

*Kikombe kinachotumika ni kikombe


cha robo lita (250 mls)
MAPISHI

1. Washa oven katika joto la 180 (C)


digrii au 350 (F) digrii

2. Wekatangawizi na bicarbonate of
soda katika unga kisha changanya
vizuri

3. Changanya
siagi katika unga hadi unga
uwe kama umeachana achana kisha
mimina sukari

4. Pasua
yai na likoroge katika bakuli
pembeni kisha mimina katika bakuli
lenye unga, kisha mimina asali na
changanya vizuri kisha anza kukanda

5. Chukua kifaa cha kusukuma ngano


kisha sukuma ngano katika unene wa
chapati nzito
6. Chukuakisu kisha katakata
vipande vinavyolingana

7. Weka vipande hivyo katika trei la


kuokea ambalo kwa juu umeweka
karatasi maalum ya kuokea au foili

8. Ingiza
trei katika oven kisha oka biskuti
kwa dakika 10 hakikisha zimekuwa na
rangi ya kahawia.

9. Toa biskuti katika trei kisha

acha zipoe 10.Kumbuka kuzima

oven
KARIBU UJIPATIE VITABU VYETU

VINGINE

You might also like